Baraza

Wajumbe waharakisha shirika la mafuta

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wamepitisha makadirio ya matumizi ya wizara ya ardhi, makaazi maji na nishati ya mwaka wa 2012/2013 huku wakitaka uanzishwaji wa shirika la mafuta la Zanzibar ifikapo Januari mwakani. Wajumbe wengi hasa ambao wasiokuwa mawaziri (backbenchers) walionesha kutoridhika na majibu ya serikali kuhusu sababu za kutoendeleza utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika visiwa vya Zanzibar. Huku wakitishia kuikwamisha bajeti ya wizara hiyo wajumbe hao walisema ni muda mrefu umepita bila ya dalili zozote za kuendeleza utafutaji wa mafuta na kuitaka serikali kuwa na msimamo usioyumba. “Ni muda mrefu kila ahadi ndio hizo kwa hivyo tunasubiri utatuzi wa kero za muungano lakini wenzetu wanaendelea na mambo yao. Tunataka sheria ya kuanzisha shirika la mafuta ya Zanzibar ifikapo Januari mwakani bila ya hivyo tutaleta hoja binafsi ya kuazishwa shirika hilo” alisema Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa huku akiwataka wenzake wamuuonge mkono. Endelea kusoma habari hii

Wajumbe watishia kuzuwia bajeti ya Ardhi

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wametishia kutopitisha makadirio ya bajeti ya wizara ya ardhi, makaazi, maji na nishati kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 kutokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi Unguja na Pemba. Wakichangia bajeti ya wizara hiyo wawakilishi wa CM na CUF waliungana kulaumu serikali kwa kutochukua hatua madhubuti ili kupunguza au kuondosha kabisa migogoro ya ardhi inayozorotesha maendeleo nchini. Walisema  licha ya malalamiko ya wananchi pamoja na rais mwenyewe lakini hakuna dalili za kumaliza tatizo hilo ambapo wameshauri kuundwa kwa kamati teule ili kuchunguza matatizo ya ardhi. “Rais amelalamika na hali katika vijiji kadhaa sio nzuri baina ya wananchi na viongozi na wawekezaji. Tatizo lipo wapi mbona ni muda mrefu?” alihoji Mwakilishi wa Jimbo la ChakeChake (CUF) Omar Ali Shehe. Alisema ili kupata jibu sahihi kutokana na kilio cha kila mtu na rais wa Zanzibar ni kuundwa kwa kamati teule ili kufuatilia tatizo la ardhi ambalo pia linaipa jina baya Zanzibar. Endelea kusoma habari hii

Bajeti ya Afya yapita kwa tabu

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wamepitisha bajeti ya wizara ya afya kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 baada ya kumbana waziri wa wizara hiyo Juma Duni aji kwa masaa kadhaa. Miongoni mwa hoja zilizomtoa jasho Waziri Duni ni kukithiri kwa uchafu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, ukosefu wa wafanyakazi, upungufu wa dawa na wataalamu pamoja na utaratibu wa kusafirisha wagonjwa nje ya nchi. Wajumbe wa baraza akiwemo Makame Mshimba Mbarouk (CCM) Mbarouk Mussa Mtando (CCM) Salum Abdallah Hamad (CUF) na Ismail Jussa Ladhu (CUF) kwa nyakati tofauti walielezea kusikitishwa na hali ya uchafu uliokithiri pamoja na wagonjwa wengi kukosa nafasi ya kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ambapo baadhi yao walisema kuna harufu ya rushwa. Akijibu hoja hizo kabla ya kupitishwa kwa bajeti hiyo waziri wa wizara hiyo Juma Duni alijitetea na kusema kuwa hali ni afadhali kuliko siku zilizopita. Endelea kusoma habari hii

Benki ya wanawake kuanzishwa Zanzibar

SERIKALI ya Zanzibar inakusudia kuanzisha benki ya wanawake itakayolenga kuwainua kiuchumi wanawake wa zanzibari lakini baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamesema mpango huo umechelewa mno kuanza. Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF) Mtumwa Kheri Mbarak na Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma waliibana serikali kuwa mpango wa kuanzisha benki umechelewa kwa muda mrefu bila ya sababu za msingi. Waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema kuanzisha benki haihitaji kwenda kwa haraka kutokana na utaratibu wa kibenki na mtaji unaotakiwa. “Mheshimiwa Spika serikali ina azima ya dhati ya kuanzisha benki ya wanawake lakini ili kuanzisha benki kwa mujibu wa taratibu kunahitaji mtaji wa bilioni 15 na maandalizi mengine ambayo hivi sasa hivi tunaendelea nayo naomba wajumbe wawe na subra” alisema. Endelea kusoma habari hii

Zanzibar haina uwezo wa kuwa na sarafu yake

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa haiwezi kuanzisha sarafu yake (fedha zake) kutokana na kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hairuhusu kufanya hivyo. Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee wakati kijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyetaka kujua sababu za Zanzibar kutokuwa na sarafu yake ili kuimarisha uchumi wake. Jussa alisema sarafu ya Tanzania inaendelea kushuka thamani dhidi ya fedha za kigeni (dola) siku hadi siku na kufanya Zanzibar kuwa katika hali ngumi kiuchumi ikiwemo wananchi wake kukabiliana na mfumko wa bei na kupelekea maisha kuwa magumu. Endelea kusoma habari hii

Serikali: Zanzibar haijawahi kutawaliwa

MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman ameshangazwa na mwanasheria mwenzake Tundu Lisu kwa kutofahamu madhumuni na malengo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliozaa serikali ya umoja wa kitaifa. Kauli ya Mwanasheria huyo aliitoa katika baraza la wawakilishi wakati akifafanua baadhi ya mambo ya kisheria baada ya wajumbe wa baraza hilo kumtaka afanye hivyo kufuatia kauli ya ya Tundu Lisu aliyoitoa bungeni wiki hii.“Sasa kuja kwa haya yametuonesha kwamba kuna wenzetu kumbe wana fikra kwamba Zanzibar iliwahi kutawaliwa. Maana mtu anaposema marekebisho ya 10 ya Zanzibar yamjitangazia uhuru maana yake ana fikra na huyu ni mwanasheria mtu kafika mpaka kuwa mbunge anayeaminika na chama chake lakini anasema kwa kufanya hivyo Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa?” Alihoji Othman. Endelea kusoma habari hii

Wawakilishi wataka uwiano sawa wa ajira

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepitisha makadirio ya mapato ya matumizi ya wizara ya nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 huku wajumbe hao wakitaka nafasi zaidi za ajira kwa wazanzibari katika serikali ya jamhuri ya muungano.Pamoja na mambo mengine wajumbe hao walizungumzia kwamba wanahiotaji mgawanyo sawa au angalau asilimia 40 ya nafasi za kazi ndani ya seikali ya muungano. Wajumbe kadhaa walisema nafasi za ajira ndani ya serikali ya muungano ni muhimu ziwe sawa ili kuondosha manunguniko kwa upande mmoja wa muungano.Wajumbe wa baraza la wawakilishi pia walitaka serikali ya Zanzibar kuondosha michango ambayo inachangishwa kwa vikosi vya ulinzi na polisi michango ya aina mbali mbali na kwamba ni kinyume na sheria za utumishi wa umma kuhusu mishahara.Aidha wajumbe wa baraza hilo walitaka serikali kufanya mabadiliko ya mishahara na maslahi kwa watumishi wa muda mrefu serikalini ambapo hupokea mishahara midogo kwa kisingizio cha kiwango kidogo cha elimu. Endelea kusoma habari hii

Wajumbe wataka sheria ya maadili ya viongozi

 WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wameishauri serikali ya Zanzibar kuleta sheria ya maadili ya uongozi kabla ya utekelezaji wa sheria ya rushwa na uhujumu uchumi. Wakichangia bajeti ya wizara ya nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora, wajumbe hao walisema kutokana na kukithiri kwa uvunjaji wa madili ya uongozi ingekuwa vyema kudhibiti vitendo hivyo mapema.Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake (CUF) Omar Ali Shehe alisema “Mheshimiwa Naibu Spika sheria ya maadili ya viongozi iletewe haraka sana hapa katika baraza la wawakilishi kwa sababu sisi viongozi ndio tunaokiuka maadili ya uongozi pamoja na kuwa wala rushwa wakubwa”.Naye Mwakilishi wa jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk alisema itakuwa vigumu kutekeleza sheria ya rushwa bila ya kuwepo kwa sheria ya maadili ya viongozi. Salmin Awadh Salim Mwakilishi wa jimbo la Magomeni (CCM) alisema baadhi ya watendaji serikalini wamekuwa wakipoteza mamilioni ya shilingi bila ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Endelea kusoma habari hii

Serikali yakamilisha sheria ya rushwa

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema imo katika kukamilisha utaratibu wa kuanzisha rasmi taasisi ya kuzuwia na kupambana na rushwa Zanzibar. Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya utumishi wa umma na utawala bora, Haji Omar Kheri wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea. Alisema kufuatia kutungwa kwa sheria ya rushwa na uhujumu uchumi mapema mwaka huu wizara yake inategemea kufungua ofisi ambayo itakuwa na majukumu ya kuchunguza mambo na vitendo vya kuwepo au kuruhusu rushwa. “Tumefikia pahala pazuri na taasisi hii muhimu ya kuzuwia na kupambana na rushwa pamoja na uhujumu uchumi, itaanza kazi zake sio muda mrefu baada ya taratibu kukamilika” alisema waziri huyo. Alisema katika kuimarisha utawala bora Zanzibar mamlaka ya kuzuwia na kupambana na rushwa na uhujumu uchumi ni muhimu na itaweza kusaidia kuimarisha utendaji kazi pamoja na nidhamu serikalini. Endelea kusoma habari hii

Vitambulisho 112,420 havina wenyewe

WAZIRI wa nchi ofisi ya rais Dk Mwinyihaji Makame Mwadini amesema jumla ya vitambulisho vya ukaazi wa zanzibar 112,420 havijachukuliwa na wenyewe katika wilaya mbali mbali kinyume na kauli zinazotolewa na wanasiasa kuwa wananyimwa vitambulisho.Akitoa majumuisho ya bajeti ya ofisi ya rais kabla ya wajumbe kupitisha bajeti hiyo Dk Mwinyihaji alijitetea na kusema kuwa idara ya vitambulisho Zanzibar imekuwa ikifanya kazi zake kwa uangalifu mkubwa na kuwataka wananchi wafuate utaratibu.Alisema kwa muda mrefu vitambulisho havijachukuliwa na vipo wilayani na kutaka wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwashawishi wananchi katika maeneo yao wakachukue vitambulisho pamoja na kuacha udanganyifu hasa vyeti vya kuzaliwa wakati wanapoomba vitambulisho. Mjadala wa bajeti ulitawaliwa zaidi katika michango yake kuhusu vitambulisho ambapo lawama zilitupiwa kwa masheha, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa pamoja na maafisa wa idara ya vitambulisho kuwa wanahusika na kufanya ubaguzi katika upatikanaji wa vitambulisho hivyo pamoja na kutoa vitambulisho kwa watu wasiostahiki wakiwemo wageni. Endelea kusoma habari hii

Uzalendo wawakimbiza Wataalamu

Serikali ya Zanzibar imesema ukosefu wa uzalendo na tamaa ndio unapopelekea wataalamu wa fani mbali mbali kukimbia Zanzibar. Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora, Haji Omar Kheri wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua sababu za wataalamu kuendelea kukimbia nchini. Mwakilishi huyo apamoja na Mwakilishi wa Salum Abdallah Hamad (CUF) wa Matambwe, Rashid Seif Suleiman (CUF) wa Ziwani na Jaku Hashim Ayoub wa Jimbo la Muyuni (CCM) wote walilalamika kuwa serikali inachangia kuwatorosha wataalamu kwa kuwawekea mazingira mabaya ya utendaji kazi na malipo duni. “Naomba nikubaliane na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa nchi nyingi zilizopo kwa janga la sahara hukimbiwa sana na wataalamu wake hususan madaktari wakiwemo pia maprofesa na wahadhiri licha ya kulipwa stahiki mbali mbali” alisema waziri Kheri. Endelea kusoma habari hii

SMZ yakerwa na vipeperushi vinavyoleta ubaguzi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haifurahishwi na tabia ya watu wanaojitokeza kuandika vipeperushi vya fitna dhidi ya wananchi wa Unguja, Pemba na Tanzania Bara. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohammed amesema hayo wakati akichangia ufafanuzi wa majumuisho ya wizara yake katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar. Alisema kumekuwepo na watu wanaosambaza vipeperushi vyenye maandishi ya ubaguzi na kuwagawa watu wa Unguja na Pemba pamoja na Bara ambapo alisema tabia hiyo haiwezi kujenga bali inazidi kuwagawa wananchi ambao wana udugu wa asili kwa miaka na miaka. Kauli ya Aboud amekuja kufuatia baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kulalamika kwamba wapo watu wanasambaza vipeperushi vyenye meneno ya kuwagawa wananchi wa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Wapemba warudi kwao lakini serikali imekaa kimya na kushindwa kukemea jambo hilo ambalo linaweza kuhatarisha amani nchini. Endelea kusoma habari hii

Hoja ya Muungano yaifunika baraza

SUALA la Muungano limezidi kutawala mijadala katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huku baadhi ya wajumbe wakitamka wazi kuwa hawataki Muungano. Katika kikao hicho ambacho tayari kimepitisha bajeti kuu ya serikali ya Zanzibar wajumbe wa baraza hilo jana walijadili bajeti ya ofisi ya makamo wa pili wa rais wakitaka serikali isimamie kupata uhuru zaidi wa kiuchumi katika muungano. Ofisi ya makamo wa pili wa rais ndio inayotambulika kuwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali ndani ya baraza la wawakilishi. “Mheshimiwa Naibu Spika mimi niseme wazi kwanza kwamba sitaki muungano na katika kitu ambacho nakichukia sana basi ni huu muungano maana kwa miaka 48 ya muungano huu kila siku tunaambiwa kuna kero wala hazitatuliwi basi ni uvunjike tu” alisema Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma. Endelea kusoma habari hii

Walemavu wengi hawana ajira serikalini

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imekiri kukabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa ajira za watu wenye walemavu nchini. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Abdulhabib Ferej wakati akijibu masuala ya wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Chukwani Mjini Zanzibar. Waziri huyo alisema bado suala la ajira kwa watu wenye ulamavu ni changamoto kubwa inayoikabili serikali. “Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikiri mbele ya wajumbe wa baraza hili tukufu kwamba suala la ajira kwa watu wenye ulemavu ni changamoto kubwa katika taifa hili” alisema. Alisema katika kuona watu wenye ulemavu wanapata ajira, tayari ofisi yake ishawashasilisha ofisi ya rais, utumishi wa umma na utawala bora taarifa ya wale ambao kwa njia moja au nyengine wenye sifa na wataweza kuajiriwa katika wizara za serikali. Awali katika suala lake la msingi Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF) Mwanajuma Faki Mdachi alitaka kujua wizara ina mpango gani wa makusudi wa kuwaajiri watu wenye ulamavu kutokana na kuwepo kwa malalamiko kuwa hawapewi ajira serikalini licha ya kuwa na sifa zitahiki. Endelea kusoma habari hii. Endelea kusoma habari hii

Wananchi watakiwa kuwa makini

KAMATI ya kudumu ya baraza la wawakilishi ya kusimamia viongozi wakuu wa kitaifa imewashauri wananchi  kuwa makini na kusoma katiba za nchi wakati wakisubiri mchakato wa kutoa maoni yao katika tume ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ali Salum Haji aliyasema hayo wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi ambapo alisema wakati huu wa kutoa maoni ya katiba mpya ni muhimu kwa wananchi wote kwani katiba ndio msingi wa Taifa. “Tunawashauri wananchi wetu kuzisoma katiba zetu zote mbili na kujua mapungufu yaliopo ili kujua kile wanachokifanya wakati wa kutoa maoni yetu, lakini kamati yangu imegundua kuwa Wazanzibari wengi  hawaijui   Katiba zote ikiwemo hiyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa hali hiyo sijui tutegemee ni kipi watakachokuja kukichangia kwenye Tume ya Kukusanya Maoni Kuhusu Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano”. Alisema Haji. Endelea kusoma habari hii

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar irejeshwe

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar leo imesema kuwa matumizi ya neno Jamhuri ya Watu wa Zanzibar inawezekana ikiwa wazanzibari wengi watatoa maoni ya kulirejesha jina hilo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakari wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Landu aliyetaka kujua kwa nini jina hilo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar lilifutwa. Endelea kusoma habari hii

Matumizi ya fedha za serikali yachunguzwe

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wamesema Zanzibar inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi pamoja na changamoto za fedha kutokana na usimamizi mbaya wa fedha za serikali kutokana na kutodai haki kutoka serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Wakichangia bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013 wajumbe walisema upo udhaifu mkubwa katika usimamizi wa fedha za serikali katika wizara mbali mbali pamoja na muungano kutotendea haki Zanzibar. Mwakilishi wa Jimbo la Chakechake (CUF) Omar Ali Shehe alisema uchunguzi unaonesha kuwa fedha nyingi zinapotea kwa kuchukuliwa na watendaji wasiokuwa waaminifu huku serikali ikitafuta fedha kwa njia za kuongeza kodi. “Hakuna sababu kuongezea wananchi mzigo wa maisha kutokana na kupandisha kodi ambazo serikali ingeweza kuepuka. Kupandisha kodi ya mafuta maana yake ni kuleta mabadiliko ya mfumko wa bei nchini” alisema Shehe. Endelea kusoma habari hii 

Wawakilishi wataka uwiano katika Muungano

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wametaka uwiano sawa katika nafasi za juu za Muungano izingatiwe uteuzi wa wazanzibari ili kutoa haki sawa kwa pande zote mbili. Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wametoa kauli hiyo katika kipindi cha masuali na majibu ambapo walihoji kwa nini nafasi za majeshi na polisi zinashikiliwa na watu kutoka upande mmoja wa muungano peke yake.Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Salim Nassor Juma alisema kutokuwepo na uwiano katiak kushika nafasi za uongozi na nafasi nyeti katika utumishi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kero na inahitaji kushughulikiwa. Endelea kusoma habari hizi 

Hatutawavulia wanaopinga Muungano

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitawavumilia wanaharakati au kikundi chochote kinatakachohatarisha amani kwa kisingizio cha kupinga Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kutumia mihadhara na makongamano. Hayo yameelezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichomalizika juzi huko Chukwani Mjini hapa. Balozi Seif alisema Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar haitaki kupoteza amani na utulivu na kurejea katika vurugu na uhasama uliojengeka katika jamii kwa maika kadhaa. Napenda niweke wazi msimamo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitakivumilia kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa wananchi wetu” alisema Balozi Seif. Alisema serikali haiku tayari kurudishwa nyuma ambako wananchi waliishi kwa khofu kubwa huku chuki na uhasama zikiwa zimetanda miongoni mwao. “Hatutasita kuvizuwia vikundi vyovyote vinavyoendesha mihadhara au makongamano tutakayobaini yanahataridha usalama wan chi yetu. Na hili hatutakuwa na muhali na mtu yeyote Yule” alisema Balozi Seif wakati wa kufunga baraza . Endelea kusoma habari hii

Fungu Mbaraka ni mali ya Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba Kisiwa cha Fungu Mbaraka bado ni mali yake licha ya kuwepo kando ya Zanzibar. Kauli hiyo imetolewa jana aktika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini hapa kufuatia suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mwakajuni (CCM) Mbarouk Wadi Mussa Mtando aliyeka akujua kisiwa hicho ni mali ya nani kati ya Zanzibar na Tanzania bara.Waziri wa Ardhi, Makaazi na Nishati, Ramadhan Abdallah Shaaban aliwambie wajumbe wa baraza hilo kwamba ni kweli kisiwani hicho kipo mbali na Kizimkazi lakini tokea asili ni mali ya Zanzibar.“Fungu Mbaraka ni mali yetu na Zanzibar mwaka 1992 serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikwenda kuweka bendera yake hapo na hakuna hata mtu mmoja aliyeuliza kwa nini ikaweka bendera hapo, ingawa watu wanaweza kujitokeza wakasema ni mali ya upande wa pili kwa kuwa kipo mbali na Kizimkazi” alisema Waziri huyo.Kisiwa cha Fungu Mbaraka kipo katika bahari kuu Mashariki ya Zanzibar ambapo eneo la bahari kuu lote ni miliki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Endelea kusoma habari hii

Wajumbe waikataa ripoti ya serikali

BAADHI ya Wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wameikataa ripoti ya serikali kuhusu baraza la Manispaa ya Mji wa Zanzibar kutokana na ripoti kushindwa kukidhi haja na makudio ya uchunguzi. Wajumbe hao wamesema sababu kubwa ya kuikataa ripoti hiyo ni kutokana na kushindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kwa wajumbe wa baraza hilo jamboa mbalo awali wajumbe hao waliomba kamati teule ya baraza la wawakilishi inudwe ili kuchunguza ubadhirifu uliofanyika katika baraza la manispaa.Wakichangia katika kikao cha baraza la wawakilishi wajumbe hao walisema ripoti iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini imeshindwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya ubadhirifu mkubwa uliofanyika katika baraza hilo. Walisema ripoti iliyowasilishwa imeleelea mambo mengine na haijagusia suala la ubadhirifu na upotevu wa fedha uliofanyika wakati wajumbe walikuwa na hamu ya kutaka kujua fedha za serikali zinavyotumiwa vibaya na kutaka kuwajua wahusika wa upotevu huo.Endelea kusoma habari hii

Mswada wa utalii wapita kwa tabu

Mswada wa sheria ya utalii jana umepita kwa tabu baada ya wajumbe kutofautiana juu ya mswada huo kuhusu suala la upendelezo la ajira kwa wazanzibari.Wakati wajumbe wasiokuwa mawaziri backbenchers wakitaka ajira katika sekta ya utalii ibaki kuwa ya wazanzibari kisheria, mawaziri wengi walitaka pendekezo la serikali kuwa ni ajira iwe ni ya mtanzania. Wakishangia mswada wa marekebisho ya sheria ya utalii ambao uliwasilishwa na waziri wa habari, utalii, utamaduni na mcihezo, Abdillahi Jihad Hassan ilibidi upite kwa kura kutokana na wajumbe hao kutokukubaliana katika kifungu hicgo kinachosomeka kuwa. “Kifungu cha 23 b. (3) mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii aliyeajiri mtu ambaye sio Mtanzania kutoa huduma iliyoelezwa chini ya kifungu cha (1) cha kifungu hiki lazima apate ruhusa ya maandishi kutoka kwa waziri baada ya kumthibitishia waziri kuwa hakuna mtu wa ndani (Zanzibar) wa kujaza nafasi hiyo.” Endelea kusoma habari hii

Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo Zanzibar

Mhe Spika, kazi yetu ya uwakilishi ni ngumu sana kwani aliyeko nje humlaumu alieko huku ndani lakini miezi miwili tu akiingia humundani utamkuta analalamika kuwa anamaombi mengi lakini uwezo wa kuyatumia unakua ni mdogo, kwa hiyo waheshimiwa wenzangu tujitahidi kufanya kazi zetu kwa bidii ili kuiondoa hali hii na njia pekee ya kuliondoa tatizo hili ni kuibua miradi mikubwa ya kiuchumi hapa Zanzibar, tuendelee kushikamana kutafuta vianzio vipya vya mapato ikiwemo utafutaji na uchimbaji wa mafuta hapa Zanzibar, ili rasilimali hiyo ije kuwasaidia Wazanzibari wote kwa ujumla na Inshaallah Kwa uwezo wa Allah atatuwezesha kwa uwezo wake, pia tujitahidi kisimamia ukusanyaji wa mapato hapa Zanzibar ili yasivuje ili Mfuko wetu Mkuu wa Fedha za Serikali upate fedha za kutosha ili Serikali yetu iwe na uwezo wa kuwahudumia wananchi wetu kwa ujumla. Endelea kusoma hutuba hii

Hatimae mswada wa mafao ya vigogo wapita

Hatimae wajumbe wa baraza la wawakilishi leo walipitisha kwa sauti moja mswada wa sheria wa maslahi ya viongozi wa kisiasa baada ya mswada huo kukataliwa kupitishwa mara mbili na wajumbe hao.  Mswada huo ambao ulijadiliwa kwa hamasa kubwa ndani na nje ya baraza la wawakilishi una lengo la kuweka utaratibu wa kuwalipa maslahi viongozi baada ya kustaafu. Kupitishwa kwa mswada huo ambao hatua inayofuata ni rais wa Zanzibar kuutia saini na kuwa sheria kamili umetokana na serikali kusalim amri kwa madai ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kukosoa baadhi ya vipengele vya mswada huo.  Baadhi ya vipengele ambavyo serikali imevifanyia marekebisho ni pamoja na kufutwa kwa kifungu kilichokuwa kinazungumzia maslahi kwa washauri wa rais pamoja na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wa viongozi wa juu kuhudumiwa na serikali baada ya viongozi hao kustaafu. Kipengele chengine ni kile kinachohusiana na utaratibu wa ulipaji wa maslahi kwa viongozi wote bila ya kubagua pamoja na kukubaliana kwamba muda uliowasilishwa mswada huo haukuwa mwafaka.  Wakati wa kujadili mswada huo wajumbe wengi akiwemo Mwakilishi wa Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk na Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu kwa pamoja walikosoa msawada huo kwa kusema kuwa serikali inajitwika majukumu yasio na lazima wakati wananchi wengi pamoja an wafanyakazi wa serikali wakikabiliwa na maisha magumu. Endelea kusoma habari hii

Mswada wa mafao ya vigogo waondoshwa

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini ametangaza kuondowa mswada wa mafao na maslahi ya  viongozi wa kisiasa wastaafu akisema unahitaji kurudishwa tena katika kamati za baraza kwa ufafanuzi wa kina. Hatua hiyo ilizusha shangwe na furaha kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi zaidi wanaotoka katika majimbo ya uchaguzi ambao wakati wa wakijadili mswada huo walipinga vikali na kusema huu si wakati muafaka wa kuleta mswada huo kwani wananchi hawatoifahamu serikali yao. Endelea kusoma habari hii

Mswada wa rushwa wawasilishwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri amewasilisha mswada wa kuzuwia rushwa na uhujumi uchumi ambao lengo lake kubwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa vinavyodhoofisha maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii hapa Zanzibar. Kheri alisema Serikali imewasilisha mswada huo kutokana na kilio cha muda mrefu cha kutokuwepo kwa taasisi hiyo kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya Rushwa. Endelea kusoma habari hii

SMZ yatakiwa kutoa maelezo juu ya nyongeza ya masafa ya bahari

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kutoa taarifa katika baraza la mawaziri suala la Tanzania kuwasilisha ombi la nyongeza masafa ya bahari kuu kwenye Umoja wa Mataifa. Kificho alisema hivyo baada ya Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna kusema kwamba yeye kama wizara taarifa anayo hiyo lakini katika baraza la mawaziri hakuna taarifa ya jambo hilo iliyowasilishwa.“Nakuomba waziri mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna kuleta taarifa hiyo baraza la mawaziri kwa ajili ya kuifanyia kazi pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi” alisema Spika Kificho. Endelea kusoma habari hii

Rais atia saini miswaada mitatu- Spika

Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba tayari rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Sheni ametia saini miswaada mitatu iliyopitishwa na wajumbe hao katika kipindi cha Baraza la Wawakilishi kilichopita na sasa kuwa sheria kamili. Kificho alisema miswaada mitatu iliyotiwa saini na rais ni pamoja na mswaada wa kuanzishwa kwa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, mswaada wa kuanzishwa kwa shirika la taifa la biashara Zanzibar (ZSTC) pamoja na usanifu wa kuendesha mazao mengine na mswada wa kurekebisha baadhi ya sheria na kuweka kanuni za baraza. Endelea kusoma habari hii

Mswaada wa maslahi ya vigogo wapingwa tena

Mswada wa maslahi ya mafao ya viongozi wa serikali wastaafu ambao umewasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi umepata pigo baada ya wajumbe waliochangia kuukata na kusema haulengi kuweka usawa wa maslahi ya wananchi walio wengi. Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu akichangia mswada huo alisema kwamba umekuja katika wakati ambao haustahiki kwa sababu wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku huduma mbali mbali za maendeleo zikiwa duni. Endelea kusoma habari hii

JUSSA AIBUA TUHUMA NZITO

MWAKILISHI wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu ameibua tuhuma nzito juu ya Zanzibar kukoseshwa haki yake katika Muungano ya mapato yatokanayo na leseni za uvuvi wa bahari kuu.Mwakilishi huyo aliibua hoja hiyo jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa fedha 2011/2012 iliyowasilisha na waziri wa wizara hiyo Said Ali Mbarouk.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WACHACHAMAA

Mwakilishi wa Mgogoni Pemba, Abubakar Khamis Bakar (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Mjimkongwe Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jana wameipitisha kwa tabu hutuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati baada ya wajumbe wengi kutaka ufafanuzi wa kina na kauli ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya hatma ya mafuta na gesi asilia kutolewa katika orodha ya mambo ya Muungano.Endelea kusoma habari hii

SMZ YAPATA KIGUGUMIZI UDHAMINI WA POMBE

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar bado imekumbwa na kigugumizi kikubwa juu ya kuruhusu udhamini wa makampuni ya bia kuja kusaidia michezo ikiwemo mpira wa miguu visiwani Zanzibar.Akijibu maswali la wajumbe wa baraza la wawakilishi Naibu Waziri Habari, Utamduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis alisema kwa kifupi sana kwamba serikali imesikia maoni ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya suala hilo la kuruhusi wadhamini wa pombe lakini ushauri huo umeuchukua na serikali itaufanyia kazi.Endelea kusoma habari hii

WAJUMBE WATISHIA KUZUWIA SHILINGI

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwasilisha mswaada wa sheria ya kuanzisha Shirika la maendeleo ya petroli Zanzibar kwa ajili ya kusimamia utafutaji na uchimbaji wa mafuta Visiwani Zanzibar na kutishia kuzuwia shilingi kwa bajeti ya wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati.Karibu Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati wameitaka Serikali kufanyia kazi kilio cha wananchi kuhusu kuyaondoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano.Endelea kusoma habari hii

MAJIBU YA ICU NI YANGU-DUNI

WAZIRI wa Afya Juma Duni Haji amesema kwa mujibu wa kanuni za Baraza la Wawakilishi yeye kama waziri wa wizara hiyo, ndiye anayepaswa kulieleza Baraza hilotaarifa za wizara kwa niaba ya serikali.Endelea kusoma hii

ALI MZEE ATEULIWA

Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amemteuwa Ali Mzee Ali kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi kupitia nafasi kumi za rais kwa mujibu wa katiba.Endelea kusoma habari hii

 

MARUFUKU KUNYANYASA WAFANYAKAZI

Wizara ya kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika, Haroun Ali Suleiman amesema waajiri watakaowanyanyasa wafanyakazi katika sehemu za watachukuliwa hatua za kinidhamu kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mikataba ya kimataifa.Endelea kusoma habari hizi

 

ICU IPO HALI MBAYA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imekiri kwamba kitengo chake cha wagonjwa mahututi (ICU) kipo katika hali mbaya kutokana na uchakavu wa vifaa vyake kuwa ni va muda mrefu.Endelea kusoma habari hii

 

TOWENI MAONI YENU

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibarimesema kwamba wazanzibari wote watashirikishwa kikamilifu katika mchakato wa hatua za maandalizi ya katiba mpya inaoendelea kujadiliwa huku lengo likiwa maslahi ya Wazanzibari yanalindwa.Endelea kusoma habari hii

Zan ID LAWAMANI

WAJUMBE Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamehoji fungu kubwa lililotengwa kwa ajili ya Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Makaazi (Zan-ID) na utumiaji mbaya wa fedha za walipa kodi na urasimu unaofanywa na idara hiyo.Endelea kusoma habari hii

 

 

MKURUGENZI MANISPAA AWAJIBISHWE

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameliweka “kiti moto” Baraza la Manispaa Zanzibarkwa kutaka Mkurugenzi wake awajibishwe kwa kwa kuikosesha serikali mapato ya mamilioni ya fedha.Endelea kusoma habari hi

ZNZ YAKARIBISHA DIASPORA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarimefunguwa milango wazi kwa Wazanzibar waliopo nje ya nchi kuja nchini na kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa nchi na kuleta maendeleo zaidi kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisiasa ya amani na utulivu nchini.Endelea kusoma habari hii

WAZIRI ASHINDWA KUJIBU SWALI

NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Dk Sira Ubwa Mamboya jana alishindwa kujibu swali aliloulizwa na mjumbe ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi akisema suali hilokubwa kuliko uwezo wake wa kujibu na kulazimika Waziri wake kusimama na kujibu.Endelea kusoma habari hii

 

MADAWA YA KULEVYA NI TATIZO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej amesema tatizo la madawa ya kulevya pamoja na ukimwi ni janga la taifa ambapo jamii inatakiwa kupambana na kuliondosha tatizo hiloambalo linaharibu nguvu kazi ya taifa.Endelea kusoma habari hii

WATAKAOCHEZEA SUK KUKIONA

SERIKALI ya mapinduzi ya Zanzibarimesema kwamba itawachukuliya hatua za kinidhamu watendaji na viongozi wa serikali ambao wataongoza nchi kwa kuweka mbele utashi wa kisiasa kinyume na dhamira na malengo ya serikali ya umoja wa kitaifa.Endelea kusoma habari hii

MAONI YA WANANCHI YAHESHIMIWE

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema imekuwa makini katika kuhakikiisha rasimu mpya ya mswaada inatoa fursa kwa wananchi kuzungumza mambo yote muhimu yanayohusu Muungano bila ya vikwazo vyovyote.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotaka kujua suala zima la Muungano ambao ni kero kubwa kwa wazanzibari.Endelea kusoma habari hii

ZNZ HAINA SHERIA YA UCHUMBAJI MAFUTA

LICHA ya Zanzibarkutokuwa na sheria ya kuchimba mafuta wala haiwezi kutoa leseni kwa ajili ya kazi hizo, Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniahaijaizuilia Zanzibarkuchimba mafuta yake.Endelea kusoma habari hizi

 

SMZ ICHIMBE MAFUTA YAKE HAKUNA KUCHELEWESHA

BAADHI ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamesema wakati umefika kwa wazanzibari kutumia rasilimali zake za asili zilizopo nchini ikiwemo uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa lengo la kujikomboa kiuchumi.Endelea kusoma habari hii

MAONI KUHUSU BAJETI YA SMZ

BAJETI ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyowasilishwa juzi na Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee imekosolewa na baadhi ya wananchi na wanasiasa mbali mbali kwa kushindwa kukidhi haja kutokana na serikali kutopunguza gharama za maisha kwa kuzingatia hali ya wananchi wa kawaida kuwa ngumu na kushindwa kuweka wazi kima cha mishahara ya wafanyakazi huku wadau kulalamikia kutoshirikishwa katika uandaaji wa bajeti hiyo.Endelea kusoma bajeti hii nzima

BAJETI YETU NDIO HII HAPA

WAZIRI wa Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar, Omar Yussuf Mzee jana alisoma hutuba ya bajeti ya kuhusu mpango wa maendeleo na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza Juni 15 mwaka huu.Endelea kusoma habari hii

Uchumi sio suala la Muungano

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wazanzibari kuzungumzia kwa kina suala la uchumi liondolewe katika orodha ya Muungano wakati wa kuchangia rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha, Mipango na Uchumi Omar Yussuf Mzee wakati akijibu swali la nyongeza katika cha baraza la wawakilishi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, aliyetaka kujua kwa nini suala la uchumi kuratibiwa wa muungano wakati sio suala la Muungano.Endelea kusoma habari hizi

 

 

Umenifahamu babu Duni?

MWENYEKITI wa Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC) Omar Ali Shehe ameishauri serikali kupitia upya sheria za fedha na kupewa uwezo “meno” ikiwa ni hatua ya kupambana na ukiukaji wa matumizi ya fedha za umma katika taasisi za serikali.Ushauri huo umetolewa jana katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huko Chukwani Mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

WASAFIRI WATAKIWA KUWA NA CHETI CHA CHANJO

29 01 2011

KUANZIA sasa wasafiri wote wanaoingia Zanzibar watalaazimika kuwa na cheti kinachoonyesha wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa manjano. Nabu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya alisema jana kuwa uamuzi huo ni hatua ya kujikinga na tishio la kukumbwa na aina fulani ya ugonjwa wa homa ya manjano uliolipuka nchini Uganda.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR YAREHEMEWA KATIKA EAC

29 01 2011

LICHA ya kuwa chini ya mwavuli wa Muungano, Zanzibar imepewa nafasi maalum ya kushiriki katika vikao vya shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Baraza la Wawakilishi limeambiwa. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Zanzibar, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema nafasi hiyo imetoa nafasi hiyo inatoa fursa Zanzibar kuwakilishwa katika shughuli za kitaalam, ikiwa ni pamoja na za kuratibu vikao vikao vya jumuiya.Endelea kusoma habari hii

VIONGOZI WOTE WATAPEKULIWA ISIPOKUWA WATANO TU-SERIKALI

28 01 2011

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga marufuku matumizi mabaya ya uwanja wa ndege utaotumiwa na wafanyabiashara maarufu, mawaziri wastaafu na viongozi mbali mbali wanaotumia sehemu ya wageni mahsusi (VIP) na kukiuka sheria ya kukaguliwa.Kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar ni viongozi watano pekee ndio waliotajwa katika sheria hiyo kuwa wanaoruhusiwa kupita VIP bila ya kukaguliwa akiwemo rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rais, Jaji Mkuu na Spika wa Baraza la Wawakilishi.Endelea kusoma habari hii

 

MALINDI ITAKUWA BANDARI YA KIMATAIFA-SMZ

27 01 2011

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema ina lengo la kuifanya bandari ya Zanzibar kuwa inakidhi viwango vya kimataifa kuanzia mwezi Mie mwaka huu.Akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Makame Mbarouk Mshimba, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad alisema kazi ya kutafuta vifaa kwa ajili ya kuboresha huduma katika bandari hiyo imeanza. Alisema nia ya mpango huo ni kuiwezesha bandari hiyo kuwa na vifaa vyote kwa ajili ya huduma muhimu, vikiwemo vya uokozi wakati wa matukio ya ajali.Endelea kusoma habari hii

MSWAADA HAUJAKIDHI HAJA-WAJUMBE

27 01 2011

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamesema muswada wa sheria mpya ya utumishi wa umma uliowasilishwa ndani ya baraza hilo haujakidhi matarajio kwa kukosa mwelekeo katika suala la uimarishaji wa demokrasia na utawala bora nchiniMuswada huo uliwasilishwa jana katika kikao cha sita cha baraza hilo na Waziri wa Nchi, anayeshughulikia Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheri ambapo pamoja na mambo mengine muswada huo unakusudia kuanzishwa sheria ambayo itakuwa na sura ya kuwa chombo cha watumishi wa umma.Endelea kusoma habari hii

BARAZA WAFANYA MABADILIKO YA KANUNI

21 01 2011

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi Zanzibar wamefanya mabadiliko ya kanuni za baraza hilo ili ziweze kwenda sambamba na mabadiliko ya mfumo mpya wa serikai ya umoja wa kitaifa ulioundwa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka jana.Lengo la kubadilishwa kwa kanuni hizo kuendana na kutoa uhuru wa kutanua demokrasia lakini pia kanuni zinazotumika ni za muda mrefu ambapo tokea mfumo wa chama kimoja kabla ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi baraza hilo limekuwa likitumia kanuni hizo hizo.Endelea kusoma habari hii

SMZ KUFANYA TATHIMINI YA KUWALIPA MADIWANI

21 01 2011

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema bado inafanya tathmini kuweza kuwalipa mishahara madiwani wanaowatumikia wananchi katika majimbo mbali mbali ya uchaguzi kwa Unguja na Pemba.Hayo yalisemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Nchi Ofisi ya rais Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu swali la nyongeza aliloulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Chambani (CUF) aliyetaka kujuwa kwa nini Serikali imeshindwa kuwalipa Madiwani.Endelea kusoma habari hii

  

 TAKWIMU ZA KISUKARI ZINATISHA ZANZIBAR

21 01 2011

WIZARA ya Afya Zanzibar imekiri kuwepo idadi kubwa ya wagonjwa wa kisukari hapa Zanzibar jambo ambalo linaonesha ugonjwa huo kuwa ni tishio katika maisha ya wananchi wengi wa Unguja n Pemba.Naibu Waziri wa Afya Dk Sira Ubwa Mamboya aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin aliyetaka kujuwa hatari ya ugonjwa huo na kupelekea wagonjwa wengi kukatwa sehemu ya viungo vyao vya mwili.Endelea kusoma habari hii

 

BANDARI YA ZANZIBAR NI MAHIRI KULIKO BARA-HAMAD

20 01 2011

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wafanyabiashara wote kuondosha makontena ya mizigo katika bandari ya Malindi katika kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuchukuliwa hatua ya kupigwa mnada makontena hayo.Makontena hayo yanadaiwa kusababisha msongamano mkubwa katika bandari ya Malindi kutokana na wafanyabiashara hao kutokwenda kuyachukua makontena yao na kuyapakua mizigo.Endelea kusoma habari hii

BARAZA LA WAWAKILISHI KUANZA KESHO

18 01 2011

KIKAO Cha Baraza la Wawakilishi kinachosubiriwa kwa hamu na wananchi kinaanza kesho Mjini Zanzibar kikiwa kimewashirikisha mawaziri kumi na sita kutoka vyama viwili vya CCM na CUF.Kikao hicho ambacho kitakuwa ni cha aina yake kitafanyika katika jengo jipya la ukumbi wa baraza hilo liliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar lililojengwa chini ya ufadhili wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Tajiri mkuu kutoka Saudi Arabia Sheikh Ally Bin Youssuf.Endelea kusoma habari hii

UWAJIBIKAJI NDIO SILAHA YETU-MAKAMU WA PILI

 

13 11 2010

MAKAMO wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema nidhamu na uwajibikaji miongoni mwao ni silaha muhimu katika kufanikisha maendeleo ya Zanzibar.Balozi Seif alitoa changamoto hiyo katika hutuba yake ya kuliahirisha baraza la nane la Wawakilishi huko Mbweni Wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WATANO WAPELEKWA BUNGENI

13 11 2010

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana walifanya uchaguzi wa kuwachaguwa wawakilishi watano ambao watahudhuria katika Bunge la Jamhuri wa Muungano kupitia baraza hilo.Uchaguzi wa kuwachaguwa viongozi hao ulifanyika ndani ya Baraza hilo na kusimamiwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Ibrahim Mzee Ibrahim ambae ndie aliyekuwa Mkurugenzi wa uchaguzi huo ndani ya baraza la wawakilishi.Endelea kusoma habari hii

TUTAONDOKANA NA MFUMO TEGEMEZI-DK SHEIN

 13 11 2010

RAIS wa awamu ya Saba wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amesema kuwa Serikali yake chini ya Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inadhamira ya kuitoa nchi yao katika uchumi tegemezi na kuwa katika uchumi wao.Hayo ameyaeleza jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akilizinduwa Baraza la Nane la Wawakilishi huko Mbweni wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii


NAHODHA AWAAGA WAJUMBE WA BARAZA

12 08 2010

Shamsi Vuai Nahodha

WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) amewaaga Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huku akielekeza matumaini yake katika uundwa wa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu.Nahodha alizungumza hayo juzi na wajumbe wa baraza la wawakilishi Chukwani nje kidogo na mji wa Zanzibar ambapo alisema wakati akimaliza ngwe yake ya pili ya uongozi anararajia mfumo mpya wa serikali utakuwa na mafanikio makubwa ya kuleta mani nchini.Endelea kusoma habari hii

BARAZA LA WAWAKILISHI LAVUNJWA

11 08 2010

RAIS Amani Abeid Karume amelivunja baraza la wawakilishi na kuwataka wananchi wa Zanzibar kuweka historia ya kushiriki uchaguzi mkuu wenye matumaini ya kubeba amani na utulivu.Karume ameuasema hayo wakati akitoa hutuba yake ya mwisho katika kikao cha baraza la wawakilishi liliopo Chukwani Mjini Unguja.“Ndugu wananchi, leo nathubutu kusimama mbele yenu kwa sababu wananchi wa Zanzibar wametumia haki yao ya kikatiba ya kumchagua Rais wanaemtaka. Wakati napokea imani yenu kwa heshima na unyenyekevu kuwa Rais wa Zanzibar, sina budi kupokea wito wa wananchi wa kutaka mabadiliko” alisema.Endelea kusoma habari hii

MABADILIKO YA KATIBA YAPITA KWA SAUTI MOJA

10 08 2010

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi juzi usiku kwa sauti moja wamepitisha bila ya pingamizi marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.Chini ya marekebisho hayo mapya Zanzibar itajulikana kwa jina la serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya umoja wa kitaifa kufuatia wananchi kutaka mfumo wa serikali ya umoja baada ya kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo ilishinda kwa asilimia 66.4.Mbali ya kifungu hicho kifungu cha 2 cha katiba kisemacho “kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atashauriana na rais aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na baraza la wawakilishi” kimebadilishwa na kuwa.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI KUJADILI MABADILIKO YA KATIBA

9 08 2010

Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Idi Pandu Hassan

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi jana wamekutana na kujadili rasimu ya sheria ya mabadiliko ya katiba itakayowezeshwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 31 mwaka huu. Wajumbe hao walikutana katika jengo jipya la baraza la wawakilishi, mtaa wa chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar walieleza umuhimu wa kuzika tofauti zao za kisiasa zilizokuwepo tokea kuaznishwa kwa mfumo wa vyama vingi 1992 ili kujenga mustakabali mpya wa Zanzibar. Baadhi ya wajumbe hao wakiwa na hamasa ya kuzingumzia serikali ya umoja wa kitaifa ambayo majimbo 10 walipiga kura ya kuikataa walimwagia sifa nyingi rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakipendekeza wapewe tunzo maalumu ya kimataifa kuwashukuru.Endelea kusoma habari hizi.

