Jamii

Vifo vya Mv. Skgit, wahusika washitakiwa kwa makosa 60 ya mauaji

WATU watatatu wanaomiliki Kampuni ya Meli ya Seagul, wamefikishwa katika mahakamani wakikabiliwa na mashitaka 60 ya mauwaji. Washitakiwa hao wanadaiwa kuhusika na mashitaka hayo, kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea Julai 18 mwaka huu, karibu na maeneo ya kisiwa cha Chumbe. Walioshitakiwa ni Mussa Makame Mussa (49) mkaazi wa Kazule, ambaye ni Kepteni wa meli hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Said Abdulrahman Juma (46) wa Mwembetanga, pamoja na Meneja wa tawi la Dar es salaam Omar Hassan Mkonje (50) mkaazi wa Magomeni. Wote hao wamefikishwa mbele ya Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar Ali Ameir Haji, na kusomewa mashitaka ya kuua bila ya kukusudia kinyume na vifungu vya 195 na 198 vya kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar. Mashitaka hayo yalisomwa mahakamani hapo na Wanasheria wa serikali Suleiman Massoud Juma na Sabra Mselem Khamis, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). Endelea kusoma habari hii

Meli tatu zafutiwa usajili kuepusha ajali

Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo. Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar. Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo. Endelea kusoma habari hii

Taarifa ya serikali ya kuzama kwa Mv. Skagit

Mara baada ya tukio hili, Kamati ya Kukabiliana na Maafa ya Taifa ilikutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya hatua za kuchukua pamoja na kuandaa taarifa rasmi ya Serikali kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. Aidha, Baraza la Mapinduzi lilikaa usiku wa tarehe 18.07.2012, na kutoa maagizo juu ya hatua za kuchukua ikiwemo kuwepo kwa matayarisho katika hospitali ya mnazi Mmoja ya kupokea majeruhi, kutayarisha eneo la Maisara kwa ajili ya mapokezi na utambuzi wa maiti; kutayarisha eneo la kuzika miili ya marehemu huko Kama; kuweka takwimu sahihi za majeruhi na waliofariki katika ajali hiyo; pamoja na kutolewa kwa taarifa rasmi ya hali ya uokozi iliyokuwa inaendelea. Endelea kusoma habari hii

Miili 16 yapatikana leo, waliofariki sasa ni 94

IDADI ya miili iliyopatikana katika ajali ya meli ya Mv. Skagit imezidi kuongezeka baada ya jana kupatikana miili 16 katika maeneo ya Zanzibar na Bagamoyo Tanzania Bara. Kwa mujibu wa waziri wa nchi ofisi ya rais makamo pili wa rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed amesema maiti hao wamezikwa haraka haraka kutokana na kuharibika vibaya pamoja na kwamba waliopatikana Bagamoyo wameshazikwa huko huko. “Ni kweli maiti zimeongezeka leo mchana na baada ya kuopolewa na zikikimbizwa haraka kuzikwa kwa sababu miili yenyewe tayari imeshaharibika” alisema Aboud. Aboud alisema kati ya maiti 16 zilizoptikana leo maiti 5 zimepatikana huko Bagamoyo ambapo matayarisho ya mazishi yao yamefanywa na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya ya mkoa huo. Maiti hizo zimekwenda kuzikwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mazishi huko Kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Alisema idadi hiyo inafikisha maiti zilizopatikana tangu kutokea kwa ajali hiyo jumatano iliyopita kufikia 94 ambapo idadi kubwa ya waliofariki ni wanawake na watoto. Endelea kusoma habari hii

Waziri Hamad ajiuzulu

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu. Endelea kusoma habari hii 

