Njama za kufisidi Uislamu Tanzania

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Katika makala zangu zitakazofuata baada ya hii itakua ni Tathmini yangu kuhusu Waislamu na Nyerere baada ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania). Nimeona bora nitangulize makala hii kwanza. Uislamu katika Tanzania. Theluthi mbili ya Waislamu wote wa Afrika ya Mashariki wanaishi Tanzania, ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote katika Afrika ya Mashariki, yaani Kenya, Uganda na Tanzania.

Hii ni pamoja na Zanzibar yenye Waislamu takribani asilimia tisini na tisa na kuna wakati ilikuwa ndio vitovu cha maarifa ya Kiislamu katika Afrika Mashariki na kati.

Takwimu za Africa South of the Sahara zinaonesha Waislamu ni wengi Tanzania kwa 60%. Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka mwaka 1982. kwa kuwa utafiti wa Waislamu wenyewe katika suala hili ni mdogo sana au haupo kabisa.

Suala la wingi wa Waislamu katika Tanzania halijafanyiwa utafiti na Waislamu wenyewe. Somo hili ni nyeti, katika nchi za Kiafrika ambazo zinawafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na Nigeria.

Uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha mgongano. Tatizo hili lipo Tanzania. Mfano mzuri ni sensa ya kwanza mwaka 1967 baada ya Uhuru jumla ya Wakristo Tanzania Bara ilikuwa asilimia thelathini na mbili 32% na Waisalamu asilimia thelathini na moja 31% na Wapagani asilimia thelathini na saba 37% sense hii inaonesha kuwa Wapagani ndiyo walio wengi Tanzania.

Sensa hii ya mwaka 1967 haikueleza kwa nini katika kipindi cha miaka kumi kwa ghafla Waislamu wamepungua nchini au kwa nini Wapagani wameongezeka katika nchi ya waumini.

Hii ndio ilikuwa sensa ya mwisho iliyokuwa ikionesha mgawanyiko wa dini. Inasemekana kuwa matokeo ya sensa hii yalifanyiwa mabadiliko kwa ajili ya sababu za kisiasa pale ilipobainika kuwa Waislamu Tanzania walikuwa wengi kupita Wakristo. Ilipobainika kuwa Waislamu ni wengi Tanzania, Idara husika ilipokea amri ya kuchoma moto matokeo yote ya sensa ya mwaka 1970.

Bahati mbaya mgao wa madaraka katika siasa Tanzania umewatupa nje Waislamu, ingawa inafahamika kuwa usalama na utulivu wa nchi yeyote unategemea mizani hii kuwa sawa.

Magawanyo wa madaraka na wingi wa wafuasi katika dini au kabila havikuwa vitu vilivyokuwa vikiwashughulisha wananchi wakati wa Ukoloni kiasi cha kuleta mifarakano katika jamii, kwa bahati nzuri ukabila hauna nguvu Tanzania lakini dini imekuwa chanzo cha Ubaguzi toka zama za Ukoloni, tofauti ni kuwa wakati wa Ukoloni waliokuwa wakiwabagua Waislamu hawakuwa Wakristo weusi bali Wazungu.

Ukristo uliingizwa katika Tanzania katika karne ya kumi na nane na umesionari kanisa na Mwafrika Mkristo ni matokeo ya Ukoloni kwa ajili hii basi historia ya Kanisa katika Afrika ni ile ya kushirikiana na kuwa tiifu kwa Serikali ya Kikoloni.

Chini ya Ukoloni, taratibu Kanisa likaweza kujenga Uhusiano maalumu kati yake na Serikali pamoja na Mkiristo Mwafrika ambae imemuelimisha katika shule zake. Mwafrika Mkiristo akawa ananufaika na mfumo wa kikoloni.

Waislamu wakawa wanataabika kwa kuwa dini yao ilikuwa inapingana na dini ya Mtawala. Mwafrika Mkiristo akawa mnyenyekevu kwa Serikali wakati wa na baada ya kupatikana kwa Uhuru akaja kushika madaraka ya Serikali. Waislamu wakatengwa na kuteswa katika Ukoloni kwa kubaguliwa na kunyimwa elimu hiyvo kuwaondolea fursa ya maendeleo, kuwepo Waislamu kama raia na ili kuinusuru dini yao ilibidi Waislamu wasimame kuutokomeza Ukoloni.

Baada ya Uhuru Kanisa likabaki na msimamo wake wa enzi ya Ukoloni wa kutii na kujipendekeza kwa Serikali mpya iliyokuwa madarakani. Ushirika huu kati ya Kanisa na Serikali, ulijengwa na tabia ya kanisa ya kukubaliana na mfumo wowote wa Serikali ili Kanisa liweze kuwa na mazingira mazuri ya kujifanyia shughuli zake bila ya kipingamizi wala wasi wasi.

Kutokana na uhusiano huu maalumu Kanisa likajifanyia msingi imara wenye nguvu kutokana na Wakristo waliowasomesha katika shule zao. Kanisa likatumia nafasi na uhusiano huu kwanza na Serikali ya Kikoloni kisha na Serikali ya Wananchi kujijengea himaya ambayo wafuasi wake wakaja kushika nafasi zote muhimu katika Uongozi wa juu Serikalini, Bunge na Mahkama katika Tanzania, katika miaka yake mia moja tu Kanisa likaweza kupata safu yake ya Viongozi ambao wanadhibiti kila sekta katika jamii ya Watanzania. Ndio hivi sasa tunauita MFUMO KRISTO.

