Steven Kanumba afriki dunia

Msanii Steven kanumba enzi za uhai wake.
Habari zilizotufikia hivi sasa zinasema msanii maarufu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa Muhimbili. Habari zaidi zitawajia baadae. Taarifa hii kwa mujibu wa Global Publishers

Wakati wazanzibari wakijitayarisha kusoma khitima ya aliyekuwa Muasisi wa Taifa lao la Zanzibar, wameamka na kupata taarifa kwamba Msanii Maarufu katika tasnia ya filamu nchini Steven Kanumba amefariki dunia jana usiku kufutia shambulio la kusukumwa ingawa taarifa kamili za kifo hicho bado hazijafafanuliwa kwa kina na vyombo vinavyohusika lakini kwa taarifa za awali zinasema kwamba alisukumwa akiwa nyumbani kwake baada ya kutokea kutofahamiana kati yake na mpenzi wake Lulu binti mwenye umari wa miaka 18.

Mashabiki wakiwa wamekusanyika katika viunga vya hospitali ya Muhimbili. Habari za awali ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Kenyela amesema kuwa Kanumba alikuwa na kutoelewana kati yake na Mpenzi wake ambazo taarifa za awali zinasema waligombana na Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi wake ambaye ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.

Bi Lulu huyo

Habari ambazo bado Spoti na Starehe haijazithibitisha zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na ndipo aliposikia mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka kumuuliza ndipo mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusumunana Kanumba alisukumwa akaanguka na kugonga kichwa chini.

Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika Pale walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.

Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi wake Maerehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. Lulu ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18 tangu kuzaliwa.

Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika kwa taabu.

Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa Tanzania bali hata nje ya nchi pia. Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa na adamu ya maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu wa rika lote. Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.

Mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha masikitiko yao ambapo kufika saa tisa usiku habari zilikuwa zikisambaa kama moto nyikani kupitia Facebook, Twitter na Blogs ikiwemo hii ya Spoti na Starehe ambayo ilikuwa moja ya wa kwanza kupata habari.

                    UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

press@ikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

              P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania –TAFF- kuomboleza kifo cha msanii maarufu nchini Steven Charles Kanumba, aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Aprili 7, 2012.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amemwomba kiongozi huyo wa TAFF kufikisha salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wana-familia ya Kanumba na kwa wasaani wote nchini ambao wamepotelewa na mdau na mwenzi wao.

Rais Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kuzunishwa na kifo cha msanii huyo ambaye amemwelezea kuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye katika uhai wa maisha yake mafupi na akiwa bado kijana sana amechangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya sanaa ya filamu nchini na kupitia sanaa hiyo kuitangaza Tanzania kimataifa.

Amesema Rais: ”Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya filamu nchini hautasahaulika.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Ndugu Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa nchi yetu.”

Nakutumia wewe Rais wa TAFF salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa wasanii wote wa filamu na sanaa nyingine kufuatia msiba huu mkubwa kwa fani yetu ya sanaa. Aidha, naomba unifikishie salamu za dhati ya moyo wangu kwa wanafamilia wote. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa. Waambie naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu cha msiba,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

Namwomba Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa sababu yote mapenzi yake. Aidha, naungana na wana-familia na wasanii wote nchini kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.”

Mwisho.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

07 Aprili, 2012

Advertisements

55 responses to “Steven Kanumba afriki dunia

 1. Very good, kapotoa wengi hapa Znz wacha afe hana umuhimu wowote hapa Zenji.
  Wacha aende akaone alichokichuma huko kwa Allah.

  • kuwa na akili timamu mwanaharamu wee yy kazi yake ni kufikisha ujmbe kwa wananchi na si kupotosha km m2 alipotoka kupitia yy kajipotosha mwenyewe roho km mchawi unafurahia mwanadamu mwenzako kufariki umesahau kwamba kila nafsi itaonja umauti

   • @hashim juma
    Allahu Akbar…… Unamjua mwanharam au unasema tuuuu ??? Kaka!!!
    Kama umenuna unaweza kuniona nipo Kwerekwe.
    Lakini ckulaumu hata kdogo wa2 kama wewe tunao wengi huku mitaani.
    Wallahi ikiwa ulimpenda Kanumba na kumsifu namna hiyo badala ya MTUME (SAW) basi labda ni kwambie tu:
    INNA LILLAAHI WAINNA ILAYHI RAJIGGHUUWN hashim juma.