Nilizimia kabla ya kuokoa’ Muddy

Muhsin Salum Muddy ni miongoni mwa wazamiaji walioshindwa kufanya kazi ya uokozi baada ya kupinduka na kupoteza fahamu wakati wa zoezi la kuwaokoa watu waliopata ajali ya meli ya Mv Skagit iliyozama katika eneo la baina ya Chumbe na Dar es Salaam jumatano iliyopita. “Sikujitambua mien a sijui nimefikaje hospitali hapa maana nafungua macho ndio najiona nipo katika kitanda na nimefunikwa branketi wakati ninavyojua niliingia katika boti ya polisi kwa kwenda kuwaokoa watu waliopata ajali” alisimulia kijana huyo na kuongeza kwamba. “Pamoja na kwenda kuwaokoa walionusurika katika boti na kuchukua maiti nilikuwa na kamera kwa ajili ya kupiga picha lakini nikashindwa kufanya kazi zote kutokana na hali ya hewa ilivyokuwa mbaya” alisema. Kushindwa kufanya kazi kwa Muhsin kunatokana na mawimbi makali baharini ambayo yalisababisha boti za uokozi kushindwa kutulia kufanya kazi ya uokozi ambapo waokoaji wengine walikubwa na mkasa kama wa kwake na wengine kujeruhiwa vibaya. “Tuliondoka bandari ya Malindi majira ya saa 9:30 jioni na tukafika kule kiasi saa 12 na baada ya nusu saa ndio tukawa tunaziona maiti zikielea na watu waliokuwa hai wakiomba msaada wa uokozi huku wakihangaika sana wakionesha kuchoka wengine tayari wameshakunywa maji mengi wanataka kusaidiwa lakini haikuwa rahisi kufanya kazi hiyo” alisema kijana huyo. Endelea kusoma habari hii

Miili 76 kuzikwa baharini

SERIKALI imesitisha rasmi zoezi la uokoaji wa miili ya watu waliozama katika ajali boti ya Mv Skagit Jumatano iliyopita kutokana na ugumu wa kazi hiyo, huku miili zaidi ya 76 ikipotea baharini. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idd alisema hayo wakati akipokea msaada kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya waathirika wa ajali hiyo. Alisema wataalamu waliokwenda kwenye eneo la ajali kwa ajili ya uokoaji wamethibitisha kutopata mwili hata mmoja kwa muda siku mbili, hivyo Serikali imeamua kusitisha zoezi hilo.“ Tumeamua siku ya kesho (leo) kusoma hitima kwenye misikiti yote ya Unguja na Pemba, lakini kitaifa hitima hiyo itasomwa katika Msikiti wa Mwembeshauri eneo la Rahaleo mjini Zanzibar,” alisema. Alisema hitima hiyo itafanyika kwenye misikiti mikuu na kwamba katika mikoa yote hitima hiyo itafanyika saa 7.00 baada ya Sala ya Adhuhuri. Endelea kusoma habari hii

Viongozi wa Uamsho watafutwa, 40 mbaroni

JESHI la Polisi Nchini, linawatafuta viongozi wa Taasisi za kidini na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki) huku likiwashikilia watu 43 wanaodaiwa kuhusika na vurugu zilizotokea juzi. Viongozi wanaotafutwa na Jeshi la Polisi na ambao wanatakiwa kujisalimisha ni pamoja na Msemaji wa Taasisi za Kidini, Farid Hadi Ahmed, Kiongozi wa Uamsho, Mselem Ali Mselem, Naibu Kiongozi wa Uamsho, Azan Khalid Hamdan na na Mhadhiri wa Uamsho Mussa Juma Issa. Lakini Naibu Kiongozi wa Uamsho, Hamdan alikanusha jumuiya yake kuhusika na vurugu hizo akisema walikuwa msikitini kuwaombea dua waliofikwa na maafa katika meli ya MV Skaget Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohamed alisema jana kuwa viongozi hao wanatafutwa kwa kosa la kuwahamasisha vijana kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu. Alisema katika vurugu hizo, vijana hao walikata miti iliyomo pembeni mwa barabara, kuvunja vioo vya nyumba na magari , kuweka mawe na vitu vizito barabarani. Kamanda alisema viongozi hao waliomba kibali cha kufanya mikutano kwenye uwanja wa mzalendo ili kuwaombea dua waliokufa kwa ajali ya meli ya Mv Skagit lakini polisi ilikataa kutokana na amri ya serikali kuzuia mihadhara. Endelea kusoma habari hii

