Habari

Waliokimbilia Somali warejea nyumbani

KATIKA hali ambayo haikutarajiwa Wazanzibari waliokuwa wakiishi Somali kama wakimbizi wamerejea nyumbani jana na kupokelewa na ndugu na jamaa zako katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. Hali ya ulinzi ulikuwa imeimarishwa na maafisa wa usalama ambapo haikuwa rahisi kwa waandishi wa habari na wapiga picha kuwasogela hadi walipotoka ndani ya ndege mbili maalumu za Umoja wa Mataifa (UN) zilizowaleta.Sura za wa wageni hao na wapokeaji zilisajika baada ya kufika uwanja huo ambapo baadhi ya watoto wakionekana wakilia muda mfupi baada ya kutua huku wazazi wao wakiwa na furaha na kukanyanga tena nyumbani.Wakizungumza na waandishi wa habari walionesha hisia zao za kufuwahia kurudi nyumbani na kusikitika kuwa baadhi ya wenzao wamekataa kurudi kutoka na kupata taarifa za maandamano yaliotokea Mei 27 mwaka huu na kusababisha mali kuharibiwa na baadhi ya watu kushitakiwa. Endelea kusoma habari hii

Makunduchi wataka Muungano wa mkataba

MCHAKATO wa kukukusanya maoni ya Katiba mpya nchini umeanza huku wananchi wakiwa na mawazo tofauti, na baadhi yao wakipendekeza Zanzibar iwe na mamlaka kamili. Maoni hayo yalitolewa jana katika eneo la Mzuri Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, ambako pia ilipendekezwa Muungano kati ya Tanzania uwe wa mkataba. MCHAKATO wa kukukusanya maoni ya Katiba mpya nchini umeanza huku wananchi wakiwa na mawazo tofauti, na baadhi yao wakipendekeza Zanzibar iwe na mamlaka kamili. Maoni hayo yalitolewa jana katika eneo la Mzuri Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, ambako pia ilipendekezwa Muungano kati ya Tanzania uwe wa mkataba. Pia baadhi ya wananchi waliwaeleza wajumbe wa Tume ya Katiba chini ya Mohammed Yussuf, wakitaka ziwepo Serikali mbili kama zilivyo sasa, huku wengine wakitaka Serikali tatu, yaani Tanganyika, Unguja na ya Kisiwa cha Pemba. Mmoja wa wananchi hao alitaka Zanzibar iwe na mamlaka ndani na nje ya nchi, na iwe na uwezo wa kujiamulia mambo yake inavyotaka, huku akitoa mfano kuwa nchi hiyo imezuiwa kujiunga na Jumuiya ya Kislamu (OIC) na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA). Endelea kusoma habari hii

Serikali itengeneze miundombinu – Balozi

Balozi wa Tanzania nchini Marekani bibi Mwanaidi Maajar amesema Zanzibar inaweza kupiga hatua kubwa katika kukuza sekta ya utalii iwapo itaimarisha miundombinu ya uwekezaji katika sekta hiyo. Balozi Maajar ameeleza hayo leo alipokuwa na mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Amesema katika kukuza sekta hiyo ni lazima serikali itenge fungu maalum litakalokidhi haja ya kuimarisha miundombinu ya utalii, ikiwa ni pamoja na kuitangaza sekta hiyo katika nchi za nje.“Ni lazima serikali ikubali kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kuutangaza utalii, sambamba na kuwekeza katika maeneo ambayo yanaweza kuwavutia watalii”, alifafanua balozi Maajar. Amesema Zanzibar ina vivutio vingi vya utalii vikiwemo mashamba ya viungo, na kwamba iwapo vitatumiwa vizuri vinaweza kuwavutia watalii wengi zaidi na kuinyanyua Zanzibar kiuchumi. Endelea kusoma habari hii 

Jadilini bajeti na punguzeni shukrani na pongezi

KATIBU wa zamani wa Baaza la Wawakilishi la Zanzibar , Ibrahim Mzee Ibrahim amewahimiza Wajumbe wa Baraza hilo kuitumia ipasavyo fursa ya kujadili bajeti ya Serikali kwa kulenga mafanikio, matatizo na changamoto ziliopo katika uendeshaji na utekelezaji wa majukumu ya serikali. Amesema ingawa Kanuni za Baraza la Wawakilishi inatowa fursa kwa wajumbe kuchangia kwa muda wa dakika zisizozidi 30, si vyema sehemu kubwa ya muda huo zikatumika kwa pongezi na shukurani badala yake Wajumbe wajikite zaidi katika maudhui ya hoja inayojadiliwa. “Kanuni ya 58 (6) inatowa muda usiozidi dakika thelathini kwa mjumbe anaechangia hoja ya bajeti. Ni vyema Waheshimiwa Wajumbe wakajizowesha kutumia ipasavyo muda huo wanaopewa kuchangia. Pongezi na shukurani ni muhimu sana lakini zisichukuwe muda mwingi wa mjumbe, muda mwingi utumike kujadili na kuchangia maudhui ya hoja inayojadiliwa” Alifahamisha Mkurugenzi huyo wa DPP. Endelea kusoma habari hii

Uamsho ni sawa na waamsha daku

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Amani Abeid Karume amewafananisha Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI) kuwa sawa na waamsha daku wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kuwataka Wana CCM kubakia na misimamo yao katika suala la Muungano. Akizungumza katika mkutano uliofanyika Jimbo la Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Dk Karume alisema kwamba CCM haijalala hivyo wanachama wa CCM hawana sababu ya kuwa na hofu na Uamsho kwani wao hawakulala na wenye kuamshwa ni wale waliolala. “Kwani nyie mmelala mpaka muamshwe, nyie mko macho eti…hao ni kama wale wanaoamsha daku utakasirika, lakini ukiamka unasema ahaa kumbe muda wa kula daku tena hofu ya nini” Alisema Dk Karume na kuwachekesha waliohudhuria mkutano huo. Makamu huyo Mwenyekiti alilazimika kutoa maelezo hayo baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja, Borafia Silima Juma kueleza wasiwasi wa wanachama wa CCM kuhusu vurugu zilizotokea mwezi Mei mwaka huu na harakati kundi la Uamsho. Endelea kusoma habari hii

Nitautetea Muungano -Dkt Shein

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema ataendelea kuutetea Muungano na hakuna atakaemlaghai wala kumchezea katika uongozi wake. Kauli hiyo ameitowa jana katika mkutano wa Jumuiya ya Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Bwawani mjini Unguja. Dk Shein amesema kwamba yeye ndie rais wa Zanzibar na ndie mwenye mamlaka na hatomuogopa mtu wala kusita kuwachukulia hatua kwa wale wote ambao watakwenda kinyume na matakwa ya kikatiba. Alisema kuwa dhamana ya nchi hii pamoja na ile ya Jamhuri ya Muungano imo mikononi mwao kati yake na Rais Jakaya Kikwete na ndio maana wakawa wanashirikiana na kushauriana kwa yale yote ambayo yana maslahi na nchi. “katika kuiongoza Zanzibar mimi ndie rais simuogopi mtu yeyote”, alisema kwa kujiamini Dk Shein. Endelea kusoma habari hii

Watu 33 wafikishwa mahakamani

WATU  33 wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisilamu Zanzibar (JUMIKI) leo walifikishwa katika mahakama ya wilaya Mfenesini wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya mkusanyiko isivyo halali.Watuhumiwa hao wakiwemo wanawake wa wanane, wanaume 25 na watoto wawili wa miaka 15 na 17 walidaiwa kutenda kosa hilo juzi huko Donge wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wamefikishwa mbele ya hakimu Fatma Muhsin Omar kujibu mashitaka hayo. Pamoja na shitaka hilo, watuhumiwa hao pia walishitakiwa kwa kosa la kukataa amri ya kutawanyika, mashitaka ambayo yaliyasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Mkaguzi wa Polisi Khamis Abdulrahman. Endelea kusoma habari hii

Sheria ya katiba mpya kuwasilishwa kama taarifa

SHERIA ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itawasilishwa kesho katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoanza kujadili bajeti ya mwaka wa fedha serikali ya mwaka wa fedha wa 2012/2013. Katibu wa baraza hilo, Yahya Khamis Hamad aliwaambiwa waandishi wa habari jana katika mkutano uliofanyika ukumbi wa baraza la wawakilishi, kwamba jambo la kwanza kuwasilishwa kwa wajumbe wa baraza ni sheria hiyo ambayo wananchi wanasubiri kuitolea maoni. Endelea kusoma habari hii

Wazanzibari watakiwa kuungana kudai haki

Wazanzibari wametakiwa kuungana katika kutetea maslahi ya nchi yao wakati wa mchakato wa katiba mpya ikiwa njia mojawapo ya kuhakkikisha madai yao yanakubaliwa. Wakihutubia kwa nyakati tofauti katika muhadhara wa kiislam uliofanyika msikiti wa Mbuyuni Unguja jana,  Sheikh Mussa Juma wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, ambaye aliwahi kukamatwa na kuzusha sokomoko kubwa nchini, alisema  bila mshikamano hakuna litakalokuwa hivyo amewahimiza Wazanzibari kushirikiana pamoja kupinga dhulma dhidi ya nchi yao pamoja na kuietete Zanzibar. Endelea kusoma habari hii

 

The Zanzibar Riots, the Union, and Religious Tolerance

Nobody in his right mind would condone the torching of churches and shops in Zanzibar last weekend. But it is a great shame that so many, including some of the top leaders in the country have made these symptoms of a socio-political malaise in the country the central issue for discussion rather than looking at the disease itself. It seems to have been a bonanza for most of the newspapers on the mainland who have used this to launch for what I can only call Islam and Zanzibar-bashing spree for more than a week. Continue reading