  • u knw lyf z a cycle….in dat cycle dez evry knd of ppo 1 of dem z u fkn fagn…. Ww mwnzako kafark unafrah¿…i dnt thnk f u hav a soul….kama unayo itx xo fkd up…..fck u man na kama unatafta umaaruf hautaupata kwa njia hii hamna hata m2 1 anaye pay attntion kwako xo b a man shw ur nutx dnt act dicklex…….stp bng a btch ad pry 4 our brthr stevn kanumba god guid his soul

  • unabwabwaja tu.wajiita mwislamu eti?maneno machafu huna hata haya.wendo utaenda kuzimu.ebu onyesha ubinadamu.

  • tatizo lako hujasoma ndo kinachokupa shida, ungepitia shule ungeona ni jinsi gani watu wanafikishiwa ujumbe.ni filam gani ambayo ameuharibu uislam? huna dini wewe bali una jina coz apo tu ushatenda dhambi mwombe Mungu akusamehe.

 2. Inasikitisha kuona kwamba mtu anafurahia kifo cha mwenzake!!! Nimeshangazwa sana na baadhi ya watu wanaofurahia kifo hiki na hata baadhi yao kutoakauli za kumsimanga maiti na hata wengine kumuombea balaa kama kwenda motoni. Kwakweli inasikitisha kwamba inafikia hali hii katika jamii yetu. Je tujiulize haya ni mafundisho gani? jee ni dini auni jambo gani linalotufunza mmoja wetu anapopatwa na mauti tutoe response kama hizi. Jee mtu atafurahi yeye au jamaa yake atapokufa akaanza kusimangwa na kuombewa dua za kwenda motoni? Kila mtu ana uzuri wake na ubaya wake kama mtu hakuwa muuwaji au alienyenyesa binaadamu wenzake wakati wa uhai wake sioni sababu ya watu kufurahia kifo chake au kumlaani.

  Anyway Mungu atuongoe tuondokane na ujinga.

  • @Huna jina!!! (chukua jina hili Kafiri wa Kitanganyika)
   Kama umesikitika unaweza kukata rufaa kwa alomtoa roho amrejesheee.
   Kwa kila muislam anafuraha ya kupindukia kw kifo cha huyu jamaa, kapotosha jamiii ya kiislam kubwa hapa Znzbar wacha tufurahie kifo chake.

  • @Huna jina!!! (chukua jina hili Kafiri wa Kitanganyika)
   Tupe mazuri alofanya ktk jamii ya kiislam hata tumuombeee dua njema, wacha kutuletea tawhid isiyokuwa na kichwa wala miguu. Kasoma hukumu ya mtu kama huyu ktk uislam ikiwa wewe ni msomaji.

 3. alikuwa mtu wa watu alielimisha zaidi tutamkumbuka daima.MUNGU ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.

  • tusiwazulie kwa hapo ni umaluuni we2 tu ndo unaopotosha mila natamaduni zetu. wanatunyanyasa kwa mengne lakin kwa upotevu wa maadili ni wetu sisi wenyewe .

 4. eeee binadamu hakuna atakaebaki ila Allah kweli lakini sioni kitu gani cha kukufurahisha hamad binadamu mauti yako leo yeye kanumba kesho wewe au jamaa yako tuwache ujinga tulokuwa nao mimi ni mzanzibar na nimesikitika kwani ni mtanzania mwenzangu na binadamu mwenzangu basi sioni sababu ya kufurahi kila mtu na kaburi lake hamad

  • @ sharife
   Kwa taarifa tu Allah hatouangalia UTanzania wenu, kinachoangaliwa ni amali njema ulizozifanya na kama hukuwa muislam hata ujenge msikiti kama Nyerere(laanatullah) Allah hatokulipa chochote.
   Mimi nakusikitikia wewe ulietakiwa kuwaombea dua wazee wako ili Allaha atuepushe na moto badala yake unamtetea kafiri alieharibu na kupotosha maaadili ya waislam.
   Sijui ni MIMI au WEWE ndio mjinga ktk kupeleka mbele harakati za Uislam.

   Tafakari saaana….?????? Muhimu uislam wako na sio Kanumba.