Mwanamke aelezea jinsi alivyonusurika

WAKATI jitihada za kuopoa miili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya meli ya MV Skagit iliyozama Jumatano wiki hii zikiendelea, walionusurika kwenye ajali hiyo wameeleza jinsi walivyokumbana na zahama, mmoja wao akiwa mkazi wa Micheweni Pemba, Makame Masoud Ali (18), ambaye alisema kilichomsaidia hadi alipookolewa ni kushikilia gunia kwa zaidi ya saa mbili akielea nalo baharini. Mbali na Ali, mwingine ni mfanyakazi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Arusha, Salome Mwambinge ambaye alisema: “Kuokoka kwangu ni miujiza ya Mungu.” Mwambinge ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar alisema: “Sijui kuogelea, lakini nilikaa kwenye maji kwa saa nne. Nilichoka na kukakata tamaa, nikajiachia ili ikiwezekana nife, lakini nashangaa leo hii ni mzima.” Mtumishi huyo Tume ya Atomiki ambaye alikuwa safarini kuelekea Pemba kikazi, alisema aliokolewa akiwa hajitambui… “Ninachokumbuka ni kwamba waokoaji walinifunga kamba shingoni nikapata maumivu makali, nikapiga kelele wakaniachia, nikatumbukia tena kwenye maji na baadaye walifanikiwa kuniokoa na kuniweka kwenye boti.” Endelea kusoma habari hii

Maiti 31 majeruhi 136 na 123 wamepotea

Ajali hiyo imetokea wakati meli hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuja Zanzibar.  Taarifa za awali za MV SKAGIT ni kuwa meli hio ilikuwa  na jumla ya watu 290. Kati ya hao wafanyakazi ni watu 9, abiria watu wazima ni 250 na watoto 31.  Meli hiyo ilipata maafa hayo maeneo ya Kisiwa cha Chumbe milango ya saa nane mchana.  Mara baada ya taarifa ya ajali hiyo kutufikia, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikishirikiana na taasisi mbali mbali zikiwemo Idara Maalum za SMZ, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Usafiri wa Baharini pamoja na vyombo vya usafiri wa baharini vya watu binafsi na wananchi kwa jumla  ilichukua hatua za haraka kufika eneo hilo kwa kazi za uokozi. Endelea kusoma habari hii 

Meneja meli iliyozama Zanzibar akamatwa

 JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo.Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu. Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo. Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneje huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo. Endelea kusoma habari hii

Suluhu haijapatikana kuhusu sensa

SERIKALI bado inaendelea kufanya juhudi za kuwashawishi viongozi wa dini na makundi mengine yaliotishia kususia zoezi la sensa ili kufikia muafaka kabla ya zoezi hilo kufanyika Agosti 26. Hayo yamebainika wakati wa mafunzo ya siku tatu ya sensa kwa waandishi wa habari waandamizi na wahariri waliopo Zanzibar ambapo walipata muelekeo wa sensa hiyo. Wawezeshaji kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu Zanzibar waliwaambia waandishi wa habari kuwa makundi hasa ya kidini ikiwemo Uamsho hawajapuuzwa na viongozi wa serikali pamoja na ofisi ya mtakwimu wamekuwa wakifanya juhudi za mara kwa mara kufanya mazungumzo. “Sensa ni muhimu na tunataka kila mtu ahesabiwe kwa hivyo viongozi wetu wanaendelea na kuwashawishi viongozi wa dini wanaosusia wasifanye hivyo” alisema Mayasa Mahfoudh ambaye ni afisa mwandamizi wa katika ofisi hiyo ya mtakwimu. Mtakwimu mkuu wa serikali Mohammed Hafidh alisema waandishi wa habari wana nafasi na mchango mkubwa wa kuhakikisha kwamba sense ya mwaka huu inafanikiwa kwa kiwango kikubwa. Endelea kusoma habari hii

