Chama cha ADC chapata matumiani

Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa kati kati, mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji na naibu msajili wa vyama siasa Rajab Baraka wakiwa katika mkutano wa tathmini huko katika ofisi ya chama hicho Bububu nje kidogo ya mji wa Zanzibar

CHAMA kipya cha Alliance for Democratic Change (ADC) jana kilipata matumaini mapya baada ya Msajiri wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kusema chama hicho kinaendelea vizuri. Tenda alitoa matumaini hayo katika hutuba yake aliyotoa kabla ya kuanza kuhakiki wanachama 200 wa chama hicho Mjini Zanzibar
Katika hutuba yake fupi aliyoitoa nje ya ofisi ya ADC mtaa wa Bububu nje kidogo ya mji Zanzibar, msajili huyo alisema tangu chama hicho kpata usajili wa muda mapema mwaka huu kimekuwa kinafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.

“Nakupongezeni kwa juhudi mnazofanya lengo la chama ni kushika dola lakini kwa mwendo wenu inaonekana azma hiyo mnayo” alisema Tendwa.

Hata hivyo alisema baada ya uhakiki wa chama hicho katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Pemba alitaka juhudi hizo ziendelea katika miko iliyobaki ili kutimiza masharti ya kupata usajili wa kudumu.

“Sheria zilizokuwepo lazima muzifate na mimi nitakuwa mkali kwa kuhakikisha kwamba sheria hizi zinatekelezwa, sitaki wanachama hewa lazima aliye na kadi ajitokeze” alisisitiza huku akifurahiwa na wanachama wa chama hicho.

Mapema mwenyekiti wa taifa wa chama, Said Miraji alisema chama chake kipo tayari kufanya kazi ili kufikia malengo na kuwaomba viongozi na wanachama wa vyama vyengine kuwa na moyo wa kuvumiliana.

“Leo hii tukipata usajili wa kudumu tutaingia katika uchaguzi mdogo wa jimbo la bububu na tutashinda kwa sababu tunapata wanachama wengi kutoka vyama vyengine” alitamba Miraji.

Miraji alisema wakati anapokea wanachama wengi kutoka vyama vyengine vya upinzani viongozi wa vyama hivyo wasieneze fitna na chuki ili kuendeleza dhana ya  demokrasia ya kweli.

Mwenyekiti huyo alikumbusha kuwa wakati wa kuanza mfumo wa vyama vingi vyama vya upinzani vilipata wanachama wengi kutoka chama cha mapinduzi kwa hivyo katika hali hiyo hiyo vyama hivyo vya upinzani vinatakiwa viwe na uvumilivu wakati wanachama wao wakiwakimbia na kuhamia ADC.

“CCM walikimbiwa na wanachama wengi na hivyo wanachama wenu wanapokukimbieni na kuja kwetu msilalamike wala msinune jitazameni makosa yako wapi kuliko kuendeleza fitna na majungu kwa sababu kila leo tunapokea fitna mpya” alilalamika.

Mkutano huo ambao ulikuwa ni wa kuhakiki chama hicho pia ulihudhuriwa na viongozi wa vyama vya upinzani wakiwemo kutoka  TADEA, AFP, NLD na SAU, wawakilishi wa CCM, CUF na CHADEMA hawakuonekana katika mkutano huo.
Kwa mujibu wa sheria za usajili kila chama kinatakiwa kiwe na wanachama hai 200 kutoka angalau mikoa kumi ya Tanzania kabla ya kupata usajili wa kudumu.

Kusajiliwa kwa chama hicho kitafanya Tanzania kuwa na vyama vya siasa 19 tangua kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ambapo CCM bado kinaendelea kuviongoza vyama vyengine vya upinzani.

Advertisements

10 responses to “Chama cha ADC chapata matumiani

 1. “Hata hivyo alisema baada ya uhakiki wa chama hicho katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Pemba alitaka juhudi hizo ziendelea katika miko iliyobaki ili kutimiza masharti ya kupata usajili wa kudumu.”
  Mie huwa nachukizwa sana kusoma kauli kama hiyo ya juu, maana visiwa vyetu ( kama hapo Pemba) kuwa ni mkoa katika mikoa ya Tanganyika, tunafananishwa na kina Tanga, Mwanza n.k.
  Waandishi wa habari vile vile kwa njia moja au nyingine wanabeba lawama kwa kaundika na kufikisha ujumbe kwa hali hii. Unguja na Pemba au Zanzibar kamili haitokuwa kamwe mkoa kati ya mikoa ya Bara.
  Kuhusu hivyi vyama mie naona ni kuengeza idadi tu.. ni kama vile katika ligi za mipira kuna ‘big three’ au ‘big two’ na kuna timu nyingine just kusindikiza tu.. ndio sawasawa na hivyo vyama vyengine.

 2. Zanzibar huru kwanza. Hatuutaki muungano. Said Miraji wakati huu ni wa kuikomboa zanziba kutoka kwa mkoloni Tanganyika si wakati wa kuimarisha chama cha siasa. Au umetumwa kupoteza malengo ya wazanzibari.? Sisi tuko makini hutubabaishi hata kidogo. HATUUTAKI MUUNGANO NA HATUNA SIASA KWA MUDA HUU TUPO PAMOJA HATUTAKI UKOLONI WA KITANGANYIKA. ZANZIBAR HURU INAWEZEKANA. Tutashinda kwa nguvu za Allah.

 3. Huyo Hamad Rashid kesha abaki hukouko na watanganyika wenzake, huku kauli mbiu ni Jamhuri ya watu Zanzibar kwanza

 4. Wewe miraji ustuletee ujinga cc tunataka nchi yetu na wenye uchungu na nchi tunawajua na wenye njaa tunawajua wacha ujinga nani asiejua kua kwenu songea ulikuja pba kus6esha.

 5. Sory alikuja pemba kusomesha skuli akapewa hifadh leo anatuletea fitna msaliti umeshasahau ulipopangiwa al-uruba hotel

 6. Waislamu Wazanzibari, hawa jamaa lengo lao ni kututoa kwenye ajenda yetu (ZANZIBAR HURU) wakati huu muhimu, shime tujikinge na mtego huu. Kanisa-CCM linaanza mitego ya kipuuzi. Mambo ya Hamad Rashid tuyapuuze. Naomba sana sana.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha ombi.

  SERELLY.

 7. Ndugu zetu Pemba jiepusheni na serikali tatu za shirikisho, sera hii ni ya Chama fulani lakini twende mbele zaidi ya hapo ili tuwe huru. Shikilieni MUUNGANO WA MKATABA.

  Nimeyasema haya baada ya mshituko mkubwa niliopata leo wakati na zungumza kwa simu na graduate mmoja alienitaka ni mfahamishe maana ya MUUNGANO WA MKATABA, pia alishangaa na kuuliza:

  “kwani hatuwezi kuukata moja kwa moja kama tulivyoazimia?

  Kumbuka huyu ni Degree holder. Je wengine?

  Misikiti, maskani, vikao, simu n.k vitumike vizuri ili kuhakikisha uwiano katika kuikomboa Zanzibar.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilishe.

  SERELLY.

  • musishangae hao ndio wanasiasa walivyo wanakwenda na upepo wa maslah said miraji ni kiongozi nilikuwa nae imani sana lakini hayo ndio mazingira ya siasa hivyo vyama havina maana yo yote kuwapo zaidi ni kutugawa inawezekana nchi kwenda bila vyama vya siasa kwasababu ni biashara kila moja anfungua duka kurkutafuta rizki

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s