   • ivi wewe kaka inaonekana wewe umefurahishwa na kifo ca kanumba ama piya na wewe nimuhusika wakifo hico ila sikulau nikwasababu ujenda shule mimi na ndo naishi holland ila kifo ca kaka huyo kimeniuma sana mungu ayilaze roho yake mahala pema amina

  • @MAJOR DAUDI
   Ni ya baba yako au umemkodia.
   Dah….!! wa2 bwana wamerogwa na wamerogeka.

 5. dont say that am also zanzibarian, sote binaadamu sisi na sote marejeo yetu ni kwa mungu mwezetu ashatangulia na ashajijua je ww unajijua utakufa kifo gani au uislam wako wajina ndo unakupa uhakika wa kuingia pepo kama alikuwa anapoteza watu wakinini hukuinua kinywa chako kwani sote ni wachunga na sote tumeambiwa tufikishe neno la mungu je wewe ulimfikishia kwa njia gani?

  • @Chum Haji Chum
   Kwani ulikuwa umejisahau kama utakufa au ndio wapenzi wa Kanumba haoo.
   Na kwanini kama wewe muislam uchukue reference kwa kanumba ?
   Wamekufa maulamaa na maustadhi wengi na hatujawackia mukiwaombea dua wala kukumbuka mauti, cjui kwanini….?
   Waislam kazi ipo kwelikweli.

 6. Hakika sisi ni wa Mwenyeenzi Mungu na hakika kwake yeye ni marejeo yetu!
  Kila nafsi itaonja mauti! Ni vizuri kujichunga nafsi zetu kwani mauti hayana hodi,
  yanapomfika mja ni lake kwa wakati wake!

  Tujitahidini kuweka kumbukumbu za kheri ndani ya jamii zetu, kwani ni faida
  yetu ya kule tuendako!

  Salma Khamis/

 7. Sawa wewe ni mzanzibari na yeye na sisi wtanganyika ila kama unapinga sisi kuwa watanganyika mlalamikie Allah ndie aliyetuleta duniani. Ila usitoe kisingizio cha Uislamu sema tu una chuki na watanganyika na una furaha kuona watanganyika wanakufa. Kwani nyinyi wazanzibari hamufanyi mabaya au ni wasafi nyinyi?

  • @Mohammed
   Kaka nilivyomuelewa Ustadh Hamad ni tofauti na ulivoelewa wewe.
   Kweli ukataka uctake maadili machafu Zenji kwa % kubwa yanasababishwa na wakristu Wakitanganyika kwa makusdi ya kusambaratisha tabia za kiislam.Jee wewe ni mkristu ?
   Usikacrike kaka huo ndio ukweli.
   Na hatuwezi kumlalamikia Allah kwa hilo

 8. Hakika asiyesikitika na kifo hiki anaroho ngumu sana kwa sababu kanumba hajaharibu jamii nikifo cha majonzi sana kwa Tanzania nzima yeye alirusha bendera ya wasanii nje ya nchi tukajulikana na sisi Tz tunamovie , tunawasanii wazuri mungu amlaze pema peponi

  • @Monica
   Una ukungu wa macho na unahitaji operation, kuna vifo vikitokea kunakuwa na majonzi lakini kwa mtu alochangia angalau kwa kheri alolifanya/kuwafanyia jamii au mtu binafsi, huyu jamaa hana la maana, kama alipeperusha bendera hilo halikuwa kwa ajili Waislam wa Kizanzibari labda wale wanaoipenda dunia na hawajui wajibu wao wa kuishi hapa duniani kama wewe Monica usie kuwa na mila hata za kabila lenu.

   Ama kuhusu movie hakuna muislam alokamilika kwa maadili akawa na huzuni kwa jamaa huyu alopotosha jamiii na kuacha athari mbaya na chafu kabisa zisizofaa hata kuigwa na binadamu mwenye heshima yake isipokuwa akina nyinyi Monica musio na malezi hata ya utamaduni wa kitanganyika.

   Poleni sana majonzi ya kipuuzi.

  • Jamaa alikuwa na kifaaa cha kasi wacha kimtoe roho!! Sijui alikuwa mkewe au ndio hivyo wa pembeni mmmmmmh……………………..nashindwa kujua !!!!!!!!!!

  • Anaweza kuipata hiyo pepo kama kaitumikia hapa duniani, ikiwa alitwanga kama kawaida yake anavyoonekana basi Mungu atampangia kwa mujibu wa kile alichikitanguliza.