Amani tunda muhimu

MOJA ya majukumu muhimu ambayo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein aliahidi kuyasimamia kama kiongozi wa nchi, wakati akizindua baraza la wawakilishi, ni kulinda amani na utulivu wa nchi. Kila mtu alielewa maana ya ahadi hii. Kwamba inatokana na kuzingatia ukweli kuwa bila ya nchi kuwa katika amani na utulivu wa kweli, hakuna maendeleo yatakayopatikana. Inashangaza kuona kwamba hata nusu ya muda wake wa uongozi ikiwa haijatimia, tayari kuna dalili kuwa uongozi wa Dk. Shein unapotea njia. Watu kadhaa wamejeruhiwa; mali zimeharibiwa; wananchi wamejaa hofu kuhusu usalama wao; na kwa kweli, amani imezorota mitaani. Kisa? Vurugu.Tunaamini kulikuwa na uzito katika kuchukua msimamo imara kuhusu hali iliyokuwa ikiendelea Zanzibar, tangu ilipopitishwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Endelea kusoma habari hii

Wanasheria wa Zanzibar wakerwa

Wakili Abdullah Juma aliondoka na kuelekea katika Mahkama ya Ardhi, Vuga Zanzibar. Majira ya saa 6.30 mchana ofisi yake ya uwakili iliopo karibu na Amani Roundabout, ilishambuliwa na Polisi ambao waliingiza mtutu/mitutu ya bunduki ndani ya madirisha na kupiga mabomu ya machozi. Sisi tunaamini kabisa kwamba askari waliofanya hivi wamefanya wakijuwa kabisa kwamba kitendo chao kinakiuka maadili yote ya kazi yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao.Wamefanya kitendo hiki kwa lengo la kumuogopesha (intimidate) Wakili Abdulla Juma na labda kuwahadharisha mawakili wengine waache au waogope kuwatetea watuhumiwa wa kesi hizi zinazoendelea na nyenginezo. Mabomu hayo yameathiri sana ofisi na kuifanya kutokalika kwa siku tatu na hadi wakati huu hatujuwi athari za kiafya zilizowakuta mawakili waliokuwemo ndani ya ofisi hiyo. Vitisho na hujma dhidi ya mawakili vina lengo la kudhoofisha ustawi wa utawala wa sheria, haki za binaadamu na utawala bora.  Endelea kusoma taarifa hii

Mhadhara wafanyika kwa amani

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana imefanikiwa kufanya mhadhara wake katika viwanja vya Malindi katika hali ya amani kabisa. Mhadhara huo awali ulipangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Lumumba lakini jeshi la polisi lilipiga marufuku na kutaka wananchi kutoshiriki katika mhadhara huo kutokana na hali ya kiuslama.Viwanja vyote vya Lumumba jana vilionekana vimezingizwa na ulinzi mkali tokea majira ya saa sita mchana huku magari ya polisi wa kutuliza ghasya FFU wakizunguka zunguka katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.Mwananchi ilishuhudia vijana mbali mbali wakiwa kando ya uwanja wa Lumumba na wengine kujibanza vipembeni wakisubiri kuingia uwanjani lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarishwa wananchi hao walishindwa kusogea na walikaa umbali mkubwa wa uwanja huo.“Ulinzi naona sio wa kawaida na inaonesha hawataki watu hata kusogea umbali wa mita mia mbili, si mnaona mabunduki yake yalivyosimamishwa? Kila mmoja amebeba bunduki yake wamefunga kabisa uwanja” alisema kijana mmoja ambaye alikuwa amekaa kusubiri kuingia uwanjani. Endelea kusoma habari hii

Raza asema kila mtu na dini yake

MFANYABIASHARA Maarufu Zanzibar Mohammed Raza amesema wazanzibari wana haki ya kuabudu wanachokiamini hata kama ni mbuyu kulingana na imani zao. Kauli ya Raza imekuja siku chache baada ya kutokea vurugu zinazoshabihishwa na taasisi za kiislamu ambapo makanisa matatu yalichomwa moto na mali za watu binafsi kuharibiwa na mamilioni ya shilingi kutopotea kutokana na purukushani hizo.Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Uzini Manzese wilaya ya kati wakati akikabidhi vifaa mbali mbali kwa wananchi wa jimbo hilo, Raza alisema wazanzibari ni watu wapole na watu wenye kuheshimu dini za wengine na hivyo watumie utamaduni wao wa kuheshimu dini nyengine.“Kila mtu ana haki ya kuabudu anachokitaka wapo wanaoabudu Mungu lakini wengine wanaabudu miti kwa hivyo hata mtu akiabudu mbuyu aachiwe na huo ni uamuzi wake kwa hivyo tusiingiliane katika imani za dini kila mtu ana dini yake” alisema Raza huku akiungwa mkono wa wananchi wa jimbo hilo. Endelea kusoma habari hii

Mhadhara wafanyika kwa amani


Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana imefanikiwa kufanya mhadhara wake katika viwanja vya Malindi katika hali ya amani kabisa. Mhadhara huo awali ulipangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Lumumba lakini jeshi la polisi lilipiga marufuku na kutaka wananchi kutoshiriki katika mhadhara huo kutokana na hali ya kiuslama.
Viwanja vyote vya Lumumba jana vilionekana vimezingizwa na ulinzi mkali tokea majira ya saa sita mchana huku magari ya polisi wa kutuliza ghasya FFU wakizunguka zunguka katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.Mwananchi ilishuhudia vijana mbali mbali wakiwa kando ya uwanja wa Lumumba na wengine kujibanza vipembeni wakisubiri kuingia uwanjani lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarishwa wananchi hao walishindwa kusogea na walikaa umbali mkubwa wa uwanja huo. Endelea kusoma habari hii

Hatutarudi nyuma – Sheikh Farid

JUMUIYA ya Mihadhara ya kiislamu (Uamsho) imetoa msimamo mkali shidi ya Serikali ikisema kuwa haitarudi nyuma katika kudai uhuru wa Zanzibar.Wakizungumza katika msikiti wa Mbuyuni uliopo eneo la Darajani mjini Zanzibar, viongozi wa Uamsho wamewataka Wazanzibari kutolegezamsimamo wao hata kama jeshi la polisi limezingira mji wao.“Umoja wetu ndiyo utakaotukombolea nchi yetu, msikubali kuyumbishwa na kitu chochoe ili kulegeza msimamo wetu. Jambo moja tu, ni mpaka kieleweke.Bila hivyo hakuna jeshi, hakuna polisi atakaye tuyumbisha” alisema Sheikh Mussa Juma wa msikiti huo na kuitikiwa na wafuasi waliokuwa wamefurika katika msikiti huo “ndiyooooo!”Wafuasi hao walikuwa wameshikilia karatasi zilizoandikwa “hatuutaki muungano, tunaitaka Zanzibar yetu”.Naye Sheikh Mussa Juma aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana aliwapongeza wanachi waliotokana kuandaana akisema kuwa hawatarudi nyuma, Tunawashukuru Wazanzibari kwa sababu mmeonyeshwa kutotaka kutawaliwa” alisema na kuwauliza wafuasi hao “mko tayari” nao wakijibu “Tuko tayariii”. Endelea kusoma habari hii

Maaskofu waitolea uvivu SMZ

JOPO la Maaskofu wa madhehebu mbalimbali nchini jana wameitolea uvivu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu wa makanisa visiwani humo. Akizungumza kwa niaba ya maaskofu hao mbele ya Waziri wa Nchi Katika ofisi ya Makamu wa Pili Mohamed Aboud, Askofu mkuu wa Kanisa la Anglican Dk Valentino Mokiwa, alisema kuwa vitendo hivyo sasa vimekithiri na kwamba hawaoni Serikali hiyo ikichukua hatua madhubuti hivyo Wakristo wamechoka.“Kanisa sasa limechoka kutokana na vitendo vya kuchumwa kwa makanisa na kuharibiwa kwa mali zake…..Leo tukirejea historia tangu mwaka 2001 kuna makanisa 25 yameshaharibiwa, yaani kuwa mkristo ni maisha ya hofu” alisema Askofu Mokiwa.Aliongeza kuwa wakristo visiwani humo wamekuwa wakiishi kwa hofu huku wakitishiwa maish yao kwa kuopigwa mawe, huku wakichukuliwa kama daraja la pili na kwamba Serikali haichukui hatua madhubuti.“Matukio yote hayo haya yameripotiwa polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Tumesikiwa mkisema eti wanaofanya hivyo ni wahuni, sisi tunasema hiyo ni lugha ya kututia ganzi. Wale siyo wahuni, ni wahalifu na kuna taratubu za kuwachukuliwa kisheria. Serikali inakemea lakini haina ‘confidence’.” alisema Askofu Mokiwa. Mokiwa pia aliitaka Serikali kueleza miakati waliyoichukuwa na kuwataja majina wahalifu waliokamatwa kwa majina ili waamini kama kweli hatua zimechukuliwa.Aliongeza kuwa Serikali pia inapaswa kuchukua hatua kwa vikundi vya dini vinavyohubiri siasa kinyume na masharti waliopewa. Endelea kusoma habari hii

Maaskofu waomba serikali kuingilia kati

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mohamed Aboud pamoja na viongozi wa dini jana walitembelea maeneo yaliyoshambuliwa katika vurugu zilizotokea visiwani hapa. Ziara hiyo imekuja wakati hali ya amani ikielezwa kurejea visiwani hapa baada ya ghasia zilizoanza Jumamosi usiku na kuendelea hadi juzi.Wakizungumza baada ya ziara hiyo, viongozi wa makanisa visiwani hapa walitoa malalamiko yao kuhusu vitendo vya uchomaji na uharibifu wa makanisa huku wakiitaka Serikali kutumia nguvu ya ziada kuingilia kati suala hilo wakisema tangu mwaka 2001 hadi sasa jumla ya makanisa 23 yameshachomwa moto Zanzibar.Katibu wa umoja wa Wachungaji wa Zanzibar Jeremiah Kobero alisema kuwa licha ya makanisa matatu yaliyochomwa na kubomolewa katika vurugu za sasa, kuna matukio 23 ya uchomaji moto makanisa yametokea tangu mwaka 2001.Aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na uchomwaji moto wa makanisa ya The Church of God na Sloam yaliyofanyika mwaka 2011, makanisa mawili yaliyoko Masunguni yote mwaka huo huo, Kanisa la EAGT la Fuoni mwaka huo, kanisa la Pefa mwaka 2009, kanisa la Mwera mwaka 2012, kanisa la Redeemed lililiopo Dilikane mwaka 2001 yote ya mkoa wa Mjini Magharibi.Alitaja pia makanisa yaliyochomwa katika mkoa wa Kaskazini kuwa kanisa la Tunguu, Unguja Ukuu, kanisa la CMF, Chukwani na Manyanya. Endelea kusoma habari hii