MUNGU HAJATAKA NIWE RAIS-NAHODHA

16 07 2010

WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai

Shamsi Vuai Nahodha

Nahodha amekiri kushindwa katika kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kutokana na mipango ya Mwenyeenzi Mungu. Nahodha amesema kwa kuwa yeye hajafanikiwa kunyakua nafasi hiyo kitakachofuata ni kumuunga mkono mgombea aliyebahatika kuchaguliwa kwa kura nyingi Dk Ali Mohammed Shein ambaye ameteuliwa na chama chake.Waziri Kiongozi aliyasema hayo wakati akifunga kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichokuwa kikijadili na kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2010-2011 kwa takriban mwezi sasa.Endelea kusoma habari hii

KUNA CHANGAMOTO KATIKA MAKUZI YA WATOTO

13 07 2010

Aziza Nabahan Suleiman

KAMBI ya upinzani katika baraza la wawakilishi imesema kuna changamoto kadhaa zinazowakabili wanawake na watoto katika kuleta maendeleo visiwani Zanzibar.Hayo yanameelezwa na Waziri Kivuli wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanwake na Watoto, Aziza Nabahan Suleman alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani katika baraza la wawakilishi linaloendelea Mjini Unguja.Alisema kambi ya upizani hairishiwi na utoaji wa huduma za afya kwa watoto katika maeneo mbali mbali hasa katika vijiji vya Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii

WAPINZANI WAIPONGEZA SMZ KWA KUTEKELEZA AHADI

28 06 2010

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi kutoka kambi ya upinzani jana

Hamad Masoud Hamad

wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutekeleza na kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM ya 2005-2010 ipasavyo katika mradi yake.Wajumbe hao wameipongeza serikali katika miradi yake ikiwemo ule mradi mkubwa wa kukipatia umeme wa uhakika uliopita chini ya bahari kutoka Tanga Pemba ambayo umefandiliwa na serikali ya Norway.Waziri kivuli wa maji, ujenzi, nishati na ardhi, Hamad Masoud Hamad aliyasema hayo wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani katika Baraza la Wawakilishi.Endelea kusoma habari hii

 

MUUNGANO WETU NI IMARA BADO -SMZ

28 06 2010

Hamza Hassan Juma

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mesema licha ya kasoro zilizopo katika muungano wa Zanzibar na Tanganyika bado upo imara ukilinganishwa na nchi nyengine zilizoungana katika bara la Afrika.Waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi, Hamza Hassan Juma amesema hayo kw aniaba ya waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Muyuni (CCM) Ramadhan Nyonje Pandu katika kikao cha baraza la wawakilishi.“Pamoja na kasoro zinazojitokeza muungano wetu bado ni imara, vikao vyetu vya kutatua kero bado vinaendelea tutahakikisha hatua kwa hatua tunazipatia ufumbuzi kero zote kwa manufaa ya watanzania” alisema waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

WAPINZANI WATAKA UFAFANUZI WA MIRADI

28 06 2010

KAMBI ya Upinzani katika baraza la wawakilishi imetaka kupewa ufafanuzi wa miradi ya maendeleo katika wizara ya elimu na mafunzo ya amali kwa

Mohammed Ali Salim

kuwa katika kitabu cha bajeti haijaelezwa matumizi ya fedha za miradi hizo zimetumiwaje.Waziri Kivuli wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar, Mohammed Ali Salim aliyasema hao wakati akiwasilisha hutuba yake katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar kwa zaidi ya wiki tatu sasa.Alisema mradi wa ukamilishaji wa ujenzi wa makao makuu ya wizara ya elimu ya mwaka 2009/2010 ulitengewa shilingi 150,000,000 na fedha hizo zote zilipatikana lakini jambo la kushangaza katika bajeti ya mwaka huu fedha hizo zimeombwa kwa mradi huo huo.Endelea kusoma habari hii

 

WAFANYABIASHARA KATENI BIMA-SMZ

23 06 2010

Dk Mwinyihaji Makame

WAZIRI wa nchi ofisi ya rais anayeshungulikia Fedha na Uchumi Dk Mwinyihaji Makame Mwadini amewataka wafanyabiashara nchi kukata bima ili kuweza kulipwa fidia wakati wanapopata maafa au ajali mbali mbali.Mwinyihaji alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais Nassor Ahmed Mazrui (CUF) aliyetaka kujuwa wafanyabiashara ambao mizigo yao iliharibiwa vibaya kwa kusagwa na makontena katika bandari ya Malindi watalipwaje fidia.“Mizigo ya wafanyabiashara mbali mbali iliharibika vibaya katika Bandari ya Malindi baada ya kuangukiwa na makontena yaliyokuwa yamepangwa katika bandari hiyo lakini serikali ina mpango gani ya kurejesha gaharama hizo” aliuliza mwakilishi huyo.Endelea kusoma habari hii

CUF WASIKITISHWA NA VITAMBULISHO

23 06 2010

BAADHI ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamesikitishwa na jinsi idara ya vitambulisho vya ukaazi wa Mzanzibari ilivyowakosesha haki ya kupiga kura mamia ya wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Mwakilishi wa kuteuliwa na rais Juma Duni Haji (CUF) alisema hayo wakati akichangia bajeti ya wizara ya nchi afisi ya rais tawala za mikoa na vikosi vya SMZ kwa mwaka wa fedha 2010-2011 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.Duni alisema ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya mipango ya makusudi ya kuwakosesha wananchi wake haki za msingi ikiwemo kupiga kura katika uchaguzi mkuu.Alisema hadi sasa zaidi ya wananchi laki moja wamekosa kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya ukaazi wa mzanzibari kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwa mwaka huu hali ya kuwa kuwa ni kitambulisho ni haki kisheria.Endelea kusoma habari hii

VIKOSI VINA KAZI KUBWA-SMZ

23 06 2010

Suleiman Othman Nyanga

WAZIRI wa nchi afisi ya rais tawala za miko na vikosi vya serikali ya mapinduzi Zanzibar ina kazi kubwa ya kuhakikisha usalama katika nchi unaimarishwa.Hayo yameelezwa na waziri wa wizara hiyo, Suleiman Othman Nyanga alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 katika kikao cha barza la wawakilishi kinachendelea mjini hapa.Nyanga amelimba baraza la wawakilishi liwaidhinishie jumla ya shilingi 25,886,300,00 kwa kazi za kawaida na shilingi 2,210,000,000 kwa kazi za maendeleo.Alisema vikosi vyake vimekuwa vikitekeleza majukumu ikiwemo uzalishaji wa mali katika mwaka wa fedha wa 2009.2010 chuo cha mafunzo kiliweza kutekeleza malengo yake ya kilimo cha vipando mbali mbali.Endelea kusoma habari hii

TUTAPIGANIA HAKI YETU HADI MWISHO -SMZ

18 06 2010

WIZARA ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi imesema Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) halipo katika wakati mzuri na Shirika la umeme Tanzania Bara (TANESCO) kutokana na sababu mbali mbali.Hayo yameleezwa na Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee alipokuwa akioa ufafanuzi wa maswali mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi yalioulizwa na wajumbe hao Mjini Unguja.“Waheshimiwa wajumbe naomba muelewe kwamba TANESCO na ZEC hatuna good time lakini sisi tutajitahidi kudai haki yetu na tunaamini tutashinda na hili napenda mlijue nyinyi waheshimiwa wajumbe wa baraza hili tukufu” alisema Mzee.Endelea kusoma habari hii

SMZ YAKIRI MAKOSA YAKE BARAZANI

18 06 2010

Hamza Hassan Juma

KUTOHUDHURIA kwenye mikutano kwa mwenyekiti wa kamati ya maadili katika kamati za uongozi ni kasoro kubwa ambayo inapaswa kurekebishwa imeelezwa.Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ifisi ya waziri kiongozi, Hamza Hassan Juma aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja.Mwakilishi huyo alitaka kujua kwa kuwa kanuni za baraza la wawakilishi lina uwezo wa kuanzisha kamati mbali mbali zikiwemo kamati za kudumu ni kamati gani ya maadili ya baraza ni miongoni mwa kamati ya kudumu ya baraza.Endelea kusoma habari hii

 

UJENZI WA JETTY HUTOA AJIRA KWA WANANCHI

18 06 2010

WAZIRI wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa jetty unaofanywa na wawekezaji katika fukwe za bahari unachangia pato la taifa pamoja na kutoa ajira kwa wananchi wa aeneo husika.Waziri Samia aliwaeleza wajumbe la wawakilishi jana kufuatia swali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Matemwe (CCM) Ame Mati Wadi aliyaka kujua fadia zinazopatikana kwa serikali na wananchi katika ujenzi huo.“Kuruhusiwa kujengwa kwa jetty ni uharibifu wa mazingira lakini jengine lakini ujenzi huu unasaidia nini wananchi na kwa nini serikali iruhusu miradi kama hii wakati inakataliwa na wananchi wenye kuishi katika ukanda wa pwani?” amesema Wadi.Endelea kusoma habari hii

SMZ KUFANYA UTAFITI WA KIMAZINGIRA

18 06 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kufanya utafiti wa kina kabla ya kupitisha ujenzi wa barabara katika maeneo yenye misitu ili kuhifadhi mazingira.Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha aliyasema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali ya nyongeza kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi jana katika kikao kinachoendelea Mjini hapa.Nahodha alisema anashangazwa na wajumbe wanaosema kwamba kupitishwa kwa barabara katika msitu wa ngezi hakuwezi kuharibu mazingira na kwamba msitu hauna faida yoyote kwa taifa.Endelea kusoma habari hii

BAJETI YA SERIKALI YAPITA KWA KISHINDO

17 06 2010

KWAMARA ya kwanza bejeti ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imepitishwa kwa sauti moja bila ya kupigwa na wajumbe wote wa baraza wa waakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF waliomo katika baraza hilo.Hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoka kambi ya upinzania kukubali kuipitisha bajeti ya serikali tokea kuingia madarakani mwaka 2000 kwa rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika vipindi vyake vya uongozi. Kupitishwa kwa bajeti hiyo ya serikali na wawakilishi wa CUF kumefuatia maridhiano ya pande mbili kati ya rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad yaliofanyika novemba mwaka jana.Endelea kusoma habari hii

SUALA YA MAFUTA KUFANYIWA KAZI BARA

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa sasa analifanyia kazi suala la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutaka utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, imefahamika.Akisoma hotuba ya bajeti ya Ofisi yake jana katika Baraza la Wawakilishi, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha aliwaambia Wajumbe kwamba tayari ameshamwandikia barua Waziri Mkuu kumjulisha suala hilo .“Nimeshamwandikia Waziri Mkuu kuhusu mapendekezo ya Zanzibar juu yakuondolewa kwa suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano” Alilimbia Baraza Waziri Kiongozi.Nahodha alisema kwamba Waziri Mkuu, Pinda kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanalifanyia kazi kwa pamoja.Endelea kusoma habari hii

 

WANANCHI WASHAJIISHWA KUPATA MIKARAFUU

17 06 2010

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar imesema imeanza kushajiisha wakulima kupanda mikarafuu mipya ili kuendeleza zao hilo katika visiwa vya Unguja na Pemba.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Khatib Suleiman Bakari aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea kwa takriban wiki mbili sasa Maisara Mjini Zanzibar. “Mheshimiwa Spika wizara yangu imeliona shauri hilo la kushajiisha wakulima wa mikarafuu na kufikiria kuanzisha utaratibu wa kuwapa zawadi kwa wale wote wakulima watakaofanya vizuri” alisema naibu waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WAHOJI UKUSANYAJI WA MAPATO

17 06 2010

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi Zanzibar wamehoji utaratibu

Said Ali Mbarouk

unaotumiwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii wa kukusanya fedha za maegesho ya magari na kuzitumia kinyume na sheria za ukusanyaji wa mapato nchini.Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF) Said Ali Mbarouk katika suala lake la nyongeza alitaka kujua sheria ipo inayompa mamlaka waziri wa afya kukusanya mapato na kuyatumia bila ya kupeekwa katika mfumo wa hazina ya serikali ambao ndio yenye mamlaka hiyo.“Sheria ya kukusanya kodi ipo kwa mujibu wa sheria na sheria hiyo imeeleza namna ya matumizi ni sheria gani iliyompa mamlaka waziri kutumia fedha za makusanyo ya maegesho ya magari na kuyatumia bila ya kupitia mfuko wa hazina” alihoji Mbarouk.Endelea kusoma habari hii

 

VIBAJAJI MARUFUKU ZANZIBAR

17 06 2010

Mzee Ali Ussi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema bado haijaruhusu kutumika kwa usafiri wa vibajaji kuchukulia abiria visiwani Zanzibar na kupiga marufuku daladala zenye maringi manne.Hayo yamelezwa na Waziri na Nchi Afisi ya Rais, Mawasilino na Uchukuzi, Machano Othman Said alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali mbali mbali yalioulizwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi Mjini Zanzibar.Alisema licha ya kuwa vibajaji vimeruhusika upande wa Tanzania bara kupakilia abiria lakini kwa kuwa mamlaka za usafiri ni tofauti na hasa kwa kuzingatia ni nchi mbili tofauti hivyo upande wa Zanzibar ni marufuku kutumia usafiri huo.“Wenzetu wao wameruhusu mpaka vibajaji kuchukua abiria lakini sisi hatujaruhusu bado maana tukiviruhusu viajaji kuingia mjini itakuwa balaa kubwa hasa kwa mji wetu huu” alisema waziri Said.Endelea kusoma habari hii

TUNA TAARIFA YA WAWEKEZAJI WAZALENDO- SMZ

16 06 2010

SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema ina taarifa kamili juu ya

Samia Suluhu Hassan

wawekezaji wazalendo kadhaa wa Zanzibar ambao bado hawajapatiwa hati za matumizi ya ardhi kutoka wizara inayosimamia ardhi kwa mujibu wa sheria.Hayo ameelezwa na Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua tatizo gani liliopelekea kukwamisha kutolewa kwa hati hizo.“Ni kweli taarifa tulizonazo ni kuwa wawekezaji mbali mbali wa Unguja na Pemba kuwa bado hawajapatiwa hati za matumizi ya ardhi kutoka wizara inayosimamia ardhi kwa mujibu wa sheria yetu” alisema Samia.Endelea kusoma habari hii

 

KITUO CHA MAGARI MICHAKAENI HAKIFAI-WAJUMBE

16 06 2010

Abubakar khamis Bakari

BAADHI ya Wajumbe wa baraza la wawakilishi wanaotokea Kisiwani Pemba wameikatalia serikali juu ya kujengwa kituo cha daladala katika eneo la Michakaeni ambalo ni mbali na Mji wa Chake Chake.Wawakilishi hao walisema serikali lazima ichague sehemu mzuri ya kuweka kituo hicho kwa kuwa sehemu ambayo imependekeza kuwekwa in umbali wa zaidi ya kilomita mbili na nuru kutoka madukani.Mwakilishi wa mwanzo kukataa suala hilo Mwakilishi wa jimbo la Mgogoni (CUF) Abubakar Khamis Bakari ambaye alisema Mava ya Mbarouk eneo la Michakaeni lillochaguliwa na serikali kujengwa kituo cha daladala ni mbali sana na mji wa chake chake hivyo wananchi itawawia vigumu kufika madukani hasa wagojwa na watu.Endelea kusoma habari hii

 

SINA FUNGU LA MAAFA –NAHODHA

16 06 2010

WAZIRI Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amesema ofisi yake haina fungu maalumu la bajeti zilizotegwa kwa ajili ya

Shamsi Vuai Nahodha

maafa yanatokea.Nahodha alisema hayo mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe hao waliotaka kujua utaratibu gani unaotumika katika kutoa fedha za kuwasaidia watu wanaofikwa na maafa mbali mbali yakiwemo ya mvua.“Mara nyingi tunapofikwa na maafa kama ya mvua au mengineyo huwa tunaomba fedha katika mfuko mkuu wa serikali na huo ndio utaratibu tunaoutumia kwa sasa nakumbuka wajumbe mnalitambua hilo kwamba hatuna fungu letu katika bajeti iliyopita” alisema Nahodha.Endelea kusoma habari hii

 

UTEKAJI NYARA MELI NI TATIZO LA KIMATAIFA-SMZ

16 06 2010

Machano Othman Said

SUALA la utekaji nyara na uvamizi wa meli katika ukanda wa bahari ya hindi linaelezwa kuwa ni tatizo la dunia nzima na sio Afrika Mashariki pekee.Hayo yameelezwa na waziri na nchi afisi ya rais maasiliano na uchukuzi, Machano Othman Said alipokuwa akijibu maswali mbali mbali ya nyongeza ya wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Mjini Zanzibar.Alisema suala la utekaji nyara meli na maharamia wa kisomali ni suala la kimataifa na linahitaji msaada kubwa kati ya nchi husika na nchi wahisani kwa kuwa katika sa hivi karibuni chi nyingi zimekuwa zikifikwa na mkasa wa kuvamiwa na kwa meli zinazopita katika bahari kuu.Endelea kusoma habari hii

 

ZNZ IUUNDE MAMLAKA YAKE YA MAPATO – WAJUMBE

16 06 2010

Nassor Ahmed Mazrui

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wameishauri serikali ya mapinduzi Zanzibar kuanzisha mamlaka yake ya mapato na kuacha kutumia mamlaka ya mapato ya Tanzania kutokana na kuwa chumi mbili tofauti.Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa kuteuliwa na rais, Nassor Ahmed Mazurui (CUF) alipokuwa akichangia bajeti ya serikali ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.Mazurui alisema kuna kila sababu serikali kuchukua uamuzi wa kuunda mamlaka ya mapato Zanzibar (ZRA) badala ya kutumia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa uchumi wa Zanzibar na uchumi wa Tanzania ni tofauti hivyo viwango vya ushuru haviwezi kuwa sawa.Endelea kusoma habari hii

  

HUDUMA YA BENKI ZIIMARISHWE PEMBA-SHAALI

16 06 2010

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wameitaka serikali ya mapinduzi ya

Haji Faki Shaali

zanzibar kuharakisha kufikisha huduma za kibenki vijijini huko Pemba kwa ajili ya kupunguza umasikini.Hayo yalisemwa na mwakilishi wa jimbo la Mkanyageni (CUF) Haji Faki Shaali wakati akichangia bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2010/2011 hapo katika baraza la wawakilishi mjini hapa.Alisema inashangaza sana kuona baadhi ya taasisi za kinenki hazipo katika kisiwa cha Pemba na hivyo kudumaza huduma za jamii na uchumi kwa wananchi kisiwani humo.Endelea kusoma habari hii

 

DOA ZA MKEKA NI TATIZO -SMZ

16 06 2010

Hija Hassan Hija

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba ndoa za mkeka ni tatizo kubwa linalowakabili wananchi wengi ambalo husababisha kuporomoka kwa maadili ya dini ya kiislamu visiwani ZanzibarWaziri wa nchi ofisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhan Abdallah Shaaban aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja aliyetaka kujuwa mazingira ya ndoa za mkeka na madhara yake yanayopatikana katika jamii hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya maadili ya kiislamu yanaporomoka.Mwakilishi huyo alisema utafiti unaonesha kwamba ndoa nyingi zinazofungwa mara nyingi hazidumu na hata watoto wanapatikana huwa wanatekezwa na wazazi wao hasa wa kiume hivyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kupunguza tatizo hilo.Endelea kusoma habari hii

 

HUDUMA ZA AFYA NI MBOVU -WAJUMBE

16 06 2010

BAADHI ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wameishauri serikali ya

Makame Mshimba Mbarouk

mapinduzi Zanzibar kutupia jicho katika sekta ya afya na ustawi wa jamii kutokana na kukosekana vifaa muhimu na huduma mbovu zinazotolewa katika hospitali zake.Wajumbe hao walikuwa wakichangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 katika kikao cha baraza la wawakilishi ambapo baadhi yao walitaka hospitali kuu ya mnazi mmoja isiitwe hospitali ya rufaa kutokana na kukosekana na vigezo vya jina hilo.Akichangia hutuba hiyo iliyowasilishwa wiki iliyopita na waziri wa nchi afisi ya rais fedha na uchumi Dk Mwinyihaji Makame, mwakilishi wa jimbo la Kitope (CCM) Makame Mchimba Mbarouk alisema hospitali na mnazi mmoja haiwezi kuitwa ya rufaa kwa kuwa haina kigezo cha kuitwa hivyo.Endelea kusoma habari hii

 

KERO ZA MUUNGANO ZAPATIWA UFUMBUZI

16 06 2010

Ramadhani Abdallah Shaaban

WAZIRI wa nchi afisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhan Abdallah Shaaban amesema baadhi ya kero za muungano tayari zimeshapatiwa ufumbuzi kupitia vikao vya kamati ya pande mbili za muungano.Alisema jumla ya mambo tisa yaliwasilishwa katika vikao hivyo ambayo yanashughulikiwa ni pamoja na ushiriki wa Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki, utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje na ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za muungano.Mambo mengine ni mgawanyo wa mapato yatokanayo na misamaha kutoka nje ya nchi, misamaha ya mikopo ya fedha kutoka IMF, faida ya benki kuu, uwezo wa SMZ kukopa ndani na nje ya nchi, na hisa za serikali ya Zanzibar zilizokuwa katika bodi ya sarafu ya Afrika Mashariki.Endelea kusoma habari hii

 

SERIKALI UCHAMBUE MAFANIKIO UPINZANI

16 06 2010

KAMBI ya upinzani katika baraza la wawakilishi Zanzibar imesema ipo haja kwa serikali kuonesha mafanikio yaliopatikana katika kipindi kilichopita

Said Ali Mbarouk

katika sekta za utalii na kilimo kwa kuyaeleza kwa kina katika bajeti yake ya mwaka huu.Hayo yameelezwa na waziri kivuli wa wizara ya nchi katiba na utawala bora, Said Ali Mbarouk alipokuwa akiwasilisha hutuba yake jana katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar.Alisema hotuba ya bajeti ya mwaka huu wa fedha umeleza kuwa serikali imepata mafanikio makubwa na kutoa mifano ya kumekuwa na ongezeko la uimarikaji wa miundo mbinu, kuanzishwa kwa shule za wakulima, kuanzishwa kwa miundo mbinu ya mabonde ya umwagiliaji maji, kununuliwa mtambo mpya wa “Liquid nitrogen.”, kutoa vifaa na maboti ya uvuvi, kutembelewa na watalii 134,954 na Kuwepo hoteli 23 zenye hadhi ya nyota 4 na 5.Endelea kusoma habari hii

 

MJUMBE AHOJI KIGEZO CHA ADA

15 06 2010

Ali Abdallah Ali

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kigezo kilichotumika kuongeza ada ya fedha za wagombea wa nafasi mbali mbali kinatokana na kushuka thamani kwa fedha za Tanzania.Waziri na nchi afisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhani Abdallah Shaaban aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi lliloulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua kigezo kilichotumika kuongeza bei za wagombea wa urais, uwakilishi na udiwani.Waziri Shaaban alizitaja sababu nyengine zilizopelekea kuongeza bei ni pamoja na uzito wa dhamana za mgombea husika kwa nafasi anayoomba,na kiwango cha dhamana kilifikiwa baada na ZEC kukaa na wadau wake wa vyama vya saisa na kukubaliana.Endelea kusoma habari hii

KILIMO YAANZISHA DARASA KWA WAKULIMA

15 06 2010

WIZARA ya kilimo, mifugo na mazingira imesema imeanzisha elimu kwa

Burhani Haji Saadat

wakulima ili waachane na kilimo cha misitu na badala yake iindeleze kilimo cha maweni ili kunusuru misitu na kulinda mazingira.Naibu waziri wa kilimo, Khatib Suleiman Bakari amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu maswali ya nyongeza kuhusiana na kilimo cha maweni ambacho kimeelezwa kuwa kina faida kubwa.Alisema wizara ya kilimo ina mikakati ya kukuza kilimo cha maweni miongoni mwa mikakati hiyo ni ile ya kutoa huduma ya elimu kwa wakulima kupitia shule za wakulima.Endelea kusoma habari hii

WIZARA YA AFYA KUONGEZA WAFANYAKAZI

15 06 2010

Sultan Mohammed Mugheiry

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imesema inaedelea na jitihada za kuongeza idadi ya wafanyakazi wa kada za afya wakiwemo wauguzi katika hospitali za Pemba.Aidha wizara hiyo imesema ipo katika mchakato wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa wizara hiyo na kuwaajiri baadhi yao kadiri ya mahitaji na uwezo unavyoruhusu.Waziri wa wizara hiyo, Sultan Mohammed Mugheiry aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba baada ya kurekebisha maslahi itawaajiri wafanyakazi wengine na madereva wa wizara hiyo.Mugheiry alikuwa swali la nyongeza lililouliza wizara ina mkakati gani wa kuboresha wiraza hiyo kutokana na kuwa sababu moja ya kuwafanya wafanyakazi wadumu na wawe na ufanisi katika kazi ni kuwa na maslahi bora.Endelea kusoma habari hii

 

 

WAZANZIBARI WACHENI MUHALI-WAZIRI

15 06 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wananchi kuacha utamaduni wa kuoneana muhali na badala yake watoe ushirikiano kwa polisi katika

Ramadhani Abdallah Shaaban

kutoa ushahidi mahakamani. Waziri na nchi afisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhan Abdallah Shaaban aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kukataa kutoa ushahidi wanapoitwa mahakamani.Waziri huyo alisema mhalifu anapokamatwa na polisi kwa tuhuma yoyote ile ni lazima ufanyike uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma zinazomkabili na baada ya upelelezi kukamilika ushahidi uliopatikana lazima uwe wa kutosha kuweza kuthibitisha kosa pasi na kuacha shaka.Endelea kusoma habari hii

BARABARA ZOTE ZANZIBAR KUTENGENEZWA-SMZ

15 06 2010

Machano Othman Said

WIZARA ya Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar imewaahidi wananchi kwamba baada ya muda mfupi barabara zote za Unguja na Pemba zitakuwa zimetengenezwa katika kiwango cha lami.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Mawasiliano na Uchukuzi, Machano Othman Said alipokuwa akijibu maswali mbali mbali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.“Zanzibar nzima tunataka iwe na barabara za lami na baada ya muda mfupi tu kazi hiyo itakamilika lakini katika mwezi mmoja mtaona mabadiliko makubwa hasa katika barabara zetu hizi za mjini” alisema waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

BAJETI YA DEMOKRASIA NA MAENDELEO-SMZ

9 06 2010

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema pato la taifa

Dk. Mwinyihaji

linatarajiwa kukuwa kutoka asilimia 6.7 mwaka jana hadi kufikia asilimia 7.3 mwaka huu huku mfumko wa bei ukitarajiwa kudhibitiwa na kubaki katika asilimia 7.8.Aidha serikali imetangaza kupandisha pencheni ya wastaafu kutoka 15,000 hadi 25,000 katika mwaka huu wa fedha huku waziri akiahidi kuimarisha hali ya wafanyakazi wa serikali baada ya marekebisho ya utumishi serikali unaoendelea hivi sasa.Hayo yameelezwa na wakati wa kusomwa mwelekeo wa bajeti ya serikali ya mapinduzi Zanzibar, ya mwaka wa fedha wa 2010/2011,waziri wa nchi ofisi ya rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini katika kikao cha baraza la wawakilishi mjini unguja.Endelea kusoma habari hii

KUWEKA MISHAHARA BENKI NI KUEPUSHA WIZI

9 06 2010

Khamis Jabir Makame

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema uamuzi wa kuingizwa mishahara ya wafanyakazi benki unatokana na kuepusha mambo mbali mbali ikwemo wizi na uporaji unaoweza kufanywa na wau waovu.Waziri wa elimu na mafunzo ya amali, Khamis Jabir Makame aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Amani (CCM) Ali Denge Makame aliyetaka kujua sababu gani za serikali kuwalazimisha wafanyakazi kutumia benki wakati suala hilo ni uamuzi binafsi wa mfanyakazi mwenyewe.Mwakilishi huyo alisema wizara ilitoa agizo kwa walimu wa shule za mjini kufungua akaunti benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na kuwataka kuchukulia fedha zao za mishahara benki wakati PBZ yenyewe haijajiandaa vyema kukabiliana na kundi kubwa la wateja jambo ambalo husababisha ufumbufu mkubwa kwa wateja wao.Endelea kusoma habari hii

TATIZO LA WADUDU WA EMBE NI LA AFRIKA MASHARIKI

9 06 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema wataalamu wa kilimo

Shamsi Vuai Nahodha

wamegundua dawa ya kuulia wadudu wanaosumbua mazao kwa kuchanganya aina ya matunda ya kungumanga na karafuu yanayopatikana visiwani Zanzibar.Hayo yameelezwa na waziri kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maswali ya wajumbe wa baraza la waakilishi lililoanza jana Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Wajumbe hao walitaka kujua serikali inafanya nini juu ya nzi wa embe ambao wamekuwa kero kwa wakulima kutokana na kushambuliwa na wadudu hao katika mazao yao. Waziri kiongozi alisema serikali itachukua juhudi maalumu za kuhakikisha wanatafuta dawa na matatizo ya wadudu wenye kuharibu mazao wanadhibitiwa ipasavyo.Endelea kusoma habari hii

TUTASIMAMIA UCHAGUZI HATA KWA FEDHA ZETU-SMZ

8 06 2010

Dk Mwinyihaji Mwadini

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) itahakikisha kura ya maoni na uchaguzi mkuu unafanyika hata bila ya fedha za wahisani.Kauli hiyo imetolewa jana na waziri wa nchi afisi ya rais fedha na uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alipokuwa akitoa muhrasari wa bajeti ya mwaka wa fedha ya 2010/2011 inayotarajiwa kusomwa kesho mjini Zanzibar.Dk Mwinyihaji alisema mafaniko ya kura ya maoni na uchaguzi ni miongoni mwa mipango ya serikali kwa mwaka ho wa fedha ili kujenga demokrasia ya kweli na utawala bora ndani ya Zanzibar.“Tumejiandaa hata kama wafadhili watachelewesha au kutotoa misaada kwetu sasa hivi ujenzi wa demokrasia ni vitu muhimu katika maendeleo ya nchi, natoa wito kwa watu wote mashirika na umma na taasisi binafsi katika harakati hizi za kujenga taifa” alisema bila ya kutaja kiwango cha fedha ambacho serikali imetenga kwa ajili ya chaguzi hizo.Akielezea muelekeo wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2010-2011, Mwinyihaji alisema kwamba hali ya uchumi mwaka ujao wa fedha natarajiwa kuimarika zaidi kwa kuzingatia maeneo yaliopewa msisitizo mfano kuimarisha afya ya jamii, elimu bora na ujenzi wa makazi bora.Endelea kusoma habari hii

WAENEZAJI SIASA CHAFU WAKEMEWA

3 04 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewakemea baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya siasa wanaopita majimboni kueneza siasa chafu dhidi ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya baadhi ya wanachama na viongozi wa chama cha mapinduzi kudaiwa kupita majimboni na katika matawi mbali mbali kuwataka wananchi wasikubali kupiga kura ya ndio wakati wa kuanzishwa mchakato wa kutafuta maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini.Akifunga baraza la wawakilishi, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha alisema wapo baadhi ya waumini wa vyama vya siasa wanatumia sera za vyama vyao lakini inapokuja suala la mamuzi huwa hawakubaliani na maamuzi ya sera katika vyama hivyo jambo ambalo alisema ni baya kwa kuwa linasababisha unafiki katika nafsi.Nahodha alitoa mfano wa muumini mmoja ambaye licha ya kuwa ni msomi lakini hawakuwa anaamini alichokisoma na matokeo yake alishindwa na mwanafunzi wake ambaye aliamini na kutekeleza kile kilichomo moyoni mwake.Alisema lazima sera na vitendo viende sambamba katika utekelezaji na haiwezekani mtu kusema jambo ambalo moyoni mwake haliamini kwa kuwa linaweza kumsababishi matatizo katika maisha yake na jamii kwa ujumla.Endelea kusoma habari hii

WAVUVI HARAMU WACHUKULIWE HATUA

31 03 2010

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wameitaka serikali kuwachukulia hatua wavuvi wanaondesha uvuvi haramu ambao umepigwa marufuku kutokana na kuharibu viumbe vya baharini na kuharibu rasilimali za bahari.Ushauri huo umetolewa na wajumbe mbali mbali wakati wakichangia mswaada wa uvuvi na kuweka masharti bora yanayohusiana na usimamizi na maendeleo ya uvuvi ndani ya Zanzibar na mambo yanayohusiana na hayo.Mwakilishi wa viti maalumu (CUF) Mwajuma Faki Mdachi alisema alisema hivi sasa kumejitokeza wavuvi wanaonedesha uvuvi haramu kwa kutumia mitego ambayo imerkuwea ikiharibu maziniora ya baharini.Alisema elimu kuhusu aina ya uvuvi wa baharini kwa sasa inatakiwa itolewe ili wavuvi waweze kufahamu na kujuwa ni aina ipi ya uvuvi ambao haufai kwa matumizi ya baharini.Mwakilishi wa jimbo la Chake Chake (CUF) Omar Ali Shehe alisema mswada huo umekuja wakati muafaka kwa ajili ya kupambana na uvuvi haramu katika maeneo ya ukanda wa bahari Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii

KURA YA MAONI YAPITA KWA KISHINDO ZANZIBAR

30 03 2010

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi kwa sauti moja wamepitishwa mswaada uliojadiliwa kwa siku mbili mfuilulizo juu ya kura ya maoni kwa ajili ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.Licha ya mswaada huo kupitishwa sauti moja lakini baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wamekwepa kuuchangia kabisa mswaada huo kwa madai ya kuogopa kuwachanganya wananchi na kuhofia kukosa nafasi katika majimbo yao ya uchaguzi ambayo yana upinzani mkali dhidi ya chama cha wananchi CUF.Mswaada huo umechangiwa na wajumbe 29 huku wajumbe tisa wakichangia kwa maandishi na wengine saba waliomba kutaka kuchangia lakini kutokana na muda hawakupata nafasi ya kuchangia.Ni mwakilishi mmoja pekee wa jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali ndiye aliyesimama na kuchangia mswaada huo huku mawaziri na wawakilishi wateule wa rais wa Zanzibar Amani Karume wakiinuka na kuuchangia bila ya khofu huku wakiwataka wenziwao kuacha woga wa kutoa maoni yao kwa kuwa kitendo cha kuchangia mswaada huo ni muhimu kwa maslahi ya umma.Akitoa mchango wake Mwakilishi huyo wa Kwahani alisema ni muhimu kupigwa kura ya maoni na elimu juu ya umuhimu wa seriakli ya pamoja klutolewa ili wananchi waelewe kwani wananchi wengi hadi sasa hawajafahamu umuhimu wa serikali hiyo inayotoka kuundwa.Endelea kusoma habari hii

CCM WATAKIWA KUUNGA MKONO MARIDHIANO

29 03 2010

MAWAZIRI wawili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wametaka makada wenzao wa CCM wawe mstari wa mbele katika kuunga mkono mpango wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar ulioanzishwa na Rais Amani Abeid Karume. Mawaziri Haroun Ali Suleiman na Machano Othman Said walitoa rai hiyo jana wakati wa majadiliano ya muswada wa sheria wa kuwepo kwa kura ya maoni Zanzibar uliowasilishwa Baraza la Wawakilishi jana. Haroun ni mwakilishi wa jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wakati Machano ni Waziri wa Nchi, Mawasiliano na Uchukuzi, akiwakilisha jimbo la Chumbuni, Wilaya ya Magharibi, Unguja. Akichangia muswada uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, Haroun alisema hoja ya kura ya maoni ni muhimu sana kwa mustakbali wa nchi kwa hivyo ni jukumu la kila kiongozi kuiunga mkono. Huku akimsifia Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza, Haji Omar Kheir kwa kueleza vizuri umuhimu wa muswada huo, Waziri Haroun alisema ni muhimu kila mwakilishi na viongozi wengine Zanzibar kuchukua msimamo ambao hautasababisha kuirudisha nchi nyuma.Endelea kusoma habari hii

MWENYE MAWAZO YA KULETA AMANI AJE-SMZ

30 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kama yupo mtu anahisi anayo njia sahihi zadi ya kuleta amani na umoja visiwani Zanzibar serikali inamkaribisha mtu huyo kufanya hivyo na suala lake litapokewa na kufikiriwa.Hayo yameelezwa na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha katika hutuba yake ya kufunga mkutano wa 18 wa baraza la wawakilishi uliochukua takriban wiki mbili Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Hata hivyo Nahodha alisema wapo baadhi ya watu walitilia shaka maridhiano hayo lakini mwisho wa yote wamekubaliana kwamba jambo la msingi linalotafutwa na kurejesha hali ya amani na utulivu wa wananchi wote bila ya ubaguzi.“Najua wapo watu watakaotilia shaka jambo hili lakini mwisho wake sote tukubaliane kuwa maridhiano ya kutafuta amani ni jambo jema. Na kama yupo mtu anahisi anayo njia sahihi zaidi ya kuleta amani na umoja basi anaweza kuipendekeza na sisi tutaitafakari safari yetu ni moja lakini njia za kutufikisha tunakokwenda zinaweza kuwa ni nyingi” alisema Nahodha. Endelea kusoma habari hii

HOJA BINAFSI YAPITA KWA SAUTI MOJA

30 01 2010

HATIMAE Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeidhiria hoja ya kuundwa kwa serikali ya kitaifa kufanyika kabla ya uchagguzi mkuu wa 2010.Hoja hiyo liyowasilishwa na kiongozi wa kambi ya upinzani Abubakar Khamis Bakari na inayotaka kuundwa kwa serikali hiyo ili kujenga umoja na marishiano kwa wazanzibari ambayo wamekuwa katika migogoro ya kisiasa kwa muda mrefu.Wajumbe wa baraza hilo wote kwa sauti moja wamekubaliana na suala hilo kwa kuridhia baaada ya Baraza la Wawakilishi kuwasilisha mapendekezo ya hoja binafsi ya Chama Cha Wananchi CUF na kujadiliwa na Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mgogoni Pemba.Hata hivyo kabla ya kufanyika kwa mabadiliko hayo Chama cha CUF kilikubali kufanya mabadiliko katika hoja zake kadhaa baada ya Wajumbe wa CCM kutaka kufanyiwa mabadiko hayo ya hoja yake.“Marekebisho ya sheria ya uchaguzi, hatua ya kutaka ridhaa ya wananchi kwa njia ya kura ya maoni, na maekebisho ya katiba endapo wananchi wataridhia uanzishwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, yote hayo yafanywe kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010” imesema kipengele hicho ambacho kimekubaliwa na wote.Endelea kusoma habari hii

WAJUMBE BADO WAVUTANA KUHUSU MSETO

30 01 2010

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi bado wanaendelea kuvutana kutokana na msimamo yao tofauti kuhusiana na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar huku mjumbe mwengine akitaka kurudi katika mfumo wa chama kimoja.Wakati wajumbe kutoka chama cha wananchi CUF wanapendekeza kuundwe kwa serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ili kuweka mazingira mazuri ya kuaminiana kabla ya kuingia katika uchaguzi wenziwao wa upande wa chama cha mapinduzi CCM wanapinga mapendekezo hayo kwa madai kwamba mazingira mazuri ya hali ya amani yapo na hakuna haja ya kuundwa kwa serikali wakati huu hadi hapo uchaguzi mkuu utakapomalizika. Mahojiano hayo yamekuja baada ya Kiongozi wa kambi ya upinzani, Abubakar Khamis Bakari kuwasilisha hoja binafsi inayotaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo katika mapendekezo yake alitaka ifanyike kura ya maoni au wajumbe waamua utaratibu watakaoona unafaa.Tofauti hizo zinakuja licha ya wajumbe wa hamlashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi iliyoketi visiwani Zanzibar na kutoa baraka zake juu ya umuhimu wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuheshimu kwa azimio la Butiama lililotaka kuwepo na maoni ya wananchi kuhusiana na suala hilo lakini bado wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa upande wa CCM wanaendelea kutofautiana.Endelea kusoma habari hii

 

CUF WATAKA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

30 01 2010

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimependekeza kura ya maoni ifanyike ili kutoa mwanya wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa za uchunguzi ambazo Mwananchi imezipata kutoka kwa baadhi ya wajumbe zinasema hoja binafsi inayotaka kuwasilishwa leo inataka baraza la wawakilishi liweke utaratibu utakaowawezesha wananchi wa Zanzibar kushiriki kwa njia ya moja kwa moja kutoa ridhaa yao kuunga mkono mfumo huo wa serikali ya umoja wa kitaifa kwa njia ya kura ya maoni (referendum).Aidha hoja hiyo ambayo itawalishwa na barazani hapo na kiongozi wa kambi ya upinzani, Abubakar Khamis Bakari inataka kura hiyo ya maoni iwe imeandaliwa na kufanyika sio zaidi ya mwezi Mei 2010 au baraza hilo liweke utaratibu mwengine kwa njia ambayo wazanzibari wenyewe kwa kupitia wawakilishi wao waliowachagua wataona inafaa.Hata hivyo kwa mujibu wa uchunguzi pia hoja hiyo imelitaka baraza la wawakilishi liiagize serikali ndani ya siku saa kuandaa na kuufikisha mbele ya baraza hilo mswaada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi ya Zanzibar nam 11 ya 1984 kwa madhumuni ya kweka utaratibu, masharti na namna ya uendeshaji wa kura ya maoni na pia kuipa mamlaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

 

HOJA BINAFSI KUWASILISHWA WIKI IJAYO

30 01 2010

HOJA binafsi ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar huenda ikawasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi wiki ijayo huku wajumbe wa baraza la wawakilishi wakiwa wanatofautiana kuhusiana na hoja hiyo.Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi ndani na nje ya kika cha baraza la wawakilishi wajumbe hao wanaonekana kuwa na mitizamo tofauti kufuatia baadhi yao kuunga mkono suala hilo na wengine kupinga kwa madai ya kupoteza nafasi zao za ungozi iwapo hoja hiyo ikikubaliwa kujadiliwa katika baraza na kukubaliwa.Juzi wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa upande wa chama cha mapinduzi (CCM) walikutana na kujadiliana suala hilo katika kikao ambacho kiliongozwa na mkuu wa shughuli za serikali katika baraza la wawakilishi ambaye ni waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha.Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya kikao hicho ambazo zilisisitizwa kutotolewa nje ya kikao hicho zimeeleza kwamba wajumbe wameshindwa kufahamiana na kutaka hoja hiyo ijadiliwe wiki ijayo baada ya wajumbe hao kutofautiana na huku wengine wakitaka kuwepo na umakini katika kulijadilia suala hilo ambalo limevuta hisia kubwa za wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba hivi sasa.Endelea kusoma habari hii

 