ZIORI YAWALETA WAZAWA KWAO

WATAALAMU wa siasa za Kiamataifa na utamaduni katika maeneo ya nchi za bahari ya Hindi (Indian Ocean) wamekusanyika mjiniZanzibarkuzungumzia maendeleo ya eneohilo  katika kipindi hichi cha kasi ya mabadiliko makubwa duniani.Endelea kusoma habari hii

Wanawake wakutana Zanzibar

MKE wa rais wa Zanzibarmama Mwanamwema Shein ametoa wito kwa serikali na taasisi binafsi kuendelea kuwasaidia wanawake ambao wengi bado wanakabiliwa na chnagamoto nyingi zinazokwamisha maendeleo yao.Endelea kusoma habari hii

 

ZANZIBAR ANZISHENI BARAZA LENU LA HABARI

WAANDISHI wa habari Zanzibar wameambiwa wanayo nafasi ya kuanzisha Baraza la Habari la Zanzibar linalojitegemea nje ya Baraza la Habari Tanzania (MCT).Ali Rashid ambaye ni Mwandishi wa habari wa siku nyingi na pia mshauri wa waandishi hapa Zanzibar, alisema kinachotakiwa ni kuwepo kwa wanataaluma ya habari wanaotaka kuwa na chombo hicho visiwani Zanzibar licha ya kuwa baraza la habari la Tanzania kufanya kazi zake hapa nchini.Endelea kusoma habari hii

AJIRA KWA WAAFRIKA ZANUKIA

IMEELEZWA kwamba nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zinatarajiwa kupata ajira mpya 23,000 baada ya miaka mitano.Ajira hizo zitatarajiwa kuwanuisha jumla ya vijana millioni 1.2 ili kukabiliana na hali ya maisha na kuondokana na umasikini.Endelea kusoma habari hii

MWANDISHI MKONGWE AFARIKI ZNZ

MTANGAZAJI Mkongwe wa Zanzibar Joseph Caitan Asama (79) amefariki dunia jana mchana nyumbani kwake Mbweni nje kidogo ya Mji waZanzibar.Marehemu Asama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na alizidiwa jana mchana wakati akiwa katika matayarisho ya kukimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu na hatimae kufariki dunia.Endelea kusoma habari hii

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na balozi wa Canada  nchini Tanzania Bwana Robert Orr na kumuelezea sekta za maendeleo ambazo zimepewa kipaumbele na serikali anayoiongoza.Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo wa Canada  kuwa miongoni mwa sekta za maendeleo ambazo serikali anayoiongoza Dk. Shein imekusudia kuzipa kipaumbele ni sekta ya elimu, afya,kilimo, huduma za kijamii na sekta nyenginezo.Endelea kusoma habari hii

TAHADHARINI NA DAWA ZA SUNNA

WAUMINI wa dini ya kiislamu nchini wametakiwa kujihadhari na wauzaji wa dawa za asili kiholela wanaopita misikitini na kuwauzia waumini dawa hizo bila ya kuwa na viwango vinavyokubalika.Imeelezwa kwamba baadhi yao huuza dawa ambazo hazijathibitishwa na Jumuia ya Tiba na Asili Zanzibar ambayo ndio iliopewa mamlaka na Wizaya ya Afya kutoa kibali.Endelea kusoma habari hii

