Makala

Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa

Wakwanza kuzungumza alikuwa Prof Abdul Sheriff na aliainisha kile alichotaka kibainike kama historia a sababu za kuwepo Muungano katika ya Tanganyika na Zanzibar. Alieleza kile alichotaka kieleweke kama mapungufu ya kisheria katika mchakacho wa kuwepo Muungano. Pia alieleza kile alichotaka kieleweke kama Muungano kukosa kuwa na uhalali wa kisiasa ( political legitimacy) kutokana na ushirikishwaji hafifu wa viongozi wa Serikari ya mapinduzi wa wakati huo na wananchi kwa ujumla. Akahitisha maelezo yake kwa kusema Wazanzibari walio wengi sasa hivi wamefikishwa mahali ambapo wanatamani kutumia mchakato wa kuandika katiba mpya uliozinduliwa hivi karibuni unaoongozwa na Jaji SJoseph Sinde Warioba kujadili Muungano kwa kina na kuingia kwenye maridhiano mapya juu ya kama Muungano uendeleee kuwepo na kama ndiyo kwa mfumo wa serikali ngapi. Ilikuwa wazi kuwa Prof Sheriff alikuwa haamini kuwa walikuwepo Wazanzibari wengi waliokuwa tayari kuendelea na Muungano wa serikali mbili kama wa sasa. Sikuwahi kusikia mahali popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti “anataka” Muungano uvunjwe, yeye kama yeye. Sasa huyu mwandishi Datus Boniface halipata wapi ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia huyu wa Kitanzania, hata kama ni Mzanzibari pia? Uandishi wa habari wa aina hii ya Datus Boniface ni wa kusikitisha sana. Endelea kusoma makala hii

Daghadagha za Ali Ameir na ushujaa wa Hassan Nassor Moyo

YEYOTE atayejaribu kuitalii jamii ya Zanzibar ya leo haitomchukua muda kutambua kuwa katika medani yake ya kisiasa kuna kambi mbili kuu. Kambi hizo zinawakilisha ajenda mbili zinazouongoza mjadala mkubwa wa kisiasa unaoendelea Visiwani: ajenda ya Tanganyika na ajenda ya Zanzibar. Hii ndiyo hali halisi ilivyo na kila siku zikisonga mbele inazidi kuwa wazi. Tulipotanabahi kuwa hii ndiyo hali ilivyo na kuanza kuieleza katika kurasa za jarida hili kuna waliotuona kuwa ni wazushi, maadui, wasaliti na wachochezi. Walitupakaza kila aina ya uovu na kutusingizia mambo ya ajabuajabu. Leo hakuna anayethubutu kukana kwamba hizo kambi mbili kweli zipo na kwamba ile ya ajenda ya Zanzibar ndiyo iliyo kubwa tena kubwa mno.  Wala hakuna anayethubutu kukana kwamba kambi hiyo imewaunganisha wengi wa Wazanzibari bila ya kujali itikadi zao za kisiasa wala za kichama. Endelea kusoma makala hii

Hutuba ya kufunga baraza la wawakilishi

Nchi ya Iran imewekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja wa Mataifa na iwapo itatokea nchi yoyote kuisaidia kukwepa Azimio hilo nchi hiyo nayo itawekewa vikwazo kama hivyo vilivyowekewa Iran. Hivyo, baada ya kugundua ukweli kwamba meli hizo zinapeperusha bendera ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika hatua za kuzifutia usajili meli hizo na pia kuifutia uwakala kampuni ya Philtex. Aidha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafanya uchunguzi zaidi kujua ni vipi usajili huo ulifanyika.  Pamoja na tukio hilo, uhusiano wetu na Iran utaendelezwa katika mambo mengine. Endelea kusoma hutuba hii

Ubakaji wa watoto Zanzibar, tatizo sugu linaloisumbua jamii

KATIKA utafiti wa hivi karibuni wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) imebainika kuwa tatizo la ubakaji limeonekana kuwa sugu visiwani Zanzibar. Wengi waliohojiwa wanasema kuwa ni rahisi kulimaliza iwapo jamii, serikali, na vyombo vya sheria kwa pamoja wataamuwa kulishughulikia kwa dhati. Ofisa Wanawake na Watoto, Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Watoto na Wanawake katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi, Hidaya Mohammed Ramadhani anathibitisha kuwa kesi za kubaka na kulawiti watoto katika wilaya yake zipo, lakini nyingi zinaishia mitaani baada ya maelewano katika familia. “Utafiti unaonyesha kuwa wabakaji wengi ni wanaume wakiwamo wanaoishi katika familia. Wapo babu, baba, kaka, mjomba, binamu, ndugu wa karibu, mwalimu au jirani. Hali hii inafanya kampeni dhidi ya udhalilishaji kuwa ngumu sana kwa sababu watuhumiwa wanakwepa mikono ya sheria kwa kuelewana katika familia,” anasema Hidaya. Endelea kusoma makala hii

Kwa hili, viongozi wa SUK wafuta ujinga

HATA kama wapo wanaojaribu kujenga imani kuwa waziri wa miundombinu na mawasiliano aliyejiuzulu, Hamad Masoud Hamad afaa kushitakiwa, uamuzi aliouchukua ni muafaka. Mjumbe huyu wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Ole, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, hajatenda kosa bali ameonesha uwajibikaji. Yeye kama waziri lazima atangulie kutoka kitini. Ingeshangaza kama angeshikilia pale. Atakaaje huku mamia ya wananchi wametokomea katika matukio mawili ya kuzama meli chini ya mwaka? Asingetenda haki kwa nafsi yake, asingetendea haki wananchi na serikali yao. Tena heko kwa Rais Dk. Ali Mohamed Shein kukubali ombi la Hamad Masoud Hamad la kujiuzulu uwaziri aliomteua tangu alipounda serikali ya umoja wa kitaifa Novemba 2010. Naye rais asingekuwa ametenda haki kwa nafsi yake kama kiongozi wala kwa wananchi na serikali. Angekuwa amejipalia makaa ya moto. Ile ni hatua ya kwanza nzuri. Kuachia wadhifa ambao kiongozi amepewa kuongoza watu pale panapotokea matatizo yaliyosababisha hasara kwa taifa – hata iwe ndogo kiasi gani, ni jambo la lazima katika dhana ya uwajibikaji. Endelea kusoma makala hii

Viongozi wenye kuzuwia maoni ya wengine washitakiwe

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleiman ameishangaa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kushindwa kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanaowatisha wanachama kwa kutoa maoni tofauti na mtazamo wao. Akichangia mada ya sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakar, Waziri Rashid Seif alisema kuna kila sababu ya kukamatwa kwa viongozi hao wa CCM wenye tabia ya kutoa matamshi ya vitisho kwa watu wenye kutaka mabadiliko ya mfumo wa muundo wa Muungano. “Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inakataza mtu au taasisi kumzuia mtu mwengine kutoa maoni yake au kumlazimisha aseme anavyotaka yeye, sasa hawa viongozi wa CCM wanaotaka kuwanyanganya kadi Wawakilishi wao si wanakiuka sheria hii” Alisema Waziri Seif. Endelea kusoma makala hii

Baadhi ya viongozi Zanzibar wana yale yale ya kale

ALEXANDER Pope, mshairi Wakiingereza wa karne ya 18, aliwahi kuandika kuwa “wapumbavu hukimbilia kule malaika wanakohofia kukukanyaga”. Niliyakumbuka matamshi hayo Jumapili wiki hii, baada ya futari hapa kwetu Zanzibar ambako siku hizi hali za hewa — ya kimaumbile na ya kisiasa — ni za kuridhisha.  Watu wanaifunga Ramadhani bila ya kuteswa na joto lililoshtadi. adhalika, utulivu uliopo na mshikamano wa wananchi wa itikadi tofauti za kisiasa unazidi kuashiria matumaini mema kuhusu mustakbali wa Visiwa hivi. Hali ya hewa imepoa na hali ya kisiasa pia kama wasemavyo vijana siku hizi ‘iko poa.’ Nilipokuwa nikiyakumbuka hayo aliyoyaandika mshairi Pope nilikuwa nikitafakari kuhusu njama za wanasiasa duniani kote wenye kujaribu kujijenga ili wajipatie ulwa. Siku mbili hizi tumewashuhudia wanasiasa aina hiyo wakiibuka hapa Zanzibar. Wanasiasa wa sampuli hiyo huwa hawajali wanapita wapi ili wafike waendako. Hata ikiwa njia inayowakabili imejaa makaa ya moto wao watakhiyari wayakanyage hayo makaa ya moto. Wanasiasa wana sababu zao zinazowafanya wautapie ulwa hata ikiwa nyayo zao zitateketea.  Wengi wao wanauona ulwa kuwa ni njia ya mkato wanayoweza kuitumia kufikia malengo mengi na kujipatia mengi. Endelea kusoma makala hii

CCM jambo la kuambiwa ongeza na lako

Katiba ya nchi sio mali ya Chama cha siasa, ingawaje baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar vyama vingi vya siasa vilifutwa na kutangazwa kuwepo kwa vyama viwili tu yaani ASP kwa Zanzibar na TANU kwa Tanganyika, hivyo kufanya katiba kuwa mali ya vyama hivyo. Ilivyokuwa katiba katika Taifa lolote la kidemokrasia, lenye kuheshimu misingi ya utu ni mali ya wananchi na hivyo ni wananchi pekee ndiyo wenye haki ya kubadili katiba ya taifa lao. Aidha, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya Watanzania wote na kamwe si ya chama tawala cha CCM, makada wake au makamanda wa vita vya ufisadi, hivyo si haki suala la mabadiliko ya katiba ya nchi yakafanywa ni maagizo elekezi ya kufuatwa na wananchi na zaidi wanachama wa CCM. Kwa sasa CCM haina uhalali sio tu wa kuhodhi katiba ya nchi bali hata kutoa agizo kwa umma kwamba wafuate mtazamo wake katika kutoa maoni juu ya katiba mpya. Natambua kuwepo kwa msimamo wa CCM kuhusu wanachama wake kuwataka wakatoe maoni katika Tume ya Jaji Warioba wasema wanataka Serikali mbili!. Endelea kusoma makala hii

CCM maslahi na vitisho vya Chui wa karatasi

Wiki hii kuna kituko cha aina yake kimetokea ndani ya Chama cha Mapinduzi upande wa Zanzibar kwa wanachama wachache wa Chama hicho Wilaya ya Mjini kuasi dhidi ya mamlaka halali ya CCM. Ni kisa,. Kituko kinachoweza kuvunja mbavu pale baadhi ya Wana CCM walipotoa tamko la kuwatuma viongozi wao wa Wilaya kuwataka Makamu Mwemyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar,Amani Abeid Karume kunyanganywa kadi kwa madai wamekwenda kinyume na msimamo wa CCM juu ya Muungano. Viongozi wale waliobariki uasi ndani ya CCM nawawafanisha na aliyekuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa African National Congress(ANC) Julius Malema. Katika mkutano huo ambao mbali ya kutaka Makamu Mwenyekiti wao Karume afukuzwe CCM,lakini pia walitaka wanachama wengine kama Mweka Hazina wa Chama hicho Zanzibar,Mansoor Yussuf Himid nae kunyanganywa kadi!. Endelea kusoma makala haya

Maruhani wa Kale katika zama mpya

Nami katika safu hii leo naungana na watu wote katika kutoa mkono wa pole kwa maafa yaliyotokea kufuatia kuzama kwa meli ya Mv. Skagit wiki iliyopita, “Inna lillahi wa inna ilayhi rajioon”. Baada ya salaam hizo za rambirambi, narejea katika mada yangu ya leo ambayo inayoanza kwa kuuliza swali kwamba mzimu wa Watanzania uko wapi? Ilivyokuwa kila shetani na mbuyu wake. Mbuyu wa shetani wa muundo wa Muungano anayeinyemelea Tanzania uko wapi? Uko kwa wanaotaka mabadiliko ya muundo kuwa na Muungano wa mkataba au uko kwa muundo wa kale wa Serikali mbili chini ya muundo wa kikatiba?. Iwe itakavyokuwa kwa mtazamo wangu na wa vijana wengi ni kuona mabadiliko ya muundo wa Muungano ikiwa kuna mtu au kundi linajidanganya kwa kujipamba kwa mauwa wanaoweza kumshika masikio na kumtuliza shetani wa mabadiliko wa muundo wa Muungano wamechelewa maana ni sawa na kufunga banda wakati Farasi keshatoka! Wakati huu ambapo mjadala wa kutaka mabadiliko katika muundo wa Muungano ukishika kasi,umejengwa uongo mtakatifu kwa baadhi ya watu kwamba kuna watu wana dhamira ya kurudisha Usultani na Utumwa. Endelea kusoma makala hii

 

Polisi wanapochafua amani watu walindwe na nani?

KUNA simulizi mbili zenye kukinzana kuhusu vurugu zilizozuka Zanzibar Ijumaa iliyopita ya Julai 20. Siku hiyo kuanzia saa za alasiri hadi kupindukia saa sita za usiku eneo kubwa la mjini Unguja lilikuwa kama eneo la msitu uliowaka moto. Ghasia zilienea takriban mji mzima kuanzia Mbuyuni, Darajani, Michenzani, Kwa Bi Ziredi, Daraja Bovu, Mombasa, Mpendae, Amani na sehemu nyingine. Waliokuwa wakisema kwamba Zanzibar ikiwaka moto hawakukosea. Matairi yalichomwa moto barabarani na watu waliokuwa wamepigwa mabomu ya kutoa machozi na kurushiwa maji ya kuwafanya wawashwe na kikosi cha askari wa kuzuia fujo. Waathirika hao wakaweka matofali na mawe barabarani wakizifanya barabara zisipitike. Simulizi rasmi ya serikali ni kwamba viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) ndio walichochea vurumai hizo. Viongozi wa Uamsho nao, kwa upande wao, wanasema kwamba walichokuwa wakifanya ni kuwaombea dua maiti na waathirika wengine wa ajali ya meli ya MV Skagit iliyozama Jumatano iliyopita. Wakati wakisoma dua zao katika Msikiti wa Mbuyuni askari wa kuzuia fujo wakaingia katika eneo la msikiti na kuanza kupiga mabomu ya kutoa machozi na ya maji ya kuwasha. Jumiki, au kwa ufupi Uamsho, ni jumuiya na si madhehebu (sect) kama gazeti moja la Kiingereza nchini lilivyoeleza. Endelea kusoma makala hii

Mvuvi atamba wakiwezeshwa wataokoa abiria

MVUVI mzoefu anayeishi kijiji cha Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja anaamini shughuli za uokoaji baharini zinaweza kufanywa kwa ufanisi mkubwa pakiwepo maandalizi mazuri. Zahor Tamali, ambaye amekuwa katika maisha ya baharini kwa miaka 20, anashauri serikali ianzishe mfuko maalum wa dharura wa fedha za kutumika wakati ajali. Katika mahojiano maalum na MwanaHALISI juzi, Tamali amesema anaona inafaa shughuli za uokoaji zikawekwa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi. Ana sababu.“Unajua idara hii inawajua wavuvi wote. Inashughulikia kamati za wavuvi Unguja na Pemba na inatoa elimu ya uvuvi endelevu. “Serikali itumie hazina ya mkurugenzi wa uvuvi, anajua wavuvi na viongozi wao, na anawasaidia sana . Kila wakati yuko nasi.“Huyu amekuwa bega kwa bega kuelekeza na kukagua shughuli zetu. Hasubiri ripoti ofisini huyu. Anakwenda mwenyewe mpaka chini ya bahari pima kumi akipiga mbizi bila hofu.“Anajua hasa oganaizesheni ya baharini. Anazijua hifadhi zote Zanzibar. Ni rahisi kuwaongoza wavuvi kwa shughuli za kuokoa watu panapotokea chombo kuzama,” anasema. Endelea kusoma makala hii

Yanayohitaji kuzingatiwa kwenye katiba

Kutokana na masharti hayo ya Katiba ni wazi kuwa Sheria zote za Mambo yote ya Muungano ambayo yameorodheshwa katika Jadweli la Kwanza (Mambo 37), Sheria zake zinapitishwa kwa utaratibu wa wingi wa kura. Kwa mfano, Sheria ya Uhamiaji, Sheria ya Uraia, Sheria ya Kuanzishwa kwa TRA, Sheria za kodi na Sheria zote za Muungano zinapitishwa Bungeni kwa wingi wa kura tu. Kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya Wabunge wa Zanzibar na Tanzania Bara, ni wazi kuwa Sheria za Mambo yote ya Muungano zinaamuliwa na upande mmoja tu wa Muungano. Endelea kusoma taarifa hii

Kuasi kisiasa ni haki ya kidemokrasia

MWAKA 1958 utakumbukwa katika historia ya ukombozi wa Afrika kwa mkutano wa All-African People’s Conference uliofanywa mjini Accra, Ghana, chini ya uenyekiti wa Kwame Nkrumah, mwanadharia wa Umajumui wa Kiafrika (Pan-Africanism). Mkutano huo ulikuwa na umuhimu zaidi kwa vile ndio uliomtoa ukumbi Patrice Lumumba na kumfanya aanze kujulikana nje ya mipaka ya nchi yake ya Congo. Wakati huo Lumumba alikuwa amekwishakuanza kupata umaarufu nchini mwake kwa harakati zake za kuupinga ukoloni Wakibelgiji lakini kimataifa, na hasa katika nchi zilizokuwa zikitawaliwa na Uingereza, alikuwa hajulikani. Endelea kusoma habari hii

Wakati ndio unaosema na kuamua

Nyota njema huonekana alfajiri, ukiona alfajiri imeingia upeo wa macho yako huoni nyota ni kiwingi kitupu kimetanda kaa ukijuwa kuwa mambo kwako sio mazuri kajipange upya kimkakati. Kinyume na matarajio ya walio wengi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanza kazi kwa wananchi wengi kujitokeza kutoa maoni yao kwa amani, utulivu na ustaarabu mkubwa kwa upande wa Zanzibar. Nimebahatika kwenda katika mikutano kadhaa ya Tume hiyo, watu ni watulivu na kwa hili lazima niwapongeze wananchi kwa uugwana wao maana siku zote muungwana ni vitendo. Jambo moja ambalo nimejifunza wakazi wa vijijini wamekuwa na uelewa mkubwa wa mambo, pengine kuwashinda hata wale walioko maeneo ya mijini, wanajenga hoja katika maoni yao na kutoa mifano hai. Wakati huu wananchi wakiwajibika kwenye Tume kutoa maoni yao,hatutegemei kuzuka watu au kikundi cha watu kikawa kinaifuata Tume kila inapokwenda, hii sio sahihi, wewe kama ni mkazi wa Fujoni subiri zamu ya eneo lako itafika, ikiwa eneo lako Tume imeshapita umetoa maoni hakuna kuwabughudhi wengine. Endelea kusoma habari hii

Chunga unaposikia CCM inalia rafu

LEO nimeguswa na mambo mawili – malalamiko ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kinahujumiwa katika utoaji wa maoni ya Katiba mpya ya Jamhuri, na kauli ya SMZ kuhusu vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi. Mawazoni mwangu, suala la vitambulisho ndio nilikusudia litawale mada wiki hii. Malalamiko ya CCM yaliibuka katikati na ni vema nikayashughulikia kabla ya kupoa. Kwa umuhimu wake, nitaanza na malalamiko haya. Nikitumia uzoefu wa utendaji katika siasa za Zanzibar , nina kila sababu ya kusema ukiona chama hiki kinalalamika hadharani kuhujumiwa, ujue kimezidiwa kete. Wakati mwingine unaposikia kelele za viongozi wake, hwenda ni dalili za mkakati wake chenyewe kugonga mwamba. Hebu sikiliza anachosema Katibu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Zainab Khamis Shomari: “Kuna jina la Said Mwema limejitokeza katika barua na baada ya barua hizo, Tume ilitaka kumjua huyo mtu mwenye jina hilo la Said Mwema lakini matokeo yake hakuna aliyejitokeza. Endelea kusoma habari hii

Viongozi Zanzibar wawe na ujasiri wa haki kuiita haki

WA KALE walisema: “Kila upepo una tanga lake.” Na upepo tulio nao leo ni upepo wa kidemokrasia.  Alhamdulillahi, leo  Watanzania wanaishi katika mazingira ya kidemokrasia ingawa demokrasia  yenyewe ni changa na ina mapungufu kadha wa kadha. Hata hivyo, Wazanzibari na wenzao wa Bara wanaweza kujifaragua kidogo kwa vile wana uhuru wa kukusanyika na wa kusema, wana uhuru wa kutoa maoni yao bila ya hofu ya kuingiliwa na vyombo vya dola.Sisemi kwamba hivyo vyombo vya dola havijaribu kuuingilia uhuru huo; vinajaribu lakini vinashindwa kwa sababu ya haya mazingira ya kidemokrasi yaliyopo.  Hii leo Tanzania haina tena mfumo wa kuwa na chama kimoja kilichojipa uhalali wa kuwa chama pekee cha kisiasa na chenye kiongozi mwenye mamlaka na uwezo unaomfanya awe na amri juu ya mzingo mzima wa kisiasa nchini.Katika enzi zilizopita kiongozi aina hiyo kwa kutumia njia za halali au za dhulma, alikuwa na tabia ya kulitaka Taifa zima lifuate amri zake, wananchi waitikie ‘amin’ kwa kila alichokisema.  Bila ya shaka kiongozi wa sampuli hiyo hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo peke yake.  Akifanya hivyo kwa kushirikiana na vibaraka wake pamoja na taasisi za usalama ambazo zilikuwa na kazi ya kuwaziba mdomo wananchi na kuwafanya wasithubutu kutamka hata ‘kwi’ dhidi ya matendo yake kiongozi. Endelea kusoma habari hii

Dk. Shein, lugha ya upole haitoshi?

KAULI aliyoitoa Dk. Ali Mohamed Shein kuhusu Muungano haimsumbui mtu yeyote; si Unguja wa Pemba – Zanzibar. Anaposema Muungano hautavunjika, hakuna anayemsumbua. Anaposema yeye ndiye rais, hivyo hakuna atakayeuvunja Muungano, hakuna anayesumbuka.Rais anaalikwa kufungua mkutano wa jumuiya ya wastaafu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema atautetea Muungano; na hakuna atakayemlaghai wala kumchezea katika uongozi wake. Waliomnukuu, wanasema Dk. Shein amesema yeye kama rais, hatomuogopa mtu wala kusita kuchukulia hatua wale watakaokwenda kinyume na matakwa ya katiba.Hili moja ni dhahiri – Dk. Ali Mohamed Shein ndiye rais Zanzibar , na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyorekebishwa mwaka 2010; inamuongezea wadhifa wa mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Katika maelezo ya Dk. Shein kwa wastaafu, kuna maneno yanasumbua kidogo labda tu kama umma utaambiwa kuna mtu amehoji mamlaka ya rais.Anaposema “sitomuogopa mtu yeyote” wengine wanauliza kwani kuna mtu anamtisha rais? Anayemtisha rais anastahili kuchukuliwa hatua haraka ya kushitakiwa. Kwa mantiki ya sheria, kumtisha rais ni kutishia mamlaka ya wananchi waliompa dhamana ya kuongoza nchi yao. Endelea kusoma makala hii

Madai ya Wawakilishi ni kilio cha samaki?

Si katika Baraza la Wawakilishi wala nje ya Baraza,katika viunga vya Zanzibar hakuna jambo linalozungumzwa katika kila pemba ya viunga hivyo ni Muungano, Muungano,kama atatembelea mgeni hii leo ataweza kujiuliza Muungano ni kitu gani,nyumba,mtu,shamba au nini hasa?Kwa kila makadirio ya Wizara yatakapowasilishwa, Wawakilishi wa wananchi hawakusita kutoa maoni yao kuhusu kero za Muungano, wiki iliyomalizika tulishuhudia mjadala mkali ukijitokeza ndani ya Baraza hilo kwa wajumbe kuelezea hisia zao na bila shaka za wananchi katika majimbo wanaoyoyaongoza.Lakini mbali ya Wawakilishi hao, watu wengine katika majukwaa yaliyorasmi na yasiyo rasmi wameendelea kzungumzia suala zima la Muungano na mustakabali wake watakiitazama zaidi ujio la Katiba mpya ya Tanzania.Yamejitokeza makundi karibu matatu makubwa, kundi la kwanza ni la wale wanaotaka kubakia na mfumo wa muundo wa Muungano wa sasa kama ulivyo,lakini ukifanyiwa marekebisho kidogo, kundi la pili wanataka Serikali tatu,lakini kundi la tatu linawakilisha kizazi kipya wenye fikra mpya kwamba umefika wakati mfumo wa muundo wa Muungano wetu uwe wa mkataba wenye Serikali mbili zenye Mamlaka kamili. Endelea kusoma makala hii

Hutuba ya Rais Kikwete ya Mei 2012

Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari.Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini Ndugu Wananchi;Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012. Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi. Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma. Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa. Endelea kusoma taarifa hii

Taarifa usajili wa meli za nje

Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi. Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi wake. Endelea kusoma taarifa hii

Polisi inawataka nini Wazanzibari?

KAMA wapo Watanzania waliobisha ushiriki kamili wa Jeshi la Polisi katika kufanya uhalifu dhidi ya binadamu Zanzibar , kwa matukio ya 26-27 Mei, basi watafakari matukio mapya ya 17 Juni. Katika matukio yale, askari wa polisi walipewa silaha na kusukumiza risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi. Wakashambulia ofisi za mawakili, gari za wananchi na nyumba za viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI). Endelea kusoma makala hii

Nani na nani wenye akaunti za siri nje na kwa nini?

MIONGONI mwa marafiki ambao sitoweza kuwatupa ni mwanasheria Enrico Monfrini. Huyu si mwanasheria mahiri tu lakini pia ni mwindaji. Kazi yake ni kuzisaka fedha zilizoibwa hasa na watawala wa kidikteta na zilizowekwa kwenye akaunti za siri nje ya nchi zao.Nilianza kujuana na Monfrini mwaka 1999 alipoajiriwa na serikali ya Nigeria kuzisaka na kuzifichua fedha ambazo Jenerali Sani Abacha alikuwa amezihaulisha na kuzificha katika mabenki ya nchi za nje. Nilijulishwa naye na rafiki yangu mmoja mkubwa wa huko Nigeria ambaye ndiye aliyekutana na Monfrini usiku wa manane mjini Geneva na kumbembeleza aisaidie Nigeria kuisaka ‘ngawira’ ya Abacha. Endelea kusoma makala hii

Sote tupige vita madawa ya kulevya

Tukiwa katika harakati za maadhimisho haya wengi wetu kwa njia moja au nyengine tumeguswa na athari za matokeo ya matumizi ya dawa za kulevya , tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya nchini linadhihirishwa na ongezeko la vijana waliojitumbukuzi katika matumizi hayo ambao wamekuwa wakifika katika vituo mbali mbali na kuhitaji huduma. Matumizi ya dawa za kwa njia ya kujidunga sindani imekuwa ni tishio na chanzo cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na maradhi mengine mbali mbali yanayopatika kwa njia ya damu ( blood borne infections). Hali hii imepekela vijana wengi nchini wanaotumia dawa za kulevya kuambukwiza ugonjwa wa UKIMWI. Utafiti uliofanywa mwaka 2005 hapa Zanzibar ulionyesha hali ya kutisha ya maambukizi hayo iliyofikia asilimia ishirini na nane ( 28%) kwa wanaojidungu na kubadilishana sindano. Endelea kusoma taarifa hii

Uamsho hai, Dola kandamizi na Muungano

SASA tunalo tatizo sugu na la msingi Zanzibar – utawala mbaya. Chembechembe za utawala wa aina hii zinapoachwa na kukua, matokeo yake ni kupandikiza chuki kati ya dola na wananchi. Pale utawala na wananchi wanapochukiana, watategana, wataviziana, watatunishiana misuli. Kila upande utataka kujithibitisha ulivyo na nguvu. Ni kawaida kwa dola kuwa na nguvu nyingi. Hizi huchangiwa na ile asili ya dola kuwa ni chombo cha mabavu; lakini pia kwa sababu utawala utataka kuthibitishia wananchi kuwa chombo hicho kweli ni cha mabavu. Endelea kusoma makala hii

Tofauti ya Muungano wa Katiba na wa Mkataba

ULE mjadala mkubwa — na mkali— unaovuma na kuchaga Visiwani Zanzibar kuhusu mustakbali wa Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar umefichua jambo moja lenye kuwagusa na kuwaunganisha Wazanzibari wengi.  Nalo ni dai la kutaka pafanywe mageuzi ya kimsingi katika mahusiano baina ya hizo nchi mbili zilizo katika Muungano wa Tanzania.Wanapoulizwa kwa nini wanasisitiza mahusiano hayo yageuzwe wanatoa kila aina ya sababu.  Baadhi yao wanazieleza sababu hizo kwa makini wakizijenga juu ya misingi ya hoja za kimantiki.  Wengine  wanajibu kwa jazba.Shutuma wanazozitoa ni nzito.  Kuna wanaosema kuwa miaka 48 ya Muungano haikuinufaisha kitu Zanzibar.  Kuna wanaosema kuwa Muungano umeifanya Zanzibar itoweke kwenye ramani ya dunia.  Kuna wasemao kuwa Muungano umeifanya Zanzibar idhurike kisiasa, kiuchumi na kijamii ikilinganishwa na visiwa vingine kama vile Mauritius na Seychelles. Endelea kusoma makala hii

Tutashiriki mchakato wa katiba – Uamsho

Kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa hapo juu na baada ya mashauriano na viongozi tofauti katika jamii, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu ndiyo imetoa uwamuzi wa kuwataka waumini na wazanzibari wote kushiriki katika kutoa maoni lakini sambamba na uwamuzi huo. Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, unapenda utoe tanbihi na tahadhari ya hali ya juu kwa tume na kuitaka ifanye kazi yake kwa uadilifu. Kwani uongozi pamoja na wazanzibari wengi kutokana na udanganyifu wa tume zote zilizotangulia za uchaguzi, bado wasi wasi mkubwa umetanda pamoja na imani ya kuwa haki haitotendeka. Vile vile tunawasiwasi mkubwa wa mamlaka za nchi kupitia watu wachache wenye lengo la kufanikisha maslahi yao binafsi, wataingilia utendaji wa tume na shughuli zake kiutendaji kwa kuiburuza katika malengo binafsi na kwa hilo hapa sisi viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu tunatamka wazi kwamba hazitonyamaza kwa udanganyifu na dhulma yoyote itakayofanyika na haitamstahamiliya wala kumuonea haya kiongozi yoyote kwa dhulma hiyo. Endelea kusoma habari hii

Uzinduzi wa Zakka Zanzibar

Napenda kutoa wito kwa kila mmoja wetu kuitumia fursa ya kutoa zaka na kuuchangia Mfuko wa Zaka ili kutekeleza wajibu wetu kwa Mola wetu na kuzingatia manufaa mengine yaliyokwishaelezwa. Vigezo vya namna ambayo mfuko kama huu unaweza kuwa nyenzo muhimu ya kuinua maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi yanaonekana katika mataifa mbali mbali duniani zikiwemo Sudan, Afrika Kusini, Uturuki na nchi nyingi nyenginezo. Wahenga walisema: “Matukio ya mwenzako ni mafunzo kwako”. Kwa hivyo, tuna fursa ya kutumia mbinu bora zinazowasaidia wenzetu kama ni mafunzo mema kwa upande wetu. Endelea kusoma habari hii

Uamsho walalamikia jeshi la polisi

Wananchi wa Donge wanasema wamechoshwa na ubaguzi na udikteta wa Shamhuna na wanaitaka serikali ya umoja wa kitaifa kupitia baraza la wawakilishi imuhoji Mh. Shamhuna kwani tuhuma zote zinamlenga yeye, kisha baraza litoe ufafanuzi wa wazi kabisa, ni kwa sheria gani wananchi wa Donge wananyimwa fursa ya kufaidi uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni pamoja na uhuru wa kuchanganyika na ndugu zao wazanzibari? vile vile haki ya kutumia TV na DVD zao mitaani uhuru ambao unaingiliwa na masheha kwa kuwazuia watu kutizama watakacho na kufikia hadi kuwatisha kuwapeleka Polisi na hata kuwanyang’anya mali hizo jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati inafahamika kuwa haki zote hizo zinalindwa na katiba ya Zanizbar kwenye ibara zifuatazo 17, 18, 19 na 20. Endelea kusoma taarifa hii

Waasisi wa Muungano na madai ya Kizazi kipya

Inaeleweka na kila mtu mwenye akili timamu na mwenye busara kwamba Muungano ni jambo la maana na lenye faida, haitazamiwi katika hali ya kawaida kutamani kuvunja Muungano, ingawa yawezekana baadhi ya watu kufikiri hivyo, lakini yafaa kufahamu kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Taifa la Marekani leo limepata nguvu na uwezo si kwa sababu ya watu wake bali ni kwa sababu ya umoja wao. Nasi katika Tanzania tunahitaji kuwa na umoja na nguvu kama zile za Mataifa makubwa pamoja na umbali na tofauti ya uchumi na maendeleo,lakini ipo siku tutakuwa kama wao. Ndoto hii inaweza kutimia ikiwa tutaweka misingi madhubuti katika kuandika katiba mpya na kubadili mfumo wa muundo wa Muungano kwa kuwa na aina inayozungumzwa na wengi inayoonekana kukubali Muungano wa mkataba.Bila shaka tutatofautiana katika mawazo,lakini naamini utofauti huo hautaweza kuviza uhuru wa maoni hasa ikitiliwa maanani kuwa Katiba zote mbili zimelinda haki hizo kama zilivyolindwa na mikataba ya kimataifa. Endelea kusoma habari hii