KICK BOXING BADO NI MARUFUKU ZANZIBAR

27 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza msimamo wake wa kutoruhusu mchezo wa ngumi za mateke (kick boxing) katika visiwa vya Unguja na Pemba.Naibu Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Mahmoud Thabit Kombo amewambia wajumbe wa Baraaza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar kwamba Serikali haijaruhusu mchezo huo hapa nchini .Mwakilishi wa Jimbo la Chambani (CUF) Abass Juma Muhunzi alisema kwa kuwa vijana wa Zanzibar sasa wanashiriki katika mashindano ya judo na ngumi za mateke ( kick boxing ) ambayo hayana tafauti sana na mchezo wa ngumi za kawaida (boxing ) ni kusema sasa mchezo wa ngumi unaruhusiwa kuchezwa Zanzibar.Waziri Kombo alisema ipo tafauti kubwa kati ya mchezo wa judo na mchezo wa ngumi kwa kuwa katika mchezo wa judo wachezaji hawapigani ngumi wala mateke isipokuwa wanaoneshana nguvu na mbinu katika kukamatana na kuangushana kwenye kiwanja kilichowekwa maalum matandiko malum ya kuangukia Mwakilishi wa nafasi za Wawanawake (CUF) Zakia Omar Juma alisema kwa kuwa mchezo wa ngumi za mateke ulipigwa marufuku na mzee Karume ili kulinda wananchi wasipigane kwa wakati huo kwa nini hivi sasa bado suala hilo linaekewa pingamizi na serikali hali ya kuwa baadhi ya Wazanzibar wanashiriki mchezo huo nje ya nchi na kushinda.Endelea kusoma habari hii

  

WAJUMBE WATAKIWA KUJITAYARISHA NA HOJA

27 01 2010

MWENYEKITI wa baraza la wawakilishi Ali Mzee Ali amewataka wajumbe wote wa baraza hilo kwenda kujitayarisha na hoja binafsi juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo inatarajiwa kuwasilishwa alhamisi wiki hii kwa ajili ya majadiliano.Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akiendesha kikao cha baraza hilo kutokana na Spika Pandu Ameir Kificho kutokuwepo barazani hapo tokea jana aliagiza nakala za hoja binafsi kugaiwa wajumbe wote na kuzipitia vyema ili watakapokuja kuchangia wawe na michango mizuri kwa kuwa wajue wanchangia nini katika hoja hiyo.“Kesho (leo) kutakuwa na maswali na majibu asubuh kama kawaida na vle vile kutakuja ripoti ya uchunguzi wa ripoti ya meli iliyozama ya Mv. Fatih, na kesho kutwa tarehe 28 kutakuwa na maswali na majibu na pia kutakuwa na uwasilishaji wa hoja binafsi kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa itakayowasilishwa na mjumbe Abubakar Khamis Bakari naagiza nakala hizi zigaiwe hii leo ili mzisome vizuri sana” alisema mwneyekiti huyo. Aidha amesema kikao cha mara hii kimemfurahisha sana kutoana na wajumbe wote wa CCM na CUF kuwa wameshikamana katika kuendesha vikao na kutokana na michango yao wanayoitoa ya kusaidia na kujenga serikali zaidi kuliko kukashifu na kuponda juhudi za serikali za kuleta maendeleo zinazofanywa na serikali ya mapinduzi Zanzibar.“Leo nimefurahi sana mnajua mimi maisha nakuwa na fursa maana mimi sio mtu wa kununa nuna lakini leo nimefurahi sana kwa namna tulivyoingia barazani safari hii tumeingia kwa furaha tumekumbatiana, tunacheka na kwa namna tunavyochangia miswaada yote iliyowasilishw ahapa imechangiwa vizuri kabisa.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WA CCM WASUSIA SERA YA NISHATI

26 01 2010

WAWAKILISHI wa CCM jana walisusa kuchangia sera ya nishati visiwani hapa iliyowasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yusuf Himid.Sera hiyo iliwasilishwa juzi usiku na kumlazimisha spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho kuahirishwa kikao hicho ili kutoa nafasi kwa wajumbe kuipitia kwa kina kwa lengo la kutoa mchango madhubuti na yenye manufaa kwa Zanzibar.Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba sera hiyo, iliyokuwa ikisubiriwa na wajumbe wa pande zote mbili, haikuchangiwa kwa uchangamfu kama ilivyotarajiwa kutokana na suala hilo kuzua mjadala mkubwa visiwani hapa.Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliwahi kutaka iundwe sera na kuwasilishwa kwa muswada wa sheria ili Zanzibar iwe na shirika lake la mafuta na kuondokana na kuchangia suala hilo na Bara, lakini hali haikuwa hivyo juzi.Suala la mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyowaunganisha Wazanzibari, hasa wa vyama vya CCM na CUF ambao wamekuwa na historia ya kuhasimiana kisiasa kwa zaidi ya miaka 10.Katika vikao vya baraza hilo mwaka jana, wawakilishi hao walikuwa wakizungumza lugha moja kuwa suala la mafuta liondolewe kwenye mambo ya Muungano, na hata baada ya mshauri wa kitaalamu kueleza kuwa uwezekano wa kupatikana mafuta ni mdogo, walisema watagawana hata kama yakijaa kwenye glasi.Lakini picha iliyoonekana jana inazua maswali kwenye mshikamano wa Wazanzibari ulioimarishwa na kitendo cha viongozi wawili visiwani humo, Rais Amani Abeid Karume na Seif Sharrif Hamad kukutana mwishoni mwa mwaka jana.Endelea kusoma habari hii

TUTASAIDIA VIKUNDI VYA AKINA MAMA-SMZ

26 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imo katika mpango wa kufufua vikundi vya miradi vya wananchi ambavyo walivibuni na kuanzisha katika shehia zao mbali mbali kwa ajili ya kuwaleta maendeleo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afisi wa Wairi Kiongozi, Hamza Hassan Juma, jana katika kikao cha Baraza la wawakilishi wakai akijibu suala la Mwakilishi Ali Abdallah Ali (CCM) aliyetaka kujua kuwa kwa kuwa baadhi ya wananchi walianzisha vikundi vyao vya miradi katika shhia zao kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi.Hata hiyo vimeweza vmekufa kwa njia mbaya sasa je? Wizara ina mpango gani wa kuwaimairishia wananchi kwa kuwafufulia vikundi hivyo ili nao waweze kuwahali nzuri kiuchumi.Waziri huyo alisema kuwa ni kweli kabisa wananchi waliunda vikundi hvyo lakini vilikufa kutokana na ukosefu wa fedha za uendeshaji, hiyo kwa kuzingatia hilo Wizara yake imo katika mipango ya kukaa pamoja na mratibu wa mradi wa (TASSAF), ili kujadili ni njia mbada ya kuwasaida wananchi hao.Alisema kuwa katika hilo zipo badhi ya fedga mabzo zikusanywa kupitia mradi huo, hivyo watakapokaa wataweza kujadli na kuangali uwezekano wa fedha hizo kuwaingizia wananchi hao atika miradi yao.Endelea kusoma habari hii

VIFAA VYA UMEME PEMBA VIMEKAMILIKA

26 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema tayari vifaa ya kumalizia utengenezaji wa huduma ya Umeme kisiwani Pemba vimeshwasili rasmi kisiwani humo kilichobakia ni umamaliziji uliosalia tu.Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee, jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akijibu suala la nyongeza la Mwakilishi Hija Hassan Hija mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF), aliyetaka kujua kuwa kwa kuwa Serikali imepanga kuwa huduma ya umeme kisiwani Pemba itakamilika Febuari mwaka huu je hilo ni kweli.Hata hivyo mwakilishi huyo alisema kuwa inasemekana kuwa baadhi ya vifaa vya ukamilishaji wa huduma hiyo havijawasili,je katika hilo ni kweli na kama kweli dhamira ya Serikali itatimia kurejesha huduma hiyo Februar kama ilivyokusudiwa.Akijibu asula hilo Naibu huyo alisema kuwa ni uhakika kabisa vifa hivyo vimeshawasili na vimeshakabidhiwa kwa wataalam wa umeme kisiwani Pemba ambapo hivi sasa kazi inaenelea vizuri.Alisema kuwa ni matumani yao makubwa kuwa huduma hiyo itakamilika kwa wakat uliopangwa kutokana na kazi hiyo kwenda kama ilivyokusudiwa na Serikal.Aidha Naibu huyo alifahamisha kuwa mara baada ya kukamilika kwa huduma hiyo wananchi wa kisiwani Pemba watanufaika vyema na huduma hiyo bila ya wasi wasi wa aina yoyote ile.Endelea kusoma habari hii

 

SOMO LA COMPUTER LIWEKWE KWENYE MITAALA

26 01 2010

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema imo katika mchakato wa kulifanya somo la komputa kuwa ni miongoni mwa masomo ambayo hufudishwa mashuleni kwa kuwekwa katika mitaala yake.Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Jabir Makame jana katika kikao cha Baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la nyoneza la Mwakilishi Najma Khafan (CUF) aliyetaka kujua kuwa kwa nini Wizara haliliingizi somo hilo mashuleni katika mitaala yake kutokana na somo hilo hivi sasa kuwa ni marufu sana mithili ya maji ya kunywa katika mahitaji yake.Naibu huyo alisema kuwa ni kweli kabisa somo hilo no marufu na ni muhimu sana katika matumizi ya shughuli mbai mbali ya jmanii, hivyo Wizara yake hvi sasa imo kaika mckao malum wa kuangali uwezekano wa kufanya hivyo.Alifahamisha kuwa katika kufanikisha hilo wamo katika mandalizi maalum ya kuangalia na kulitathmini kwa kwa kiasi gani wataweza kulifisha mashuleni ili kutoa fursa nzuri kwa wanafunzi.Hivyo alisema kuwa mara bada ya mchakato huo na kuona kuwa somo hilo ip haja ya kuliingiza katika orodha ya masomo Wizara yake italiingiza bila ya pingamizi ya aina yoyote ile.Endelea kusoma habari hii

 

KUKOSEKANA UMEME KUMEATHIRI SANA

26 01 2010

SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema tatizo la ukosefu wa umeme limeathiri kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali yanayotokana na taasisi mbali mbali hasa sekta ya utalii visiwani hapa.Hayo yameelezwa na waziri na nchi afisi ya rais fedha na uchumi, Mwinyihaji Makame Mwadini alipokuwa akijibu swali ya wajumbe katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Unguja.Mwakilishi wa jimbo la Chambani (CUF) Abass Juma Mhunzi katika swali lake ya msingi alitaka kujua n kiasi gani cha makusanyo ya mapato ya serikali yameathirika kutokana na tatizo la hilo la umeme lililoikumba Zanzibar tangu Novemba 10 mwaka jana.Waziri alisema kwamba vyenzo vingi vya mapato ya serikali vinategemea kuwepo kwa umeme wa uhakika pamoja na harakati za uchumi ambazo hutegemea kuwepo kwa umeme.Alisema kutokana na kukosekana kwa umeme katika kisiwa cha Unguja kutaathiri kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato ya serikali hasa katika sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kwa sababu ya kutumia umeme mbadala wa majenereta kwa muda mrefu.“kukosekana kwa umeme katika kisiwa chetu kumeathiri sana ukusanyaji wa mapato ya serikali hasa katika sekta utalii kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kwa sababu ya kutumia umeme mbadala wa majenereta kwa muda mrefu” alisema waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

 

MATUKIO YA KUZIMIKA UMEME YAWE NI FUNZO

26 01 2010

KAMBI ya upinzani katika baraza la waakilishi imesema matukio ya kuzimika kwa umeme katika visiwa vya Zanzibar ambayo husababisha shida kwa wananchi na hasara kubwa kwa serikali yawe ni fundisho kwa siku za baadae katika visiwa hivi.Akiwasilishwa hutuba ya kambi hiyo Waziri Kivuli wa Wizara wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Hamad Masoud Hamad mbale ya wajumbe wa baraza hilo katika kikao kinachoendelea Mjini hapa amesema lazima serikali ijipange upya katika kukabiliana na suala hilo ambalo huleta usumbufu mkubwa. “Matokeo ya Mei 2008 na haya tunayoendelea nayo yaliyotokea tarehe 10/12/2009 ya kukosa umeme kwa karibu ya siku 40 leo yawe ni mafunzo tosha kwa Serikali. Hasara kwa Uchumi wa Serikali na ugumu wa maisha ya wananchi yako wazi. Serikali ipange mipango yake upya, ikate pua iunge wajihi kuhakikisha kwamba kunapatikana japo mashine mpya za umeme (Generators) zitakazokidhi japo nusu ya mahitaji ya matumizi kwa hapa Unguja na huko Pemba” alisema Hamad.Alisema hata kama kuna miradi mipya ya kupatikana kwa umeme kutoka Tanzania Bara kwa kutumia waya wa baharini (submiarine cable) inayofadhiliwa na NORAD kwa Pemba na MCC kwa Unguja lakini umakini wa masuala hayo unahitajika zaidi.Alisema kutokana na kukosekana kwa Nishati ya Mafuta ya mara kwa mara hapa Zanzibar pamoja kwamba kuna wawekezaji kadhaa waliopewa jukumu la kuipatia mafuta Zanzibar wakati umedhihiri wa Serikali kuwa na akiba yake wenyewe (Reserves) ya mafuta hayo endapo hali hiyo itakuwa inajitokeza iweze kudhibitiwa.Endelea kusoma habari hii

TUNASIKITISHWA NA WATOTO-SMZ

22 01 2010

WIZARA ya kazi, maendeleo ya vijana, wanawake na watoto Zanzibar imesema inasikitsihwa na viendo vya unyanyasaji watoto vinavyoendelea kila kukicha katika maeneo mbali mbali ya Unguna na Pemba.Hayo yameelezwa na waziri wa kazi, maendeleo ya vijana na watoto Asha Abdallah Juma alipokuwa akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Mfenesni (CCM) Ali Abdalah Ali aliyetaka kujua wizara ina mkakati gani kuliondosha tatizo la unyanyasaji wa watoto wadogo kwa kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile.Waziri Asha alisema wizara yake inasikitishwa sana na ongezeko la vitendo viovu dhidi ya watoto ambapo alisema wizara inaendelea kuchukua hatua mbali mbali kukabiliana na wimbi la unyanyasaji wa watoto ikiwemo kubakwa na kuwaingilia kinyume na maumbile.Alisema katika kukabiliana na vitendo hivi,Wizara inaendelea na mchakato kuandaa sheria ya mtoto sheria ambayo itajumuisha masuala yote ya haki ulinzi na maendeleo ya mtoto ambapo alisema wizara ina imani kwamba baada ya kumkamilika kwa sheria hiyo na kuanza kutumika vitendo hivi viovu dhidi ya watoto vitadhibitiwa kwa kiasi kikubwa.Aidha alisema wizara imeshirikiana na Taasisi nyengine zinzoshughulikia masuala ya watoto kama vile idara ya Ustawi wa jamii ,Tume ya haki za binadamu, Jumuiya ya walemavu, Jumuiya ya wanasheria wanawake, wizara ya katiba na Utawala bora, Polisi na Magereza .kuunda kamati ya kudumu ya kushughulikia masuala haya ulinzi ,ustawi wa maendeleo ya watoto kwa ujumla.Endelea kusoma habari hii

HATUNA UTAFITI -SMZ

22 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema bado haijafanya utafiti wa kitaalamu kupima mwamko wa jamii kuhusu umuhimu wa haki za binaadamu kuenziwa.Waziri na nchi afisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhani Abdallah Shaaban ameyasema hayo wakati akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini Unguja.Amesema utafiti wa kitaalamu na tathmini ya kina haitawezekana kufanya kwa Zanzibar ndio kwanza imeanza kuadhimisha maadhimisho ya haki za binaadamu mwaka jana hivyo kabla ya kufanya tathmini kunahitajika elimu kwa wananchi ambapo wizara ya katiba na utawala bora imeshaanza utaratibu wa kutoa elimu katika maeneo mbali mbali ikianzia kwa vyombo vya ulinzi na usalama na masheha mbali mbali. Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali alitaka kujua kwa kuwa wizara ya utawala bora ndio inayoratibu sherehe za haki za binaadamu disemba 10 kila mwaka na tangu kuanza kwake wizara imefanya utafiti wowote kujua kama imesaidia kuleta mwamko kwa jamii kuhusu umuhimu wa haki za binaadamu kuenziwa.Akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni (CUF) Haji Faki Shaali aliyetaka kujua ni lini serikali itaondokana na tatizo la magereza kutoa huduma za choo ndani ya ndoo (mtondoo), waziri amesema hali hiyo ni jukumu la viongozi wa magereza wenyewe kuondokana nalo na sio wizara.Endelea kusoma habari hii

DPP KUONGEZEWA MAMLAKA

22 01 2010

MKURUGENZI wa mashtaka Zanzibar (DPP) atakuwa na uwezo wa kuelekeza taasisi yoyote ya upelelezi kuchunguza tuhuma zozote za jinai ambazo atakuwa amepatiwa taarifa kutoka taasisi ya upelelezi.Uwezo huo umo katika mapendekezo ya mswaada wa sheria wa kuweka ya uazishwaji na uendeshaji wa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar uliowasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi na waziri wa nchi afisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhan Abdallah Shaaban.Mswaada huo katika vipengele vyake vinaeleza kwamba bila ya kujali masharti ya sheria nyengine yoyote mkurugenzi huyo atakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote ambalo ni muhimu kufanyika katika utekelezaji wa kazi zake ikiwemo ya kuratibu upelelezi wa jinai.Aidha mswada huo umeeleza kwamba endapo kesi ya jinai imefunguliwa au inakusudiwa kufunguliwa au pale ambapo mkurugenzi amechukua mashitaka kutoka kwa mtu au chombo chochote anaweza kuieleza taasisi ya upelelezi kufanya zaidi kwenye kesi hiyo na kuelekeza masuala maalumu ya kufanyiwa upelelezi au taasisi maalumu anazotaka zitafutwe.Baada ya kukamilika upelelezi huo au kukusanywa huko kwa taarifa, jalada la upelelezi litapelekwa kwake kwa maamuzi.Endelea kusoma habari hii

  

WAWAKILISHI WATAKA MGAO WAO WA SAMAKI

22 01 2010

BAADHI ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wametaka mgao wao wa samaki waliovuliwa katika bahari kuu ya Tanzania waletwe Zanzibar licha ya kutokuwepo umeme katika visiwa hivi.Hayo yameelezwa na wajumbe mbali mbali wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.Hivi karibuni taasisi za Zanzibar zilizoomba kupatiwa mgao wa samaki zimeelezwa kwamba hazitaweza kupata kutokana na ukosefu wa umeme uliovikumba visiwa vya Zanzibar kwa takriban mwezi sasa. Wajumbe hao wamesema hata kama hakuna umeme bado mgao wa Zanzibar unapaswa kuletwa kwa wananchi kwani samaki hao wanapogaiwa hakuhitajiki kuwekwa kwa ajili ya kuhifadhiwa katika barafu kwa kuwa wananchi wana shida ya kiteweo na hawatohitaji kuhifadhi katika majokofu.Akijibu hoja hizo waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema samaki wa magufuli hawawezi kuletwa kutokana na utaratibu wa kuhifadhiwa unahitaji gharama kubwa na serikali ya mapinduzi Zanzibar haiwezi kujiingiza katika hasara kwa jambo ambalo halina uhakika nalo.“Ni hatari hao samaki kwa sababu wameshakaa katika mabarafu kwa muda mrefu na barafu yake sio ile ya kawaida kwa hivyo tunaweza kwenda kuwachukua lakini tukaja nao hapa matokeo yake ikawa baada ya kupata samaki tukampa mheshimiwa mugheiry shida ya kutibu watu kwa matumbo ya kuharisha” amesema waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

WAJUMBE WAPYA WAAPISHWA

21 01 2010

SPIKA wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho jana aliwaapisha wajumbe wawili wapya kutoka chama cha wananchi (CUF) walioteuliwa hivi karibuni na rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.Wajumbe hao wapya wote kutoka chama cha wananchi (CUF) ni naibu katibu mkuu Zanzibar, Juma Duni Haji na Nassor Ahmed Mazrui ambaye ni mwekezaji katika sekta ya utalii visiwani Zanzibar.Ukumbi wa baraza la wawakilishi jana ulifurika watu waliokuja kushuhudia kuapishwa kwa wawakilishi hao wapya ambao walifuatana na wapambe wao wa kike na kiume wakiongozwa na mkurugenzi wa mawasiliani ya umma wa chama hicho, Salim Bimani. Kuapishwa kwa wajumbe hao kunatokana na uteuzi wa hivi karibuni uliofanywa na rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume baada ya chama cha wananchi (CUF) kumtambua kuwa rais halali wa Zanzibar.Kwa mujibu kifungu cha 66 cha sheria ya Zanzibar rais ana uwezo wa kuteuwa wajumbe wawili kutoka kambi ya upinzani katika baraza la wawakilishi baada ya kupelekewa majina mawili na kwa kushauriana na kiongozi wa kambi ya upinzani.Uamuzi rais Karume kuwateuwa wajumbe hao wawili umetokana na mazungumzo yaliofanyika Novemba 5 mwaka jana Ikulu Mjini Unguja kati yake na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.Endelea kusoma habari hii

 

WAJUMBE KUTUMIA GARI ZA TAASISI NI VIBAYA

21 01 2010

UTARATIBU wa kuendelea kutumia msaada wa usafiri kutoka taasisi zinazochunguzwa na kamati za baraza la wawakilishi umeelezwa kuwa haupendezi lakini kufanyika kutokana na ukosefu wa fedha unaolikabili baraza hilo.Hayo yameelezwa katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza jana Maisara Mjini Unguja na Waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma alipokuwa akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Koani (CCM) Haji Mkema Haji.Katika swali lake Haji alisema wakati wa vikao vya baraza la wawakilishi wajumbe wanalazimika kuomba usafiri kutoka wizara au taasisi wanayoitembelea na kuhoji iwapo utaratibu huo ni mzuri kuendelezwa.“Utaratibu wa kuendelea kutegemea msaada wa usafiri kutoka kwa taasisi zinazochunguzwa na kamati za baraza wakati wa kufanya kazi za kamati za baraza si mzuri na haupaswi kendelezwa” alisem awaziri huyo.Alisema wajumbe wa kamati za baraza wanalazimika kutumia utaratibu huo kutokana na hali halisi ya mazingira ya sasa yalivyo ambapo baraza halijaweza kujitegemea kwa vyombo vya usafiri.Endelea kusoma habari hii

 

WAHALIFU WAPATA MWANYA-SMZ

21 01 2010

TATIZO la ukosefu wa umeme visiwani Zanzibar limeelezwa kusababisha kutoa mwanya kwa wahalifu kuiba nyaya za umeme nyakati za usiku.Hayo yameelezwa na naibu waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi, Tafana Kassim Mzee wakati akijibu maswali mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar.“Ni kweli hivi sasa ni jambo la kusikitisha kabisa kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wizi wa nyaya za umeme unaofanywa na watu wajinga na wazembe bila ya kujijua wanaharibu nyaya hizo kwa kuzivuta na kuziiaba bla ya kuzingatia athari zake ambazo zitaweza kuwakabili katika masiaha yao” alisema naibu huyo.Naibu huyo alikuwa akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujua serikali ina mpango gani ya kupata umeme mbadala utakaosaidia kupunguza tatizo la umeme litakapotokea tatizo la kukatika umeme kutoka Tanzania bara, Naibu huyo alisema serikali ina mpango wa kukabiliana na suala hilo.Alisema wizara yake kwa kushirikiana na wataalamu kutoka shirika la umeme wanaendelea na juhudi za kutafuta umeme mbadala kwa kuzingatia gharama za uzalishaji, uhakika wa kuwepo umeme huo kwa matumizi ya kila siku na wenye kutunza mazingira.Endelea kusoma habari hii

 

 TUME YA UTANGAZAJI ISIMAMIE MAADILI-WAJUMBE

21 01 2010

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wametaika tume ya utangazaji Zanzibar iwe mstari wa mbele kusimamia leseni wanazozitoa kwa vyombo vya watu binafsi katika kurusha matangazo yao kutokana na kuwepo kwa baadhi vyombo vya habari kukiuka madili ya habari.Wajumbe hao wameyasema hayo katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Unguja wakati wakichangia mswaada wa sheria wa marekebisho ya tume ya utangazaji, sheria namba 7 ya mwaka 1997 iliyowasilishwa na waziri na nchi afisi ya waziri kiongozi, Hamza Hassan Juma.Wajumbe hao wamesema baadhi ya vyombo vya habari vinakiuka maadili pamoja na utamaduni wa Zanzibar kwa kutangaza matangazo ya pombe hadharani na matumizi ya mipira ya kinga ya ukimwi kwa kutaja jina moja kwa moja bila ya kificho.Walisema kuna baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo radio hasa za FM hata matamshi ya lugha ya Kiswahili fasaha hawaezi na hawajui kutamka vizuri ambapo watangazaji wake na kulitaja jila la Zanzibar linawashinda kulitamka na kutaka tume ya utandazaji kulifuatilia jambo hilo.Wajumbe hao walisema serikali idhibiti matangazo ya kitaifa yasitolewe kiholela na radio binafsi kama kuandama kwa mwezi wa ramadhani hadi hapo chombo cha serikali kitangaze ndio vyombo vyengine vichukue taarifa kwao ili kudhibiti mkanganyiko unaotokea katika jamii juu ya mfungo wa mwezi huo wa ramadhani.Endelea kusoma habari hii

HATUNA TAKWIMU ZA WATALII-SMZ

21 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haina utaratibu maalumu wa ukusanyaji wa takwimu kutokana na aina ya daraja ya watalii wanaoingia nchini.Hayo yameelezwa na waziri wa utalii, biashara na uwekezaji, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM), Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua watalii wangapi wanapokewa Zanzibar ambao wa daraja la kwanza.“Tunasikia watalii wa daraja la kwanza hupatikana kwanza tutimize mambo yote muhimu na ubora wa huduma, kwanza uwanja wa ndege uwe na sifa zote za kimataifa, miundo mbinu ya usafiri, ubora wa usafiri wa ndani, mawasiliano, usalama wao na mali zao na mwisho dio hoteli na huduma zake zinazotolewa jee hao w adaraja la kwanza na sisi hapa kwetu tunapokea? Aliuliza mwakilishi huyo.Akijibu swali hilo waziri Samia alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi zenye kupokea watalii wa aina hiyo ambao ni wa daraja la kwanza.Alisema kwamba takwimu za mapato hazibagui aina ya watalii wanaopokewa ambao hungia Zanzibar lakini watalii wa daraja la kwanza huwa wanafikia hoteli za nyota 4 na nyota 5.Waziri Samia alisema kwa upande wa Unguja zipo hoteli 17 ambazo ni za nyota 5 na hoteli 15 ni za nyota 4 kwa sasa ambapo kwa upande wa kisiwani Pemba hakujawa na hoteli kama hizo lakini wageni huwa wanafikia katika hoteli mbili kuu ambazo zina viwango vya hali juu.Endelea kusoma habari hii

 

MFUMO WA ANALOG UNAKUJA

21 01 2010

IMEELEZWA kwamba wananchi wote watalazimika kununua vifaa vitakavyoweza kupokea matangazo ya digital ifikapo mwaka 1015 kutokana na mitambo ya analogi kutofanya kazi kabisa.Hayo yameelezwa na naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo, Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza jana katika ukumbi wa baraza hilo Maisara Mjini Unguja.Naibu huyo alisema kutokana na mabadiliko ya teknolojia na gharama zake vituo hivyo vya utangazaji vitalazimika kubadilisha mitambo yake kwa kuwa vitakuwa haviwezi kupokea matangazo yoyote kutokana na mfumo huo kubadilishwa.Alisema kutokana na hali hiyo serikali itashauriwa kutoa msamaha wa kodi wa vifaa vitakavyoingizwa nchini ili kuwahamasisha wafanyabiashara kuagiza vifaa hivyo na wananchi kuweza kumudu kununua.Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hija Hassan Hija aliyetaka kujua serikali imejiandaa vipi na mfumo mkongwe na kujitayarisha na mfumo mpya wa kiteknolojia.Kombo alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ilianza kuchukua hatua za utekelezaji wa mpango wa mageuzi mara baada ya kupitishwa kwa azimio la Shirika la Mawasiliano la Kimataifa (ITU) juni 2006 kwa kutekeleza mambo kadhaa.Endelea kusoma habari hii

MUUNDO MPYA WA POSHO ZA WALIMU WAANDALIWA

21 01 2010

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema imeandaa muundo mpya wa utumishi wa kada ya ualimu na kuiwasilisha serikalini kwa mazingatia zaidi.Hayo yameelezwa jana na naibu waziri wa elimu na mafunzo ya amali, Khamis Jabir Makame alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi.Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hija Hassan Hija alitaka kujua ni lini maslahi ya walimu kwa ujumla scheme of service yataangaliwa upya na kuondokana na matatizo kama hayo. “Wizara yangu yatari imeshaandaa muundo wa utumishi yaani scheme of service wa kada ya ualimu na kuiwasilisha serikalini na huko bila ya shaka tutapata mazingatio kwa hivyo walimu wasiwe na wasi wasi serikali yao inawajali na kuwatizama sana” alisema Naibu Waziri huyoAidha Mwakilishi huyo alisema kwamba mwaka 2006 katika sherehe za walimu duniani zilizofanyika wete kisiwani Pemba Rais Karume baada ya kuzingatia malalamiko ya walimu aliiagiza wizara kuwalipa walimu posho la asilimia 25 la ufundishaji lakini tangu muda huo agizo hilo.Endelea kusoma habari hii

 

HOJA BINAFSI KUWASILISHWA KWA SPIKA

21 01 2010

KIONGOZI wa kambi ya upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari jana aliwasilisha rasmi hoja binafsi ya kutaka kutenguliwa kwa vifungu vya katiba ya Zanzibar ili kumpa fursa Rais Amani Abeid Karume kukamilisha kazi ya kufungua milango ya serikali ya umoja wa kitaifa.Zanzibar imekuwa na matumaini ya kumalizika kwa siasa za chuki tangu Rais Karume afanye mazungumzo na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mazungumzo ambayo yalisababisha chama hicho kitangaze kumtambua Karume kuwa rais wa visiwa hivyo.“Ndio nimewasilisha hoja yangu leo kwa katibu wa baraza,” alisema mwakilishi huyo kutoka chama kikuu cha upinzani visiwani hapa, CUF baada ya kuwasilisha hoja yake jana asubuhi kwa katibu wa baraza.“Nina haki ya kuwasilisha hoja hiyo na kama nilivyozungumza na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam kuwa nitawasilisha kwa hivyo nimetekeleza azma yangu.”Kwa mujibu wa kanuni ya 50 (1) ya Baraza la Wawakilishi, iwapo mjumbe anataka kuwasilisha hoja binafsi katika kikao, atatakiwa kuiwasilisha kwa spika siku mbili kabla.“Iwapo kwa mujibu wa kanuni hizi taarifa ya hoja inatakiwa kutolewa, basi taarifa hiyo itabidi itolewe kwa maandishi, itiwe saini na mjumbe anayeitoa na ipelekwe kwa katibu ili aipokee kufuatana na masharti ya fasihi ya (1) ya kanuni hii,” inaeleza kanuni hiyo.Endelea kusoma habari hii

SERA YA NISHATI KUWASILISHWA BARAZANI

18 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekusudia kuwasilisha sera ya nishati kuhusiana na mafuta na gesi asilia katika kikao cha baraza la wawakilishi kitakachoanza januari 20 mwaka huu.Kwa mujibu wa sera hiyo ambayo gazeti hili imepata nakala yake inaeleza kwamba utafiti wa awali wa jiografia ya Zanzibar unaonesha uwezekano wa kuwepo kwa hifadhi ya mafuta na gesi asilia.Sera hiyo imesema kwamba wawekezaji wameonesha hamu ya kufanya uchunguzi na utafiti ili kufufua utafiti wa rasilimali ya mafuta ambapo mipango iliyopo hivi sasa ya usimamizi na ugawaji wa faida lazima upangw upya.“Mbali ya utafutaji wa hifadhi ya mafuta na gesi asilia ni muhimu sana kuangalia kwa karibu maendeleo ya teknolojia katika maeneo yote yanayotumia nishati. Zanzibar itafungua milango kwa kutoa fursa za aina zote za vyanzo vya nishati ikiwa ni pamoja na nguvu za nyuklia” imesema sehemu ya sera hiyo.Sera hiyo imesema Zanzibar itaanzisha mazingira yake ya kisheria na usimamizi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na utafutaji na itahakikisha udhibiti wote wa hifadhi ya mafuta katika maeneo yake yakiwemo maalumu ya uchumi.Endelea kusoma habari hii

KIKAO KUANZA JANUARI 20 MWAKA HUU

18 01 2010

KIKAO Cha Baraza la Wawakilishi kinatarajiwa kuanza Janauri 20 mwaka huu na kuwasiliwa jumla ya miswaada ya sheria miwili, sera moja nishati na jumla ya maswali na majibu 118 kuulizwa katika kikao hicho.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Maisara, Katibu wa baraza la wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim alisema miswaada itakayowasilishwa ni pamoja na ule wa sheria ya kuweka masharti ya uanzishwaji na uendeshaji wa ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka Zanzibar ambayo utawalishwa na waziri wan chi afisi ya rais katiba na utawala bora, Ramadhan Shaaban.Alisema mwengine ni mswaada wa sheria wa marekebisho ya sheria ya tume ya utangazaji Zanzibar ambayo ni sheria namba 7 ya mwaka 1997 ambapo pamoja na mambo mengine chini ya sheria hiyo kutakuwepo na marekebisho ya matumizi ya vyombo vya utangazaji kutoka katika mfumo wa analogi na kwenda digitali.Mswaada huo wa sheria utawalishwa na naibu waziri kiongozi, Ali Juma Shamhuna, na sera ya nishati Zanzibar itawalishwa na waziri wa maji, ujenzi,nishati na ardhi ambayo itawalishwa na Mansour Yussuf Himid katika kikao hicho.Endelea kusoma habari hii

NORWAY KUTOA MAFUNZO JUU YA MAFUTA

12 11 2009

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameandaliwa mafunzo maalumu ya siku mbili yenye lengo la kufahamishwa dhana nzima ya utawala bora katika suala la mafuta na gesi asilia Visiwani Zanzibar.Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambapo wajumbe wote wa baraza la wawakilishi watapata kujadili kwa kina suala hilo pamoja na kuuliza maswali kwa wataalamu wenye fani hiyo.Kwa kujibu wa taarifa ya Wizaya ya Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, zinasema kwamba mafunzo hayo yataanza kesho Mjini hapa ambapo Balozi wa Norway hapa nchini, Jon Lomoy atahudhuria katika mafunzo hayo.Habari zaidi zinaeleza kuwa katika mafunzo hayo mada mbali mbali zitawasilishwa na wataalamu waliobobea katika fani ya mafuta na gesi asilia, ambapo mada ya kwanza ni rasilimali ya mafuta itakayowasilishwa na Farouk Al-Kasim, Al-Kasim A.SMtaalam Nils Raestad ambaye mada yake itakuwa ni mahitaji ya uvumbuzi wa mafuta, na hali ya mafuta Zanzibar itakayotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Mwalimu Ali Mwalimu na mada nyengine inayohusu rasilimali itakayotolewa na Inge Amundsen.Endelea kusoma habari hii.

WIMBO WA TAIFA KUPIGWA BARAZANI-SMZ

29 10 2009

hassanSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kupiga wimbo wa taifa katika kikao cha baraza la wawakilishi kijacho kutokana na marekebisho ya kanuni za baraza la wawakilishi zilizofanywa na wajumbe wa baraza hilo.Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma aliwaambia wajumbe wa baraza hilo wakati akifanya majumuisho ya kanuni za baraza la wawakilishi toleo la mwaka 2007 katika kikao hicho kinachoendelea kwa wiki ya tatu sasa.“Kuimbwa wimbo wa taifa katika baraza letu hili tukufu litawathibitishia wale wanaosema Zanzibar sio nchi wanajua sasa kama hii ni nchi kamili ninachoomba kwa wajumbe hivi sasa waanze kujifunza wimbo huo wa taifa waaze mazoezi ya kuuhifadhi mapendekezo yakipita tu kikao kijacho tunaanza na kuweka CD yetu ambayo itatuongoza na sisi wajumbe sote tutaanza kuimba” alisema Waziri huyo kwa kujiamini.Kwa mujibu wa marekebisho ya kanuni ya 27 pendekezo la kupigwa wimbo wa taifa limeelezwa kuwa ni kujenga utaifa na kukuza uzalendo wa wajumbe na wananchi wote kwa jumla pamoja na kutoa ishara ya umuhimu wa shughuli zinazofanywa na baraza kitaifa.Katika marekebisho mengine ya kanuni hizo imependekezwa kwua utaratibu wa uchaguzi katika kuwatafuta wajumbe wa baraza wanaochaguliwa na baraza ili kuwa wajumbe wa tume ya bajeti urekebishwe ili wanaochaguliwa wasiwe mawaziri, wala manaibu wala wakuu wa mikoa na angalau mmoja kati yao ni lazima awe mwanamke.Endelea kusoma habari hii

 

MAREKEBISHO YA CHUO SUZA

29 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mswaada wa Haroun Ali Suleiman(CCM)marekebisho ya sheria ya Chuo kikuu cha taifa cha SUZA ya mwaka 1999 nambari 8 lengo lake kubwa ni kuongeza ufanisi na kujenga mazingira mazuri ya Chuo katika utekelezaji wa majukumu yake.Hayo yalisemwa na waziri wa elimu na mafunzo ya amali wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman wakati akiwasilisha mswada wa marekebisho ya Chuo kikuu cha taifa SUZA kiliopo hapa.Suleiman alisema marekebisho hayo yatakijengea uwezo chuo kikuu cha taifa na kuweza kulingana na vyuo vyengine katika masuala ya kitaaluma.Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamefanyiwa marekebisho kwa ajili ya kukipa uwezo chuo hicho ikiwemo mitaala ya elimu kuweza kulingana na Vyuo vyengine vya Tanzania Bara.”Marekebisho haya yanakwenda sambamba na mikakati ya serikali ya kuimarisha vyuo vyake kwenda na wakati wa sayansi na teknolojia”alisema Haroun.Alisema baadhi ya sheria zilionekana wazi kupitwa na wakati na hivyo kuwa kikwazo katika uendeshaji wa Chuo kikuu cha taifa.Endelea kusoma habari hii

 

WENYE KUDAI NGONO WATEGWE-SMZ

29 10 2009

zaSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewataka wanawake wenye kuombwa ngono ya mapenzi wakati wanapotafuta ajira sehemu za kazi watumie simu zao za mkononi kuwarekodi watu wenye tabia hiyo ili kupatikana ushahidi wa madai hayo.Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu maswali mbali mbali aktika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.“Wanaodaiwa ngono ya mapenzi wasema na wasikae kimya na siku hizi mambo yameendelea si watu wana simu za mkononi tunawaambia wanawake wenye simu watege sauti wanaozotakiwa kimapenzi za hao watu wenye tabia hiyo angalau mtu aje na ushahidi wa anayoyasema” alisema Waziri huyo. Alisema wizara yake ineendelea na usimamizi wa sheria ambapo ina jukumu kubwa la kusuluhisha migogoro hiyo ya wafanyakazi kwa kuwarejesha kazini wale wote ambao wamefukuzwa kinyume cha sheria au kupatiwa maslahi yao ya kazi na inaposhindwa yote hayo suala hilo huwasilishwa mahkama ya kazi kwa hatua zaidi za kisheria.“Wizara kwa nyakati tofauti imekuwa ikiwaita ofisini mameneja na maafisa wanaotuhumiwa kuwalazimisha kingono wafanyakazi hao, kwa kuwaonya ba baadhi yao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na waajiri wao baada ya hatua yetu ikiwemo kuonywa vikali wengine kufukuzwa kazi na wengine kuondoshwa nchini” alisema Waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

 

UKUTA WA CHUO KUTENGENEZWA

29 10 2009

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameelezwa kwamba serikali nimeshaanza kazi ya ujenzi wa ukuta unaolizunguka gereza kuu la wafungwa liliopo Kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Othman Nyanga wakati akijibu swali la msingi aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujuwa kama serikali inafahamu ukuta unaolizunguka gereza kuu liliopo Kilimani upo katika hali mbaya.Waziri Nyanga alisema analifahamu suala hilo na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa sasa ni kufanya ukarabati mkubwa wa ukuta wa gereza hilo ambalo lina idadi kubwa ya wafungwa.Mwakilishi huyo pia alisema kwa kuwa chuo cha mafunzo wakati mwengine hufanya shughuli za mbali mbali ndnai ya jengo la chuo jee Waziri anafahamu kuwa upande wa kusini na magharibi ya jengo hilo hakuna ukuta uliyo madhubuti wa kuwazuwia wanafunzi wao ambao ni wafungwa wasikimbie.“Nifahamu mheshimiwa spika kwamba ukuta unaoliznguka gereza liliopo Kilimani upo katika hali mbaya ambao ni hatari unaweza kusababisha wafungwa kukimbia kwa hilo nakubaliana na mheshimwia aliyeuliza swali hili lakini ndio serikali tumeona ipo haja ya kutengeneza na kulifanyia ukarabati jengo hilo” ‘alisema Nyanga.Endelea kusoma habari hii

SERA YA VIJANA IPO KATIKA MATAYARISHO

28 10 2009

ZWIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) kutayarisha sera ya vijana nchini kwa lengo la kuwasaidia vijana kujitambua.Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma aliyasema hayoa wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa matayarisho ya sera ya vijana yalipofikia.Mwakilishi huyo alisema katika jitihada za kuona kwamba wadau wa maendeleo ya vijana wanaitambua na kuielewa vyema sera ya maendeleo ya vijana idara kwa kushirikiana na jumuiya za Zanzibar Youth Forum imeendesha mafunzo mbali mbali kwa jumuiya zaidi ya kuchambua na kujadili vipengele na matakwa mbali mbali yaliomo katika sera ya maendeleo ya vijana na kuyatolea ufafanuzi na kuyafanyia uchambuzi wa kina ili yaweze kueleweka kwa urahisi.Alisema kwa kuwa sera hiyo ya maendeleo ya vijana bado haijaeleweka kwa kundi kubwa la vijana ambao ndio walengwa na kutaka kujua wizara ina mikakati gani katika suala hilo. Waziri Asha alisema ili kuifanya sera hiyo kueleweka kwa vijana wengi, wizara kwa kushirkiana na UNICEF imechapisha nakla 2,000 za vitabu zimetolewa kwa ajili ya kuwapatia vijana kuhusu umuhimu wa sera yao.Endelea kusoma habari hii

SMZ YAKARIBISHA VIKUNDI VYA MAZINGIRA

28 10 2009

moSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imefurahishwa na juhudi za halmashauri za wilaya katika kubuni miradi ya usafi wa mazingira katika maeneo ya miji.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Othman Nyanga wakati akijibu swali maswali mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.Katika maswali hayo Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa maendeleo ya vikundi vya usafi wa mazingira katika wilaya ya magharibi.Mwakilishi huyo alisema katika halmashauri ya magharibi ilianzisha mradi wa uzoaji taka katika maeneo ya Mombasa, Chukwani na sehemu nyengine na watu wenye kukusanyiwa taka walikuwa wakilipa shilingi 2,000 kwa nyumba na shilingi 6,000 kwa wenye maduka lakini hivi sasa zoezi hilo limetanua wigo wake na kufikia maduka ya kuanzia Kwanyanya, Kihinani, Bububu na Mtoni ambapo wafanyabiashara za nguo na maduka hulipishwa jee serikali inalifahamu suala hilo.Na kama serikali inahafahamu zoezi hilo kwa kuwa leseni za biashara ya maduka yanapatikana jee maduka yepi yanayolipa shilingi 6000 na ni kweli kuanzia Kwanyanya hadi Mtoni wamo katika mpango huo.Endelea kusoma habari hii

 

UPUNGUZAJI WA MASHARTI YA MIKOPO

28 10 2009

WIZARA ya Kazi Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar aimesema ni mapema sana kufanya tathmini ya maendeleo ya mikopo ya fedha za wajasiriamali zilizotolewa na viongozi wakuu wa nchi.Hayo yalisemwa na Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdalla Juma wakati akijibu swali la msingi la aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Amani (CCM) Ali Denge Makame aliyetaka kujuwa iwapo kuna mchango wowote wa fdha unaotolewa kwa vikundi na wizara ina mpango gani wa kupiguza masharti ya mikopo hiyo ili kupunguza urasimu wa kupatikana fedha hizo kwa wakati.Waziri Asha alisema zoezi hilo la utoaji wa fedha hizo ndiyo kwanza limeanza ambapo wananchi wamepata fedha hizo kwa upande wa Unguja na Pemba.“Naomba kufahamisha kwamba zoezi hili ndio kwanza limeanza ni mapema kulitolea uamuzi ila kuna taratibu zake. Baada ya kutuzama mwaka mmoja tangu kutolewa mikopo kutafanywa tathimini ya kupima mafanikio na kasoro/ matatizo ya utoaji na urejeshaji wa mikopo” Waziri Asha aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi.Hivyo alisema kwa sasa ni mapema sana kupunguza masharti ya mikopo ya fedha hizo na kutaka kupatiwa muda wa mwaka mmoja kwa ajili ya kufanya tahmini hiyo ikiwemo mafanikio ya mikopo hiyo pamoja na kasoro na matatizo ikiwemo urejeshaji wa mikopo.Endelea kusoma habari hii

 

SPIKA AKERWA NA UTORO BARAZANI

28 10 2009

chiefSPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho amewajia juu wajumbe wawakilishi na kuwaka kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika vikao vya baraza hilo na kuacha tabia ya kutokatka nje ovyo.Hatua ya Spika kutoa angalizo hilo limekuja kufuatia wajumbe wengi kutoka ndani ya vikao wakati shughuli za vikao zikiwa vinaendelea na baadhi yao wamekuwa hwaonekani kabisa kwa siku nzima katika shughuli za baraza hilo.“Hapa naona kuna tatizo ngoja kwanza naomba wajumbe mnatakiwa kuwa makini na kuhakikisha mnashiriki kikamilifu katika vikao vya baraza maana naona mahudhurio hapa hayaridhishi na kwa namna tunavyokwenda hapa kuna shughuli kubwa ya kupitisha miswaada ya serikali sasa ikiwa tutakuwa na idadi ndogo ya wajumbe nadhani itakuwa tatizo…sasa niwaombe kwa wale waliopo nje waingie ndani” alisema Spika ambaye amekuwa akirudia mara kwa mara agizo hilo tokea kwa kikao hiki bila ya kufanyiwa kazi na wajumbe hao.Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamekuwa wakitoroka na wengine kutoridhuria kabisa wakiwa wanafanya shughuli katika majimbo yao kwa madai ya kuogopa kuangushwa katika uchaguzi mkuu ujao ambayo unatazamiwa kufanyika mwakani.Endelea kusoma habari hii

MSWADA WA USAFIRISHAJI FEDHA HARAMU WAPITA

28 10 2009

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha mswada wa usafirishaji SHwa fedha haramu na kutaka kufanyiwa kwa marekebisho kwa kuondolewa kwa baadhi ya vifungu.Wajumbe wote kutoka katika kambi ya upinzani na chama tawala wamekubaliana kwa pamoja na kutaka baadhi ya vifungu kuondolewa hadi makubaliano ya pamoja kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yatakapofikiwa.“Mswada huu ili uwe na mafanikio na maslahi kwa taifa na wananchi wa Zanzibar baadhi ya vifungu vitatu vifanyiwe marekebisho”’alisema Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF) Said Ali Mbarouk.Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM) Ame Mati Wadi ambaye alisema kuna haja ya vifungu hivyo kufnayiwa marekebisho ili kuleta usawa na sheria hiyo kuwa na nguvu ya kisheria katika utekelezaji.Alisema ipo haja ya sheria hiyo kuwa kali kwa watu watakaopatikana na hatia kwani suala la uhalifu na usafirishaji wa fedha haramu unafanywa kwa siri kubwa na hivyo wenye kuendesha biashara hizo wanakuwa na fedha na sio rahisi kuweza kupatikana katika mipango yao hiyo haramu.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI PEMBA WAWEZESHWA KWA MIKOPO

27 10 2009

Mtumwa Kheri Mbarak(CUF)wanawakeSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema imetumia jumla ya sh.Millioni 185 kama ni mikopo na kuwawezeshaji wananchi na wajasiriamali katika kisiwa cha Pemba.Hayo yalisemwa na waziri wa kazi, maendeleo ya vijana wanawake na watoto Asha Abdalla Juma wakati akijibu swali aliloulizwa na mwakilishi wa Jimbo la Mfenesni (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa mpango wa serikali kuhusu mikopo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na biashara huko Pemba.Asha Abdalla alisema hadi kufikia mwezi wa Septembar 2009 kwa upande wa mkoa wa kusini Pemba benki imetoa mikopo kwa watu 66 yenye thamani ya sh.Millioni 185.Alisema kati ya fedha hizo sh.Millioni 151 zimetolewa kwa wananchi wa wilaya ya Chake Chake na jumla ya sh.Millioni 33.7 Millioni zimetolewa kwa wilaya ya Mkoani na kaskazini Pemba ambapo watu 11 wamepata mikopo yenye thamani ya sh.Millioni 24.9.Endelea kusoma habari hii

 

WIZARA YA WANAWAKE KUJENGWA PEMBA.