Viongozi wakutana, hali bado ni tete

HALI bado ni tete katika visiwa vya Zanzibar kwa baadhi ya maeneo ambayo vitendo vya uvunjifu wa amani vinaendelea licha ya juhudi za kutaka kurejesha hali ya amani nchini. Juhudi za pamoja zimeanza kuchukuliwa katika kurejesha hali ya utulivu Zanzibar baada ya machafuko ya siku mbili zilizopita zilizosababishwa na wafuasi wa Uamsho na jeshi la polisi na kusababisha hasara za mimilioni ya fedha na uharibifu wa mali. Kikao cha pamoja kilichowashirikisha waziri wa mambo ya ndani Tanzania, Emmanuel Nchimbi, mkuu wa jeshi la polisi Said Mwema na viongozi wa taasisi za kiislamu Zanzibar jana walikubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kurejesha hali ya amani.Katika mkutano huo uliofanyika katika makao makuu ya polisi ziwani zanzibar na pia kuwashirikisha maafisa wa sekta ya utalii na baadhi ya maafisa wa kibalozi kutoka Marekani, Ungereza na Norway. Waziri Nchimbi alisisitiza kuwa suala la kulinda amani ni la wote na akawataka viongozi wote wa kidini na wanasiasa kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa na amani.“Kwa mwaka mmoja na nusu hivi sasa serikali ya umoja wa kitaifa imefanya kazi nzuri na tunawapongeza viongozi wote kwa kazi hiyo, rais Dk Shein, Makamu wake wa kwanza Maalim Seif na makamo wake wa balozi Seif Ali Idd, sasa tusiwavunje moyo” alisema Nchimbi.Alisema kuendelea kwa vurugu Zanzibar ni kuonesha viongozi hao wameshindwa kazi jambo ambalo sio sahihi na kwamba vurugu zinaweza kusababisha watalii kuondoka kabisa nchini na hasa kwa kuzingatia kipindi hiki cha msimu wa utalii kukaribia. Endelea kusoma habari hii

Watu 30 wafikishwa mahakamani

JUMLA ya watu 30 wakiwemo wanaodaiwa kuwa viongozi wawili wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, leo walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashitaka ya uzembe, uzururaji na uvunjifu wa amani.Shitaka jengine walilosomewa mahakamani chini ya Hakimu Mohammed Ali Mohammed Shein hapo ni pamoja na kufanya mkusanyiko usivyo halali ambapo Mbarouk Said Khalfan (45) Mkaazi wa Taveta Meli nne na Mussa Juma Issa (57) Mkaazi wa Makadara wote wakaazi wa Mjini Zanzibar.Washtakiwa hao ambao walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa aman, walifikishwa mahakamani hapo wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi.Viongozi hao kwa pamoja walisomewa mashitaka ya kujikusanya na kufanya maandamano kinyume na sheria kifungu 55 (1)(2)(3)  sheria nambari 6 ya mwaka 2004. ambapo Hakimu Shein alisema mahakamani hapo kwamba mnamo Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:30 za  mchana viongozi hao walijikusanya kinyume na sheria za Zanzibar. Endelea kusoma habari hii

Uamsho wakanusha kuhusika na uchomaji wa kanisa

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu. Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe. Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao. Endelea kusoma taarifa hii

Hali bado ni tete Zanzibar

WASIWASI mkubwa umetanda kwa siku ya pili mfululizo katika mitaa ya miji ya Zanzibar baada ya askari wa jeshi la polisi kupiga mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya wafuasi wa taasisi za kidini zinaozongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI). Wafuasi hao ambao walikusanyika katika makao makuu ya polisi mkoa wa mjini magharibi Madema jumamosi jioni, kushindikiza kutolewa kwa viongozi wao wanaoshikiliwa kituoni hapo. Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba watu saba wanaotuhumiwa saba wamekamatwa na jeshi hilo. Akizungumzia kuhusu hali hiyo ofisini kwake Ziwani Mjini Unguja Kamishna Mussa alisema kwamba jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga fujo hizo pamoja na viongozi wote wa jumuiya ya Uamsho. Endelea kusoma habari hii

Watoto zaidi ya 55 walazwa kwa kuharisha

WATOTO wanane wamefariki dunia na zaidi ya watoto 55 wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kutokana na matumbo ya kuharisha huku chanzo cha ugonjwa huo kikiwa hakijajulikana hadi sasa. Muunguzi dhamamana wa hospitali hiyo Khadija Muombwa Ame alisema amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo tokea mwezi uliopita hadi sasa na kusema kwamba ugonjwa huo bado haujajulikana kama ni maradhi ya mripuko au laa. Ni kweli kuna tatizo hilo la watoto kuharisha sana tokea mwezi uliopita tatizo hili limekuwa likijirejea lakini watoto wanakuja hospitali na kurudi vifo sio vingi lakini watoto wanane ndio waliofariki na watoto kama 58 ndio waliokuwa wamelazwa na sasa hivi hivyo hivyo” alisema Muuguzi dhamana. Kufuatia wagonjwa hao ambao wamekuwa wakiletwa kwa wingi katika hospitali hiyo ya Mnazi Mmoja Muunguzi Dhamana alisema wanalazimika kuwalaza watoto watatu hadi watano katika kitanda kimoja. Daktari huyo alisema watoto wengi waliolazwa katika hospitali hiyo ni wenye umri kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano ambapo baadhi yao wamekuwa wakiruhusiwa lakini baada ya siku mbili wanarejeshwa tena kutokana na tatizo hilo hilo la kuharisha mfululizo. Naye mama mzazi ambaye mtoto wake amelazwa katika hospitali hiyo Fatma Juma Omar Mkaazi wa Tomondo Unguja, amesema hajui kilichomsibu mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili lakini amempeleka hospitali ili kupata matibabu. Endelea kusoma habari hii

Bei ya umeme sasa ni 85% Zanzibar

Wakati wananchi katika visiwa vya Zanzibar wanalalamikia kupanda kwa bei za mahitaji muhimu ikiwemo vyakula, serikali katika visiwa hivyo imepandisha bei ya umeme kwa asilimia 85 ambapo wananchi watalazimika kulipia huduma ya umeme kuanzia tarehe mosi mezi ujao. Zanzibar yenye idadi ya watu wanaokisiwa zaidi ya million moja, ina watumiaji wa umeme zaidi ya laki moja na elfu tano. Kasi ya matumizi ya Umeme Zanzibar imekuwa ukiongezeka kila mara kutokana na matumizi ya nishati hiyo kuongezeka pamoja na kampeni za kutaka wananchi watumie zaidi umeme na kupunguza ukataji miti ili kuepuka uharibifu wa mazingira. Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Ali Mbarouk akitangaza hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema bei mpya itaanza kutumika Juni 1, mwaka huu. Endelea kusoma habari hii

Mv. Seagull yazua kizaazaa baharini

ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi. Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea. Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine. Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele” alisema Masoud. Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake. Endelea kusoma habari hii

Kesi ya wapinga Muungano kusikilizwa Juni 6

KESI inayowakabili watu 12 walioshitakiwa kwa kosa la kubeba mabango ya kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ushahidi wake umekamilika na inatarajiwa kusikilizwa Juni 6 mwaka huu. Mwendesha Mashitaka Said Ahmed Mohammed, aliieleza Mahakama ya Mwanakwerekwe mbele ya hakimu Omar Mcha Hamza jana kuwa upelelezi umekamilika wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa kutajwa mahakamani hapo. Endelea kusoma habari hii

Tanzania imejaaliwa kuwa na Rasilimali

IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali asili na iwapo zitatumiwa ipasavyo zitaweza kuleta manufaa makubwa nchini. Hayo yameelezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Kazi, Uwezeshaji na Ushirika Zanzibar, Asha Abdallah wakati akifungua mkutano wa siku mbili kwa watendaji wa wizara, na idara za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.Katika mkutano huo ambao imeshirikisha mamlaka mbali mbali zinasimamia maendeleo ya sekta ya ujasiriamali, Katibu Mkuu huyo alisema Tanzania licha ya kuwa na raslimali nyingi lakini bado hazijatumika kikamilifu kwa faida za kiuchumi kwa taifa. Akizitaja rasilimali zilizopo nchini, Katibu Mkuu huyo alisema bahari, na ardhi ya kilimo zina uwezo mkubwa wa kuiwezesha  Tanzania kuongoza katika soko la biashara ya ushindani katika bara la Afrika. Tanzania ina rasilimali kubwa sana tena ni rasilimali asili mfano bahari na ardhi tulizonazo kama zitatumiwa vyema basi tunaweza kuwa matajiri wakubwa katika bara letu” alisema Katibu Mkuu huyo. Endelea kusoma habari hii