UHURU WA HABARI WAJADILIWA

WATAALAMU kadhaa wa vyombo vya habari kutoka Barani Afrika wamesema bado sekta ya habari inakabiliwa na changamoto kadhaa barani Afrika na kutaka vyombo vya habari vishikamane katika kukabiliana na changamoto hizo.Wakiwasilisha mada katika mkutano wa siku mbili uliowajumuisha wataalamu mbali mbali ambapo wamesema licha ya kumekuwepo na juhudi mbali mbali katika kuimarisha vyombo vya habari vya Afrika lakini bado kunahitajika nguvu za ziada katika kukabiliana nazo.Endelea kusoma habari hii

25 02 2011

HUDUMA za maji zimetoweka kwa siku ya pili katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja mjini Zanzibar na kuathiri wagonjwa wasiopunguwa 400 mjini ZanzibarFundi Mkuu wa Hospitali hiyo, Juma Ali Hamad amethibitisha kutokea kwa tatizo hilo na kuathiri wodi za wagonjwa 12 waliolazwa katika hospitali hiyo.Amesema tatizo hilo limeanza kujitokeza jana majira ya saa 10:00 za jioni na kulazimika uongozi wa hospitali hiyo kuitisha kikao cha dharura kujadili uhaba huo wa maji. Endelea kusoma habari hii

25 02 2011

WAKULIMA wa mpunga wa mabonde ya Mkoa wa Kaskazini Unguja yaliokumbwa na ukame wameiomba Serikali kuwapatia mbegu ndogo wakati wa mvua za masika ili wazipande tena katika konde zao zilizoharibika kwa jua kali.Ombi hilo la Wakulima liliwasilishwa kwenye ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika mabonde ya Mpunga ya Kilombero, Kibokwa, Machekechuni na Kibonongwa alipofika kuwapa pole kufuati mpunga wao kuunguliwa na jua kali.Endelea kusoma habari hii

25 02 2011

RAMADHANI Handa Tuma (28) Mkaazi wa Mombasa wilaya ya magharibi Unguja, aliyekuwa akituhumiwa kwa kosa la kuchoma moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya kiislamu amehukumiwa kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi 24 pamoja na na adhabu hiyo mshtakiwa huyo ametakiwa kulipa faini ya fedha taslim shilingi 200,000.Adhabu hizo zimetolewa na Hakimu Khamis Ali Simai wa mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, baada ya kumtia hatiani dhidi ya mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani pamoja na kukashifu dini makosa ambayo yalikuwa yakimkabili mahakamani hapo.Endelea kusoma habari hii

23 02 2011

WAKULIMA wa zao la Mpunga katika bonde la Tumbe Magharibi Kisiwani Pemba, wameshauriwa kulima zao hilo kwa wingi huku wakizingatia ushauri wa wataalamu ili kuweza kuepuka balaa la njaa linaloendelea kutokea katika baadhi ya mataifa duniani.Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, kabla ya kusitisha ziara yake kisiwani Pemba wakati akizungumza na wakulima wa bonde hilo baada ya kukagua tuta lililojengwa kwa msaada wa Mfuko wa TASAF na waananchi.Endelea kusoma habari hii

22 02 2011

JUMUIYA ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), imeeleza haja kwa nchi wanachama kuimarisha uchumi na kusifu amani na utulivu iliyopo hapa Zanzibar tokea kufanyika kwa uchaguzi mkuu Octoba mwaka jana.Wakizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), waliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

21 02 2011

MIKAKATI maalum imewekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwajengea uwezo wakulima hapa nchini hivyo uwamuzi wa Serikali ya Iran kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya kilimo utasaidia kwa kiasi kikubwa. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania. Mohsin Movahhedi Ghomi, Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

18 02 2011

IMEELEZWA kwamba zaidi ya watu 7,000 wanakabiliwa na uhaba wa chakula na ukosefu wa mazao katika vijiji vya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.Hali hiyo imejitokeza kwa muda wa mienzi mitano sasa baada ya eneo kubwa la mashamba ya wakulima kuonekana kutokuwa na uzalishaji wa chakula cha aina yoyote kutokana na hali ya hewa ya jua kali (Kiangazi) inayoikabili kisiwan humo ambapo tayari miti kadhaa imeonekana kukauka.Endelea kusoma habari hii