27 10 2009

WIZARA ya Kazi Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibarasha
imesema inakusudia kujenga ofisi mbali mbali za serikali kisiwani Pemba kwa ajili ya kurahisisha maendeleo kwa wananchi wa kisiwa hicho.Hayo yalisemwa na Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa lini wizara hiyo itajenga jengo la ofisi yake katika kisiwa cha Pemba.Waziri huyo alisema awali wizara ilikuwa na mipango hiyo ya kujenga jengo la ofisi kwa ajili ya kushungulikia maendeleo ya wanawake katika kisiwa hicho lakini wizara ilikuwa na juhudi hizo katika kipindi cha muda mrefu lakini ilipata kiwanja ambacho baada ya kuangaliwa kilionekana ni kidogo na hakitoshi kwa kujengea ofisi.Alisema baada ya kuonekana kiwanja hicho kuwa ni kidogo ombi hilo limerudishwa katika wizara ya maji,ujenzi,nishati na ardhi kwa ajili ya kupatiwa kiwanja chengine.“Nia yetu ipo pale pale ya kutafuta kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya wizara lakini kiwanja tulichopatiwa ni kidogo hivyo tumewajulisha wenzetu Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na ardhi”alisema.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WAIBANA TUME YA PAMOJA YA FEDHA.

27 10 2009

aminaSERIKALI imesema Tume ya pamoja ya fedha ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria inayo sura ya muungano katika utekelezaji wa majukumu yake.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afsi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Nungwi (CCM) Ame Ussi Juma aliyetaka kujuwa majukumu ya tume hiyo na kama kweli inayo sura ya muungano katika utekelezaji wa majukumu yake.Mwinyihaji alisema katika muundo wa tume hiyo wapo wajumbe saba ambao wanateuliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwemo makamo wa mwenyekiti na wajumbe wawili wa tume hiyo wanatoka Zanzibar.‘Katika muundo wa tume hii wapo wajumbe watatu kutoka Zanzibar na hivyo tume hiyo katika muundo wake unaonesha wazi kuwa na sura ya muungano’alisema Mwinyihaji.Akizitaja changamoto zinazoikabili tume hiyo, Mwinyihaji alisema kwanza imefanya kazi kubwa kujijenga katika kitaasisi na kandaa mapendekezo ya muundo wake.Alisema tume hiyo kwa mujibu wa katiba ipo tangu mwaka 1977 lakini haikuweza kutekeleza majukumu yake hadi katika mwaka 2003 ilipoundwa na kuanza kufanya kazi zake.Endelea kusoma habari hii

BIDHAA MBOVU HAZIHARIBU MAZINGIRA

27 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema bidhaa zinazoangamizwa Ame Ussi Juma(CCM)Nungwibaharini haziwezi kusababisha uharibifu wa mazingira.Hayo yalisemwa na waziri wa .utalii,biashara na uwekezaji Samia Suluhu Hassan wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesni (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa kama bidhaa zinazoharibiwa kwa kutupwa baharini kama hazileti madhara kwa mazingira.Samia alisema bidhaa zinazotupwa baharini kama Mchele.kunde pamoja na maharage na choroko hazina madhara kwa sababu hazitupwi sehemu moja.Aidha alisema za makopo kama tindikali,jiisi na soda za aina hiyo hizo hazitupwi baharini kwani zinaweza kusababisha madhara kwa baadhi ya viumbe vya baharini ikiwemo samaki.Alisema uangamizaji wa bidhaa hizo hufanywa kupitia nchi kavu chini ya usimamizi wa maofisa wa idara ya mazingira.Endelea kusoma habari hii

HAKUNA MGOMO WA KARAFUU

27 10 2009

Bihindi Hamad Khamis(CCM)wanawakeSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema hakuna mgomo kwa wakulima na wachumaji karafuu wa kususia kuvuna zao hilo huko Pemba.Hayo yalisemwa na waziri wa utalii,biashara na viwanda wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Samia Suluhu Hassan aliyekuwa akijibu swali aliloulizwa na mwakilishi wa jimbo la Mfenesni (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa kama kuna mgomo wa kuchuma karafuu kwa wakulima za zao hilo huko Pemba.Samia alisema si kweli kama wakulima na wachumaji karafuu katika kisiwa cha Pemba wamegoma.Alisema kilichojitokeza ni kwamba baadhi ya wakulima wa zao la karafuu walichelewa kuvuna karafuu kwa wakati uliowekwa.Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa wa kusini Pemba kuwahamasisha wakulima kuvuna karafuu ili kuliokowa zao hilo.Samia alisema zao la karafuu bado ni uti wa mgongo wa wananchi wa Unguja na Pemba na kuwataka wakulima kuliendeleza zao hilo.
Alisema zao la karafuu bado linahitajika katika soko la dunia licha ya kushuka kwa bei yake ambapo hilo ni suala la soko kupanda bei na kushuka.Endelea kusoma habari hii

 

TUNAWAJUA WALIOSABABISHA FUJO-SMZ PEMBA

23 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema watu waliofanya fujo na hassanvurugu katika zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura wote wanajulikana na hatua za kisheria dhidi yao zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani.Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma ameyasema hayo wakati akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar.Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali alisema daftari la kudumu la wapiga kura limeanza uandikishaji wake katika Mkoa wa Kaskazini kwa majimbo mbali mbali lakini kwa habati mbaya baadhi ya wananchi wasiolitakia kheri daftari hilo walifanya fujo kwa lengo la kuvuruga mpangilio mzima kwa wapiga kura.Alisema vurugu hiyo ni pamoja na nyumba kuchomwa moto, kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni tindi kali kiongozi mmoja wa serikali, kupigwa watu mawe pamoja na mambo mengine hivyo serikali inafahamu kutokea kwa vitendo hivyo na serikali inachukua hatua gani dhidi ya watendaji wa vitendo hivyo?Akijibu swali hilo Juma alisema vitendo vyote vya fujo vilivyofanywa katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura vinajulikana na serikali na baadhi ya matukio ya matukio mwenyewe ameyashuhudia na mengine amearifiwa na watendaji wake katika ngazi tofauti.Endelea kusoma habari hii

 

MAZINGIRA HUHARIBIWA DUNIANI KOTE

23 10 2009

Burhan Saadat (CCM)WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar, Burhani Saadati Haji amesema kwamba uhifadhi wa mazingira ni suala la dunia nzima na sio Zanzibar peke yake.Amesema uchafuzi wa mazingira unaofanyika duniani athari zake ni kubwa na ndio amana kukachukuliwa juhudi mbali mbali za kurejesha hali nzuri ya kuhifadhi mazingira kwa kuwa kumekuwepo na tishio kubwa la uharibifu wa mazingira ulimwenguni kote.Alisema athari hizo ni pamoja na baadhi ya visiwa kuwepo hatarini kutoweka kabisa, kima cha maji kuongezeka baharini pamoja na barafu kuanza kuyayuka katika sehemu nyingi za dunia.Haji alisema hayo wakati alipojibu swali la nyongeza na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujuwa mikakati ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira visiwani Zanzibar.Alisema hivi karibuni katika mkutano wa Geneva ambao yeye mwenyewe alihudhuria Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alikiri kuwepo kwa hatari ya baadhi ya visiwa kupotea kabisa kufuatilia kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na mataifa makubwa yenye viwanda vyenye kutoa kemikali.Alisema ni kweli vipo baadhi ya visiwa vinakabiliwa na tishio hilo ambapo baadhi ya visiwa vidogo viliopo vikiwemo vile ya kisiwani Pemba kuonekana kukumbwa na tishio la kuvamiwa na maji ikiwemo Kisiwa Panza ambacho Kisiwani Pemba.Endelea kusoma habari hii

SMZ KUTAFUTA MASOKO ZAIDI ULAYA

22 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea na jitihada DSC_8798zake madhubuti za kutafuta masoko mengine ya utalii badala ya nchi zilizokuwa zikileta watalii wengi kukubwa na msitikiso wa kifedha ulimwenguni.Hayo yameelezwa katika kipindi cha maswali na majibu ya wajumbe wa baraza la wawakilishi na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini alipokuwa akijibu maswali katika kikao hicho kinachoendelea Mjini Zanzibar.“Serikali inaendelea na mipango mbali mbali madhubuti ya kutafuta masoko mengine ya utalii mbali na nchi ambazo zimekuwa zikileta watalii zaidi na ambazo ndizo zilizoathirika na msukosuko huo wa kifedha kama vile Uingereza na Marekani” alisema Mwadini.Akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM) Ame Mati Wadi aliyetaka kujua kutokea kwa mtikisoko wa kifedha Zanzibar imenufaika au imeathirika, Waziri huyo alisema aliwataka wajumbe hao kutofautisha kati ya vitu viwili vya kuanguka kwa uchumi huo.Alisema kulikuwa na mtikisiko wa fedha katika mataifa makubwa uliopelekea makampuni na mabenki makubwa makubwa kufilishika na baadhi ya viwanda kuporomoka kwa biashara hali iliyosababisha wafanyakazi wake kupunguzwa kazi kutokana na kushindwa kudhibiti hali hiyo.Endelea kusoma habari hii

ZSTC KUMUDU KUNUNUA KARAFUU

22 10 2009

Samia SuluhuLICHA ya kukabiliwa na ukata mkubwa wa fedha shirika la taifa la biashara Zanzibar (ZSTC) tayari limenunuwa jumla ya tani 1,424 zenye thamani ya sh.4,124,951,000 za karafuu kutoka kwa wakulima Unguja na Pemba.Hayo yalisemwa na Waziri wa Utalii,Biashara na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Samia Suluhu Hassan wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa maendeleo ya shirika katika kipindi cha msimu wa manunuzi ya karafuu.Samia alikiri na kusema licha ya juhudi kubwa za shirika la (ZSTC) kununuwa karafuu kwa wakulima lakini linakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha.Alisema kufuatilia kukukabiliwa na tatizo hilo shirika linanunuwa karafuu kwa kukopa fedha kutoka katika Benki ya watu wa Zanzibar PBZ na kulipa riba asilimia 15%.Aidha alisema utaratibu wa shirika linafanya biashara katika mazingira magumu hivyo uwezekano wa kupata hasara ni mkubwa sana.Samia aliyataja baadhi ya matatizo ambayo yanalikabili shirika hilo ikiwemo kukabiliwa na madeni mengi pamoja na kudai fedha zake ziliomo mikononi.‘Kama shirika la biashara la taifa likilipwa fedha zake basi litaweza kufanya biashara bila ya matatizo wala kukopa kupitia katika Benki ya watu wa Zanzibar’alisema Samia.Alisema hata hivyo licha ya kukabiliwa na matatizo yote hayo shirika linaendelea na kutekeleza majukumu yake ya kununuwa karafuu kutoka kwa wakulima bila ya matatizo.Endelea kusoma habari hii

 

WAJUMBE WATAKA KULIBUSU KOMBE LA DUNIA

22 10 2009

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameomba kupatiwa fursa ya(0) kulikamata kwa mikono na kulibusu kombe la dunia linalotarajiwa kuingia nchini mwezi wa Novemba mwaka huu.Ombi hilo limetolewa muda mfupi na wajumbe hao baada ya Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Juma Shamhuna kumaliza kuwasilisha ripoti ya serikali juu ya ujio wa kombo hilo nchini katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisra Mjini Unguja.Wajumbe hao wakiwemo mawaziri wa serikali waliomba wapatiwe nafasi japo kidogo kwa ajili ya kulishika kwa mikono yao na kulibusu kombo la dunia wakati litakapowasilia visiwani hapa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.Hata hivyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mtu pekee atakayeruhusika kulishika kombo la dunia linalotarajiwa kuletwa nchini Novemba 22 mwaka huu ni Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.Akijibu ombi hilo Waziri Shamhuna alisema ingawa wajumbe hao wana hamu kubwa ya kulishika kombo hilo na kutaka angalau wapewe nafasi ndogo ya kulikamata na lakini kutokana na hali ya kiprotokoli anayepaswa kulishika ni rais wan chi pekee na sio mtu mwengine yoyote.Endelea kusoma habari hii

 

KILIMO CHA MPIRA KUENDELEZWA- SMZ

22 10 2009

kWIZARA ya Kilimo, Mifugo na Mazingira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema malengo yake makubwa ni kuliendeleza zao la kilimo cha mpira na kuwa tegemeo la taifa kwa kuwa zao la karafuu bei katika soko la dunia.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Khatib Suleiman Bakari amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu maswali mabli mbali katika kiako hicho kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.Awali Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali alisema ni muda mrefu sasa mashamba ya zao la mipira ya Unguja na Pemba yamekodishwa kwa wafanyabiashara binafsi ili kuongeza mapato katika mfuko mkuu wa seriakli huku zao hilo husafirishwa nje ya nchi kwa kuwa hakuna viwanda vya kutengenezea mipira jee ni kiasi gani cha fedha kinachopatikana katika kukodisha mashamba hayo kwa mwaka kwa Unguja na Pemba? Alihoji Mwakilishi huyoWaziri Bakarli alijibu kwamba kwa kuwa jukumu la ukodishaji wa mashamba hayo ya mipira linatekelezwa na wizara ya fedha na uchumi, suala la kujua kiasi cha fedha kiachopatikana katika ukodishaji wa mashamba hayo linaweza kujibiwa vizuri na wizara ya fedha amabyo inahusika moja kwa moja na suala hilo.Alisema wizara ya kilimo mpango wake ni kuliendelea zao hilo ikiwa ni pamoja na kuhimiza waannchi kupalilia na kuotesha miti mipya ili kuziba mapengo kwa miti iliyozeeka na ile iliyokufa kwa aeneo yote ya Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii

 

WAWAKILISHI WATAKA MFUKO WA JIMBO

22 10 2009

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameambiwa kwamba upo mpango wa serikali wa kuanzishwa mfuko wa maendeleo wa jimbo kwa ajili ya IMG_5929kuharakisha maendeleo ya wananchi katika majimbo ya uchaguzi.Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma aliyasema hayo jana katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Unguja wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa lini serikali itaanzisha mfuko wa maendeleo ya jimbo kama ilivyo kwa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano.Waziri huyo alisema kuna mhumuhi mkubwa wa kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi katika majimbo yao uchaguzi ambapo wasimamizi wa maendeleo ya mfuko huo ni wote wakiwemo wabunge, wawakilishi na wananchi wenyewe.Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafuatilia kwa karibu sana suala hilo mfuko huo ambapo tayari ujumbe wa baraza la wawakilishi ukiongozwa na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ulifanya ziara nchini Kenya kujifunza kazi za mfuko wa jimbo zinazofanywa huko na kuona kuwa kuna mafanikio makubwa katika mfuko huo.‘Ile ripoti ya ziara ya ujumbe wa spika wa baraza la wawakilishi iliyofanywa huko Kenya kwa ajili ya kuona kazi za mfuko wa jimbo itawasilishwa hapa mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi lakini niseme kwamba mfuko huu una manufaa makubwa sana na tumejifunza mambo mengi kutoka kwa jirani zetu Kenya” alisema Waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

 

TUNATAKA OFISI ZETU-WAJUMBE

21 10 2009

bigdadyWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wametaka kutengewa fedha maalumu kwa ajili ya kujengewa nyumba katika majimbo yao kama ilivyokuwa zimetengwa fedha hizo na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayo nia ya kujenga ofisi za wajumbe wa baraza la wawakilishi katika majimbo ya uchaguzi kwa Unguja na Pemba kama ilivyokuwa kwa wabunge.“Napenda kuwahakikishi wajumbe kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar inayo ni ya kujenga nyumba kama hizo kwa ajili ya waheshimiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi majimboni mwao, hali itakaporuhusu kwa muda huu tunawaomba waheshimiwa wawe na subira mpaka uwezo wa kufanya hivyo utakaporuhusu” alisema Waziri huyo.Hata hivyo baadhi ya wawakilishi wamemwambia Waziri huyo kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar haina nia ya kuwajengea ofisi na ndio maana hadi leo hii hakuna michoro ya ujenzi wa nyumba hizo wala kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kazi hiyo.“Pamoja na majibu mazuri ya mheshimiwa waziri lakini mimi nina wasi wasi na aliyoyaeleza kama kweli kuna nia basi angalau kungekuwepo na michoro au vifungu vilivyotengwa angalau lini au mwaka gani lakini sio kuambiwa kuna nia ya serikali ya kujenga wakati hakuna hata huo mpango uliopwangwa” alisema Ame Mati Wadi Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM).Endelea kusoma habari hii

SMZ HAINA FEDHA ZA KULIPA FIDIA

21 10 2009

JUMLA ya wananchi 355 katika kipindi cha mwaka 2002 walioanguka thkutoka juu ya mikarafuu hawajalipwa fidia na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan alisema kutolipwa kwa watu hao serikali inafahamu sana kuwa ina deni ya watu walioanguka juu ya mikarafuu katika kipindi hicho lakini hali ya fedha ndio hairuhusu.Samia ameyasema hayo kufuatia swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa kama serikali inafahamu kuwepo kwa watu 355 walioanguka katika mikarafuu ambao hawajalipwa fidia hadi sasa.Mwakilishi huyo alisema maagizo na ushauri wa kamati ya maendeleo ya wanawake na ustawi wa jamii ya baraza la wawakilishi kwa mwaka wa fedha 2008/2009 iliitaka serikali kuwalipa watu 355 walioumia kutoka juu ya mikarafuu tokea mwaka 2002.Alisema idara ya ustawi wa jamii imeshakamilisha hatua za utengenezaji wa malipo kiichobaki ni wizara kupitia shirika la ZSTC kutoa malipo hayo ambapo alimtaka Waziri kumfahamisha iwapo suala hilo analijua au halijui.Waziri Samia alisema pamoja na serikali kujua kwamba ina deni kwa wananchi hao lakini Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) linakabiliwa na hali mbaya ya kifedha na kushindwa kuwalipa watu hao wanaoanguka katika mikarafuu.Endelea kusoma habari hii

 TUTAKABILIANA NA EL NINO-SMZ

20 10 2009

HSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema tayari imeshaomba msaada wa vifaa Umoja wa Mataifa (UN) na washirika mbali mbali wa maendeleo ili kukabiliana tishio la mvua za Eli Nino.Hayo yameelezwa jana katika kikao cha baraza la wawakilishi na Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe hao waliotaka kujua Zanzibar itakabiliana vipi na maafa yatakayoweza kujitokeza wakati wa mvua hizo ambazo zinatizamiwa kuja wakati wowote kuanzia sasa.Katika swali lake la msingi Mwakilishi wa Jimbo la Nungwi (CCM) Ame Ussi Juma alitaka kujua kwamba serikali inafahamu tishio la kuja el nino na imejiandaa vipi kukabiliana na mvua hizo ambazo zinaelezwa kuleta athari kubwa katika nchi.Waziri Juma aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba taarifa ya utabiri ya kuwepo kwa mvua za al nino kwa kipindi cha septemba 2009 hadi machi 2010 Tanzania ikiwemo Zanzibar ni sahihi.“Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imeshawasiliana na washirika wa maendeleo na umoja wa mataifa juu ya kupata vifaa na madawa mbali mbali kwa tahadhari ya mvua zinazotarajiwa kunyesha mwishoni mwa mwezi huu” Juma aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi.Endelea kusoma habari hii

MAMILIONI KUGHARIMU UJENZI MICHEWENI

20 10 2009

JUMLA ya shilingi 157,400,000 zinatarajiwa kugharimu ujenzi mzima wa Dwa jengo jipya la radio jamii (Community Radio) katika kijiji cha Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji na Michezo, Mahmoud Thabit Kombo aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujua jengo hilo la radio jamii hadi kumalizika kwake litagharimu kiasi gani cha fedha pamoja na vifaa vyake.Akijibu swali hilo Kombo alisema jengo la Micheweni hadi kumalizika kwake litagharimu kiasi cha shilingi 157,400,000 kwa ujenzi wa jengo lenyewe na shilingi 45,000,000 kuweka transfoma na kuvuta umeme kutoka katika kituo cha umeme hadi kituoni hapo.Alisema gharama hizo za ujenzi zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo vifaa vya radio hiyo pamoja na gharama za teknolojia ya habari na mawasiliano vinakadiriwa kugharimu kisi cha shilingi 100,000,000 ambazo zitagharamiwa na Shirika la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).Naibu huyo alisema mbali ya Shirika hilo la UNESCO kusaidia lakini pia wapo washirika wengine wa maendeleo wakiwemo UNDP na Umoja wa Mataifa (UN) pia wamesaidia sana katika kufanikisha ujenzi wa kijiji hicho cha Micheweni ambacho kimeteuliwa kuwa ndio kijiji pekee cha Millenia kwa Unguja na Pemba.Endelea kusoma habari hii

SMZ KUJENGA OFISI ZAKE PEMBA

20 10 2009

ame matiWAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Zanzibar Mwinyihaji Makame Mwadini amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na mipango yake ya kujenga majengo ya kudumu ya ofisi za serikali Kisiwani Pemba.Waziri huyo aliyasema hayo wakati ukijibu mswali mbali mbali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi yaliouliza kuhusiana na jengo jipya la wizara ya fedha na uchumi linalotazamiwa kujengwa katika kisiwa cha Pemba.Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali alitaka kujuwa wizara ya fedha na uchumi imeanza kujenga jengo lake jipya katika eneo la Tibirinzi ambapo ujenzi huo ulianza julai 2009 na umechukua wiki 12 na hatua iliyofikiwa ni kutadnika kwa jamvi la chini jee wizara inajua kwamba afisi ya wizara ya fedha na uchumi Pemba haikushirikishwa katika ujezi huo.Waziri Mwadini alisema wizara ya fedha na uchumi inayo mashirikiano mazuri sana na afisi yake iliopo Pemba katika ujenzi wa jengo lake jipya na mashirikiano hayo yanawahusisha tangu hatua za awali ikiwa ni pamoja na utafutaji wa kiwanja, mahitaji ya afisi zinazotarajiwa kuwemo katika jengo hilo na mchakato wa kumpata mshauri wa ujenzi na hatimae kumpata mjenzi mwenyewe.Aidha alijibu kwamba afisi ya wizara ya fedha na uchumi Pemba inashiriki kikamilifu katika vikao vya pamoja baina ya wizara, mjenzi na mshauri kwa madhumuni ya kufanya tathmini ya maendeleo ya ujenzi (site meetings) ambapo wizara ya fedha na uchumi Pemba kwa kushirikiana na mkandarasi imefuatilia upatikanaji wa huduma muhimu katika kufanikisha ujenzi unaoendelea ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma za maji, umeme na eneo la kutunzia vifaa.Endelea kusoma habari hii

GOMBANI KUFANYWA WA UWANJA WA KIMATAIFA

20 10 2009

SERIKALI ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kuufanya matengenezo makubwa uwanja wa michezo wa Gombani Kisiwani Pemba ili kufikia Ali Juma Shamhuna(CCM) Dongekiwango cha uwanja wa kimataifa.Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo awaliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM) Ame Mati Wadi aliloulizwa ni hatua gani umefikia uwanja huo wa Gombani katika matengenezo yake.Kombo alisema serikali ina lengo la kuutengeneza vyema uwanja huo ili ufikie hadhi ya kimataifa ambapo aliitija baadhi ya mikakati inayokusudiwa kufanywa katika kufikia kiwango cha hadhi ya kimataifa ni kuwekwa nyasi bandia na kuwekwa taa za kungara katika uwanja huo.Alisema uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba unatazamiwa kuwekwa nyasi bandia kwa msaada mkubwa wa shirikisho la Soka la Ulimwenguni (FIFA) ambapo gharama zake ni dola za kimarekani laki nne.“Hatua ya kuimarisha uwanja wa michezo wa Gombani Pemba hatua za awali za matayarisho ya uaplekaji wa umeme mkuwa katika uwanja huo kwa lengo al ufungaji wa taa zimeanza. Kazi hiyo inakdiriwa kugharimu shilingi 33,000,000 ambazo hadi kufikia juni 2009 zishalipwa shilingi 18,000,000 jee fedha hizo zinalipwa na serikali au washirika wa maendeleo?” alihoji Mwakilishi huyo.Naibu Waziri alijibu kwamba fedha zote za matengenezo hayo zimelipwa kutoka katika mfumo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kazi ya uwekaji wa taa itafanyika kwa msaa wa Mfadhili Sheikh Al Youseif kutoka Saudi Arabia.Endelea kusoma habari hii

 

TUTAWASAIDIA WENYE VIWANDA-SMZ

sSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea na juhudi za kuvisaidia kwa kusimamia na kuvipa ushauri wa kupunguza gharama za uzalishaji viwanda ili kuzalisha bidhaa bora nchini.Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuhakikisha inavilinda viwanda vya maji vilivyopo.Mwakilishi huyo ameuliza pia kama kuna mpango wowote wa kiwanda cha soda ambacho hivi sasa vinapata ushindani mkubwa wa kibiashara kutoka Tanzania baraWaziri huyo alisema serikali imekuwa ikitoa ushauri kwa wenye viwanda wa kupuguza gharama za uzalishaji na kuzalisha kwa wingi bidhaa zenye ubora unaokubalika na kutosheleza.Alisema kutokana na maelezo ya wahusika na ukusanyaji wa kodi ya ‘trade levy’ kwa bidhaa zinazotoka Tanzania Bara, imebainika kwamba ni kweli kuna ugumu katika kuitekeleza kazi hiyo ipasavyo. Endelea kusoma habari hii

MTIKISIKO WA KIUCHUMI WAATHIRI Z’BAR

FAMILIA nyingi zinazotegemea kupata misaada kutoka kwa jamaa zao mwaliopo nje ya Zanzibar zitakabiliwa na upungufu wa fedha, utaotokana na kuwapo kwa mtikisiko wa Uchumi duniani. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachojadili makadirio ya matumizi na mapato ya serikali ya mwaka 2009/2010 kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar. “Msukosuko huu unatarajiwa pia kupunguza misaada inayotumwa na jamaa kutoka nje, kulingana na makadirio ya mtazamo wa uchumi wa dunia katika miaka ya usoni uliotolewa na Shirika la Fedha la dunia (IMF) Aprili 2009, uchumi wa dunia unakisiwa kushuka kwa asilimia 1.3 mwaka 2009 kutoka ongezeko la asilimia 3.2 mwaka 2008″ alisema Waziri huyo. Endelea kusoma habari hii

ZNZ TAYAKIWA KUWAVUTIA WAWEKEZAJI

SHSERIKALI  ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetakiwa kuelezea matayarisho na mikakati yake thabiti ili kuweza kuwavutia zaidi wawekezaji wa mitaji mikubwa,kampuni na uendeshaji wa viwanda katika hali ya uhakika kwenye dunia hii ya kukua kwa teknolojia. Balozi wa Ujerumani nchini Bwana Guido Herz jana alimuuliza Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha akitaka kujua mandalizi ya serikali ya SMZ kuhusiana na uhakika wa nishati ya umeme,mtandao wa kimawasiliano na upatikanaji wa maji safi na salama katika visiwa vya Unguja na Pemba. kijibu maswali hayo Nahodha alisema SMZ kwa kiasi kikubwa imejenga miundombinu ya barabara,bandari na uwanja wa ndege licha ya kuwepo kwa waya wa umeme uliopita chini ya bahari toka kidatu juhudi zinaendelea kuufanyia ukarabati waya huo. Endelea kusoma habari hii

“WABARA WALIPE KODI”

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mkakati mpya wa kuwataka wawekezaji na watu wneye asili ya Tanzania bara kusajiliwa na kuanza chibuikulipa kodi ya ardhi ya dola 5000 kila mwaka kwa kila hekta moja ya ardhi. Mpango huo umetanganzwa na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Mohammed Hashim Ismail kufuatia bodi hiyo kupewa uwakala wa kusimamia na kukusanya kodi ya ardhi kuanzia machi mosi mwaka huu na waziri wa Maji, Ujenzi Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid. Alisema kwa mujibu w asheria ya ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 ni mzanzibari tu ndio ana haki ya kumiliki ardhi lakini wageni wote wanapaswa kukodishwa wakiwemo wageni na watu wenye asili ya Tanzania bara. “Hatua hii itatuwezesha pia kuwafahamu wamiliki wote wakubwa na wadogo wadogo wa vipande vyote vya ardhi hapa Zanzibar pamoja na wale ambao wanatajwa kuhodhi maeneo kinyume na utaraibu” alisema Kamishna huyo. Endelea kusoma habari hii

WAZANZIBARI WAKOMALIA MAFUTA YAO

CUFWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wametaka ukanda maalumu wa kiuchumi (EEZ), Serikali ya Mapinduzi Zanzibar isishirikiane na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hayo yamefikiwa jana katika Baraza hilo ikiwa ni maagizo ya Wajumbe hao kwa SMZ kwamba ukanda maalumu wa kiuchumi sio vyema kukawepo na ushirikiano na CCMserikali ya muungano kwa kuwa eneo hilo ni muhimu katika uchumi wa nchi na hasa katika suala zima la nishati ya mafuta. Wawakilishi hao kwa ujumla wao walipinga pendekezo la tatu la SMZ la kutaka kuwepo kwa ushirikiano na serikali ya muungano kuhusu EEZ (Exlusive Economic Zone) ambapo wote walipiga kura ya hapana katika hoja hiyo. Endelea kusoma habari hii

MSHAURI MWELEKEZI AREJESHE FEDHA Z’BAR

WAKATI leo ndio siku ya mwisho ya mjadala wa mafuta na gesi asilia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoa azimio kuondolewa kwenye iddi pandumambo ya Muungano au la, Idadi kubwa ya Wawakilishi wamemtaka Mshauri Mwelekezi kurejesha fedha za SMZ kwa kuwa majukumu aliyopewa hakuyafanya na kushambikia upande mmoja. “Mambo alielekeza mshauri elekezi wala sina haja nayo kwani ametuweka kona ameelemea upande mmoja tunamwambia uturejeshee fedha zetu…hatuna radhi naye kwa sababu fedha hizi ni za walipa kodi wa Jimbo langu ambao wavuja jasho” alisema Mwakilishi wa Jimbo la Koani (CCM), Haji Mkema Haji. Mkema alisema kitendo cha Mshauri Mwelelezi, David Reading kutoka kampuni ya AUPEC ya Uingereza hakufanya kama alivyotarajiwa kwani licha ya Wawakilishi kumshauri mambo kadhaa muhimu ameyapuuza na kufanya anavyotaka yeye. Endelea kusoma habari hii

HATUJAONDOA FEDHA ZETU – SMT

Rashid seifTATIZO la kuwapo kwa Mtikisiko wa fedha Duniani, Serikali ya Zanzibar imesema bado haijaamua kuziondoa fedha zake za kigeni katika benki ambazo imeamua kuziweka. Waziri anaeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk, Mwinyihaji Makame, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman aliyetaka kujuakama serikali ina mpango wakuziondoa fedha zakigeni katika mabenki yanje kutokana nabaadhi mataifa kufanya hivyo. Akijibu hilo alisema ni kwelibaadhi ya mataifa yameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuzihamishia fedha zao katika maeneo salama lakini serikali ya Zanzibar bado haijaamua kuchukua hatua hiyo. Endelea kusoma habari hii

  MAFUTA YAONGEZA MGOGORO WA MUUNGANO

KUNA kila dalili kuwa mzimu wa  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhusu Zanzibar unaanza kuumomonyoa taratibu muundo wa DSC_8679Serikali ya Muungano baada ya wawakilishi wa CCM na CUF kuungana na kudai kuna mapungufu mengi katika mambo yaliokubaliwa katika hati ya Muungano mwaka 1964. Hilo limejitokeza wazi wazi jana wakati wajumbe wa Baraza la wawakilishi walipokuwa wakichangia mjadala kufuatia SMZ kuwasilisha taarifa yake juu ya mapendekezo ya uendeshaji wa kazi ya utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia Zanzibar. Kikao hicho kiliketi chini ya uenyekiti wa baraza hilo, Ali Mzee Ali baada ya Spika Pandu Ameir Kificho kutokuwepo nyakati za jioni kilielezea mengi kutoka kwa wajumbe kuhusiana na kutoridhishwa na ushauri wa Mshauri Mwelekezi juu ya utafutaji na mafuta na gesi asilia. Endelea kusoma habari hii

MAFUTA NA GESI SIO ZA MUUNGANO – SMZ

Mansour Yusuf HimidSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema suala la mafuta na gesi asilia halikuwepo katika orodha ya mkataba wa Muungano uliosainiwa na viongozi na waasisi wawili wa mataifa mawili Zanzibar na Tanganyika. Akitoa tamko hilo lililochukua muda wa zaidi ya saa moja ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wazanzibari mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi jana, Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid amesema serikali inataka kuondolewa kwa suala la mafuta na gesi asilia kwenye orodha ya mambo ya Muungano kwa sababu haliwanufaishi Wazanzibari na pia suala hilo halikuwemo kwenye mkataba wa Muungano 1964. Alisema kwamba sasa suala la mafuta na gesi asilia kuwemo kwenye mambo ya Muungano ni ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kila mmoja katika nchi. Endelea kusoma habari hii

 ZNZ YAGUSWA NA MTIKISIKO WA KIUCHUMI DUNIANI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema sekta ya utalii issa ahmedimeyumba kutokana na mtikisiko wa kifedha ulioikumba dunia kwa sasa. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Issa Ahmed Othman wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Sebleni Mkoa wa Mjini Magharibi. Amesema sekta ya utalii hivi sasa imeathirika kwa kiasi fulani kutokana na mwenendo mzima wa kupunguwa kwa watalii wanaiongia nchini huku safari za ndege kutoka nchi mbali mbali zimepungua kwa kiasi kikubwa. Mwenyekiti huyo alisema baadhi ya watalii ambao tayari walitoa ahadi ya kuja pamoja na kukamilisha matayarisho yao wengi wameahirisha safari hizo huku mashirika ya ndege yakipunguza safari za kuleta watalii nchini. Endelea kusoma habari hii

AFRIKA YAATHIRIWA NA MTIKISIKO WA KIUCHUMI

WAJUMBE wa Shirikisho la Mamlaka zinazoshughulikia soko la mitaji katika Afrika Mashariki wamekutana kwa siku mbili na kujadili msukosuko wa kifedha duniani na umuhimu wa elimu ya mitaji ya umma katika nchi hizo. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za tawi la benki kuu (BoT) Gulioni Mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa kikao hicho, Japheth Katto alisema nchi zao zimeathirika kutokana na msukosuko wa kifedha ulioikumba dunia kwa sasa. Alisema kikao chao kimejadili namna ya kuweka mikakati ya kuweza kukabiliana na hali hiyo ambayo imekuwa ikitishia hali ya uchumi katika nchi mbali mbali hasa katika bara la Afrika ambalo nchi zake zinayumba haraka itokeapo hali kama hiyo ya kuyumba uchumi wa mataifa makubwa. Endelea kusoma habari hii  

SMZ IMELIPA KISOGO ZAO LA KARAFUU 

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameitupia lawama Serikali ya SHAMapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kushindwa kulipa kipaumbele zao la karafuuu ambalo ndio zao tegemeo kwa wananchi wa Zanzibar.  Akichangia makadirio ya mapato na matumzi ya serikali ya mwaka wa fedha wa mwaka 2009/2010 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini Zanzibar, Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni (CUF) Haji Faki Shaali alisema serikali imepuuza zao la karafuu ambalo kwa sasa sio tena uti wa mgongo lakini imekuwa uti wa mguu kutokana na kulipa kisogo zao hilo. Alisema zao la karafuu linajulikana kwamba ndio zao pekee linalowasaidia wananchi wa Unguja na Pemba na ndio tegemezi kuliko huo utalii ambao husemwa sana kuwa ndio mbadala wa zao hilo. Shaali alisema karafuu bado ni tegemeo la taifa katika kuingiza fedha za kigeni pamoja na wananchi kwa ujumla katika kupata fedha za kuendesha maisha yao. Endelea kusoma habari hii

SMZ YAKIRI KUFELI MAENEO HURU

SALMSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kutoyaendeleza maeneo huru ya uchumi yaliotengwa kwa ajili hiyo na serikali ya awamu iliyopita iliyokuwa ikiiongoza na Rais Mstaafu Dk. Salmin Amour Juma. Akijibu maswali na majibu ya wajumbe mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi, Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan alisema maeneo ya huru yaliotengwa huko Micheweni Kisiwani Pemba bado hayajaendelezwa. Waziri Samia alisema katika eneo la Micheweni yametengwa maeneo kwa ajili ya uendelezaji wa maeneo huru ya uchumi. Maeneo yenyewe yana ukubwa wa jumla ya hekta 808.8 ambapo kati ya hizo ni hekta 547.4 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya viwanda na gala na hekta 261.zilizobaki ni kwa ajili ya ujenzi wa makaaazi ya wafanyakazi wa miradi itakayoanzishwa. Endelea kusoma habari hii

 “MKUZA UMEFELI”

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kukumbwa na mtikisiko wa kiuchumi ambao kwa kiasi kikubwa umezikumba nchi mbali mbali mkangazilizoendelea na kusababisha uchumi wa nchi hizo kuathirika. Mtikisiko huo umeelezwa kwamba umegusa katika sekta mbili zaidi ambapo sekta ya utalii na kilimo ndizo zilizoathirika kutokana na sekta ya utalii kupungua kwa idadi ya wageni wanaotembelea katika visiwani Zanzibar. Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema katika kikao cha baraza la wawakilishi wakati akijibu hoja za wajumbe wa baraza hilo waliochangia makadirio na matumuzi ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2009-2010. Endelea kusoma habari hii

SMZ YATELEKEZA MAENEO HURU

ASHASERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema wananchi wa Unguja na Pemba sasa wameanza kufaidika na fedha za wajasiri amali zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Rais Amani Karume maarufu kama mabilioni ya KJ. Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa lini wananchi wa Zanzibar watafaidika na fedha hizo kwa ajili ya kupunguza umasikini. Waziri Makame alisema hayo kwa niaba ya Waziri wa Kazi, Ajira, Maendeleo ya Wanawake na Watoto, Asha Abdallah juma ambaye kwa sasa hayupo nchini. Alisema fedha hizo zimeanza kutolewa Januari mwaka huu kwa vikundi mbali mbali ikiwemo SACCOS zinazo wajumuisha wanawake na wanaume ambao wameunda vikundi vyenye nia ya kuendesha miradi tofauti katika shehia zao. Endelea kusoma habari hii

UFISADI MKUBWA Z’BAR

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema zaidi ya shilingi 26 zainabmillioni zimeibiwa na wafanyakazi wawili wa Shirika la Bima Zanzibar. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu suala la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyeuliza iwapo serikali inafahamu kuwa kumekuwepo na udanganyifu mkubwa kwa baadhi ya wateja ambao husababisha fedha nyingi kupotea na kiasi gani cha fedha hizo zilizopotea. Waziri Mwadini alisema ni kweli serikali inalifahamu suala hilo na wizara ya fedha na uchumi imepokea mahesabu ya shirika la bima yaliokaguliwa kwa kila mwaka ambapo taarifa zinaonesha mapato na matumizi, madeni na mambo mangine. Akijbu swali la msingi la Mwakilishi huyo ambalo alitaka kujua kwa wateja na mafias waliobainika kuhusika na upotevu huo pamoja na adhabu gani watapewa baada ya kufanya vitendo hivyo vya udanganyifu, Waziri Mwadini alisema tayari serikali imewafungulia kesi watuhumiwa hao ambapo mmoja amefukuzwa kazi kutokana na wizi huo. Endelea kusoma habari hii.