Dhana ya ‘utalii kwa wote’ yazinduliwa

 Naamini kwa dhati kabisa kwamba tukishirikiana kwa pamoja, tukizitekeleza sera na mipango yetu tuliyonayo na kwa kuzingatia sheria ya utalii iliyopo, tunaweza kuendeleza Utalii huku tukilinda desturi na mila zetu. Kama nilivyosema awali, Watalii ni watiifu wa sheria. Nchi ya Italy imekuwa ikivutia watalii kwa kutumia historia ya mji wa Vatican. Watalii kutoka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu kila mwaka wanafika sehemu hii yenye historia kubwa. Katika matembezi ya sehemu hii muhimu haizingatiwi dini ya mtu, ila kinachosisitizwa ni ufuataji wa sheria na kuheshimu desturi ya sehemu hii muhimu kwa wafuasi wa Dini ya Kikirsto hasa wa madhehebu ya Kikatoliki. Jambo muhimu la kujifunza hapa ni kwamba watalii wanaheshimu misingi ya dini za wengine na ndio maana wanapenda kutembelea majengo ya kihistoria. Hapa Zanzibar tunayo majengo ya fahari ya kihistoria ya dini na majengo ya kale, ambayo yanaweza kuchangia katika kukuza utalii. Ni juu ya viongozi wa dini na jamii kutoa ushauri na maelekezo yanayofaa juu suala hili. Endelea kusoma hutuba hii

Wazanzibari wacheza ngoma wasioijua – vyama vya siasa

Kupitia mkutano huu tunawaomba sana Wananchi wa Zanzibar, Unguja na Pemba na wale wanaoishi nje ya Visiwa hivi kuwa makini sana na kundi hili. Tunawatanabahisha akinamama wasikubali kutumiwa namna hiyo kwani hatua hiyo inaweza kuwaletea maafa. Dalili zinaonesha kuwa viongozi hao wako tayari kusababisha maafa na kuwatupia lawama watu wengine mradi tu waweze kufikia malengo yao. Ninawasihi sana wasicheze ngoma wasiyoijua. Sehemu nyengine duniani, vikundi kama hivi vimesababisha matokeo mabaya sana na kusababisha maafa makubwa. Kwa mfano Alkayda, Bokoharam kule Nigeria, na Al-Shabab kule Somalia. Hali za nchi zenye makundi haya zinasababisha kuondoka kwa hali ya usalama na amani. Endelea kusoma taarifa hii

Hatutawasaliti wazanzibari- Maalim Seif

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi wametokana na Wazanzibari wenyewe. Viongozi hao ni Wazanzibari kindaki ndaki, wenye kujawa na kiwango kikubwa cha uzalendo. Wanaipenda Zanzibar kama Mzanzibari mwengine yoyote yule.Viongozi wapo kulinda maslahi ya Zanzibar na watu wake, kama vile viongozi wa Tanganyika walipo kulinda maslahi ya wananchi wenzao wa Tanganyika. Kwamwe viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hawata wasaliti wananchi wa Zanzibar. Tutaheshimu na kutetea maoni yenu wananchi kama mlivyo yatoa kwa Tume ya Jaji Warioba. Muhimu jitokezeni kwa wingi mtoe maoni yenu. Endelea kusoma hutuba hii

Hutuba ya Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar


Haitoshi kuona idadi kubwa ya semina za utoaji wa elimu ya haki za binadamu lakini tungelipenda kuona matunda au matokeo ya semina hizo katika jamii. Swali kuu likiwa – Je! jamii yetu inabadilika au tunaendelea na ule mtindo wa “mambo ni kama kawaida” – business as usual. Kwa mfano: Wazazi waliotalikiana wanaendelea kutoa malezi bora kwa watoto wao, kuwatunza vizuri na kuwapatia huduma zote muhimu ikiwemo elimu afya na upendo? Na wazee wasiojiweza wanahudumiwa? Uhuru wa kutoa maoni na kuabudu unaheshimiwa?. Endelea kusoma hutuba hii 

Nyerere na fitina za Upemba na Uunguja

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya kuyatathmini maisha yake. Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka aliyowahi kuyasema Mwenyekiti Mao wa China kumhusu Josef Stalin, mtawala wa pili wa Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin. Nami nikayatumia maneno hayohayo kuanzia makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was “a great leader who made great mistakes,” as one ruler once famously said of another.(“Julius Nyerere alikuwa “kiongozi mkubwa (adhimu) aliyefanya makosa makubwa,” chambilecho mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo mtawala mwenzake.) Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake. Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki sifa. Endelea kusoma makala hii

Union and Constitutional Review in Tanzania

Constitution – making is normally supposed to be a purely civilian exercise through which citizens are expected to effectively exercise and make use of their fundamental democratic right to self determination. Participation in the process is the right of every citizen. The main actors in constitution – making are the people themselves. The whole process will be futile and just a sham if it is monopolized or hijacked by any person or a group of persons. Government, political parties, civil societies and private individuals have their roles to play in the process of constitutional review. During the debates for constitutional making or review, differences of opinions may become obvious but they should be settled by a democratic method of discussion, criticism, persuasion and education, and not by method of coercion or repression. Continue

Ewe muumba, waangamize wafitini Zbar

NINAHOFU kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejipanga. Naona imefikwa; imo katika tihani, tena mgumu. Uongozi wa juu na matawi yake – wizara, idara zinazojitegemea na mashirika yake – lazima wafikiri upya namna nzuri ya kuwatumikia wananchi.Imewasilisha bajeti yake Baraza la Wawakilishi. Sawa, hili ni moja ya mahitaji muhimu ya kikatiba ambayo serikali inatakiwa kuyatekeleza.Tatizo ni kwamba akili za wananchi hazipo kabisa huko. Kwa kiwango kikubwa, wananchi wanaotakiwa kufuatilia mjadala wa bajeti mpya, akili zao zipo kwengine.Kila ninavyopima, nabaini kwa kipindi chote hiki, wamezielekeza kwenye Muungano na ndio suala linalowasumbua zaidi kwa sasa.Wazanzibari wanataka kujua hatima ya nchi yao. Wanataka kujua kwani wakitoa maoni itakapokuja Tume ya Mabadiliko ya Katiba, watanufaika kwa lipi. Wanajiuliza ni nini hasa maana ya wao kutakiwa kutoa maoni yao kwa tume hii? Wala si uongo kwamba Muungano ndio suala linalochukua nafasi kubwa zaidi katika akili za wananchi wa Unguja na Pemba. Si bajeti ya serikali kamwe. Endelea kusoma makala hii

Serikali kuongeza kodi maeneo manane

Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza mbele ya Baraza lako tukufu kwa mwaka wa fedha 2012/13 kukusanya jumla ya shilingi bilioni mia sita na arobaini na nane na mia tisa na arobaini na nne milioni (TZS 648,944 milioni) pamoja na matumizi ya shilingi bilioni mia tatu na saba na mia saba tisini na saba milioni (307,797 milioni) kwa kazi za kawaida na shilingi bilioni mia tatu na arobaini na moja na mia moja na arobaini na saba milioni (341,147milioni) kwa kazi za maendeleo. Endelea kusoma makala hii

Kuvunja makanisa si kuvunja Muungano

UKILALA unaamka. Kama huamki na bado una uhai basi unaamshwa. Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiko) ya huko Zanzibar inasema kwamba imejitweka jukumu la kuwaamsha Wazanzibari kuhusu mengi — ya dini na dunia. Miongoni mwa hayo ni Muungano wa Tanzania ulioziunganisha nchi za Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili mwaka 1964. Kwa ufupi, Jumuiya ya Uamsho inaupinga Muungano. Hamna shaka yoyote kwamba kwa hilo ina wafuasi wengi sana Visiwani.Jumuiya hiyo imekuwa ikiandaa mihadhara ya kuwapa elimu ya kiraia waumini wa dini ya Kiislamu kuhusu masuala ya katiba likiwamo suala la Muungano na uhalali wake.Tukumbuke kwamba wanao uhuru wa kufanya hivyo na wakati huohuo tusiyasahau maneno ambayo Mwalimu Julius Nyerere alimwambia mwandishi Colin Legum wa gazeti la Obsever la Uingereza mwaka 1965 kwamba hatowapiga mabomu Wazanzibari wamridhie endapo watakataa kuendelea na Muungano.Endelea kusoma makala hii

Muungano wa Speed and Standard

Sasa kumepambazuka,mapabazuko mapya yanatarajiwa kutokeza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sio jambo jengine ni lile linalozungumzwa kila siku la wananchi kutaka kuwepo kwa Muungano wenye kumaliza malalamiko ya miaka mingi. Watu hawataki kusema kweli, sijui wanaogopa kitu gani,lakini hakuna anayeweza kusimama mbele ya umma akisema kwamba wanaodai kuwepo kwa mabadiliko katika muundo wa Muungano ni watu wachache,ikiwa anaamini hivyo, anatakuwa anajidanganya nafsi yake. aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Wilson Churchill aliweza kubashiri mabadiliko katika mataifa ya Afrika ambayo yalikuwa yakitawaliwa na wakoloni, waingereza wenzake hawakuamini kama ambavyo aliyekuwa Gavana kule Rhodesia ya Kusini (sasa Zimbabwe) Ian Smith. Wakati ndio unaofanya watu kuwasukuma kwenye maamuzi, sio jambo jengine kwani mwaka 1970 au miaka ya mwishoni mwa 1980s mijadala ya Muungano haikuwa na nguvu kama hivi leo.Endelea kusoma makala hii

Muungano huu unahitaji dawa mseto

Upepo mbaya ulivuma sio ule wa kimbunga, hapana huu ulikuwa ni upepo uliotaka kuyumbisha chombo chetu ili kienda mrama,lakini tumevuka salama katika mtihani tulioupata wa vurugu zilizotokea. Madai ya Wazanzibari ni madai ya miaka mingi tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano huu umeelzwa katika tafiti nyingi za wasomi na wasiokuwa wasomi kwamba muundo wake ndio wenye matatizo.Kuwepo kwa fursa ya kutoa maoni katika Tume ya katiba ni jambo muhimu hasa kwa Wazanzibari ambao walikuwa na dukuduku la siku nyingi wakilalamika bila kusikilizwa maana wasilikizaji ndio wale wale wanaolalamiwa.Wananchi walio wengi wamejizatiti kwenda kwa wingi wakati Tume itakapoanza kukusanya maoni, lakini kuna jambo ambalo linazungumzwa sana katika maeneo ya Unguja na Pemba kuhusu Zanzibar kupiga kura ya maoni kwanza kabla ya kuingia katika utoaji wa maoni ya katiba mpya. Endelea kusoma makala hii

Mpanga ubaya mwisho humrudia

KUNA uhalifu umefanywa Zanzibar. Ni katika matukio mabaya yaliyoanza usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Watu wamechochewa kupambana na dola. Hili halijaelezwa na serikali. Polisi wamevamia nyumba za viongozi wa Uamsho na kuvunja milango huku wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi na familia zao sambamba na kuwatishia maisha. Polisi hawajalieleza hili. Amir (kiongozi) wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), Sheikh Farid Ahmed Hadi anasema usiku wa Jumamosi hiyo, akiwa kwake, alipata taarifa anafuatwa na polisi wa kuzuia fujo (FFU).Akajiandaa. Mnamo saa 7.30 kweli wakafika. Wakataka mlango ufunguliwe. Hakuna aliyewatii. Wakarusha risasi hewani. Hakuna aliyetoka. Hakuna aliyepiga kelele kutokea ndani. Lakini, baada ya kuona vishindo vimezidi, Sheikh Farid akasema kwa sauti, “Nipo ndani na familia yangu tumepumzika. Kama mpo tayari, fanyeni chochote nje ila, ninaapa kwa jina la Allah, anayekuja ndani, tutakabiliana mimi sina bunduki.” Endelea kusoma makala hii

Nilisema, nikasihi, serikali haikusikiliza

HALI mbaya ya usalama iliyoanza Jumamosi usiku, imesadifu nilichokieleza wiki mbili zilizopita. Nilimsihi Rais Dk. Ali Mohamed Shein, kupitia safu hii, kuwa asikubali maneno ya fitna anayolishwa na wasaidizi wake. Nikasema akikubali fitna, atajishawishi kukasirika; na matokeo ya mtu kukasirika, ni kuchukua hatua yenye madhara makubwa.Ilikuwa katika makala iliyojadili uhuru wa watu kusema na kujadili mambo ya nchi yao – ilitoka na kichwa cha habari kisemacho, “Hasira zako Dk. Shein, ni hasara kwako.”Kweli, hasira zilizowajaa viongozi wa serikali na vyombo vyao, zimezaa hasara. Sasa nchi, iliyokuwa imetulia kabisa, watu wakienda na kurudi kwenye shughuli za kutafuta maisha, imerudi kwenye hofu kubwa.Rais hakuongoza vizuri au walioelekezwa kuongoza hawakutenda vizuri. Hapa, hapakutumika hekima na busara kwa kiwango. Hapa, kuna hali ya serikali kutoonyesha uvumilivu kwa raia.Kwa kuwa Rais Dk. Shein ndiye kiongozi mkuu Zanzibar, analazimika kubeba lawama kwa madhara yaliyotokea. Yeye atatafuta wengine wa kuchangia lawama hizo.Kosa kubwa lililofanywa katika kadhia hii, ni uongozi kuruhusu Jeshi la Polisi kukamata kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mussa Juma.Hapana. Kumkamata mtu si kosa, ila mazingira yaliyotumika. Ya Sheikh Mussa yalikuwa ya kigaidi na kijambazi. Yaliwashtua walioshuhudia. Wakajenga chuki dhidi ya serikali.Hebu nitangulize hali ilivyokuwa Jumapili kabla ya kurudi kueleza kilichotokea Jumamosi usiku. Endelea kusoma makala hii

Dk Shein akiongea Ikulu

Kama tunavyoelewa kwamba Zanzibar ina watu wa makabila na dini tofauti. Wazee wetu wa asili walisema “Zanzibar ni njema atakaye na aje”. Ustaarabu huu ulianza kutumika tangu ulipoanza kuingia Uislamu na kuendelea hadi kufika wageni kutoka Uajemi (washirazi), Ureno na Oman walioanzisha utawala wao katika karne mbali mbali hadi ya 18. Uislamu uliingia Zanzibar mara tu baada ya kuwepo katika nchi ya Saudi Arabia. Kadhalika, Ukristo uliingia Afrika Mashariki alipofika Mvumbuzi wa Kireno, Vasco da Gama mwaka 1498 na hatimae kuja Wamishionari wa kwanza wakiongozwa na Ludwig Krapf mwaka 1844. Mfalme wa wakati huo wa Zanzibar aliwaruhusu kujenga Kanisa la Anglikana la Church Missionary Society (CMS) liliopo Mkunazini. Krapf baadae aliruhusiwa kujenga mishionary Mombasa. Madhehebu mengine ya kikristo yaliingia Zanzibar katikati ya karne ya Kumi na Tisa na kuenea sehemu za bara kutokea hapa Zanzibar, na kanisa la pili kubwa la Minara Miwili lilijengwa katika eneo la Shangani Mjini Zanzibar. Endelea kusoma taarifa hii

Zanzibar ingekuwa nyingine wangepatanishwa Abeid Karume na Ali Muhsin

 HALI za maisha Zanzibar ni ngumu. Watu wanaishi lakini wengi wao wanaishi maisha ya taabu. Imekuwa kana kwamba Wazanzibari wa leo ni mahuluki taabu. Asilimia kubwa ya vijana hawana ajira, wenye ajira wanalipwa mishahara ya chini kabisa kulinganishwa na wanavyolipwa wafanya kazi wenzao katika nchi jirani za Afrika ya Mashariki. Wazanzibari wanayapata maji kwa taabu. Umeme vivyo hivyo. Ukija upande wa huduma nyingine zinazotolewa na Serikali ya Zanzibar mambo ni hayohayo. Matatizo huzidi kuzuka pale serikali inapolazimika kutumia fedha nyingi isizoweza kuzimudu. Serikali hulazimika kufanya hivyo ama kutokana na shinikizo za kisiasa au uendeshaji na usimamizi mbovu wa wakuu wa idara. Kati ya matatizo ya Zanzibar ni kwamba serikalini hakuna udhibiti wa kutosha wa madeni ya serikali na dhamana au rahani za madeni hayo. Wizara ya Fedha ina mfumo maalumu wa matumizi ya kipindi cha wastani. Lengo la mfumo huo ni kuhakikisha kwamba fedha zinagawanywa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa vipaumbele vya kitaifa na vya sekta maalumu. Hadi sasa lakini utaratibu huo haufanyi kazi sawasawa. Bado masuala ya matumizi ya fedha za serikali yanapangwa kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja na hakuna mahusiano baina ya makadirio ya matumizi ya mwaka mmoja na viwango vya juu vya bajeti vya mwaka unaofuatia. Endelea kusoma makala hii

Hata tuyazime, maswali yale yale kuhusu Muungano yanaturejea

HUKO nyuma nimeeleza kwamba haiwezekani kuijadili Tanzania pasipo kuujadili Muungano, na kwamba dalili za makundi ya watu kuhoji Muungano wetu kama ulivyo leo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. Fursa tuliyo nayo hivi sasa ya kujadili na kuandika katiba mpya ni fursa adhimu tunayoipata kuujadili Muungano kwa kina na kuupatia ufumbuzi utakaotupeleka masafa marefu kidogo. Ye yote anayetaka kujua jinsi masuala ya Muungano yalivyotusumbua katika historia yetu ya takriban nusu karne atakumbuka mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na tume na kamati mbalimbali zilizoundwa katika jitihada za kujaribu kurekebisha baadhi ya masuala yaliyoonekana kukera makundi ndani ya nchi, na jinsi ambavyo jitihada hizo zote na kamati na tume hizo hazikufanikiwa kuondoa malalamiko kuhusu Muungano. Sasa itakuwa ni jambo la ajabu iwapo, wakati tunasema tunataka kuandika katiba mpya, tutajinyima wasaa wa kuujadili Muungano kwa kuwauliza wananchi wa pande mbili (Tanganyika na Zanzibar) ni nini wanachotaka, iwapo wanataka Muungano au hawautaki. Swali hilo la msingi likiiisha kupatikana, na jibu likawa kwamba wanautaka Muungano, ndipo sasa itawezekana kuangalia kwa undani ni mambo gani ndani ya mfumo na taratibu za Muungano yafanyiwe marekebisho ili kuyaweka sawa na kukidhi matarajio ya pande mbili zilizoungana. Binafsi nakataa dhana ya kuwaambia watu kwamba kuujadili Muungano ni sharti tujadili namna ya kuuboresha. Mtu huboresha jambo analotaka kuendelea nalo, na kama hataki kundelea nalo ni upuuzi kuanza kuliboresha. Haina maana hata kidogo. Na si kweli kwamba hatujasikia sauti za watu wanosema kwamba hawautaki Muungano, na wala pia si kweli kwamba hawana haki ya kuwa na mawazo kama hayo. Endelea kusoma makala hii

Bajeti ya pili SUK na changamoto mtawalia

RAFIKI zangu, wakiwemo wasomaji wa safu hii wamenijia juu. Wananisema. Wanadai namsakama Dk. Ali Mohamed Shein bila ya kuangalia mazonge yanayomsibu. Mmoja anasema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ana hali ngumu. Kwamba kama ni mshambuliaji hodari katika timu ya mchezo wowote ule, inasihi kusema amebanwa kulia, kushoto, mbele, nyuma na katikati pia.Kwa lugha rahisi kueleweka, wanasema Rais Dk. Shein hafurukuti. Wanataja mambo mawili kuwa ndiyo yanayomsumbua akili kwa sasa.Kwanza, shinikizo kutoka kwa Baraza la Wawakilishi likitaka awatie adabu mawaziri na watendaji wa serikali ambao wameguswa na tuhuma za ufisadi.Pili, wanasema Rais anasongwa na harakati za asasi za kiraia chini ya mwamvuli wa UAMSHO, zinazohamasisha wananchi kuukataa muungano. Shinikizo ni kubwa. Uamsho wamesambaza fomu maalum wanazohimiza Wazanzibari wazijaze kuibana serikali iitishe kura ya maoni itakayoamua wabaki nao au waondokane nao. Wakati hayo wanayaita mambo magumu kwa sasa kuyatafakari na kujua hatima yake, inajulikana bado Rais Dk. Shein hajatoa majibu ya matatizo kemkem yanayokabili serikali katika kutimiza ahadi zake kwa wananchi. Endelea kusoma makala hii

Ngonjera za CCM na upepo wa mabadiliko

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Pius Msekwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Ujerumani wiki iliyopita aliweka bayana msimamo wa Chama chake kubakia na sera ya Serikali mbili katika Muungano. Katika mahojiano na DW Msekwa alisisitiza na kuwakumbusha wanachama wa CCM wakati watakapotoa maoni mbele ya Tume ya Katiba kukumbuka sera ya Chama hicho katika Muungano ni kubakia na Serikali mbili. Ama kweli Msekwa ameachwa nyuma katika wakati mpya, anaonekana wazi kuwa anashindwa kubaini hisia za Wazanzibari na hata zile za wanachama wake ndani ya CCM kwamba wamechoka na sera zisizowaletea manufaa. Muundo wa Serikali mbili umeelezwa na watu wengi kwamba ndio kiini cha matatizo mengi ya Muungano,lakini mtu kama Msekwa ambaye ameshiriki kuandika katiba ya mwaka 1977 angeweza kutoa ushauri ambao unaendana na mazingira ya sasa. Wazanzibari wengi hawautaki Muungano wa kikatiba, wanapendelea kuwepo na muundo mpya wa Muungano usio wa Serikali mbili wenye manufaa kwao. Sera ya Serikali mbili ni sawa na nyumba kongwe na nguo iliyochakaa, lakini kwenye macho ya CCM bado inaonekana mpya, fikra za watu wengi walitegemea kikao cha NEC kingekuja na mkakati wa ujenzi wa nyumba mpya iwe na haiba mpya na yenye mvuto hata kwa wapiti njia wakatamani nao kuwa na nyumba ya aina hiyo au ramani yake. Endelea kusoma makala hii

Hasira zako Dk. Shein, ni hasara kwako


RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ni dhahiri amepandwa na hasira. Naona tayari “watu wake” wamemlisha fitna. Inawezekana kweli amechukizwa kubaini kundi kubwa la wananchi wa Zanzibar limepata hamasa ya namna ya kuja kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Katiba ya Tanzania au kuikwepa wasiione. Wapambe watakuwa wamempa taarifa sizo. Na desturi inaonyesha mtu alopewa taarifa za uongo na kuziamini kwa kuwa waliompa ni “watu wake” anaowaamini, hujenga hasira. Sasa rais amepandwa na hasira. Nimethibitisha kwa matamshi yake alipokuwa kwenye hafla ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) – katika kijiji cha Koani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Wakati nilipokuwa naandaa makala hii, pembeni yangu alikuwepo jamaa yangu mmoja kutoka Fuoni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, aliyekuja kunisalimia ofisini, akanihoji, “Mbona unasema hafla ya chama chake wakati taarifa nilizosoma zimeonyesha rais alikuwa katika ziara ya kiserikali akizuru mikoa yote ya Zanzibar na alianzia kisiwani Pemba.” Sasa niseme sina hakika ziara yake ni ya kiserikali au ya kichama. Sikupata mtu wake ili kuthibitisha jambo hili. Angalau katika moja ya picha nilizoziona kupitia vituo vya televisheni vya Dar es Salaam, nimeona wanaokuwa chini yake ni wakuu wa mikoa zaidi ya ilivyo wenyeviti wa CCM wa mikoa anamopita.Lakini hiyo si mada leo. Akili yangu imenielekeza katika kile ninachokiona kama matokeo ya watu wa Dk. Shein kumpotosha rais, na sasa kukuta tunaye rais aliyejaa hasira rohoni.Tatizo la hasira, ni kwamba mtu mzima anapokasirika hata watoto watagunduwa haraka atakapojitokeza kwao. Wananchi wa Unguja na Pemba, tayari wanajua “baba yao” – Rais Dk. Shein – amekasirika. Sikiliza anachokisema Dk. Shein: “Naelewa fika kuna watu wanaoleta mambo ya ajabu ajabu lengo lao likiwa ni kuvuruga amani tuliyonayo.” “… lakini nasema tena, maana nimeshasema hakuna mwenye ubavu wa kuivunja amani ya Zanzibar na kama mtu kachoka na amani iliyopo, ahame hapa hapamfai; atafute sehemu nyingine akaishi.”. Endelea kusoma makala hii

Hatuwezi kuijadili Tanzania bila kuujadili Muungano

KATIKA muktadha wa mjadala kuhusu kuandika katiba mpya, nimekuwa nikisema kwamba yapo masuala ya kikatiba ya aina mbili: aina ya kwanza ni yale ambayo, hata kama yanaumua hisia kali miongoni mwa wanasiasa, bado yanaweza kupata ufumbuzi wake ndani ya muda mfupi.Aina ya pili ni ile ya masuala ambayo, hata kama hayaibui hisia kali miongoni mwa wanasiasa na watawala, lakini yana umuhimu mkubwa, ufumbuzi wake hauwezi kupatikana kirahisi au katika muda mfupi. Aina ya kwanza, kama naruhusiwa kukariri yale niliyokwisha kuyasema, ni ile inayohusu matatizo ya kiutawala na yanayogusa mgawanyo wa madaraka katika ngazi mbalimbali za utawala.Kuna mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mitatu ya dola (Utawala, Bunge na Mahakama); ukomo wa madaraka ya ofisi za watawala; ukomo wa madaraka ya Bunge; ukomo wa mamlaka ya Mahakama; maingiliano kati ya mihimili hiyo, na kadhalika.Katika kuyaandikia vipengele vya kikatiba, masuala ya aina hii yatapatiwa majibu kwa kufuata utashi wa kisiasa wa wale walio madarakani pamoja na raia wenzao wenye ujuzi wa mambo na ari ya kuchangia katika maendeleo ya taifa lao. Endelea kusoma makala hii

Vigogo wa CCM hamkani wakijipanga kutosana…


VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanajikaza kisabuni lakini ukiyachambua matamshi yao ya karibuni utaona wazi kwamba wamekwishakuanza kuingiwa na hofu za aina kwa aina. Hofu yao moja ni ya kudhoofika kwa chama chao. Nyingine na pengine iliyo kubwa ni ya maadui — wa kweli na wa kujidhania.Kile ambacho labda hawakijui ni kwamba maadui wakubwa wa CCM wamo ndani ya CCM yenyewe.Chama hicho, kilicho kikubwa kuliko vyote vinavyotawala katika eneo zima la Afrika ya Mashariki, hii leo kinakabiliwa na kitisho kikubwa cha kung’olewa kwenye madaraka. Kila siku zinavyoukaribia uchaguzi mkuu ujao ndipo kitisho hicho kinavyozidi kufukuta ndani ya chama chenyewe.Hofu nyingine inayowakumba viongozi wa CCM inatokana na ufisadi wa baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho au serikali yake. Inaeleweka kwa nini viongozi hao wazidi kuwa na hofu hiyo. Sababu ni kwamba wanatambua ya kuwa katika enzi hizi za leo za uwazi hawawezi tena kuwafumba macho wananchi au kuwalaghai.Juu ya kuwa mfumo wa kidemokrasia haujashamiri vilivyo katika jamii, viongozi hao wanajua kuwa hawana nguvu za kisheria za kuzizima kelele na hasira za wananchi. Na sheria pia inaifunga mikono yao wasiweze kutumia mabavu dhidi ya wananchi na kuwakandamiza.Sababu kubwa inayoifanya serikali ya CCM ikabiliwe na hizo ghadhabu za wananchi ni kushindwa kwake kuwachukulia hatua za haraka na zinazostahiki viongozi kadhaa wa zamani na wa sasa wanaoshtumiwa kwa maasi kadha wa kadha ya ama ufisadi, utumizi mbovu wa madaraka, ubadhirifu wa fedha za umma au uzembe kazini.
Kuna visa mbalimbali vya ufisadi vilivyoibuka rasmi hivi karibuni ingawa vimekuwa midomoni mwa watu kwa muda. Hivyo, visa hivyo si vigeni kwa wananchi na kashfa za ufisadi zimekuwa zikiwaandama viongozi kwa muda mrefu. Ushahidi umejaa tele wenye kuonyesha kwamba viongozi wamezoea kuyatumia madaraka yao kwa kujinufaisha binafsi kinyume cha sheria. Walio waadilifu. Endelea kusoma makala hii

 

Kwa Muungano huu mabadiliko ni lazima

Wakati tukielekea katika mchakato muhimu wa kutoa maoni yetu juu ya uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania, ni wazi kuwa jambo litalokuwa na mjadala mkubwa , hasa kwa upande wa Zanzibar , ni suala la Muungano. Hii ni kutokana na sababu kuu tatu.Kwanza , kwa vile Wazanzibari kama ilivyo kwa Watanzania Bara, hawajahi kupata fursa ya kuutolea maoni na ridhaa Muungano huu kwa ujumla wake, muundo wake na uendeshaji wake – na kwa vile umedumu hivyo ukielekea kutimiza nusu karne, hii ni fursa muhimu ya kuufanyia tathmini yakinifu kwa kuzingatia wakati mpya tulionao , mahitaji tuliyonayo na mazingira ya kisiasa na kiuchumi yanayotuzunguka wakati huu. Pili ni kutokana na ukweli kuwa Wazanzibari , kwa mujibu wa muundo wa Muungano huu wao wana mfumo wao kamili unaoongoza mambo yao yote yasio ya Muungano – wana Katiba yao, Serikali yao , Mahkama zao, Bunge lao (Baraza la Wawakilishi). Endelea kusoma makala hii

Watawala na haki ya maoni Zanzibar

Ujio wa mchakato wa katiba mpya na katazo la baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar kuzuia mikutano ya hadhara ya wananchi na Asasi zisizokuwa za kiserikali kuzungumzia suala zima la mchakato wa katiba ni mwendelezo wa kubana uhuru wa kujieleza. Tumewasikia Wakuu wa Mikoa ya Pemba,Dadi Faki Dadi wa Kaskazini na yule wa Kusini, Juma Kassim Tindwa wakiweka masharti magumu na urasimu usiokuwa wa lazima eti kama Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam(JUMIKI) mikutano yake haifai. Wakuu hao wa Mikoa wamekataza kabisa kufanyika kwa mikutano ya aina yoyote katika Mikoa yao. Sababu zao hazikubaliki hata kidogo kwani ukiacha haki ya asili ya watu kukusanyika,lakini Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatoa haki kwa wananchi kukusanyika na kutoa mawazo yao kupitia katika makongamano,mihadhara,semina na siku hizi wengine wameamua kutoa mawazo kupitia mitandao ya kijamii. Kabla ya wakuu hao wa Mikoa, SMZ kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohammed Abad Mohammed ilitoa tamko la kuelekeza iwapo kuna vikundi au Asas iza kiraia zinazotaka kufanya mikutano,makongamano kuhusu mchakato wa katiba mpya sharti wawasiliana na Tume ya Katiba kupata Kibali. Endelea kusoma makala hii

Viongozi hawalindi muungano, bali maslahi yao

WAKATI tuliopo, hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuzuia watu kusema. Ni muhimu na haki kwa binadamu kusema anavyojisikia. Zama za “serikali” kuchagulia watu cha kusema zimekwisha. Katika hali yoyote ile, na hata kama Rais Jakaya Kikwete amesema Watanzania wasijadili kuwepo au kutokuwepo kwa muungano, hakuna kinachosimamisha wananchi kuujadili muungano na hatima yake. Kwa sababu hiyo, kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mohamed Aboud Mohamed kwamba wanaotaka kuelimisha umma kuhusu maoni ya katiba mpya, waombe Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ni kutisha watu. Hata kama waziri na serikali nzima watasema kauli hiyo imetolewa kwa nia njema, kwa desturi ya viongozi wa Zanzibar, unaposikia kauli kama hiyo basi huwa imelenga kuminya haki.Desturi kama hii imezoeleka sana.Viongozi hujifanya wanajua kila kitu na kujitia wao ndio wanaona mbele zaidi ya wananchi wanaowaongoza. Ninaitazama desturi hii kama ishara ya viongozi kujipendekeza kwa Serikali ya Muungano, na hasahasa kwa chama chao – Chama Cha Mapinduzi (CCM). Endelea kusoma makala hii

Kukusanyika ni haki yetu- Uamsho

Kwa maana hiyo Jumuiya baada ya kushauriana na wanasheria itachukua hatua zote za kisheria za kumfikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mahakamani kwa uvunjifu huu wa amani na ukiukwaji wa katiba unaofanywa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzibar na wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma. Inaonesha kuwa kuna ajenda ya siri iliyokabidhiwa kikundi hicho cha watu wachache kilichoanza na Mh. Balozi Seif Ali Iddi ikafuatiwa na Mh. Mohammed Aboud (waziri katika ofisi yake) pamoja na kumuamuru Mh. Fadhil Suleiman Soraga na kumburuza katika uvunjifu huu wa amani. Sasa wameanza kujitokeza wakuu wa Mikoa kwa ajenda ya wazi kabisa ya kuvunja katiba ya Zanzibar na kuhatarisha neema ya amani iliyopo nchini. Endelea kusoma taarifa hii