18 02 2011

WATU wasiojulikana jana wamemwagia tindi kali Mkurugenzi wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Rashid Ali Juma (45) karibu na nyumbani kwake Amani Mjini Zanzibar wakati akioka msikitini majira ya 2:00 usiku.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya familia yake Mkurugenzi huyo alkutwa na tukio hilo wakati akiwa njiani na kuelekea nyumbani ambapo wanasema hali yake bado haiatengamaa licha ya kupata huduma ya kwanza huko katika hspitali ya Mnazi Mmoja ambapo ameumia sehemu za usoni, kifuani na mapajani.Endelea kusoma habari hii

14 02 2011

BARAZA la Manispaa Zanzibar limesema kuwa halitahusika na uharibifu wowote wa mali yoyote wakati wa kuyahamisha makontena yaliyopo katika eneo la Darajani mjini Zanzibar.Mkurugenzi wa Baraza hilo, Maalim Rashid Ali Juma aliwambia waandishi wa habari wakati wa mazungumzo yake maalumu yalioandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) huko katika ofisi zake Kikwajuni Mkoa wa Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

14 02 2011

WAKATI hali si shuari kwa baadhi ya vyuo vikuu nchini Tanzania Bara wanafunzi kugoma na wengine kutimuliwa vyuoni hali kama hiyo imeanza kujitokeza katika chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA) baada ya wakufunzi wake kutishia kugoma na kuzuia matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa chuo hicho.Madai mengine wanayodai wanataaluma hao ni pampja na kutopandishwa madaraja kwa kipindi cha miaka saba wakiendelea kutoa mihadhara kama wahadhiri wasaidizi huku watendaji wa idara za utawala wakilipwa stahiki zao.Endelea kusoma habar hii

6 02 2011

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuandaa sheria na kupitia upya muundo wa mashirika ya umma kwa kupunguza wafanyakazi wake kwa mashirika ambayo yatashindwa kujiendesha kibiashara na kutakiwa mshirika yote kuanzia sasa kulipa kodi serikalini na kuachana na tabia ya kuomba misamaha ya kodi.Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango, Omar Yussuf Mzee alipokuwa akiongea na wakurugenzi na watendaji wakuu wa mashirika ofisini kwake Vuga jana ambapo alisema baadhi ya mashirika yamekuwa ni mzigo kwa serikali kutokana na kushindwa kuyaendeleza kibiashara.Endelea kusoma habari hii

5 02 2011

SIKU chache baada ya wananchi wa Mji Mkongwe kutoa malalamiko yao kudharauliwa amri ya mahakama ya kutaka baadhi ya baa zilizopo katika makaazi ya watu zifungwe, watu wasiojulikana wameripua na kuiteketeza kwa moto baa moja iliyopo Mji Mkongwe Zanzibar.Wimbo hilo la watu kujichukulia sheria mikononi limeanza wiki iliyopita katika maeneo ya Darajabovu na Mwanyanya kuzichoma baa mbili zilizopo katika maeneo ya makaazi ya watu baada ya malalamiko yao ya muda mrefu kutochukuliwa hatua yoyote.Endelea kusoma habari hii

4 02 2011

MKURUGENZI British Council, Sally Robinson amesema progaramu ya vipindi vilivyoandaliwa na shirika hilo ambavyo vitatangazwa na Sauti ya Tanzania Zanzibar, vimelenga kuinua kiwango cha ufundishaji wa lugha ya kiingereza kwa walimu wa Zanzibar.Mkurugenzi huyo alieleza hayo jana katika kituo cha walimu Bububu (TC), kwenye uzinduzi rasmi wa urushwaji wa vipindi hivyo.Endelea kusoma habari hii