 

 Z’BAR HAIPATIWI GAWIO LAKE

saidSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haipati gawio lake la kodi kutoka kwa tawi lolote lile la benki zilizopo visiwani Zanzibar. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali alitetaka serikali inapata kiasi gani cha fedha kutokana na uwekezaji wa mabenki yaliopo Zanzibar.“Serikali ya mapinduzi Zanzibar haipati gawio lake la kodi kutoka kwa tawi lolote lile la banki zilizopo hapa nchini, pamoja na kukosa mapato hayo vile vile inakosa mapato yatokanayo na faida ya uwekezaji kwa wateja wao haoa nchini” aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi Waziri huyo.Alisema kodi ya ushuru wa dhamana kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje, au kodi itokanayo na kipato cha mishahara kwa wafanyakazi wanaoajiriwa na mabenki hayo visiwani Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

SMT HAIISAIDII Z’BAR KIFEDHA

Ali Abdallah Ali(CCM)MfenesiniWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameambiwa sio kweli kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania husaidia bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kutenga fedha za matumizi.“Sio kweli kwamba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania husaidia bajeti ya SMZ kwa kutenga fedha za matumizi isipokuwa husaidia katika upatikanji wa fedha zinazotokana na washirika wa maendeleo kwa Tanzania kama ni msaada wa kibajeti (GBS) ambayo hutolewa kwa njia ya misaada (GBS Grants) au mikopo (GBS Loans).Akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua kama kuna ukweli wowote wa kuwa serikali ya muungano ndiyo yenye kutoa fedha za kusaidia bajeti ya Zanzibar, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame amesema hilo sio sahihi.Akijibu swali la kiasi gani cha mgao wakipatacho Zanzibar, Waziri huyo alisema serikali ya Zanzibar hupokea kiwango cha asilimia 4.5 ya fedha zote za misaada ya kibajeti inayotolewa kwa Tanzania kutoka kwa wafadhili.Endelea kusoma habari hii

 

SHERIA YA KODI ITAONGEZA UFANISI-SMZ

19 10 2009

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema uamuzi wa kuzifanyia Dk. Mwinyihaji Makame(CCM)marekebisho sheria za kodi Zanzibar una lengo la kuongeza ufanisi na uwajibikaji na kuondosha usumbufu kwa walipa kodi.Kwa mujibu wa mswada huo sheria hiyo itaweka adhabu kali kama faini, kifungo na utaifishaji wa mali itakayokamatwa ili kukomesha vitendo hivyo.Mswada huo una madhumuni ya kuiwezesha Serikali ni kuweka utaratibu mzuri wa kusimamia kodi zinazokusanywa Zanzibar ambapo pamoja na hayo utaweza kuwasajili walipa kodi ili waweze kuwafuatilia pamoja na kuhakikiwa itapotokea mlipa kodi kushindwa kufanya hivyo.Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akiwasilisha mswaada wa marekebisho ya usimamizi wa kodi zinazosimamiwa na bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi.Aidha alisema upo mkanganyiko mkubwa katika utoaji wa adhabu baina ya sheria moja na nyengine, mambo ambayo yanaleta matatizo makubwa kiasi ya bodi ya mapato kupata ugumu katika utekelezaji wa sheria zake.Endelea kusoma habari hii

PBZ IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA

19 10 2009

bWaziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini amesema hivi sasa benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imepata mafanikio makubwa baada ya kufikikia kiwango cha mtaji wa Sh. billioni tano kiwango ambacho kinatakiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).Hayo wameelezwa wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu maswali na majibu ya wajumbe mbali mbali waliokuwa wakitaka ufafanuzi kuhusiana na benki.Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali katika suali lake la msingi alitaka kujuwa iwapo kumekuwepo na mafanikio yoyote kwa benki hiyo na kama kumekuwepo na kiasi gani cha mikopo kwa wafanyakazi.Waziri huyo alisema tokea Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa fursaya mikopo kwa wafanyakazi wa serikali mwaka 2002 hadi kufikia mwezi wa juni maka 2009 tawi la Chake Chake Pemba limeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi billioni 10.077 kwa jumla ya wateja 10,109.Alisema katika kipindi cha robo mwaka ambacho kimeishia mwezi wa machi 2009 tawi hilo la chake chake limetoa mikopo yene thamani ya shilingi billioni 1,126 kwa wafanyakazi 603.Waziri huyo alisema katika mikopo iliyotolewa na benki tokea kuanzia mwaka 2002 hadi kufikia mwezi wa machi 2009 banki imepata faida ya shilingi 2.131 billioni.Endelea kusoma habari hii

SERA YA UTALII ITAINGIZA MAPATO

19 10 2009

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kupitishwa kwa sera ya cutalii ni moja ya maandalizi mazuri ya kuhakikisha sekta hiyo inakuwa moja ya muhimili wa uchumi wa nchi na kuingiza mapato.Hayo yameelezwa katika kikao cha baraza la wawakilishi na Waziri wa Utalii,Uwekezaji na Biashara, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifanya majumuisho ya mswaada wa kufuta sheria ya kamisheni nao 9 ya mwaka 2996 na kutunga sheria mpya ya utalii Zanzibar.Waziri Samia alisema mikakati ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ni kuendeleza sekta ya utalii kwa kutumia utaalamu unaokubalika duniani kote ikiwemo kuimarisha utalii wa mazingira na utamaduni.“Katika sheria mpya ya utalii tunakusudia kuimarishga utalii wa mazingira na utamaduni ambao nafasi yake katika kuingiza watalii ni kubwa sana”alisema Samia.Alisema katika mswada huo nafasi ya wananchi wazalendo katika kuendeleza sekta ya utalii imepewa kipaumbele cha kwanza kuona wananchi ndiyo wanaoendesha biashara hiyo kwa faida yao na vizazi vijavyo.Samia alisema ndio maana kamisheni ya utalii ya Zanzibar ikatenga maeneo ya Paje, Bwejuu pamoja na Jambiani ni maalumu kwa ajili ya kutumiwa na wananchi wazalendo kuendeleza biashara zao na wazalendo wamekuwa wakisaiodiwa zaidi iliw aweze kujimarisha kibiashara zaidi.Endelea kusoma habari hii

SERIKALI ICHUNGUZE WAKWEPA KODI

19 10 2009

Mustafa Mohd Ibrahim(CCM)Mkuu w amkoa kusini ungujaWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameishauri serikali ya mapinduzi Zanzibar kusimamia suala zima la kodi kwa kuwa kumekuwepo na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi katika mahoteli ya kitalii na baa. Ushauri huo umetolewa na wajumbe mbali mbali wakati wakichangia mswaada wa kufuta sheria ya kamisheni no 9 ya mwaka kwa vijisheria vidogo vidogo ili kuleta ufanisi wakati wa kukusanya kodi. Wajumbe wao pia wameishauri Serikali kuweka sheria moja ya kodi itakayosimamia pahali pamoja kuliko kuwepo utitiri wa ukusanyaji wa mapato unaoleta usumbufu kwa walipa kodui na wageni visiwani hapa.Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mustafa Mohammed Ibrahim amesema hayo wakati akichangia mswaada wa sheria ya kodi katika kikao cha baraza la wawawakilshi kinachoendelea Mjini Unguja ambapo alisema walipa kodi wamekuwa wakisumbuka sana katika ulipaji kodi kwa kuwa kumekuwepo na utitiri wa kulipa kodi sehemu nyingi lakini na kuna watu wanakwepa kulipa kodi.“Vifungu vingi vimefutwa katika sheria na kuna vyengine vimebakia, kwa vile sheri hizi zote pamoja na sheria kubwa zote zinazungumzia kodi kwa nini zisikusanywe pahali pamoja ikawa ni moja kubwa inayozungumzia mambo ya kodi” alihoji Kiongozi huyo.Endelea kusoma habari hii

SMZ KUPIGA MARUFUKU MISUMENO

19 10 2009

KUFUATIA uharibifu mkubwa wa mazingira na ukataji wa miti kiholela kSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itapiga marufuku misumeno yote ya kukatia miti kutumika visiwani Zanzibar.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira,Khatib Suleiman Bakari aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa viti maalumu wa (CUF) Mwanajuma Faki Mdachi aliyetaka kujuwa kwa nini serikali haipigi marufuku misumeno hiyo ambayo inaonekana kuwa tishio kubwa katika suala la kuhifadhi mazingira.Naibu huyo alisema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar lengo lake ni kuhifadhi mazingira na kuyatunza hivyo ina mpango huo wa kupiga marufuku kwa kuwa imeshabainika kuwa athari kubwa za kimazingira zinatokana na kukatwa kwa miti ovyo.Bakari alisema serikali imebaini kuwepo kwa kasi ya ukataji miti ya aina mbali mbali huku wananchi wengi wakiwa wanakimbilia katika kufanya kazi hiyo ya kukata miti ovyo bila ya kujali athari zake za kimazingira jambo ambalo linaweza kusababisha jangwa kwani miti yote ikishakwatwa kutakuwa hakuna miti na kukosekana kwa mvua nchini.Alisema wananchi wengi hivi sasa wamehamasika na elimu inayotolewa na ukataji wa miti lakini bado wapo watu wachache ambapo wanatumia misumeno ya moto kwa kukata miti mikubwa ambayo hutegemewa kwa matumizi ya kutunza mazingira.Endelea kusoma habari hii

MGAO HAUTUHUSU ZNZ -SMZ

19 10 2009

mansourSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mgao wa umeme ulionaza huko Tanzania Bara hautovikumba visiwa vya Zanzibar kwa kuwa wao ni walipaji wazuri huduma hiyo.Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kasssim Mzee aliwaambia waandishi wa habari nje ya ukumbi wa baraza la wawakilishi jana waliotaka ufafanuzi kuhusiana na mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa katika sehemu mbali mbali za Tanzania bara.“Huo mgao sisi hautotukumba kwa sababu sisi ni walipaji wazuri tu wa huduma hiyo na hivyo suala la mgao ni huko Tanzania bara kwetu sisi tumesalimika katika suala hilo” alisema Mzee.Alisema Zanzibar inalipa kiasi cha shilingi 1.2 billioni kila mwezi kuilipa shirika la TANESCO hivyo haoni kama kuna sababu ya kupewa mgao huo ambao hutolewa hivi sasa katika maeneo mbali mbali ikiwemo mikoani.Mzee alisema Zanzibar kwa wastani wa matumizi ya umeme huwa inatumia karibu megawati 47 kiwango ambacho kinatosha kwa matumizi ya kawaida kinatosha sana.“Nadhani mgao wa umeme uliopo Tanzania Bara kwa sasa hautoathiri Zanzibar….sisi matumizi yetu tunayopewa ya umeme yanatosheleza kwa ujumla na hakuna sababu ya kukatiwa umeme kwa sasa”’alisema Tafana.Endelea kusoma habari hii

MAPATO YA SERIKALI YATIZAMWE-UPINZANI

16 10 2009

KAMBI ya upinzani katika baraza la wawakilishi imesema bila ya kuwepo Rashid Seif Suleiman(CUF)Ziwanimazingira mazuri ya kudhibiti ukusanyaji wa fedha na mapato yanayotokana na biashara ya utalii itakuwa ni ndoto ya mafanikio katika sekta ya utalii. Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo, Waziri Kivuli wa Utalii, Biashara na Uwekezaji Zanzibar, Muhiddin Muhammed Muhiddin alisema ni vyema serikali ikazingatia suala hilo kwani kumekuwepo na udhaifu mkubwa katika ukusanyaji wa fedha za umma.“Kutokana na hali ya mambo yanayoendeshwa kiutashi na sio kwa kufuata maelekezo ya sheria mama hali hiyo inahatarisha katika sheria inayofutwa kumekuwepo na udhaifu mkubwa wa ukusanyaji wa mapato yanayotokana na biashara ya utalii, wasiwasi wangu ni kwamba hilo litaendelea hata sheria hii ikipita kwani sikuona kipengele kinachozungumzia udhibiti huo na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mkorofi atakapojitokeza” amesema Waziri Kivuli.Waziri Kivuli huyo ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile (CUF) Muhiddin alisema suala la mazingira na udhibiti wa takataka zinazotoka mahotelini pamoja na maji machafu ni miongoni mwa mambi yanayompa mashaka katika utekelezaji wake.Endelea kusoma habari hii

WEZI WA MISHAHARA WADHIBITIWA

16 10 2009

Dk. Mwinyihaji Makame(CCM)SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wafanyakazi hewa baada ya kutumia mfumo mpya wa kutumia compyuta kwa wapokeaji mishahara kupitia benki.Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi aktika kikao kinachoendelea Mjini hapa wakati akijibu maswali na majibu yalioulizwa katika kikao hicho.Mwadini amesema ni kweli katika utaratibu wa zamani kulikuwa na tatizo sugu la kupotea mishahara ya wafanyakazi baada ya kutokezea wafanyakazi hewa lakini chini ya mfumo mpya suala hilo limeweza kudhibitiwa.“Nadhani nikiri kwamba hapo nyuma tulikuwa na hili tatizo sugu la wafanyakazi hewa lakini baada ya marekebisho haya ya mfumo mpya wa kutumia payment system imetusaidia sana na wizi hizi sasa tumeudhibiti kila mtu anakwenda kuchukua mshahara wake benki bila ya matatizo yoyote na utaratibu huu ndio tunaoendelea nao hivi sasa” alisema Mwadini.Akijibu swali la msingi aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Nungwi (CCM) Ame Ussi Juma aliyetaka kujua kwamba kumekuwepo na utaratibu wa wafanyakazi wa serikali kupokea mishahara yao benki ya watu wa Zanzibar lakini utaratibu huo una malengo gani na utazihusisha wizara ngapi, Mwandini alisema lengo kuu la kuanzishwa utarayibu huo kwa wafanyakazi ni kudhibiti ubadhirifu.Endelea kusoma habari hii

UTALII NI SEKTA KIONGOZI-SMZ

16 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema sekta ambayo inaonesha Samia Suluhumatumaini makubwa na kuchangia katika ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi ni sekta ya utalii.Akiwasilisha mswada katika kikoa cha baraza la wawakilishi wa kufuta sheria ya kamisheni no 9 ya mwaka 1996 na kutunga sheria mpya ya utalii Zanzibar, Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan amesema utalii ndio sekta muhimu kwa Zanzibar hivi sasa.Alisema mipango yote ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini imetambua mchango mkubwa wa sekta ya huduma hasa ya utalii baada ya kutegemea sekta chache za biashara na kilimo hasa zao la karafuu ambalo limenaguka bei katika soko la dunia.Waziri huyo alisema biashara ya utalii kwa visiwani Zanzibar inasimamiwa na sheria namba 9 ya mwaka 1996 baada ya kuitekeleza sheria hiyo kwa muda mrefu, kubadilika kwa hali ya utalii na usimamizi wake pamoja na mipango ya kitaifa ya kuondoa umasikini na kukuza uchumi.Alisema serikali imeona ipo haja ya sheria hiyo kuifanyia mabadiliko kwa kutunga sheria mpya ya utalii itakayoendana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa biashara hiyo na usimamizi wake kwa ujumla.Aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo sehemu ambayo zitafanyiwa mabadiliko ni pamoja na muundo wa uongozi wa kamisheni chini ya sheria iliopo sasa ambapo uongozi wake upo chini ya mwenyekiti ambae hana bodi ya wakurugenzi, katibu mtendaji akisaidiwa na wakurugenzi wawili jambo ambalo halileti mtiririko mzuri wa usimamizi wa chombo kikubwa na muhimu kama hicho.Endelea kusoma habari hii

HATUTATIA ULIMI PUANI-SMZ

16 10 2009

Mansour Yusuf HimidSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kamwe haitaweka ulimi puani kama ngo’mbe katika suala la mafuta na gesi asilia kusimamiwa na mamlaka ya wazanzibari wenyewe.Akizungumza katika kikao cha baraza la wawakilishi katika kipindic ha maswali na majibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi Mansour Yussuf Himid aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba utaratibu na azma ya kulisimamia suala la magta na gesi asilia upo pale pale na hakuna kitu kilichobadilika hadi sasa.“Nataka mfahamu vizuri sana kwamba kamwe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitageuka ngombe kutia ulimi puani dhamira na lengo letu lipo pale pale na tumo katika matayarisho mazuri sana” alisema Himid huku akishangiriwa na wajumbe wote wa pande mbili katika baraza hilo.Akijibu maswali la ngongeza aliyoulizwa na wajumbe hao kwamba kwa nini katika kikao hiki haukuletwa mswaada kuhusiana na suala la mafuta kama ilivyaohidiwa katika kikao kilichopita, Himid aliwatoa khofu wajumbe hao na kuwataka wavute subra kidogo hadi katika kikao kijacho ambapo kazi hiyo itakuwa imeshakamilika.“Ni kweli tulisema katika kikao kilichopita kwamba tutaleta sera ya nishati ya Zanzibar lakini niwatoa khofu kuwa dhamira ipo pale pale na sera tutaileta bila ya khofu wala wasiwasi kwani ikishakamika mara moja aktika kikao kinachokuja inshaallah mtaiona na tutaijadili kwa pamoja kwa maslahi ya nchi yetu” alisema Himid.Endelea kusoma habari hii

SMZ LENGO NI KUPOKEA WAGENI ZAIDI

16 10 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kupokea wageni millioni mbili kwa mwaka ifikapo mwaka 2015 hadi 2020 baada ya kukamilisha viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba.Malengo hayoMzee Ali Usi (CCM) Chaani yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Mawasiliano na Uchukuzi), Machano Othman Said wakati akijibu swali na nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman aliyetaka kujua mikakati ya kukifanyia ukarabati viwanja cha ndege cha Karume imefikia wapi.Said alisema lengo la serikali ni kuvifanyia ukarabati mkubwa viwanja vyake vyote viwili ili viweze kupokea wageni kutoka nje ya nchi ambao wataweza kuisaidia sana Zanzibar kimapato kwa kuwa hivi sasa wageni wanaofika Zanzibar wanafikia laki tano kwa mwaka.Alisema uwanja wa ndege wa Karume uliopo Pemba utafanyiwa ukarabati mkubwa na kuweza kufikia hadhi yakimataifa ambapo utakapokamilika utaweza kutoa nafasi kubwa ya kupokea wageni kwa kuwa lengo ni kuupanua zaidi katika maeneo yake yote ya uwanja huo.Waziri huyo alisema tayari serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imefanya mawasiliano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) katika kukifanyia ukarabati kiwanja che ndege cha Karume kwa ajili ya kuweka taa za uwanjani na matengenezo mengine.Endelea kusoma habari hii

CCM NA CUF NI WAMOJA-SPIKA

Pandu Ameir Kificho(Spika)SPIKA wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amesifu mashirikiano mazuri yaliooneshwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Wananchi (CUF) katika baraza la wawakilishi hasa wakati wa utekelezaji wa majukumu katika baraza hilo.Kificho alisema hayo wakati alipokutana na Balozi mdogo wa Ujarumani nchini, Clement Hach aliyefika ofisini kwake Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi kusalimiana naye na kuzungumzia masuala mbali mbali kisiasa kwa lengo la kubadilishana mawazo.Spika Kificho alisema kwa kadri siku zinavyokwenda yamekuwepo mashirikiano mazuri kati ya wajumbe wa baraza hilo ambao ni kutoka vyama viwili vikuu vilivyopo hapa Zanzibar ambavyo ni CUF na CCM.Alisema moja ya kazi nzuri inayofanywa na wajumbe hao kwa pamoja ni kazi zile za kamati za baraza la wawakilishi mbali mbali za kufuatilia shughuli za serikali ambapo wajumbe wake ni kutoka pande mbili za vyama hivyo ambapo hufanyika vyema bila ya kujali misingi na itikadi za vyama vyao.Endelea kusoma habari hii

SIRUHUSA KUWEKA MATUTA-SMZ

machanoSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewaonya wananchi wanaojichukulia sheria mikononi mwao kwa kuweka matuta katika barabara bila ya kushauriana na wizara inayohusika kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha migongano isiyokuwa ya lazima.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Mawasiliano na Uchukuzi, Machano Othman Said alipkuwa akijibu maswali na amjibu katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza jana Maisara Mjini Unguja.Said alisema wapo baadhi ya watu hivi sasa wamekuwa wakiweka matuta katika barabara zao bila ya kushauriana na wizara ya mawasiliano na kusema kwamba jambo hilo ni kinyume cha sheria na halikubaliki kwa kuwa serikali ndio mamlaka ya kuweka matuta katika sehemu ambayo inaona kuwa inafaa.“Wananchi wa wengine wanaweka matuta katika barabara bila ya kuishauri serikali jambo hilo halikubaliki na ni kinyume na sheria na taratibu za barabara kwa hivyo tunawambia wananchi wa barabra ya mshelishelini kuelekea pwani mchangani wamefanya makosa kuweka matuta bila ya kuishirikisha serikali” alisema Said huku baadhi ya wajumbe wakicheka.Waziri huyo amesema mbali ya wananchi kuweka matuta barabarani lakini wapo baadhi yao wamekuwa wakiiba alama za barabarani na kuwataka waache tabia hiyo kwani viashiria vya usalama barabarani ni muhimu na kuviondoa kunaweza kusababisha ajali na matukio mengine ya hatari.Endelea kusoma habari hii

WIZARA HAIFAHAMU VIGEZO-MZEE

zNaibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee amesema wizara yake haiwezi kujua ni kigezo gani kilichotumika kwa wafanyakazi wa baraza la manispaa kuwatoza madereva wa gari zinazoegesha katika bustani ya Mji Mkongwe Zanzibar.Mzee alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM), Ali Suleiman Ali aliyetaka kuelezwa ni kigezo gani kilichotumika kwa baraza la manispaa kuwatoza madereva kiasi cha shilingi 1000 wanaokwenda kuegesha magari yao kando ya bustani mpya ya forodhani iliopo Mji Mkongwe Mkoa wa Mjini Magharibi.Amesema kiwango cha kutozwa shilingi 1000 ni kikubwa na haoni sababu ya kiwango hicho wakati maeneo mengine ya mji mkongwe hutozwa shilingi 200 kwa kuegesha gari katika eneo lolote la mji huo.Mwakilishi huyo pia ameiomba serikali kuyaangalia upya maeneo ya ngambo kwa ajili ya kuwatengenezea bustani kwani baadhi ya bustani zimekwua zinakufa bila ya kushughulikiwa na wananchi wamekuwa wakifuata bustani ya forodhani amabyo ipo mbali na makaazi yao wanayoishi.Akijibu swali hilo Naibu Waziri alisema ni kwlei wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakipendelea sana kukaa katika maeneo ya bustani lakini bustani za michezani na jamhuri zimekuwa hazikidhi kiwango cha kuitwa bustani kwa kuwa hazijafanyiwa matengenezo mazuri kama ilivyo bustani ya forodhani lakini aliahidi serikali kwa kushirikiana na wataalamu wake watalifanyia kazi suala hilo.Endelea kusoma habari hii

KESI 132 ZA MADAYA YA KULEVYA HAZINA HATIA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema jumla ya kesi 132 za shawanmadawa ya kulevya zimeendeshwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar na hakuna hata mtu mmoja aliyehukumiwa kifungo katika kesi hizo.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar, Sultani Mohammed Mugheiry amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu maswali na majibu katika kikao cha baraza la wawakilishi Mjini Unguja.Mugheiry alitasema hayo baada ya swali la msingi aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua ni watu wangapi walioshitakiwa na kuhukumiwa na kifungo kuanzia januari hadi septemba mwaka huu.Waziri Mugheiry alisema kwa mujibu wa takwimu zilizopo katika vyombo vya sheria ndani ya kipindi kilichoanzia mwezi wa jenuari hadi septemba 2009 kesi zilizoendeshwa za madawa ya kulevya bi 132 na kesi 49 zimeshatolewa hukumu katika mahakama ya Zanzibar ambapo hakuna mtu aliyehukumiwa kifungo.Akiuliza kwali la ngongeza Mwakilishi huyo alitaka kujua iwapo dawa hizo zilizokamatwa baada ya utafiti imegundulika kuwa si dawa za kulevya?, waliokamatwa na madawa hayo ni watoto wadogo na ndio wakaachiwa au wafanyabiashara hao ndio kwanza wanaaza biashara hiyo na ndio maana wakaachiwa waendelee kujiimarisha zaidi.Endelea kusoma habari hii

HATUNA TAARIFA YA KUZAGAA KONDOM-SMZ

fatmaSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kwamba haina taarifa za kuzagaa kwa mipira ya kondom katika maeneo ya shule zinazotumiwa na wanafunzi wa masomo ya ziada (tuitions)Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Jabir Makame alipokuwa akijibu maswali na majibu ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotaka kujua iwapo kuna mafunzo maalumu ya kutumia mipira ya kondoma amabyo hupewa wanafunzi wa shule.Makame alisema kwamba moja ya mafunzo wanayopewa wanafunzi ni kujiepusha na ngono za mapema na kujizuwia kufanya ngono wakiwa na umri mdogo na sio kutumia mipira ya kondom lakini suala hilo la utumiaji wa mipira ya kondoma serikali haijui wala wizara yake haina taarifa hizo.Mwakilishi wa Jimbo la Koani (CCM) Haji Mkema Haji ndiye aliyeuliza swali hilo la nyongeza ambapo alitaka kuelezwa iwapo mipira ya kondom ni sehemu ya mafunzo yanatofundishwa mashuleni kwa vitendo au laa kwa kuwa baadhi ya shule zinazosomwa na wanafunzi wa kujiendeleza vimekuwa vikipatikana mipira ya kondom ikiwa nje ya shule hizo.Endelea kusoma habari hii

UCHOMAJI TAKATAKA NI HATARI-WAJUMBE

WIZARA ya Afya na Utawi wa Jamii Zanzibar imesema hivi sasa itachukua hatua madhubuti ya kuhakikisha takataka zote zinazotokana na mwili wa jidawibinaadamu zinadhibitiwa ipasavyo na hazitawaathiri wagonjwa.Hayo yameelezwa na Waziri wa wizara hiyo, Sultan Mohammed Mugheiry wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujua iwapo serikali ina mpango gani juu ya takataka zinazotokana na miili ya binaadamu haziwakeri wagonjwa wakati wa uchomaji wake.Mwakilishi huyo alisema takataka za hospitali kuu ya mnazi mmoja huchomwa karibu na hospitali hiyo wakati wa usiku na kupelekea harufu mbaya hadi siku ya pili kwa kuenea hadi hospitali na kuleta usumbufu mkubwa kwa wagonjwa na wananchi wanaokwenda kuwakagua wagonjwa wao. Waziri huyo alisema anakubaliana na Mwakilishi huyo kwamba takataka hizo huchomwa nyakati za usiku na harufu mbaya huwasimbua wagonjwa lakini wizara yake kupitia uongozi wa hospitali ya mnazi mmoja umechukua hatua mbali mbali za kuwakinga wagonjwa na moshi pamoja na harufu mbaya hivi sasa.Endelea kusoma habari hii

KIKAO CHA BARAZA CHAANZA LEO

Ali Mzee Ali(CCM)kuteuliwaKIKAO cha Baraza la Wawakilishi kinaanza leo hii Maisara Mjini Zanzibar kikitarajiwa kujadili mambo mbali mbali ikiwemo jumla ya miswaada sita ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao hicho.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Mwandishi wa Habari za Baraza hilo, Talib Enzi Talib amesema matayarisho ya kikao hicho yote yameshakamilika ikiwemo takriban wajumbe wote wameshawasili kutoka kisiwani Pemba kujumuika na wenzao wa Unguja kwa lengo la kuhudhuria kikao hicho ambacho kitachukua wiki mbili.Kikao hicho ambacho ni mkutano wa 17 kutawasilishwa mswaada sita ikiwemo maswali na majibu ambapo mapendekezo ya mswada wa sheria utaodhibiti usafirishaji fedha haramu na mapato ya uhalifu na mambo mengineyo.Miswada mingine ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao hicho ni pamoja na wa Sheria ya Kukuza Utalii, Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sheria ya Kubadili Sheria ya Bodi ya Mapato, Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na sheria ya Dawa za Kulevya na kudhibiti usafirishji haramu wa dawa hizo.Kutokana na mswaada huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inakusudia kuanzisha Kitengo cha taarifa za fedha na Kamati ya Kitaifa, ambayo itaweza kuwanasa wasafirishaji wa fedha haramu na mapato ya vitendo vya uhalifu, zikiwemo fedha za mitandao ya ugaidi.Endelea kusoma habari hii

KUIFUTA SMZ NI UHAINI-WAZIRI

Waziri wa Nchi katika Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma amesema kuwa matamshi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa suluhu ya matatizo ya Muungano wa Tanzania itapatikana kwa kuondoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ya kihainiHayo ameyaeleza mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wakatin akizungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi siku ya kufunga kikao cha Bajeti, Waziri Juma alisema Hamza Hassan Juma (CCM) Kwamtipuramatamshi ya Pinda yanafaa kuchukuliwa hatua na vyombo vya kisheria.Juma alisema “ Unaposema utaifutilia mbali Serikali ya Zanzibar ni uhaini. Sisi tunasema kuwa vyombo vya ulinzi vipo na kwa hivyo vitafanya kazi zao..na mwenye kusema maneno hayo ni shauri yake.”Pinda alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akijibu suala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano jambo ambalo limewakasirisha sana wajumbe wa Baraza hilo ambao walitaka kujua ni kwa nini Serikali ya Zanzibar haijatoa tamko lolote lile.Juma alisema, “ Kwa hakika si yeye tu Pinda lakini watu wengi sana wana hamu kutaka.Zanzibar isiwepo katika ramani ya dunia. Na kusemwa yashasemwa mengi na yatasemwa mengi, lakini kutekelezwa ni vigumu.”Akishangiriwa na Wajumbe wa Baraza hilo Juma alisema haitawezekana kabisa kuiondosha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar labda iwe kwa kile alichokiita “ mtutu wa bunduki.”Endelea kusoma habari hii.

MJADALA WA MAFUTA HAUTAKI JAZBA-NAHODHA

Shamsi Vuai Nahodha(CCM)WAZIRI Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha amesema kwamba mjadala wa mafuta na gesi asilia hakuhitajiki jazba katika kufikia ufumbuzi wa suala hilo iwapo lipakie aktika orodha ya mambo ya muungano au liondolewe na kusimamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Nahodha aliyasema hayo wakati akiakhirisha kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, ambapo alisema jambo hilo linahitaji busara zaidi kuliko jabza.Msimamo huo wa Waziri Kiongozi unaonekana kwenda kinyume na hoja nyingi za wajumbe wa baraza la wawakilishi ambao mara kwa mara wamekuwa wakisisitiza kwamba uamuzi wa kuliondoka suala hilo katika orodha ya mambo ya muungano halihitaji mjadala zaidi ya utekelezaji.Tayari baraza la wawakilishi pamoja na baraza la mapinduzi limeamua kuliondoa suala hilo katika muungano, lakini maamuzi hayo yanaonekana kupingana na hutuba ya waziri kiongozi.Nahodha alisema kamwe suala hilo halitaachwa kuweza kusababisha kuvuruga amani na utulivu uliopo ambao kwa muda mrefu serikali ya Tanzania iansifikana kwa kuwa na hali ya mani ya utulivu katika Bara la Afrika.Endelea kusoma habari hii

CUF WAKASHIFIANA BARAZANI

OPERESHENI Zinduka ya Chama cha CUF, imeingia doa baada ya Abass Juma Mhunzi (CUF)ChambaniMwakilishi wa Jimbo la Chambani Abass Juma Muhunzi na Abubakar Khamis Bakary kurushiana ‘makombora’ ya shutuma Barazani.Kwa upande wake,Muhunzi alidai kuwa Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Abubakar Khamis Bakary na wenzake wamemuundia zengwe akataliwe Jimboni kwake.Mwakilishi huyo alitoa matamshi hayo juzi alipochangia hotuba ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi katika kikao cha Baraza hilo kinachoendelea Mjini UngujaMwakilishi huyo alitoa shutuma hizo baada ya wajumbe wa Baraza hilo kurudi safari ya kimichezo mjini Dodoma ambapo ilidaiwa kuwa Upinzani uliisusia safari hiyo na yeye kujikuta akiwa peke yake safarini.Miezi michache iliyopita, viongozi hao walitupiana maneneo ya kashfa hadharani kila mmoja akidai kumshutumu mwenzake baada ya kuwepo tuhuma nzito za wizi wa fedha zilizoelekezwa kwa Muhunzi.Endelea kusoma habari hii.

VIASHIRIA VYA UFISADI VYAGUNDULIKA ZNZ

Dk. Mwinyihaji Makame(CCM)UKOSEFU wa kumbukumbu za matumizi ya fedha na mali za serikali matatizo ambayo ni viashiria vya ufisadi ni miongoni mwa kasoro kadhaa ambazo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amezibaini katika idara nyingi za serikali ya Zanzibar katika mwaka wa fedha wa 2007/8. Akiwasilisha ripoti hiyo katika kikao cha baraza la wawakilishi, Waziri wa Nchi (Katiba na Utawala Bora) Ramadhani Abdallah Shaabani alisema kuwa bado matatizo yapo ya kiuntendaji katika taasisi na idara za serikali. “Mheshimiwa Spika, Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu za Serikali amegunduwa kuwa idara nyingi za serikali hakuna daftari la kumbukumbu ya mali za serikali, kwa hivyo kukosekana taarifa sahihi ya mali yakiwemo, magari and mashamba ambayo pia hayana hati (title-deed),” alisema Ramadhani. Alisema Mkaguzi aligunduwa kuwepo kwa makusanyo ya fedha ambazo hazikupelekwa benki, matumizi ya fedha za masurufu (imprest) bila marejesho, na kuchelewa kuwasilishwa kwa taarifa katika idara za serikali.Endelea kusoma habari hii.

SERIKALI ICHUNGUZE-WAJUMBE

WAJUMBE wa Baraza wameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar rayakufuatilia kwa kina upoteaji wa watoto wadogo katika maeneo mbali mbali pamoja na kushughulikia suala la utumiaji wa madawa ya kulevya nchini.Wajumbe hao wakichangia bajeti ya Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Unguja wamesema hivi sasa kumezuka wimbi kubwa la kupotea kwa watoto wadogo.Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake (CCM), Raya Suleiman Hamad, alisema kuna haja kwa serikali kuanzisha uchunguzi huo kwani watoto wamekuwa wakipotea ovyo katika mitaa yao huku wazazi wao wakiwa wanahangaika kuwatafuta bila ya mafanikio.Alisema kwamba inavyonekana wapo baadhi ya watu wanaoendesha biashara ya kuiba watoto jambo ambalo tayari limeanza kuwatia hofu baadhi ya wazazi nchini.Mwakilishi huyo alisema kwamba watu wanaoendesha vitendo hivyo hutumia njia za kuwahadaa kwa kuwafuata watoto na kuwapa fedha kisha huwaambia wawafuate ili wakawanunulie nguo.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WAMLAANI PINDA

PINDAWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamewataka wazanzibari kulaani kwa nguvu zote matamshi yaliotolewa jana na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ya kutaka kuifuta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)na kubakia serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Matamshi hayo yametolewa na wajumbe hao wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.Wawakilishi hao walisema Waziri Mkuu Pinda ni Kiongozi asiyeitakia mema Zanzibar kutokana na kauli zake za mara kwa mara za kuidharau na kuikejeli serikali ya mapinduzi ambapo walisema wanalaani matamshi hayo lakini pia wamewataka wanzanziri wote kulaani vikali matamshi yake aliyoyatoa juzi bungeni.Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu (CCM) Haji Omar Kheri amemtaka Waziri Mkuu Pinda aanze kujizuia kutoa matamshi yake yanayoiweka Zanzibar katika wakati mgumu na wasiwasi wa utatanishi.Kheri ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema kutokana na Zanzibar kuwa na nia njema na Muungano ilisamehe na kukubali kupoteza hata Utaifa na utambulisho wake kwa kuungana na Tanganyika mwaka 1964, jambo ambalo alisema halionekani kuthamininwa na Watanganyika hivi sasa.Endelea kusoma habari hii

NAHODHA AMVAA BALOZI KARUME

Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai Nahodha amekana kubebwa katika nafasi ya uwaziri kiongozi kama ilivyodaiwa hivi karibuni na vyombo vya habari.Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya baraza la DSC03487wawakilishi Maisara Mjini Unguja kufuatia kauli zilizotolewa na Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Ali Abeid Karume katika mahojiano maalaumu na gazeti mmoja linalochapishwa wiki mara moja nchini kuhusu nafasi ya urais wa zanzibar.Juzi gazeti moja litolewalo kila wiki liliripoti kwamba Balozi wa Tanzania Nchini Italia Ali Abeid Karume alisema kwamba wadhifa wa aliopewa waziri kiongozi ni wa kubebwa tu.“Kama mtu anasema mimi nimeokotezwa na kubebwa sasa ajiulize yeye amefika hapo kwa uwezo wa nani….hata yeye alibebwa na na kufanyiwa hivyo na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye alimchagua kuwa balozi katika kipindi cha miaka kumi ya urais wake na sasa ni Rais Jakaya Kikwete ambaye amemchaguwa kubwa balozi wa Tanzania nchini Italia au amesahau hilo” alihoji Nahodha ambaye anaonesha hakufurahishwa na kauli ya Balozi Karume.Endelea kusoma habari hii

WANAUME WALALAMIKIWA

Jua_kali_market_znzTABIA ya wanaume kufanya biashara za aina zote imelalamikiwa na baadhi ya wajumbe wanawake katika baraza la wawakilishi Mjini Zanzibar.Mwakilishi wa Viti Maalumu Wanawake (CCM) Ashura Abeid Faraji ameyasema hayo alipokuwa akichangia hutuba ya bajeti ya maendeleo ya vijana, wanawake na watoto ya mwaka wa fedha wa 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.Mwakilishi huyo alihoji iwapo kila biashara inayobuniwa Tanzania wanaume ndio kwa kwanza kuikimbilia na kutaka wao ndio wawe wataitekeleza wanawake watafanya biashara gani katika ulimwengu huu ambao una ushindani mkubwa wa kibiashara.Alisema wanawake wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na kuwa na majukumu makubwa ya kifamilia na hivyo kutaka kuwezeshwa kwa kupewa mikopo na kusaidiwa zaidi katika kujikwamua na umasikini.“Kazi zote zinazobuniwa waneume wao ndio wa kwanza kukimbilia sasa wanwake wao watauza nini ikiwa hata shanga wanaume wanaziuza wakati ilipaswa kuuzwa na wanawake? Mheshimiwa spika bora wanawake wapewe mikopo kwa ajili ya kumudu hali ya maisha” alisema Mwakilishi huyo ambaye ana miaka zaidi ya 70.Endelea kusoma habari hii.

MAOMBI KADHAA YAPOKEWA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema jumla ya maombi 1,034 yamepokelewa kwa ajili ya mchanganuo wa kupata fedha za mfuko wa bi ashauwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa uapnde wa Unguja na Pemba.Waziri wa kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma aliyasema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar.Alisema mfuko huo ulichelewa kuanza kutoa mikopo kwa sababu mbali mbali ikiwemo kwanza kutoa mafunzo kwa watendaji wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa (masheha) na vikundi vya wazalishaji ambavyo vitapatiwa mikopo hiyo ili wakipewa fedha waweze kuzitumia kwa malengo yaliokusudiwa.Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba hadi sasa jumla ya maombi 1,034 yamepokelewa ambapo kati ya hayo 799 kwa upande wa Unguja na maombi 235 yamewasilishwa kutoka katika kisiwa cha Pemba.Alisema hadi kufikia Mei mwaka huu jumla ya shilingi millioni 184.3 zimetolewa kupitia mfuko huo kwa vikundi vilivyounda SACCOS pamoja na watu binafsi ambao wamewasilisha masharti ya maombi ya kupata fedha hizo.Endelea kusoma habari hii

WAJUMBE WAFURAHISHWA NA BARABARA

Hasnuu Mohd Haji(CCM)kuteuliwaBAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika uimarishaji wa miundo mbinu ya barabara Unguja na Pemba.Hayo yameelezwa na wajumbe hao wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara ya mawasiliano na uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rais, (CCM) Hasnuu Mohamed Haji alisema serikali imefanya kazi kubwa katika miundo mbonu kwa kuzifanyia ukarabati barabara za kisiwa cha Pemba ambazo zilikuwa katika hali mbaya.Alisema miundo mbinu ya barabara katika kisiwa cha Pemba zilikuwa zimetengenezwa kwa kiwango cha lami lakini hivi sasa zimo katika mchakato wa kumalizika kabisa jambo ambalo linapaswa kupongezwa seriakli kwa kutekeleza ilami yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.“Juhudi kubwa zimechukuliwa katika ukarabati wa barabara pamoja na nyengine kujengwa kwa kiwango cha lami hata mfuko wa barabara umefanya kazi kubwa kuzikarabati baadhi ya barabara kwa hili nadhani tunapswa kushukuru serikali yetu” alisisitiza Mwakilishi huyo.Endelea kusoma habari hii

VYOMBO VYA HABARI VYA SERIKALI VYAPONDWA

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamesikitishwa na hali mbaya ya uwezo wa utendaji kazi wa vyombo vya habari vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inamiliki vyombo Fatma Tamim(CCM)vitatu vya habari ikiwemo Televisheni Zanzibar (TVZ), Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) na Gazeti la Zanzibar Leo gazeti ambalo lisilo na rangi (black and white) ambalo huchapishwa kila siku nchini.Wajumbe wamesema hayo walipokuwa wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya habari utamaduni na michezo katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoenelea Maisara Mjini Unguja.Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF) Said Ali Mbarouk alisema kwamba licha ya kuwa ni televisheni Zanzibar (TVZ) kuitwa ni televisheni ya taifa lakini katika kisiwa cha Pemba hakuna mawasiliano ya kituo hicho jambo ambalo alisema haipaswi kuitwa ni ya taifa kwa kuwa haifiki popote.Alisema kwa sasa wananchi wa kisiwani Pemba wakiwemo wa jimbo la Gando tayari wamesahau kuona matangazo ya Televisheni kwa muda mrefu kutokana na kuwa matangazo ya kituo hicho kutopatikana na badala yake wananchi wa kisiwa hicho wamekuwa wakiangalia televisheni vyengine zinazorushwa na vituo vyengine kutoka Tanzania bara na nchi nyengine za ulaya.Endelea kusoma habari hii

BWAWANI HAITOBINAFSISHWA-SMZ

Zainab Omar Mohd(CCM)wanawakeSERIKALI Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haitoibinafsisha hoteli ya Bwawani na badala yake itafanyiwa matengenezo makubwa ya ukarabati ili ifikie kiwango cha hoteli za kimataifa.Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo wakati akifanya majumuisho ya michango iliyotolewa na wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati wakichangia bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2009.10 Mjini Unguja.Waziri Samia alisema kuendelea kutoa kila kitu kwa kubinafsisha ni hatari sana kwani itafika wakati serikali itakuwa omba omba na kuhangaika hata kushindwa kufanya shunguli zake.“Mimi naona ni bora kuendelea kumiliki hoteli ya Bwawani kwa sababu mbali mbali ….unajuwa tutafika wakati omba omba kwa sababu ya kubinafsisha kila kitu kwa sababu sio kila kitu kinabinafsishwa tu”alisisitiza Samia.Waliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba bado serikali ya mapinduzi ya zanzibar inahitaji kuwa na hoteli kwa ajili ya kufanya shunguli zake mbali mbali ikiwemo mikutano pamoja na sehemu ya kufikia wageni wake wa kitaifa ambao wamekuwa wakipendelea kufikia hapo kutokana na mandhari ya hoteli hiyo yanayovutia.Endelea kusoma habari hii

SMZ YAINGIA MKATABA NA JOHSONS

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imeingia mkataba na Kampuni ya Johsons kwa ujenzi wa Afisi ya Wizara ya Fedha na Uchumi wenye ghorofa tatu.Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) dk. Hasnuu Mohd Haji(CCM)kuteuliwaMwinyihaji Makame Mwadini ameyasema hayo wakati akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar.Awali Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake (CCM) Amina Iddi Mbarouk alitaka kujua kwa kuwa ni kiasi gani cha fedha kitakachogharimu ujenzi wa afisi hiyo ambayo tenda wa ujenzi huo imepewa kampuni ya Johnsons.Akijibu swali hilo Waziri Mwadini alisema malipo ya mwanzo ya asilimia 20 ya gharama za ujenzi yatafanywa baada ya kutia saini mkataba na wizara ya fedha na uchumi sambamba na ujenzi kuwasilishwa hati ya dhamana (performance bond).Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba kutokana na asilimia 10 ya gharama za ujenzi mpango kazi wa ujenzi (work plan) na madai (invoice) malipo mengine yatafanywa kwa mujibu wa kazi atakazozifanya.Endelea kusoma habari hii.