   • we mpumbavu tu unamwombea mwenzako mabaya je wewe hutakufa au tangu umezaliwa unajua umetenda mema mangapi? we sema unaleta ubara na uzenji.

 9. dah @hamad, kuwa mstaarab usitumie maneno ya kejeli laiti mtume angetumia kama njia yako kufikisha ujumbe basi asingempata mtu hata mmoja na kilichobaki ni kuomba husnu hatma kaka bado uko duniani na dunia imezungushiwa matamanio hujiw nawe pengine utateleza (mungu akuepushie), kifo cha kanumba ni somo tosha ukikaa ukitafakari na machozi yanaweza kukubugujika kwamba dunia ni sehemu ya kupita tu

  • @ Duh dada Aziza..
   Kila mtu ataonja mauti kwa muda na wakati alopangiwa, hapo hapana ubishi.
   Lakini kilichonickitisha ni kuwaona baadhi ya waislam kwa mapenzi makubwa waliyonayo kwa jamaa huyu mpaka kufikia hadi kumuombea alazwe peponi, nauliza ??? kwa jema gani alilolifanya ktk uislam…….???
   Jee uislam umeamrisha kumuombea dua mtu alokuwa akiikebehi dini yetu tena kwa mbwembwe na kicheko huku akifikiria anawalani waislam na kutoa filam zenye kuonyesha kuwa uislam ni ushirikina….????
   Jeee bado tukae na kumsikitia badala ya kumshukuru Alllah kwa kuondoka kwake ……???
   Tumuombee dua njema tu kwasababu ya usanii wake na sifa aloipatia Tz….. ???

   Ushauri wangu:
   Tujitahid kufuata mila na desturi za kiislam kwa nguvu zote tuachane na kushabikia mambo ya kipuuuzi kama haya, tuswalini sala 5 na suna zake, tufungeni Ramadhan na funga za suna na kuomba magh-fira kwa wingi angalau mara 300 kwa siku badala ya kukaa kwenye FACEBOOK.
   Omba dua hiii: Yaaa Rabbi tunakuomba utupe mwisho mwema ktk dunia na Aakhera.

   • @hamad
    ushaona kama wamekosea wanamuombea dua basi wakosoe kwa maneno ya busara na ukarimu kwani sisi binaadam ni wepesi wa kusahau au pengine kuna wengine hajui kama kumuombea mtu dua ambae c muislam vibaya lakini usitumie maneno makali kama mnayotumia kwa mfano ukimwambia,” ndugu yangu kumuombea dua mtu aliye kuwa karifi ni vibaya, mtume ametukataza siku nyengine ucfanye hivi” then unaweza kumpa na ushahidi wa haditi au aya uone atakujibu maneno gani lakini sis wenyewe hatujui kumfahamisha mtu, unamwambia mtu kitu kwa jazba unadhani mtu huyo atakujibu vipi.
    insha allah ushauri nimeusoma na nitaufanyia kazi

 10. jamani tusiseme sana ila mungu atamlipa kwa jema ikiwa kalifanya na atalipwa baya ikiwa kalifanya kila kifo kina sababu yake ilikuwa ahadi yake tayari imeshafika

 11. huyu jamaa ameondoka tuangalie mtume (s.a.w) aliusia vipi akiondoka duniani kafir kama huyu tusemeje lakini sisi waislam tutafakari je ujumbe wa allah unawafikia hawa wenzetu maana tutaulizwa tuwanusuru tujinusuru sisi pia huko tunapokwenda kugumu sana ni kweli tukitafakari sisi waislam huyu jamaa ana mashaka kuanzia sasa ,basi sisi tufikishe ujumbe kwa waliobakia ni jukumu la waislam
  kila la kheri

 12. sikufurahishwa na baadhi ya coment unamuombea mwenzio ende motoni wakati wewe hujajijuwa ni wawapi badala ya kumuomba mungu akujaalie mwisho mwema unamuhukumu ande motoni wakati yako hujayajuwa ila tu kwa sababu una jina la kiislam sijaona katika quran hata hadidh za mitume kusema mkiristo akifa muislam afuhahi kwa kweli inasikitisha sana ila nasema mauti tunatembea nayo anyway kila mtu na anavyojisikia ila si mafundisho ya ya mtume mwaacheni m/mungu amuhukumu sio binaadamu

 13. kusema ukweli hakuna asiyekua muislamu akaingia peponi, haya ni kulingana na imani na taratibu za kiislamu, na hilo kila muislamu analifahamu, so, waislamu wakisema alazwe mahali pema peponi sijui wanamanisha nini.