2 02 2011

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ramadhan Abdallah Shaban amemgonga na baadae kufariki Askari Polisi, Koplo Ali Khamis Haji (40), akiwa amepakiwa katika pikipiki huko katika mtaa wa Mombasa Mjini Zanzibar.Mkasa huo ulitokea Januari 13 mwaka huu, baada ya Waziri Shaban kukatisha katika barabara kuu akitokea katika mtaa wa SOS, na kuwagonga watu hao waliokuwa wamepakiana katika Vespa yenye namba za usajili Z 830 CA iliyokuwa ikitokea katika eneo la Mwanakwerekwe kuelekea Kiembesamaki.Endelea kusoma habari hii

2 02 2011

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuanzia sasa wasafiri wote wanaoingia Zanzibar watalaazimika kuwa na cheti kinachoonyesha wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano ambayo imeenea katika baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika ya Kusini. Nabu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya aliwaambia waandishi wa habari katika jana ofisini kwake jana Mnazi Mmoja Mjini Unguja kwamba serikali imeamua kutoa agizo hilo kufuatia tishio la ugonjwa huo hatari kutokea katika baadhi ya nchi.Endelea kusoma habari hii

2 02 2011

WANANCHI wa Mji Mkongwe wamevitaka vyombo vya vinavyohusika kuchukua hatua dhidi ya wamiliki vya baa zinazokwenda kinyume na taratibu za kisheria kabla ya wananchi kuchukua hatua mikononi mwao.Tukio la hivi karibuni wananchi walichukua hatua mikononi huko Darajabovu, Peace Love, maarufu Kwamzushi na baa ya Mwanyanya kuchomwa moto baa mbili zilizopo maeneo hayo.Endelea kusoma habari hii

1 02 2011

Ismail Jussa LadhuMWAKILISHI wa Mji Mkongwe Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amewataka vijana wanaoacha madawa ya kulevya visiwani hapa kuendelea na ujasiri waliouonesha ili vijana wenzao waweze kuiga mfano wao.Jussa alisema hayo muda mfupi baada ya kuwakabidhi vijana hao shilingi millioni 1.2 wakati alipowatembelea katika vituo vya nyumba za vijana hao ‘Sober House’ ambapo jumla ya vijana 300 wameonesha nia yak taka kuachana na madawa ya kulevya haa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

HUKUMU HII NAMUACHIA MUNGU-MAMA GHAILAN

26 01 2011

Mama Ghailan

KUFUATIA hukumu ya kifungo cha maisha cha Mtanzania, Ahmed Ghailan, Mama Mzazi wa kijana huyo, Bimkubwa Suleiman amesema hawezi kuongea chochote kwa kuwa hali yake sio nzuri kutokana na hukumu hiyo ya mwanawe.Bimkubwa ambaye amekuwa akifuatilia hukumu ya mwanawe huyo jana alionekana akiwa na simanzi kubwa na kushindwa kuzungumza tofauti na siku moja iliyopita ambapo alisema chochote kitakachoamuliwa na mahakama hiyo kitakuwa kimeshapangwa na Mwenyeenzi Mugu na hakuna wa kuweza kukipangua.Endelea kusoma habari hii

WATU 17 WAHOFIWA KUFA MAJI KISIWANI PEMBA

25 01 2011

WATU 17 wanahofiwa kufa maji katika kisiwa cha Pemba baada ya jahazi waliokuwa wakisafiri kuelekea Tanga kupasuka vipande viwili huko Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.Ajali hiyo inaelezwa kutokea jumapili iliyopita ambapo watu 18 walikuwa wanasafiria chombo hicho aina ya jahazi ambalo haikufahamika mara moja kama lilikuwa limeondoka kwa ajili ya kusafirisha abria au kwa ajili ya ya shughuli za uvuvi.Endelea kusoma habari hii

UKIMWI UPO ZANZIBAR MJIHADHARI -MAALIM

25 01 2011

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ameziagiza taasisi zote visiwani humo kujipanga upya katika suala la kusimamia vita dhidi ya ukimwi.Alisema ingawa Zanzibar ina kiwango kidogo cha maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, juhudi mpya inahitajika kuhakikisha kiwango hicho hakiogezeki.Endelea kusoma habari hii