PEMBA KUPATA RADIO JAMII

Ali Juma Shamhuna(CCM) DongeSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kituo cha Redio Jamii kinatazamiwa kukamilika huko Micheweni Pemba na kitasaidia kutoa habari mbali mbali za kuelimisha jamii ikiwemo kuondokana na umasikini.Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini hapa.Shamuhuna alisema redio ya jamii ni muhimu sana kwa sababu itasaidia kutoa elimu kwa makundi mbali mbali katika wilaya ya Micheweni Pemba ambayo inakabiliwa na matatizo mbali mbali.“Redio jamii iliopo Micheweni ni muhimu sana kwa sababu itasaidia kutoa elimu kwa makundi mbali mbali ya wananchi ikiwemo kupambana na umasikini na kuinuwa uchumi kwa ujumla”alisema Aliipongeza shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi,utamaduni la UNESCO kwa kazi kubwa ya kuhakikisha redio hiyo inafanya kazi zake katika kisiwa cha Pemba.Endelea kusoma habari hii.

SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI WA MIONZI

KAMBI ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi imetaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kufanya uchunguzi juu ya hali ya mionzi katika kituo chake cha televisheni kutokana na madai kwamba wafanyakazi Najma Khalfan Juma(CUF)wanawakekadhaa wameshapoteza maisha kwa shaka ya kuathiriwa na mionzi.Madai hayo yametolewa na Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Najma Khalfan Juma wakaki alipokuwa akitoa hutuba mbadala wa bajeti ya wizara hiyo katika kikao cha bajeti cha mwaka wa fedha wa 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi.Alisema kuna taarifa kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu hadi miaka miwili karibu wafanyakazi saba wa kituo cha televisheni Zanzibar (TVZ) wamefariki na khofu imetanda kwamba inawezekana kuwa inatokana na kutanda kwa mionzi katika sehemu yao ya kazi.“Tunaamini kila mtu hufa kwa siku yake na siku ikiwadia hairudi nyuma wala haiongezeki lakini ni tabia ya mwanadamu yoyote kufanya wasi wasi juu ya maisha yanapotoweka kwa wenzao katika kipindi hiki kifupi” alisema Khalfan.Endelea kusoma habari hii

UFANYWE UTAFITI WA KISUKARI-MWAKILISHI

Mtumwa Kheri Mbarak(CUF)wanawakeWIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kufanya utafiti wa kina kujuwa chanzo cha kuenea kwa kasi ya ugonjwa wa kisukari nchini zaidi katika miaka ya hivi karibuni.Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Jimbo la Ole (CUF) Hamad Masoud Hamad wakati akichangia bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa mwaka wa fedha 2009/10 hapo katika baraza la wawakilisdhi mjini Zanzibar.Hamad alisema hivi sasa kumejitokeza kwa kasi ya ugonjwa wa kisukari ambao umekuwa tishio kwa afya ya wananchi wengi wa Unguja na Pemba,ambapo tatizo hilo limekuwa likiwatia hofu watu wengi.“Tunaitaka serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kufanya utafiti wa kina kujuwa chanzo cha maradho haya ambayo yamezuka katika miaka ya hivi karibuni”alisema Hamad.Alisema katika miaka ya nyuma ugonjwa wa kisukari ulikuwa ukiwakumba zaidi watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea lakini katika miaka ya hivi karibuni inaonesha kwamba ugonjwa huo umekuwa ukiwashambuliya watu wa rika mbali mbali kiasi ya kuanzishwa kwa jumuiya mbali mbali za kupambana na ugonjwa huo.Endelea kusoma habari hii.

TCAA HAIJACHANGIA MAPATO-SMZ

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetakiwa kuimarisha maeneo huru ya uchumi pamoja na bandari huru kwa ajili ya kuimarisha uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.Hayo Salmin Awadh Salmin(CCM)Magomeniyalisemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi juu ya makadirio ya mapato na matumizi ya Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa mwaka wa fedha 2009/10 Mjini Unguja.Salmin alisema maeneo huru ya uchumi pamoja na bandari huru ni muhimu sana kwa zanzibar kwa ajili ya kuimarisha uchumi pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wake hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekubwa na mtikisiko wa kiuchumi.Alitaka maeneo hayo kuhakikisha yanaimarishwa kwa miundo mbinu ya maji safi pamoja na barabara ili kuhakikisha wawekezahji wanaotaka kuwekeza wanapata faida hizo muhimu na kurahisisha kazi hiyo.Endelea kusoma habari hii.

CHUO CHA UTALII KIIMARISHWE

Muhiddin Mohd Muhiddin(CUF)MtambileKAMBI ya Upinzani katika baraza la wawakilishi imesema kuna kila sababu ya Chuo Cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar kuimarishwa kwa kuwa ni utalii ni sekta kiongozi kwa uchumi visiwani Zanzibar.Waziri Kivuli wa Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, Muhiddin Mohammed Muhiddin aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani juu ya makaridio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/10 Mjini Zanzibar.Muhiddin alisema sio muhimu kuwa na chuo peke yake lakini cha muhimu kwa chuo hicho kuwa na uwezo wa kutoa taaluma inayohitajika kwa kuwa na madarasa ya kutosha, vifaa vya kufundishia,wanafunzi wenye taaluma husika kwa viwango vya juu na wanafunzi wenye sifa zinazostahiki.Waziri Kivuli huyo asema kwamba chuo hicho kimejiwekea malengo kwa mwaka ujao wa fedha ni mazuri lakini alihoji iwapo ni kweli chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kuyatekeleza malengo yake kutokana na fedha ndogo kinayopatiwa au kina mikakakati gani ya kufanikisha malengo hayo.Endelea kusoma habari hii

KARAFUU ZIBINAFSISHWE-WAJUMBE

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetakiwa kubinafsisha zao la karafuu kwa ajili ya kuongeza ufanisi kwa wakulima na kuongeza kipato sanjari na kupambana na umasikini na kukuza uchumi.Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Utalii, Biashara na karafUwekezaji kwa mwaka wa fedha wa 2009/10 katika baraza la wawakilishi wajumbe wa baraza hilo wamesema kuna haja ya kubinafsishwa zao la karafuu kwa ili kulirejesha katika hadhi yake katika soko la dunia Mwakilishi wa Jimbo la Amani (CCM) Ali Denge Makame aliitaka serikali ya mapinduzi Zanzibar kuimarisha Kikosi Cha Maalumu Cha Kuzuwia Magendo (KMKM) kwa ajili ya kupambana na magendo ya karafuu ambayo husafirishwa na kupelekwa nchini Kenya.Alisema magendo ya karafuu bado yameshamiri kwa wingi katika kisiwa cha Pemba na hivyo kudhoofisha uchumi pamoja na zao la karafuu ambapo kwa kiasi kikubwa inakosesha kuingiza mapato serikalini hivyo serikali inawajibika kukiimarisha kikosi cha KMKM ili kunusuru fedha za serikali kupotea ovyo.“Kwa muda mrefu magendo ya karafuu yamekuwa yakishamiri katika kisiwa cha Pemba na hivyo kulikosesha mapato taifa serikali inawajibika kuimarisha kikosi cha KMKM kukabiliana na magendo maana karafuu hupelekwa nchini Kenya na hili linatuathiri hapa kwetu”alisema Denge.Endeleo kusoma habari hii

MIRADI MINGI IMEIDHINISHWA-SMZ

Samia SuluhuSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema jumla ya miradi 49 yenye thamani ya dola za kimarekani 766.82 Millioni imeidhinishwa hadi kufikia Machi 2009 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 22.5% ya lengo la uwekezaji nchini.Kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa sasa ni kuhamasisha wawekezaji kuwekeza nchini huku yakiwepo mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na amani na utulivu.Hayo yalisemwa na Waziri wa Utalii, Biashara na uwekezaji, Samia Suluhu Hassan wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2009-2010 hapo katika baraza la wawakilishi mjini kinachoendelea Maisara Mjini hapa.Samia alisema takwimu zinaonesha kwamba mamlaka ya uwekezaji nchini hadi kufikia Machi 2009 ipo jumla ya miradi 383 yenye thamani ya dola za kimarekani Millioni 2,887.47 ambapo kati ya miradi hiyo, miradi 174 yenye thamani ya makisio ya mtaji wa dola za kimarekani Millioni 987.95 tayari inatoa huduma.Endelea kusoma habari hii

ADA YA WAZAZI NI KUBWA-WAJUMBE

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wamepinga ada ya shilingi 40,000 wanayotozwa akina mama waja wazito wanaokwenda kujifungua katika hospitali kuu ya mnazi mmoja kutokana na kuwa wananchi wengi Thuwaiba Edington Kisasi(CCM)wanawakewanashindwa kumudu kiwango hicho.Wajumbe hao wameikwamisha kupitishwa kwa makadirio ya bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii ambapo yamepita kwa taabu kufuatilia wajumbe kupinga malipo ya shilingi 40,000 ambazo hutozwa mama hao wajumbe wengi walitaka kiwango hicho kupunguzwa ili wananchi wengi waweze kuhudumiwa bila ya shida.Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho alilazimika kuingilia kati na kuitaka kamati ya afya na ustawi wa jamii kulifanyia kazi suala hilo kwa kukaa pamoja na watendaji wa wizara ya afya na ustawi wa jamii ili kupunguza kiwango hicho.Makadirio hayo yalianza kupata wakati mgumu wakati wajumbe wakipitisha vifungu vya bajeti hiyo ambapo Mwakilishi wa viti maalumu (CCM) Thuwaiba Edington Kisasi alipohoji kwa nini akinamama wajawazito watozwe kiwango cha shilingi 40,000 ambacho alisema ni kikubwa na wengi hushindwa kulipia gharama hizo.Endelea kusoma habari hii

UFANYWE UTAFITI WA KISUKARI-MWAKILISHI

Adam Mwakanjuki (CCM)WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kufanya utafiti wa kina kujuwa chanzo cha kuenea kwa kasi ya ugonjwa wa kisukari nchini zaidi katika miaka ya hivi karibuni.Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Jimbo la Ole (CUF) Hamad Masoud Hamad wakati akichangia bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa mwaka wa fedha 2009/10 hapo katika baraza la wawakilisdhi mjini Zanzibar.Hamad alisema hivi sasa kumejitokeza kwa kasi ya ugonjwa wa kisukari ambao umekuwa tishio kwa afya ya wananchi wengi wa Unguja na Pemba,ambapo tatizo hilo limekuwa likiwatia hofu watu wengi.“Tunaitaka serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kufanya utafiti wa kina kujuwa chanzo cha maradho haya ambayo yamezuka katika miaka ya hivi karibuni”alisema Hamad.Alisema katika miaka ya nyuma ugonjwa wa kisukari ulikuwa ukiwakumba zaidi watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea lakini katika miaka ya hivi karibuni inaonesha kwamba ugonjwa huo umekuwa ukiwashambuliya watu wa rika mbali mbali kiasi ya kuanzishwa kwa jumuiya mbali mbali za kupambana na ugonjwa huo.Endelea kusoma habari hii

NASHANGAA KWA NINI HAWATAKI KONDOM-WAZIRI

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Shawana Bukheti Hassan ameshangazwa na tabia ya wazanzibari ambao hukataa matumizi ya mipira ya kondom wakati wanaendeleza Amina Salim Ali (CCM)vitendo vya ngono uzembe.Shawana alisema hayo wakati akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi waliokuwa wakichangia makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.Naibu huyo alisema licha ya ukweli kwamba maradhi ya ukimwi yapo lakini wananchi hawataki kubadilika huku wengine hata kondom wakiwa hawazitaki kwa ajili ya matumizi yake kama kinga ya ugonjwa huo na badala yake wamekuwa wakiendekeza ngono uzembe.“Zina imechukuwa nafasi kubwa na watu wengi hawataki kubadilika kwa kutumia kondom na badala yake wamekuwa wakifanya vitendo hivyo bila ya kinga yoyote hali ambayo ni hatari kwa afya za wananchi sasa sisi viongozi hili ni jukumu letu la kuelimisha jamii katika hatari ya ugonjwa wa ukimwi na suala zima la maambukizi” alisisitiza Shawana.Endelea kusoma habari hii

BAJETI YA AFYA IONGEZWE-UPINZANI

Rashid seifKAMBI ya Upinzani katika baraza la wawakilishi imependekeza kuongezwa kwa bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu hasa kwa wanannchi wasio na uwezo.Ushauri huo umetolewa na Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Rashid Seif Suleiman wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani katika bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Maisara Mjini hapa.“Kutokana na umuhimu na uzito mkubwa wa sekta ya afya serikali ilitakiwa itoe kipaumbele kwa sekta hii ya afya kwa angalau kukaribia kwenye lile lengo la 15% kwa azimio la Abuja kwa nchi za Afrika. Kwa bahati mbaya sekta hii inaendelea kusota na kumega asilimia 6.1% ya bajeti serikali 2009/10 bajeti ya afya ya Uganda ni 11%, Kenya 12% ya bajeti ya serikali” alisema Suleiman.Endelea kusoma habari hii

MADEREZA WATUNGIWE SHERIA-NABHAN

SERIKALI imetakiwa kuangalia uwezekano wa kutunga sheria ambayo itaweza kuwabana makondakta na madereva wanaokataa kuwapakia AZIZA NABAHAN (WAZIRI KIVULI WANAWAKE NA WATOTO)wanafunzi.Mwakilishi wa Wanawake Aziza Nabahani, aliliambia Baraza la wawakilishi wakati akichangia bajeti ya Wizaraya elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwaka wa fedha 2009/2010.Mwakilishi huyoalisema vitendo vya unyanyasaji wa wanafunzi vimekuwa vikiongezeka siku hadi skiku na ni vyema kwa Wizara hiyo ikafikiria kuandaasheria itayoweza kuwabana matingo na Madereva wa gari za dala dala.Alisema baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakichelewakufika maskuli kutokana na kuachwa na matingo kwani wamekuwa wakiwafukuza mithili ya kuwa sio binadamu wanaohitaji kupta msaada wa magari hayo.Alisema Mgari ya daladala yamesajiliwa kisheria kupakia abiria lakini haiwezekani kuachwa ya kiendelea kuwanyanyasa wanafunzi.Endelea kusoma habari hii

WALIMU WAKAGULIWE-WAJUMBE

Abdallah Juma AbdallahWAJUMBE wa Baraza la wawakilishi wameishauri serikali kuliangalia suala la kuwafanyia ukaguzi walimu katika skuli mbali mbali za serikali kwa vile wanaonekana kuwa ni wavivu na hawatimizi wajibu wao.Wajumbe ambao walitoa ushauri huo ni pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) Abdalla Juma, Mwakilishi wa Mkanyageni Haji Faki Shaali wakati wakichangia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwaka wa fedha 2009/2010, huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mjini Zanzibar.Wajumbe hao walieleza suala la ukaguzikatika skuli nyingi hivi sasa halifanyiki ipasavyo jambo ambalo linachangia kujitokeza kwa viwango vidogo vya upasishaji katika masomo mbali mbali.Mwakilishi wa Chonga alisema wengi wa walimu wanaonekana hivi sasa kuwa ni wavivu na hawajibiki ipasavyo taizo ambalolinatokana na kutokaguliwa.Alisema hivi sasa baadhi ya walimu wamekuwa wanashindwa kuingia madarasani na wameanzisha mtindo wa kuwapatia kazi za kufanya majumbani bila ya kuwapa mafunzo kuwapo jambo ambalo sio sahihi kwani ufundishaji wa ina hiyo hutakiwa kutumika katika elimu ya juu.Endelea kusoma habari hii

SERIKALI YASHAURIWA

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wametaka kurejeshwa upya mfumo wa zamani wa kuwachapa wanafunzi viboko pamoja na kurejeshewa utaratibu wa kupewa uji wanafunzi wa shule hasa shul za maandalizi.Mwakilishi wa kaa_chiniChonga (CUF) Abdallah Juma Abdallah aliishauri Wizara hiyo kuona haja ya kurudisha matumizi ya viboko mashuleni kwa vile inaonekana baadhi ya wanafunzi kukosa adabu kwa kuwatukana walimu kwa vile wanajua kuwa hawatapigwa.Alisema utaratibu wa kuwapa ushauri nasaha unaonekana kuwa ni wenye matatizo kwa vile vitendo vya utovu wa nidhamu hasa kwa wanafunzi wanawake vimekuwa vikiongezeka.Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Fatma Fereji Abdulhabib ambaye alieleza shule ya Hurumzi naKajificheni zimekuwa zinaongoza kwa kuwa na wanafuzi watoro na huenda tabia hiyo ikawa inaongezeka kutokana na kugundua kuwa hawapigwi.Alisema katika shule hizo kumekua na wanafunzi ambao hukimbia masomo yao na kwenda katika vibanda vya kompyuta kucheza gemu na kuchati na wanafunzi wenzao jambo ambalo Wizara itapaswa kuangaliwa kwa makini ili kuepusha tabia hiyo isije kuendelea.Endelea kusoma habari hii.

WIZARA BADO HAIJAJIPANGA-UPINZANI

Mohd Ali Salim(CUF)MkoaniKAMBI ya Upinzani katika baraza la wawakilishi imesema Zanzibar bado haijapiga hatua katika sekta ya elimu na kunahitajika juhudi zaidi ili kukabiliana na ushindani uliopo ili kutoa viwango bora vya elimu nchini.Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo, Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mohammed Ali Salim (Mulla) amesema juni 20 mwaka huu katika kongamano la elimu lililofanyika visiwani hapa lilibainisha kasoro mbali mbali za kutokuwepo ushindani katika sekta hiyo pamoja na matokeo ya mitihani ya mwaka huu ambapo Zanzibar iefeli vibaya.“Mfumo wa elimu hapa kwetu unaanzia skuli za maandalizi, unapitia skuli za msingi na kumalizia skuli za sekondari ikiwa ni elimu ya lazima mtiririko huu ni mnyororo ambao vikuku vyake vimeshikana, kimoja tu kati ya vijino hivyo kikiacha kufanya kazi kwa ubovu au kwa kuacha njia mnyororo mzima haufanyi kazi” alisema Mulla ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Pemba.Endelea kusoma habari hii

 

HAKUNA RUHUSA SOKO USIKU- WAZIRI

WIZARA ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema soko la samaki la darajani litafungwa sasaSuleiman Othman Nyanga(CCM) 12.00 jioni ili kutoa nafasi kwa wafanyakazi wa baraza la mji kufanya usafi katika eneo hilo.Hayo yameelezwa na waziri wa wizara hiyo, Suleiman Othman Nyanga alipokuwa akijibu swali la msingi lililolizwa na Mwakilishi wa Viti Maalumu (CCM) Ashura Abeid Faraji aliyetaka kujua sababu zilizopelekea kufungwa soko la samaki muda wa sasa 12:00 badala ya wafanyabiashara kuachiwa kuendelea kuuaza hadi sasa 2:00 usiku.Akijbu swali la la Mwakilishi huyo lililouliza kwa nini utaratibu huo unaopelekea usumbufu mkubwa kwa wateja ambao kwa kawaida hutyoka kazini kufuata samaki haufutwi na kurejeshwa utaratibu wa zamani, Waziri Nyanga alisema hilo haliwezekani.Alisema utaratibu wa kufungwa soko nyakati hizo hauwezi kubadilishwa kutokana na kuwepo misongamano ya wafanyabiashara na wateja ambapo mazingira ya kuweka usafi sokoni yanahitajika kupata muda wa kutosha wausafishaji.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WAIPONGEZA WIZARA YA ELIMU

Ali Suleiman Ali(CCM)WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wameipongeza wizara ya elimu na mafunzo ya amali kwa kuandaa muondo mpya wa utumishi wa walimu visiwani hapa ikiwa ni mkakati wa wizara hiyo kuweka maslahi stahiki kwa walimu.Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya elimu na mafunzo ya amali ya mwaka wa fedha 2009/10 Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii, Ali Suleiman Ali alisema kwamba kwa muda mrefu kumekuwa na kilio kwa walimu kuhusu maslahi duni wanayoyapata.Alisema kwamba hizi ni habari njema kwa wafanyakazi hao katika maendeleo ya elimu visiwani Zanzibar kwa kuona kuwa na wao wanakuwa sehemu ya chemchem ya mafanikio katika kukuza elimu nchini.“Kamati ina unga mkono kuandaliwa kwa muundo mpya wa walimu ambao tayari umeshawasilishwa serikalini kwa hatua zaidi” alisema Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM).Endelea kusoma habari hii.

VINU BADO NI MALI YA SMZ

samia suluhu hassanWIZARA ya Utalii, Biashara na Uwekezaji Zanzibar imesema vinu vya kukamulia mafuta ya viungo bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na vina mikataba maalumu kati yake na wananchi.Hayo yameelezwa na Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua iwapo vinu hivyo vimekodoshwa au vinaendeshwa kwa biashara ya ubia.“Vinu hivi bado ni mali ya shirika la ZSTC na kwa kila eneo kilichopo kinu hicho kuna mikataba maalumu kati ya ZSTC na wananchi wa eneo husika” alisema Waziri Samia.Akijibu swali la Mwakilishi huyo aliyetaka kujua tokea kununuliwa vinu hivyo hadi sasa ni kiasi gani cha fedha kilichokusanywa,Waziri Samia alisema tangu kununuliwa vinu vya kukamulia mafuta na kuvisambaza katika maeneo tofauti huko Pemba fedha walizolipwa wananchi kwa mafuta waliyoyakamua na kuyauza kiwandani ni nyingi.Endelea kusoma habari hii

WANAFUNZI WENGI WAOLEWA -SMZ

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema katika kipindi cha mwaka 2008/2009 jumla ya wanafunzi 40 wameripotiwa kufunga ndoa katika Haroun Ali Suleiman(CCM)shule mbali mbali Unguja na Pemba.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman ameyasema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2009/10 mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Mjini Unguja.Waziri Suleiman amesema wanafunzi hao 40 waliofunga ndoa na kukatisha masomo yao kati yao kesi 4 baina ya wanafunzi kwa wanafunzi na wengine wameolewa na kuoa watu wengine ambao sio wanafunzi kutokana na ridhaa za wazazi wao.Hata hivyo Waziri huyo amesema wanafunzi hao waliochukua uamuzi huo wa kuolewa au kuoa kabla ya kuhitimu mafunzo yao wamefukuzwa shule kwa kumujibu wa sheria ya elimu iliyopo hivi sasa.Endelea kusoma habari hii

MIFUKO BADO NI MARUFUKU-SMZ

IMG_6161SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haijafuta marufuku ya mifuko ya plastiki visiwani Zanzibar ambapo hadi sasa ni wafanyabishara wawili waliokamatwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa mifuko hiyo nchini.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Burhani Saadati Haji alisema hayo wakati akifanya majumuisho ya michango mbali mbali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi mjini hapa.Saadati alisema kwa sasa kesi moja ipo mahakamni wakati kesi ya mfanyabiashara ya kampuni ya Bopar jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ambapo katuni saba zilizokamatwa katika ghala lake mataa wa Malindi zimehifadhiwa katika kituo cha polisi Malindi.Alikiri kwamba mfanyabiashara huyo kumdhalilisha Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira aliyekuwa kazini katika operesheni ya usakaji wa mifuko ya lpasitiki na kulaani kitendo hicho kuwa sio cha kiungwana na kauhidi serikali kulichukulia suala hilo kwa mujibu wa sheria.Endelea kusoma habari hii

WAZIRI ACHUKULIWE HATUA-UPINZANI

KIONGOZI wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari amesema kwamba juhudi za serikali za kudhibiti uingizaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku, zinakwamishwa na abubakarbaadhi ya watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri.Bakari alimtaja waziri wa nchi ofisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma kuwa ni miongoni mwa watendaji ambao wamekuwa wakitoa vibali kwa baadhi ya wafanyabiashara ili kuingiza nchini biashara ya mifuko ya plastiki.Akichangia mapendekezo ya bajeti ya wizara ya kilimo, mifugo, na mazingira kiongozi huyo wa upinzani alitaka baraza la wawakilishi liunde kamati ya kuchunguza tuhuma hiyo dhidi ya waziri Juma na kushauri kwamba ikithibitika apewe adhabu.“Mh Mwenyekiti, haiwezekani wafanyabiashara wadogo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la mifuko, lakini wengine wenye dhamana ya kuhakikisha sheria zinatekelezwa wanakwenda kinyume. haikubaliki,” Bakari alisema.Endelea kusoma habari hii

SEKTA YA KILIMO YATIKISIKA

Burhan Saadat (CCM)WAJUMBE wa baraza la wawakilishi Zanzibar wameelezwa kwamba sekta ya kilimo imekubwa na mtikisiko wa kiuchumi uliotokea duniani kote.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Burhani Saadat Haji amesema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi Maisara Mjini Zanzibar.“dunia hivi sasa imekabiliwa na changamoto kubwa ya kuporomoka kwa uchumi na soko la fedha hali ambayo imeathirika sekta za uzalishaji Zanzibar kama nchi nyengine ulimwenguni imeanza kuathirika na hali hiyo katika sekta zake za uchumi ikiwemo kilimo” alisema Waziri huyo.Amesema tatizo hilo limesababisha kupanda kwa bei za pembejeo za kilimo na kuwaathiri wakulima kushindwa kumudu kununuwa vifaa vya kilimo na hivyo sekta hiyo kuyumba kutokana na tatizo hilo.Haji alisema jambo jengine ni kupungua kwa soko la mazao ya kilimo na kushuka kwa bei ya mazao yanayosafirishwa nje ya nchi zaidi karafuu utapunguza kwa kiasi kikubwa mapato ya taifa na kipato cha wazalishaji kwa ujumla.Endelea kusoma habari hii

 

SMZ YAKASIRISHWA MAWAZIRI BARA

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema Wabunge na mawaziri wa Serikaliya Muungano wanaokejeli Maaumuzi ya Baraza la Mapinduzi juu ya kuliondoa suala la utafutaji mafuta na uchimbaji wa gesi asilia katika Kamal Basha Pandu(CCM)Rahaleomambo ya Muungano wameishiwa na hoja.Waziri wa Maji, Ujenzi,Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, Aliliambia Baraza la Wawakilishi wakati akijibu hoja mbali mbali zilizotolewa walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wafedha 2009/10.Waziri Mansour, alisema kauli ya Baraza la Mapinduzi iliyoiwasilisha mbele ya Baraza la Wawakilishi, juu ya maamuzi ya haikuwa yake binafsi na ni ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar’.“Wizara yangu inawajibika kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayoongozwa na Rais Dk. Amani Abeid Karume na Baraza hili lipo chini yake yeye Rais Karume na wewe Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho ndie unaeliongoza na siwajibiki kwa Wabunge” alisema Waziri huyo.Alisema kwamba “Ni hulka ya mwanadamu anapokosa hoja usishangae kwani atatukana na anaweza kutupa mawe sasa na ndio hao wabunge wamekosa hoja anapojuwa amewatendea wenzake dhambi na wizi wa mchana” alisisitiza Waziri huyo.Endelea kusoma habari hii

SMZ YAPUNGUZA VIWANGO VYA MAJI

mansoorSERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepunguza viwango vya utumiaji wa huduma ya maji kutoka shilingi 4,000 hadi shilingi 2,000 mwezi.Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi Mansoor Yussuf Himid wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake ya mwaka wa fedha za 2009/10 kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi Maisara Mjini Unguja.Waziri alisema kwa kuzingantia kilio cha wanannchi cha kutaka bei ya utoaji wa huduma hiyo ipunguzwe serikali imeamua kushusha viwango vya sasa vinavyotumika katika utoaji wa huduma ya maji.“Katika kujali kilio cha wananchi nikiwa Waziri wa taasisi inayoitumikia wananchi, kuanzia mwezi wa Julai 2009, mchango wa huduma ya maji kwa matumizi ya nyumbani utakuwa ni shilingi 2000 kwa mwezi badala ya 4,000″ alisema Waziri Mansoor alisema hatua hiyo ya serikali inakuja ikiwa ni moja ya malengo ya kuifanya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuweza kutekeleza majukumu yake vizuri katika mwaka ujao wa fedha.Endelea kusoma habari hii

WAWAKILISHI WAKASIRISHWA NA MALIMA

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamemshambulia Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Adam Kighoma Ali Malima kuwa anajifurahisha katika suala la mafuta na gesi asilia kwa zakia omar juma (CUF) WANAWAKEkuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imshaamua kuliondoa kwenye orodha ya mambo ya Muungano.Mashambulizi hayo yamekuja nyakati za asubuhi jana wakati wajumbe hao wakijadili makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara ya maji, ujenzi, nishati na ardhi katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.“Mheshimiwa Spika leo tumemsikia Mheshimiwa Malima akieleza bungeni kule lakini sisi tunamwambia kuwa anajifurahisha na ajuwe kuwa Uwaziri wake mwisho Dar es Salaam, Zanzibar tuna wetu waziri tena ni jabali hayumbishwi na matamshi ya Bungeni, na tujue kuwa mafuta si ya Muungano tena watajijuwa wenyewe sisi tumeshaamua” Alisema Mwakilishi wa Viti Maalum(CUF) Zakia Omar Juma.Mwakilishi huyo aliyasema hayo kufuatia majibu yaliyotolewa Bungeni jana na Naibu Waziri Malima wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo alisema suala la uamuzi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar ameusiki kupitia vyombo vya habari.Endelea kusoma habari hii.

 

SMZ YAUZA NYUMBA ZAKE

Wonder_znSERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kuziuza baadhi ya nyumba zaserikali ziliopo Mjini na vijijini kwa Unguja na Pemba.Waziri wa Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akiwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2009/10.Waziri Himid alisema serikali imeamua kuziuza nyumba hizo ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa serikali wa kujiondoa katika umiliki wa majengo ya nyumba zilizo chini ya usimamizi wa serikali.Alisema uuzaji wa nyumba hizo unafanyika ikiwa ni moja ya utekelezaji wa sera ya taifa ya nyumba ambayo ilipitishwa na baraza la  wawakilishi mwezi Aprili 2008, ambapo miongoni mwa matamko ya sera hiyo imeelezea azma ya serikali kujiondoa kwenye umiliki na ukodishwaji wa baadhi ya nyumba za Maendeleo Mjini na Vijijini.Waziri huyo alifahmisha kuwa hatua hiyoya serikali inakuja kwa vile nyumba inazomilikiwa na serikali mjini na vijijini hivi sasa zipo katika hali mbaya kutokana na kushindwa kuzisimamia kunakosababishwa na ufinyu wa bajeti ya kuzihudumia nyumba hizo kwa kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu sasa.Endelea kusoma habari hii.

WEMA WAPANDISHE VYEO ASKARI-WAJUMBE

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania Inspekta Generali, Said Mwema ameombwa na wajumbe wa wawakilishi kuwatazama askari wanne walionusuru maisha ya wajumbe 10 wa baraza hilo katika safari yao ya kuelekea Kigoma walipovamiwa na majambazi miezi miwili iliyopita.Baraza hilo lilitoa tamko hilo jana wakati askari hao pamoja na madereva wawili walipofika mbele ya Baraza la Wawakilishi kwa mwaliko maluum wa Baraza hilo kupitiaKamatiya mawasilianona Ujenzi.Mwezi uliopita Kamati ya Mawasilainona Ujenzi wakati ikifanya kazi zake katika Mkoa wa Kigoma, ilinusurika kuvamiwa na majambazi wakati wakiwa njiani kurudi Dar es Salaam kuendeleana kazi zao.Kamati hiyo ilikuwa katika Mkoa huo kwa lengo la kujifunza shughuli za uendeshaji wa umeme wa majenereta lakini wakati wakirudi Wilaya yaKibondo walivamiwa namajambazi hao waliokuwa na silah aina ya SMG huku njia wakiwa wamewekewa kizuizi cha gogo.Endelea kusoma habari hii.

UJENZI WA ZRB HIVI KARIBUNI-SMZ

utawala boraWAJUMBE wa baraza lawawakilishi wameipongeza serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa kusikia kilio cha wananchi wanyonge kwa kupunguza bei ya viwango vya maji yanayotolewa na serikali.Awali wananchi wa Zanzibar walitakiwa kulipia maji kwa kiwango cha shilingi 4,000 kwa mwezi jambo ambalo lilizusha malalamiko makubwa miongoni mwa wananchi mbali mbali wa Unguja na Pemba kutokana na upatikanaji wa maji hayo ukiwa mdogo huku mamlaka ya maji ikitaka wananchi hao walipie maji kwa bei hiyo.Kiwango kipya cha sasa wananchi hao watatakiwa kulipia shilingi 2,000 kwa mwezi badala ya shilingi 4,000 kwa mwezi na kwa wale wenye visiwa watalazimika kulipia shilingi 50,000 huku wenye maofisi na mahoteli watalipa kiwango kikubwa cha bei kulingana na matumizi yao.Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara ya maji, ujenzi, nishati na ardhi kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi wajumbe hao wamesema wamefurahishwa na maamuzi ya serikali kupunguza kiwango kicho cha bei ya maji.Endelea kusoma habari hii

SMZ IMESIKIA KILIO CHA WANANCHI

WAJUMBE wa baraza lawawakilishi wameipongeza serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa kusikia kilio cha wananchi wanyonge kwa kupunguza bei ya mwalimuviwango vya maji yanayotolewa na serikali.Awali wananchi wa Zanzibar walitakiwa kulipia maji kwa kiwango cha shilingi 4,000 kwa mwezi jambo ambalo lilizusha malalamiko makubwa miongoni mwa wananchi mbali mbali wa Unguja na Pemba kutokana na upatikanaji wa maji hayo ukiwa mdogo huku mamlaka ya maji ikitaka wananchi hao walipie maji kwa bei hiyo.Kiwango kipya cha sasa wananchi hao watatakiwa kulipia shilingi 2,000 kwa mwezi badala ya shilingi 4,000 kwa mwezi na kwa wale wenye visiwa watalazimika kulipia shilingi 50,000 huku wenye maofisi na mahoteli watalipa kiwango kikubwa cha bei kulingana na matumizi yao.Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara ya maji, ujenzi, nishati na ardhi kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika baraza la wawakilishi wajumbe hao wamesema wamefurahishwa na maamuzi ya serikali kupunguza kiwango kicho cha bei ya maji.Endelea kusoma habari hii

MISALI YANYEMELEWA NA KENYA

P1010026SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haijawahi kusikia kwamba Kisiwa cha Misali kinanyemelewa na Serikali ya Kenya kama ilivyotokea kwa mlima Kilimanjaro.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Khatib Suleiman Bakari aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali na nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua kuwa serikali inafahamu kwamba Kenya wameanza kukitangaza kisiwa cha Misali kwamba kipo katika nchi yao.Naibu Waziri huyo alisema serikali hadi sasa haijawahi kusikia kama Kenya imeanza kukinyemelea kisiwa hicho na tayari wameanza kukitangaza katika nchi za ulaya kwamba kipo katika nchi yao lakini serikali itafuatilia suala hilo.Akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani (CUF) Mohamed Ali Salim (Mulla) aliyetaka kujuwa wananchi wanaozungukwa na eneo hilo wanafaidika vipi na mapato ya utalii, Naibu huyo alisema wananchi wa kisiwa cha Misali ambacho kipo chini ya hifadhi ya mazingira wananchi wanaozungukwa na eneo hilo wanafaidika na mapato yanayopatikana kutokana na utalii unaofanywa katika kisiwa hicho.Endelea kusoma habari hii.

MAFUTA NA GESI NI YETU -SMZ

mansoorSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetoa msimamo wake rasmi wa kutaka suala la mafuta na gesi asilia liondolewe katika orodha ya mambo ya muungano.Uamuzi huo wa serikali umetolewa na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoour Yussuf Himid wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2009/10 katika baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar.Himid alisema wizara yake iliandaa waraka maalumu kupeleka serikalini wenye kumbukumbu namba Nam. 25/2009 na baadae uliwasilishwa katika kikao cha baraza la mapinduzi febuari 27 2009 ikiwa na azma kamili ya kikao hicho kupata dira na msimamo wa serikali ya Zanzibar katika suala hilo nyeti.Naomba utulivu mkubwa wajumbe maana hili suala ni nyeti naomba musikilize kwa umakini sana” alisema Spika Kificho baada ya kuona wajumbe wa wa baraza hilo kuwa na shauku kubwa ya kutaka kupiga makofi kwa mfululizo.Himid aliendeleza kusema kwamba baada ya majadiliano hayo ya wajumbe wa baraza la mapinduzi kwa kuzingatia hoja kikao hicho kilipitisha maamuzi matatu mazito.Endelea kusoma habari hii.

 

TUTAPUNGUZA VIKUNDI VYA HIJA -SMZ

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kupunguza utitiri wa vikundi vya watu wanaopeleka waumini wa dini ya kiislamu katika ibada ya hijja huko Makka Sauda Arabia.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abdallah Shaaban wakati akijibu hoja mbali mbali za wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochangia makadirio mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2009-2010.Shaaban alisema utaratibu huo utapunguza utitiri wa Mazoko6vikundi vinavyosafirisha mahujja kwenda katika ibada tukufu ya Hijja huko Makka.“Huo ndio msimamo wa serikali ya Sauda Arabia inataka kupunguza vikundi vya ibada ya hijja vinavyosafirisha mahujaji kwenda Makka kila mwaka”alisema Shaaban.Alisema lengo hilo ni kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za mahujaji wanaokwenda kufanya ibada ya hijja ambayo ni moja ya nguzo tano za kiislamu.Shaaban alisema katika miaka ya nyume kumejitokeza kwa malalamiko mbali mbali kwa mahujaji kukosa huduma nzuri zinazotolewa kwa vikundi vinavyosafirisha mahujaji na wakati mwengine mahujaji kuchelewa kuondoka nchini kwenda Makka kwa wakati.Endelea kusoma habari hii.

UFAHAMU MDOGO WACHELEWESHA KESI

Ramadhan Abdallah ShaabanSerikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema tatizo la wananchi kuwa na uwelewa mdogo katika masuala ya sheria na mahakama limechangia kwa kiasi kikubwa kuchelewa kusikilizwa kwa kesi na kutolewa maamuzi yake.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora Ramadhan Abdallah Shaaban wakati akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2009/10.Shaaban alisema kesi nyingi zimekwama kusikilizwa au kutolewa maamuzi yake kutokana na wananchi kushindwa kutoa ushahidi katika mahakama mbali mbali za Unguja na Pemba.Alisema wananchi wengi wanashindwa kutoa ushahidi katika kesi zinazohusiana na mambo mbali mbali ikiwemo ubakaji,udhalilishaji wa watoto kwa sababu mbali mbali ikiwemo kuogopa.“Hilo ndiyo tatizo kubwa linalosababisha kukwama kwa kesi mbali mbali katika mahakama za hapa wananchi wanaogopa kutoa ushahidi na hivyo hakimu au jaji hawezi kusikiliza kesi au kutoa hukumu kwani ushahidi ambao humtia mtu hatiani umekosekana”alisema Shaaban.Akatoa mfano wa mdogo wake ambaye alitelekezwa na mumewe muda mrefu amabpo mahakama ya kadhi ilimuamuru mdogo wake alipe fidia ya mahari na gharama zote za huduma alizopatiwa wakati akiwa katika ndoa.Endelea kusoma habari hii.

MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MTIKISIKO IPO

WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepanga vizuri na kuweka mikakati kadhaa kutokana na mtikisiko wa kichumi unaoendelea duniani kote.Akiitaja mikakati hiyo ni pamoja na kuongeza bajeti ya Dk. Mwinyihaji Makame(CCM)huduma za kilimo ili kuwalinda wananchi ambao wengi wao wanategemea kilimo na ufugaji na kuongeza programu mbali mbali na miradi muhimu itakayoweza kuwasaidia katika kujiendeshea maisha yao.Akitaja mikakati mengine Waziri huyo alisema ni kuweka mazingira mazuri ya biashara pamoja na uwekezaji wa ndani na nje ya nchi kuharakisha utekelezaji wa miradi ya umeme na maji safi na salama na kugharamia uimarishaji wa miundo mbinu ambapo serikali itahakikisha utulivu wa uchumi.Mwadini alikuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Amani (CCM) Ali Denge Ali aliyetaka kujua serikali imejipanga vipi katika kuandaa mikakati ya kuimarisha uchumi wa Zanzibar ili kupunguza athari za mtukisiko wa kiuchumi ambapo umeikumba dunia hasa mataifa yalioendelea.Endelea kusoma habari hii.

IUNDWE TUME YA MADILI -WAWAKILISHI

zakia omar juma (CUF) WANAWAKEBAADHI ya Wajumbe wa baraza la wawakilishi wameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuunda Tume ya Kupambana na Rushwa na Maadili ya Viongozi ili kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi vinavyofanywa na viongozi wa serikali wasio na uaminifu kazini.Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa Viti Maalumu (CUF) Zakia Omar Juma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora ya mwaka wa fedha wa 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Unguja.Mwakilishi huyo wapo baadhi ya watendaji wamekuwa wakikiuka maadili ya kazi na kujishirikisha na vitendo vya kupokea rushwa hasa katika taasisi ambazo vinahitajika na wananchi jambo ambalo limekuwa likiwanyima haki wananchi kupata haki zao.Mwakilishi huyo pia ameitaka wizara ya katiba kuangalia kwa undani utendaji wazi wa mahakama ili kurejesha imani ya wananchi kwani wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia utendaji kazi kwa kukosekana haki katika mahakama hiyo.Endelea kusoma habari hii.

HUKUMU ZA WATOTO ZITIZAMWE UPYA

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wametaka kutizamwa upya kwa sheria na hukumu zinazotolewa na mahakama dhidi ya watoto wadogo ambazo zinaonekana zinasababisha kuwaweka katika mazingira mabaya katika vyuo vya mafunzo kwa kuchanganya na watu wazima.Hayo yameelezwa na Zahra Ali Hamad(CUF)wanawakeMwakilishi wa Nafasi za Wanawake (CUF) Zahra Ali Hamad wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo, Ramadhan Abdalla Shaaban katika kikao cha Baraza la Wawakilishi cha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2009/10.“Sio vizuri Mheshimiwa Spika kuwachanganya watoto wadogo na watu wazima kwani tunajua watu wazima walivyo na hawa watoto kweli wana makosa ndio wakapelekwa huko lakini kuwaweka na watu wazima ni matatizo na huenda wakajifunza mambo mabaya huko huko na vyema kuangalia suala hilo ili watoto wanapotoka wasiwe wamejifunza usugu na mambo mabaya” alisema Zahra.Sambamba na hilo Mwakilishi huyo alitaka kuangaliwa namna ya utekelezaji wa adhabu ya kutumikia jamii kwani inaonekana haitekelezwi vilivyo na badala yake wanaopewa adhabu hiyo wamekuwa wakitumikia vyuo vya mafunzo.Endelea kusoma habari.

 

KATIBA IBADILISHWE-WAWAKILISHI

iddi panduWajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kufanya marekebisho ya katiba ya Zanzibar kwa lengo la kuweza kumpa uwezo Rais kuteuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Wajumbe hao wamesema kukosekana kwa mwanasheria mkuu wa serikali katika kikao cha baraza la wawakilishi kunaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za baraza hilo ambapo hivi sasa amekosekana kwa kipndi kikubwa kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.Wajumbe hao wametoa ushauri huyo wakati wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar.Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM), Ame Mati Wadi, alisema Baraza la Wawakilishi, lipo hatarini kupata matatizo katika shughuli zake ikiwa serikali haijafikiria kufanya mabadiliko ya katiba, yatakayomuwezesha Rais kuwa na uwezo kuteuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali.Alisema kutokana na mfumo unaotumika katika kuliendesha Baraza hilo kuwa ni lazima liwe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na ni lazima serikali ibadili Katiba na kuweka cheo hicho badala ya kutegemea kufanywa na Mwanasheria Mkuu pekee.Endelea kusoma habari hii.