Maadhimisho ya Mei Mosi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali anayoingoza itaendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi huku akitoa wito kwa wafanyakazi kutimiza wajibu wao makazini . Dk Shein aliyasema hay oleo  katika hotuba yake aliyoitoa katika kilele cha sherehe za wafanyakazi duniani (Mei Mosi), zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na wafanyakazi na viongozi mbali mbali kutoka sekta ya umma na sekta binafsi. Katika hutoba yake hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa kuanzia sasa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lifanye jitihada ya  kuwataka wafanyakazi watimize wajibu wao tena kwa umuhimu zaidi wakiwa makazini. Alieleza kuwa imefika wakati Shirikisho hilo liwashajiishe, liwaelimishe na ikibidi liseme na kuwakemea watumishi wanaochelewa kufika kazini na kuondoka kabla ya wakati kwani huo si utaratibu wa kazi. Dk. Shein alisema kuwa  Shirikisho lisisitize kwa wananchama wake na wafanyakazi wengine suala la kuzingatia nidhamu kazini na kuzingatia taratibu zilizowekwa kukiwa na lengo la kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na kuepukwa matakwa binafsi badala ya matakwa ya umma. Alieleza kuwa hatua hiyo italeta msukumo katika kuimarisha dhana ya Utumishi Bora inayozingatia kuleta ufanisi na uwajibikaji katika sehemu za kazi sanjari na kuimarisha uhusiano mwema kati ya Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri ikiwemo Serikali anayoiongoza.  “Hii serikali yetu sote na kila mmoja anahitajia maslahi mazuri hata mimi pia”,alisema Dk. Shein. Endelea kusoma habari hii

Wazanzibari wakusanya saini ya kutaka kura ya maoni juu ya Muungano

JUMUIYA ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar imetoa fomu maalumu ya kuorodheshwa idadi ya yatu wanaotaka kuitishwa kura ya maoni juu ya mustakabali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya katiba mpya. Jumuiya hiyo imeshirikiana na taasisi nyengine za dini ya kiislamu imeanza kusambaza fomu hizo hapo jana na kuzitawanya sehemu mbali mbali Unguja na Pemba na jijini Dar es Salaam. Lengo la kujaza fomu hizo ni kuchukua majina kamili, saini na namba ya vitambulisho vya wazanzibari au namba ya pasi ya kusafiria kwa wanaotaka kuitishwe kura ya maoni ya kuulizwa wazanzibari iwapo wanautaka au hawautaki Muungano uliopo wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya tume iliyoteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kuanza kazi. “Tunataka kuulizwa kwanza iwapo tunautaka Muungano au hatuutaki halafu tena tume ya rais ianze kazi ya kukusanya maoni ya kuundwa kwa katiba mpya ya Tanzania lakini wakati huo tuwe tumeshaamua tunataka au hatutaki” alisema Kiongozi wa Jumuiya hiyo, Sheikh Azzan Khalid Hamdan. Hatua hiyo ni muendelezo wa harakati zinazofanyika hapa Zanzibar zinazofanywa na taasisi hizo ambapo kwa zaidi ya mwezi sasa kumekuwepo mikusanyiko na mikutano mbali mbali ya kuelezea faida na hasara za Muungano uliopo lakini pia matatizo na kero ambazo kwa takriban miaka 48 zimeshindwa kutatuliwa na viongozi waliopo madarakani. Endelea kusoma habari hii

ZLS kuzindua huduma za kisheria bure CHAMA Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimezindua mpango mpya wa utoaji wa huduma ya ushauri wa kisheria kwa watu wasio na uwezo wa kifedha. Mpango huo ni miongoni mwa huduma zinzoztolewa na chama hicho kwa wananchi wasio na uwezo ambao pamoja na mambo mengine pia utapunguza kwa kiasi kikubwa cha mizozo na msongamano wa kesi mahakamani. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za watu wneye ulemavu Kikwajuni Mjini hapa, Rais wa chama hicho, Awadh Ali Said kwamba lengo la mpango huo ni kuwasaidia wananchi wasio na uwezo kifedha katika kupata ushauri wa kisheria. Alisema pia utoaji wa huduma hiyo utapunguza kesi zinazokwenda mahakamani ambazo baadhi yao hazina ulazima wa kufikishwa mahakamani lakini kwa kuwa watu wamekosa kupata ushauri wa kisheria inakuwa vigumu kuelekezwa wakati ameshafika mahakamani na kufungua kesi. Rais huyo ambaye pia ni Wakili Maarufu Zanzibar alisema miongoni mwa malengo yao ni kuwapa wananchi uwezo wa kujua hatua za  awali za kuepukana na matatizo ya kisheria kabla ya kufikisha shauri lao katika mahakama jambo ambalo litasaidia upunguzaji wa kesi ndani ya mahakama. Endelea kusoma habari hii Wapinga Muungano washitakiwa kwa uhuni KESI ya watu 12 wanaopinga Muungano jana imesomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar huku baadhi ya watu kadhaa wakiwa wamefurika katika Mahakama hiyo kusikiliza. Kesi hiyo imesikilizwa chini ya hakimu Omar Mcha Hamza na kusomewa mashitaka matatu tofauti ambayo hata hivyo wote kwa pamoja waliyakana makosa hayo. Waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na kiongozi wao Rashid Salum Ali (48) mkaazi wa Kikwajuni, Khamis Hassan Hamad (51) wa Jang’ombe, Rashid Ali Rashid (21) anayeishi Mombasa, Hashim Juma Issa (54) mkaazi wa Mbweni,Wengie ni pamoja na Suleiman Mustafa Suleiman (31) anayeishi Mombasa pamoja na Haji Sheha Hamadi (49) anayeishi Chumbuni, Rami Mbaraka Ahmed (48) wa Michenzani na Salum Masoud Juma (38) anayeishi Rahaleo,Wengine walioyajwa katika kesi hiyo ni Mussa Omar Kombo (67) mkaazi wa Mpendae, Omar Kombo Is-hak (21) wa Magogoni, Ali Omar Omar (54) anayeishi Bububu na Masoud Faki Massoud (31) mkaazi wa Kilimahewa. Endelea kusoma habari hii  

Hatutawavulia wanaopinga Muungano

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitawavumilia wanaharakati au kikundi chochote kinatakachohatarisha amani kwa kisingizio cha kupinga Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kutumia mihadhara na makongamano. Hayo yameelezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichomalizika juzi huko Chukwani Mjini hapa.Balozi Seif alisema Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar haitaki kupoteza amani na utulivu na kurejea katika vurugu na uhasama uliojengeka katika jamii kwa maika kadhaa. Napenda niweke wazi msimamo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitakivumilia kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa wananchi wetu” alisema Balozi Seif.Alisema serikali haiku tayari kurudishwa nyuma ambako wananchi waliishi kwa khofu kubwa huku chuki na uhasama zikiwa zimetanda miongoni mwao.“Hatutasita kuvizuwia vikundi vyovyote vinavyoendesha mihadhara au makongamano tutakayobaini yanahataridha usalama wan chi yetu. Na hili hatutakuwa na muhali na mtu yeyote yule” alisema Balozi Seif wakati wa kufunga baraza. Endelea kusoma habari hii

Polisi wawakamata watetezi wa kura ya maoni

JESHI la Polisi Zanzibar limewatia mbaroni zaidi ya watu 12 wakiwemo viongozi wa kundi la wanaotaka kuitishwe kura ya maoni kuhusu Muungano, baada ya kukataa kutii amri ya jeshi hilo iliyowataka kuondoka katika viwanja vya baraza la wawakilishi jana.Kundi la watu zaidi ya 40 lilifika katika viwanja vya baraza la wawakilishi huko Chukwani wakitaka kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ambapo kabla ya kukutana Spika alimuagiza Katibu wake Yahya Khamis Hamad kuongea na wananchi hao. Endelea kusoma habari hii

Watumishi hewa wasakwa serikalini

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuwatafuta wafanyakazi hewa ‘Gost Workers’ katika taasisi zake  na mashirika ya umma na kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika na vitendo hivyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, Haji Omar Kheri amewaambie wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akifanya majumuisho ya ripoti ya kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika ya (P.A.C) ya mwaka wa 2011/2012 kuhusu ufuatiliaji hoja za ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu wa ya mwaka 2008.2009. Alisema zoezi la kuwatafuta wafanyakazi hewa wa serikali ilianza mwezi uliopita kwa watumishi wote kuhakikiwa upya na kutakiwa kuleta vieleelzo vyao ikiwemo kupokea mishahara yao wizarani kupitia kwa wahasibu.“Mheshimiwa Spika kazi ya kuwahakiki watumishi wa serikali imeanza na tunataka kujuwa idadi yao kamili na kutafuta watumishi hewa, pia tunawatafuta wale watumishi wanaopokea fedha mara mbili pamoja na wale ambao wamefariki lakini wameingizwa katika mtandao wa mishahara na wanalipwa licha ya kuwa wapo makaburini” alisema. Aidha Kheri alisema kazi hiyo ilianza kwa wizara ya miundombinu na mawasiliano, wizara ya elimu na mafunzo ya amali na wizara ya kazi na uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuendelea katika wizara nyengine za serikali. Endelea kusoma habari hii

CCM kutoa muongozo wa katiba mpya

Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekusudia kutoa muongozo maalumu na msimamo wake juu ya suala la utoaji wa maoni katika kupatikanaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.“kwa kuzingatia umuhimu wa suala hilo la katiba mpya, Chama cha Mapinduzi kinakusudia kutoa muongozo maalum utaowawezesha Wanachama wa CCM kuutumia ili kuweza kuelezea msimamo wao” alisema Balozi Seif.Balozi Seif ameyasema hayo juzi katika nyakati tofauti wakati akizungumza na wanachama wa CCM wa Kitope, Matetema na Upenja katika ziara yake ya kugawa vifaa mbali mbali vya ujenzi na mashuleni ikiwemo shule ya Kinduni. Endelea kusoma habari hii

Maalim Seif atoa somo la Muungano wa Mkataba

KATIKA kuondosha manunguniko juu ya Muungano wa serikali mbili ya Tanzania na Zanzibar, njia pekee ya kuondosha hilo ni kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni wakati wa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya. Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad jana alipokuwa akihutubia kwenye mikutano ya hadhara ya Chama cha Wananchi CUF huko Kisiwa Panza na Wambaa, Mkoa wa Kusini Pemba ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wazanzibari bila ya woga kutoa maoni yao ili kupata Muungano usiokuwa na manung’uniko na wenye kujali maslahi ya pande zote. Endelea kusoma habari hii