 14. kwanza inasikitisha sana tena sana kuona waislaam eti wana muombea kiumbe kilicho mkataa kipenzi cha mwenyeenzi mungu mtume wetu muhammad (saw)yaani kanumba, hakua muislaam vipi wewe muisllam useme eti m/mungu amlaze mahala pema peponi, wewe ulie muisllam basi kama hukujitahidi kuiacha dunia nakushukhulikia akhera basi pepo utaisikia tu kwenye titabu, sikwa mbii asiekua muislam kwa ushahidi (al imraan aya ya 85) mwenyeenzi mungu anasema( yoyote yule anaefuata au kuamini dini isiokua uislaam basi haikubali dini hio au imani hio na akhera atakua nimwenye kula khasara) kua msanii hakumfanyi apendwe na muuba bali kuamini na kutenda yale alioamrishwa na mola wake ndio yatakayo mfanya aipate hio pepo nasio kuiletea tanzania sifa, hakuletwa duniani kuja kuiletea jamii filamu nzuri au tanzania sifa .Waislamu amkeni musikipende kiumbe mpaka mkajisahau nakusahau maadili yenu.eeeeweeee khiari zenu.

 15. INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJIUN.Kufa ni haki kila mmoja atakufa wakati wake utakapofika,nasikitika sana mwenzetu huyu ameondoka bila ya kutamka shahada.Inshaallah Mungu atu[pe mwisho mwema na yeye amueke mahali panapostahiki……..amin

 16. Kufa tutakufa wote ila nnachotaka kukumbusha ni kwamba waislam tumeambiwa kuwa mtu atafufuliwa na anaempenda/anaowapenda sasa jiulizeni nyinyi mnaempenda, kumsifia kwa wema kanumba mngependa kufufuliwa nae, Allah kasema “hawatakubali mayahudi na manasara hadi mfate mila zao” na hiyo ndo kazi alioifanya huyu jamaa kwa jamii ya Tanzania hasa kwa waislam wakati wa uhai wake, alifundisha watu usaliti, mapenz ya uongo, uzinzi, ulevi na kuwa na w’ke wengi, aliukashif uislam, alifanya uharibif ktk ardhi ya Allah ikiwemo uzinzi na ulev. Je nani kakubali kudata mila zake? Allah amlaze mahala anapostahili. Tumeambiwa “fadhakir, inna dhikra tanfaul-muuminina”

 17. wow! i’m a Kenyan from western Busia county but i’m really shocked with some Tanzanians, kwa kweli hata ikiwa mtu alikuwa mbaya kiasi gani, hauwezi kumwombea mabaya.kwani adinasi yupi aliye na uwezo wa kutuma mwezake motoni? we kaumbwa 2 kama yule, ni kwa hiari yake kusaidia au kujenga msikiti. kwani mwamanisha kuwa waisilamu wote wakijenga msikiti nani ata swali kwa zote.

 18. YESU KRISTO NDIYE YEYE YULE JANA LEO NA HATA MILELE HIVYOO KAMA MTU AKIMPOKEA YEYE HATA HIYO NAFASI YAKUTAMKA MANENO MACHAFU HUTAPATA KWAKUA MFUASI MZURI WA DINI HUWA HATUKANI WALA HAKASHIFU MAREHEMU BALI ANAOMBA REHEMA KWA MUNGU AISHI MAISHI MATAKATIFU ILI AWE NA MWISHO MZURI.

 19. A’ alaykum naongea na waislam tu, dini yetu haijaacha kitu chochote huwezi kumuombea dua mtu yyte aliyekwishakufa na akawa hakutamka shahada Allah amesema uislam ndio dini ya haki na atakaefuata dini nyengine haitakubaliwa mbele ya Allah na watakua na adhabu kali swali kwa waislam wa humu munajua dini ya kanumba? Au hatuijui dini yetu? Tafadhalini tusomeni dini yetu Allah atupe uongofu na amlipe kanumba yale yanayostahiki kwake amin

 20. I’m Burundian.
  Kupitia filamu zake,nilijifunza mengi.
  Tunamuombea MUNGU ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Amina

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s