DPP AMWAGIWA SIFA NA WAWAKILISHI

DPPWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameridhishwa na utendaji kazi wa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) kutokana na kutimiza majukumu yake ipasavyo.Hayo yalielezwa Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni (CCM) Ali Haji Ali wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao cha katika baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini hapa.Alisema yeye binafsi ameridhishwa na utendaji kazi wa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo tangu kuanzishwa kwake imefanya kazi kubwa ikiwemo kusimamia mwenendo mzima wa mashtaka na kuendesha vyema kazi zake katika afisi hiyo.Ali alisema kitendo cha kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni kutekeleza dhana ya misingi ya haki za binaadamu na utawala bora, ambayo serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutekeleza suala hilo kwa vitendo.“Tumerishishwa sana na kijana wetu huyu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kweli amefanya kazi kubwa tangu kuchaguliwa kwake pale amefanya mambo makubwa ya kusimamia na kuweza kuimarisha ofisi lakini kubwa zaidi kuwapa fursa vijana kusoma na kujingezea taalamu ni jambo zuri sana anastahiki pongezi kubwa” alisema Mwakilishi huyo.Endelea kusoma habari hii

 KARAKANA HAINA BODI YA WAKURUGENZI

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar imekiri kuendesha shughuli zake katika karakana ya matrekta bila ya kuwa na bodi ya wakurugenzi kwa miaka minne sasa.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Khatib Suleiman Bakari aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kufuatia swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa sababu zilizokwamisha kukosekana kwa bodi ya wakurugenzi katika taasisi hiyo.Mwakilishi huyo alisema karakana ya matrekta iliyopo eneo la Mbweni Mjini Unguja ni kitengo muhimu katika maendeleo ya kilimo lakini jambo la kusikitisha kitendo hicho kimedharauliwa na hata vifaa vilivyopo ni vikongwe mno pamoja na wataalamu wake kutopatiwa mafunzo ya kujiendeleza jambo ambalo linaawathiri kisaikolojia.Mwakilishi alimuuliza Naibu Waziri kwamba haoni kwamba karakana hiyo inakosa wateja kutokana na mafundi wake kuwa hawana utaalamu nab ado wanatumia zana duni, Naibu huyo alisema licha ya kukosekana kwa bodi ya wakurugenzi katika taasisi hiyo serikali pamoja na wizara kwa ujumla imekuwa ikitoa ushirikiano wa kina katika kuhakikisha karakana hiyo inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Endelea kusoma habari hii.

SERIKALI IWAWAJIBISHE WATENDAJI WABOVU

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetakiwa kuyafanyia kazi makosa ya kihesabu yaliobainika sambamba na kuwachukulia hatua wafanyakazi waliohusika na upotevu wa fedha bila ya ubaguzi wowote.Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya baraza la wawakilishi, Haji Omar Kheri alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Nchi, Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Mjini hapa.“Kamati yangu inaunga mkono kilio cha Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Mheshimiwa Fatma Ferej kwa kutokufnayia kazi yale makosa ya kihesabu yaliobainika jambi hilo linawarejesha nyuma watendaji wa afisi hii kwa kuwa wamepoteza nguvu zao nyingi bila ya kuchukuliwa hatua yoyote kwa waliobainika na makosa” alisema Mwenyekiti huyo.Kamati hiyo imeioomba serikali kuiangalia kwa kina suala hilo kwa lengo la wale waslioshirikia kwa njia moja au nyengine wawajibishwe kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza na sio sheria hiyo kutekelezwa kwa baadhi ya watendaji na wengine kuachwa bila ya kuchukuliwa hatua.Endelea kusoma habari hii.

SHANGA NA BATIKI MARUFUKU FORODHANI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema biashara za shanga, batiki, vinyago na mikoba hazitaruhusiwa kuuzwa ndani ya eneo la jipya la bustani ya Forodhani iliyopo ndani ya Mji Mkongwe Mkoa wa Mjini Foro_Leo_znzMagharibi.Hayo yamelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga wakati akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdallah Ali aliyetaka kujua akina mama wajasiri amali waliokuwepo eneo la mji mkongwe watapatiwa nafasi gani wakati bustani hiyo itakapokamilika matengenezo yake.Waziri Nyanga alisema kwa mujibu wa taratibu na sheria za kulinda urithi wa Mji Mkongwe biashara hizo hazitaruhusiwa kuuzwa nje na badala yake zinatakiwa kuuzwa ndani ya milango ya maduka ili kuweka mandhari ya mji huo vizuri.Akijibu swali la Mwakilishi huyo kuwa ni kiasi gani kitatakiwa kulipwa kwa kila eneo la kufanyia biashara na watu waliokodi sehemu hizo za bustani ya forodhani,Waziri Nyanga alisema wafanyabiashara watalipa viwango tofauti vya malipo kulingana na aina ya biashara na ukubwa wa nafasi atakayotumia mfanyabiashara huyo.Endelea kusoma habari hii.

GARI 900 ZIMEKAGULIWA

JUMLA ya gari zipatazo 900 zimefanyiwa ukaguzi wa barabarani na jeshi la polisi katika kipindi cha mwezi mmoja wa mei mwaka huu katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Mawasiliano na Uchukuzi, Machano Othman Said, wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali DSC00556aliyetaka kujua kwa nini serikali iliamua ghafla kuzifanyia ukaguzi gari hizo bila ya taarifa maalumu kwa wahusika.Waziri Machano alisema gari hizo zilifanyiwa ukaguzi kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo baadhi ya waendeshaji kutokuwa na leseni, ubovu wa magari yenyewe pamoja na uksoefu wa vifaa mbali mbali katika gari hizo.Alisema katika zozezi hilo la ukaguzi wa magari hayo yapo baadhi ya magari yamepatikana yakiwa hayana matatizo yoyote ambapo idadi yake ni 700 lakini yapo mengine magari 200 yamepatwa yakiwa na matatizo mbali mbali.Kupitia zoezi hilo Waziri Machano alisema katika kipindi hicho cha mwezi mmoja Serikali ilipata mapato makubwa kutokana na ukaguzi wa gari hizo ambapo wamiliki wengi walikamilisha taratibu za gari zao.Endelea kusoma habari hii.

VITAMBULISHO VYAZUA BALAA ZNZ

fatmaSWALA la vitambulisho vya mzanzibari mkaazi, utendaji wa viongozi wa serikali za mitaa, na njaa kisiwani vimeendelea kuzuwa mabishano katika kikao cha baraza la wawakilshi kinachoendolea mjini hapa.Baadhi ya wajumbe wa kambi ya upinzani wamesema kwamba upo mkanganyiko wa takwimu za idadi ya watu waliyopewa vitabumlisho tangu kupitisha sheria no 7 ya vitambulisho mwaka 2005 na baraza la wawakilishi. Fatma Abdulhabib fereji Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), na Mwakilishi wa Jimbo la Gando (CUF) Said Ali Mbarouk walisema hayo wakati wa kujadili bajeti ya wizara ya tawala za mikoa na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwa wizara imekuwa ikirudia takwimu hizo kwa hizo kila mwaka na kushindwa kutoa takwimu mpya kulingana na hali halisi. “Siku zote unapopanga takwimu zinazohusu wananchi mabadiliko yatakuwepo, kuongezeka au kupunguwa, lakini takwimu kwamba Idadi ya watu 500,000 imekuwa ikitolewa wakati katika mchanganuo wa wilaya takwimu ni nyengine. Tunamuomba waziri aje aondowe wasi wasi huu,” alihoji Fatma. Katika hotuba yake ya bajeti waziri Nyanga alisema kwamba jumla ya wazanzbari 505,606 walikuwa wameandikishwa ambayo ni sawa na asilimia 101 ya makadirio ya watu 500,486 huku akisema kwamba zoezi la uandikishaji linakwenda vizuri. Endelea kusoma habari hii.

MSONGAMANO WAGEREZA NI MKUBWA

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Suleiman Othman Nyanga amekiri kuwepo kwa msongamano wa mahabusu katika magereza yaliopo zanzibar na kuwepo idadi kubwa ya watoto walio chini ua umri wa miaka 18 katika magereza tv photo 019hayo.Waziri Nyanga aliyasema hayo katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2009/10. Nyanga alisema ipo idadi kubwa ya mahabusu pamoja na vijana waliotiwa hatiani ikiwemo watoto chini ya umri wa miaka 18 kwa makosa mbali mbali ambapo pia alikiri kukabiliwa na hali ya uchakavu magereza hayo ambayo kwa muda mrefu sasa hayajafanyiwa matengenezo.Alisema magereza ya zanzibar yanakabiliwa na idadi kubwa ya mahabusu ambapo katika mwaka 2008-2009 zaidi ya mahabusu 2164 walifikishwa katika magereza ya Unguja na Pemba ambapo kati ya mahabusu hao 2100 ni wanaume na 64 ni wanawake ambapo kwa sasa ni mzigo mkubwa kwa serikali kwani mahabusu kwa kawaida huwa hawafanyi kazi hivyo mzigo huo huielemea serikali kwa kuwashughulikia katika mahitaji yao.Endelea kusoma habari hii.

SMZ YAKIRI KUNUNUA MAGARI YA KIFAHARI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imekiri kununua magari ya kifahari kwa ajili ya matumizi ya viongozi wa ngazi za juu ikiwemo mawaziri na manaibu wake yapatayo 80 ambayo yameanza kutumiwa na wahusika visiwani hapa.Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali alilolulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujuwa serikali imenunuwa gari ngapi za kifahari kwa viongozi wa ngazi za juu na vipi matengenezo yake yatafanywa huku akitaka kujua ni nani anayehusika kuyatengeneza iwapo tayaharibika.Dk. Mwinyihaji alisema serikali ya mapinduzi zanzibar imetumia jumla ya shilingi billioni 2 kwa ajili ya kununuwa gari za kifahari ambazo zitatumika kwa mawaziri, manaibu mawaziri wakuu wa mikoa, huku makamanda wa vikosi vya SMZ nao wakiwa ni miongoni mwa wanaofaidika na magari hayo.Alisema magari hayo tayari yanatumika kwa sasa kwa viongozi hao wakiwemo wakuu wa wilaya za Unguja na Pemba kwa ajili ya kurahisisha usafiri na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuwahudumikia wananchi na shughuli nyengine za kikazi wanazopangiwa na wakuu wao wa kazi.Endelea kusoma habari hii.

VIKOSI VYOTE VIFUTWE-UPINZANI

Wawakilishi wa Kambi ya upinzani (CUF) wamesisitiza tena msimamo wao wa kuitaka serikali ya mapinduzi zanzibar kuvifuta kabisa vikosi vya ulinzi vya SMZ kwa madai kwamba vinatumia kodi kubwa ya wananchi huku kazi wanayofanya haina tofauti na ile wanayofanya jeshi la polisi ambalo ni la Abdallah Juma Abdallah(CUF)Chongamuungano.Waziri Kivuli wa wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Abdallah Juma Abdallah ameyasema hayo katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kwa wajumbe wa baraza hilo.Abdallah alisema kikosi cha jeshi la kujenga uchumi (JKU) pamoja na kikosi cha Valantia havina kazi za kufnaya na vinahitaji kufutwa ili fedha za bajeti zilizotengwa kwa ajili yao zitumike kwa mambo mengine ambayo ni muhimu kwa wananchi ikiwemo huduma za kijamii kama za matibabu na nyenginezo.“Mheshimiwa Spika hivi vikosi vya SMZ vinatumia fedha nyingi sana za walipa kodi katika kipindi cha miaka mitano jumla ya shilingi billioni 30 zinatumika kwa vikosi hivyo ambavyo kazi zake hazionekani nadhani ni wakati sasa serikali ikaamua kuvifuta kabisa kwani suala la ulinzi tayari jeshi la polisi linafanya kazi hiyo” alisema Abdallah.Endelea kusoma habari hii.

BAJETI YA VIKOSI YAPITA KWA MBINDE

Pandu Ameir Kificho(Spika)SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho amelazimika kuingilia kati nha kuitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutoa ufafanuzi juu ya baadhi ya hoja za wajumbe ikiwa pamoja na fedha millioni 151 zilizolalamikiwa na wajumbe wa baraza hilo kwamba hazina melezo.Awali akifanya majumuisho ya wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga alitoa majibu ya jumla jumla na haraka haraka ambayo kwa kiasi kikubwa inaonekana kutowatosheleza wajumbe wa baraza hilo na kusababisha kupigiwa mabuti wakati wa kupitisha vifungu vya bajeti hiyo.Spika Kificho amelezimika kutoa agizo hilo kwa serikali kutokana Waziri Nyanga kuonesha jawabu zake wakati akitoa ufafanuzi na kujibu hoja zake hazikuwa za kina na kuwatosheleza wajumbe wa baraza hilo jambo ambalo wajumbe hao wamelalamikia jawabu zinazotolewa na baadhi ya mawaziri wanapokuja kufanya majumuisho ya bajeti zao huwa zizikidhi haja ya maswali yalioulizwa.Baadhi ya hoja hizo ikiwemo maelezo ya matumizi ya jumla ya shilingi millioni 151 za matumizi ya ofisi ya vitambulisho vya mzanzibari mkaazi ambazo kwa mujibu wa kamati ya mahesabu ya serikali PAC hazina vielelezo vya kina na wajumbe walitaka kupatiwa maelezo ya kina juu ya matumizi ya fedha hizo zilivyotumika. Endelea kusoma habari hii

MKUU MKOA PEMBA LAWAMANI

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani katika baraza la wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari amesema baadhi ya wakuu wa mikoa wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kinyume dhana ya utawala bora nchini.Hayo DADIyameelezwa na Kiongozi huyo wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar.Bakari alisema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba amekuwa akiwazuwia wananchi kulima katika maeneo ambayo ni mali ya serikali na badala yake amekuwa akiyachukua yeye na kufanyia shughuli hizo kwa kutumia wafungwa kwenda kumlimia.Kiongozi huyo amesema tabia hiyo ni mbaya na haikubaliki katika nchi inayoongozwa katika misingi ya sheria na utawala bora ambapo Zanzibar imekuwa ikijisifia hasa katika siku za hivi karibuni kwamba ipo mstari wa mbele katika kufuata sheria.“Mimi sikubaliani na vitendo vinavyofanywa na viongozi wa serikali mfano mkuu wa mkoa kule pemba amewanyanganya wananchi eneo la ardhi ambalo wananchi masikini za mungu walikuwa wakilitumia kwa kilimo lakini wamenyanganya na sasa eneo hilo kazi ile ile waliokuwa wakilitumia wananchi sasa analitumia yeye sasa nasema tabia hii na kutumia madaraka vibaya ni mbaya sana” alisisitiza Kiongozi huyo. Endelea kusoma habari hii.

 

HALMASHARI HAZISIMAMII FEDHA VIZURI

 

VIONGOZI wa Halmashauri za mkoa wa kaskazini Unguja wameshutumiwa kushindwa kusimamia mapato ya serikali kuu katika mkoa huo na kusababisha migogoro kati yao na madiwani wa sehemu hiyo.Shutuma hizo zimetolewa mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM) Ame Mati Wadi alipokuwa akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao kinachoendelea Mjini Zanzibar.matiMwakilishi huyo alisema huenda kukawa na mchezo mchafu unaofanywa na viongozi hao na kusababisha kutokea migongano kati ya madiwani na wakuu wa mkoa na wilaya hiyo kutokana na matatizo yalioanza kujitokeza katika mkoa huo.Mwakilishi huyo alieleza kwamba Halmashauri za Mkoa huo zimekuwa zikishindwa kusimamia ukusanyaji mapato huku kukijitoleza kutoelewana kati ya madiwani na viongozi hao jambo ambalo limekuwa likiisababishia hasara serikali kuu.Alisema hivi sasa katika mkoa wa kaskazini kumejitokeza mivutano kati ya viongozi hao inayotokana na kasoro za ukusanyaji wa mapato ya serikali yanayohusu miradi ya uwekezaji hasa katika uuzaji wa ardhi ambao umeshamiri sana katika ukanda wa pwani. Endelea kusoma habari hii.

KUINGIA ZNZ KWA VITAMBULISHO

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema unaanzisha utaratibu kwa wageni wote wanaotoka nje ya Zanzibar kuingia na vitambulisho visiwani hapa.Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma hassanamewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana kwamba hatua hiyo ni moja ya mikakati ya serikali kudhibiti wimbi la uhalifu nchini.Alisema serikali itawasiliana na wizara ya mawasiliano na uchukuzi kuona namna gani ya kuweza kudhibiti watu wanaoingia Zanzibar bila ya shughuli maalumu ambapo uhalifu umekuwa ukizidi kukua kila kukicha.Waziri Hamza amesema serikali imeamua kutumia utaratibu huo kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wawakilishi ambao ndio wawakilishi wa wananchi katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.“Tunanzisha utaratibu wa kuingia Zanzibar kwa vitambulisho yaani wenzetu kule bara wanavyo vitambulisho kutoka kwa wakuu wao kama vile serikali za mitaa kwa hivyo mtu akingia Zanzibar atabidi aoneshe kitambulisho ikiwa ni pass port au kitambulisho chochote kile hata cha benki na hili ni kwa sababu ya kudhibiti uhalifu” aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi. Endelea kusoma habari hii.

WABUNGE WATATU WAHAJACHUKUA KADI

Suleiman Othman Nyanga(CCM)JUMLA ya Wabunge watatu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Hamad Rashid Mohammed wameelezwa kuwa bado hawajachukuwa kadi mzanzibari mkaazi zinazotolewa Mjini Zanzibar.Hayo wameelezwa wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Suleiman Othman Nyanga wakati akifanya majumuisho ya mbali mbali ya wajumbe waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2009/10.Nyanga aliyasema hayo kufuatia malalamiko makubwa ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati wakichangia bajeti ya wizara yake ambapo malalamiko hayo yalioelekezwa dhidi ya serikali kuhusiana na wananchi wengi kukoseshwa haki ya kupata vitambulisho vya mzanzibari mkaazi huku idadi kubwa ya wananchi wa kisiwani pemba wakiwa ndio waliokosa haki hiyo.Waziri Nyanga alisema licha ya kasoro za hapa na pale katika utoaji wa vitambulisho hivyo vya mzanzibari mkaazi lakini malalamiko mengine yaliotolewa na wajumbe hayana msingi kwa kuwa wapo baadhi ya wananchi utaratibu wa utoaji wa vitambulisho vyao upo yatari wakiwemo wabunge ambapo wanatakiwa kwenda kuvichukua lakini hadi sasa wameshindwa kuvichukuwa. Endelea kusoma habari hii.

KAMATI HAIJARIDHISHWA

KAMATI ya Katiba, Sheria na Utawala Bora ya Baraza la Wawakilishi imesema haijaridhishwa na ofisi ndogo ya tume ya uchaguzi iliyopo kisiwani Pemba kutokana na mazingira yake kuwa mabaya.Hayo yameeleza na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Haji Omar Kheri alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi ambapo alisema ofisini hiyo majengo yake ni machakavu na hasa katika kipindi cha uchaguzi kinachokuja yatatumika kwa shughuli za uchaguzi.“Kamati yangu hairidhishwi na jengo hili, hivyo inashauri serikali kujenga jengo jengine katika eneo linalofaa kimazingira na kiusalama zaidi. Kutokana na sababu hiyo kamati yangu inashauri kuwekwa ulinzi kutoka katika vikosi vyetu vya SMZ kwa sababu askari wa jesghi la polisi hivi sasa hawatoshi kulinda katika taasisi za serikali” alisema Mwenyekiti huyo.Mwenyekiti huyo amesema kamati yake pia haijaridhishwa kabisa na ugawaji wa fedha za matumizi ya kazi za kawaida kwa taasisi zilizokuwa hazina mafungu, yaani taasisi zilizopo ndani ya fungu la 13 afisi ya waziri kiongozi ambapo kuna dosari zimebainika wakati wa kupitia bajeti ya afisi hiyo.Endelea kusoma habari hii.

SMZ KUWA NA MKAKATI MPYA

 

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inakamilisha miundo mipya ya utumishi ambayo itazingatia usawa wa kazi na malipo kwa wafanyakazi. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Afisi ya Dk. Mwinyihaji Makame(CCM)Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba hatua hiyo itasaidia kuyapatia ufumbuzi malalamiko ya wafanyakazi kuhusu mishahara na uwiano wake kati ya watendaji mbali mbali wa serikali.  Amesema idara ya utumishi serikalini tayari imeshakamilisha miundo ya utumishi kada ya habari na afya na miundo ya taasisi nyengine inatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu. Waziri huyo alisema idara ya utumishi inaendelea kuzifanyia uhakiki takwimu za wafanyakazi ukilinganisha taarifa zilizowasilishwa katika vianzio vyengine kama mfuko wa hifadhi ya jamii, mfumo wa ulipaji wa mishahara hatua ambayo itasaidia kuweka sawa takwimu za watumishi wote wa Serikali. Endelea kusoma habari hii.

KITENDO CHA USALAMA LAAMANI

WAJUMBE wa Baraza la wawakilishi wamekitalumu kitengo cha Usalama Serikalini (GSO), kwamba kinachangia kuajiriwa kwa wafanyakazi wabovu ambao husababisha kutokea wizi katika wizara za serikali. Wajumbe hao waliyasema hayo wakati wakichangia mjadala unaoendelea wa kujadili Bajeti ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la msimbaMapinduzi kwa mwaka wa fedha 2009/10. Walisema ni jambo la kusangaza kuwapo ongezeko la vitendo vya wizi katika idara na wizara za serikali ambapo huenda kitengo hicho kinashindwa kufanya kazi zake vizuri na uadilifu katika kuwachunguza wafanyakazi wanaopewa ajira nchini. Wajumbe hao wamesema kwamba wizara pia imeshindwa kuwapata wale wafanyakazi hewa ambao wameiibia mamilioni ya shilingi serikali jambo ambalo kwa kuwa wafanyakazi hao wapo huenda wakawa wanaendelea na vitendo hivyo vya kuibia serikali kwa kuwa serikali hadi sasa imeshindwa kuwachukulia hatua yoyote dhidi yao. Akichnagia mjadala huo Mwakilishi Jimbo la wa Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk alisema kinachoonekana kwa kiasi kikubwa kitengo hicho kimelala kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya wizi katika maidara ya serikali jambo ambalo limekuwa likiitia hasara serikali.Endelea kusoma habari hii.

MAHINDI KUOTA MNAZI MMOJA

 

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imekiri kuwepo kwa shamba la mahindi katika jengo jipya la ‘Physiotherapy unit’ katika hospitali kuu ya mnazi mmoja lililomaliza kujengwa hivi karibuni kwa msaada wa washirika wa maendeleo. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Shawana Buheti Hassan alipokuwa akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Magogini (CCM) Salmin Awadh Salmin aliyetaka kujua ni kwa nini wizara hiyo imekuwa haithamini juhudi za wafadhili na Salmin Awadh Salmin(CCM)Magomenibadala yake jengo lililofanyiwa ukarabati hivi karibuni limekuwa shamba la mahindi bila ya matarajio ya wengi. “Ili kuweka jengo hilo katika hali nzuri na ya kuvutia kitendo cha physiotherapy kimetengeneza bustani ya maua. Suala la kuchomoza hindi moja moja katika hiyo ni bahati mbaya na sasa hali hiyo imesharekebishwa” alisema Naibu huyo. Alisema kutengenezwa kwa bustani hiyo kunaleta faraja kwa wagonjwa wanaokuja kupatiwa matibabu hivyo sio jambo baya lakini kasoro zilizojitokeza zote zimeweza kurekebishwa ikiwemo kuchomoza kwa mahindi katika bustani hiyo. Endelea kusoma habari hii.

MJI MKONGWE KUKAGULIWA

Ali Suleiman Ali(CCM)SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imekusudia kufanya ukaguzi maalumu wa majengo ya Mji Mkongwe ambayo hivi sasa yapo katika hali mbaya ya kuporomoka. Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujua wizara ina mpango gani ya wa kufanya ukaguzi kwa lengo la kuwanusuri wananchi wanaoishi katika majengo hayo machakavu. Naibu Waziri huyo alisema wizara yake kupitia mamlaka ya mji mkongwe ina mpango mahsusi wa ukaguzi wa majengo ya mji mkongwe ambapo mara katika majukumu makubwa ya mamlaka ni kufanya ukaguzi wa mejengo ya mji huo ambayo yapo katika hali tatu. Akizitaja hali hiyo alisema ni majengo yaliokuwa katika hali mbaya kabisa, majengo yaliokuwa kati na kati kiuzima na majengo yaliokuwa katika hali nzuri ambayo inaridhisha. Endelea kusoma habari hii.

ZNZ KUTANGAZA UTALII NDANI NA NJE

WIZARA ya Utalii, Biashara na Uwekezaji imesema licha ya kukabiliwa na ukosefu wa fedha katika kamisheni ya utalii lakini inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa wa kuitangaza Zanzibar kiutalii katika nchi za nje. Akijibu swali la msingi katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini ali dengeZanzibar, Waziri wa wizara hiyo, Samia Suluhu Hassan amewaambai wajumbe kwamba moja ya mikakati ya kazi nyingizi za kamisheni ya utalii ni kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi. Jibu hilo limefuatia swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Amani (CCM) Ali Denge Makame ni mikakati gani iliyowekwa ya kuitangaza Zanzibar kitalii hasa kwa kuwa hoteli ngizi za kitalii zinazidi kuongezeka. Akiitaja mikakati inayofanywa na kamisheni ya utalii alisema ni pamoja na kushiriki katika maonesho ya kimataifa ya utalii ambayo hufanyika katika nchi mbali mabli duniani. Endelea kusoma habari hii.

ZNZ HAINUFAIKI NA GESI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema hadi sasa haijafaidika na mgao wa gesi inayozalishwa Tanzania licha ya kuwa mambo ya mafuta na maliasili hizo kuwa chini ya orodha ya mambo ya muungano.Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma aliyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani hassan(CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujuwa Zanzibar imefaidika vipi na gesi inayozalishwa Tanzania Bara. Hamza alisema Zanzibar haijafaidika na mgao wa gesi inayozalishwa Tanzania Bara, licha ya suala hilo kuwa chini ya muungano yaani mgawanyo wa maliasili ya mafuta na gesi. Aidha Hamza alisema kwamba Zanzibar atika mikakati ya kuunda chombo ambacho kitashungulikia uchimbaji wa mafuta na tayari suala hilo limeshazungumzwa mara kadhaa. Endelea kusoma habari hii.

WAWAKILISHI WAIJIA JUU SERIKALI

Ali Mzee Ali(CCM)kuteuliwaWAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi, wameijia juu serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutokana na ucheleweshaji wa utoaji wa mikopo ya mfuko wa mabilioni ya Jakaya Kikwete na Amani Karume. Wajumbe hao waliojekana kuja juu baada ya kauli ya Waziri kiongozi kueleza kuwa hadi sasa serikali imeweza kutoa shilingi milioni 203,700,00 ikiwa ni sawa na asilimia 19.6 kwa wananchi kati ya fedha zilizotolewa na marais hao shilingi bilioni 1.2. Nahodha, katika maelezo yake alifahamisha kati ya fedha hizo Mkoa wa Mjini Magharibi ulipatiwa shilingi 116,350,000, Mkoa wa Kaskazini Unguja shilingi 6,150,000 huku Mkoa wa Kusini Pemba ukipatiwa shilingi 81,2000,000, na Kusini Unguja ni shilingi 31,500,000 ambapo Kaskazini Pemba bado hawajaanza kupata mikopo hiyo. Kutolewa kwa maelezo hayo yameonekana kutowarisha baadhi ya wawakilishi ambapo walieleza kuwa kwa kiasi kikubwa ni yenye kuitia aibu serikali. Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM), Ali Suleiman Ali, alisema idadi iliyotolewa bado ni ndogo kwa watu waliopewa fedha hizo jambo ambalo linawasababishia kero kwa wananchi katika majimbo yao na niabu kwa serikali. Endelea kusoma habari hii.

SIJARIDHISHWA NA RIPOTI -NAHODHA

Shamsi Vuai Nahodha(CCM)Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, amesema hajaridhika na ripoti ya hali ya ajira nchini iliyofanywa na Kamisheni ya Kazi na Idara ya Uhamiaji kwa kuwa ina udanganyifu mwingi. Amesema kwamba ripoti hiyo huenda kukawa na udanganyifu ndani yake kwa kutokana na kiwago kilichoanishwa cha wageni wanaofanyakazi nchini ni kidogo ikilinganishwa na hali halisi ilivyo. Akiwasilisha bajeti ya matumizi na mapato ya Wizara ya Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi kwa mwaka wa fedha 2009/10, Nahodha, alisema kwa kiasi kikubwa serikali haijaridhika na ripoti iliyowasilisha na Idara ya kazi katika kufuatia hali ya ajira nchi. Amesema kuna haja ya kutayarishwa ripoti nyengine katika kipindi cha mwezi mmoja kwa kuwa maeneo mengi katika ripoti hiyo yaijataja hivyo kumekuwepo na upungufu wa taarifa. Kauli ya waziri Kiongozi inakuja baada ya taarifa ya Idara hiyo kueleza kwamba katika utafiti waliagizwa kuufanya na kiongozi huyo kikao kilichopita kuonesha kwamba kuwapo wageni 605 waliopewa vibali vya kufanyia kazi hapa nchini. Endelea kusoma habari hii.

SMZ HAINA ZANA ZA UOKOZI

DSC_8647Mwakilishi wa Jimbo la Kitope (CCM) Mshimba Mbarouk Makame amesema amesikitishwa kitendo cha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushindwa kuwa na timu ya uokozi wakati yanapotokea majanga ikiwemo yale kuzama kwa vyombo vya baharini. Akichangia makadirio ya serikali ya bajeti ya wizara Ofisi ya waziri kiongozi kwa mwaka wa fedha 2009/10 katika kikao cha baraza la wawakilishi mjini hapa Makame alisema ni kitendo cha aibu kwa mamlaka ya bandari kukosa timu ya uokozi wakati ilipotokea ajali ya Mv. Fatih mwezi uliopita uokoaji haukuwa mzuri. “Kweli ni kitendo cha kushangaza sana kuona taasisi za serikali zinakosa timu ya uokozi wa majanga ya kuzama kwa vyombo vya baharini….ajali ya Meli ya Fatihilitusikitisha sana kwa sababu ilizama katika eneo la bandari ya Zanzibar lakini uokoaji wake sote haukuturidhisha” alisema Mwakilishi huyo. Endelea kusoma habari hii.

BAJETI YA WAZIRI KIONGOZI YAPATA VIKWAZO

BAJETI ya Wizara ya Afisi ya Waziri Kiongozi imepata vikwazo na kupita kwa tabu baada ya mafungu ya shughuli ya Idara ya Maafa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kusababisha hiyo kupata mikwaruzo ya kukwama wakati wa kupitishwa kwa vifungu kupigiwa mabuti kadhaa. Hali hiyo Abubakar khamis Bakari (CUF)MGOGONIilijitokeza wakati Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakiwa katika Kamati ya Baraza hilo kwa ajili ya kupitisha makadirio ya mapato na Matumizi ya afisi ya Waziri Kiongozi kwa mwaka wa fedha 2009/10. Wakati Watendaji wa Baraza hilo wakitaja mafungu hayo yalijikuta yakipata kizuizi cha kutoendelea baada ya Mwakilishi wa jimbo la Mgogoni (CUF) Abubakar Khamis Bakari kuzusha utata wa kisheria barazani hapo. Endelea kusoma habari hii.

TUME YA UCHAGUZI LAWAMANI

DSC_8680WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kusitisha haraka zoezi la uandikishwaji wa wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa madai kwamba maandalizi yake hajakamilika. Kauli hiyo imetolewa na wajumbe wa baraza hilo kutoka kambi ya upinzani waliokuwa wakichangia bajeti ya waziri kiongozi katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa ambapo Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) imepanga kuanza shunguli za zoezi hilo mwezi ujao Micheweni Kisiwani Pemba. Wajumbe wa baraza hilo walielezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu wananchi wengi kukosa haki zao za msingi za kupiga kura kwa kuwa tayari baadhi ya vitimbi na mizengwe imeshaanza kuoneshwa katika zoezi lililopita wakati wa uchaguzi mdogo wa Magogoni ambapo baadhi ya wananchi walikoseshwa haki hiyo. Endelea kusoma habari hii.

SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA CHUO

Ali Suleiman Ali(CCM)SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) itahakikisha inamaliza ujenzi wa Chuo kipya kitachukuwa kikitoa mafunzo ya utumishi baada ya jengo linalotumika sasa kuchakaa na kuwatia ghofu ya kuporomokewa na jengo hilo wafanyakazi na wanafunzi.Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali, katika kikao kinachoendelea kufanyika Mjini hapa. Mwakilishi huyo alieleza kwamba jengo la Chuo cha Utumishi linalotumika sasa liliopo huko Forodhani Mjini Unguja, lipo katika hali mbaya na kiasi cha kuhatarisha maisha ya wanachuo na serikali ina mpango gani wa kuweza kupatikana jengo jengine kwa vile wazanzibari wengi wanataka kupata elimu katika Chuo hicho. Endelea kusoma habari hii.

SERIKALI KUWEKA WAZI VIDOKEZO VYA VIFO

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imesema katika bajeti ijayo ya Wizara hiyo 2009/2010 itaweka wazi vidokezo hatari vinavyoonekana kuwa ni hatari kutokea kwa vifo vya Mama na Mtoto wakati wa ujazito na kujifungua. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar, Sultan Mohammed Mugheiry, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la nyongeza la Thuwaiba Edington Kisasi(CCM)wanawakeMwakilishi wa Wanawake, (CCM) Thuwaiba Editongton Kisasi ambaye alitaka kujua ni kwa sababu gani vifo vya akina mama vinaendele akutolea wakati wa kujifungua na sababu za kutokea vifo hivyo. Mwakilishi huyo alidai kuwa ni kwa nini suala hilo halipatiwi ufumbuzi licha ya kelele zote zinazopigwa na wawakilishi ambapo alisema huenda likawa linatokana na gharama za uchangiaji kiasi ambacho huwafanya baadhi yakina mama kutomudu gharama hizo na ndipo hujichukulia uamuzi wa kujifungulia nyumbani na kusababisha vifo hivyo. Endelea kusoma habari hii.

HAKUNA UPENDELEO KATIKA MIRADI

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Mazingira imekanusha kugawa miradi ya bishurakilimo ambayo iko chini miradi ASSP kwa upendeleo bali imekuwa ikifanya hivyo baada ya wananchi kujichagulia wenyewe katika maeneo yao. Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Mazingira, Khatib Suleiman Bakari, aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu masuala ya nyongeza ya baadhi ya wawakilishi walitaka kujua ni vigezo gani vinavyotumika katika kutoa miradi hiyo kwa wananchi. Wajumbe wao walisema kumekuwepo na upendeleo wa miradi kwa wakulima ambapo Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile (CUF) Muhiddini Mohammed Muhiddin, alitaka kujua kwa nini wananchi wanapewa miradi na wengine hanakoseshwa huku akitaka kujua vigezo ambavyo serikali imekuwa ikivitumia kutoa miradi hiyo kwa kuwa amekuwa akiona kuwa Unguja imepatiwa miradi mingi kuliko Kisiwani Pemba. Endelea kusoma habari hii.

MAFUTA NA GESI YANASHUGHULIKIWA

Dk. Mwinyihaji Makame(CCM)

Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema suala la mgawanyo wa rasilimali ya mafuta na gesi asilia linashungulikiwa na ngazi husika. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea mjini hapa. Mwinyihaji alisema tayari baraza la wawakilishi kupitia wajumbe wake wamelichangia na kutoa maoni yao na sasa lipo katika ngazi husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Endelea kusoma habari hii.

WAZIRI APUUZA YAKWIMU ZA WAPINZANI

Said Ali Mbarouk(CUF)GandoWaziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini amesema hakubaliani na takwimu zinazotolewa na Kambi ya upinzani katika baraza hilo kwa kuwa takwimu hizo sio sahihi. Mwadini alisema hayo wakati akijibu hoja za wajumbe mbali mbali waliochangia bajeti ya serikali ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 katika kikao kinachoendelea mjini hapa. “Waheshimiwa wajumbe hii bajeti iliyowasilishwa na waziri kivuli ni ya kujifurahisha tu….haina ukweli kwani takwimu zilizotumika ni za kuokota na sio sahihi kabisa” alisema Waziri huyo. Mwadini alikuwa akijibu bajeti kivuli iliyowasilishwa na Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Said Ali Mbarouk ambaye katiak hutuba yake alisema bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 haijitegemei kwani nguvu zake nyingi zimeelekezwa kwa kwa wafadhili na hivyo kubaki kuwa ni majeti tegemezi. Endelea kusoma habari hii.

FAIDA ZA BOT BADO HATUJANUFAIKA NAZO -SMZ

Shamsi Vuai Nahodha(CCM)Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema suala la hisa za Zanzibar katika Benki Kuu Tanzania (BOT) na gawio la faida zake bado halijapatiwa ufumbuzi hadi sasa. Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009-2010 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa. Waziri Kiongozi amesema wizara mbili za fedha na uchumi ya serikali ya mapinduzi zanzibar pamoja na wizara ya fedha na uchumi ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania zimeagizwa zikutane kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo hali bado ufumbuzi wake haijapatikana. Nahodha alisema wizara mbili hizo zinatakiwa kukutana na kutoa ripoti ya mwisho katika kikao kijacho lakini hakuwaambia wajumbe wa baraza hilo kuwa kikao hicho lini kitafanyika. Endelea kusoma habari hii.

 

TUMEJIPANGA KUPUNGUZA VIFO-SMZ

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imesema imejipanga vyema katika kuhakikisha inapunguza kwa kasi vifo vya akina mama waja wazito wanaojifungua katika hospitali zake za Unguja na Pemba. sultan mohd mugheiry waziri wa afya na ustawi wa jamii  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Sultani Mohammed Mugheiry alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi kutokana na swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin aliyetaka kujuwa mikakati ya wizara katika kukabiliana na vifo vya akinamama wajawazito. Mugheiry alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha inaimarisha huduma za afya kwa mama wajawazito na kuwa bora zaidi kwa lengo la kuwasaidia akina mama hayo kujifungua kwa urahisi zaidi na kuwahamasisha kujifungulia katika vituo vya afya. Endelea kusoma habari hii.

 

WAPEMBA WATENGWA -MWAKILISHI

Muhiddin Mohd Muhiddin(CUF)MtambileKAMBI ya Upinzani katika baraza la wawakilishi imeilalamikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwamba imekuwa ikikitenga kisiwa cha Pemba kwa kushindwa kuffikisha miradi ya maendeleo sawa na miradi inayofanywa Unguja.  Mwakilishi wa Mtambile (CUF) Muhiddin Mohammed Muhiddin aliyasema hayo wakati akichangia bajeti ya maendeleo ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2009-2010 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini hapa. Muhiddin alisema kisiwa cha Pemba kimetengwa katika utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ukilinganisha na kisiwa cha Unguja ambapo hivi sasa kisiwa hicho kimekuwa kinakosa wawekezaji kutokana na hali mbaya ilivyo. “Tumeshasema sana kuhusiana na susla hili na leo tunasema tena kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imekitenga kisiwa cha Pemba katika miundo mbinu ya barabara….angalia zaidi ya kilomita 47.2 zimekamilika katika kisiwa cha Unguja wakati katika kisiwa cha Pemba ni barabara kilomita 6.5 za Mkoani na Konde huu ndio usawa gani jamani” alilalamika Mwakilishi huyo. Endelea kusoma habari hii.

KILIMO KILETE MABADILIKO ZNZ

Abass Juma MhunziWajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema ili kilimo kiweze kuwa na mabadiliko hivi sasa kauli mbiu ya siasa kilimo iwachwe na badala yake iwe uchumi ni kilimo na serikali ifikirie kuondoa kila asilimia tano zilizotengwa kwa matumizi ya kila sekta kupelekwa katika kilimo. Wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajete ya serikali katika kikao kinachoendelea, Mwakilishi wa Jimbo la Chambani (CUF), Abass Juma Mhunzi, amesema serikali inapaswa kuyaangalia maeneo makubwa zaidi ikiwemo sekta binafsi ambayo yatawezakuchangia katika kilimo kutokanna kuonekana eneo hilo limeachwa kutoa mchango wake katika sekta ya kilimo. Mwakilishi huyo alisema ni vyema kwa vyanzo vya uchangiaji wa mapato ya taasisi za Muungano vinavyopata huduma hapa Zanzibar, kuona kodi zao zinaingia katika mfuko wa hazina wa Zanzibar, ili kuweza kusaidia katika uinuaji wa shughuli za sekta mbali mbali. Endelea kusoma habari hii.

SHAMHUNA ASHANGAZWA

Serikali ya Mapinzuzi Zanzibar (SMZ) imewashangazwa na watu wanaoibeza bajeti ya mwaka 2009/2010 wakati mchumi aliyebobea katika masuala ya uchumi Profesa Ibrahim Lipumba imeitaja kama ni bajeti iliyoshiba matumaini kwa jamii Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na ali juma shamhunaMichezo na Utamaduni Ali Juma Shamuhuna ametoa kauli hiyo leo wakati akichangia bajeti hiyo ya serikali katika baraza la wawakilishi na kusema wanaoitaja bajeti hiyo imejaa utegemezi wanajaribu kuposha ukweli ulivyo. Alisema Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF ni mchumi aliyesomea na kufuzu masuala ya uchumi na kimsingi aliisifu bajeti hiyo na kuiona imebeba maslahi ya umma kimaendeleo hasa katika suala zima la kuweka mkazo kuhusu utoaji wa huduma kwa jamii. Endelea kusoma habari hii.

WATENDAJI WA SMZ WALAUMIWA

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamewashutumu watendaji wakuu wa serikali kuwa ndio chanzo kikuu cha kuongezeka kwa migogoro kadhaa visiwani hapa ikiwemo migogomoro ya ardhi inayotokea kila mra katika vijiji mbali mbali visiwani hapa. Wajumbe hao wameyasema hayo wakati akichangia bajeti ya makaridio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010 kikao kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar. DSC_8658Wamesema kwamba tabia inayooneshwa na watendaji wa ngazi mbali mbali serikali haiwezi kumsaidia Rais na serikali yake bali baadhi ya watendaji hao wanafanya hivyo kwa makusudi ili kuiporomosha na kuiondoshea hadhi serikali inayoongozwa na Rais Karume. Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe(CCM) Ame Mati Wadi alisema kwamba amekuwa na khofu juu ya kuwapo kwa hujuma za makusudi zinazofanywa na baadhi ya watendaji hao waovu zinazotaka kuiharibia serikali juhudi zake za kutaka kusukuma maendeleo nchini na kusababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha migogoro ya ardhi inayojitokeza kila kukicha hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba. Endelea kusoma habari hii.

BAJETI YA SMZ YAPONDWA

Salmin Awadh Salmin(CCM)MagomeniWakati baadhi wa wawakilishi wakiisifia bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 2009/10 kama imetizama zaidi maslahi ya jamii Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Awadhi Salmin Awadh ameiponda vibaya na kuiiti bajeti hiyo ni tegemezi mno. Mwakilishi huyo ameizodoa bajeti iliyowasilisha na Waziri Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk Mwinyihaji Makame Mwadini akisema ni tegemezi kwa asilimia 89 ikitegemea misaada ya nje huku mchango wa SMZ ni asilimia 17 jambao ambalo alisema ni hatari kwa nchi. Alionya akisema kuwa utegemezi huo ni mkubwa na kwamba iko siku wahisani na taasisis za nje wakisusa nchi na serikali inaweza kukwama na kupoteza wasta wake kwa wananchi. Mwakilishi huyo akisema kwa ujasiri na kujiamini alidai hatua hiyo ya utegemezi mkubwa mno kwa misasada ya nje bila ya njia mbadala ya vyanzo vya mapato inaweza kuifanya serikali ishindwe hata kutengeneza barabara. Endelea kusoma habari hii.

POLISI JAMII IMELETA MAFANIKIO -SMZ

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abddalla Shaaban amesema dhana ya polisi jamii ipo katika nchi nyingi duniani ikiwa na lengo la kuwashirikisha wananchi katika kusaidia jitihada za kuweka ulinzi katika nchi husika. Waziri Shaaban ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Koani (CCM) Ramadhan Abdallah ShaabanMkema Haji Mkema aliyetaka kujua iwapo jitihada za serikali zimefikia kikomo na ndio maana kukaanzishwa polisi jamii kwa kuwashirikisha wananchi. Waziri huyo amesema kwamba serikali wala jeshi la polisi halijashindwa na kazi zake lakini kinachofanyika ni kuwashirikisha wananchi kwa kwa kuwa polisi waliopo ni wachache ikilinganishwa na idadi ya wananchi nchini. Amesema mfumo huo wa kuwashirikisha wananchi kusaidia jeshi la polisi upo katika nchi nyingi duniani hivyo Tanzania kuazisha dhana hiyo sio jambo geni kwani tayari limeshakuwepo katika nchi nyengine. Endelea kusoma habari hii.

