Tusipoujadili Muungano kwa makini, utavunjika

Makamishna wa tume ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wakisikiliza na kuandika maoni yanayotolewa na baadhi ya wananchi huko mkoa wa kusini Unguja

Tumeshuhudia na kujionea jinsi muungano wa siku nyingi, kati ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini ulivyogubikwa na mitafaruku, ikiwa ni pamoja na hoja tata juu ya uhalali wa Wabunge wa Bunge la Muungano kutoka Ireland ya Kaskazini kupigia kura bungeni mambo yasiyoihusu Ireland Kaskazini. Ni sawa tu na hapa kwetu juu ya uhalali wa Wabunge kutoka Zanzibar kupigia kura mambo yanayohusu Tanzania Bara au Tanganyika. Kuna hoja pia juu ya Wazanzibari kuruhusiwa kumiliki ardhi Tanzania Bara; au Wazanzibari kushika nafasi za uongozi katika Serikali ya Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, wakati Watanzania Bara hawaruhusiwi kugusa mambo hayo Visiwani. Kwa nini tunaendelea kuwa na Wazanzibari na Watanzania Bara, wakati wote hao ni Watanzania ndani ya nchi moja? Je, Zanzibar ni nchi au Taifa kiasi cha kuwa na watu wenye utaifa wa Zanzibar – Wazanzibari; au Watanzania Bara nao wana Taifa lao, Taifa la Watanzania Bara? Continue reading

Maalim awataka wananchi kushiriki sensa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na viongozi wa CUF kwa ngazi ya majimbo na Wilaya nne za Pemba katika ukumbi wa Chuo cha Benjamin Mkapa Wete Pemba.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makaazi, ili kuirahishia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa uhakika. Maalim Seif ametoa wito huo leo katika ukumbi wa chuo cha Benjamin Mkapa Wete Pemba alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwa ngazi za Wilaya na Majimbo. Continue reading

Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa

Professa Issa Shivji akiwa katika moja ya mikutano iliyotayarishwa na kigoda cha Mwalimu Nyerere katika chuo kikuu cha Dar es Salaam

Sikuwahi kusikia mahali popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti “anataka” Muungano uvunjwe, yeye kama yeye. Sasa huyu mwandishi Datus Boniface halipata wapi ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia huyu wa Kitanzania, hata kama ni Mzanzibari pia? Uandishi wa habari wa aina hii ya Datus Boniface ni wa kusikitisha sana. Continue reading

Daghadagha za Ali Ameir na ushujaa wa Hassan Nassor Moyo

Mzee Hassan Nassor Moyo akizungumza na waandishi wa habari akitoa historia yake na Mzee Abeid Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar kabla ya kufanyika kwa muungano wa Zanzibar na Tanganyika

Ahmed Rajab

YEYOTE atayejaribu kuitalii jamii ya Zanzibar ya leo haitomchukua muda kutambua kuwa katika medani yake ya kisiasa kuna kambi mbili kuu. Kambi hizo zinawakilisha ajenda mbili zinazouongoza mjadala mkubwa wa kisiasa unaoendelea Visiwani: ajenda ya Tanganyika na ajenda ya Zanzibar. Hii ndiyo hali halisi ilivyo na kila siku zikisonga mbele inazidi kuwa wazi. Continue reading

Hutuba ya kufunga baraza la wawakilishi

Nchi ya Iran imewekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja wa Mataifa na iwapo itatokea nchi yoyote kuisaidia kukwepa Azimio hilo nchi hiyo nayo itawekewa vikwazo kama hivyo vilivyowekewa Iran. Hivyo, baada ya kugundua ukweli kwamba meli hizo zinapeperusha bendera ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika hatua za kuzifutia usajili meli hizo na pia kuifutia uwakala kampuni ya Philtex. Aidha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafanya uchunguzi zaidi kujua ni vipi usajili huo ulifanyika.  Pamoja na tukio hilo, uhusiano wetu na Iran utaendelezwa katika mambo mengine. Continue reading

Soma Gazeti la ANNUUR kila Ijumaa

Umati uliohudhuria Dua mwezi 17 wa Ramadhani huko Msikiti wa Afraa Kidongo Chekundu Zanzibar

Serikali yakiri kukoroga sensa Yamtukanisha Mufti Zanzibar, Masheikh, Hakuna aliyetoa hoja ya Qur’an, Hadithi

  • Zanzibar wasoma Dua siku ya Badri

 Mawakala mfumokristo Arusha atumia Alshabab

Katika jitihada za kunusuru sensa, Afitini Waislam kwa Usalama Taifa

  • Rais JK atakiwa kuuliza wanaume Kama Karume alivyomkabili Nyerere 1970

Moyo akumbusha ya Nyau, Twalla, Hanga, Afichua uhuni aliofanyiwa Salum Rashid

Ilikuwa wakati nyeti wa kujadili muungano.

  • Nani Moyo na aliyofanya ZNZ kabla ya Mapinduzi

  • Tamko la umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar kuunga mkono utetezi wa wawakilishi kwa maslahi ya nchi ya Zanzibar

  • Waislamu watatumiwa mpaka lini?. Yasiyojulikana Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

  • Mbunge Msigwa kachefua Waislamu. Haya na mengine mengi fungua gazeti lako la ANNUUR

Kwa Kusoma Gazeti lako Tafadhali Bonyeza hapa.ANNUUR 1029

Uhuru wa habari sasa kitanzini

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Omar Yussuf Chunda

Kutokana na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo vya habari ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wasemaji katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo vya habari kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar. Continue reading