Tutasisitiza masomo ya sanyansi katika skuli zetu- Maalim

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi itahakikisha kuwa inazijengea mazingira mazuri skuli za Zanzibar ili kuwapa matumaini wanafuzni wanasoma masomo ya sayansi. Amesema wanafunzi wengi wamekuwa wakikata tamaa kusoma masomo hayo kutokana na visingizio kuwa ni magumu, sambamba na ukosefu wa vifaa vya sayansi, mambo ambayo amesema serikai imejidhatiti kakabiliana nayo, ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kusoma masomo hayo. Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo  huko skuli ya Mwanakwerekwe “C” katika mahafali ya tatu ya kidato cha sita na michepuo katika skuli hiyo. Amesisitiza haja kwa wadau wa elimu kuwahamasisha wanafunzi  kusoma masomo ya sayansi, hisabati na teknolojia, ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la Afrika Mashariki na maendeleo ya kiuchumi duniani. Amesema Zanzibar bado inakabiliwa na upungufu  wa wataalamu wa fani mbali mbali zikiwemo uhandisi, udaktari na jiolojia, na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili kuziba pengo hilo. Endelea kusoma habari hii

Aprili 13 wajumbe wa tume kuapishwa

Tume hiyo itazinduliwa na wajumbe wake kuapishwa kulingana na matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 iliyounda Tume hiyo. Aidha, Tume hiyo itazinduliwa rasmi wiki moja baada ya kuwa imetangazwa rasmi. Rais Kikwete alitangaza Tume hiyo jana, Ijumaa, Aprili 6, 2012, kwenye mkutano wa wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Endelea kusoma taarifa hii   Mahusiaono ya serikali na NGOs yaimarika Mahusiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jumuiya zisizo ya kiserikali (NGOs) umeanza kuimarika kutokana na serikali kuanzisha mahusiano mazuri baina ya pande mbili hizo na kuondosha udhalilishaji (stigma) kwa taasisi hizo. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taasisi zisizokuwa za Kiserikali Zanzibar (Angoza) Bi Salama Kombo Ahmed katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Bwawani Mjini hapa jana ambapo alisema licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa lakini hivi sasa uhusiano wao unaridhisha tofauti na siku za nyuma ambapo serikali ilikuwa ikiwaona kama ni wapinzania au wakosoaji wa serikali. “Ni kweli kwa muda mrefu hatukuwa na mahusiano mazuri katika kuleta maendeleo kati yetu na serikali na kwa sababu mazingira yalikuwa yakichangiwa na hali ya kisiasa wakati wote tukihusishwa na kudhaniwa kama ni wapinzani kwa sababu tunaikosoa serikali lakini stigma ile sasa imeondoka na tumekuwa tukishirikiana vizuri na serikali ingawa tunataka mahusiano haya yaendelee na kuzidi” alisema Mwenyekiti huyo. Endelea kusoma habari hii

Polisi Pemba adaiwa kubaka

Mahakama ya Kijeshi Kisiwani Pemba jana imesikiliza tuhuma za Askari Polisi John Joseph Bundala anayedaiwa kumbaka Mwanafunzi wa miaka 17 na kumsababishia maumivu makali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba Hassan Nassir amesema mahakama hiyo imesikiliza tuhuma zinazomkabili mfanyakazi wao na kisha kukusanya ushahidi wa kina kabla ya kupandishwa katika mahakama za kiraia kwa mujibu wa taratibu za ofisini yake. Endelea kusoma habari hii Maprofesa wazalendo waahidi kuisaidia Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na Wahadhiri wa Kimataifa wakiwemo wenye asili ya Zanzibar na kupongeza azma yao ya mikakati ya kutaka kuanzisha masomo ya Uzamili, Uzamivu na Uzani katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Dk  Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipokuwa na mazungumzo na Wahadhiri hao wa Kimataifa ambao walikuja hapa nchini kwa lengo la kutayarisha Mitaala ya Masomo ya juu ya Kiswahili kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha SUZA. Endelea kusoma habari hii

ZECO yashutumiwa kwa rushwa

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo na Wanawake wa Baraza la Wawakilishi Hija Hassan Hija amekusudia kupeleka hoja binafsi ya ubadhirifu na rushwa unaofanywa katika shirila la umeme zanzibar katika kikao cha baraza la wawakilishi kitakachofanyika hivi karibuni.Mwakilishi huyo amelishutumu Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) akidai kuhusika na ubadhilifu, ufisadi na rushwa zinazotokana na uungwaji wa umeme kienyeji na watendaji wasio waminifu bila ya kulihusisha shirika hilo. Kuali hiyo ameitangaza wakati akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Idara ya habari (maelezo) Zanzibar ambapo alisema wafanyakazi wa shirika la umeme wamekuwa wakijiungia umeme kiholela na kuwepo kwa wafanyakazi walioajiriwa kwa ubaguzi akimaanisha ni watoto wa wakubwa na watendaji wa shirika hilo. Endelea kusoma habari hii

Meneja wa ZECO awekwa kiti moto mbele ya Dk Shein

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein amemtaka Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Ali Mbarouk kutoa maelezo ya kina mbele yake kutokana na kushindwa kuweka transfoma ya kusambaza umeme katika shule ya Kianga iliyopo wilaya ya Magharibi, Unguja. Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa mradii wa maji huko Selem, Mfenesini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuitembelea miradi ya maendeleo  na  shughuli nyengine za kichama na serikali Unguja na Pemba, ziara iliyoanza leo rasmi. Hayo yamefanyika jana katika ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali katika mkoa wa Mjini Magharini ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Khamis  alipokuwa anajibu risala ya kamati ya shule hiyo juu ya shule kutopata huduma ya umeme licha ya Dk Shein kutoa msaada wa shilingi milioni 3.6 za kununulia transfoma mwaka 2004. Endelea kusoma habari hii.

ZECO yashutumiwa kwa rushwa

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo na Wanawake wa Baraza la Wawakilishi Hija Hassan Hija amekusudia kupeleka hoja binafsi ya ubadhirifu na rushwa unaofanywa katika shirila la umeme zanzibar katika kikao cha baraza la wawakilishi kitakachofanyika hivi karibuni. Mwakilishi huyo amelishutumu Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) akidai kuhusika na ubadhilifu, ufisadi na rushwa zinazotokana na uungwaji wa umeme kienyeji na watendaji wasio waminifu bila ya kulihusisha shirika hilo. Kuali hiyo ameitangaza wakati akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Idara ya habari (maelezo) Zanzibar ambapo alisema wafanyakazi wa shirika la umeme wamekuwa wakijiungia umeme kiholela na kuwepo kwa wafanyakazi walioajiriwa kwa ubaguzi akimaanisha ni watoto wa wakubwa na watendaji wa shirika hilo. Hija alisema uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma na ndio sababu iliyopelekea na kumsukuma kutaka kupeleka hoja binafsi kuliomba baraza la wawakilishi kuunda tume ya kuchunguza ubadhilifu huo. Hatuwezi kukubali fedha za umma zitumike ovyo hili ni jambo kubwa linalopaswa kuundiwa tume ya kuchunguza ili kubaini hasara za ubadhilifu uliopo katika shirika hilo ”alisema Hija. Endelea kusoma habari hii

Waziri Jihad ‘alipuliwa’ mbele ya wafanyakazi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad ‘amemlipua’Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na  Michezo, Abdillah Jihadi Hassan  mbele ya wafanyakazi wa Wizara yake kwa kushindwa kutoa maelezo aliyotakiwa na Kiongozi huyo. Akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa Wizara ya habari utamaduni utalii na michezo katika hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar, Makamu wa Kwanza alisema anashangazwa na kitendo cha Waziri Jihadi licha ya kumwandikia barua kumtaka maelezo ya sakata zima la kuondolewa  wahariri wawili Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) hakuna jibu alilopewa hadi ameitisha mkutano huo. Amesema aliitisha mkutano huo makusudi kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi, huku akiweka wazi kuwa hawezi kusikiliza maelezo ya viongozi pekee, kwa kuwa wakati mwengine hutoa maelezo ya kujilinda na kujijenga kuliko kuwasilisha mawazo ya wafanyakazi. Maalim Seif ameitaka Wizara hiyo kuacha tabia ya kutoa majibu ya mkato kwa wafanyakazi kuwa matatizo yao “yatashughulikiwa”, bali ametaka malalamiko yaliyotolewa yawekewe utaratibu wa kuyashughulikia, na yeye apewe ripoti juu ya utekelezaji huo.Endelea kusoma habari hii

Uvumi wa vyandarua wasambazwa

Mradi wa Malaria Zanzibar unaofadhiliwa na Mashirika ya Global Fund pamoja na Marekani umeingia matatani baada ya kuwepo uvumi kwamba vyandua wanavyogawa kwa wananchi vinasababisha watu kupoteza maisha na wengine kuzimia baada ya kuvitumia. Uvumi huo umekuja siku moja baada ya hatua ya serikali kugawa vyandarua hivyo kwa wananchi huku wanaovumisha wakiwemo baadhi ya viongozi wa dini wakisema kwamba vyandarua hivyo vinasababisha ukosefu wa uzazi, kuvuruga akili na kupoteza maisha. Endelea kusoma habari hii

Takwimu husaidia maendeleo nchini

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka watendaji wa serikali kufuatilia matokeo ya tafiti mbali mbali zilizofanywa ili yaweze kusaidia mipango ya maendeleo. Akizungumza na watendaji wa Idara ya watu wenye ulemavu ikiwa ni mfululizo wa ziara zake za kutembelea ofisi za serikali, Maalim Seif amesema taarifa za tafiti mbali mbali zikiwemo sensa ni muhimu katika kupanga shughuli za maendeleo kwa maidara ya serikali na taifa kwa jumla. Endelea kusoma habari hii