ELIMU MBADALA HADI PEMBA SASA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kituo cha elimu mbadala katika kisiwa cha Pemba kinatazamiwa kujengwa mwakani baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kukubali kungaramia ujenzi huo. Haroun Ali Suleiman(CCM)Akijibu maswali na majibu wa wajumbe wa baraza la wawakilishi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman alisema Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imekubali kujenga kituo hicho katika kijiji cha Wingwi kisiwani Pemba. Mwakilishi Mfenesini Ali Abdalla Ali (CCM) alisema kwa kuwa Unguja tayari kuna kituo cha elimu mbadala ni lini kituo kama hicho cha elimu mbadala kitajengwa kwa upande wa kisiwani Pemba. Waziri Suleiman alisema serikali na mpango huo wa kuhakikisha vituo kama hivyo vinavyojengwa Unguja na Pemba kujengwa ili kuwapunguzia gharama wananchi wa Pemba ambao hufuata huduma za elimu Unguja. Endelea kusoma habari hii.

MNADHIMU WA CUF ATEULIWA

 

Haji Faki Shaali (CUF)Chama Cha Wananchi (CUF) kimemteuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni, Haji Faki Shaali (52) kuwa Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi kupitia Kambi ya Upinzani barazani hapo. Uamuzi huo umetangazwa na Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho alipokuwa akitoa tangazo hilo kabla ya kuanza kikao hicho ambapo aliwajulisha wajumbe kuwa kuanzia sasa mnadhimu wa kambi ya upinzani atakuwa Shaali kufuatia yaliyofanywa na kambi ya upinzani baada ya aliyekuwa mnadhimu wake kufariki dunia mwezi uliopita. “Waheshimiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi napenda kuwajulisha kwamba Mheshimiwa Haji Faki Shaali ameteuliwa kuwa mnadhimu wa baraza la wawakilishi wa kambi ya upinzani kuanzia sasa “ alisema Spika Kificho na kupigiwa makofi. Spika Kificho alisema kifo cha Mwakilishi wa Wawi Soud Yussuf Mgeni aliyefariki dunia mwezi uliopita kumefanya kutokee kwa mabadiliko hayo na kutakiwa kambi ya upinzani iteuwe mjumbe mwengine atakayeweza kushikilia nafasi hiyo. Endelea kusoma habari hii.

KITI CHA WAWI KIWAZI -SPIKA

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ametangaza kiti cha Jimbo la Wawi Kisiwani Pemba kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Soud Yussuf Mgeni (CUF) aliyefariki dunia mwezi uliopita kutokana na ugonjwa wa saratani. Pandu Ameir Kificho(Spika) Spika Kificho amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba kiti cha uwakilishi wa jimbo la kwa sasa kipo wazi na tayari wameshawaarifu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kama utaratibu unavyoelekeza. ”Wahesimiwa wajumbe tayari nimetoa taarifa kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuhusiana na kifo cha mwakilishi wa jimbo la Wawi kwa tiketi ya CUF, Marehemu Soud Yussuf Mgeni kuhusu kifo chake kama utaratibu unavyonielekeza” alisema Spika Kificho. Alisema pamoja na kuwa ameshaitaarifu Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) lakini jawabu ilitoka katika tume kuhusiana na kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Wawi kwa sasa haupo. Endelea kusoma habari hii.

BAJETI BADO NI TEGEMEZI-LIPUMBA

DSC00418Mwenyekiti wa Chama Cha wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haroun Lipumba amesema inashangaza kwa serikali zote mbili ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kutegemea zaidi misaada ya wahisani kwa asilimia 40 katika bajeti zake za mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya kuwasilishwa kwa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 nje ya viwanja wa Baraza la wawakilishi Mjini Zanzibar Professa Lipumba alisema kitendo cha serikali kutegemea bajeti za nchi wahisani ni aibu kubwa. Alisema nchi za Afrika tayari zimejikomboa na zinapaswa kuweka mipango madhubuti katika kufanikisha uchumi wake katika nchi hizo na sio vyema kutegemea wahisani kwa kuwa rasilimali za zao ni nyingi hasa Tanzania ambayo ina utajiri mkubwa wa rasilimali zake. “Haipendezi kuona nchi wahisani ndio wanaotegemewa saa katika bajeti zetu kwani bajeti zote mbili bado ni tegemezi ni aibu kubwa na kwa kweli ni tatizo kubwa kwa taifa letu” alisema Professa Lipumba. Endelea kusoma habari hii.

MISHAHARA YA SMZ YAPANDISHWA

kondeSERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesoma bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2009/20010 katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza jana na kuongeza kima chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa serikali kutoka TSh. 80,000 kufikia TSh. 100,000 kwa mwezi. Akiwasilisha bajeti hiyo mwa wajumbe wa baraza la wawakilishi Waziri wa Fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010. Waziri Mwinyihaji alisema hatua hiyo serikali inaichukua ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume katika sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi 2009, ambapo aliagiza kuangaliwa uwezekano wa kuongeza kima cha chini cha mshahara.  Alisema kutokana na uduni wa maisha ya wafanyakazi wa SMZ, serikali imeamua kima chini cha mshahara kitakuwa ni shilingi 100,000 kutoka TSh. 80,000 walizokuwa wakipata kwa mwezi. Endelea kusoma habari hii.

KHATIB ANATAKA URAIS WA ZNZ -WAJUMBE

 

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamemkaanga Waziri wa mohammed-seifNchi Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano) Mohammed Seif Khatib na kusema kwamba asitegemee kuitumia nafasi kwa kujipendekeza katika suala zima la mafuta na gesi asilia kwa ajili ya kumsafishia njia ya kugombe nafasi ya urais wa urais wa Zanzibar mwaka 2010. Wajumbe hao wamedai kwamba Khatib hana maslahi ya wananchi wa Zanzibar na amekuwa akijipendekeza kwa ajili ya kutaka urais wa Zanzibar kupitia mgongo wa muungano na kumtaka kusahau urais wa Zanzibar.Akichangia hoja ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu mependekezo ya Mshauri Mwelekezi juu ya suala la mafuta na gesi asilia iliowasilishwa juzi Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali alisema hakuna Khatib anajipendekeza katika serikali ya Muungano. Endelea kusoma habari hii.

WAFANYAKAZI HEWA WASHITAKIWE

Mwakilishi wa Jimbo la Koani (CCM) Haji Mkema Haji ameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwachukulia hatua wafanyakazi waliobainika kuiba fedha za serikali kwa njia ya kutumia mishahara hewa ya wafanyakazi. Mkema alisema sambamba na hilo kabla ya kupandishwa mahakamani kwa wafanyakazi hao watakiwe pia kuzirejesha haraka fedha zote walizoiba ili iwe fundisho kwa wengine ambao nia yao ni kuiibia serikali na mali za umma. Mkema aliyasema hayo katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa wakati akichangia ripoti ya kamati ya kuchunguza hesabu za serikali na mashirika ya umma (PAC) ambayo imewasilishwa na Kaimu Mwenyekiti Fatma Ferej Abdulhabib baada ya Mwenyekiti wake, Abass Juma Mhunzi kujiuzulu mwezi mmoja uliopita. Endelea kusoma habari hii.

SANA ENTERPRISES WAONYWA

Hamza Hassan Juma(CCM)WIZARA ya Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi imesema kuwa katika kuweka mazingira mazuri ya biashara katika kituo cha biashara cha Saateni imetoa barua za onyo kwa mmiliki wa Kampuni ya SANA Enterprises Ltd, kwa kuvamia eneo hilo na kujenga maduka yake binafsi. Waziri wa Wizara hiyo Hamza Hassan Juma, aliyasema hayo jana mbele ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati akisaidia masuala ya nyongeza baada ya kuhojiwa nabaadhi ya Wajumbe haokwama kuna eneo ambalo tayari limejengwa maduka ya kudumu huku serikali ikidaikuwa ina mpango yakulifanya eneo hilo kuwa kubwa zaidi. Waziri Hamza alisema ni kweli hali hiyo wameiona na katika hatua za awali tayari wamemuandikia mmiliki wa maduka hayo barua ya kumtahadharisha juu ya matumizi anayoyafanya katika eneo hilo kuwa hayapo rasmi. Endelea kusoma habari hii.

 HATUJAAMUA KUONDOA FEDHA ZETU-SMZ

TATIZO la kuwapo kwa Mtikisiko wa fedha Duniani, Serikali ya Zanzibar, imesema bado haijaamua kuziondoa fedha zake za kigeni katika benki ambazo imeamua kuziweka. Waziri anaeshughulikia Fedha naUchumi, Dk, Mwinyihaji Makame, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman aliyetaka kujuakama serikali ina mpango wakuziondoa fedha zakigeni katika mabenki yanje kutokana nabaadhi mataifa kufanya hivyo. Rashid Seif Suleiman(CUF)ZiwaniAkijibu hilo alisema ni kwelibaadhi ya mataifa yameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuzihamishia fedha zao katika maeneo salama lakini serikali ya Zanzibar bado haijaamua kuchukua hatua hiyo. Waziri huyo alisema madhara ya mtikisiko huo bado hayajaonyesha kuwa ni makubwa katika msuko suko huo wafedha lakini tayari nchi za Afrika ikiwemo Tanzania wanalifanyia kazi suala hilo. Endelea kusoma habari hii.

WANAOUZA MBOLEA WASEMWE

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar inawataka Wakulima ambao wataouziwa mbolea ama dawa ya magugu kwa bei ya juu badala yake iliyowekwa na Serikali kutoa taarifa kwa uongozi wa wizara hiyo. Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Khatib Suleiman,alitoa tamko hilo jana wakati akijibu suala la nyengeza la mmoja wa Mwakilishi wa CCM ambae alidai kuwapo kwa kwa baadhi ya Watendaji wanaouza dawa ya magugu kwa bei ambayo sio iliyotangazwa na serikali. Akijibu suala hilo alisema Wizara yake bado haijapata malalamiko hayo na pindipo itapoya baini iko tayari kuwachukulia hatua watendaji wataokuwa wamehusika na Wakulima wawe tayari kuwabainisha wakorofi hao. Endelea kusoma habari hii.

TATIZO LA MAJI WANAWAKE WAWA WAFUPI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kurekebisha haraka suala bishuraupatikanaji wa maji safi na salama katika visiwa vya Unguja na Pemba ili kuwanusuru wanawake wasidhurike kutokana na kufuata huduma hiyo masafa marefu. Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake, Ashura Abeid Faraja, amesema kwamba tatizo la maji likidumu kwa muda mrefu  katika maeneo kadhaa ya Zanzibar litaweza kuwafanya wanawake wawe wafupi tofauti na maumbile yake. “Mheshimiwa Spika hili tatizo la maji mnajua kuwa limechangia sana kuwafanya wanwake wawe wafupi kutokana na kubeba madoo ya maji kila siku na kila wakati? Jee mnajua kuwa wanawake wanahangaika sana na madoo na madumu kwa kujitwisha kichwani? Alihoji Mwakilishi huyo ambaye ana umri wa miaka zaidi ya 70 na kuwaacha wajumbe wengine na kicheko. Endelea kusoma habari hii.

WAMILIKI WA ARDHI NI SERIKALI

DSC_8615 Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema serikali ya Zanzibar haitakubali kuona wananchi wanakoseshwa ardhi katka nchi yao na kumilikishwa watu wasiostahiki. Alisema bado serikali itabakia kuwa mlinzi wa ardhi ya Zanzibar kwa ajili kuweza kuwafaidisha wananchi na haitakuwa tayari kuona wanamilikishwa watu ambao watasababisha vizazi vijavyo kukosa makaazi. Waziri Kiongozi aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati akijibu suala la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mtamwe (CUF) Salim Abdallah Hamad aliyetaka kujua ni sababu zipi zinazopelekea serikali kungangania kuwa wamiliki ardhi badala ya kuwaachia wananchi maeneo ya ardhi kuwa mali yao. Endelea kusoma habari hii.

BIMA ZNZ YAKUSANYA BILLIONI 7 MWAKA JANA

Ali Mohd Bakari(CUF)TumbeWAZIRI wa Nchi, Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayeshughulikia Fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini amesema kiasi shilingi  7,607 Bilioni zimekusanywa na Shirika la Bima Zanzibar ikiwa ni mapato yanayotokana na bima mbali mbali kwa vituo vya Tanzania na Zanzibar. Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake, (CCM) Amina Iddi Mbarouk aliyetaka kujua Shirika la Bima Zanzibar limefanikiwa kwa kiasi gani katika ukusanyaji wa mapato Tanzania Bara na Visiwani, Waziri huyo alisema zaidi ya billioni saba zimekusanywa kwa mwaka jana pekee. Alisema Shirika la Bima limefanikiwa kwa kiasi kikubwa tangu kuanzishwa kwa matawi sehemu mbalimbali za Tanzania Bara na kwamba mapato yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka. Endelea kusoma habari hii.

HATUJAMSAIDIA MWEKEZAJI -SMZ

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kuwa Serikali haijachukua hatua yoyote ya kumsaidia mwekezaji wa kiwanda cha sukari cha Mahonda Unguja kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar, Burhan Saadat Haji(CCM) KikwajuniBurhan Saadat Haji aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba baada ya Shamba la miwa liliopo mahonda kuungua moto hivi karibuni kumekuwepo na maneno mengi kuwa mwekezaji huyo amesaidiwa na serikali jambo ambalo sio la kweli. Waziri Haji, aliyasema hayo kufuatia swali la nyongeza aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujua ni hatua gani Serikali imechukua baada ya kuungua kwa shamba la miwa la mwekezaji wa kiwanda hicho na moto huo ulisababishwa na nini. Endelea kusoma habari hii.

 SMZ YAKIRI UHABA WA WALIMU

Ali Abdallah AliSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kuwepo kwa upungufu wa walimu kwa baadhi ya mikoa yake ya Unguja na Pemba. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khamis Jabir Makame, aliyasema hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu swali na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujua ni kwa nini Mkoa wa Kaskazini Unguja umefanya vibaya katika matokeo ya kidato cha pili na darasa la saba. Alisema kufanya vibaya huko kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na upungufu wa walimu, sambamba na kuweko chini ufundishaji wa walimu pamoja na usimamizi dhaifu kwa baadhi ya walimu kutowajibika ipasavyo ikiwemo wanafunzi kujishughulisha na biashara ya utalii badala ya masomo. Endelea kusoma habari hii.

 BANDARI YA MALINDI INAKUSANYA MAMILIONI

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Ali Mzee Ussi, amesema jumla ya shilingi 1,061,492,461.96 zimekusanywa kutokana na shughuli za bandarini kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu. Alisema katika kipindi hicho jumla ya meli 29 zenye uzito wa GRT 284,838.00 zimehudumiwa ambapo kati ya hizo meli sita zilikuwa za mizigo mchanganyiko, meli 13 za makontena na meli 10 za kitalii. Naibu huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali, aliyetaka kujua tangu kufunguliwa kwa gati mpya ya Malindi ni kiasi gani kimekusanywa kwa shughuli za bandarini na ni meli ngapi zimeingia katika kipindi hicho. Endelea kusoma habari hii.

 MASHAMBA YA MIPIRA YANA FAIDA-SMZ

juma Kassim Tidwa(CCM)mkuu wa mkoa kusini pembaJUMLA ya shilingi 498,750,000 sawa na dola za Marekani 375,000 zimepatikana kutokana na ukodishwaji wa mashamba ya mipara yaliyopo maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba. Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayeashughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, aliwaambia wajumbe hao wakati akijibu maswali mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi Maisara Mjini Zanzibar. Akijbu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni (CCM) Anaclet Thobias Makungila, aliyetaka kujua Serikali imefaidika kwa kiasi gani kutokana na ukodishwaji wa mashamba ya mipira yaliopo Unguja na Pemba. Endelea kusoma habari hii.

 BAA ZINAZOKWENDA KINYUME NA MAADILI KUFUNGWA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea kuzifunga baa zote zilizopo kwenye maeneo ya makaazi ya watu ambazo zinakiuka sheria na taratibu za vileo pamoja na kukiuka mila silka na desturi za wazanzibari. Suleiman Othman Nyanga(CCM)Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Suleiman Othman Nyanga, ameyasema hayo wakati akijibu maswali katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar. Nyanga alisema kutokana na malalamiko mengi yanayofikishwa katika mahakama za vileo Serikali imechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzifungia baa hizo zinazolalamikiwa ili kulinda mila na silka za wazanzibari. Endelea kusoma habari hii.

SMZ KUFANYA MAZUNGUMZO NA CHINA

Aziza Nabahan Suleiman(CUF)wanawakeSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inafanya mazungumzo na serikali ya China kuhusu kupata soko la zao la mwani kwa wakulima wa visiwa vya Unguja na Pemba. Hayo yalisemwa na waziri wa kilimo,mifugo na mazingira Burhani Saadati Haji wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mwakilishi wa viti maalumu CUF Aziza Nabahani aliyetaka kujuwa juhudi za serikali kupata soko la mwani huko China. Burhani alisema mazungumzo ya awali katika kupata soko la mwani kwa wakulima wa zao hilo Unguja na Pemba yamefanyika na kinachosubiriwa kwa sasa ni kujuwa maendeleo yake yamefikiwa wapi. ‘Tumefanya mazungumzo ya awali ya juu ya soko la mwani kwa wakulima wa zao la mwani Unguja na Pemba kwa wenzetu wa China….tunafuatilia zaidi kujuwa maendeleo yake’alisema Sadatti. Endelea kusoma habari hii.

 ZANZIBAR YADHIBITI MAUAJI YA ALBINO

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar Kupitia Jumuiya ya Walemavu Zanzibar, inakusudia kukutana na taasisi mbali mbali za ulinzi na Usalama ili kuweza kuweka Mkakati utaoandaa mbinu mbali mbali zitazoweza kudhibiti matukio ya mauaji ya Watu wenye Ulemavu wangozi ‘Albino’ yasitokee hapa Zanzibar. Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Ali Abdallla Ali huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mjini Zanzibar. Mwakilishi huyo aliambia Baraza hilo kwamba hivi sas kumekuwa na wimbikubwala mauaji ya Albino matukio ambayo yamekuwa yakitokea Tanzania bara wakati huku Zanzibar wakiwepo watu wenye ulemavu wa ngozi na ni vipi serikali imejiandaa kuzuia hilo lisitokee kwa Zanzibar kwa vile Tanzania bara ni nchi moja na visiwani. Endelea kusoma habari hii.

WAWAKILISHI WAKUNWA NA SERA YA AJIRA

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamefurahishwa kwa kuanzishwa kwa sera ya ajira na Zanzibar kwa kuwa sera hiyo itafungua ukurasa mpya kwa wazanzibari kuweza kusaidia nchi yao kutokana na michango ya kiutaalamu walionayo wazanzibari wengi wanaoishi nje ya nchi ambao hivi sasa bi ashahainufaiki nayo. Sera hiyo ambayo iliwasilishwa juzi katika kikao cha baraza la wawakilishi na Waziri wa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma ilichangiwa na wajumbe wengi wakiwemo wapinzani. Akiwasilisha hutuba ya kambi ya upinzani barazani hapo, Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Aziza Nabahan Suleiman alisema kwamba kutambau mchango kwa wazanzibari waliopo nje ya nchi yao utaharakisha maendeleo ya nchi na serikali ifanye juhudi za kushirikiana na wazanzibari hao. Endelea kusoma habari hii.

 SMT IMEPATA KIGUGUMIZI KWA SMZ

Haroun Ali Suleiman(CCM) SERIKALI ya Mapinduzi (SMZ) imesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imekuwa na kigugumizi juu ya kuwaajiri walimu wanaohitimu masomo yao katika vyuo na shule mbali mbali za Zanzibar. Akijibu maswali kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman alisema amekuwa akishangazwa na kigugumizi hicho wakati walimu wenye kuhitimu Zanzibar hawana tofauti na walimu wanaohitimu Tanzania Bara kwa kuwa mitihani wanaofanya ni ya aina moja kutoka baraza la mitihani taifa. “Mie nashangaa sana kwa nini wenzetu wamekuwa na kigugumizi na wasi wasi juu ya suala hili eti wanasema walimu wetu hawana sifa za kwenda kusomesha huko lakini mitihani wanaofanya bara na Zanzibar ni ile ile mimi nasisitiza kuwa walimu wetu wana sifa zote zinazotakiwa” alisema Waziri huyo. Endelea kusoma habari hii.

SMZ YABADILI MUELEKEO WAKE

asha abdallah waziri wa wanwake na watotoSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imebadili muelekeo wa sera zake juu ya wazanzibari wanaoishi nje ya nchi kwa kuwataka wachangie katika maendeleo ya Visiwa vya Unguja na Pemba kwa kutoa misaada pamoja na maendeleo ya nchi yao. Hayo yameelezwa na Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma wakati akiwasilisha sera ya ajira Zanzibar kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Zanzibar. Waziri Asha aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba kwa muda mrefu wazanzibari wanaofanya kazi nje ya nchi wamekuwa wakikosa fursa ya kushiriki katika maendeleo ya Zanzibar na kuwa kuja kwa sera hiyo itaziba pengo hilo na kuitaka jumuiya ya ajira Zanzibar kufanya juhudi za kuwasiliana na wazanzibari hao. Endelea kusoma habari hii.

ZANZIBAR HAKUNA MAUAJI YA VIKONGWE

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema hakuna kesi hata moja iliyowahi kuripotiwa katika mahakama ya Zanzibar kuhusiana na vizee vikongwe kuuliwa kwa kushukiwa kuwa ni washirikina au wachawi kama ilivyo kwa upande wa Tanzania Bara. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba ya Utawala Bora, Ramadhan Abdaallah Shaaban aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) aliyetaka kujua mauaji hayo yakoje kwa upande wa Zanzibar na ni vikongwe vingapi vilivyouawa. Waziri huyo alisema kwa kuwa hakuna kesi iliyotokezea na kuripotiwa katika mahakama ya Zanzibar hivyo hakuna kumbukumbu yenye kuonesha idadi ya vizee vikongwe waliokubwa na kadhia hiyo ya kuuawa. Endelea kusoma habari hii.

 SERA YA AJIRA YAWASILISHWA BARAZANI

Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Asha Abdalla Juma amesema lengo kubwa ni sera ya ajira ni kulinda ajira kwa wazalendo katika sekta mbali mbali za uwekezaji nchini. Akiwasilisha sera ya ajira kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi Waziri Asha alisema kwa muda mrefu kulikuwa malalamiko kuhusiana na suala hilo ambapo hivi sasa limeanza kupatiwa ufumbuzi kwa kuwasilishwa sera ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo yanayoikabili sekta hiyo ya kazi. Alisema kutokuwepo kwa sera hiyo ilikuwa ikitoa mwanya kwa wawekezaji kukwepa kutoa ajira kwa wazalendo zaidi katika sekta ya utalii na uwekezaji ambayo imechukuwa nafasi kubwa katika pato la taifa kutokana na kuinua sekta ya utalii nchini. Endelea kusoma habari hii.

 WIZARA YAPOKEA MALALAMIKO

bi asha mshuaWAZIRI wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdaalla Juma amewaambiwa wajumbe wa baraza la wawakishi kwamba wizara yake imekuwa ikipokea malalamiko na kuyashughulikia inayotokana na migogoro ya kazi ikiwemo mahoteli makubwa ya kitalii. Akijibu swali la Mwakilishi wa nafasi za wanawake, Amina Iddi Mabrouk aliyetaka kujua kamisheni ya kazi nahusika vipi katika ajira za wafanyakazi wa sekta binafsi hasa katika hoteli za kitalii na biashara nyengine za kitalii na wizara ina shughulikia vipi migogoro katika kazi. Waziri Asha alisema kwa mujibu wa sheria ya ajira Nam. 11 ya mwaka 2005 wizara ya kazi kupitia kamisheni ya kazi imepewa jukumu la kusimamia ajira katika sekta zote ikiwemo sekta ya umma na binafsi. Endelea kusoma habari hii.  

CHANJO YA CHOLERA SIO YA MAJARIBIO

 SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema chanjo ya kinga dhidi ya kipindupindu iliyoanza kutumika visiwani Zanzibar sio ya majaribio kwa kuwa imekubalika na kusajiliwa zaidi ya miaka 10 katika nchi za ulaya. Akijibu swali la Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake, Amina Iddi Mabrouk aliyataka kujua chanjo ya Cholera ambayo imeanza kufanyiwa majaribio hapa Zanzibar ina uwezo gani wa kukinga marahi hayo ya kipindupindu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Sultan Mohammed Mugheiry amesema chanjo hiyo sio ya majaribio. “Mheshimiwa Spika chanjo ya kinga dhidi ya Cholera iliyonza kutumika Zanzibar inaitwa Dukoral ni chanjo imetengenezwa na Kampuni ya Crucelli kutoka Sweden. Chanjo hii sio ya majaribio kwani imekubalika, na imesajiliwa na kutumika kwa zaidi ya miaka 10 katika nchi za Jumuiya ya Ulaya” alisema Waziri Mugheiry. Endelea kusoma habari hii.

 MARUFUKU KUUZA ARDHI

 SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepiga marufuku tabia ya uuzwaji wa ardhi unaofanywa na wananchi katika maeneo ya makaburi na mizimu ambao husababasha usumbufu mkubwa kwa baadhi ya wananchi. Mansour Yusuf HimidWaziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid alisema hayo wakati akijibu masuala mbali mbali katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza jana visiwani Zanzibar. Himid alisema tatizo la uuzwaji wa ardhi unaofanywa na wananchi kwa wawekezaji limekuwa ni tatizo kubwa ambalo husababisha migogoro kwa wakaazi katika vijiji mbali mbali hivi sasa. Endelea kusoma habari hii.

 WACHAFUZI WA MAZINGIRA WADHIBITIWA

 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewasilisha mswaada wa Kuundwa Mamlaka ya Kusimamia Usafiri wa Bahari Zanzibar ambao utawadhibiti watumiaji haramu wa raslimali za bahari na wachafuzi wa mazingira katika ukanda wa Zanzibar. Akiwasilisha mswaada huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mawasiliano na Uchukuzi) Machano Othman Said katika kikao cha baraza la wawakilishi waliwambia wajumbe kuwa mswada huo utakuwa na adhabu zitazokuwa na viwango tofauti pamoja na kutozwa faini zinazotarajiwa kutumiwa na Mamlaka hiyo baada ya sheria hiyo kupitishwa na kuanza kutumika rasmi nchini. Chini ya sheria hiyo watu watakaobainika na kupatikana na hatia ya kutumia rasilima ya bahari kwa njia haramu na kusababisha kutokea uharibifu ama uchafuzi wa mazingira katika bahari watachukuliwa hatua kali dhidi yao. Endelea kusoma habari hii.

WAJUMBE WAPITISHA MSWAADA WA KARUME

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jana wamepitisha mswada wa Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia uliwasilishwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman. Akijibu hoja wa wajumbe mbali mbali waliochangia mswaada huo Waziri Suleiman alisema kuanzishwa kwa taasisi hiyo kutasaidia kuongeza taaluma katika sekta ya elimu na kuleta maendeleo na ufanisi zaidi. Alisema huu ni DSC03908ulimwengu wa sayansi na teknolojia hivyo kuwepo kwa Chuo hicho kutasaidia sana kuongeza wigo wa elimu ya sayansi ambayo inahitajika katika karne hii. “Tumeamuwa kuanzisha Chuo cha Karume cha sayansi na teknolojia kwa ajili ya kuimarisha elimu ya sayansi na teknolojia ambayo mahitaji yake katika karne hii ni makubwa sana….hivyo mikakati yetu katika suala hili ni kuongeza wataalamu katika fani hiyo” alisema. Endelea kusoma habari hii.

BARABARA ZA PEMBA KUTENGENEZWA

 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeahidi kuzitengeneza barabara za Kisiwani Pemba katika kiwango cha lami baada ya wafadhili kukubali kutoa fedha za matengenezo ya barabara hizo. Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Mawasiliano na Uchukuzi) Machano Othman Said aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Ole (CUF) Hamad Masoud Hamad aliyetaka kujuwa mikakati ya ujenzi wa barabara za kisiwani Pemba imefikia wapi. Machano alisema kukamilika kwa ujenzi wa barabara katika kiwango cha lami kutasaidia kuweka mazingira mazuri katika uwekezaji kwa kuimarishwa kilimo na miundo mbinu ya barabara zote zilizopangwa kutengenezwa. Alisema mfuko wa Millenium wa Marekani (MCC) tayari umekubali kuzifanyia matengenezo makubwa barabara tano za kisiwa cha Pemba ambazo zitajengwa kwa kiwango cha lami ambapo serikali ya Norway imekubali kuzifanyia matengenezo barabara sita za kisiwa hicho ikiwemo barabara ya Kengeja, Kangani, Ole Pujini na barabara za Mkoa wa Kaskazini Pemba. Endelea kusoma habari hii.

SMZ YASIFIA MFUMO WAKE WA KUENDESHA KESI

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abdallah Shaaban amesema Afisi ya Mkurugenzi wa Mashataka imefanya kazi kubwa katika kuimarisha mfumo wa kuharakisha uendeshwa wa kesi nchini. Waziri huyo ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni (CCM) Anaclet Thobias Makungila aliyetaka kujua utaratibu gani unaotumika kuimarisha mfumo wa uendeshaji wa mashtaka kwa kujenga utaratibu wa kukamilishwa upelelezi kabla ya kufunguliwa mashtaka ili kupunguza usumbufu usio wa lazima kwa kisingizio cha ushahidi kutokamilika wakati wa mashataka yameshafunguliwa. Waziri Shaaban alisema kabla ya kuanza kutekeleza mpango huo ofisi ilifanya mazungumzo na wakuu wa upelelezi wa jinai wa mikoa yote ya Unguja kupitia vikao vyake vya kila mwezi vinavyofanywa kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Polisi. Endelea kusoma habari hii.

 SMZ YAWALIPA WALIOVUNJIWA

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema jumla ya shilingi 42,320,000 zimelipwa kwa wananchi 24 katika eneo la fukwe ya bahari kutokana an eneo hilo kuchukuliwa na mwekezaji mgeni kutoka Mauritius. Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Ramadhan Nyonje Pandu aliyetaka kujua wananchi wangapi njonyewamelipwa fidia ya vipando vyao na kiasi gani kilicholipwa kwa kila mmoja wao. Mwakilishi huyo pia alitaka kujua kwa kuwa serikali iliwataka wananchi wa shehia hizo kuwa na mashirikiano ya pamoja kulidhibiti eneo hilo kwa faida ya vijiji vyao ni wananchi wa vijiji hivyo watafaidika vipi na mradi huo wakati tangu awali ilionekana hali ya wananchi wa vijiji hivyo kudhulimiwa kwa baadhi yao kutolipwa fidia ya vipando vyao au kulipwa pungufu ya malipo halisi. Endelea kusoma habari hii.

WAPINZANI WAUNGA MKONO MSWAADA

Kambi ya Upinzani ya baraza la wawakilishi Zanzibar imeunga mkono uanzishwaji wa bodi ya sensa na filamu za maonyesho na mambo yanayohusiana na hayo iliwasilishwa katika kikao hicho jana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Juma Shamhuna.najma khalfan juma(CUF-WANAWAKE)  Akiwasilisha mswaada huo katika kikao hicho, Shamhuna alisema lengo la mswaada huo ni kurekebisha kasoro zilizopo katika bodi iliyokuwepo mwanzo pamoja na kudhibiti mmomonyoko wa maadili visiwani Zanzibar ambao umeanza kukua kwa kasi kubwa. Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni na Michezo, Najma Khalfan Juma alisema umefika wakati mwafaka taifa la Zanzibar kuwa na dira yenye mwelekeo wa kudhibiti viashiria vyote vyenye kudhamiria upotoshaji wa maadili ya mzanzibari. Endelea kusoma habari hii

ADHABU KALI ITOLEWE KWA WABAKAJI

Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wameishauri serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutoa adhabu kali dhidi ya wabakaji na watu wenye kulawiti watoto kinyume na maumbile. Wajumbe hao wametoa ushauri huo kufuatia taarifa zilizorushwa katika chombo cha habari za serikali asubuhi kufuatia mahakama ya mkoa vuga kumuachia mzee mmoja mwenye umri wa miaka 43 aliyehukumiwa kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 12. Wajumbe hao wamesema ingawa hawataki kuingilia mahakama lakini adhabu iliyotolewa ni ndogo kutokana na kosa kubwa lililofanya ambalo mara nyingi masuala kama hayo yanapofanyika kesi humalizika kirahisi au kukosekana ushahidi na mtuhumiwa kuachiwa bila ya kupewa hukumu inayostahiki. Endelea kusoma habari hii.

SMZ YASHAURIWA KUTUMIA KISWAHILI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kutumia lugha ya Kiswahili katika sheria zinazotumika ndani ya nchi kwa kuwa asilimia 90 ya wazanzibari wanatumia Kiswahili. Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali alipokuwa akiuliza swali la ngongeza wakati akitaka kujua kwa nini inatumika lugha ya kingereza katika miswaada inayowasilishwa katika baraza la wawakilishi hali ya kuwa wawakilishi wote wanatumia lugha ya Kiswahili. Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin alitaka kujua kwamba kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 87 (2) kila mswaada, kila sheria inayotungwa na baraza la wawakilishi iaandikwa kwa lugha ya Kiswahili jee zipo sheria zilizotungwa na baraza la wawakilishi na zikaandikwa kwa lugha ya kiswahili na kama zipo ni sheria zipi. Endelea kusoma habari hii.

 ZANZIBAR HAIHUSUDU RWANDA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma amesema wananchi wa nchi ya Rwanda wanaheshimu sheria za nchi yao zinazotungwa na mabaraza ya sheria na ndio sababu kubwa ya kufika malengo yao katika suala zima la usafi katika nchi yao. “Wenzetu wa Rwanda wamefanikiwa kwa kuwa wanafuata sheria zilizotuungwa katika nchi yao na wanajitahidi sana katika kusafisha miji yao na wana siku maalumu kwa ajili ya kufanya usafi nchi nzima hata mabari ya mabalozi na ambulances pia hutumika siku hiyo kwa ajili ya usafi wa miji yao” alisema Waziri Hamza. Hayo yameelezwa na katika kikao cha baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Suleiman Ali aliyetaka kujua kuwa Zanzibar haiwezi kuiga mfano wan chi hiyo kwa kuwa imepata mafanikio makubwa katika kuwaamasisha wananchi wake juu ya usafi wa mazingira. Endelea kusoma habari hii.

 RAIS ASAINI MISWAADA MINNE

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba jumla miswada minne ya sheria iliyopitishwa na wajumbe hao katika kikao kilichopita tayari imetiwa saini na 103Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na kuwa sheria kamili. Spika Kificho alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuhusu masuala mbali mbali muhimu kwa wajumbe hao wakati akifungua mkutano wa 14 baraza la saba la kikao hicho kilichoanza jana Mtaa wa Maisara visiwani hapa. Miswaada hiyo ilijadiliwa katika mkutano wa 13 wa baraza la wawakilishi uliofanyika Octoba 15 mwaka 2008 na kujadiliwa kwa kina na wajumbe mbali mbali. Endelea kusoma habari hii.

WAWEKEZAJI WAKWEPA KODI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekiri kwamba kuna baadhi ya wawekezaji wenye kuwekeza katika sekta ya utalii visiwani hapa huwa wanakwepa kulipa kodi hasa katika maeneo ya wawekezaji katika ukanda wa pwani. Hayo wameelezwa wajumbe wa baraza la wawakilishi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Mwinyihaji Makame Mwadini alipokuwa akijibu swali la ngongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM) Ame Wati Wadi aliyetaka kujua ardhi inayokodishwa kwa miaka 30 hutozwa kodi ya kiasi gani kwa wawekezaji. Akisaidia jibu la suala hilo Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid alisema kodi ya ardhi ina historia kubwa tokea kuasisiwa sheria ya ardhi ya mwaka 1990’s ambapo kodi iliyokuwa ikitozwa ilikuwa ni Dola 100 za kimarekani kwa kila hekta moja. Endelea kusoma habari hii.

HAKUNA DAWA YA UKIMWI

 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imesema bado juhudi za kutafuta kinga na tiba za dawa za kutibu virusi vya ukimwi zinaendelea duniani kote bila ya kufikia mafanikio hadi sasa na wenye kujigamba kuwa wana uwezo wa kutibu ukimwi watachuliwa hatua za kisheria. Akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni (CCM) Anaclet Thobias Makungira aliyetaka kujua kama kuna mafanikio yoyote yaliofikiwa katika utafutaji wa dawa za ukimwi, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Sultan Mohammed Mugheiry alisema hadi sasa bado hakuna dawa zilizopatikana. Alisema dawa pekee zinazotumika kwa sasa ni (ARV) ambazo hupunguza makali ya maradhi hayo lakini sio tiba kamili na tiba kubwa kwa inayotakiwa ni kuwa mwaminifu katika ndoa na kacha kufanya zinaa. Endelea kusoma habari hii. 

MAWAZIRI WASHITAKIWA KWA SPIKA

Pandu Ameir Kificho(Spika)Kambi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi imewalalamikia mawaziri wanachelewesha miswaada kwa wajumbe hao kwa Spika, Pandu Ameir Kificho na kumtaka achukulie hatua kwa kuwa yeye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za baraza hilo. Malalamiko hayo yametolewa na Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mohammed Ali Salim alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi hiyo juu ya mswaada wa sheria ya kuanzishwa taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknilojia na mambo mengine yanayohusiana nayo, katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja. Salim alisema kanuni ya baraza hilo kifungu cha 78 (2) kinaeleza wazi ni muda gani mdogo wa mwisho unaostahiki mswaada kutolewa kwa wajumbe wa baraza hilo lakini barua ya mwaliko wa baraza wa mkutano huo miswaada imepokelewa Janauri 9, 2009 siku 11 tu kufikia siku ya kusomwa mswaada huo. Endelea kusoma habari hii

 KERO ZA MUUNGANO ZATATULIWA         

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema imeanza kupata mafanikio katika kutatua kero za Muungano na hivi sasa kuna mambo kadhaa ambayo yameshapatiwa ufumbuzi baada ya kukaa viongozi wakuu wa pande mbili za Muungano na kujadili. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abdallah Shaaban aliwaambiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi alipokuwa akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Anaclet Thobias Makungila(CCM)FuoniJimbo la Fuoni (CCM) Anaclet Thobias Makungila aliyetaka kujuwa hadi sasa serikali zimefikia hatua gani katika suala la kuanzishwa kwa mamlaka ya bahari kuu na kutatua kero za Muungano. Waziri Shaaban alisema miongoni mwa kero kubwa ya muungano ilikuwa ni suala la kuundwa kwa mamlaka na mgawanyo wa mapato yanayopatikana katika uvuvi wa bahari kuu. Endelea kusoma habari hii.

WIZARA YAPOKEA MALALAMIKO

WAZIRI wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdaalla Juma amewaambiwa wajumbe wa baraza la wawakishi kwamba wizara yake imekuwa ikipokea malalamiko na kuyashughulikia inayotokana na migogoro ya kazi ikiwemo mahoteli makubwa ya kitalii. Akijibu swali la Mwakilishi wa nafasi za wanawake, Amina Iddi Mabrouk aliyetaka kujua kamisheni ya kazi nahusika vipi katika ajira za wafanyakazi wa sekta binafsi hasa katika hoteli za kitalii na biashara nyengine za kitalii na wizara ina shughulikia vipi migogoro katika kazi. Waziri Asha alisema kwa mujibu wa sheria ya ajira Nam. 11 ya mwaka 2005 wizara ya kazi kupitia kamisheni ya kazi imepewa jukumu la kusimamia ajira katika sekta zote ikiwemo sekta ya umma na binafsi. Endelea kusoma habari hii.

WIVU WA MAPENZI NI TATIZO ZANZIBAR

WAJUMBE wa Baraza la wawakilishi wameelezwa kwamba wivu wa mapenzi umekuwa ukichangia kutokea kwa ugomvi na mauaji kwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar. Akijibu swali la msingi kwa wajumbe hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhan Abdalla Shaaban amesema wivu wa mapenzi ni chanzo vifo vingi vya mauaji vinavyotokea hasa katika maeneo ya starehe ambapo baadhi ya watu huuawa kwa silaha za kienyeji ikiwemo kupigwa mapanga. Waziri Shaaban alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali aliyetaka kujuwa hatua gani zinazochukuliwa katika kukabiliana na wimbi la mauaji yanayotokea na nini chanzo chake. Endelea kusoma habari hii.

MITAJI MIDOGO INAUWA HOTELI ZNZ

Samia Suluhu Hassan (CCM) KUTEULIWAWaziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji Samia Suluhu Hassan amesema mitaji midogo ya Wawekezaji wa Mkoa wa Kusini, ndio iliyosababisha kufa kwa baadhi ya Hoteli katika Mkoa huo ikilinganishwa na Wawekezaji wa Mkoa wa Kaskazini. Waziri huyo ameyasema hayo katika kikao cha baraza la wawakilishi alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Mfenesini (CCM) Ali Abdalla Ali, aliyetaka kujua kwanini Wawekezaji wengi wa hoteli za kitalii wanawekeza zaidi Kaskazini Unguja huku maeneo mingine yameachwa utalii wake ukifa. Waziri Samia alisema ni kweli nyingi ya Hoteli ziliomo katika Mkoa wa Kusini Unguja, zimeonekana kukabiliwa na matatizo mbali mbali kulikotokana na ukosefu wa mitaji na Wawekezaji wake wameshindwa kujibadili kwakuendeleza utalii wa kizamani. Endelea kusoma habari hii.

MABILLIONI YA JK SIO YA SADAKA  

bi ashaWaziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma, amesema baadhi ya watu wanadhani mabilioni ya JK yanatolewa kama sadaka hivyo wanajaza fomu haraka haraka ili kupata fedha hizo bila ya kuzingatia masharti yaliomo katika fomu hizo. Akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Matemwe (CCM) Ame Mati Wadi aliyetaka kujua tatizo liko wapi katika kucheleweshwa fedha hizo kwa walengwa ambazo hata Rais Kikwete alipotembelea Mkoa wa Kaskazini aliulizwa na wananchi kuwa kwa nini fedha hizo zinachelewa kufika kwa wahusika licha ya kutimiza masharti. Waziri Asha alisema suala la fedha linahitaji uangalifu na sio kukurupuka kwani wapo baadhi ya wananachi waliopewa fomu kujaza walikosea hivyo ikaleta usumbufu kwa wahisika wa fedha hizo. Endelea kusoma habari hii.

Advertisements

5 responses to “Baraza

 1. SALAAM ALYKUM:

  TUNAKUOMBA BI-SALMA SISI WASOMAJI WAKO HUWA HATUWAFAHAMU MAJINA YAO HAO WATU KATIKA BAADHI YAPICHA,
  BASI UNGEJARIBU KWA KILA CHINI YA PICHA UKATUANDIKIA JINA LA MWENYE PICHA HIYO HATAKAMA ITAJIREJEA REJEA HAITOATHIRI KITU.
  AU JINA LA PICHA KAMA ITAKUWA SI INAYOONESHA PICHA YA MTU.
  MFANO: MTAA AU SKULI AU HOSPITALI.
  ALIMRADI KILA PICHA IWE NA JINA CHINI.
  AHSANTE
  FATMA KHALFAN.( ZANZIBARDAIMA@HOTMAIL.COM )
  ‘PONGEZI KWA KAZI ZAKO NZURI ZA KUELIMISHA JAMII BI-SALMA,MALPO YAKO KWA MUNGU ISHA-ALLAH’

 2. Asante kwa kuwepo nafasi ya kuchokoza. Sina utaalamu lakini waonaje kama kutakueko na muda maalumu wa makala kubakia katika website. Kuna makala za miezi mitatu na picha zizo kwa hizo. Ukitaka uitazame na hata ikiwa umeichoka bado uanyo labda isifungue. Tangu Nyanga na Burhani Saadati wangali vujana. Ikiwa hamna jipya domo jumba ya maneno. Hata historia za aina yeyote zitakuwa ni mpya. Alumradi nazo zisibakie muda mrefu . Hapakosekani jipya la kuandika. Basi ni hayo tu lakini ni pamoja kuomba radhi sana kwa usumbufu wowote ule.

 3. Tunakushukuruni sana kwa mchango wenu M/mungu akupeninguvu ya kuelimisha jamii. Lakini bado muko polepole sana watu wanataka habari zakila siku tunakua tunasubiri muda kupata habari mpya jitahidini M/mungu atawasaidia.

 4. Nahani sasa iko haja ya kututilia picha mpya za mawaziri wapya wa zanzibar.

  Tunaomba orodha kamili ya mawaziri wote wa serikali ya umoja wa litaifa ikiwa ni pamoja na picha zao na nyadhifa zao.

  Shukrani

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s