Mwaka 1 sasa, Dk. Shein arudi kutafakari

NILIJUA tangu siku ile Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar, amekosea. Aliposema kuwa serikali haipaswi kuhojiwa kwa kuuza au kukodisha mali yake, hakika niliamini alijikwaa. Nikajua itafika siku atalazimika kufikiria upya kauli yake hiyo aliyoitoa kwa sauti ya kutisha huku mbele yake akizongwa na kamera na vinasa sauti. Dk. Shein, mtaalamu bingwa wa tiba ya binadamu, alikuwa ndio kwanza ametua Uwanja wa Ndege wa Zanzibar akitoka ziarani nchini Uturuki.Kauli yake hiyo ilitokana na swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi wa habari wa serikali kuhusu wananchi kuhoji hatua ya serikali  kuuza majengo ya kihistoria yaliyopo eneo la Mji Mkongwe.Serikali haifanyi makosa, serikali ina uamuzi wake hasa kwa kuuza mali zake na hakuna anayeweza kuihoji. Ikiamua kuuza jengo itauza tu. Mambo Msiige ni jengo la serikali hatujauza mali ya mtu.“… Wengine wanasema hatujatangaza tenda kuuza majengo haya, kwani lazima kutangaza tenda? mbona hayo mengine tuliyoyauza hatukutangaza tenda.Anaongeza kusema ni khiyari yetu… kama kuna wananchi wanaopinga uamuzi huu wa serikali, serikali ninayoiongoza haiwezi kuwazuia kwenda katika vyombo vya sheria maana huko ndiko kwenye haki kwa yeyote anayehisi imevunjwa. Lakaini nawahakikishia tutawashinda.”. Endelea kusoma makala hii

Shivji na mapambano ya wanyonge

USTADHI Issa Shivji ni mtu mwenye sifa nyingi. Ni mwalimu, mwanasheria anayeheshimika duniani na mwanaharakati. Lakini kwa maoni yangu zaidi na hata unyenyekevu wake sifa yake iliyozipiku zote hizo ni ile ya kwamba yeye ni msomi wa umma. Tena ni msomi wa umma anayejiamini. Katika taifa kama la Tanzania lililojaa wachochole, kaumu ya watu walio hohehahe, sifa hiyo inampa Shivji dhima kubwa katika jamii. Ni dhamana anayoibeba bila ya kuchoka, bila ya kunung’unika na bila ya woga kwani kila siku kazi yake ni kuwaelimisha na kuwatetea walio wanyonge. Anapokuwa anawaelimisha anakuwa papohapo ‘anawawezesha’ yaani anawapa nguvu au uwezo wa kutumia hoja za kuwawezesha kuuondosha unyonge wao. Katika sahafu au safu hii nimeamua kukizungumza kitabu chake kilichozinduliwa hivi majuzi wakati wa Tamasha la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere lililofanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kitabu chenyewe — Insha za Mapambano ya Wanyonge — ni mkusanyiko wa makala mbalimbali za Shivji. Takriban insha zote hizo zimekwishachapishwa kwenye majarida na magazeti mbalimbali. Endelea kusoma makala hii

 

Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI

Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibari tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani. Endelea kusoma hutuba hii 

Serikali yasema mihadhara na makongamano sasa basi

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza kuwa Tume ya marekebisho ya Katiba iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imezinduliwa rasmi leo na Mawaziri husika na kuanzia sasa itaanza kazi yake rasmi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Akitoa taarifa rasmi ya Serikali Ofisini kwake Vuga mbele ya waandishi wa habari, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed amesema katika kufanya kazi zake Tume inaongozwa na hadidu rejea mahasusi ambazo madhumuni yake ni kupata maoni ya kuwa na Katiba muafaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amesema maoni yatayotolewa nje ya hadidu rejea yanaweza kusikilizwa na Tume lakini inaouwezo wa kuyakataa, hivyo ni vyema wananchi wazingatie sana msingi huo. Endelea kusoma habari hii

Muungano usio na ridhaa hauna maana- Tawfiq

Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.Kifungu cha 2A nacho kimetowa mamlaka kwa Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo. Pia viko vifungu vyengine vinavyoonesha dhahir kujibu kejeli ya kaka zetu wakubwa kwamba Zanzibar ni mkoa tu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunafahamu jinsi mara kadhaa wanasiasa wa Tanzania Bara na hata Mahkama ya juu kabisa ya Tanzania (Mahkama ya Rufaa) walivyosisitiza kwamba Zanzibar si Nchi. Kwa maana hiyo hata ukifanya njama ya kutaka kumuondoa Rais wa Zanzibar madarakani kwa mtutu wa bunduki, hiyo haitokuwa uhaini (treason). Ni sawa sawa na kujaribu kuiondosha Halmashauri ya Mji wa Chake Chake, si jambo la kushtua!Mimi naamini kabisa kitendo cha Baraza la Wawakilishi kupitisha Marekebisho hayo kimekuja katika wakati muwafaka kabisa. Unapokuwa na mwenzako ambae hafahamu lugha unayozungumza inabidi utafute lugha pekee atakayoifahamu. Kubadilisha Katiba imekuwa lugha muwafaka kuwafanya wenzetu waone nini tunataka. Marekebisho ya Katiba yameibua lawama tele kutoka kwa wanasiasa na hata miongoni mwa wanasheria mahiri wa Tanzania Bara. Wengine wamesema Muungano wa Tanzania haupo tena pale Zanzibar ilipojitangaza kuwa ni Nchi! Mie naziona hizi zote ni kelele za mlango tu. Kwa upande mwengine naamini Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 pamoja na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) ndiko kulikopelekea kaka zetu wakubwa kuleta kiini macho cha Tume ya Katiba. Kama kweli lengo la Tume ni kushughulikia kero za Muungano na kuufanya Muungano wetu kuwa madhubuti basi hilo lilipaswa kufanywa zamani sana, pale kelele za Wazanzibari na hata za makundi kama G 55 ya Tanzania Bara yalipoibuka kudai Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar. Badala yake hali ya kisiasa ikawachwa kuwa tete. Waliokosoa Muungano wakaitwa wasaliti wasioitakia mema Tanzania. Kuunda Tume ya Katiba sasa hivi ni sawa na kujaribu kuyazuia maji ya bahari yasifike ufukweni wakati wa bamvua!. Endelea kusoma hutuba hii

 

Karume alidhani amesaini Shirikisho la Afrika Mashariki

WAKATI Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ukitimiza miaka 48 mwaka huu, kumekuwa na harakati nyingi visiwani Zanzibar za kutaka uhuru mpya wa visiwa hivyo na kuupinga Muungano wazi wazi. Watu wamekuwa wakijadiliana kupitia kwenye makongamano, mabarazani na hata kwenda mahakamani kutafuta uhalali wa Muungano. Kupitia njia hizo Wazanzibari wametoa sababu mbalimbali za kupinga Muungano. Katika kongamano la uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania na suala la muungano kwa Zanzibar, hali ya kutokubalika kwa Muungano ilijionyesha wazi wazi. Akitoa mada katika kongamano hilo, Profesa Abdul Sharif anasema kuwa ikiangalia historia ya Muungano imejaa kasoro zinazoondoa kabisa uhalali wake. Anasema suala la Muungano lilikuwapo barani Afrika kabla hata ya nchi zake kupata uhuru ambapo zilitaka Muungano wa Shirikisho.Nchi za Afrika Mashariki zilikubaliana kwamba, zikipata uhuru zitaanzisha Muungano wa Shirikisho (East African Federation). Hata Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kwamba, yuko tayari kuahirisha uhuru wa Tanganyika mpaka nchi zote za Afrika Mashariki zitakapopata uhuru kwa pamoja ili kuunda ‘federation’, ” anasema Profesa Sharif na kuongeza;.Endelea kusoma makala hii

Utawala ng’ang’anizi na Muungano tata

MUUNGANO wa Tanzania , zao lililopatikana baada ya kuunganishwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika , unazidi kutikiswa. Ukiwa umeasisiwa tarehe 26 Aprili, 1964, hivyo leo 25 Aprili, kuwa siku ya mkesha wa maadhimisho yake ya miaka 48, Wazanzibari wanauombea dua “mbaya.” Ni katika mkusanyiko ulioandaliwa na Jumuiya ya Uamsho, moja ya jumuiya za kiraia zilizo mstari wa mbele kuelimisha raia kuhusu haki zao, ambapo wataongoza sala na dua maalum kwenye uwanja wa wazi. Waandaaji wanasema dua zilizotajwa zaidi ni dua ya kuombea Zanzibar izidi kuwa nchi ya amani, leo na siku za usoni; na irudi katika kuwa dola inayojitegemea. Muungano umekuwa katika mjadala mpana Zanzibar tangu pale Rais Jakaya Kikwete alipotangaza nia ya kuanzisha utaratibu wa kupatikana kwa katiba mpya ya kwanza itakayoshirikisha maoni ya Watanzania. Endelea kusoma makala hii

Viongozi msiogope kutoa maoni yenu katika katiba mpya

Mara nyingi shuwari ya meleji inashangaza wavuvi na wasafiri wengi wa baharini,ukimya na uvumaji utafautiana sana na pepo nyengine,aghalab kipindi cha mwezi wa Juni ndio kipindi cha upepo huu. Mnasaba wa hilo unakaribiana na kuanza kazi kwa Tume ya Katiba ya Tanzania ambayo yenyewe inaanza mwezi Mei ikiwa shuwari imeingia katika upwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wajumbe wa Tume wameshakula kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete,kama ni safari basi tayari Nahodha wa chombo ameshaanza kukiondoa gatini.Kama inavyoeleweka Katiba ya nchi ni mali ya umma,sio ya kikundi,Chama cha siasa,Asasi za Kiraia,Dini au Kiongozi,hivyo inakubalika kwamba Taifa lolote lenye kufuata demokrasia,katiba inasalia kuwa ni mali ya wananchi na hivyo ni wananchi pekee ndiyo wenye haki ya kubadili katiba ya Taifa lao kama ilivyo sasa hapa Tanzania.Kwa msingi huo,katiba ya Tanzania ni mali ya Watanzania na si vyenginevyo,hatutaraji kujitokeza kikundi cha watu kuhodhi Mamlaka ya umma kwa niaba yao. Endelea kusoma makala hii

Serikali yavuliwa nguo

Kamati imebaini kwamba, Mikataba yote ya mauziano iliyofungwa baina ya Serikali na Ndg. Juma Ali Kidawa na baina yake na Ndg. Amina Aman Abeid Karume ni batili na ya udanganyifu. Aidha, Hati ya Matumizi ya Ardhi aliyopewa Ndg. Amina Aman Abeid Karume na Mhe. Mansour Yussuf Himid, kama tulivyoitolea ufafanuzi wake katika ukurasa wa 182-183, imekiuka taratibu za kisheria na kiutawala.Mhe. Spika: Pia tumegundua kuwa: Mzee Juma Ali Kidawa sio Mmiliki halali kisheria wa Nyumba. iliyokuwa imefuatiliwa na wala hakuhusika na Uuzaji wa Nyumba hiyo kwa mtu yoyote na hakuwahi kufuatilia Utengenezaji wa Warka wa Nyumba hiyo.Mhe. Spika:Hata hivyo, kwa mujibu wa nia njema na mazingira halisi yalivyojitokeza yanaonesha Mzee Juma Ali Kidawa alihusika na kufanya kazi kwa Mhindi aliyeimiliki nyumba hiyo kabla ya kutaifishwa na Serikali.Mhe. Spika:Kamati imejiridhisha kwamba:Ndg. Ramadhan Abdalla Songa na Mama Fatma Karume walishiriki katika Udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano uliofungwa baina ya Serikali (Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati) na Ndg. Juma Ali Kidawa. Mhe. Spika:Maelezo haya yanafafanuliwa katika ukurasa wa 178 hadi wa 180 wa ripoti yetu.Mhe. Spika: Mbali na taarifa hizo, lakini pia Kamati imebaini kwamba:Ndg. Mwalimu Ali Mwalimu kama Katibu Mkuu, amechangia kufanyika kwa udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano baina ya Wizara yake na Ndg. Juma Ali Kidawa. Endelea kusoma ripoti hii

Serikali yatoa tamko kuhusu eneo la bahari kuu

Usimamizi wa masuala ya madai ya Onezeko la mwisho wa Ardhi baharini uko chini yakamisheni ya Ukomo wa mwisho wa Ardhi Baharini(Commision on the limites of the Continental Sheif –CLCS ) iliyo chini ya Divisheni ya masuala ya baharini na sheria ya bahari (Division for Ocean  Affeirs and the low of the sea –Doalos ) kamisheni  hii ndio msimaizi wa utekelezaji wa kifungu namba 76,aya  4-7 ya makubaliano hayo, ambazo ndizo zinazoruhusu madai ya nyongeza za mwisho wa  Ardhi ya nchi baharini kwenye utekelezaji wa zoezi hili, kamisheni hii ilitoa agizo kupitia hati yake namba DOALOS/07-01406 ya tarehe 14 Agst 2007 kuzitaka nchi zote wanachama ambao hazijatangaza nia ya kudai nyongeza ya mwisho wa ardhi zao baharini ziwe zimeiarifu Sekriterieti ya kamisheni azma hiyo si zaidi ya tarehe 30 Novemba 2007 nchi 27 ziliitikia wito huo ikiwemo Jamhuri ya Muunano wa Tanzania. Kadhalika kwa hati namba SPLOS/INF/20 ya tarehe 16 Januar 200, Kamisheni ikatoa atiba ya muda wa kila nchi kuwasilisha maombi yake kwa mujibu wa ratiba hiyo, Jamhuri ya Muunano wa Tanzania ilitakiwa iwe imewasilisha maombi yake kabla ya Mei 2009 ilifanya hivyo tarehe 5 Mei 2009 ,na ikatakiwa iwasilishe rasmi andiko la madai yake ifikapo taehe 13Mei 2011. Endelea kusoma taarifa hii

Imani ya wazanzibari kwa serikali yao imeingia dosari

Wiki iliyopita faida ya teknolojia ilionekana wazi wazi kwa Wazanzibari na ile dhana ya uwazi ikawa ina maana halisi kwao, maana kwa kweli kila kitu kilikuwa wazi kwao. Safi kabisa bila mizengwe. Kilichokuwa safi bila mizengwe ni mjadala juu ya mabadiliko ya Sheria ya Utalii ambayo yalikuwa yamefikishwa Baraza la Wawakilishi  katika kuiimarisha sekta hiyo  kisheria kwa vile kwa sasa sekta hiyo inaitwa Sekta Kiongozi na kiongozi kwa ajira na mapato. Na hivi karibuni pia Sekta ya Utalii imepewa bango jipya ambapo ingawa bado halijaenea lakini angalau katika rubaa za juu limeanza kutumiwa nalo ni lile la Utalii kwa Wote ambapo mabadiliko hayo pia yalilenga hilo. Endelea kusoma makala hii

Mabadiliko madogo ya mawaziri mzaha

HALI inaonesha kuwa wananchi hawajaelewa hasa ni nini lengo la Rais Dk. Ali Mohamed Shein kufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri kwa kuwabadilisha nafasi mawaziri sita. Lakini, mchambuzi mmoja ametokea kuamini anachokiona kwa kunieleza, “Sina shaka, Rais Shein alitaka kuwahifadhi mawaziri wawili. Waziri mmoja ni mzoefu; mwengine ni mwanagenzi.”Ufafanuzi wake ni kwamba Dk. Shein ametaka kubaki na Ali Juma Shamhuna, ambaye hatima yake imekuwa ikisubiriwa kuwadia baada ya kutuhumiwa na wawakilishi wenzake kuwa amedharau azimio la Baraza la Wawakilishi.Pia Dk. Shein ameamua kumpa muda zaidi Abdillah Jihad Hassan, ambaye amethibitisha kupwaya katika kusimamia wizara ya habari, utalii, utamaduni na michezo.Kwa hivyo, alichokifanya Dk. Shein ni kumlinda Shamhuna sasa kabla ya serikali kuwasilisha msimamo rasmi wiki hii kuhusu uamuzi wa (Shamhuna) kushiriki kupeleka ombi Umoja wa Mataifa la Serikali ya Muungano kuongezewa eneo la bahari kuu kwa shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia. Endelea kusoma makala hii

Kama Jussa, kama Mohamedraza

ISMAIL Jussa Ladhu na Mohamedraza Hassan Dharamsi, ni wajumbe wapya wa Baraza la Wawakilishi, chombo mahsusi cha kutunga sheria kwa Zanzibar.Wanafanana.
Jussa, kiongozi mwandamizi katika Chama cha Wananchi (CUF) na mwakilishi mchaguliwa wa jimbo la Mji Mkongwe, amemtangulia Raza kuingia barazani.Wakati Jussa aliingia kupitia uchaguzi mkuu wa 31 Oktoba 2010, Raza ameingia baada ya kula kiapo cha utii wiki tatu hivi tangu achaguliwe katika uchaguzi mdogo wa kujaza kiti kilichobaki wazi kufuatia kifo cha Mussa Khamis Silima, aliyekuwa mwakilishi. Wajumbe hawa wamezalikana kutoka asili ya Kihindi, hata kama wanatoka sehemu (sectarian).Kizazi cha Jussa kimejichimbia Makunduchi, kusini mwa kisiwa cha Unguja, wakati cha Raza kimetoka Shakani, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Kwa maudhui ya hoja yangu, mfanano unaowaunganisha kifikra Jussa na Raza, unakuja pale ninapoangalia mshindo uliotokea baada ya kuingia barazani.Pamoja na kujua ukakamavu alioonesha akiwa mwakilishi, nachukua mwanzo wa Jussa alipokuwa mbunge bunge lililokoma Oktoba 2010. Alitumikia ubunge kwa miezi minane baada ya kuingia kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete tarehe 10 Februari mwaka huo.Ilichukua muda mfupi sana Jussa kuchukiza wabunge wa CUF, wakiwemo wakongwe wa aina ya Hamad Rashid Mohamed ambaye ni dhahiri sasa amejiinamia kwa kuvuliwa uanachama na kubaki akisubiri hatima ya kesi yake Mahakama Kuu Dar es Salaam. Jussa, baada ya kujulishwa haki zake za ubunge, na akiwa amelipwa angalau mshahara wa mwezi, aligundua kuwa wabunge waliomtangulia walidanganya chama. Endelea kusoma makala hii

Wazanzibari wana haki ya Muujadili Muungano

Labda leo makala hii ivunje ukimya juu ya hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa Zanzibar, maana vyombo vya habari vyote vya Tanzania vimefanya kama kwamba hakuna kilichopo, yaani mambo kama kawaida. Kwa hakika mambo si kama kawaida. Kuna harakati nyingi na ziko wazi kabisa ambazo zinafaa kuandikiwa kwa sababu ni kwa kuandikiwa ndio zitajulikana lakini si kujulikana tu ila hata kufanyiwa uchambuzi. Hali ya kisiasa ya sasa ya Zanzibar inatokana na kukaribia au kuelekea kwenye mchakato wa Katiba ya Muungano ya Tanzania kuridhi matakwa ya Sheria Namba 8 ya 2011 ambapo imetandika misingi ya Watanzania kujadili Muungano ikiwa ni miaka 48 tokea ulipoasisiwa. Harakati zinazoendelea zimo au zinatarajiwa kuwemo ndani ya wigo wa kuelimisha umma juu ya mchakato ujao, lakini kwa kiasi kikubwa zimechukua mkondo mkubwa zaidi pengine hata ambao haukuwa ukitarajiwa. Kwa busara kubwa Serikali ya Zanzibar imeruhusu mjadala huo kuendelea ili kutoa fursa ya Kikatiba kwa watu kutoa maoni yao, na kwa sababu hakuna fujo zozote zilizotokea hadi sasa, ukitoa kauli zisopendeza, basi mambo yamekuwa yakishika kasi. Endelea kusoma makala hii

Zama mpya, fikra kongwe tutafika?

Mataifa mengi hivi sasa yapo katika harakati kubwa kugeuza mambo kutoka zama za teknolojia duni kwenda kwenye teknolojia zilizo bora na kisasa. Wavumbuzi wanaendelea na kazi ya kufikiria wanaweza kuvumbua jambo gani lenye maslahi na binadamu. Dunia ya leo sio ya mtu kulala usingizi, ni ya kufanya kazi kwa bidii, kuibua mawazo mapya,kujituma zaidi na kubwa kutanguliza uzalendo na upendo kwa raia wenzako. Wakati wana sanyansi na vijana wakitafakari hali hiyo, mambo kwa mizimu,waganga wa jadi, wapiga ramli, nao wanatafakari namna gani wanaweza kuboresha huduma zao kwa wateja wao,lakini baadhi yetu hapa Zanzibar tukiwa katika usingizi mzito fofofo! Usingizi wetu tunaweza kuamshwa kwa kumwagiwa maji baridi,lakini si kwa kuliondoa godoro au mkeka kwenye kitanda cha kamba. Kasi ya uwajibikaji kwa watendakazi wa umma hairidhishi,setka binafsi angalau kidogo,lakini bado tuna masafa marefu kufika safari ya maendeleo endelevu. Kila uchao kwenye luninga, Radio, mitandao ya kijamii, tunapewa taarifa za Mataifa mengine kuendelea kiuchumi, kiviwanda, kiteknolojia huku tukishuhudia ubunifu na uvumbuzi wa wasomi na watafiti vijana katika taaluma mbali mbali za sayansi za jamii, sayansi asilia na umbile, sayansi tumizi, bioteknolojia na nyanja nyinginezo za sayansi na utafiti. Endelea kusoma makala hii

Maruhani hawakupindua Zanzibar

SINA tabia ya kusutana, kubishana au hata kujibizana na wasomaji wa makala zangu wenye kutoa maoni tofauti na yangu. Ninaamini kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yoyote ayatakayo hasa pale maoni hayo yanapokuwa ni ya ufafanuzi au uchanganuzi wa matukio ya kihistoria. Kufanya ufafanuzi lakini ni tofauti na kuuelezea ukweli hasa ule ukweli wenye kuhusika na tendo ama vitendo fulani. Nimekuwa nikisubiri kwa shauku kubwa hitimisho la makala za mwandishi mwenzangu wa Raia Mwema, Joseph Mihangwa, kumhusu John Okello. Mfululizo huo wake wa makala zake kuhusu Okello na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ulikuwa ni majibu ya maandiko yangu juu ya mada ya Okello. Kwenye sahafu (safu) ya leo nataka kuyajibu baadhi ya yaliyomo kwenye majibu yake. Kuna baadhi ya Wazanzibari wanaoona kwamba hakuna faida yoyote kujadili yaliyopita hasa sasa wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Lakini wanakosea kwani tunaposonga mbele ni lazima tujue si tu hapa tulipo lakini pia tulikotoka. La sivyo tutajikuta tunajikwaa kila tunapopiga hatua. Kuna tatizo kubwa kumtathmini Okello na dhima yake katika Mapinduzi ya Zanzibar. Sababu yake ni kuwako kwa simulizi zenye kukinzana kuyahusu Mapinduzi hayo na walioshiriki kwenye matukio yaliyoanzia Januari 12, mwaka 1964. Endelea kusoma makala hii

Viongozi wanachuma madhambi tu

WATENDAJI wa staili ya Ali Mwinyikai wamejaa serikalini. Hawajali kama wanakosea, asilani abadan. Hawajali kwa sababu labda wanajua, hata wakibainika kutenda sivyo, wanaachwa vivyo. Huu ni utamaduni uliozoeleka katika serikali ya Zanzibar – wakosaji kulindwa.Hakuna wamuogopae.Wahasibu fulani walipata kunieleza miaka miwili iliyopita, mkasa wa kuhamishwa kutoka Wizara ya Fedha kwa sababu tu hawaelewani na Mhasibu Mkuu wa Serikali. Niliripoti mkasa huu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kutazama maslahi ya wahasibu hawa. Na inajulikana wazi jinsi wahasibu walivyo wachache nchini. Jamii inayopiga hatua ya maendeleo, hata kusifiwa na jamii nyingine, huwa inaamua hasa kujali utu, muda, raslimali za nchi, haki, usawa na inaridhia haja ya kila mtu kupata fursa ya kutenda linalomsaidia kuendelea na papohapo kuendeleza nchi yake.Watu hawajui. Penye jamii inayoishi katika kuamini mambo hayo muhimu maishani, amani husawiri. Amani husawiri pasipo chuki, fitina na hasadi. Watu ni kupendana tu. Endelea kusoma makala hii

Tumejitayarisha kwa mvua za masika

Leo ni March 28 na kwa mujibu wa kalenda ya misimu tumo ndani ya wiki moja tokea kuanza kwa msimu wa mvua wa Masika kama ilivyo ada ya kila mwaka. Hizi ni tarehe ambazo mwananchi wa kawaida kama ilivyo kwa Serikali, anatakiwa azijue kwa sababu ni tarehe ambazo zina athari katika maisha yetu ya kila siku kwa sababu misimu ni jambo la lazima kwetu. Msimu wa Masika unakuja kuanzia Machi 21 hadi Mei 21 na ndio msimu mkubwa wa mvua katika eneo letu na ndio mvua zinazotegemewa kwa aina nyingi ya kilimo na mazao. Endelea kusoma makala hii

Ripoti ya uchunguzi, chanzo cha udanganyifu wa mitihani

Wakati NECTA imetoa ushahidi, kwa kutumia barua za walimu wachache sana, wanaosemekana kuiandikia barua NECTA kwamba wamekubali kuwa udanganyifu umefanyika na wanafunzi, na kwamba wanaomba wasamehewe, sisi katika uchunguzi wetu tumegundua kuwa, baadhi ya waalimu, waliiandikia NECTA barua ya kutoridhika na maamuzi yake, kwa kutowashirikisha wakuu hao, lakini hawakupata jibu lolote, pamoja na kuwa madai yao mengi yalikuwa na msingi. Kwa upande mwingine, tumegundua kuwa baadhi ya waalimu, waliandika ripoti ya yale yaliyotokea wakati wa mitihani, mara tu baada ya mitihani kumalizika, na kupeleka wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali hapa Zanzibar. Jambo la kushangaza ni kwamba, barua na ripoti kama hizi NECTA hatujasikia kuzitaja. Hivyo kutokana na hali kama hii, bado tunapata mashaka makubwa na utendaji huu wa taasisi hii na wizara kwa ujumla. Endelea kusoma ripoti hii

Hutuba ya wiki ya maji duniani

Licha ya jitihada tunazozichukuwa katika suala hili, nafahamu kuwa tumekabiliwa na changamoto nyingi katika sekta ya maji hapa Zanzibar. Ili kuishinda changamoto zilizotukabili katika sekta ya hii ni muhimu kuiamini na kuitekeleza ipasavyo ile rai ya kuwajibika kwa pamoja “Collective responsibility”. Nachukuwa nafasi hii kuwataka wananchi kuiendeleza vizuri rai hii, kila mmoja wetu aamini kwa dhati kuwa anawajibu wa kuchangia ipasavyo kwa kila kitu muhimu kinachohusu maendeleo yake binafsi, maendeleo ya jamii iliyomzunguka pamoja na maendeleo ya nchi yetu kwa jumla. Endelea kusoma hutuba hii

Maisha na nyakati za Wahafidhina Zanzibar

Ujio wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na mageuzi ya hali ya siasa ni moja kati ya mambo ambayo leo yameifanya Zanzibar na watu wake kuwepo katika ramani ya mwelekeo wa kilele cha demokrasia sio tu Afrika,bali kuzishinda hata nchi za Ulaya ambazo baadhi yake demekrasia inasuasua. Ingawa haikuwa jambo jepesi kubadili mambo yaliyokuwa yamezoeleka kwa miaka mingi,lakini hatimaye viongozi waliweka kando utashi binafsi na kutanguliza maslahi ya wengi katika ujenzi wa jamii mpya Zanzibar. Tatizo kubwa ambalo linazikabili nchi nyingi hususan zile zinazoendelea na zaidi Mataifa ya Afrika ni uwajibikaji mbovu kuanzia kwa watumishi wa umma,viongozi na hata jamii yenyewe kukosa vipaumbele katika mambo yao. Zanzibar ya leo imetulia, ni shwari kabisa hakuna upepo mbaya unaovuma,maji yametulia baharini. Ni mwaka wa pili unaingia tangu kufanyika kwa kura ya maoni iliyoamua kuzika ‘maiti’ kisasi na chuki zitokanazo na tofauti ya itikadi ya siasa na ushabiki wa vyama vya siasa miongoni wa wananchi.Endelea kusoma makala hii

Viongozi wa wizara ya habari ni hamnazo

Na Salim Said Salim


Yapo mambo katika maisha ambayo  mtu hawezi kutoa au kupokea nusu. Ni lazima mtu aamue kutoa au kupokea chote kiliopo mbele yake na sio nusu nusu. Miongoni mwao ni mapenzi, ya aina moja au nyengine. Hivyo hivyo ni kwa suala la chuki na uhasama. Hapa nataka kutoa mfano wa mafunzo ya kihistoria yaliyopatikana wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia (1938-45)  wa mtihani uliomkuta dada mmoja wa Poland, Sophie Zawistowka.  Dada huyu alikuwa na asili ya Kiyahudi (angalia filamu ya sinema iliopata tunzo mwaka 1982 iitwayo “Sophie’s Choice”, yaani Chaguo la Sophie). Dada Sophie alikamatwa Austria na wanajeshi wa Kinazi wa Ujerumani na kupelekwa katika kambi. Siku moja alitakiwa aamue mtoto wake yupi kati ya wawili aliokuwa nao atiwe kwenye tanuri la gesi na kuangamizwa na yupi abakishiwe. “Unanitaka nichaguwe?”, Sophie alimuuliza daktari wa kijeshi huku machozi yakimtoka na kutoamini aliyokuwa akiambiwa. Daktari alimjibu :” Tumekuonea huruma. Wengine wanapoteza maisha ya watoto wao wote na baadaye wenyewe”. Huku akilia na kusema “ Siwezi…siwezi” mwanajeshi mmoja alimchukuwa mtoto aliyekuwa mdogo kati ya wale waili na kumpeleka kuangamizwa na gesi. Hali hii ukiitafakari utaona jinsi chuki zinavyomfanya mtu awe jahili na jinsi mzazi anaposhindwa kuchagua mtoto wake yupi auawe na yupi abakie naye. Ninapoangalia namna Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar inavyofanya kazi ninaona  yaliomkuta Sophie ndio waliyonayo baadhi ya viongozi wa ngazi za katikati, hasa katika Wizara ya Habari. Endelea kusoma makala hii

Wahujumu uchumi walianza zamani Z’bar

MTU mmoja ameniambia, “Unaandika kimafumbo ilhali unajua nani wanaiibia nchi na nani wanafuja raslimali zetu. Si uwataje.” Huyu ni msomaji wa makala za safu hii. Yawezekana wengine mnafikiri kama yeye. Ni rahisi kutaja majina ya watu wakiwemo viongozi serikalini na watu binafsi, kwa sababu “wanatajwatajwa” kila mahali. Kweli, wamekuwepo watu wawili watatu wanaotajwa hadharani na wananchi na kuelezwa kuwa ndio wanyonyaji uchumi wa nchi. Lakini, katika kazi ya uandishi wa habari na hata wa vitabu, kutaja majina ya watu kwa kuwatuhumu ubaya, kunamaana pana zaidi ya hiyo. Ukitaja mtu unaeneza mawasiliano; unasambaza ujumbe na ukitaja unafahamisha watu wengi zaidi na kuwaweka katika kujiuliza kulikoni juu ya hao uliowataja. Swali kubwa linakuwa, “Hivi hawa ni wahujumu kweli.” Ni swali hilohilo chombo cha habari kitatakiwa kueleza kwa kina kitapoitwa mahakamani. Hatuogopi mahakama. Mimi siiogopi; na wenye taasisi ninayofanyia kazi hawaiogopi. Wanaodhani kuishitaki MwanaHALISI ndio njia ya kujihami, wanakwenda. Wao wataeleza yanayowakuta huko. Endelea kusoma makala hii

Ripoti ya Utafiti wa vyombo vya habari

Utafiti umeonyesha kwamba asilimia 61 ya wasikilizaji na watazamaji wa ZBC wana mtazamo chanya na asilimia 39 wana mtazamo hasi kuhusu ZBC. Wale wenye mtazamo chanya wamekiri kwamba utangazaji wa umma ni muhimu lakini wametaka hatua za haraka zichukuliwe ili nao wasije wakawa na mtazamo hasi. Wale wenye mtazamo hasi wamesema ZBC imeendelea kuwa sauti ya seriakli wakati vituo binafsi vya utangazaji vimekuwa sauti ya wananchi wanyonge. Wafanyakazi 33 (49%) wana mtazamo hasi kuhusu ZBC na 18 (23%) wana mtazamo chanya. Wafanyakazi 22 (28%) hawakujibu swali. Wafanyakazi wenye mtazamo hasi kuhusu ZBC wanaamini ufinyu wa bajeti na msukumo wa kisiasa ndiyo matatizo sugu yanayoathiri utendaji kazi wa ZBC. Wamedai kwamba ZBC ina wafanyakazi wenye uzoefu, weledi na moyo wa dhati kulitumikia shirika kuhakikisha linafanya kazi vizuri, lakini wanaamini seriakli imeshindwa kuwawezesha kuifanya kazi hiyo na hivyo kuwavunja moyo. Wafanyakazi hao, kwa ujumla wao, wanakiri kwamba jinsi shirika linavyofanya kazi hivi sasa ni utangazaji wa dola na ndiyo maanda wana mtazamo hasi kuhusu ZBC kufanyia kazi ya utangazaji wa umma. Endelea kusoma muhtasari wa ripoti hii