Speech By H.E. The Ambassador of Italy

Tourism is indeed an important element in the economic development of each country and particularly of this Country as it contributes to about 25% of Gross Domestic Product, 70% of the Foreign Direct Investment Exchange. In addition, it employs about 15,000 people and another 45,000 people are involved in activities related to this sector. There is no doubt that it is a major component of the Tanzanian economy. I am pleased to emphasize that, although Italy is famous worldwide for its natural and historical attractions, over 36% of tourists in Zanzibar are Italians. This means that Zanzibar is obviously a place of unquestionable fascination. We therefore need to preserve not only Zanzibar’s environmental assets but also help overcome the inefficiencies that arise. Please Read More

ZATI Speech

Let me start by apologizing to the 60% of ZATI members who have all been victims of crime in the last 12 months. This crime wave could turn off the money tap in 24 hours if allowed to continue. Over the years, as an association ,we together have made many gestures to assist the police force. We have built police posts, provided fuel and equipments, built barracks, and donated bicycles for patrols. Still the crime is on the increase. We are urging the police force and the Government to give us an island of safety and peace – or we will not have a tourism industry. We want a Police force that prevents crime, catches criminals and is backed by a proper judiciary services. If we lose this industry due to being unsafe, we will all – be very sorry. So please – STOP THIS CRIME WAVE – in whatever – the experts in crime prevention – see fit, it is within your means to save us and the industry at large.Please Read more

NECTA yasua kizaazaa Zanzibar

Wiki iliyopita ilikuwa ni kubwa kwa habari za matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne kwa taifa lakini zaidi kwa upande wa Zanzibar. Ni hizo zilitikisa bahari ya Hindi hadi visiwa vikawa vinatetemeka. Ilibidi Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Joyce Ndalichako afanye ziara ya kuja Zanzibar kuelekezea nini kimejiri mpaka yakatokea yaliotokea ambayo wazee na wanafunzi bado hawajaamini. Chanzo ni habari za kufutiwa na matokeo na kufungiwa kufanya mitihani kwa wanafunzi zaidi ya 3,000 kote Tanzania kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa ni udanganyifu unaotokana na mfanano usio wa kawaida. Lakini pia ikaelezwa kuwa kuna mambo mengine yasio ya kawadia yaliotokea kama vile wanafunzi kuandika matusi, kuchora picha kadhaa lakini pia kuandika nyimbo za Bongo Fleva, si matunda ya kizazi kipya bwana. Basi hiyo ikawa ndio habari. Endelea kusoma makala hii

Serikali kuchunguza ukosefu wa mafuta

SAKATA la kuwapo kwa uhaba wa mafuta katika Mji wa Zanzibar, limeishtua serikali na imetangaza kuendesha uchunguzi ili kubaini tatizo hilo limetokeaje kwa vile haliko katika mazingira ya kawaida. Mji wa Zanzibar kwa kipindi cha wiki mbili sasa ulikumbwa na tatizo la uhaba wa mafuta aina ya petroli na kusababishwa bidhaa hiyo kuuzwa kwa shilingi 6000 kutoka shilingi 2000 kwa lita moja. Hali hiyo ilisababisha wananchi wengi kupatwa na wakati mgumu wa kupata huduma hiyo, kwa kulazimika kuinunua bidhaa hiyo kwa njia ya magendo baada ya baadhi ya watu kutembeza biashara hiyo ikiwa katika vidumu, huku vituo vya kuuza mafuta kuonekana kuwepo misongomano ya watu. Endelea kusoma habari hii

Maalim Seif awaponza wahariri Zanzibar

SERIKALI ya Zanzibar imekiri kuwawaondoa Wahariri wawili wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kwa madai ya kuwagonganisha vichwa (fitna) Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuumpa muda zaidi Maalim Seif kwenye ZBC TV. Akizungumza na waandishi wa habari jana Mjini Zanzibar,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari  Utamaduni Utalii na Michezo,  Ali Saleh Mwinyikai alisema wahariri hao waliondolewa katika nyadhifa hizo kwa kukiuka taratibu na mwongozo wa shirika hilo ambapo walionekana watasababisha fitna kwa viongozi hao. Wahariri walioondolewa ni pamoja na aliyekuwa Mhariri Mkuu, wa Televisheni, Juma Mohammed Salum na Msaidizi wake, Ramadhan Ali ambao wamehamishiwa Idara ya Habari (MAELEZO). Mwinyikai aliyasema hayo kufuatia masuali ya waandishi wa habari waliotaka kujua nini chanzo cha wahariri hao kuondoshwa katika nyadhifa zao hizo na kuhamishiwa Idara ya Habari Maelezo. Endelea kusoma habari hii

Mkutano wa elimu ya uraia juu ya katiba

Bi Maryam Aboud akichangia katika mkutano wa elimu ya uraia kuhusu katiba katika mkutano ambao uliandaliwa na baraza la katiba la Zanzibar Bi Maryam alisema ni lazima kwanza watu wajipange vyema na nani na nani wajulikane kuwa watasimama kutuwakilisha wazanzibari lakini suala la elimu mjini mashamba Unguja na Pemba ni muhimu sana kwa kila raia wa nchi hii, lakini pia na alisema tuwe tayari wazanzibari maana nyinyi hampo tayari mnasema tu kwani tunapita humu mitaani na tukiwasikia wengine wakisema hayo ni ya watu fulani na sio yetu kwa hivyo kwanza tabia hiyo iondolewe ndipo tutakapofaulu. Akichangia katika mkutano huo Khaleed Suleiman Said yeye alisema kwamba hakuna kisichowezekana na tukiamua wazanzibari tunaweza, tuanze kwanza na mkataba na sio katiba sasa kama hatuna mkataba tutakuwa vipi na katiba? tuwe na mamlaka kwanza ya zanzibar tuwe na jamhuri ya watu wa zanzibar kwanza, Khaleed anasema yeye hapingi mkataba lakini mkataba huo utasimama wapi bila ya nchi, pili vigezo vinavyohalalisha nchi kuwa nchi moja wapo ni serikali, lakini zanzibar licha ya kuwa serikali ipo lakini ukweli mamlaka yote yapo tanzania bara, jambo la msingi tunachotaka ni kuitishwa kura ya maoni tuulizwe tunataka muungano au hatuutaki, wenzetu wanaonesha dhahiri kuwa hawana nia njema na zanzibar, kwa hivyo sisi tuna haki kikatiba kutishiwa kura ya maoni kwa kuwa sheria zetu zinaturuhusu kuitisha kura ya maoni na mbona tuliweza wakati wa kutaka serikali ya umoja wa kitaifa vipi leo tushindwe katika hilo? Alihoji Khaleed. Endelea kusoma habari hii

Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba

UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya mwaka 2009 na Septemba 2010 unaonyesha, asilimia 47.05 ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba.Malengo ya utafiti huo uliosimamiwa na Dk Henry Mwakyoma, yalikuwa ni kubaini ni kwa kiasi gani wanaume huweza kuathiriwa katika via vyao vya uzazi na hatimaye kushindwa kutungisha mimba.Endelea kusoma habari hii

Mkurugenzi wa Bandari ahamishwa

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kutekeleza taarifa ya ripoti ya Tume ya kuchunguza ajali ya meli ya Mv. Spice Islander  kwa kumuondowa katika wadhifa wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari la Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe. Jumbe katika barua yake ametakiwa kuripoti kazi katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano na atapangiwa kazi nyengine. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa wizara hiyo aliyohamishiwa alikiri kuwa Jumbe aliripoti katika wizara ya miundombinu lakini alisema hajui amepewa kazi gani kwa kuwa ndio kwanza barua yake ya kufika katika wizara hiyo amepewa na atalazimika kuhudhuria katika ofisi yao. Endelea kusoma habari hii

Zanzibar yapinga Tanzania kudai eneo zaidi la mpaka wa bahari kuu

Ombi hilo tayari limeshawasilishwa katika  Umoja wa Mataifa, New York, na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi wa Tanzania, Professa Anna Tibaijuka, akitaka kilomita 150 zaidi za bahari. Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa aliyeliibua suala hilo kwenye Baraza la Wawakilishi hapo juzi, Amina Abubakar amezungumza na Ismail Jussa kuhusiana na msimamo huo kwa kusikiliza mahojiano hayo. Tafadhali bonyeza hapa Dar es Salaam. Dr Asha-Rose Migiro is leaving her high profile posting as deputy secretary-general of the United Nations.  Having served the UN for five years as the second in command following a surprise appointment in 2007, she is expected home in the next few weeks.

Uzembe chanzo cha maafa ya Mv Spice Islander – Ripoti

Maafisa kadhaa wa bandari ya Zanzibar pamoja na wamiliki wa Meli ya Mv Spice Islander iliyozama na kuua watu zaidi ya 200 mwaka jana wametajwa kuwa wazembe, katika  ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza ajali ya meli hiyo. Akitoa muhtasari ya ripoti hiyo kwa waandishi wa habari mjini Zanzibar leo, Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee alisema tume iliyoundwa na rais kuchunguza ajali hiyo imebaini kuwepo kwa uzembe mkubwa, kutofuata sheria, usimamizi mbaya wa sheria, na rushwa katika bandari ya Zanziba. Endelea kusoma habari hii

Ripoti yawatia hatiani wakurugenzi wa bandari

Katibu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ameiweka hadharani ripoti ya ajali ya meli ya Mv Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kusababisha vifo vya idadi kubwa ya watu. Ripoti hii imetaja uzembe kama chanzo cha ajali, idadi kamili ya wailokuwemo katika meli na waliokufa, mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya wahusika na fidia kwa waliothiriwa. Sudi Mnette wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle amezungumza kwanza na mwandishi wa habari Issa Yussuf aliyepo Zanzibar, na kisha na Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa Chama cha Wananchi (CUF) kuhusiana na ripoti hiyo na mapendekezo yake. Kusikiliza mahojiano ya Sudi Mnette na Issa Yusuf, tafadhali bonyeza hapa na kusikiliza mahojiano yake na Salim Bimani, tafadhali bonyeza hapa.