Wamisionari walipotia mguu pwani ya Afrika ya Mashariki, nia yao hasa ilikuwa kuufuta Uislamu. Wakazi wa pwani hii iliyokuwa ikijulikana kama Zanj waliuona Ukristo kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1498 Wareno walipofika sehemu hizo mwaka 1567 wamishionari wa Agustinian waliingia Afrika ya Mashariki ili kupambana na Uislamu ili Ukristo uwe dini ya dunia nzima. Kadinali Lavigire alianzisha The White Fathers, taasisi ya Kanisa Katoliki kwa kusudi maalum la kupiga vita Uislam.

Wakati huo huo Chirch Missionary Society (CMS) ilikuwa imejitwisha kazi ya kuondoa Ulimwengu kutokana na Uislam, ujinga na giza. Hadi hii leo White Fathers wapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiendelea kufanya kazi iliyowaleta Tanganyika zaidi ya miaka mia iliyopita. Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameilimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwing Kraph alipofika kwa chifu Kimweri wa Usambara mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma. Herufi waliokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu. Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani Serikalini.

Wamisionari na Wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislamu. Wamewakuta watu walistaarabika na wenye utamaduni wao wa kupendeza. Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na Shule zake. Hapo ndipo zilipoanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na baada yake watu walazimishwa kujifunza herufi za Kirumi. Muislam ambaye jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameilimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika. Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katika Mkutano wa Berlin Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lilioachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya Kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza. Kanisa linaeleza uongo na propaganda kuwa lenyewe ndio lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika. Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za Kanisa bali katika Madras.

Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia moja Kanisa likaelekeza nguvu zake katika kuwatayarisha raia ambao wengi wao walikuwa Wakrisho, watakaokuwa watiifu kwa Kanisa na Serikali. Ni katika mtanuko huu ndio Wakristo wanamiliki Serikali na chama cha Mapinduzi na kuimarisha ifanye linavyopenda Kanisa, wakati Waislam na Uislam ukafanywa kama vitu visivyokua na maana yoyote.

Hadi kufikaia mwaka wa 1960 Kanisa likawa taasisi kubwa inayomiliki mamilioni ya dola ya misaada inayopokelewa kutoka wahisani na wafadhili walioko katika ulimwengu wa Kikristo.

Kanisa sasa hivi linahodhi mahospitali, misururu ya ndege binafsi, viwanja vya ndege, makampuni ya uchapishaji na mitambo ya kupigia chapa, steshini za Radio na magazeti.

Kanisa limekuwa na nguvu na udhibiti wa mambo kiasi kwamba wakati mwingine watendaji, hasa Wakristo katika Serikali na ndani ya Chama tawala cha CCM hawajui utii wao uwe Serikalini bali wana amini moja kwa moja kwamba wao wanawajibika kwa Kanisa zaidi kuliko Serikali.

Ni katika kuchanganyikiwa huku kwa watendaji wa Serikali na Chama kuhusu uhusiano wao na Kanisa ndiko kulikoamsha kutoaminiana kati ya Waisalam na Serikali na Chama cha Mapinduzi. Serikali na Chama ikaonekana kama ni miongoni mwa taasisi za Kanisa na Waislam wakiwa ni watazamaji tu.

Baada ya Uhuru kupatikana, Kanisa likaanza kusikika likisema kuwa lina haki na wajibu kuwa na ushawishi ndani ya Serikali, kuikosoa Serikali na kuiongoza pale inapoona Serikali haifanyi mambo sawa kwa matarajio yake. Kanisa likajipa fursa ya kuwa msemaji wa watu. Huu ulikuwa ni muelekeo katika mambo ya siasa na utawala..

Chanzo ni Gazeti la Anuur

Makala imeandikwa na Ibrahim Muhammed Hussein-0715-498 363

Advertisements

7 responses to “Njama za kufisidi Uislamu Tanzania

 1. Nakushukuru kwa kuonesha moyo wa kuwa ni miongoni mwa watu wanaojali na kujitambua katika dini. Allah akuongezee ujasiri ulionao ili uweze kuendelea na ufahamisho huu kwa wale wote wasiofahamu na wanaopotosha ukweli juu ya Uislam na waislam nchini.

  Niko pamoja na wewe na niko tayari kuchangia pale penye mapungufu. Allah Karim.

 2. Unachanganya sana kwani lugha ya kiarabu na uislamu vina uhusiano? Pili biashara ya utumwa na uislamu pia vina uhusiano?

 3. Mbona haukuelezea wakati wa biashara ya utumwa na uislam kulikuwa na uhusiano gani?
  Mbona mwislam alikuwa hanyanyasiki wala kuchukuliwa mtumwa? Kulikuwa na uhusiano gani kati ya biashara ya utumwa na uislam?

 4. we Mukolo na Saguge kwanza kiarabu ndiyo lugha ya msingi katika kutekeleza ibada katika dini ya kiislam
  halafu pili watumwa siyo kwamba walikuwa wanachaguliwa bali ilikuwa wanachukuliwa wale wenye nguvu za kufanya kazi
  keanza walikuja kundi la kwanza la wapelelezi kuja kupeleleza Africa ya mashariki kuijua ilivyo na kutuma ripoti kwao ulaya then likaja kundi lingine la wamisionari ambao walileta Ukristu wakiwa wanalainisha mioyo ya watu ili waweze fanya wanavyotaka bila ya vikwazo lakini walikuwa wana plani zao zingine
  pia likaja kundi lingine la wafanyabiashara ambapo ndo ilihusisha walifanya biashara na watu Africa hadi wakafikia kwenye UKOLONI

  kwahiyo walikuwa wakitumia hiyo mbinu ya kutanguliza makundi ilikusafisha njia ya ukoloni wakiwa hawakujionesha nia yao

  kitabu cha HISTORY OF EAST AFRICA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s