Hutuba ya ofisi ya makamo wa kwanza juu ya utafiti

Naomba nimalizie kwa nasaha zifuatazo kabla ya kufanya hiyo kazi niliyotakiwa kuifanya, ripoti hii imetuonyesha hali halisi tulivyo, hivyo niwaombe watendaji wenzangu wa shirika la utangazaji la Zanzibar, kwanza, kutengeneza ramani ya utekelezaji (road map) kulingana na matokeo ya utafiti huo ili kukabiliana na udhaifu ulioonyeshwa na kupambana na changamoto zilizotolewa. Pili, katika kuyaangalia mapendekezo yaliyotolewa na kuyafanyia kazi lazima muyaangalie kwa kutafsiri mazingira ya Zanzibar na utamaduni wa Wazanzibari. Si kila zuri linalofanywa na vyombo vya habari vya nje kuwa litakuwa zuri kwa mazingira ya Zanzibar kwa sababu tu ya visingizio vya ushindani. Mimi kama mimi msimamo wangu ni kuandaa vipindi vinavyopendwa na umma na vinavyoheshimu maadili ya kizanzibari, vinavyotoa taarifa za ukweli zilizofanyiwa uchunguzi na bila kuegemea upande wo wote wa siasa na unaoheshimu dini zote, unaoheshimu makundi yote ya watu na kuamini kwamba binaadamu sote tuko sawa na ni maumbile tu yaliyotufanya tuwe ama mwanamke au mwanamme, ama una ulemavu kwa sasa au huna. Tatu, Prof. MacKinon, profesa na mtaalamu wa masuala ya mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, amesema ‘New time calls for new Thinking’ (Zama Mpya huhitaji mawazo mapya) na Rais wetu Dr. Ali Mohd Shein anatwambia ‘TUBADILIKE’. Kwa hiyo basi, Zama Mpya zinahitaji mawazo mapya.Tubadilike. Endelea kusoma hutuba hii 

SMZ ipanie kuanzisha makumbusho ya Kiislamu

Katika miaka hii mitatu nimeshuhudia matukio ya vifo matatu ambayo kwangu nimeona ni makubwa na kwa kweli yalinitikisa pamoja na kujua kifo ni wajibu kwa kila binaadamu na kila moja kati yetu ataona mauti. Na sio tu yalinitikisa lakini kwa kweli yameniwachia kumbukumbu kubwa moyoni na akilini mwangu na ningependa kubaki na kumbukumbu hizo maana vifo vya watu hao ni alama kubwa ya mafanikio na uzalendo wa watu hao. Huku nyuma nilikuwa siamini kuwa kufa kunaweza kusherehekewa baada ya kusikitika, sio badala ya kusikitika. Kwa maana kifo kitaleta huzuni na utasikitika lakini baada ya masikitiko kuna nafasi ya kusherehekea. Lakini sio vifo vyote vinavyosherehekewa. Inategema mtu na mtu na kwa maana ya makala haya juu ya watu ambao nimewataja kuwa ni matukio yalio kwangu ni makubwa vifo vyao tumevisikitikia lakini kisha tumevisherehekea na kila mmoja bado anavisherehekea na vizazi kwa vizazi watavisherehekea. Ila hofu yangu isie tu kuvisherehekea kwa maana ya kuvitukuza lakini ifuatiwe na kuvihifadhi na kuvijengea kumbukumbu kwa sababu kusherehekewa kwao kunatokana na kufanya mema wakati wa uhai na sio mema tu lakini kutumikia ubinadamu kadri walivyoweza. Endelea kusoma makala hii

Adhabu ya miaka mitatu ni kubwa -Maalim Seif

Kwa kweli suala hili limewafadhaisha sana wanafunzi hao waliofanya mtihani wa kidato cha nne, walimu na wazazi, lakini pia serikali. Pamoja na uongozi wa Baraza la Mitihani Taifa kujaribu kutoa maelezo na ufafanuzi wa kilichotokea hadi wanafunzi hao kufutiwa matokeo kwa wingi, bado inaonekana sehemu kubwa ya jamii ya Wazanzibari haijaridhika na maelezo hayo.Nashawishika kusema hivyo, kwa sababu mara kwa mara tumekuwa tukiona makongamano na mikutano mingi ya wazazi, wanafunzi na wadau wengine kujadili suala hilo, na baadhi ya wakati washiriki, huwa wakali juu ya jambo hilo. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatambua kuwepo kwa hali hiyo na kwa kweli kuna haja pande zote zijiridhishe na hali iliyotokea hadi kuzua mtafaruki huo, ili isitokee tena. Hivyo basi imebidi Wizara zetu mbili za elimu ya hapa Zanzibar na Tanzania Bara kukubaliana kufanya uchunguzi wa kina kwa minajili ya kuchimbua sababu halisi za hali hiyo kutambua udhaifu uliopo katika skuli na hata katika Baraza la Mitihani lenyewe. Moja ambalo ni dhahiri ni kuwa adhabu ya kuwafungia wanafunzi waliohusika miaka mitatu bila ya kufanya tena mitihani ni kubwa mno na hivyo Baraza la Mitihani linapaswa kuiangalia tena adhabu hiyo. Endelea kusoma hutuba hii

Chanzo na Sababu za Kero za Muungano

Kwa bahati mbaya, Serikali ya Tanzania hawakujali onyo la Profesa Shivji, baada ya miaka miwili tu, waliporejesha mfumo wa vyama vingi, wakaendelea na mtindo wao wa kawaida. Wakachukuwa fursa ya kumnyima Rais wa Zanzibar, anaechaguliwa na watu wa Zanzibar, nafasi yake kama Makamo wa Rais wa Tanzania, iliyotajwa katika Hati ya Muungano. Yeye alikuwa kiungo muhimu kati ya SMZ na Serikali ya Muungano. Sheria hii ilipitishwa na Bunge bila kuhitaji kura ya Thuluthi Mbili (2/3) kwa pande zote mbili. Wabunge wengi wa Zanzibar waliogopa kupinga msimamo wa chama tawala, na wakihiari kwenda kunywa chai au kwenda kujisaidia chooni badala ya kupinga chama chao. Baadaye tu wakazinduka na wakaamua kumuingiza Rais wa Zanzibar kama Waziri bila Kazi Maalum katika Baraza la Mawaziri la Tanzania, ambayo ni kumvunjiya heshima yake. Badala yake, wakaleta mfumo wa Makamo Mwenza anaechaguliwa na Watanzania wote, na anatakiwa awashughulikie Watanzania wote, lakini hana nafasi katika SMZ. Kwa ufupi, ongezeko la Mambo ya Muungano baada ya 1964, na kumuondosha Rais wa Zanzibar kutoka nafasi yake ya Makamo wa Rais wa Tanzania, yamevuruga kabisa muundo wa Muungano. Vilevile, yamevunja Hati ya Muungano, ambayo ilikuwa mkataba wa kimataifa kati ya Tanganyika na Zanzibar. Hati ya Muungano ndio Katiba Mama ya Tanzania. Kwa kiasi kikubwa, mambo yaliofanyika baada 1964 kwa makusudi hayakutaka kuheshimu makubaliano kati ya Marehemu Mzee Karume na Mw. Nyerere, na kuheshimu utaifa wa Zanzibar. Sasa, hata Jaji Mkuu na Waziri Mkuu wanathubutu kusema Zanzibar si nchi. Endelea kusoma makala hii

Sheikh Karume na kilio cha sasa cha Wazanzibari

MENGI yameandikwa na mengi yataendelea kuandikwa kumhusu Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa mwanzo na wa pekee wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambaye Aprili, mwaka 1964 alikubali kuiunganisha nchi yake na ile ya Tanganyika. Hadi sasa walioandika kumhusu Karume ni waandishi wa habari, wanahistoria na wataalamu wa fani ya sayansi ya siasa. Waandishi wa riwaya hata wa riwaya sahili na wa tamthilia bado hawajajitokeza uwanjani kumuandika Karume. Sitoshangaa pakitokea magwiji watanzu hizi mbili za fasihi watakaoamua kumtoa ukumbini Sheikh Karume kwa kumjadili na kumzungumza ama katika riwaya za kisiasa au katika michezo ya kuigiza. Pengine tutaweza kupata taswira iliyokamilika ya Sheikh Karume endapo atachambuliwa katika fani zote hizo mbili au mojawapo ya fani hizo kwani hutokea simulizi za kubuni zikaukaribia sana ukweli kushinda simulizi za kitaalamu, ziwe za wanahistoria au za wataalamu wa sayansi ya siasa. Endelea kusoma makala hii

Watoto wa Kizanzibari muhimu walindwe

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar inayoendeshwa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imepiga hatua katika kukomesha ufisadi na kulinda na kumhifadhi mtoto. Kwa mara kwanza katika miaka 20 hivi, SUK imefanikiwa kutunga sheria ya kupambana na ufisadi, au rushwa; iliyokuwa imekwama kwa sababu watawala hawakujiamini kuipitisha. Nitaijadili sheria hii wakati muafaka, baada ya kwanza kujadili tatizo linalokua la kudhalilisha na kunyanyasa watoto. Rais Dk. Ali Mohamed Shein amesaini Sheria Na. 6 ya mwaka 2011 baada ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi katikati ya mwaka uliopita. Kujua ukubwa wa tatizo la unyanyasaji watoto, fuata mtiririko huu: Katika kitongoji cha Kwarara, jimbo la Fuoni, Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, kuna mtu anajivuna kwa kuharibu watoto. Endelea kusoma makala hii

Viongozi Zanzibar wacheni ubaguzi

Leo nataka nizungumzie kuhusu suala la ubaguzi ambalo limekuwa tatizo sugu hapa Zanzibar na zaidi ubaguzi huo ni ule wa kumtizama mtu kwa dhana za kisiasa, jambo ambalo linaviza maendeleo ya visiwa hivi.Tokea mabadiliko makubwa ya kisiasa ya 1964 kufuatia Mapinduzi nimekuwa nikisema mara nyingi Zanzibar kama nchi ilishindwa kuandaa mikakaati ambayo ingesaidia kuondosha tatizo la chuki za kisiasa zilizojengeka kabla ya Mapinduzi hayo. Chuki za Zanzibar Nationalist Party ZNP, Zanzibar and Pemba Peoples Party ZPPP kwa upande mmoja na upande mwengine ikiwa ni chama cha ASP, nja ambazo zilifikia kilele pale vyama hivyo vilipouungana na kuchanganya kura zao na kwa hivyo kuchukua Serikali ya kwanza ya Uhuru hapo 1963. Ubaya ni kuwa chuki hizo zimeachwa zikuwe na zimee, pengine wengine wamekuwa wakifaidika nazo na ndipo pia zikajitokeza wakati siasa za vyama vingi 1992 ziliporudi na kuzagaa kwa hatari sana hata katika kizazi kipya ambacho hakikuwa kikijua ZNP, ZPPP wala Afro Shirazi zaidi ya ngano walizokuwa wakisikia. Endelea kusoma makala hii

Mradi wa Wanawake wa kupinga ukatili Zanzibar

Kwa masikito makubwa jamii ya Wazanzibari ni miongoni mwa zinazokabiliwa na aibu hii ya ukatili dhidi ya wanawake pamoja na watoto. Tafiti chache zilizofanyika katika baadhi tu ya maeneo zinadhihirisha ukubwa wa tatizo hilo, hali ambayo inatulazimisha tusimame kidete kukabilina na vitendo hivyo, ili wanawake nao waishi kwa amani bila ya bughdha kutoka kwa watu wengine na waweze kuchangia kikamilifu kukuza maisha yao na taifa lao.
Hapa Zanzibar miongoni mwa sababu zinazoelezwa kuchangia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ni kuwepo mitazamo potofu juu ya wanawake, ukimya miongoni mwa wanawake wenyewe na jamii inayowazunguuka, kuona aibu na muhali kwa wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo na hivyo kushindwa kuwafikisha wahusika mbele ya sheria. Matokeo ya hali hiyo ni matukio mengi ya udhalilishwaji wanawake kutoonekana kuwa ni makosa ya jinai, na badala yake jamii inayaona kama ni masuala ya kifamilia na hivyo kuyamaliza nje ya taratibu za kisheria ambapo haki za waliodhulumiwa hazizingatiwi. Kwa upande mwengine kupungua kwa imani ya wananchi kwamba wanaweza kupata haki katika mifumo rasmi, kama vile Polisi na Mahakama kutokana na hali ya ucheleweshwaji wa kesi, ada za mahakama, gharama za usafiri kufuatilia kesi, pamoja na kuwepo vitendo vya rushwa, ambapo hata wale wanaotiwa hatiani ni wachache, hakuzuwii wahalifu kushawishika kuachana na matendo kama hayo. Endelea kusoma makala hii

Nyakati za dhiki na dhima aliyonayo Shein

RAIS Ali Mohamed Shein ana dhamana kubwa kushinda kiongozi yeyote mwengine wa Zanzibar, tangu nchi hiyo iungane na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dhamana yake ni kubwa hivyo kwa sababu Wazanzibari wenzake wanasubiri kwa hamu matokeo ya mchakato wa kuipatia Jamhuri ya Muungano Katiba mpya.Imepangwa kwamba kazi hiyo imalizwe Aprili, mwaka 2014 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano. Miaka 50 ni muda mwingi, uhai wa mtu wa kuzaa na kujukuu ingawa kwa kipimo cha kihistoria huo ni muda mfupi sana kama wa kufumba na kufumbua macho. Shein ana bahati. Bahati yake ni kwamba hakabiliwi na upinzani licha ya shida za kiuchumi na za kijamii zilizozagaa huko Visiwani. Kama wapo wenye kumpikia majungu chini kwa chini basi hawathubutu kujitokeza. Hali iliyopo Visiwani haiwaruhusu. Shein anaiongoza nchi wakati ambapo Wazanzibari wameungana baada ya kuziyayusha chuki zao za kisiasa na kukubaliana, Novemba mwaka 2010 kuwa na suluhu ya kitaifa kwa Maridhiano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). Endelea kusoma makala haya.

Hizbu ut- Tahrir watathmini matokeo ya mitihani

Baadhi hulikabili suala la muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika kimakosa kwa jazba na hulifanya daraja la hukuza hisia za kiaswabia/kiubaguzi baina ya wakaazi wa Bara na Visiwani. Jambo ambalo ni kinyume na Uislamu. Aidha, wengine hususan baadhi ya wanasiasa katika kujificha kushindwa kwao na kuwashughulisha watu wasikabiliane na tatizo msingi, huonesha kimakosa kwamba matatizo ndani ya muungano na muungano wenyewe ndio chanzo cha dhiki zote, badala ya kuonesha kiusahihi kwamba muungano ni tunda (product) linalotokamana na tatizo msingi. Kimsingi maumbile ya wanaadamu huwalazimu kutaka kuishi pamoja na kushirikiana katika muamalat/maingiliano na mambo yao ya kila siku, lakini tatizo huzuka juu ya msingi unaojengewa mahusiano baina ya watu hao. Na katika suala la muungano, tatizo ni msingi batil wa uliojengewa uhusiano huo. Msingi uliojengewa muungano huu unatokamana na nidhamu potofu na ya kikafiri ya kibepari/kidemokrasia. Vivo hivyo, tukumbuke pia kwamba vyama, chaguzi na michakato ya katiba zetu zote zimesimama juu ya msingi sawa na muungano, ambao ni msingi batil wa kidemokrasia ya kimagharibi. Kwa hivyo, kwa hakika ni kuchanganyikiwa kusikokuwa na mfano, upande mmoja kupinga muungano kwa kuwa unaidhulumu Zanzibar, na upande wa pili kuunga mkono vyama vya kidemokrasia na kuchangia mchakato wa katiba ya kidemokrasia, ilhali hivi vyote msingi wake ni mmoja wa kibepari na ndio uliotufikisha katika mashaka tuliyonayo. Suluhisho la suala la muungano huu sio kuwa na serikali tatu, nne au tano, bali ni kuondosha msingi dhaifu wa kibepari katika kusimamia mambo yetu yote, yawe ni katika muungano, katiba, vyama, uchumi, jamii na mengineyo. Kwa sababu huu ndio msingi wa tatizo. Endelea kusoma habari hii

Mchele wa mapembe na bei iumizayo Z’bar

HISIA za wananchi wa Zanzibar hazitofautiani sana na watu wa jamii nyinginezo, mara tu utajapo bei za vyakula. Lakini unapotaja bei ya mchele, sukari na unga wa ngano, ujue unagusa nyongo zao. Bei za bidhaa hizo kwao ni siasa kuu inayofanana na pale wanaposikia huduma ya maji, elimu na tiba. Zaidi ya asilimia 90 ya watu Unguja na Pemba wanaamini katika kula wali kama chakula chao kikuu. Vyakula vingine kwao ni nyongeza tu. Katika takwimu kama hii, ni dhahiri kupanda holela kwa bei za bidhaa hizi, ni siasa ingawa hapajawahi kutokea vurugu kwenye nyanja hii. Ni tofauti na ilivyowahi kutokea Zambia miaka ya 1990 serikali ilipopandisha bei ya unga wa sembe. Nchi ilitikisika kwa ghasia. Utamaduni wa Wazambia ni kula ugali tu, vyakula vingine ni nyongeza. Endelea kusoma makala hii


Hutuba ya Balozi Seif kwa waandishi wa habari

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais imeendelea kufanya vikao na mazungumzo kadhaa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia ya kuleta maelewano mema ya kudumisha na kuimarisha Muungano wetu. Vikao hivi viliwahusisha maafisa wa ngazi zote kutoka Wizara zote hapa nchini. Katika mwaka huu, vikao vitatu vya ngazi za Mawaziri vilifanyika, vikao 6 vya ngazi ya Makatibu Wakuu na vikao 15 vya ngazi ya Wakurugenzi wa pande zote mbili vilikaa kwa madhumuni ya kukuza maelewano baina ya Taasisi za pande mbili za Muungano. Endelea kusoma Hotuba hii

Kamati ya wazee wa wanafunzi waliofutiwa matokeo, Zanzibar

Kamati ya wazee haikubaliani na uamuzi wa kuwafutia matokeo wanafunzi wale tu walioshutumiwa kufanya udanganyifu bali kuwafutia wote kwa kuwa mitihani ulivuja. Kufuatia hoja hizo za msingi Baraza halina budi kukubali kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, na Baraza litapungukiwa na ubebaji wa lawama kwa kuondoa dhana hii ya kuvuja kwa mitihani kwa kurejewa kuliko kubakia katika kung’ang’ania kutorejewa na kuanza kuibua msuguano mwengine wa mvutano kati ya Zanzibar na Tanzania Bara katika suala la elimu na hatimae kuweza kuhatarisha Muungano.Endelea kusoma taarifa hii

Nyakati za dhiki na dhima aliyonayo Shein

RAIS Ali Mohamed Shein ana dhamana kubwa kushinda kiongozi yeyote mwengine wa Zanzibar, tangu nchi hiyo iungane na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dhamana yake ni kubwa hivyo kwa sababu Wazanzibari wenzake wanasubiri kwa hamu matokeo ya mchakato wa kuipatia Jamhuri ya Muungano Katiba mpya. Imepangwa kwamba kazi hiyo imalizwe Aprili, mwaka 2014 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano. Miaka 50 ni muda mwingi, uhai wa mtu wa kuzaa na kujukuu ingawa kwa kipimo cha kihistoria huo ni muda mfupi sana kama wa kufumba na kufumbua macho. Shein ana bahati. Bahati yake ni kwamba hakabiliwi na upinzani licha ya shida za kiuchumi na za kijamii zilizozagaa huko Visiwani. Kama wapo wenye kumpikia majungu chini kwa chini basi hawathubutu kujitokeza. Hali iliyopo Visiwani haiwaruhusu. Shein anaiongoza nchi wakati ambapo Wazanzibari wameungana baada ya kuziyayusha chuki zao za kisiasa na kukubaliana, Novemba mwaka 2010 kuwa na suluhu ya kitaifa kwa Maridhiano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).Endelea kusoma makala hii

Ushindi wa Raza, salamu za mabadiliko

WANANCHI wa jimbo la Uzini wamekinusuru chama wakipendacho – Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya anguko la kihistoria. Wamemchagua Mohamedraza Hassanali Mohamedali, kada wa CCM na mfanyabiashara maarufu Zanzibar, kuwa mwakilishi wao. Raza amechaguliwa kwa kura 5377, sawa na asilimia 91 ya kura 5903 zilizopigwa katika uchaguzi mdogo wa mjumbe wa baraza la wawakilishi uliofanyika 12 Februari. Uchaguzi huo ni wa kujaza kiti kilichokuwa wazi kufuatia kifo cha Mussa Khamis Silima, aliyekuwa mwakilishi. Raza anasubiri kula kiapo (kuapishwa) katika mkutano ujao wa baraza utakaofanyika Aprili mwaka huu, ili kuanza rasmi kutumikia wananchi wa jimbo hilo. Kwa kumchagua Raza, wananchi wa Uzini wamekilinda chama chao, wamempa ridhaa na wamethibitisha imani kwake kama kiongozi mwakilishi wa matatizo na matumaini yao. Endelea kusoma makala hii

Sheria na utawala bora

Wiki iliyopita Zanzibariliiadhimisha Siku ya Sheria ambayo sasa imeanza kuwa kalenda muhimu katika rubaa ya fani hiyo adhimu hapa Zanzibarna kuongezeka haiba yake kila mwaka. Tunaomba siku hii iendelee kusherehekewa kwa vile ni fursa ya kukumbushana mambo mengi lakini pia ni nafasi nzuri sanaya kuwajuvya wananchi juu ya mambo yanavyoendelea na kwa kila njia kuwashirikisha katika mabadiliko na miamko inayohitajika. Fani ya sheria hapa Zanzibarina muda mrefu kwa vile miaka na kaka fani imejikita katika jamii ya Kizanzibari tokea ukoloni ambapo pamoja na uchache wa watu wake Zanzibarilikuwa na mfumo imara wa mahakama na tabaan mawakili wa kiwango cha juu. Suala la utoaji wa haki lilikuwa la uzito mkubwa na Serikali kwa mfano ya Kikoloni ilichukua juhudi kubwa kuhakikisha mfumo huo wa utoaji haki sio tu unakuwa imara lakini kwa hakika ulijaribiwa na ukashinda majaribu.Endelea kusoma makala hii

Majumuisho ya mkutano wa Redet

Washiriki walisisitiza kwamba mijadala yote ya sasa na ijayo juu ya uimarishaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar iendeshwe kwa kuzingatia ukweli kwamba uimara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa unategemea zaidi na uwezo wake wa kutatua kero mbalimbali za wananchi. Kero zinazopaswa kupatiwa suluhu ni pamoja na huduma za msingi za kijamii hususan afya, elimu na maji, ajira kwa vijana, mfumuko wa bei na vitambulisho vya Uzanzibari. Washiriki walishauri kwamba wanachi nao wana wajibu wao wa kushirikiana na serikali kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayoisibu jamii ya Zanzibar. Endelea kusoma majumuisho haya.

Majumuisho ya mkutano wa Redet

 Washiriki walisisitiza kwamba mijadala yote ya sasa na ijayo juu ya uimarishaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar iendeshwe kwa kuzingatia ukweli kwamba uimara wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa unategemea zaidi na uwezo wake wa kutatua kero mbalimbali za wananchi. Kero zinazopaswa kupatiwa suluhu ni pamoja na huduma za msingi za kijamii hususan afya, elimu na maji, ajira kwa vijana, mfumuko wa bei na vitambulisho vya Uzanzibari. Washiriki walishauri kwamba wanachi nao wana wajibu wao wa kushirikiana na serikali kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayoisibu jamii ya Zanzibar. Endelea kusoma majumuisho haya

Hakuna nchi kubwa na ndogo – Maalim Seif

Huwezi kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kwa ufasaha kabisa bila ya kugusia suala la Muungano wa Tanzania, na ndio maana utaona masuala ya Muungano kwa Zanzibar hupewa uzito na umuhimu wa kipekee na wananchi wetu. Hivi sasa wananchi wana shauku kubwa na hamu ya kutoa maoni yao juu ya Katiba mpya, wakiamini kwamba ndio njia mfuaka kumaliza malalamiko yao ya siku nyingi. Miongoni mwa hayo ni yale yanayogusa uchumi wa Zanzibar na siasa kwa ujumla. Endelea kusoma hutuba hii

Tuendelee kuvumiliana – Balozi Seif

Lakini hata hivyo, ni vyema pia tukaelewa kuwa hatuwezi kujenga nyumba imara ya jiwe kwa siku moja na tukaishi humo. Utamaduni ule ule wa kustahamiliana utahitajika kufikia hatua nyengine tunayoitaka. Utamaduni tulioutumia wa kuleta mabadiliko bila ya kujali maslahi ya mtu au kikundi fulani bado unahitajika kwani gharama ya kufanya mabadiliko kwa lengo la kutaka mtu au watu, kikundi au vikundi fulani vinufaike ni kubwa inayoweza kuturejesha tunakotoka. Endelea kusoma hutuba hii

Hutuba ya ZLSC

Mheshimiwa Mgeni Rasmi uzinduzi wa Siku Ya Sheria Zanzibar utabaki na deni endapo tutasahau kukumbuka na kutambua mchango mkubwa alioutoa Mwanasheria Msomi Mashuhuri wa Zanzibar Professor Haroub Othman ambaye katika uhai wake sio tu kuwa aliasisi fikra hii bali aliipigania sana Zanzibar iwe na Maadhimisho haya. Kwa kuwa leo hii tunaadhimisha maadhimisho ya mwanzo akiwa yeye hayupo nasi na ameshatangulia mbele ya haki tunamuomba Mweyenzi Mungu amuweke mahali pema peponi. Aamin. Mh. Mgeni Rasmi, katika taaluma ya sheria mawakili wanajukumu kubwa la kuelekeza kwa njia ya ushawishi wa kitaaluma njia iliyo bora na sahihi ya kupita lakini uamuzi wa mwisho wa njia ipi ndio sahihi na bora ya kupita hubaki kwa waheshimiwa majaji wetu baada ya mazingatio ya kina ya mapendekezo ya mawakili. Wakati tunaadhimisha sherehe hii njia aliyoionesha Mh. Jaji Mkuu ya kuwa na ubunifu, kuongoza kwa umakini, bidii , busara na ushirikiano ni njia ambayo hatuna budi kuienzi na itoshe tu kusema kuwa hii ni “precedent” tosha ya kufuatwa katika uendeshaji wa shughuli zetu.Mh. Mgeni Rasmi, kama unavyojua, kauli mbiu yetu katika maadhimisho haya inasema “Kupiga Vita Rushwa Katika Utoaji Haki”. Uchaguzi wa kauli mbiu hii haukuja kama sadfa. Kama inavyoeleweka, yapo matukio makubwa ya kisheria, kwa mfano mchakato wa uandaaji katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yangetegemewa kwa wakati huu yawe na ushawishi mkubwa katika kuweka kauli mbiu ya maadhimisho kama haya. Hata hivyo baada ya kuzingatia kwa kina ukweli kwamba mfumo wetu wa utoaji haki haukunusurika na janga hili la maangamizi la rushwa, athari zake kwa jamii na Taifa letu kwa ujumla ndio ikaonekana haja ya kutoa umuhimu na kuzipa kipaumbele juhudi za kusafisha mfumo wetu wa utowaji haki. Endelea kusoma hutuba hii

Siku ya Sheria Zanzibar

Kwanza kabisa, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu (S.W) kwa kutujaalia kufika siku hii ya leo kuiadhimisha siku ya Sheria Zanzibar tukiwa wenye afya njema na furaha tele huku tunaendelea na joto la kiangazi.Pili, napenda niwapongeze waandaaji wa maadhimisho haya kwa uamuzi wao wa kuandaa maadhimisho haya kwa mara ya kwanza hapa Zanzibar. Hili ni jambo zuri na nawashukuru kwa dhati kwa kunialika ili niwe Mgeni Rasmi katika sherehe hii ya kihistoria nchini kwetu. Naipongeza zaidi Mahakama kwa kuiandaa na kuiongoza shughuli hii.Tatu, nimefarajika sana leo kupata bahati hii ya kusimama mbele ya hadhara hii ya Majaji, Mahakimu na Wanasheria wasomi (learned friends) kutoka katika Taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi. Katika maisha yangu ya kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar niliwahi kuteuliwa na Rais Mstaafu Dk. Amani A. Karume kuwa Waziri wa Katiba na Utawala Bora katika Awamu ya Sita na kwa kipindi hicho ingawa kilikuwa kifupi nilipata bahati ya kufanya kazi na Wanasheria wenye ujuzi mkubwa akiwemo Mwanasheria Mkuu wa wakati huo Mheshimiwa Idi Pandu Hassan na Katibu Mkuu wa wakati huo Ndugu Othman Masoud ambae kwa sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kutoka kwao nilijifunza mambo mengi ya thamani yanayoweza kuufanya umma au wananchi kuwa na imani na Mahakama na vyombo vya sheria na kwa pamoja tuliweza kuyatekeleza majukumu yetu katika kuendeleza utawala bora. Hivi sasa nimepata fursa nyengine ya kufanya kazi na wataalamu na mabingwa wengine wa sheria na ninatarajia kwamba nitaendelea kujifunza kutoka kwao na kwa pamoja tutatekeleza wajibu wetu.Serikali imeamua kwa makusudi kuliimarisha jengo, viwanja na historia ya jengo hilo ambalo ndio Baraza la Kutunga Sheria la mwanzo hapa Zanzibar. Endelea kusoma hutuba hii. 

Hapatakuwa na NGO za ‘briefcases’ kama zitawezeshwa

Mwishoni mwa wiki Rais wa Zanzibar, Dk Ali Muhammed Shein alizindua Jumuia ya Kuzuia na Kukinya Maafa (DCPM) na kuzungumzia mambo mbali yanayohusu Asasi Zisizo za Kiserikali (NGO) hapa Zanzibar.Kwa hakika DCPM imekuja baada ya tukio la mwaka jana la Septemba 10 ambapo meli ya MV Spice Islander ilizama na kusababisha kupotea kwa maisha ya watu 1370 wakiwemo maiti zao zilizopatikana na wengine ambao Mwenye Enzi Mungu hakujaalia kuwa hivyo.Kabla ya hapo Zanzibar imekuwa ikipata majanga mbali mbali ambapo fikra pia ya kuanzisha asasi kama hiyo ilikuwa ikija na kuondoka na hata Serikali yenyewe si zamani sana ilianzisha idara yake mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na majanga. Majanga ya upepo, moto na hata mafuriko baada ya mvua kubwa yamekuwa ni baadhi ya matukio yanayoitikisa Zanzbibar pale yanapojitokeza lakini hata wakati mwengine matukio ya miripuko mikubwa ya maradhi kama cholera pia hutikisa jamii ya Zanzibar na huhesabiwa ni majanga ya taifa. Tukio la Septemba 10, 2012 limetoa mafunzo mengi juu ya haja ya kukinga na kukabili majanga ambapo pamoja na kufanyika juhudi kubwa lakini kumeonekana kuwepo na upungufu mkubwa pia wa zoezi hilo zima kuanzia meli ilipokuwa inazama hadi tulipokunja mabanda katika Uwanja wa Maisara.Endelea kusoma makala hii.

Shamhuna amejisahau au amejaribu ujinga?

KATIKA wadhifa wa Waziri wa Maji, Ardhi, Nyumba na Nishati anaoshikilia, Ali Juma Shamhuna amejisahau. Pengine sivyo. Yawezekana amejaribu ujinga.Ameshiriki kutunga ombi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano bila ya kuihusisha serikali iliyompa madaraka kiutendaji–Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayoendeshwa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).Ombi hilo liliwasilishwa Umoja wa Mataifa 18 Desemba mwaka jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Profesa Anna Tibaijuka.Tanzania inataka kuongezewa eneo la bahari kuu tengefu la kushughulikia harakati za kiuchumi juu ya eneo la awali la maili 200. Eneo linaloombwa limo katika maji ya Bahari ya Hindi ambayo Zanzibar inayatambua kuwa katika eneo lake la utawala.Shamhuna mwenyewe alikiri kwenye Baraza la Wawakilishi alipotakiwa kueleza kilichotokea kwa kadri ajuavyo. Kwa sauti ya kujiamini kama ilivyo kawaida yake, alisema: Kama mimi waziri ndio serikali, basi nitasema serikali tumeshirikishwa. Lakini kama tafsiri ya serikali ni kwa maana ya Baraza la Mapinduzi, basi niseme hapa kuwa serikali yetu haikushirikishwa katika suala hili.” Endelea kusoma makala hii

Tuiache Zanzibar iende kwa amani

NASHINDWA kuelewa ni kwa nini wahusika wamekuwa wakiilazimisha Zanzibar iendelee kubakia katika Muungano uliozaa Tanzania wakati wenyewe wameonyesha kuwa hawaridhiki na jinsi Muungano huo ulivyo.Kwa wahusika hapa namaanisha Serikali ya Muungano pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa upande mmoja, serikali ya Muungano ndio mlezi mkuu wa Muungano huu na CCM ndicho chama pekee ambacho kimeonyesha kuutaka Muungano kwa sura yake ya sasa ya serikali mbili, ambayo nayo imekuwa ni chanzo cha malalamiko kutoka Zanzibar.Zanzibar wanazo sababu nyingi tu za kuonyesha kutoridhishwa na Muungano jinsi ulivyo ambazo wao wanaamini kuwa ni za msingi. Wahusika wanaweza wasizione sababu hizo kuwa za msingi; lakini hilo nalo halizuii Zanzibar kujiondoa katika Muungano.Kimsingi, Zanzibar ni mbia katika Muungano huo na kwa maana hiyo ina haki ya kuamua kuendelea kuwapo ndani ya Muungano au kujitoa.Hata kama sababu za kutaka kujitoa hazitaonekana kuwa za msingi sana kwa upande wa pili, lakini hiyo haiondoi haki yao ya kutaka kujitoa kwenye Muungano pale wanapoamini kuwa Muungano huo hauwanufaishi tena. Endelea kusoma makala hii

Mungelisoma mukafahamu, ndipo mukamtaka Jussa aombe radhi!