Siri ya mafanikio yetu ni umoja- Dk Shein

Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amaan zimefana huku zikionesha umuhimu wa kuwepo kwa mshikamano mkubwa wa wananchi wa Unguja na Pemba. Sherehe hizo zinafanyika huku Wazanzibari wakiunganishwa na Serikali ya umoja wa kitaifa inayotokana na maridhiano ya kisiasa ambayo lengo lake kuondosha siasa za chuki na uhasama. Mbwembwe za viongozi wa kitaifa wakati wakiingia katika uwanja wa amaan pamoja na gwaride la vikosi vya ulinzi ni miongoni mwa matukio muhimu ambayo yalifanikisha na kuzipamba sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amaan. Wananchi waliwashangilia viongozi wakuu wa kitaifa akiwemo rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Sheni ambaye aliingia uwanjani hapo akisindikizwa na mapikipiki ya askari wa polisi yapatayo 10. Lakini kiongozi aliyevutia mara baada ya kuingia katika uwanja wa Amaan ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya Kikwete ambapo kwa kawaida wanajeshi humsalimia kwa kupiga wimbo wa taifa. Endelea kusoma habari hii

Huduma ya maji Kiuyu Pemba

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuimarika kwa miundombinu katika Wilaya ya Micheweni kutalifanya eneo hilo kutimiza azma ya serikali ya kulifanya kuwa eneo huru la kiuchumi. Amesema wawekezaji watavutiwa zaidi kuwekeza vitega uchumi vyao ikiwa watahakikishiwa upatikanaji wa huduma muhimu zikiwemo maji, barabara na umeme.Makamu wa Kwanza wa Rais alieleza hayo jana huko Micheweni Pemba baada ya kufungua mradi wa maji wa Kiuyu na Maziwang’ombe, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Maalim Seif ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kuutunza mradi huo na kuhakikisha kuwa huduma hiyo inawafikia wananchi kwa wakati wote. Endelea kusoma habari hii Tendwa, Werema wajichanganya Katika hili nahisi tendwa amepotoka kisheria na halikadhalika Jaji Werema amepotoka.tuanze na Tendwa. hoja ya tendwa ni kuwa kufukuzwa kwa hamad rashid ni hasara kwa taifa kwa sababu kutalazimisha kuitishwa uchaguzi mdogo. na wakati wa kufukuzwa kwa kafulila wa NCCR  alinukuliwa akisema kuwa gharama za kuitisha uchaguzi mpya ni karibu 7bn. lakini katiba ya nchi inaruhusu chama kumfukuza mbunge kwa maana ya kuwa mbunge kudhaminiwa na chama kuingia katika siasa na kwa hivyo chama kina mashiko kwake. kama tendwa anaona hili linatia gharama basi apendekeze kubadilishwa kwa sheria na kifungu kipya kiingizwe juu ya utaratibu mpya na mwepesi kupata mbunge mpya kujaza nafasi ya mbunge aliyechukuliwa nguvu zake na chama. Endelea kusoma habari hii Walemavu hawajafikiriwa katika majengo mapya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameelezea haja kwa majengo ya kisasa ya serikali kuwa mfano katika kuwajali watu wenye ulemavu nchini. Amesema majengo mengi yanayoendelea kujengwa bado hayajatoa umuhimu kwa watu wenye ulemavu na kuwafanya kushindwa kuyatumia kwa shughuli mbali mbali za kijamii ambazo zinapaswa kuwafikia wananchi wote. Makamu wa Kwanza wa Rais ametoa changamoto hiyo leo wakati akifungua jengo la ghorofa tatu la mfuko wa barabara Zanzibar lililoko Maisara ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Endelea kusoma habari hii

Aboud apinga urais wa kupokezana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mohammed Aboud Mohammed amesema ni hatari Rais wa Muungano kupatikana kwa zamu katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika Zanzibar. Tamko hilo amelitoa alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar huko Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar jana. Alisema kuwa na mfumo wa kutoa urais kwa zamu ni mwanzo wa kuligawa taifa na kuvuruga umoja wa kitaifa wa Tanzania. “Ni hatari kuwa na mfumo wa kutoa urais wa muungano kwa zamu kwa sababu ni mwanzo wa kuligawa taifa vipande,” alisema Waziri Aboud. Endelea kusoma habari hii

Athari za mafuriko waliokufa kufikia 41

MIILI saba ya watu imeopolewa eneo la Jangwani na kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanya idadi ya waliokufa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 20 na kuhifadhiwa hospitalini hapo, kufikia 22 hadi jana.Kadhalika maiti za watu wanne zimefikishwa katika hosipitali ya Mwananyamala na kusababisha chumba cha kuhifadhia maiti cha hosipitali hiyo kufurika hivyo kusitishwa kwa upokeaji wa maiti zaidi. Endelea kusoma habari hii

Maafa ya mvua Jijini Dae es Salaam watu kadhaa wafariki

WATU 11 wakiwamo watatu wa familia moja, wameripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mvua zilizoendelea kunyesha jana katika Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake na kuvuruga mfumo wa usafiri na shughuli za kiuchumi.Miondombinu mbalimbali ya Jiji hilo ikiwamo madaraja na nyumba vilivunjwa na kusababisha adha kubwa kwa wakazi ambao wengi wao, walishindwa hata kwenda kazini. Endelea kusoma habari hii

Polisi jipangeni kupambana na uhalifu-Maalim

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amelitaka Jeshi la Polisi kuzidisha bidii katika kuwapa watendaji wake taaluma ya utambuzi wa njia zinazotumika kufanikisha uhalifu kupitia mtandao (cyber crimes) kwa nia ya kukomesha uhalifu wa aina hiyo hapa nchini.Endelea kusoma habari hii

Norway itaendelea kuisaidia Zanzibar

Norway imesema itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za kudumisha umoja na mshikamano uliopatikana baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa, kwa vile hali hiyo imeonesha dalili nzuri za kukuza maendeleo ya wananchi katika kipindi cha mwaka mmoja chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.Endelea kusoma habari hii

Serikali ya Muungano yalaumiwa na wawekezaji Zanzibar

WAWEKEZAJI Zanzibar, waliilaumu vikali Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kishindwa kulinda usalama wao na mali zao visiwani Zanzibar. Walisema usalama wao na mali zao unatishiwa na vitendo vya uhalifu na juhudi za polisi kupambana na wimbi hilo ni mdogo. Endelea kusoma habari hii

Ujamaa uliziunganisha Tanganyika na Zanzibar

Na Fidelis Butahe

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa rais wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa rais wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, Aprili 26 hadi 27, 1964. Endelea kusoma habari hii

Makahaba wasambazwa Unguja

Pamoja na hujuma mbali mbali za kudhoofisha jamii na maadili ya Kiislamu katika Visiwa vya Unguja na Pemba,kamailivyo kote walipo Waislamu, mbinu mpya zimebainika, hali iliyoibua hoja mbali mbali za waumini.Katika siku za karibuni Waislamu waZanzibarwameripoti kubaini wimbi la harakati za mfumokristo zinazolenga kuudhoofishaUislamu,Tanzania Visiwani.Endelea kusoma habari hii Kamata kamata Al Shabaab yatua Mwanza Vijana wanne (4) wa Kiislamu wamekamatwa jijini Mwanza wakituhumiwa kuwa ni Al Shabaab. Vijana hao ambao walikamtwa katika muda na mahali tofauti, wa kwanza akikamtwa Jumatatu huku wawili wakikamatwa Jumanne na mwingine akikamatwa juzi Jumatano.Waliokamatwa wametajwa kuwa ni Hassan Jumanne Hassan mkazi wa Igogo na mfanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Mlango mmoja.Endelea kusoma habari hii Mashirikiano ya pamoja yanahitajika kutokomeza mifuko ya plastiki Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema mashirikiano zaidi yanahitajika katika kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki Visiwa Zanzibar.Sambamba na hiloMaalim Seif amesisitiza elimu zaidi itolewe kwa wananchi ili kutambua athari za matumizi ya mifuko hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa kuwa chanzo kikuu cha uchafu katika manispaa ya mji wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii Barza zina historia kubwa katika siasa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad ameanza utekelezaji wa mpango wake wa kutembelea baraza za mazungumzo (Barza) kwa lengo la kuwa karibu zaidi na wananchi na pia kutoa wito kwa wananchi kuhuisha baraza zao kwani zina mchango mkubwa katika harakati za kisiasa nchini.Endelea kusoma habari hii   Atakayebainika kuwadharau wenye ukimwi kuwajibishwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitaacha kumchukulia hatua ya kumuwajibisha mtendaji yeyote wa serikali  atabainika kwamba anafanya dharau na kuwanyanyapaa watu wenye kuishi na virusi vya ukimwi nchini, sambamba na hilo serikali imesema hivi sasa wananchi wa Zanzibar wamepata mwamko mkubwa katika vita dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na Unyanyapa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo.Endelea kusoma habari hii   Lengo ni kuinua kilimo na uvuvi-Maalim Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema sekta za uvuvi na kilimo zitapata mafanikio makubwa iwapo mipango iliyopo inatatekelezwa kamainavyotarajiwa. Amesema kampuni kadhaa zinatarajiwa kuwekeza katika shughuli za mazao ya baharini ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda vya usindikaji vya samaki kwa lengo la kuinua kipato cha wavuvi hasa wadogo wadogo.Endelea kusoma habari hii Sitavumilia Wazanzibari kubaguliwa-Seif Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema cha chake hakiwezi kukubali kuona baadhi ya wazanzibari wanaendelea kunyimwa haki yao ya kupatiwa vitambulisho vya uzanzibari ukaazi.Endelea kusoma habari hii Sitta na kamati yake hoi Zanzibar Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano”.Endelea kusoma habari hii Dk Shein afanya uteuzi Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika uteuzi huo, Rais Dk Shein amemteua Profesa Idris Ahmada Rai kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA). Profesa Rai ni Profesa wa Sayansi aliwahi kusomesha Chuo Kikuu cha Makerere Uganda.Endelea kusoma habari hii   Serikali nilipeni haki yangu Gari la Katibu Mkuu  Wizara wa Fedha, Uchumi na Maendeleo ya Mipango wa Zanzibar limeshambuliwa kwa mawe na  Ali Salim Ali(49) Mkazi wa Fuoni Mjini Unguja  ambaye anaidai Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kufanya kazi ya ujenzi wa jengo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.Endelea kusoma habari hii   VIFAA VYA TV PEMBA VYAZAMA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar; Hassan Abdulla Mitawi amesemna kuwa matumaini ya Kisiwa cha Pemba kuanza kupata matangazo ya Television wiki ijayo yamevunjika kutokana na baadhi ya Vifaa Vya Mitambo iliokuwa ikipelekwa huko Pemba kuzama.Endelea kusoma habari hii   DK SHEIN AHIMIZA UADILIFU RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza suala la uadilifu katika sehemu za kazi na kusema ndiyo kipimo cha imani ya mtu na kumfanya kuwa raia mwema.Akilihutubia baraza la Eid El Fitri katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani, alisema mfanyakazi mwaminifu hutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo kwenda kazini kwa wakati na kuondoka kazini.Endelea kusoma habari hii RAZA ATAMBA KUMALIZA KERO ZA MUUNGANO Mfanyabiashara na kada wa CCM maarufu Zanzibar Mohamed Raza ametangaza kuomba kazi ya ubunge, mshauri, au, mjumbe wa tume ya marekebisho ya katiba ya Muungano kwa rais Jakaya Kikwete ili aweze kumaliza kero zote ndani ya muungano.Endelea kusoma habari hii   BEI MPYA YA CHAKULA YATANGAZWA Katika kudhibiti Mfumko wa bei serikalini, Serikali ya Zanzibarimetangaza kuanza udhibiti wa bei za bidhaa muhimu hasa vyakula kuanzia leo (jumapili), na kuonya kuwa mfanyabiashara yoyote atakayekwenda kinyume na hiloataadhibiwa.Endelea kusoma habari hii Mpango wa kuleta mapinduzi ya kilimo muafaka! Kalamu – 27 Julai 2011 NIMEFARIJIKA sana kusikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) inaamini mapinduzi kwenye sekta ya kilimo.Nimevutwa na mkakati wake wa kusaidia wakulima hasa wa mazao ya chakula, ikiwemo mpunga ambao chakula chake – wali – ndio chakula kikuu cha watu wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii SERIKALI ZA UMOJA WA KITAIFA YATIMIYA MWAKA MMOJA SERIKALI visiwani Zanzibar imsema inajiandaa muswada wa kuunda sheria ya kusimamia vita dhidi ya rushwa visiwani humo.Hayo yalisema jana na makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad katika kongamano la kumbukumbu ya siku ya umoja wa kitaifa mjini hapa.Maalim Seif Sharrif Hamad alisema anaamini baada ya mandalizi kukamilika,muswada huo utapelekwa katika kikao kijacho cha Baraza la Wawakilishi.Endelea kusoma habari hii  

SMZ YATOA CHANJO MPYA

 

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekusudia kuanzisha zoezi la kutoa chanjo ya kipindupindu (Choleras) Januari mwaka huu katika maeneo sita kwa Unguja na Pemba ili kukabiliana na ugonjwa huo. Maeneo ambayo yamepangwa kutolewa chanjo hiyo ni yale yanayojulikana kuwa ni sugu kwa ugojwa huo ambapo idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu hupatikana katika maeneo hayo siku za nyuma ambapo tayari Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imeshafanya sensa ili kujua idadi ya wakazi wa maeneo hayo. Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii, Juma Rajab amewaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake Mnazi Mmoja kwamba chanjo hiyo itatolewa bure na kwa watu wenye kutaka kwa hiari na hakuna kulazimishwa mtu. Endelea kusoma habari hii.

 

 

KUFUNGWA KWA GUANTANAMO KUMEFURAHIWA 

Mama wa Mtuhumiwa wa Ugaidi, katika Balozi za Marekani Jijini Dar es Salaam na Nairobi, Bimkubwa Said Abdallah (56) amesema amefurahishwa na uamuzi wa Rais mpya wa Marekani Barack Husein Obama kwa kutaka kufungwa kwa jela ya Guantanamo Bay . “Ninamshukuru sana sana Rais wetu mpya wa Marekani kwa kutoa amri ya kulifunga jela ya Guantanamo bay lakini pia tunshukuru kuwa watoto wetu watafutiwa kesi walizokuwa wamebambikiziwa…” amesema huku akitokwa na machozi mama huyo. Amesema haoni kama kuna haja ya kufungua kesi dhidi ya serikali ya Marekani kwa kumuweka jela kwa miaka kadhaa lakini jambo kubwa analolitaka ni kurejeshwa mwanawe nyumbani na iwapo atakuwa ameathirika ataomba atibiwe. Endelea kusoma habari hii.

 

 

WAZIRI HAROUN AKATAA KUJIUZULU

 

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman amesema haoni sababu za msingi za kuchukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake kutokana na wanafunzi kutoka Zanzibar kufanya vibaya katika kidatu cha nne mwaka huu. Tamko hilo amelitoa jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Mazizini Mjini hapa baada ya kujitokeza shindikizo kutoka kwa baadhi ya wananchi na wana siasa wakimtaka achukue uamuzi huo. Amesema utamaduni wa kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya mitihani ya wanafunzi haupo Zanzibar na kama ungekuwepo hata kiongozi wa upinzani Maalim Seif Sharif Hamad asingesalimika kutokana na matokeo ya mitihani ya mwaka 1980. Endelea kusoma habari hii.

Advertisements

9 responses to “Habari

 1. You really make it appear really easy together with your presentation however I find this matter to be actually one thing which I feel I’d never understand. It sort of feels too complicated and extremely vast for me. I’m taking a look forward for your subsequent submit, I?ll attempt to get the grasp of it!

 2. X Paster Gaidi wa Kitanzania aliye mafichoni Ireland

  Habari za kuaminika zinasema kwamba, Watanzania wameanzisha kikundi cha JIHAD kinachoitwa Al Jihad Islamic, chenye mwenendo, maadili, mahusiano na Harakati Al Shabab ya Somalia
  .
  Chanzo cha habari hizi kinasema kuwa, Mmoja na Mwanzilishi wa kikundi hicho cha kigaidi ni Dr. Suleima Seif Suleiman anaye julikana kwa jina la Dr. Sule na Mtanzania mwenzake anae ishi kwa kujificha nchini Ireland ambaye ni Ustaad wa Dawah Islamic Group of Ireland anaye tumia “nick name” ya X-Paster ambaye vile vile ni Katibu Mkuu wa AJIPC. Gaidi X-Paster ni blogger wa Amua Sasa anaye tumia jina lingine la Besty katika blog hiyo.

  Habari za kuaminika zinaendelea kusema kuwa, gaidi huyu, X Paster ambaye vilevile ni mhariri wa Jamii Forum anampango wa kuleta michafuko ya kidini nchini Tanzania kwa nia ya kuigeuza Tanzania kuwa Nchi ya Kiislam. Gaidi huyu alisikika akijigamba kwa kusema kuwa, taasisi yake ya kigaidi itafanya vitendo vya kigaidi ikiwa ni pamoja na kutumia magari kama mabomu na kulipua sehemu nyeti za Serikali ya Tanzania. Zaidi ya hapo, Gaidi huyu alidai kuwa, taasisi yake ya kigaidi inampango wa kufanya vitendo kama hivyo vya kigaidi nchini Marekani na Israeli. Chanzo cha habari hizi kinasema kuwa, gaidi huyu anapokea misaada kutoka taasisi mbalimbali za kiislam ambazo si za kiserikali na kwa njia nyingine ambazo si halali na za jinai.

  Source: CPI News

  • HAO NI WALE WASIOIPENDELEA MEMA ZANZIBAR. TANGU LINI MTU AKAFURAHIA KUWA MTUMWA? TENA WA FUKARA ANAYESHINDWA KUJIPATIA CHAKULA CHAKE

 3. BOLG YETU NI NZURI LAKINI NAOMBA KILA MADA INAYOWEKWA KWENYE MTANDAO ITANGULIWE NA TAREHE

 4. we iddi mimi naijuwa zanzibar tena sana mi ni mzanzibari halisi., muungano ni kitu kizuri na wazanzibar halisi wanapenda muungano , wanapenda tuwe pamoja sababu wanajuwa bila ya muungano zanzibar tungepinfuliwa tena na wale wanaojita waarabu .,, sisi ni wazanzibari sio waarabu sisi ni waafrika sio waarabu na unazungumza kuhusu utumwa utumwa wanafanya wale wanao jita waarabu na sio muungano, munguano ni kitu kizuri sana katika nchi yetu , kwanza
  kwa ajili ya muungano tunachance nyingi ya watalii nchini yetu
  pili kwa wale watu wanaoishi nchi za nje ni vizuri kwao .. ni kuomba visa ya tanzania na wanaweza kutembeya bila ya kuomba visa 3 ya tanzania pemba na unguja ..
  nataka munjuwe kama muungano nikitu kizuri sana ata kwenye kuraan imelezwa kuwa jirani yako ni familiya yako .,, watizame wenzetu wa somali wanapigana hawajui wanapiganiya nini,kenya vita uganada vita ethiopia elitrea vita burundi rwanda vita zembabwe vita ,, tanzania zanzibar shwari hakuna vita munajuwa sababu gani hatuna vita sababu ya muungano , sisis tumefundishwa tusibaguwane na nani aliyesema ivyo .. nyerere tizameni sasa nani anaetubaguwa . ni wale watu wanaosema wao waarabu ni ndugu zetu wenyewe wa kipemba , wanajita ndugu zetu lakini ukweli ndugu zetu ni wale wanaopendana , , halafu wanajita waislam
  zanzibar njema atakae aje ..
  nou they talk about, watanzania nia makafiri please musifanye mazambi watanzania sio makafiri makafiri ni wale watu wanaoita wenzao makafiri , mukumbuke kama kule tanzania kuna ndugu zetu wengi wa kipemba na wa unguja… wanatafuta maisha

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s