Nimesoma makala ambayo inaelekea kuwa imechapishwa katika gazeti moja la Kiswahili kuhusu matamshi ya Waziri wa Muungano wa Ardhi na Makazi, Professa Anna Tibaijuka na kufadhaishwa na udhaifu wa ufahamu wake katika suala linalohusu Hoja Binafsi ya Mheshimiwa Ismail Jussa. Kama Profesa Ana Tibaijuka na gazeti hilo wangefahamu Hoja Binafsi ya Jussa basi wasingetamka kabisa kuwa Jussa aombe radhi, wala asingetamka kabisa kuwa Serikali ya Zanzibar ilirishirikishwa. Alichosema Jussa na anachokisema Professa Tibaijuka ni vitu viwili tofauti, na kama Professa Tibaijuka alipita baina ya mstari kwa mstari wa Tamko la Jussa basi kwa hakika wao walipaswa kuilaumu Serikali ya Zanzibar na sio Jussa. Lakini hata hilo la kuilamumu Serikali ya Zanzibar halipo, kama ambavyo nitaeleza. Anavyodai Profesa Tibaijuka ni kuwa mchakato si wa leo na jana na kwamba ulianza tokea mwaka 2007 na wakati wote kulikuwa na ushiriki kamili wa maafisa wa Serikali ya Zanzibar na hata kushiriki katika safari ya kwenda New York kukabidhi andiko hilo. Endelea kusoma maoni haya.

Jibu la Prof. Sheriff kwa Prof. Tibaijuka

The controversy about the extension of the sea boundary has come at the right time when Zanzibaris have shown that they will no longer be hijacked when their vital national interest are at stake, regardless of party affiliation. It was rather disingenuous for Prof Tubaijuka to try to introduce party divisions when she claimed that CUF was claiming thatZanzibarwas not consulted. If she heard the debate in the House of Representatives, it was almost unanimous, and prominent CCM backbenchers made a point of saying that this was not the question of CUF but of the whole ofZanzibar. She should not try to divide Zanzibaris again. We have suffered enough from such tactics. It seems that mainland leaders feel that if you have a few Zanzibaris in your gang, then Zanzibaris are represented – and it is never difficult to get a few vibaraka, as we know all too well from our history. The question is whether the people inZanzibareven knew this business was cooking – certainly the House of Representatives, a body that was elected by the whole people ofZanzibar, did not know about it until the professor was inNew Yorkpresenting the document to the UN. I and many of my friends who try to keep up with events affecting our country were taken by surprise. Endelea kusoma maoni haya.

CC-CCM imemteua Raza, imejinusuru

WAKATI huu ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya kile walichokitarajia wananchi wa jimbo la Uzini, wengine wananuka. Nimesimuliwa kuwa wapo viongozi waliochukizwa na nilichokieleza wiki ililiyopita. Tatizo hawa ni wachache mno – hawajai hata mkono. Hawa ni viongozi maslahi na wazibaji riziki kwa wengine. Katika jimbo la Uzini, wapo viongozi waliojaa woga wa kuadhirika. Wao wamekuwepo kwa miaka mingi, hawajasaidia wananchi. Hawawajali.Balibado wanatamalaki madaraka. Viongozi hawa wamewaingiza mkenge wananchi wanyonge kwa kuwatumia katika walichodai “Barua ya Wazi kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.” Hawajui mwenzao ana mtandao mkubwa. Anasoma alama za nyakati. Amechoka kuingizwa mjini kila siku na wapuuzi, wakiwemo makada wa CCM waliochokakamahawa wenye maslahi jimboni Uzini. Eti wanajimbo hao wamejigamba kuwa wanaenzi mapinduzi ambayo wazee wa jimbo walichangiasanakuyafanikisha. Kutaka Raza achinjiwe baharini kihilakamaalivyopata kufanyiwa Adamjee jimboni Kawe, ni kuenzi mapinduzi! Ninaamini Haji Juma Kibwana anayetajwa kutoka kijiji cha Uzini; Omar Haji Moh’d anayetajwa kutoka Umbuji; Kassim Juma Khatib anayetajwa kutoka Mgeni Haji, Selemani Bakari Bushiri anayetajwa kutoka Tunduni, Fatma Herezi Said anayetajwa kutoka Bambi na Mustafa Khamis Mustafa anayetajwa kutoka Kiboje hawakujua athari za walichotumwa kukifanya. Endelea kusoma makala hii.

Kadhia ya mipaka ya bahari Bara haijali uwepo wa Zanzibar
Habari ambayo ilivuma sana wiki iliyopita ni ile ya kuhusu suala la Tanzania kupeleka ombi katika Umoja wa Mataifa juu ya kuongeza eneo la bahari la nchi hii jambo ambalo kwa hakika ni la kisheria. Hatua hio ilielezwa kuwa ni kupeleka andiko katika taasisi hiyo yenye nguvu kuliko zote duniani na ambayo ndio mratibu wa masuala yote ya kimataifa ya kiulimwengu likiwemo suala la bahari au tuseme mipaka yote ya nchi na nchi na pia ile ya kimataifa. Jambo hilo ni la kisheria kwa sababu linatokana na Sheria ya Kimataifa ya Bahari ambayo Tanzania ni mtia saini wake na kuwa bila ya kuwepo kwa mkataba huo wa kimataifa hali itakuwa ni ya vurugu tupu. Sheria ya kimataifa inaipa fursa kila nchi iliyo mkabala na bahari kupata eneo fulani za awali awali mbele ya fukwe zake ili zitumike pamoja na mambo mengine kwa ajili ya ulinzi na pia kuwa ni eneo lake la kujidai. Kisha kila nchi kama hiyo inapata eneo la maili nyengine nyingi kuelekea bahari kuu kwa ajili ya kulitumia kiuchumi kama vile masuala ya uvuvi na hata kutafuta rasilmali chini ya bahari. Inaeleweka kwa hakika kuwa chini ya bahari kuna rasilimali kubwa sana ambayo wanadamu bado hawajaweza kufikia, lakini tayari kuna nchi nyingi zimefaidi utajiri huo kwa sababu ya uwezo wake wa kisayansi. Endelea kusoma makala hii

Kwa upotoshaji huu, Ismail Jussa aombe radhi

LEO tumechapisha habari zinazomnukuu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishangazwa na kauli iliyotolewa katika Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Mji Mkongwe kwa tiketi ya CUF, Ismail Jussa kwamba andiko lililowakilishwa katika Umoja wa Mataifa (UN) na waziri huyo kuomba eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) halikufanywa kwa niaba ya Serikali ya Muungano kwa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haikushirikishwa.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri Tibaijuka alisema andiko hilo liliwasilishwa Januari 18 mwaka huu kama ombi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuongeza kuwa, SMZ ilishirikishwa kikamilifu tangu mchakato wa kuandaa mradi huo ulipoanza mwaka 2007. Waziri alitoa kauli hiyo baada ya mwakilishi huyo kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi mwanzoni mwa wiki, akilitaka Baraza kutolitambua andiko hilo lililowasilishwa UN na kuliomba liiagize SMZ kutojihusisha na mpango huo kwa namna yoyote kwa madai kwamba ni mpango wa kuhujumu eneo la bahari la Zanzibar. Mwakilishi huyo alikwenda mbele zaidi na kumtaka Waziri wa Ardhi, Ali Juma Shamhuna ajiuzulu, vinginevyo awajibishwe na Rais, huku akiungwa mkono na wajumbe waliosimama kuchangia hoja hiyo. Endelea kusoma maoni haya.

SMT ilipuuzia maazimio halali ya BLW – Jussa

Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 1 inaeleza, “Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar” . Endelea kusoma hoja hii

 

Zanzibar bila ya rushwa na wahujumu uchumi yawezekana

Hatimaye kuna uwezekano mkubwa wa Zanzibar kuwa na sheria yake ya kupamba na na rushwa kwa kuwa Serikali imetoa muswada ambao unapelekwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea hivi sasa. Lakini pia sheria hiyo mbali ya masuala ya rushwa itajikita pia katika makosa yanayohusiana na uhujumu uchumi na kwa pamoja yatakuwa ndio msingi wa muswada huo ambao umeona mwanga baada ya siku nyingi kuwa katika makabrasha. Hii ni hatua nzuri kuchukuliwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa hatimae kufanya maamuzi ya makusudi kulimaliza tatizo la ukosefu wa sheria kama hiyo ilhali vitendo vya rushwa na kuhujumu uchumi ni vya usiku na mchana. Sheria hii ilikuwa imetengenezwa miaka kadhaa iliyopita, lakini Serikali zilizopita kwa sababu moja au nyengine hazikuwa na moyo wa kuisukuma katika chombo cha utungaji wa sheria ili kufanywa iwe sheria ni kuwabana wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi. Endelea kusoma makala hii

Boko Haram Nigeria

Wiki iliyopita nilipata ujumbe wa maandishi wa simu (sms) kupitia msomaji. Ujumbe huo ulisema, nanukuu: “Habari za kazi wapendwa, mimi ni msomaji sana wa gazeti lako pamoja na kwamba ni Mkristo. Kuna suala la Boko haram nilitegemea gazeti lako lingeandika habari hizo kwa sababu linakemea uovu, lakini wapi au ni kwa sababu waliouliwa ni Wakristo na wanawalazimisha kuhama wawapishe Waislamu. Uwe mkweli Shehe wangu kwani Uislamu unasema hivyo. Sema kweli hata kama ni mchungu.” Ujumbe huu ambao niliupata Ijumaa mchana Januari 6, 2012 nadhani mwandishi aliutuma baada ya kusoma makala yangu juu ya Al Shabaab na jinsi baadhi yetu ama kwa ujinga au kutokujua tunavyoshabikia vita dhidi ya Al Shabaab (ugaidi) bila kujua inakotoka na malengo yake. Kwanza nianze kwa kusema mambo mawili, tunapoandika mambo haya, tunachozingatia ni masilahi ya umma, masilahi ya jamii na masilahi ya binadamu kwa ujumla. Gazeti hili na mwandishi ameandika sana juu ya uharamia uliofanywa na Marekani kule Nicaragua, Chile, Panama, Cuba, El Salvador, Ecuador na Latini Amerika kwa ujumla. Kule wengi ni Wakristo. Tumefanya vile kwa sababu tunachojali ni ubinadamu. Endelea kusoma makala hii

Raza anavyochochea mabadiliko Uzini

SIKUSUDII kamwe kushinikiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya maamuzi kisiyoyaamini. Ila najua wakithubutu, wataumbuka. Nimependa tu leo kueleza hisia za wananchi wa jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini, Unguja, walioamua kumsogeza karibu Mohamed Raza, mfanyabiashara mashuhuri na kada mkubwa wa chama hicho. Maelezo ya fitna, ubaguzi uliopitiliza, udhalilishaji dhidi ya wananchi wa jimbo hili na kampeni ya kijinga dhidi ya matakwa yao inayofanywa na baadhi ya watu ndio yaliyonipeleka huko. Chimbuko ni uchaguzi mdogo. Wapigakura wa jimbo hili wanajiandaa kumchagua mjumbe wa Baraza la Wawakilishi mwezi ujao. Endelea kusoma makala hii

 

 

Mapinduzi yetu na fikra mpya, vitu ambavyo haviepukiki kamwe

Kwa mara nyengine tena Zanzibar inapita katika sherehe za mapinduzi yake, ambaye kwa watetezi wake wakubwa huitwa matukufu, na hii ikiwa ni miaka 48 tokea tukio hilo la Januari 12, 1964. Mapinduzi hayo yalitokea chini ya mwezi mmoja tokea Zanzibar ilipopata uhuru wake hapo Disemba 10, 1963 na kuipa Zanzibar kiti katika Umoja wa Mataifa Disemba 18, 1963. Kwa hivyo Uhuru wa Zanzibar na Mapinduzi ya Zanzibar ni matukio yaliopishana kwa mwezi mmoja tu, lakini kwa kiasi kikubwa imani iliopo hivi sasa na kwa miaka 48 kuwa hapakuwa na Uhuru wa wananchi, bali Mapinduzi ndio ambayo yamekuwa ni ya umma. Hayo ya kipi halali na kipi haramu, kwa sababu pia kuna hoja kuwa Mapinduzi hayakuwa ya lazima mbali ya matendo ya ziada yaliokithiri, yasiwe ni mjadala wetu wa leo, lakini zaidi haja yetu ni kutizama mbele tuendeko. Endelea kusoma makala hii.

Zanzibar: Busara za Moyo zazaa matunda

HATUNA budi tushukuru kwamba mwaka jana visiwa vya Zanzibar viliweza kukwepa machafuko, migawanyiko na migogoro ya kisiasa iliyozikumba nchi kadhaa barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla. Kinyume na kawaida, mwaka ulipita bila ya kuzuka vituko vyovyote au mapambano yoyote ya kisiasa baina ya wafuasi wa vyama vikuu viwili vya CCM na CUF Visiwani humo au kama ilivyokuwa zamani baina ya vyama vya ZNP na ASP. Hilo ni jambo kubwa hasa kwa vile mwaka huo ulizaliwa miezi isiyotimu hata mitatu baada ya Uchaguzi Mkuu uliokuwa na matokeo ambayo wengi wa wafuasi wa chama cha CUF waliyapinga. Na hapa hekima iliyotumiwa na uongozi wa CUF inastahili pongezi. Kulikuwa na hatari kwamba matokeo hayo yangesababisha vurugu nyingine za kisiasa visiwani humo. Vurugu aina hizo ndizo zilizokuwa zamani zikizusha mifarakano miongoni mwa Wazanzibari na kuleta mpasuko katika jamii, mpasuko ambao wengi wakidhani hauna dawa. Endelea kusoma habari hii

Mwaka mwingine wa uhuni na vurugu chama tawala

HAUHITAJI kuwa nabii kugundua kwamba mwaka huu utakuwa na mivutano na misuguano mingi ya kisiasa. Hili ni jambo linaloeleweka hata kwa wale tunaoweza kuwaita mbumbumbu-mzungu-wa-reli katika masuala ya kisiasa. Mwaka huu zitafanyika chaguzi nyingi na za ngazi mbali mbali ndani ya CCM, chama-tawala, kuanzia ngazi za mashina hadi kileleni, ngazi ya uongozi wa taifa, hatima yake ikiwa ni uchaguzi wa halmashauri kuu na mwenyekiti wa chama hicho. Chaguzi zote hizi zinaingia katika mantiki ya kawaida ya kukihuisha chama, kukipa uhai mpya kwa kukipa uongozi mpya na kukiwekea malengo mapya au kushadidia yale ya zamani kwa mwamko mpya. Chama chochote, hata chama cha wacheza ngoma, hakina budi kufanya kazi ya kujikagua kila mara, kwa vipindi vilivyokubaliwa ndani ya chama husika. Kwa sababu hili ni jambo la kawaida, halitakiwi kuzua mijadala yoyote mizito.Endelea kusoma habari hii

SUK lazima itafune jongoo 2012

KWA miezi miwili sasa kumekuwa kukishuhudia vikao vya serikali kujitathmini. Alianza kiongozi mkuu wa Zanzibar , Dk. Ali Mohamed Shein. Alikutana na waandishi wa habari waandamizi na kuwaeleza tathmini yake ya utendaji tangu ashike usukani wa kuiongoza nchi hii ya visiwa. Alitaja kile alichoamini ni hatua mbele. Akataja alivyoona ni vikwazo kwa serikali kupiga hatua nyingine zaidi mbele. Alitaja chimbuko la vikwazo hivyo. Alikemea wanaovileta – maana aliamini vingi vimetokana na tabia mbaya za watendaji aliowapa dhamana ndani ya serikali anayoiongoza.Basi Dk. Shein alikiri zipo changamoto mbilitatu zinazohitaji kufanyiwa kazi ili kujenga msingi imara wa kuiwezesha serikali kufanikisha malengo yake kwa kipindi kilichoanza. Sasa umemalizika mwaka mmoja wa SUK. Mwezi mmoja wa ziada, Disemba, umepita. Tulikuwa tunazungumzia yaliyohusu mwaka 2011. Umekwisha na umepita. Tunaingia mwaka mpya wa 2012. Miaka miwili tu kabla ya kuukuta mwaka wa uchaguzi mkuu, 2015. Endelea kusoma makala hii

Muungano sasa uwe wa Mkataba, si wa Katiba

KUNA sababu moja kuu inayowafanya Watanzania waukaribishe kwa msisimko mwaka mpya wa 2012. Nayo ni kwamba, mwakani ndipo suala la Katiba mpya ya nchi hiyo litapoanza hasa kutokota. Hatuhitaji wapiga ramli kutwambia kwamba mwaka ujao hilo ndilo litalokuwa suala kubwa la kisiasa nchini Tanzania. Kwanza kuna wenye kuupinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011 kama ulivyo hivi sasa. Wanahoji kwamba muswada huo una taksiri kadha wa kadha ambazo zitazuia isipatikane Katiba iliyo halali na itayotungwa kwa kuwashirikisha vilivyo wadau wote wanaostahiki kushirikishwa. Miongoni mwa wapinzani hao ni asasi za kiraia ambazo zitaendelea kuupinga muswada huo kwa hamasa kuu na wataishtaki Serikali mahakamani katika jaribio la kuuzuia. Wakishinda mahakamani watakuwa wamepata mradi wao. Wakishindwa wataendelea kuwa nguvu ya kutosha itayoweza kuwashawishi wananchi waikatae Katiba itayoibuka baada ya kumalizika kwa mchakato wake. Endelea kusoma mala hii

Serikali ya maridhiano na watendaji wakorofi

Utumishi wa umma ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) unaumwa na unatumiwa vibaya na baadhi ya watu kwa maslahi binafsi. Watendaji wakorofi ndio wagonjwa wenyewe. Kwa muda mrefu, wananchi wamekuwa wakipata simulizi mara kwa mara za misuguano ya kiutendaji inayotokea katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambayo kwa mwaka mmoja sasa imeanza kuendeshwa kwa muundo wa serikali ya ushirikiano kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) Mara utasikia mtendaji fulani amekwaruzana au haelewani na waziri wake; au mtendaji wa wizara fulani anadharau wananchi anaokutana nao ili kuhudumiwa, au utasikia fedha hazijatolewa kwasababu katibu mkuu au mkurugenzi wa mipango na uendeshaji amezuia kasma husika. Endelea kusoma makala hii

Chokochoko ndani ya CUF zimalizwe haraka

Na Khalid S Mtwangi

Chama cha Wananchi, ama Citizen United Front (CUF), sio chama cha siasa cha Kiislamu wala si cha Waislamu. Kisingeweza kuwa hivyo na kikasajiliwa na kikaruhusiwa kutangaza sera zake nchi nzima, Bara na Visiwani, kwa vile sheria ya nchi hii imepiga marufuku kabisa vyama vya siasa vyenye mlengo wa kidni na kikabila. Sheria hii lakini huweza kupigwa chenga bila Serekali kuchukua hatua zozote. Endelea kusoma makala hii

Kwa nini twashindwa kuwapandisha wakubwa kizimbani?

Na Ahmed Rajab

UKWELI, ingawa ni adhimu, una tabia mbaya. Una tabia ya kuudhi na hata ya kuuma. Ndiyo maana haishangazi tunapojikuta tunaukwepa. Alhamisi iliyopita nilikuwa Bush House, jijini London, kwenye studio za BBC Focus on Africa, kusajili kipindi cha mwisho wa mwaka niliposikia kwamba mahakama moja nchini Ufaransa imemhukumu rais wa zamani wa nchi hiyo Jacques Chirac, baada ya kumpata na hatia ya ufisadi. Nilishtuka nilipojisikia nikijiambia: ‘Ndiyo maana wazungu wanatushinda. Endelea kusoma makala hii

Wazanzibari wana akili, na utamaduni wao

Kalamu ya 14 Des 2011

KWA kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshatia saini muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , ni rahisi kuamini hatua zinazofuata zinaandaliwa. Hatua mojawapo ni ya kiongozi huyo kuunda tume itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya wanayoitaka.Endelea kusoma makala hii

 

Sheria ya kulinda watoto itekelezwe

Na Ally Saleh

Sasa ni miezi 6 tokea Dk. Ali Muhammed Shein, Rais wa Zanzibar amesaini sheria muhimu sana katika maisha, makuzi na maslahi ya mtoto wa Kizanzibari ambayo ni thamini kupita thamani yoyote ile. Sheria Namba 6, 2011 imekuja baada ya juhudi, vilio na misukumo mbali mbali ya wana harakati kutokana na madai mengi ya unyanyasaji wa watoto wa Kizanzibari hali ambayo ilikuwa inaelekea kiwango cha kutisha.Endelea kusoma makala hii

Ubabe wa Karume ulimuaibisha Nyerere na taifa

Ahmed Rajab

SIKU moja nilipokuwa nikiongea na rais mmoja wa Zanzibar sebuleni Ikulu, Unguja, alinigeukia ghafla na kuniuliza: ‘Unafikiri Ukarume utarudi hapa?’ Sikudiriki kumjibu na wala sidhani kama alitaraji nimjibu maana mbiombio alijijibu mwenyewe, tena kwa mkazo, kwa kusema: ‘Hautorudi tena.’ Alipoutaja ‘Ukarume’ nilijua alichokikusudia: Ubabe wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.Endelea kusoma makala hii.

 

Zanzibar inaishi, Tanganyika ilikufaje?

Na Joseph Mihangwa

NCHI yetu inaingia kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya. Tayari Bunge limepitisha muswada wa kuanzisha mchakato huo. Moja ya mambo yanayoyumbisha nchi ni suala la Muungano usioeleweka. Je, Katiba mpya itaweza kutatua kero hizo? Na ni zipi kero hizo?.Endelea kusoma makala haya

Mzanzibari atafutika ifutikapo dunia

Kalamu ya Jabir Idrissa 7 Des 2011

MBUNGE wa Uzini, Muhammed Seif Khatib anasema kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hakuna mtu anayeitwa “Mzanzibari.” Katiba aliyoinukuu ilitokana na kuunganishwa kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar , People’s Republic of Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika , Republic of Tanganyika , tarehe 26 Aprili 1964.Endelea kusoma makala haya

 

Unaotakiwa ni ujabari kuwang’oa mafisadi wa CCM…

Ahmed Rajab

SI kweli kwamba Bwana Mkubwa Kabisa nchini Tanzania ana sikio la kufa. Akitaka kusikia anasikia. Hivyo ndivyo alivyofanya baada ya kushauriwa na mawaziri wakuu wa zamani Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim kuwa Serikali yake inapaswa ikutane na wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuzungumzia mustakbali wa mchakato wa kupata katiba mpya ya Tanzania. Ni muhimu maoni ya CHADEMA yasikilizwe kwa vile ni chama kikuu cha upinzani nchini.Endelea kusoma makala hii

Uhuru wa Tanganyika uliamsha ari kwa Zanzibar kujitawala

Na Salim Said Salim

WAKATI Tanganyika (Tanzania Bara) ilipopata uhuru nilikuwa na miaka 15, lakini nilielewa kwa kiasi mambo ya kilimwengu. Nilikuwa darasa la 10 (Fomu 2) na msomaji wa kila siku wa magazeti na nikiandika habari, fani niliyoitumikia tokea utoto wangu hadi leo. Siku siku mbili kabla ya uhuru nilimuona mmoja wa wazee walionilea na jirani, kama pua na mdomo katika mtaa niliozaliwa wa Kisimajongoo, hayati Sheikh Abeid Amani Karume, akiwaarifu wazee wenzake kuwa alialikwa kwenda Bandari ya Salama (Dar es Salaam) kuhudhuria sherehe za Uhuru.Endelea kusoma makala hii

Kwa nini naadhimisha Tanzania?

Lula wa Ndali Mwananzela

KWA haraka haraka kabisa mtu anaweza kukimbilia na kusema “Tanganyika”. Na sababu iko wazi kwamba nchi iliyopewa uhuru Desemba 9, kutoka udhamini wa Umoja wa Mataifa uliokuwa chini ya Mwingereza, iliitwa Tanganyika. Na ni kweli taifa lililokuwepo baadaye hadi wakati wa Muungano wa Aprili 26, 1964 liliitwa Tanganyika. Ni kweli walikuwepo raia wa Tanganyika na nchi inayoitwa Tanganyika. Kwa hiyo, kiufundi na kimantiki ni sahihi kusema kuwa ni “uhuru wa Tanganyika”. Ukiishia hapo utafanya makosa. Endelea kusoma makala hii

Wazanzibari hawautaki Muungano

Hakika ni ajabu kuwa baada ya miaka arobaini na saba ya Muungano wa Tanganyikana Zanzibarleo wanajitokeza vijana huko Zanzibarambao wanaukataa huu Muungano. Kamakungetokea wazee ndio wamekuwa na rai hiyo labda kungekuwa na mantiki kuwa hao wanaukumbuka Uzanzibari wao ule ambao si sawa na ulivyo leo.Endelea kusoma makala hii

Zanzibar inahitaji ukombozi ili kufika, maridhiano yanastahiki kulindwa

Na Mohammed Ghassany

Uumini wangu kwa Maridhiano ya Wazanzibari hautetereki au hauporomoki. Niliyaamini yalipozaliwa miaka miwili iliyopita na ninayaamini leo yakiwa yamefanikisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUKZ) iliyodumu madarakani kwa mwaka mzima sasa. Nitayaamini kesho, keshokutwa na milele.Endelea kusoma makala hii

Tamasha la busara linaakisi utamaduni wa Mzanzibari lilindwe

Wiki iliyopita wengi wetu tuliokuwa katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort tulipata mshtuko kutokana na matamshi ya Mkurugenzi wa taasisi ya Busara Promotion, Yussuf Mahmoud. Yussuf Mahmoud ni raia wa Uingereza aliyehamia Zanzibaryapata miaka 10 iliyopita na anavyoniambia ni kuwa ameamua maisha yake yatamalizia hapa hapa Zanzibarkwa maana hana nia ya kurudi tena Ulaya.Endelea kusoma makala hii

Katiba Mpya yaweza kuidhoofisha CUF kama ufisadi kwa CCM

Mohammed Ghassany,

Baada ya kufuatilia alichokisema leo (22.11.2011) Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Aboubakar Khamis Bakari, kuhusiana na kadhia ya mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na namna kilivyopokelewa na wachangiaji kadhaa kwenye majukwaa ya mtandaoni, utabiri wangu ni huu kwa Zanzibar: katika uchaguzi wa 2015, vyama vyote viwili vinavyounda leo Serikali ya Umoja wa Kitaifa vitakuja kulazimika kuiba kura kusalia madarakani.Endelea kusoma makala hii

Wasaidizi wanamsaidia au wanamwangusha Rais?

Kalamu ya Jabir Idrissa.  16 Nov 2011

SIAMINI kama kutokuwepo kwangu katika mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kulipunguza mvuto wa mkutano.Ni kweli sikuwepo, na baadhi ya waliogundua kwa kutoniona televisheni zilipoonesha baadaye, wameuliza sababu. Ila waandishi walikuwepo, tena wengine wakubwa tu kiumri na uzoefu kazini kunizidi.Endelea kusoma makala hii

Muungano, Mswaada na Zanzibar: kamba ya kuvuuka ama kitanzi cha kujitundika?

Muungano huu haujadiliki kwa sababu haupo. Kwa hiyo kuulinda kwake ni kuweka hijabu nzito baina ya kitu ambacho hakipo na akili ambazo zikiachiliwa kuujadili zitakhitimisha kuwa haupo! Na ndio maana tumeletewa tuujadili muswada wa “Sheria kwa ajili ya kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa madhumuni ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba…” Na maoni ya wananchi yatakusanywa wakati tayari kazi ya kuusambaratisha uongozi wa CUF na CCM uliosimamia Maridhiano imeshaanza kufanyiwa kazi.Endelea kusoma makala haya

Sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011

Sekretarieti 13.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume itakayoongozwa na katibu.
(2) Katibu atateuliwa na Rais baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar. (3) Mtu atakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa katibu endapo mtu huyo ni mtumishi wa serikali na ana taaluma ya sheria na amefanya kazi hiyo kwa muda usiopungua miaka kumi na ana mwenendo na tabia nzuri. (4) Katibu atawajibika kwa Tume na atafanya kazi na kutekeleza majukumu ya Sekretarieti. (5) Watendaji wengine wa Sekretarieti watateuliwa na waziri kwa makubaliano na waziri mwenye dhamana ya mambo ya katiba wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (6) Sekretarieti itakuwa na idadi ya watumishi wa umma kwa kadri itakavyohitajika kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu na matumizi ya mamlaka ya Tume. Gharama za Tume 14.-(1) Gharama za shughuli za Tume wakati wa mchakato wa mapitio ya katiba kwa mujibu wa sheria hii zitalipwa kutoka mfuko mkuu wa Hazina. (2) Wajumbe wa Tume na Sekretarieti watalipwa kwa kadri waziri atakavyoamua kulingana na sheria na kanuni za nchi.Endelea hotuba hii

Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni

Mapendekezo haya yanaonyesha sio tu nafasi na ushawishi mkubwa wa Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya, bali pia ni mwendelezo wa dhana potofu kwamba Zanzibar ni mshirika sawa wa Jamhuri ya Muungano. Hii inathibitishwa pia na pendekezo la ibara ya 24(3) ya Muswada inayotaka Katiba Mpya ikubaliwe na theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Tanzania Bara na vile vile theluthi mbili ya wajumbe wanaotoka Zanzibar.Ni wazi, kwa hiyo, kwamba iwe ni kwa masuala ya Muungano yanayoihusu Zanzibar pia, au kwa masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo hayaihusu, Zanzibar itakuwa na kura ya turufu kwa mujibu wa mapendekezo ya Muswada huu.Endelea kusoma makala hii

 

Wawakilishi:Muswada haukidhi haja bado

Na Ally Saleh

Kwa mara nyengine tena mbele ya umma Serikali ya Tanzania imepeleka Muswada wa marekebisho ya Katiba ili utayarishe mazingira ya wananchi kuifanya kazi hiyo baada ya miaka karibu hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Haya yanatokea kutokana na yale yanayoonekana ni madai ya umma ya kutaka mabadiliko ya Katiba kama alivyosema wangu Professa Josephat Kanywanyi kwamba kilio hiki ni cha wananchi kutaka kujua haki za kiuchumi, ugawaji wa rasilmali, namna ya kudhibiti watu wanaowachagua na jinsi Serikali yao inavyotumia fedha za umma.Endelea kusoma makala hii

SUK na changamoto zake

Ilikuwa ni siku njema kwa hakika kwa waandishi wa habari wa Zanzibar na Tanzania Bara kukaa na Dk Ali Muhammed Shein kwa zaidi ya saa tano ndani ya mjengo wa Ikulu ya Zanzibar ambao mara nyingi wengi wetu huwa tunaiona paa tu.Si aghlabu viongozi wa Kiafrika kukubali kukaa na waandishi wa habari kuzungumza nao juu ya uendeshaji wananchi, ambao kikatiba wana wajibu wa kuwaarifu wananchi juu ya kitu gani kinaendelea kila baada ya muda. Endelea kusoma makala hii

Wazanzibari wana hofu ya papa kummeza dagaa

SHEREHE ya hivi majuzi ya kuapishwa Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, kuwa waziri asiye na wizara maalum katika Serikali ya Muungano imewashangaza na kuwaudhi watu wengi huko Zanzibar. Wanavyohisi ni kwamba Rais wao hatambuliwi kuwa ni Rais huko Bara kwa vile huko anakuwa waziri tu na pingine anakuwa chini ya amri na uongozi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama ilivyo ada ya mawaziri wote wa Serikali ya Muungano wa Tanzania. Endelea kusoma makala hii

Ni kejeli Rais wa Zanzibar kuwa waziri bila wizara

HIVI karibuni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Mohamed Shein, alizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini mjini Zanzibar ambapo, pamoja na mambo mengine, alizungumzia lawama zinazoelekezwa kwake kwa kula kiapo kuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba inadhalilisha hadhi na nafasi ya Rais wa Zanzibar na Serikali ya Watu wa Zanzibar kwa ujumla. Endelea kusoma makala hii

Zanzibar kupewa nguvu kubwa ni haki yao – Zitto

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ametoa maoni yake kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Katiba mpya unaotayarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano ulioanza mapema wiki hii bungeni mjini Dodoma. Ili kufahamu zaidi kuhusu maoni ya Zitto, endelea kusoma makala haya. Endelea kusoma makala haya.

Zanzibar na Mauritius — kisa cha nchi mbili katika bahari moja…

HAYA ni masimulizi ya nchi mbili: Zanzibar na Mauritius. Zote ni mchanganyiko wa visiwa vilivyo katika Bahari ya Hindi. Zote zina wakazi wapatao milioni moja na laki mbili. Zote zina watu wa mchanganyiko wa makabila. Zote zikitawaliwa na Waingereza. Zote zinapendwa na watalii wa kimataifa.Wakati nchi hizo mbili zilipopata uhuru- Zanzibar mwaka 1963 na Mauritius mwaka 1968 zote zikitegemea mauzo ya zao moja tu (sukari ikisafirishwa na Mauritius na Zanzibar ikijinata kwa karafuu zake.)Endelea kusoma makala hii

Busara itumike kwenye karafuu

Katika tukio la mwanzo ambalo Serikali ya Umoja wa Kitaifa ililifanya
katika ngazi ya kitaifa na kutaka kuonyesha uwezo wake lilikuwa ni
hili suala la uchumaji wa karafuu hasa Kisiwani Pemba.Endelea kusoma makala hii

 

Serikali ilikataa-uwazi wawakilishi wairudisha chuoni

KAMPENI ya kuilinda karafuu ya Zanzibariliyoanzishwa na Rais Dk. Ali Mohamed Shein, inalenga kupambana na ufisadi – uovu unaotafuna uchumi wa taifa lolote duniani liwe tajiri kiuchumi, linalokua au taifa maskini kama Tanzania.Ufisadi unapoiandama nchi masikini kama Zanzibar – sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – athari zake huwa kubwa zaidi maana vitendo vya kifisadi huumiza zaidi wananchi wenye maisha duni.Endelea kusoma makala hii

UBABE NDIO UNAOWAPONZA AKINA GADDAFI

Na Ahmed Rajab

MAJUZI hivi jijini Nairobi rafiki yangu mmoja alinisimulia mkasa alioushuhudia siku moja alipokuwa nyumbani kwa Mzee Jomo Kenyatta huko Gatundu katika Mkoa wa Kati wa Kenya. Aliniambia kwamba akiwa kwenye mlango wa sebule ya Gatundu, alimsikia Kenyatta akiwaambia hivi baadhi ya mawaziri wake (ambao majina yaoninayahifadhi): ‘Ondokeni hapa karibu nami nendeni mketi kule. Mkiketi hapa nikaja kuhamaki naweza kuwapiga. Na mkiketi huko mkumbuke kwamba kamba yangu ni ndefu na naweza kuirusha nikawaburuta.Endelea kusoma makala hii

TANZANIA INASIMAMA WAPI KUHUSU LIBYA

Na Ally Saleh

 

AJENDA YA ZANZIBAR IJADILIWE

Ahmed Rajab

KATIKA utamaduni wetu wa Kiswahili tuna usemi usemao: ‘Ukimstahi mke ndugu huzai naye.’ Staha na kuoneana haya ni miongoni mwa sifa za uungwana wetu. Hata hivyo, kuna nyakati ambapo huwa hatuna budi ila tuziweke kando sifa hizo ili tuweze kuambizana ukweli kwa madhumuni ya kujenga, si kubomowa.Endelea kusoma habari hii

WAHARIRI WATEKELEZE WALICHOAZIMIA

Kwa siku mbili Wahariri mbali mbali wa vyombo vya habari walikutana mjini Arusha katika kile kilichoitwa mkutano wa kujitzama upya na dhana kuu ya mkutano huo ikipewa jina la Uandishi wa Dhamana (Responsible Journalism).Endelea kusoma makala haya.Endelea kusoma makala haya.

NAAPA CCM HAITAMJADILI MANSOOR

WAKATI huu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapokabiliwa na mtihani mgumu wa kurejesha imani kwa wananchi kupitia kaulimbiu yake ya “kujivua gamba,” siamini kamakina nafasi ya kumjadili Mansour Yussuf Himid.Endelea kusoma habari hii

MAFUTA YANAVYOHANGAISHA UTAWALA Z’BAR

KATIKA mazingira ya mfungamano wa kiutendaji uliopo ndani ya Jamhuri ya Muungano imekuwa vigumu Zanzibarkujizongoa na kile kinachoonekana kama mnyororo ili kujitegemea kiuchumi.Ukweli huu unajengwa na ushirikiano uliotokana na kuunganishwa dola mbili zilizokuwa huru kabla – Jamhuri ya Watu wa Zanzibarna Jamhuri ya Tanganyika– kwa mkataba uliasainiwa 26 Aprili 1964.Endelea kusoma habari hii

NCHI NDANI YA KANDA

Afrika Mashariki kabla Ukoloni- makabila na watu- misingi ya awali ilitandikwa- dhana ya ushirikiano ilianzishwa- ukoloni ukapata wepesi- ukoloni wa Kiingereza ukarahisisha.Endelea kusoma makala haya

 

DK SHEIN HAMJUI FRANCIS CORNISH

RAIS Dk. Ali Mohamed Shein, pengine kwa alichojifunza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaalikokuwa makamu wa rais kwa miaka minane, amehamishia semina elekezi Zanzibar.Endelea makala haya

HUTUBA ZA UONGOZI WA ZIRPP

 Hotuba fupi ya Dr. Ahmed Gurnah katika uzinduzi rasmi wa taasisi ya sera za umma (zirpp) jumamosi tare 18 juni 2011, hoteli ya bwawani, zanzibar.Endelea kusoma hutuba hizi

 

HUTUBA YA DK SALIM AHMED SALIM

WAZIRI Mkuu Mstaafu Tanzania, Dk Salim Ahmed Salim amesema ni jambo la kufurahisha kuiona Zanzibarimetulia kisiasa kwa kuwa Bara la Afrika lilikuwa na shauku ya kubwa kuiona Zanzibarikiwa imeondokana na siasa za chuki na ugomvi.Endelea kusoma hutuba hii

 

UCHANGIAJI DAMU KWA HIYARI

Tukumbuke kuwa UKIMWI unabaki kuwa tishio kubwa katika dunia.  Mpaka sasa hapa kwetu watu 6 kati ya kila watu 1000 (0.6%) wana UKIMWI.  Na iwapo kama Serikali isingechukua hatua hii ya Damu Salama na hatua nyenginezo zifaazo basi UKIMWI ungeweza kukua kwa kasi kubwa sana .    Hatua hii ina mchango mkubwa katika kudhibiti kasi ya ongezeko la maradhi haya thakili ya UKIMWI pamoja na maradhi mengine yanayoambuzikwa kwa njia ya damu kama vile homa ya ini (hepatitis) na kaswende (syphilis).Endelea kusoma hutuba hii

BAJETI MPYA NDANI YA USIRI MCHAFU

MPAKA naandika makala hii, sifahamu vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika bajeti ya kwanza itakayotekelezwa na serikali ya umoja wa kitaifa.Kupata taarifa za mwelekeo wa bajeti imekuwa jambo gumu isivyofikirika. Hakuna kiongozi aliyetayari kujitolea kueleza.Endelea kusoma makala hii

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameipongezaTanzaniakatika jitihada zake za kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI na akasisitiza kuwa,Tanzaniani nchi ya mfano licha ya kuwa jitihada zaidi zinatakiwa kuendelezwa katika uhakikisha kuwa maambukizi mapya yanapungua katika kipindi hiki.Endelea kusoma taarifa hii

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal yupo mjini New York, Marekani ambapo anahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Ukimwi ulioandaliwa na UNAIDS/.Endelea kusoma taarifa hii

 

PRESS RELEASE

British Business in Tanzania– Partners for Long-Term Economic Growth
The theme of the Queen’s Birthday party this year is celebrating British business in Tanzania. And to help us celebrate we’ve got a list of sponsors who all help to showcase British business talent here, drawn together by our flourishing British Business Group.Continue reading

KAULI ZA UBAKAJI WATOTO ZATAKA VITENDO

Kauli nyingi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa na viongozi wetu
kuhusiana na suala la unyanyasaji na ubakaji wa watoto wa hapa kwetu
Zanzibar lakini matokeo yake yamekuwa si ya kupendeza na kwa hakika
yanatisha.Endelea kusoma habari hii

SERIKALI MSIWE KAMA KONOKONO

NI Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyenipa sababu ya kuendeleza mjadala wa kadhia ya moto Pwanimchangani.Nilikuwa nimetia tamati nilipojiridhisha kwamba ujumbe niliolenga ufike kwa serikali, umefika vizuri. Nimethibitishiwa viongozi wakuu na wasaidizi wao japo sijui idadi yao, wamesoma neno kwa neno.Endelea kusoma habari hii

KADHIA YA MOTO,MAHKAMA YAFURIKA

PWANIMCHANGANI imegeuka gharika. Tangu pale wanakijiji walipoteketeza mabanda ya biashara ya wajasiriamali kutoka Tanzania Bara, polisi wamepiga kambi na kukamatakamata watu.Endelea kusoma habari hii

 

WANANCHI WALITAKA KULINDA MILA ZAO

WATANZANIA kadhaa wanaotoka Bara wamepoteza makazi na biashara. Makazi na biashara zimeteketezwa moto na waharibifu. Wamerudishwa nyuma hatua nyingi. Wanahitaji kusaidiwa. Hakuna anayepata maumivu makubwa kamawao. Wapo wanaofurahia kilichowakumba. Naapa wapo. Tena wengi wakiwemo wenyeji wa maeneo yale.Endelea kusoma habari hii

Fungate ya SUK imekwisha

Wiki iliyopita Rais wa Zanzibar Dk Ali Muhammed Shein alifanya ziara
rasmi katika eneo muhimu la kiutawala yaani Mkoa wa Mjini na Magharibi
kutizama harakati mbali mbali. Ni ziara iliyokuwa ikitarajiwa ingawa
sisemi kuwa imechelewa.Endelea kusoma makala haya

WAZANZIBARI HAWADAI UPENDELEO,WANATAKA HAKI

WAZANZIBARI wanaweza kutafsiriwa vyovyote kuhusu hisia zao juu ya muungano wa Tanganyikana Zanzibar, unaotimiza miaka 47 Jumanne ijayo.Wanaonekana hawajatulia akili, walalamishi, wana jazba wanapozungumza, na wanafiki. Kwa hivyo, “watu wa kupuuzwa tu.” Endelea kusoma makala hii

TUMECHOSHWA NA MUUNGANO

 Inasikitisha kuwa Jamhuri ya Muungano imekuwa ikifanya mbinu na njama za makusudi kupopotoa mamlaka ya Zanzibarilhali jeuri kubwa ikifanywa kwa kutumia nguvu za kisiasa na hila za kisheria na wakati huo huo wananchi kuwekwa kizani.Endelea kusoma barua hii

JAKAYA SIKILIZA KILIO CHA WAZANZIBARI

Jakaya Kikwete

Mheshimiwa Rais, sisi wazee tunaowakilisha wenzetu wa mikoa mitano ya Zanzibartunaunga mkono kwa nguvu zetu zote wale wote waliokataa na kuupinga mswada huo (rasimu ya mswada ya utaratibu wa kutunga katiba). Sambamba na hili, tunachukua nafasi hii kutoa pongezi kwa wazanzibari wote walioacha tofauti zao zote na kuweza kusimama kidete na kwa pamoja kwa hoja za wazi na madhubuti katika kupinga mswada huu unaoonekana wazi kuandaliwa kwa makusudi mazima ili kuiteketeza na kuimaliza Zanzibar. Hii ni haki ya kikatiba kwao kwa sababu Zanzibarni nchi yaohalali na hivyo hawana budi kuonyesha uzalendo na kuchokeshwa kwao na dharau, kebehi za serekali ya muungano kwa nchi yao.Endelea kusoma barua hii ya wazi

MASUALA YASIYO NA MAJIBU KATIKA MUUNGANO

Tokea kuasisiwa hapo tarehe 26 Aprili, 1964 Muungano wa Tanganyikana Zanzibarambao ndio uliozaa Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaumekuwa na sifa mbili kuu.  Sifa moja ni ile ya kuwa nyenzo au kitambulisho cha umoja wa kitaifa             Tanzania,na hivyo wale wanaojinadi kwa uzalendo na hisia za    umoja wa kitaifa wamekuwa wakijinasibisha na kuupenda mno Muungano na kuahidi kuulinda kwa gharama zozote.  Mapenzi haya ya Muungano yamepelekea hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuwa na kifungu mahsusi cha kuwataka Viongozi wa Kitaifa (Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamo wa Rais, Waziri Mkuu na Rais wa Zanziba) kula kiapo cha kuulinda Muungano kabla ya kuanza kazi zao (Kifungu cha Katiba ya Muungano).Endelea kusoma habari hii

HIVI GAMBA LA CCM KWELI LIMEVUKA?

Tumesikia mengi wiki iliyopita kuhusiana na Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho

Pius Msekwa

kinachotutawala hapa nchini, Zanzibar na Tanzania kwa jumla bda ya ushindi wake wa mwaka jana tu.Chama hiki wiki hiyo iliyopita kilifanya mabadiliko makubwa ya ndani ambayo yamepelekea kujiuzulu taasisi mbili kubwa za ndani na kusaidia kuuna upya tasisis hizo ambazo zilikuwa na majukumu makubwa ndani ya chama hicho kikongwe kabisa nchini.Endelea kusoma habari hii

UPEPO MPYA ZAMA MPYA-KIZAZI KIPYA

NI dhahiri sasa muungano wa Tanganyikana Zanzibarumefikia kiwango cha juu kabisa cha kudhoofika. Kama ilivyo ngoma inapolia sana, uko nchani kuvunjika.Huko nyuma waliokuwa wakiusema muungano, hata kamani kwa nia njema ya kuuimarisha, walikuwa ni wale walioitwa wapinzani wa serikali.Endelea kusoma habari hii

 

MLEMAVU ANAYEPANGA KUMUAJIRI MUMEWE

23 08 2010

Bi Amina akimpa mkono rais Amani

BAADA ya kujifungia zaidi ya miaka 25 katika maisha yake. AMINA Abdallah Said (38) mama wa watoto wawili ambaye ni mlemavu wa miguu anayeishi Changaweni Mkoani Mkoa wa Kusini Kisiwani Pemba amepata nuru mpya ya maisha.Alikuwa amejifungia kwa muda wote huo kutokana na ulemavu wa miguu alionao. Alifanya hivyo kwa kuhisi kwamba jamii ingemtenga kutokana na hali yake lakini zaidi ni umasikini alionao.Hata hivyo, kukaa kwake ndani kwa kipindi hicho hakukumfanya asiwe na ndoto. Aliamini ya kuwa wapo walemavu wa miguu kama yeye wanaojishughulisha na kazi mbali mbali zinazowapatia fedha hivyo kumudu maisha yao na hata kusaidia jamii.Endelea kusoma makala haya.

WAGOMBEA 11 WA URAIS WA ZANZIBAR

10 07 2010

Dk Shein na Nahodha wakipeana mkono huko Dodoma

KINDUMBWE ndumbwe cha urais ndiyo kimekwisha anza mjini Zanzibar. Wagombea 11 wamejitokeza hivyo kuifanya kazi ya Kamati Kuu Maalum ya CCM kuwapa alama wagombea hao kuwa ngumu. Kamati Maalum itakutana Julai 3 na kujadili majina ya waliojitokeza kugombea nafasi ya Urais Zanzibar na hatimaye kupeleka mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambayo nayo itayapeleka majina ya wagombea yaliyopitishwa kwenye Halmashauri Kuu ya CCM na mwisho kabisa Mkutano Mkuu wa CCM ndio utakaopitisha jina moja. Makala hii iliyoandaliwa na waandishi wetu HAWRA SHAMTE na SALMA SAID inaelezea wasifu wa wagombea wa nafasi ya uongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Endelea kusoma makala haya

MUUNGANO WENDE NA MABADILIKO YA KISIASA

28 04 2010

WATANZANIA leo wanaadhimisha miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika

Salum Juma Othman

na Zanzibar ambao tokea kuanzishwa kwake hadi sasa umekuwa mfano kwa nchi nyingi hasa katika Bara la Afrika kutokana na kudumu kwake. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar licha ya kudumu kwa miaka 48 sasa lakini umekuwa ukipata misukosuko ya hapa na pale na wakati mwengine hujikuta katika kipindi kigumu cha misukosuko hiyo lakini bado unaendelea kuwepo kutokana na uvumilivu wa wananchi na viongozi wao wa nchi mbili hizo ambao waasisi wao ndio walioungana kwa maslahi ya mataifa hayo. Waasisi wawili wa mataifa mawili huru yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika na Mzee Abeid Amani Karume wa Zanzibar ambao wote ni marehemu kwa sasa waliunganisha nchi mbili na kugeuzwa kuwa nchi moja iliyopewa jina la Tanzania . Katika kipindi chote cha uhai wa waasisi hao hakukuwa na matatizo makubwa kama ambavyo yanayojitokeza hivi sasa ambapo baadhi ya wananchi wanahoji kuwa tutaendeleaje na muungano uliounganishwa na watu wawili bila ya kuwashirikisha wananchi wenyewe? Jambo ambalo wapo baadhi ya watu wanaosema kwamba muungano huu ni batili kwa kuwa haujawashirikisha wananchi mbili bali ni wa viongozi wawili tu.Endelea kusoma makala hii.

KINDUMBEDUMBWE CHA URAIS ZANZIBAR

23 04 2010

Dk. Mohammed Gharib Bilal

WAKATI CCM imeshapuliza kipenga chake kuashiria kwamba kinyanganyiro cha kitufe cha Urais, Ubunge na Udiwani kinatarajia kuanza, kimbembe kikubwa kiko Zanzibar ambako mara hii wanatarajia kumpata rais mpya baada ya Rais Amani Karume kumaliza muda wake wa kuwatumikia wananchi kwa mihula miwili ya miaka mitano mitano. Habari zinazosemwa mitaani kuhusu nani atagombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM zimekuwa nyingi, hivyo makala hii imedhamiria kuelezea nafasi walizonazo baadhi ya watu wanaotajwa kuwa huenda wakajitokeza kuchukua fomu hapo Julai mosi na kuzirudisha Julai 8 mwaka huu. Anayetajwa sana katika duru za siasa kwamba huenda akachukua fomu ya urais mwaka huu kujaribu tena bahati yake baada ya kutopewa nafasi mwaka 2000 ni aliyekuwa Waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa uongozi wa Rais Mstaafu Salmin Amour, Dk Mohamed Gharib Bilal. Dk Bilal ambaye kabla ya kuwa Waziri Kiongozi katika miaka ya 1995 hadi 2000 alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika fani ya Fizikia aliingizwa katika siasa na Komandoo Dk Salmin Amour kwa kumwita aje Zanzibar amsaidie, na kwa kweli katika kipindi hicho alitoa mchango mkubwa wa kifikra.Endelea kusoma uchambuzi huu.

MARIDHIANO ZANZIBAR NI MTIHANI

15 04 2010

ZANZIBAR ni miongoni mwa nchi katika bara la Afrika ambazo bado hazijatulia katika harakati za kisiasa tokea kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi katika mabara hayo.Wapo baadhi ya wachambuzi wa siasa katika nchi kadhaa bara hilo wanaosema mfumo wa kidemokrasia katika nchi za bara la Afrika sio wa hiyari bali ni wa kulazimishwa kutokana na mabadiliko ya kidunia na mifumo ya nchi za magharibi kutaka iwe hivyo zenye kufuata misingi ya demokrasia hali ya kuwa nchi zenyewe hazipo tayari kufuata mifumo hiyo.Na hilo ndilo linalochangia kwa kiasi kikubwa kuzusha migogoro na mapigano katika nchi hizo na kusababisha mamia ya watu kujeruhiwa, kuuawa na hata baadhi ya wananchi katika nchi hizo kuhama na kuhamia nchi jirani jambo ambalo linaonesha kuwa hakuna utulivu na amani hukosekana katika nchi hizo.Lakini sio tatizo la viongozi pekee kutokujua uelewa wa demokrasia lakini pia hata wananchi wenyewe uelewa wao bado ni mdogo katika kujua dhana nzima ya demokrasia na utawala bora unaotakiwa kufuatwa ili nchi ziwe na amani lakini nchi nyingi zimefuata mkumbo wa kidunia kuendana na wakati unaotakiwa uwe na mataifa makubwa ambayo huitwa ni vinara wa demokrasia.Tutakumbuka kwamba hapa kwetu tokea kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mwaka 1992 kumekuwepo na matokeo yasioridhisha kuhusiana mivutano na migogoro ya muda mrefu inayotokana na siasa za ushindani na vurugu za hapa na pale.Endelea kusoma habari hii.

ELIMU NI MKOMBOZI WA MAISHA

18 02 2010

ELIMU ndicho chanzo muhimu kitakachomletea maendeleo na ukombozi wa kweli kwa mwanadamu na kitamsaidia kupambana na dunia inayoendelea kwa kasi katika Sayansi na Teknolojia.Katika dunia inayoungana kimawasiliano na kugeuka kuwa chumba, elimu inakuwa nguzo, hazina na daraja litakalomvusha binadamu katika hali yake ya unyoge wa fikra, mawazo na atayatanua maisha yake kuendana na maendeleo endelevu.Elimu ni chimbuko la ukombozi kwa sababu ndiyo inyosaidia kuwafumbua macho wajinga na wakaitumia elimu hiyo kudai haki zao za msingi wanazostahiki, hebu ukumbuke wakati wa nyuma kabla ya nchi zetu za Afrika kupata Uhuru, jinsi wazee wetu walivyokuwa wanafungishwa mikataba ya ulaghai kama ule wa Sultan wa Msovero Tanga na Bwana Karl Peters Mjerumani aliyesifika kwa utesaji wa Waafrika.Wazee wetu wengi walitoa ardhi yao kwa kutojua ama kusoma na kuandika, lakini kutokuwa na elimu ya kutosha kiasi cha wageni walowezi kunyakua ardhi ya Waafrika bila ya ridhaa yao nap engine ufahamu mdogo wa mambo ya mikataba kwani kwa wakati huo wasomi wa Kiafrika walikuwa ni nadra sana.Si dhamira ya makala haya leo kuzungumzia mikataba ya ulaghai, lakini nilikjuwa najaribu kuonyesha jinsi jamii kama ikikosa elimu inavyoathirika na kupoteza rasilimali muhimu katika maisha yao.Ni miaka saba sasa tangu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume alipoanza kuliongoza Jahazi walilopanda Wazanzibari kwa ajili ya safari ndefu ya Maendeleo endelevu ambayo wananchi wameanza kushuhudia Nahodha wa Jahazi hilo kuwafikirha salama katika Bandari ya Wapendanao.Endelea kusoma makala haya

MALALAMIKO YA WALIMU KUSHUNGULIKIWA

18 02 2010

WALIMU wa Zanzibar kwa muda mrefu wanalilia posho la kufundishia la asilimia 25 ambalo waliahidiwa na rais wa Amani Abeid Karume katika kilele cha kusherehekea elimu bila ya malipo zilizofanyika kisiwani Pemba mnamo 2007 lakini ahadi hiyo imekuwa ikipigwa danadana kila uchao.Siku ya walimu huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Octoba 5 kila mwaka ambapo walimu wa Zanzibar waliahidi kuboreshewa maslahi yao ya mishahara na hapo ndipo rais Amani Karume kuwaahidi kuwa atawaangalia zaidi kwa kuongezewa posho la ufundishaji la asilimia 25 kwa kila mwalimu. Baada ya kipindi kirefu kupita mnamo Octoba 2009 baadhi ya walimu hao walikutana na kutoa waraka maalumu ukiwashawishi walimu wote kutia saini waraka huo kama njia moja ya kutaka ahadi hiyo itekelezwe na waweze kupatiwa asilimia 25 ya posho waliloahidiwa.Lakini baada ya kukata tamaa kwa walimu hao sasa wameanza kufurahia kusikia kauli kutoka kwa mwenyewe rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kwamba itatekelezwa hivi karibuni baada ya kukamilika kwa baadhi ya mambo na taratibu ambazo ndizo zilizokuwa zikikwamisha ahadi hiyo ikiwa pamoja na upatikanji wa fedha za kutosha.Katika kilele cha siku ya walimu duniani ambapo sherehe zake zilifanyika Wete Kisiwani Pemba rais wa zanzibar Amani Abeid Karume alisema maslahi ya walimu pamoja na muundo wa kada hiyo sasa utafanyiwa marekebisho makubwa na kuona taaluma hiyo inaheshimika katika jamii kama zamani.Endelea kusoma makala haya.

UKOSEFU WA AJIRA NI TATIZO SUGU AFRIKA

18 02 2010

TATIZO la kukosekana ajira kwa wananchi limekuwa ni jambo la kawaida katika nchi nyingi Afrika hususan hapa kwetu Tanzania pia tunakabiliwa na shida ya wananachi wanaomaliza masomo yao lakini kupata ajira inakuwa ni vigumu sana kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa mipango madhubuti ya serikali katika suala hilo.Watu ambao ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa kukosa ajira ni walimu ambao humaliza masomo yao ya kila mwaka katika fani mbali mbali na ngazi tofauti hutegemea na sehemu husika anayomalizia masomo mwanafunzi huyo.Walimu wa Unguja na Pemba wengi wao hujikuta wakiwa na kukosa la kufanya ama kutafuta kozi nyengine na kubadilisha kada baada ya kumaliza masomo yao ya ualimu kufuatia kukosa shule za kufundishia jambo ambalo lilimsukuma waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman na kutaka waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Tanzania bara kuwachukua walimu wanaohitimu masomo yao ambao bado inatokea hawajapata ajira.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mara kadhaa imekuwa na ukosefu wa walimu wa ngazi tofauti kufuatia walimu wengi wanaomaliza masomo yao kutafuta ajira nje ya nchi au kwenda katika shule za binafsi kutafuta maslahi bora zaidi lakini waziri wa elimu Zanzibar ameshawahi kueleza kwamba iwapo ndugu zao wanahitaji walimu basi Zanzibar wapo na wapo tayari kuwatoa na kwenda kufundisha Tanzania bara lakini kumekuwepo na vikwazo ambavyo havifahamiki vinatokea wapi.Endelea kusoma makala haya.

PAMOJA NA MARIDHIANO, UANDIKISHAJI PEMBA BADO TATIZO 

11 02 2010

wananchi wakiwa wamejiziba nyuso zao

PAMOJA na kuwa maridhiano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa CCM na CUF Zanzibar yameleta matumaini kwa wazanzibari kwamba siasa za chuki sasa zimefikia hatima lakini hali haionyeshi hivyo kwa watendaji wa serikali na baadhi ya wananchi ambao kwa njia moja au nyengine wanaonekana kuendelea kwa makusudi kuweka mbele utashi wao wa kisiasa bila ya kuzingatia nia ya kuweka kuondosha uhasama na kushirikiana kwa maslahi ya Wazanzibari. Nasema hivyo kutokana na hali halisi inaendelea hivi sasa katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaendelea katika mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba ambapo baadhi ya kasoro zilizokuwa zikitokea awali zilipaswa wakati huu kupunguzwa kama sio kumalizwa kabisa. Wakati viongozi wakitaka kufungua ukurasa mpya na kuzika tofauti za kisiasa wananchi walipaswa kuachana na mambo ambayo yanaweza kuhatarisha mazungumzo hayo kwa kufuata taratibu zilizowekwa na tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ili kudumisha amani na kuaminiana katika kipindi hiki ambacho wananchi wanajitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura ili kuonyesha kama kuna dhamira ya kweli ya maelewano.Wakati zoezi la uandikishaji wapigakura likiendelea kisiwani Pemba, siku moja nilikuwa nakwenda Mkanyageni kuangalia zoezi hilo linavyoendelea, njiani katika barabara ya Mtuhaliwa kuelekea Mkanyageni nilikutana na vizuizi vya barabara (road block) ambapo gari nililopanda likasimama ili kukaguliwa.Endelea kusoma makala haya.

SHIDA YA UMEME SASA ITABAKI NI HISTORIA PEMBA

3 01 2010

KISIWANI Pemba kwa miaka mingi wamekuwa wakitumia umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta ya IDO yaani vinu vya umeme, sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kuona umuhimu wa nishati ya umeme na suala zima la kukuza utalii na mpango wa kupunguza umasikini inatekeleza mradi huo mkubwa wa aina yake katika upwa wa Afrika Mashariki.Ni ukweli usiokuwa na ubishi kuwa watu wa Kisiwa hicho kwa miaka nenda kwa miaka rudi, maendeleo kwao yalikuwa ni ndoto tena zile za mchana na za Abunuwasi. Nasema hivyo kwa sababu katika kipindi chote cha tawala zilizotangulia yapata miaka 300 iliyopita watu wa huko wamekosa umeme, wamekosa maji safi na salama na walikosa elimu.Ni miaka ya mwanzoni mwa Utawala wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pale Rais wa kwanza wa Visiwa hivi, marehemu Abeid Amani Karume aliwawahakikishia wakaazi wa Pemba kupata nishati ya umeme .Mengi yalisemwa na wananchi juu ya kuwepo khofu ya kutimizwa ahadi hiyo ya kuhusu suala la umeme wa uhakika Kisiwani Pemba, lakini ukweli utabaki kuwa dhamira ya dhati ya Serikali kwa wananchi wake ndio inayofanya kazi kuona kwamba Pemba inaunganishwa na gridi ya Taifa kutoka Pangani Tanga hadi Wesha Chake Chake Pemba.Wataalamu kutoka Norway waliwasili mwishoni mwa mwaka jana kwa ajili ya kuanza kazi mbapo walifika Mkoani Tanga wakiwa katika Meli yenye vifaa maalum vya kuweka waya kwenye bahari kuanza utafiti wa njia za kupitishia waya huo.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Mwalimu Ali Mwalimu alisema kwamba meli kubwa kutoka Norway ikiwa na timu ya wataalamu iliwasili Mkoani Tanga mwishoni mwa mwaka jana ambapo ilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa na Maafisa wa Shirika la Umeme Zanzibar na TANESCO.Endelea kusoma makala haya.

KIINI CHA MAZUNGUMZO NI MIMI-ALI KARUME

23 12 2009

HIVI karibuni, mahasimu wakubwa wa kisiasa Zanzibar, Rais Amani Karume ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani), na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad waliamua kuweka kando tofauti zao na kukutana kwa mazungumzo ya amani yaliyopewa jina la maridhiano.Wakati wananchi wengi wakijiuliza nani mwanzilishi wa usuluhishi huu ambao dhahiri umeonekana kuwa na manufaa makubwa zaidi kulinganisha na jitihada nyingine za kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa Zanzibar, amejitokeza mwanadiplomasia akisema kwamba yeye ndiye kinara wa mazungumzo hayo.“Sitaki kujisifu lakini mimi najiona kama ni mkunga wa mtoto huyu (maridhiano) aliyezaliwa maana miaka miwili iliyopita niliyasema hayo yaliyofanyika Novemba 5 mwaka huu ya kukutana kwa Rais Karume na Maalim Seif,” anasema Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume.Amesema mazungumzo kati ya Rais Karume na Maalim Seif Hamad hayana tofauti na mtoto mchanga aliyezaliwa ambaye atahitaji malezi mema na mazuri kutoka kwa wazazi wake ili aweze kukuwa katika hali nzuri.Anasema ndoto yake sasa itakuwa imetimia kwani siku zote alikuwa akiota suala hilo la kuwepo kwa maelewano ya Wazanzibari bila ya kujali itikadi zao za kisiasa kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo wao wenyewe wanahitajika kuyafanya ambayo yanahitaji ushirikiano.Endelea kusoma makala haya

HATUTAKI CHOKOCHOKO-FEROUZ

18 12 2009

CHAMA cha mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kuanzishwa kwa mazungumzo ya pande mbili zinazovutana ni sawa na ujenzi wa reli ambayo treni yoyote inaweza kupita katika njia hiyo.“Rais Karume yeye amejenga njia ya reli kwa hiyo sio kwa kuwa amejenga yeye tena treni nyengine haiwezi kupita katika njia hiyo laa yeye ameanzisha ujenzi tu wa hiyo njia lakini treni yake au treni nyengine zitakuwa zinapita katika njia hiyo” ametoa mfano huo Naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz. Alisema mazungumzo ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif yaliofanyika novemba 5 mwaka huu ni ukurasa mpya ambao umefungua njia ya watu kukaa pamoja na kuzungumza jambo ambalo halikutegemewa.“Kila jambo lina chanzo chake na chanzo la haya maridhiano ni katibu mkuu wa CUF Maalim Seif kumuandikia barua mheshimiwa rais kutaka kuonana naye na yeye hakurudi nyuma akaipokea na kumwimbia njoo kwa hivyo hicho ndio chanzo” alisema.Na katika chimbuko la ugomvi ni vizuri likafanywa suluhu na wenye kugombana kwani wazanzibari wenyewe waligombana hivyo sasa wameona kuwa wamechoka kugombana na wanataka kukaa pamoja na kuelewana lugha jambo ambalo Ferouz anasema liungwe mkono na kupewa moyo viongozi hao.Endelea kusoma makala haya.

RIPOTI YA HAKI ZA BINAADAMU YAZINDULIWA

9 12 2009

Hivi karibuni Kituo Cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kilizindua ripoti yake ya Haki za Binaadamu ya 2006 katika kitabu kimoja ambapo kilibeba ripoti mbili moja ya Tanzania Bara na nyengine ya Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kutayarishwa ripoti ya aina hiyo.Katika hafla hiyo, ambayo ilitarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora, Ramadhani Abdallah Shaaban lakini kwa bahati mbaya hajahudhuria na wala hakuleta mtu wa kumuwakilisha mtu katika uzinduzi huo ambao ulikuwa na faida kubwa khasa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Katika ripoti hiyo ambayo hakuwepo kiongozi hata mmoja wa serikali wala mtu aliyewakilishwa kutoka SMZ licha ya kupewa mialiko kadhaa kwa wahusika kumetafsiriwa na washiriki wa uzinduzi huo kwamba serikali ya SMZ haikuridhishwa na ripoti hiyo na khasa kwa vile baadhi ya viongozi wa SMZ walishindwa kutoa ushirikiano katika mchakato mzima wa utayarishaji wa ripoti hiyo.Washiriki wa uzinduzi huo baadhi yao walisema wazi wazi kwamba serikali ya SMZ haikuridhishwa na jambo hilo la kuandikwa ripoti ya Haki za Binaadamu kutokana na kufahamu kwao kwamba baadhi ya vyombo vya dola ndio watekelezaji wakubwa wa ukiukwaji wa haki za binaadamu nchini.Endelea kusoma makala haya.

UHURU WA HABARI ZANZIBAR BADO NI NDOTO

8 12 2009

“Tunao uhuru lakini bado tunayo matatizo, hasa Zanzibar safari ya kuelekea kwenye uhuru wa habari haijaanza kwa waandishi wa habari kule Zanzibar.Waandishi wa habari wa Tanzania Bara angalau wanapigani haki zao,wanajaribu, wanathubutu lakini Zanzibar bado kugumu.”Hayo ndio maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Anthony Ngaiza wiki iliyopita katika mahojiano na Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (D.W) Mohammed Abdulrahman wakati akitathimini uhuru wa vyombo vya nchini Tanzania ambapo siku ya leo huadhimishwa duniani kote.Nakubaliana na mawazo hayo ya Ngaiza khasa nilikinganisha na tukio la wikimbili zilizopita waandishi wa habari Zanzibar walipopata pigo kubwa la kukandamizwa tena kwa kutungiwa sheria ambayo itazidi kuwabinya na
kuwakosesha fursa ya uhuru wao wa kufanya kazi kwa upeo bila ya kuingiliwa uhuru wao.Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hivi karibuni imepeleka katika kikao cha Baraza la Wawakilishi mswaada wa Uwezo Kinga na Fursa za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambapo wandishi wa habari nao wataathirika katika mswaada huo.Waandishi wa habari wa Zanzibar baada ya kupata nakala za mswaada huo hawakuwa nyuma walijikusanya haraka na kuujadili baadhi ya vifungu vinavyowatia kitanzi na hapo hapo walifanya maamuzi ya kumwandikia barua Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir Kificho na kuzisambaza kwa wajumbe wote.Endelea kusoma makala haya.

MARIDHIANO YALETE TIJA NA MAFANIKIO

7 12 2009

NOVEMBA 5 mwaka huu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad alikwenda Ikulu ya Vuga Mjini Zanzibar na kuzungumza na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume mazungumzo ambayo yameelezwa kuwa yenye nia ya kuleta ushirikiano na kufungua ukurasa mpya wa mazungumzo katika kujenga Zanzibar yenye amani.Katika mazungumzo yao ya faragha viongozi hao ambayo yalichukua saa mbili wakiwa wamejifungia na kuteta huko ndani tunaambiwa yamepewa jina la MARIDHIANO na sio Mwafaka ule tuliouzowea kama kawaida ya miafaka mengine iliyowahi kuafikiwa hapa kwetu Zanzibar.Viongozi hao katika mazungumzo yao wamegusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote wanaoishi katika visiwa vya Unguja na Pemba. Tumeelezwa kwamba viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa. Jengine lililozungumzwa na viongozi hao na kuarifiwa kwa ufupi ni kwamba wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo. Ikiwa pamoja na kuahidiwa kuwa mchakato wa mazungumzo hayo kuwa endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla.Naam ni maneno mazuri, matamu na yenye matumani makubwa katika maisha ya binaadamu na kwa kila mpenda amani ambaye atasikia maneno haya atasema sasa wazanzibari wamefika pale walipokuwa wanataka wafike katika kukaa kujadili na kuzungumza lugha moja ambayo inahimiza mashirikiano na umoja wa kujenga nchi kwa pamoja na kuweka kando tofauti za kisiasa.Endelea kusoma uchambuzi huu

PIYDO IMETUKOMBOA- WANAWAKE PEMBA

3 12 2009

MPAKA ulipokuja mradi wa stadi za maisha uliokuwa ukitekelezwa na Pemba Investiment and Youth Development Organization (PIYDO) bi Sabiha Muhsin Said, mkazi wa Jadida Wete.- Mkoa wa Kaskazini Pemba Alikuwa akijihesabu zaidi kama mama wa nyumbani. Mchango wake mkubwa aliodhani anaweza kuutowa kwa familia yake ilikuwa ni kufanya kazi za nyumbani kama vile kuweka usafi wa nyumba, kupika, kuchota maji na kuwashughulikia watoto. Hata hivyo mwaliko wa kuhudhuria mafunzo ya siku tano ya stadi za maisha yaliyolenga kuwasaidia wananchi wa kisiwani Pemba mbinu za kukabiliana na ukali wa maisha yalibadili mwelekeo wote wa maisha wa mama huyu wa watoto wa tano. “sasa najiona kabisa kuwa nami inamchango ninaoweza kutoa katika kuendesha maisha yetu, si yule bi Sabiha wa zamani” alisema bi sabiha.Akielezea hadithi nzima ya kubadilika kwa mwelekeo wa maisha yake anasema kuwa wakati wa kuhudhuria mafunzo hayo walifundishwa mbinu mbali mbali wanazoweza kuzitumia kujiongezea kipato na aina ya miradi ambayao wanaweza kuitekeleza. Anasema mafunzo pia yaliwajenga moyo na ujasiri wa kuanzisha miradi yao wenyewe, Bi Sabiha anakumbuka kuwa walipomaliza yeye na wenziwe wengine kumi waliohudhuria mafunzo hayo waliamaua kuanzisha kikundi cha ushonaji charahani na ufumaji hapo kwao Wete.“Japo wazo la kuanzisha kikundi lilikuwa la kwetu wenyewe lakini tulikuwa tumejaa woga iwapo tutaweza kweli. Tukijitizama kuwa tulikuwa wanawake watupu tuliona kuwa kulikuwa na kazi kubwa mbele yetu ila tukajipa moyo” alisema.Endelea kusoma makala hii

KARUME- TUSAHAU YALIOPITA TUGANGE YAJAYO

24 11 2009

KAULI muhimu iliyokuwa ikitakiwa na kusubiriwa kwa hamu na wananchi wengi wa Zanzibar kutoka kwa Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kuhusiana na mazungumzo ya Rais Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad imetolewa huku maelfu ya wazanzibari wakiwa wamemiminika katika viwanja vya Demokrasia eneo la Kibanda Maiti kusikiliza mkutano wa hadhara uliofanyika nyakati za jioni.Novemba 5 mwaka huu viongozi hao walikutana Ikulu katika mazungumzo yao ya faradha ambayo yalichukua takriban masaa mawili wakipanga na kubadilishana mawazo mbali mbali juu ya mustakabali wa kisiasa katika visiwa vya Unguja na Pemba. Tayari Chama Cha Wananchi (CUF) kilishawatangazia wafuasi wao juu ya mazungumzo hayo lakini Chama Cha Mapinduzi kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu ili kitoe kauli kama hiyo ambayo imeelezwa ina nia ya kumaliza uhasama na chuki za kisiasa Zanzibar.Katika umati mkubwa uliokusanyika katika viwanja vya Demokrasia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume ameeleza kwa undani yaliyojiri katika mkutano kati yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na kuwaomba wafuasi wa CCM kukubaliana na suala hilo ambalo lina faida kubwa kwa kuelekea katika kuijenga Zanzibar mpya na yenye matumaini kwa wote.Rais Karume alianza hutuba yake kwa kukitaka kikundi kimoja cha muziki kurejea wimbo mmoja unaosema: “Kukupenda wewe inawachoma” jambo ambalo lilitafsiriwa na watu kuwa kitendo cha yeye kukutana na Maalim Seif na kukubaliana kufuta tofauti zao hakikufurahisha baadhi ya watu.Endelea kusoma makala haya.

TUMEONA NJIA TUPITAYO SIYO-MAALIM SEIF

18 11 2009

HAKUTARAJIA, lakini ilitokea. Kama ambavyo wananchi hawakutarajia kumsikia Maalim Seif Sharif Hamad kuzungumza vile alivyozungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa uliofanyika Novemba 8 katika viwanja vya Kibandamaiti ambapo umati wa wafuasi na wapenzi wa Chama Cha Wananchi CUF walihudhuria kumsikiliza kiongozi wao.Shauku yao kubwa ilikuwa kusikia nini walizungumza na Rais wa Zanzibar, Amani Karume alipokwenda kumtembelea Ikulu, Novemba 5. Maalim Seif kwa kujiamini kabisa alieleza yaliyojiri na kwamba Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililokutana mjini Zanzibar hivi karibuni limeamua kumtambua Karume.Dah! Ni heshima tu ndiyo iliyowazuia wafuasi kuvurumisha mawe, lakini maneno yaliyowatoka, yalitosha kumhuzunisha Maalim Seif. Katika mkutano huo ambao tofauti sana na mikutano mengine ambayo huanza kwa burudani za muda mrefu na baadaye viongozi mbalimbali wa CUF kupanda jukwaani na kuleta vibwagizo kadhaa wa kadhaa lakini siku hiyo hali ilikuwa vyengine kabisa. Aliyeanza kupanda jukwaani alikuwa ni msomaji wa dua ya kufungulia mkutano baadaye kukaribishwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma, Salim Bimani ambaye kama kawaida yake huutayarisha umma ili masikio na mawazo yao yote yawe katika mkutano huo. Bimani anapopanda jukwaani huwa ana maneno yake anayoyatumia ambayo mengine ni vichekesho na mengine ni kejeli kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mfano wa maneno hayo ni kuwa tumechoshwa na serikali hii ya Chai Jaba (Rais Karume).Endelea kusoma makala haya.

NCHI SIO YENU -WACHENI KUPOTEZA FEDHA

13 11 2009

KWA takriban wiki sasa kumekuwepo na malalamiko mengi ya wananchi kadhaa katika kila sehemu ya nchi hii kutokana na serikali kuvumbua ghafla ziara za Mawaziri, Manaibu na wasaidizi wao kuzunguka katika mikoa ya Tanzania kufafanua Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2007/2008 iliwasilishwa katika kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miezi minne iliyopita.Wananchi wengi wanaona jambo hilo halina umuhimu mkubwa kwao na ni kutumia vibaya fedha za serikali ambazo zinatokana na walalahoi jambo ambalo fedha zingeweza kupelekwa katika huduma za kijamii kama mahospitali, mashuleni na kazi nyengine muhimu ambapo baadhi ya sehemu zinakosekana huduma muhimu za wananchi.Inakisiwa kuwa Mawaziri na Manaibu wao 60 pamoja na maafisa wao na madereva wapo mikoani wakizunguka na waheshimiwa ambao jumla yao ni 181 wanaolipwa kwa fedha za wavuja jasho kwa kiwango kikubwa huku maafisa wakipatiwa kila mmoja kati ya 45,000 hadi 55,000 kwa siku.Posho za Mawaziri na Manaibu ni kubwa kutokana na nafasi zao lakini pia gharama zao za usafiri wa ndege zinakisiwa kuwa ni 400,000 kwenda na kurudi katika baadhi ya mikoa huku gharama nyengine za mafuta ya gari na ngarama nyenginezo zikiwa zimebaki bila ya kujulikana ni kiasi gani.Hizi ni fedha nyingi sasa kwa Taifa la Tanzania ambalo ni tajiri kinadharia lakini ni maskini kupindukia ambapo baadhi ya wananchi wanashindwa kumudu hata mlo mmoja kwa siku.Endelea kusoma uchambuzi huu.

HALI HALISI YA TAKA ZANZIBAR

13 11 2009

Taka ni tatizo moja lenye kuleta mashaka duniani kote na kuzidhibiti kwake takataka zilizotapakaa katika manispaa ya mji wa znztatizo kubwa kwa kuzingatia kuwa kila siku mwanadamu anapokuwa yuhai ujuwe kuwa anazalisha kiwango fulani cha taka ikiwa taka ngumu (solid waste) au taka za maji machafu (liquid waste). Suala la ukusanyaji wa taka na uangamizaji wake ndio jambo kubwa, nchi nyingi duniani hasa nchi za ulimwengu wa tatu au tuziite nchi zinazoendelea. Inafahamika kuwa katika nchi nyingi za ulimwengu wa tatu inakadiriwa tu kila mtu mmoja anazalisha kiwango cha kilo mbili hadi tatu kwa siku za taka ngumu na kiwango cha lita ishirini za maji machafu kila siku, nchi zilizoendelea kwa siku mtu mmoja huzalisha baina ya kilo tatu hadi sita za taka ngumu na lita mia za maji machafu kwa mujibu wa takwimu za kimataifa.Chochote kile ukitumiacho na kisha kukitupa huwa ni taka na ndio maana taka ni moja ya nyenzo inayozalishwa na mwanadamu kwa wingi kila siku duniani kote.Mara nyingi watu hujiuliza kazi kubwa ya Manispaa ni kitu gani? Manispaa takriban zote duniani kazi zao kubwa ni kuangalia maeneo yao ya Manispaa katika kuweka hali ya usafi, kushughulikia miundo mbinu, taa za barabarani, taa za kuongozea magari nk.Na kiongozi wa Manispaa au Baraza la Mji ni huitwa MEYA huwa ni mtu ambaye ndio mwenye mamlaka makuu ya kuuangalia mji, na Serikali kuu, kazi yake ni kumsogezea hiyo miundo mbinu na Meya kufanya kazi zote za kuratibu ikiwemo kutunga sheria ndogondogo (kanuni) kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa.Endelea kusoma makala haya

MIFUKO YA PLASTIKI ADHA AU FARAJA?

13 11 2009

1Inabidi tuielewe plastiki kabla hatujaichambua athari zake katika mazingira. Plastiki ni mabaki ya malighafi ya mafuta na tunaweza kusema kuwa plastiki ni mkombozi kwani hii dunia yenye idadi ya watu wasiopungua bilioni 6 ambao wana mahitaji ya vitu mbalimbali ikiwemo kamba, mabodi mbalimbali ikiwa ya gari, computer, meza, vitu vya kuchezea watoto na mengi mengineo vyote hivyo asilimia Kubwa hutegemea plastiki. Tunaelewa kuwa katani ndio ilikuwa ikitoa kamba na kamba za katani zilikuwa nzuri, lakini tusisahau kuwa katani ni mti ambao hukuwa kisha ukabidi kuvunwa lakini kwa sasa kamba nyingi tuizitumiazo ni za nayloni ambazo hutokana na plastiki na kama nilivyokwisha kusema hapo mbele kuwa plastiki ni mabaki ya mwisho yanayotokana na malighafi ya mafuta na kupatikana na ufanyaji wake ni upo rahisi kabisa.Inaweza kusema maelezo haya ni kitendawili lakini hichi sio kitendawili ila ni lazima tuangalie pande mbili za fedha na kuweza kuzitia kwenye mizani.Hivi sasa duniani kote kunasumbuliwa na utumiaji mbaya wa plastiki, ambapo plastiki zinapoingia kwenye mazingira yetu huleta maafa mbalimbali. Nchi zilizoendelea wamebahatika kwa kiasi kikubwa kutokana na nguvu za kiuchumi kuweza kutengeneza mitambo ambayo husadia kuzibadilisha plastiki na kuzitumia kwa mara nyengine na nchi kama Cambodia na Vietnam wao kwa upande wao mabaki ya plastiki hutengeneza viungo bandia. Jee visiwani Zanzíbar na kadhia ya Plastiki ikoje?Endelea kusoma makala haya.

USANII USAIDIE JAMII -MOHD ILYAS

“LAZIMA  tuwe makini katika usanii kwa sababu tunaweza tukasababisha janga katika nchi. Wenzetu Burundi na Ruwanda tumesikia na kushuhudia yaliowakuta na yote yalisababishwa na baadhi ya wananchi wa nchi hiyo hiyo kuchochea na hatimae kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mohdwasanii nao walichangia kwa kiasi fulani katika vita vile” hivyo ndivyo alivyoanza Gwiji la Muziki wa Taarab visiwani Zanzibar Mohammed Ilyas.“Nyimbo kama inayotumika katika majukwaa ya kisiasa ‘Wasohana wana mji wao’ ina lengo la kuwagawanyisha wananchi wa Unguja na Pemba hiyo haifai katika jamii ya wazanzibari ambao tayari ni ndugu wa damu lakini vyombo vya habari vya serikali wanashadidia kuipiga nyimbo hiyo kila mara unapofungua radio utaisikia wakati hakuna asiyejua kama nyimbo hiyo ina mashairi ya kuwabagua watu” Alisema.Alisema sanaa ni kuelimisha jamii na kuwakewa pamoja na sio kuwatenganisha, alisema ikumbukwe kwamba wasanii wana jukumu kubwa katika jamii na wasipokuwa makini wanaweza kuitumbukiza nchi katika dimbwi la mapigani vita na ubaguzi ambapo athari zake ni mbaya zaidi katika nchi.Alisema wasanii wana mchango mkubwa katika nchi khasa katika nchi ambazo hazina amani wasanii wanatakiwa kutumia fani zao kwa kuhamasisha jamii waishi kwa amani na utulivu.Mohammed Ilyas ni muimbaji maarufu ambaye anajulikana kama Professa wa muziki wa taarab ya asili ambaye amezaliwa katika Mtaa wa Vikokotoni Mjini Zanzibar mwaka 1942 na kupata elimu yake ya msingi skuli ya Darajani hadi darasa la nane.Endelea kusoma makala hii.

UBAKAJI WA WATOTO KWA ZNZ NI TATIZO SUGU

mttKATIKA hali ya kawaida si rahisi mtu yoyote kuamini kuwa tatizo la unyanyasaji wa watoto Zanzibar ni kubwa kwa vile ni imani ya wengi kuwa visiwa hivi vina watu wenye imani kubwa ya kidini na pia utamaduni unaojali mapenzi ya watu na hasa watoto.Lakini Mwandishi wa habari na mwana harakati wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Shifaa Said Hassan anaelezea namna gani tatizo hili lilivyo kubwa kwa kutoa takwimu za maovu hayo dhidi ya watoto, “Mwaka juzi utafiti ulionyesha kuwa kulikuwa na matukio 800 ya unyanyasaji wa watoto na kati ya yote hayo hakuna hata moja ambalo hukumu yake imepatikana.”Tafsiri ya kauli hii ni kuwa kuna kazi kubwa mbele hata kama kuna juhudi ambazo zimeshaanza kuchukuliwa na taasisi mbali mbali ziwe za Kiserikali au za Kiraia.Ushahidi unaonyesha kuwa matukio hayo hayana mipaka katika visiwa hivi kimaeneo, umri, jinsia na wala aina ya watoto ambao wanafanyiwa ukatili huo, wakiwamo wale ambao ni walemavu wa akili, kama ambavyo utafiti wa makala hii ulivyogundua wasichana kadhaa wenye ulemavu wa akili wanavyofanywa kuwa ni kimbilio la wabakaji kama ambavyo msichana mmoja eneo la Mwembe Makumbi, Mkoa wa Mjini Magharibi alivyonielezea mama yake jinsi alivyotendewa unyama na mwanamme mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 majira ya saa 1.30 usiku.Endelea kusoma makala haya.

PROF. HAROUB HAJAFA, AMETUTANGULIA TU

SIJAWAHI kufanana nae kwa hali yoyote. Tulikuwa tumepishana kiumri kiasi mimi ni wa kizazi chengine na yeye wa chengine kabisa na hilo kwa siasa na hali ya kijamii ya Zanzibar ni muhimu sana. Sina sifa ambazo professor%20Haroub%20Othmanzinaweza kumfikia kwa namna yoyote ile. Mimi ni kichuguu na yeye ni mlima. Kama walivyo watu wengi wa kizazi changu waliowahi kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaa, Profesa Haroub alikuwa mwalimu wetu. Na ndie yeye aliye tuendesha tata ya uchambuzi wa masuala ya siasa na jamii. Tunamkubuka wengi alivyokuwa akijiamini kwa kuingia kutoa mihadhara akiwa na kipande cha karatasi lakini mambo yakatiririka kama maji katika mlima. Sehemu kubwa ya maisha yangu nilikuwa natamani kuwa kama yeye mpaka pale ndoto zangu zilisokotwa na maamuzi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuninyima fursa ya kupata digrii yangu ya pili ya sheria hata baada ya kukamilisha kuandika kazi yangu mwaka 1996. Kwa hivyo sitakuwa professa kama alivyokuwa Profesa Haroub. Endelea kusoma makala haya.

MWANAFUNZI HUMSHINDA MWALIMU

karume&railaUCHAGUZI Mkuu uliofanyika hivi karibuni Nairobi Kenya umemalizika huku Rais Mwai Kibaki akirejeshwa tena madarakani kumaliza miaka yake mitano uchaguzi ambao uligubikwa na malalamiko kadhaa wakadhaa. Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Kenya (ECK) Samuel Kivuitu kwenye Ukumbi wa KICC Jijini Nairobi, alimtaja Kibaki kuwa mshindi kwa kupata kura 4,584,721 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Raila Odinga wa Orange Democratic Movement (ODM) aliyepata kura 4,352,993 huku Mgombea Chama Cha ODM- Kenya, Stephen Kalonzo Musyoka akiambulia kura 879,093. Mwenyekiti huyo wakati akiendelea kutangaza matokeo ya urais ya Jimbo la Kajiado hali ilianza kubadilika ambapo baadhi ya wananchi walianza kumzomea na kufanya vurugu jambo ambalo lilisababisha Polisi kulazimika kuingilia kati na kumtoa nje ya ukumbi huo Mwenyekiti huyo kutokana na hali ya usalama kutoweka ukumbini hapo. Waandishi wa Habari na wanasiasa hawakuruhusiwa kuingia tena ndani ya ukumbi huku Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) ndilo lililoruhusiwa kuingia wakati Mwenyekiti huyo akimtangaza Kibaki kuwa mshindi wa kinyanyanyiro hicho cha uchaguzi. Pamoja na malalamiko mengi yalioelekezwa kwa Tume ya Uchaguzi Kenya (ECK) kulalamikiwa kuchelewesha matokeo hayo huku shutuma za wizi wa kura zikitajwa ndio zilizochangia kuzorotesha matokeo kuchelewa. Endelea kusoma makala haya.

SERIKALI IWEKE MIKAKATI MADHUBUTI

TAKRIBANI mwezi sasa wakaazi zaidi ya 10,000 wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na mazao yao kuathirika na hali ya hewa ya kiangazi iliyosababisha wananchi kuteremka mashambani na kutafuta chakula aina ya chochoni ambacho kinaweza DSC00530kuhatarisha maisha ya walaji kisipotengenezwa vyema. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuthibitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Abdallah Ali Juma zinasema kwamba tatizo hilo linatokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo kila mwaka tatizo hilo hujirudia kutokana na hali halisi ya ardhi ya Mkoa huo pamoja na mazao kushambuliwa na wadudu. Naye Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kongozi, Machano Othman Said katika ziara yake hivi karibuni alipotembelea Mkoa huo na kujionea hali halisi ya maisha wanayoishi wananchi wa Micheweni ambapo alithibitisha kuwepo upungufu wa chakula pamoja na kuvitaja vijiji sita ambavyo vinakabiliwa zaidi na tatizo hilo na kuahidi baada ya kukusanya ripoti kamili wananchi wa Mkoa huo watasaidiwa kupatiwa msaada wa chakula na serikali. Endelea kusoma uchambuzi huu.

ZNZ BADO KUFIKIA DEMOKRASIA YA KWELI

salma21KATIKA siku za hivi karibuni kuna kauli imetolewa na Kiongozi wa ngazi za juu katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambayo ina maswali mengi ya kujiuliza hasa kwa kuwa kiongozi huyo amenukuu maneno ambayo yana faida kubwa katika jamii yetu kupitia uchambuzi huu nataka kuigusia kidogo na kuichambua hutuba yake hiyo kwa faida ya watanzania wenzangu. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha wakati wa uzinduzi wa jumuiya ya wahitimu wa chuo cha demokrasia Zanzibar ambapo Nahodha alipingana na wasomi wenzake wengi wanaosema kwamba tatizo la Zanzibar linatokana na historia na ninamnukuu “Wapo wanaosema hali hii ni matokeo ya historia ya Zanzibar. Wakati wa kudai uhuru hali ya Zanzibar ilitawaliwa sana na siasa za kitabaka na baada ya kuja mfumo wa vyama vingi vya siasa vikaathiri mitizamo na itikadi ya vyama vya zamani ikiwemo A.S.P na Z.N.P”. Nahodha aliendelea kusema kuwa watu wanaweza kuendeleza historia kwa mabaya lakini pia wanaweza kuitumia hostoria kwa kujenga umoja na mshikamano ambao ndio muhimu katika taifa lolote duniani huku akitoa mifano ya nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ambazo nazo ziliingia madarakani baada ya kuwapindua watawala wa kikoloni waliowakuta kama ilivyotokea kwa Zanzibar. Endelea kusoma uchambuzi huu.

TUKUMBUKE LENGO LA MUASISI WETU

WAKATI leo tunaadhimisha siku muhimu ambayo wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba waliweza kujikomboa kutoka mikononi mwa watawala wa wa kisultani na kukabidhiwa madaraka ambayo hadi leo yamo mikononi mwa waafrika kuna mengi ya kuyatafakari na kutathmini juu ya siku hii ya leo ambayo mnamo Januari 12 mwaka 1964 wazanzibari walifanya Mapinduzi. Katika tafakuri hiyo tusisahau lengo na madhumuni ya kufanyika Mapinduzi ambapo utawala wa kisultani ulijikita zaidi katika kutoa huduma kwa wananchi walio wachache huku masikini walishindwa kupata elimu ya juu kutokana na hali zao duni, huduma za umma zikitolewa kwa watu maalumu pamoja na ardhi kumilikiwa na wachache. Kuwepo kwa kundi la walio nacho na wasio nacho pia ni tatizo jengine ambalo lilikuwa likitawala jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wananchi kujiona wanyonge katika nchi yao hali iliyoyochechea harakati za kufanyika Mapinduzi sanjari na kuwepo usawa na umoja. Waafrika baada ya kuona hali hiyo ikiendelea waliamua kukamata silaha na kuuondosha utawala huo ambao ulijikita kwa miongo kadhaa visiwani hapa ambapo wazalendo walikataa kuona wacheche wakifaidi huku walio wengi wakiteseka kwa kuonekana watumwa. Endelea kusoma uchambuzi huu.

SUALA LA VYETI FEKI NI KIINI MACHO TU

DSC04833MCHAKATO wa kubaini wafanyakazi waliopata ajira kwa kutumia vyeti vya kughushi ulioanzisha Baraza la Taifa Mitihani Tanzania unaweza kupata kikwazo katika taasisi vyeti hasa za ulinzi kama vile Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Polisi amapo haikuelezwa pia kama mchakato huo utawahusu watumishi hao. Tatizo la kughushi kwa vyeti linaonekana kushika kasi katika asasi nyingi hapa nchini ambapo mtu mwa mfano wazazi wake wamemuita kwa jina la Omar lakini kazini kwake anatumia kwa jina la Joseph hivyo mkanganyiko huo wa majina husababisha hata wana familia kushindwa kuelewa anapofanya kazi mtoto wao. Vyeti vingi ikiwemo ile ya kuzaliwa pamoja na kumalizia masomo vimekuwa vikitumika kujipatia ajira kwa njia ya udanganyifu huku wahusika wakipandishwa vyeo katika taasisiz ao wakiamini kuwa wana ujuzi wa fani husika. Shaka iliyopo sasa na swali amablo wananchi wengi wanaulzia jee Barala hilo la Mitihani litakuwa wa ubavu wa kuwanasa kadi watoto wa vigogo au itakuwa ni watoto wa walala hoi tu ambao watafukuzwa kazi kwa kukutikana na vyeti vya kughushi. Endelea kusoma uchambuzi huu.

WANANCHI WANAHITAJI HUDUMA BORA

TAKRIBAN siku 24 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, alipiga kambi Kisiwani Pemba katika ziara ya kutembeleamaalimseif majimbo yote ya kisiwani hicho akikagua uhai wa chama hicho pamoja na kusaka wanachama wapya ambapo kwa muda mrefu hajaonekana kisiwani humo kutokana na kushughulikia mazungumzo yanayoendelea ya mpasuko wa kisiasa Zanzibar kati CCM na CUF. Katika ziara hiyo alifanya mikutano kila wilaya huku akihitimisha mkutano mkubwa uliofanyika Chokocho Jimbo la Mkanyageni bahati nzuri nilikuwa miongoni mwa waandishi waliokuwepo uwanjani na kusikia kila kilichozungumzwa hapo. Maalim Seif alipiga siasa kwa kukabidhiwa na viongozi wa chama hicho funguo za majimbo yote ya Pemba na kuondoka nazo ufukoni huku akiahidiwa ngome yake kutovunjwa na chama chochote. Nauliza hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina ubavu? Mimi nawashauri CCM watafute master keys waende Pemba kufungua majimbo yote wayachukue mbona ya Unguja waliweza kwa nini washindwe na ya Pemba kuna nini huko?. Endelea kusoma makala haya.

MBINU ZA KUPATA KURA ZIPO NYINGI

hamad masauniMWANZONI mwa mwezi huu wananchi wengi wa Tanzania walikuwa wakifuatilia kwa karibu sana kile kilichokuwa kikiendelea kujiri katika Mji wa Dodoma ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanya mkutano wake mkuu wa nane wa kuchagua wagombea wapya watakaoshika nafasi za Halmashauri Kuu ya chama hicho. Mimi ni miongoni mwa Watanzania waliokuwa wakifuatilia kwa makini juu ya uchaguzi huo tokea kuanza kwa heka heka za kampeni ambapo nilishuhudia mwenyewe baadhi ya wagombea wakiwemo mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliofika Visiwani hapa tulionana uso kwa uso sehemu tofauti wakiwa na wenyeji wao wakiwaongoza kwa wapiga kura ili wawasaidie kuungwa mkono na wajumbe wa Unguja na Pemba. Katika heka heka hizo wengine walitumia njia ya safari za kwenda mikoa ya Tanzania bara na kuzunguka huku na kule na wengine walikuja Zanzibar wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kufutarisha waumini wa dini ya Kiislamu na wengine hawakusafiri walitumia mitandao ya simu kwa kutumiana sms kwa wajumbe na kuomba kura zao. Endelea kusoma makala haya.

MJI MKONGWE ZNZ NI HIFADHI YA KIMATAIFA

Zanzibar Photos 235[1]MJI Mkongwe wa Zanzibar umeingizwa katika hifadhi ya urithi wa kimataifa miaka saba iliyopita ambapo hivi sasa inaonekana baadhi ya masharti yaliotolewa bado hayajatekelezwa ipasavyo jambo linalotishia kufutwa katika hifadhi hiyo kutokana na kuzorota kwake katika utekelezaji. Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ilianza katika mwaka 1985 kama taasisi ndogo ambayo haina sheria wala mipango ya uhifadhi mji ambapo wazo la kuanzishwa kwa chombo kama hicho lilikuja baada ya baadhi ya majengo ya mji huo kuanguka chini huku mengine yakiwa na nyufa za ukutani kutokana na uchakavu wa majengo hayo na serikali kushindwa kuyafanyia matengenezo kwa muda mrefu. Mji Mkongwe eneo la mraba ni hekta 125 ina jumla ya wakaazi 16,000 na watuamiaji wa mji huo ni 100,000 usanifu wake una athari kutoka Uarabuni, India Afrika na Ulaya. Mkurugenzi wa Mji Mkongwe Issa Sariboko Makarani alisema baada ya kuonekana umuhimu wa kuwepo chombo ambacho kitaratibu na kushungulikia Mji Mkongwe Timu ya wataalamu walipeleka ombi Serikalini kwa kuanzishwa chombo hicho na serikali haikurudi nyuma iliamua kuchukua juhudi za makusudi kuanzishwa chombo hicho cha kuratibu mwenendo wa uhifadhi ya mji mkongwe ambapo suluhisho la kuyafanyia ukarabati majengo yalioporomoka na kuanza kuyatunza kwa lengo la kuwaweka wakaazi wa Mji huo katika hali ya amani kutokana na khofu iliyowakumba wakaazi hao kutokana na ubovu wa majengo ya nyumba hizo lilipatikana. Endelea kusoma makala haya.

WATAALAMU WA MAZINGIRA HAWAHESHIMIWI

WATAALAMU wa mazingira husema kwamba mazingira hayana mipaka, kwani mazingira yana sehemu zake kuu nazo ni ardhini, baharini na angani, nako huko kote mazingira huwa yana kazi zake maalumu, wataalamu pia PICT0330husema kuwa hayatakuwepo mazingira ikiwa uhai unakosekana na hiyo ni kujenga dhana kuwa kwenye sayari zote zijulikanazo ukiitoa sayari ya dunia (earth) mazingira huwa hayapo, mazingira yanapatikana kwenye sayari waishao wanaadamu. Nani ahusishwe na nani mwenye dhamana wa mazingira hili ndio suala ninaloliangazia leo katika makala haya.  Mazingira kwa Zanzibar idara yenye kuhusika ipo chini ya Wizara ya Kilimo, vilevile kuna taasisi ambazo zingekuwa bora zikafanywa kuwa ni sehemu ya idara ya mazingira ili kuweza kutekeleza uhifadhi wa mazingira visiwani na kuweza kupatikana kwa maendeleo endelevu, sehemu hizo ni misitu, uvuvi, nishati, maji pamoja na utalii kwani mazingira yalipo yanashindikana kudhibitiwa. Eneo kuu la mazingira nalo ni ardhi tunayoishi (land/terrestrial). Ardhi ni eneo ambalo haliongezeki huwa linapungua siki hadi siku kutokana na kukosekana kuwepo mpangalio madhubuti wa udhibiti na mipango ya ardhi iliyojengeka kisheria (land use plan), ukosekanaji wa hayo huwa ni janga kwenye taifa lolote lile na hili ndilo linaloendelea hivi sasa visiwani. Endelea kusoma makala haya.

MFUMO WA SERIKALI MBILI SIO MBAYA -DK. ADOLF

MWALIMU Dk. AdolfJulius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume ni Waasisi wa Jamhuri mbili tofauti ambazo mwaka 1964 walikubaliana kuunganisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa Tanganyika na kuunda Taifa moja linalojulikana kama Taifa la Tanzania. Lakini miaka kadhaa sasa imepita baada ya waasisi wawili hao kutangulia mbele ya haki kumekuwepo na malalamiko ambayo yanaendelea kulitafuta Taifa la Tanzania ambapo pande mbili hizi zikiwa zinavutana huku baadhi ya wananchi wakianza kukaa tamaa na kuhoji nini khatma ya Muungano huu. Wasomi, wananchi na wanasiasa mbali mbali wameanza kuuchambua mfumo ulitumika wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukiwa kama kigezo cha nchi nyingi za Afrika ambapo umedumu kwa miaka kadhaa lakini sasa baadhi ya wananchi wanasema umefika wakati kuuungalia upya Muungano huu kwa kuwashirikisha wananchi wote lakini wengine wanasema mfumo ulitumika ndio sahihi kabisa katika Muungano huu. Mhadhiri Mwanadamizi wa Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Adolf Faustine Mkenda amesema mfumo wa Muungano uliopo ndio unaofaa kwa sasa na mapungufu yanayojitokeza yanaweza kurekebishwa ndani ya serikali mbili: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT).Endelea kusoma makala haya.

MWAFAKA WA BUTIAMA

p21WAJUMBE wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikwenda kukutana Butiama Mkoa wa Mara ambako ndiko alipozaliwa na kuzikwa Mwaasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na muanzilishi wa mawazo ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Watanzania wengi hasa wazanzibari kwa siku ile hawakuwa na usingizi na wengine walichelewa kulala wakisubiri kitakachoamuliwa kikaoni na walikuwa wakisubiri hayo maamuzi mazito walioahidiwa na Rais wao Jakaya Kikwete hadi karibu na saa za kufungwa studio ya TBC ndipo ilipotoka tamko lililotangazwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa. Katika tamko CCM walisema wamepokea na kuridhia kimsingi makubaliano ya mazungumzo ya Mwafaka kati ya chama hicho na CUF lakini kuundwa kwa serikali ya mseto suala hilo haliwezi kuamuliwa hadi hapo wananchi wa Zanzibar watakaposhirikishwa kwa kuitishwa kura ya maoni.  Matumaini ya watanzania walio wengi yalikuwa ni maamuzi mazuri na yenye busara ambayo yangezingatia umuhimu wa mustakabali wa mazungumzo ya Mwafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Wananchi (CUF) ambayo yamechukua muda wa miezi 14 na vikao 21 kufanyika huku fedha kadhaa za wavuja jasho na wafadhili kutopotea katika mazungumzo hayo. Endelea kusoma makala haya.

JOHARI AKIDA NA KAZI ZAKE

MNAMO mwaka 1982 Mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Meya wa Mji wa Zanzibar ambaye aliyeteuliwa na Rais wa awamu ya pili, Aboud Jumbe Mwinyi ni Bi Johari Yussuf ambapo hivi sasa ana umri miaka 69 na Bi Joharianaonekana bado ana afya nzuri ila uwezo wa kushika nafasi yeyote ile hanao tena. Bi Johari ni mmoja wa wanaharakati na waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania ambapo huwezi kuizungumza historia ya Chama hicho kwa upande wa Visiwani bila ya kumuelezea ambaye kwa muonekano ni Mwanamke wa makamo mchangamfu na anayeonesha ukakamavu wakati wa ujana wake. Licha vikwazo mbali mbali alivyokumbana navyo akiwa mwanachama machachari, Bi Johari alifanikiwa kujaza fomu ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mjini Magharibi mwaka 1977 akiwa ni Mwanamke pekee kuwania nafasi hiyo nyeti kutokana na enzi hizo wanawake kujitokeza hadharani ilikuwa ni vigumu sana lakini yeye alijiamini kutokana na uzoefu alioupata wakati akiwa na umri mdogo kabisa katika Chama Cha Afro Shirazi (ASP). Endelea kusoma makala haya.

TUSIKILIZE MAONI YA WANANCHI

karume MWENYEWE“LAITI angelikuwepo Mzee Karume haya yote yasingefanyika wazanzibari leo hii tumekuwa kama watoto yatima hatuna mtu wa kututetea tokea kufa kwa Muasisi wa Taifa letu Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume” Hayo ndio maneno ya aliyoanza nayo aliyewahi kuwa Askari wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Khamis Haji Mussa wakati wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume. Bw. Mussa anasema Muungano haukuwa na lengo baya kwani walipokutana Wenyewe waasisi wawili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walikubaliana kuungana kama nchi mbili zilizo huru kiutawala. Nchi mbili hizi zimeingia katika makubaliano ya kuungana ambapo Tanganyika ikiwa imepata uhuru kutoka kwa wakoloni na Zanzibar imepata uhuru wake baada ya kufanyika Mapinduzi. Wazanzibari wanajivunia nini katika miaka 44 ya Muungano? Bw. Mussa anasema hakuna cha kujivunia kwa sababu waliotarajia yote hayajaweza kufanikishwa kutokana na nchi moja Tanzania Bara kujifanya wana nguvu dhidi ya nchi nyengine ambayo ni Zanzibar. Endelea kusoma makala haya.

NI HATARI TUPU NYEUSI ZANZIBAR 2010

KADHI Mkuu wa zamani wa Kenya Marehemu Sheikh Al- Amin Bin Mahzumy aliwahi kuwaasa watu wa Mombasa kwa kuandika Kitabu alichokiita na said mohedkukipa jila la “Khatar Asuad” yaani Hatari Nyeusi kabla ya Uhuru wa nchi hiyo mwaka 1963. Kwa nini aliandika au alitaka kuielezea nii kuhusu hatari nyeusi,mwenyewe alisema baada ya kubaini kwake kuwa watu wa Mombasa wanafanya Maskhara katika kuitafuta ilimu na hasa baada ya kuwaona watumishi wa ndani, matopasi na madobi toka Mikoa ya Bara wakijiingiza katika masomo ya jioni, masomo kwa njia ya posta nje ya nchi huku wakinunua vijitabu mbalimbali na kujisomea. Kila akitupa macho kwa kundi la wapwani yaani wakaazi wa Mombasa kazi ni kula miraa,kusikiza taarab na kupiga soga katika Baraza za mazungumzo kama vile Mwembetayari, Changamwe, Malindi Nyali ,Kisauni nk. Akasema Khatari Nyeusi bila shaka itawanyemelea watu wa Mombasa na iko siku hawa wapagazi na matopasi toka Bara ya miji kama vile ya Kakamega, Kisumu, Naivasha, Nakuru na Meru watakuwa mabwana na wale mamwinyi watatumwa na wahamiaji taka wasitake kwa sababu wanaitania ilmu (elimu). Endelea kusoma makala haya.

HISTORIA YA MAPINDUZI IMEPOTOSHWA

flagKWA mara nyengine tena Wazanzibari wanasherehekea miaka 45 ya Mapinduzi yaliyokhitimisha Utawala wa Kifalme katika visiwa viwili vya Unguja na Pemba. Mapinduzi hayo ya tarehe 12/1/1964 yaliyofanywa na Chama cha Afro Shirazi Party (ASP) kilichokuwa kinaongozwa na Mhe. Abeid Amani Karume na pia kusaidiwa na baadhi ya waliokuwa wafuasi wa Umma Party ambao wakijulikana kama‘Makomredi’ na wakiongozwa na Mhe. Abdul-rahman Babu.  Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa tofauti na kama vile zilivyozoeleka kauli ya SMZ kuwa nchi ya Zanzibar ilipinduliwa kutoka kwa Mfalme au utawala wa Waarabu. Wengi wanaotafautiana na kauli hizi wanasema ukweli wa mambo umepotezwa kwa makusudi na viongozi wa SMZ.  Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10/12/1963 kutoka mkoloni wake Mngereza ambapo wakati huo kulikuwa na Serikali ya Waziri Mkuu ya Mhe. Mohamed Shamte ambae alichaguliwa kwa njia ya demokrasia ya vyama vingi chini ya muungano wa vyama viwili vya Zanzibar and Pemba People Party (ZPPP) na Zanzibar National Party (ZNP) na Chama cha Afro Shirazi Party kilikuwa chama rasmi cha upinzani. Hivyo basi pamoja na kuwepo utawala wa kifalme wa Sayyid Jemshid lakini iliopinduliwa hasa ilikuwa Serikali iliyokuwa chini ya Waziri Mkuu Mhe. Mohamed Shamte. Endelea kusoma makala haya.

MIAKA 45 YA MAPINDUZI YA ASP ZNZ

TAREHE 12 Januari tunaadhimisha miaka 45 tokea Chama cha Afro- Shirazi kungo’oa ubwanyenye wa kisultan na aila ya Jemshidi bin Abdallah bin Haroub , sultan ambae alibahatika kupata hifadhi ya ukimbizi nchini Ngome_kongwe_znzUingereza badala ya kwao Oman ambapo mpaka muda huu hatathubutu kutia mguu wake hata kwa matembezi ya siku moja yeye na familia yake. Wenye busara na wakweli hapa wajiulize kulikono mtu nchini kwao anakataliwa kurudi na kuachwa akihemewa nchi ya kigeni bila uraia wake. Katika miaka ya 45 hii ya Mapinduzi bado yapo Masimbi ya Hafidhina na vijukuu vyao wanaokejeli na kuhoji ati uhalali wa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 wanakebehi hadharani na kudai ati maisha ya Zanzibar ni magumu na yamejaa uonevu lakini bado hawakubali kuungana na wenzao walioihama Zanzibar baada ya kupinduliwa wafalme wao Jemshid bin Abdallah bin Khalifa bin Haroub mwaka 1964 na kwa kujali kidhati taathira ya muadhara wa kupinduliwa na mahadimu wao hawatamani hata kuisikia Zanzibar licha ya kuja kutembea. Endelea kusoma makala haya.

MIAKA 45 TOKEA KUFANYIKA MAPINDUZI ZANZIBAR

ZANZIBAR ilipata uhuru wake tarehe 10 Disemba 1963 kutoka kwa Uingereza na kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN) mnamo tarehe 16 Disemba 1963. Uhuru huo wa watu wa Zanzibar ulidumu kwa siku 33 tu. Siku hiyo ya zmcbuilding[1]kupewa uhuru wao watu wa Zanzibar, Marehemu Abdurahman Moh’d Babu, aliekua Kiongozi wa Chama cha Umma Party, alizitoa salamu za uhuru kwa kusema:- “Peaneni uhuru mupendavyo, watu wa Zanzibar wanangojea saa na wakati uwadie wachukue hatamu za Serikali mikononi mwao”. Maneno yake Kiongozi huyo hayajaanguka chini.Ilipofika tarehe 12 Januari 1964 yalifanyika Mapinduzi na kufaulu tukasikia Serikali ya uhuru ilotolea na Waingereza. Sasa suala kubwa la kujiuliza hapa ni jee!! waliachiwa Wazanzibari kuzikamata hatamu za Serikali ya Mapinduzi ya Watu wa Zanzibar? Endelea kusoma makala haya.

MIAKA 45 YA MAPINDUZI JAN 1964 –JAN 2009

Stonetown_view_znzHAKUNA kitu ardhini katika maisha ya taifa kama historia ya nchi na waandishi wa historia ni wengi sana katika nchi na kila mmoja ataandika katika muelekeo wake hususan wa kisiasa lakini wanahistoria halisi huandika kutokana na ukweli wa matukio ya wakati uliopita huku historia inaweza kuwa yakupendeza au ya kuchukiza ya karaha au ya raha lakini vyovyote iwavyo ni matukio ya kweli yaliopita katika mwenendo wa maisha ya mwanaadamu. Nani atakataa kwamba nchi ya Zanzibar ilitawaliwa na waarabu wa Oman wa kabila la Al- Bunsaidy kutoka 1832 mpaka 1964 siku iliofanyika Mapinduzi ya tarehe 12 januari 1964 haya anayoadhimisha leo hii? Nani atakana kuwa waingereza waliitawala kwa mtindo wa kuihami Zanzibar iliokuwa chini ya utawala Sultani wa kabila la Al- Bun Saidy tangu 1890 mpaka Dec 10,1963 siku aliyoipa uhuru Zanzibar?. Nani atakana historia hii ya Muingereza kuipa Uhuru Zanzibar? suali litakuja jee uhuru huu uliopatikana Dec 10,1963 uliwapa uhuru wa kweli wananchi wa Zanzibar. Kwa mtizamo wa kichama kitalingania vyake Taaban chama cha ASP wanaona kuwa uhuru aliekabidhiwa ni Sultan ambae na yeye kwa mtazamo wao ni mkoloni mkongwe wa Zanzibar kama tulivyoonesha hapo awali. Endelea kusoma makala haya.

HATUNA CHA KUJIVUNIA ZNZ

Wonder_znNINI cha kujivunia wananchi wa Zanzibar, samahani, “wakaazi wa Zanzibar” baada ya kupita miaka 45 ya Mapinduzi yetu? Hapana isipokua maumivu ya kuipoteza hadhi ya visiwa hivi mbele ya macho ya Mataifa ya nje na huzuni ziliotanda kwenye vifua vya Wazanzibari.Pamoja na kuambiwa mjadala wa suala hilo umeshafungwa, lakini bado ni suala linaloendelea kuumiza vichwa vya watu wa nchi hii.Sawa, Zanzibar ni nchi kamili kama tunavyoamini sisi wenyewe, lakini kwanini ndugu zetu hilo walikatae? Huo sasa ni mvutano baina yetu ambao ni hatari kuwepo kwake. Utasababisha mgawiko baina ya huko na huku. Haya yanaibuka baada ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Na vipi hali za wakaazi wa visiwa hivi baada ya umri huo wa miaka 45? Tumerudi kule kule kwenye matabaka ya walionacho na wasionacho, matajiri na masikini. Hali hiyo ndio iliopigiwa kelele na Chama cha Afroshirazi huko miaka ya nyuma na ndio malengo ya kufanyika kwa Mapinduzi? Jee!! hivi sasa hali hiyo haipo visiwani mwetu? Iko nakuzidi wakati wa ukoloni. Hebu tuangalie ikiwa leo miaka 45 imepita ya Muungano wetu ndio kwanza Wabunge wetu wanaomba angalau tuletewe lami ili tuimarishe barabara zetu pana kitu hapo? Endelea kusoma makala haya.

MAPINDUZI YAIMARISHE MSHIKAMANO

HAKUNADSC01398 mwenye uwezo wa kubisha kwamba nia na madhumuni ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalikuwa ni kumkomboa Muafrika, si kwa maana ya Mswahili pekee bali kwa wale wote ambao hawakuwa na nafasi ya kuishi kama watu ikiwa ni pamoja na kujiletea maendeleo yao kama watu huru kwenye nchi yao.Ni ukweli kwamba Mapinduzi yamejitahidi kuleta maendeleo kwa watu wake pamoja na tofauti zilizopo kati ya utawala na utawala kuanzia mwaka 1964 ambapo Rais wa kwanza kushika madaraka baada ya kufanyika Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na walifuatia wote kila mmoja alikuwa na namna yake ya uongozi wake hadi awamu ya sasa. Pamoja na upungufu uliyopo lakini kumekuwa na maendeleo ya kupigiwa mfano kwenye suala la elimu, afya, maji, miundo mbinu ya mawasilianao na mengi mengine ambayo hatuna budi kuyaenzi na kuyaendeleza na bila ya shaka kuyalinda kwa nguvu zetu zote. Endelea kusoma makala haya.

MIAKA 45 YA MAPINDUZI: ZANZIBAR HAIJAWA HURU

KWA  mara nyengine tena Mapinduzi yaliyofanywa Zanzibar mwaka 1964 yanaadhimishwa huku nchi ikididimia kwenye umasikini na mfarakano wa kijamii ukiwa unaongezeka. Watawala wana maneno matamu na takwimu nzuri za kukuwa kwa uchumi na kutulia kwa hali ya kisiasa, lakini maisha halisi ya Wazanzibari ni shuhuda wa namna nchi yao inavyorudi Marikiti_2005_znzkinyumenyume.Mwendo wa Zanzibar ndani ya miaka 45 hii unafanana na ule wa ngoma ya Mbwa Kachoka, ambayo wachezaji wake hupiga hatua kumi mbele kisha wakarudi tisa nyuma. Ni kama kwamba baada ya lile povu la soda la muongo wa kwanza wa Mapinduzi (zilipojengwa nyumba za Michenzani, viwanda vidogo vidogo na miundombinu mingine), Zanzibar ilisimama na kuanza kurudi nyuma badala ya kwenda mbele.Na sasa tunaona kuwa uhuru ule ‘uliotokana’ na Mapinduzi haujamaanisha kitu katika maisha halisi ya Mzanzibari wa sasa. Kuwa huru ni kuwa na nyenzo na uwezo; bali pia ni hali ya kuishi bila khofu na woga.Alionao leo Mzanzibari ni uhuru wa kuwa na skuli na vyuo vya elimu visivyo elimu, hospitali na vituo vya tiba visivyo matibabu, mifereji isiyotoka maji, maduka ya vyakula na masoko ya vitoweo lakini wengi wanashinda na njaa.  Endelea kusoma makala haya.

BI KIDUDE BADO HUKO FITI

kidudeNI majira ya saa kumi na moja jioni, kijua cha hapa visiwani Zanzibar kinachwea na hali ya ubaridi kiasi inaanza, naingia nyumbani kwa msanii maarufu wa mziki wa mwambao Fatma binti Baraka ‘Bi Kidude’ maeneo ya Raha Leo mjini hapa. Napokelewa na bibi huyo ambaye nimekumta akijifumua nywele uku akijisuka makonga ‘mabutu’ nywele zake zote nyeupe kutokana na mvi za uzee uliomuingia, namtania kwa kumuuliza ee! Bibi na uzee huo unasuka nywele ? “Tena! hata kama ndo nyeupe kichwa kizima ndo ninyoe?” anajibu kwa kuuliza na kuendelea “Ninyoe kwa kutaka nini? Na Mungu ndo kashanipa cheo changu, kama mzee mzee tu, alhamdulillah nimekuwa na nywele zangu nyeusi mpaka sasa nimejaza mvi tele tena ninazisuka hivi hivi na mvi zake wala sitaki kuweka madawa kama nyie, hata hiyo ya kuzifanya nyeusi siweki, nitaka nini mpaka nijishughulishe hivyo.”anasema Bi Kidude. Bi Kidude kama anavyofahamika na wengi mbali na kujisuka pia bibi huyo bado ananguvu zake za kufanya shuguli zake za nyumbani kama kufagia nyumba yake, kuwasha moto na kazi nyingine ndogo ndogo kama Mwanaspoti ilivyomshuhudia.Endelea kusoma makala haya.

KUSIFU NA KUKOSOA KAZI YANGU-WAINAINA

UKITAJA orodha ya wanamuziki wa Kenya basi halitakosekana jina la Eric Wainaina ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuimba BUSARAnyimbo za kusifu taifa lake na hata kukosoa serikali ya nchi hiyo. Msanii huyo ni mkenya wa kwanza kupata tuzo ya Kora mwaka 2002 na pia alipata tuzo ya Mnet mwaka 2001 nchini Afrika Kusini ‘Favourite Male vocalist’. Akizungumza na Mwanaspoti kwenye mgahawa wa kitalii wa Mecury uliopo viwani hapa Wainaina anasema “Ndoto yangu ilikuwa ni kuwa daktari, lakini Papa Wemba, Yousondor wamechangia kuififisha ndoto hiyo na kujikuta nikifuata nyayo zao za mziki.”anasema Wainaina ambaye ameambatana na mkewe katika shoo yake aliyofanya kwenye tamasha la tano la Sauti za Busara linaloendelea visiwani hapa. “Niliwapenda wasanii hao na kipaji changu kilianza kuonekana pale wazazi wangu walipomnunulia kaka yangu Simon Piano, ingawa kaka hakupenda yeye hobi yake ilikuwa ni kucheza Kandanda mimi nikawa ndio naitumia kujifunza mziki. “Shule niliyokuwa nasoma St. Marys walimu pia walisisitiza vipaji binafsi ingawa nilikuwa napenda mziki nilicheza pia Tenesi na basketball. Endelea kusoma makala haya.

UONGOZI HADI UWE JASIRI – BI RUFEA

6“Ukitaka kuwa kiongozi lazima uwe jasiri, usipendelee majungu, ufuate haki na misingi ya sheria na uepukane na majungu kwa sababu kwenye wanawake hakukosi ufisadi, fitana na kutopendana hayo yote utakabiliana nayo” “Njia ni ndefu mno kwa mwanamke kufikia kwenye uongozi kwa sababu utakabiliana na majungu migogoro, vikwazo mbali mbali na kuna ngazi nyingi unatakiwa uzipande ili ufikie malengo yako” hivyo ndivyo alivyoanzamwanasiasa wa siku nyingi Bi Rufea Juma Mbarouk ambaye ameshakamata nafasi mbali mbali katika serikali ya mapinduzi zanzibar. Bi Rufea ni mwasiasa mkongwe ambaye alizaliwa miaka 61 iliyopita kisiwani Pemba na ametokana na familia ya kimasikini na ameanza kuitumikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mwaka 1965 alipoanzia na nafasi ya Mwakilishi, Mbunge, Naibu Waziri wa Elimu Utamaduni na Michezo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi na Maziri wa Mawasiliano na Uchukuzi nafasi ambayo amedumu nayo kwa miaka minane. Katika maisha yake amekamata nafasi mbali mbali serikalini na katika chama chake cha Mapinduzi (CCM) huku akiwa amepata shida sana katika kufikia nafasi hizo amekabilia na majungu na vikwazo mbali mbali lakini amefanikiwa. Endelea kusoma makala haya.

MAGOFU YALIOKOSA MUENDELEZO

Sio watu wengi ambao huona umuhimu wa kufahamu vitu vyenye thamani katika nchi yao hasa katika utamaduni wa kiafrika hasa watanzania P1010058wamekuwa wakipuuza sana kutembelea sehemu za kihistoria zenye kuvutia na wanaamini kwamba watu wanaopaswa kutembelea sehemu za kihistoria ni watalii peke yao. Utamaduni huu wa kuacha kutembelea sehemu za kihistoria au kusoma vitabu vya zamani vinawakosesha mengi watanzania ambao wanapaswa kwa hali yoyote ile kujua historia ya nchi yao na utajiri mkubwa uliokuwa katika nchi yao na sio kuwasubiri watalii ndio nao wafuatane kwenda huko kuangalia magofu au vitu vya zamani ikiwemo majengo ya kale na ngome mbali mbali zilizopo katika nchi hii. Kuna umuhimu wa kipekee wa kujua historia ya watu wa mwanzo wa Visiwa vya Pemba, kujua asili ya miji ya visiwa, lugha, watu hata vifaa walivyokuwa wakitumia watu wa asili na muhimu zaidi ni kutunza maeneo ya historia kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo. Ingawa Historia ina umuhimu wa kipekee, kwani inapendeza kwa kila mtu kujua asili yake na asili ya sehemu aliyopo ama aliyotokea na hata sehemu aliyotembelea ambapo hivi sasa wananchi wameanza kuamka na kujua umuhimu wa kuthamini historia yao. Endelea kusoma makala haya.

MNAZI NA FAIDA ZAKE LUKUKI

vinyago vya mnaziMNAZI kwa jina la kitaalamu unajulikana kwa jina la Cocos nucifera ambao huchukua miaka kadhaa kufikia umri wa kutoa mazao ambapo kufikia urefu baina ya mita 30-50 na mazao yake hutengenezewa vitu mbali mbali kuanzia mafuta ya kupikia sambuni, ulevi, siki, kamba, mafuta ya urembo, mafuta ya nywele, nishati, kutengenezea mshumaa, majarini ya kulia na kupikia na matumizi kadhaa yasiopungua 100.Visiwa vya Unguja na Pemba navyo haviko nyuma katika kutengeneza vifaa vinavyotokana na mnazi ambapo Mfuko wa Kujitegemea katika mikakati ya kuwakomboa akina mama Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la SWISS CONTACTS wameweza kuwapatia mafunzo akina mama kutoka sehemu mbali mbali visiwani hapa kujifunza mambo mbali mbali ya kutengeneza bidhaa kadhaa kutokana na mnazi.Wana historia wengi wanaona kuwa mnazi umefika katika maeneo mingi ya nchi ya joto kwa njia ya bahari, kusukumwa na kuangukia kwenye fukwe na kukuwa lakini wengine wanaamini kuwa minazi imefikishwa nchi za joto na wafanyabiashara waliotoka nchi za mashariki ya mbali.Asili ya minazi wapi ilipotokea ni vigumu kueleweka lakini wachambuzi wengi wanafahamisha kuwa minazi asili yake ni nchi ya Malaysia na nchi ya Indonesia. Katika kumbukumbu zilizonukuliwa na Sanskrit zimefahamisha kuwa watu wa India wakitumia nazi kama chakula na matumizi mengi kwa mambo tofauti. Katika nchi ya India, Mnazi unajulikna kwa jina la kalpa vriksha, ikimaanisha kuwa “mti ambao utakupatia mahitaji yako yote yakukuwezesha kuishi”.Endelea kusoma makala haya.

PEMBA WAONGOZA KUWATUMIKISHA WATOTO

WAKATI nchi nyingi duniani zimeanzisha kampeni maalumu ya kupiga vita utumikishwaji wa watoto wadogo ikiwemo Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi zilizosaini mkataba wa kimataifa bado hali hiyo haijaweza DSC03246kudhibitiwa katika baadhi ya maeneo kadhaa Visiwani Zanzibar. Maeneo mengi hasa vijijini watoto wadogo hufanyishwa kazi kutokana na sababu mbali mbali zinazoelezwa ikiwemo ile ya wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu hivyo hulazimika kubakia nyumbani na kuwasaidia wazee wao katika kazi za nyumbani ambazo nyengine kubwa kuliko uwezo wao. Hivi karibuni nilikuwa katika Kisiwa cha Pemba na kushuhudia watoto kadhaa wanaofanya kazi nzito ambazo haziendani kabisa na umri wao kutokana na kazi zenyewe ni mzito ambazo zinahitaji nguvu na uwezo mkubwa wa kiafya. Maeneo mengi Kisiwani Pemba utawakuta watoto wakicheza mitaani nyakati za kwenda shule huku wengine wakiwa wanauza biashara mikononi , kuvunja kokoto, kuvua samaki baharini na kupara samaki kando ya bahari ambapo baadhi yao wamebuni kazi mpya wa kwenda uwandani na kufanya kazi za kukata matufali ambao ni mgumu na mzito kulingana na umri wao mdogo. Endelea kusoma makala haya.

MACEMP NI MKOMBOZI WETU

P1010048Tujiendeleze na maisha bora” jina hili ni moja kati ya vikundi vya ushirika vilivyoanzishwa na wanavijiji mbalimbali katika visiwa vya Unguja na Pemba.Kikundi hiki kilichopo katika kijiji cha Wingwi Njuguni katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kinajishughulisha na shughuli za usokotaji wa kamba za makumbi ya mnazi almaarufu usumba. Kikundi hiki kina historia ndefu tokea enzi za ukoloni wa sultani aliyetawala visiwani hapa ambapo vikundi hivi vya ushirika vilikuwa vikijulikana kwa jina la Cooperative Society (Jumuiya za Mu’awana).Kikundi hiki pamoja na vyengine vingi vilivunjika kufanya shughuli zake kutokana harakati za Mapinduzi ya mwaka 1964 katika visiwa vya Unguja na Pemba.Kama msemo wa Kiswahili unaosema “Mungu haachi mjawe” vikundi hivi vimeibuka tena upya baada ya kupata misukumo ya aina mbalimbali ikiwemo ile ya uwezeshaji wa kihali na mali kutoka kwa wananchi wenyewe, jumuiya, miradi na mashirika tofauti ya ndani na nje ya nchi na pia serikali. Moja kati ya miradi inayofanya kazi hiyo visiwani hapa ya kuwasaidia wananchi, wanavikudi vya ushirika ni mradi wa MACEMP (Marine and Coastal Environment Management Project). Endelea kusoma makala haya.

MISALI KISIWA CHENYE MVUTO

Hifadhi ya Bahari ya Mkondo wa Pemba , Pemba Channel Conservation Area (PECCA) ambayo ina ukubwa wa kilomita za 1,000 inaanzia Ras P1010026Kigomani na kuelekea Kangani na Kisiwa Panza ambayo ni Kusini mwa Kisiwa cha Pemba. PECCA eneo lake lipo Magharibi mwa Kisiwani Pemba eneo hilo lililoanzishwa mwaka 2005 na kuanza kazi zake rasmi 2006, uanzishwaji wake umetokana na sheria ya uvuvi No 8 ya mwaka 1988 chini ya kifungu no 7/1 na kifungu cha 32 ambavyo vinampa uwezo Waziri anayesimamia shughuli za uvuvi kulitangaza eneo lolote la bahari kuwa hifadhi. Madhumuni ya kutangazwa eneo hilo ni kuhifadhi Baianwai (Viumbe vya Bahari) vilivyomo pamoja na kuweka matumizi endelevu ya mali asili za bahari kwa maslahi ya jamii inayotegemea maliasili hizo. Lengo jengine la eneo hilo ni kuanzishwa hifadhi inayojitegemea kwa kuendesha shughuli za kitalii bila ya kuharibu mazingira na kuinufaisha jamii sanjari na mkakati wa kupunguza umaskini nchini. Endelea kusoma makala haya.

MAPINDUZI HAYAJAFIKIWA

p14 Swali: Nini maana ya mapinduzi, na Jee unayafahamu mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964? Jawabu: Kwa maana halisi mapinduzi ni mabadiliko, mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na mabadiliko mengine katika jamii. Mara nyingi huwa ni kuondosha mfumo fulani uliopo labda una mapungufu ama hauna manufaa kwa wananchi katika nyanja zozote zile. Mapinduzi haya yalipofanyika mimi bado nilikuwa mdogo ila kuna mambo mengi yaliyoambatana na mapinduzi nayakumbuka. Na pia hali ilivyokuwa ikiendelea baada ya mapinduzi kabla ya kuuwawa Karume.  Swali: Ni yepi yalikuwa malengo ya mapinduzi hayo ya 1964? Jibu: Mapinduzi yalikuwa na nia nzuri kwa wananchi wake,lengo ilikuwa ni kuwakomboa wakulima na wakwezi kutokana na aina zote za ubaguzi na uonevu waliokuwa wakifanyiwa na wakoloni. Pia mapinduzi hayo yalikusudia kuwaunganisha wazanzibari wote na kuwa kitu kimoja. Unajua hapa Zanzibar kabla ya mapinduzi kulikuwa na matabaka na makabila tofauti, kwa mfano waarabu walikuwa na skuli zao, wahindi, wangazija, kwa hiyo watu wengine walikuwa hawana nafasi katika sehemu kama hizo, wanyonge walikuwa hawana sauti. Sasa haya mapinduzi chini ya kiongozi wa mapinduzi haya Abeid Karume, alitaka kuyaondosha haya yote, watu wote waliokuwa na uwezo wa kusoma basi wasome bila ya kipingamizi chochote, na kuondosha hii skuli ya muhindi, ya mngazija, aaah wote ni wazanzibari wana haki sawa.Endelea kusoma makala haya.

KUSHUKA KWA ELIMU NINI TATIZO?

Kwanza ni vyema kabisa tuizungumzie hali ya elimu ilivyo kwa sasa Zanzibar. Kwa kuangalia hali ya elimu ilivyo, tutaona kuwa kwa macho mepesi kuwa elimu imepanda katika nyanja tafauti lakini kiundani kaa_chiniutagundua kuwa kuna mapungufu makubwa, hali ambayo utakubaliana nami kuwa elimu yetu bado haijaridhisha, kiufupi sekta ya elimu ina mapungufu makubwa. Tukianzia na elimu ya msingi kwa mujibu wa hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mwaka wa fedha wa 2008/2009 katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman alisema ni kuwa idadi ya wanafunzi wote wanaosoma shule za msingi ni asilimia 104.4 ya watoto wote wenye umri wa miaka 7 hadi 13. Katika mwaka 2008 jumla ya wanafunzi 31,412 kwa darasa la kwanza waliandikishwa na wote walipatiwa nafasi. Kwa undani tukilichunguza hili tutagundua kuwa elimu ya msingi ndiyo inazidishiwa matatizo makubwa, hii ni kwa sababu mbalimbali, moja ni kuwa katika shule kuna upungufu mkubwa ya walimu, hivyo ni kuyafanya madarasa yawe na wanafunzi wengi lakini walimu ni kidogo. Endelea kusoma makala haya.

MZALENDO AWEKEZA KATIKA ELIMU ZNZ

Ahmada Yahya Abdulwakil ni Mzanzibari wa kwanza kuwekeza katika sekta ya Elimu Visiwani Zanzibar huku ndoto yake ikiwa ni kuwasaidia wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwaendeleza kielimu katika shule za sekondari. Ahmada ni Mfanyabiashara ambaye anamiliki Kampuni ya SHA Timber kwa miaka mingi ameamua kujenga shule kubwa eneo la Mombaza nje kidogo na Mji wa Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia watoto masikini na pia kuondosha kiu yake ya kufanya kitu kikubwa katika nchi yake ambayo wafanyabiashara wengi wameshindwa kubuni kitu kama hicho licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha.Ndoto yake hiyo ilionesha kutimia baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuamua kuweka wazi fursa ya wale wenye uwezo ambao wako tayari kuwekeza katika sekta ya elimu. Endelea kusoma makala haya.

WAHITIMU HUKIMBIA ZANZIBAR KWA NINI?

waziri wa elimu na mafunzo ya amali Haroun Ali SulimanWahitimu wengi wa elimu ya juu katika fani mbali mbali ikiwemo ile ya ualimu mara nyingi hukimbilia katika sekta binafsi kwa ajili ya kujipata ajira, kuliko kuajiriwa serikalini, na hata wengine hukimbilia nje ya nchi kabisa. Katika hali kama hiyo nchi inajikuta kuwa na ukosefu wa wataalamu licha ya kuwa na vyuo vinavyotoa wasomi wa fani tofauti kila mwaka. Tabia hii imekuwa ni kitu cha kawaida visiwani Zanzibar ambapo katika miaka ya nyuma visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa vikisifika sana kwa kutoa wataalamu wa fani mbali mbali ambao walikuw awazalendo zaidi kuliko hivi sasa. Tukiangalia katika sekta ya ualimu Zanzibar ina vyuo vikuu viwili vinavyotoa fani ya ualimu, mbali ya vile vyuo vyengine vinavyotoa taaluma hiyo katika ngazi ya stashahada na cheti. Kwa ujumla vyuo hivi vinatoa wahitimu wengi kila mwaka, lakini ukipita katika shule hususan za sekondari tatizo la uhaba wa walimu umekuwa ni wimbo wa taifa. Endelea kusoma makala haya.

Advertisements

2 responses to “Makala

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s