ASKOFU AVUTIWA NA HALI YA AMANI ZANZIBAR

22 01 2011

ASKOFU Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, (TAG) Barnabas Mtokambali amevutiwa na maendeleo ya kisiasa yaliopo hivi sasa Zanzibar na kuwataka wanasiasa wa Tanzania Bara kuiga mfano huo.Kauli hiyo ya Askofu imekuja muda mfupi baada ya kumsimika Mchungaji Mwandamizi, Dickson Kaganga, kuwa Askofu wa jimbo la TAG, Jimbo la Zanzibar hapo jana katika Kanisa la Assemblies of God liliopo Kariakoo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

VYUO VIKUU VYATAKIWA KUFUNGUA MATAWI ZNZ

22 01 2011

SERIKALI imevitaka vyuo vikuu duniani kote kufungua matawi yao hapa Zanzibar kutokana na kuwepo mazingira mazuri ya kuwekeza katika elimu, pamoja na soko kubwa la wanafunzi wa ndani na nje ya nchi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito huo jana alipohutubia katika mahafali ya tano ya Chuo Kikuu cha Elimu cha Zanzibar kilichopo Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

ZOGO LA DARAJANI POLISI MMOJA AJERUHIWA

22 01 2011

WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar jana aliingilia kati mgogoro kati ya Manispaa ya Zanzibar na wafanyabiashara katika eneo la Darajani mjini hapa. Hatua ya Waziri Nassor Ahmed Mazrui imekuja siku moja baada ya juhudi ya manispaa kukwama kuwaondoa wafanyabiashara katika eneo hilo kwa kutumia polisi juzi.Endelea kusoma habari hii

WALEMAVU WASINYIMWE ELIMU-MAALIM SEIF

22 01 2011

MAKAMU WA Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ametaka suala la elimu lipewe nafasi ya kwanza katika mipango ya maendeleo ya taasisi zinazosimamia ustawi wa wamelavu. “Elimu ndio njia pekee kwa sasa ya kuwaondolea walemavu kikwazo cha kuingia katika soko la ajira,” alisema Maalim Seif jana mwishoni mwa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea idara zinazotoa huduma kwa wananchi chini ya ofisi yake.Endelea kusoma habari hii

MAALIM ATOA ONYO KWA WAHARIBIFU MAZINGIRA

17 01 2011

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad leo aliishtukia tabia ya utumiaji magari ya serikali kwa kazi ya kuchimba na kusomba mchanga na kuagiza yaorodheshwe na orodha hiyo ipelekwe ofisini kwake kwa haraka. Maalim Seif alitoa agizo hilo katika eneo la Donge, Chechele, mwanzoni mwa ziara yake ya siku tatu katika taasisi za umma zinazofanyakazi chini ya Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais katika mkoa wa Mjini Magharibi.Endelea kusoma habari hii

PAKISTANI NA ZANZIBAR KUBADILISHANA UZOEFU

14 01 2011

PAKISTAN imeeleza azma yake ya kuzidisha uhusiano na ushirikiano wake wa kihistoria na Zazibar kwa kuleta ujumbe maalum kwa ajili ya kuangalia maeneo ya kushirikiana hasa katika sekta ya uekezaji na utalii.Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Tajammul Altaf aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Ali Mohammed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WANAHITAJI KUSHAJIISHWA-DK SHEIN

13 01 2011

Dk Shein na Shamsi Nahodha

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa usimamizi, elimu na ushajishaji unahitajika kwa wananchi katika ushiriki wao kwenye programu ya ulinzi shirikishi.Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha, aliyefika Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii.

ASKARI OMBA OMBA WAMKERA MAALIM SEIF

11 01 2011

MAKAMU wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

Maalim Seif na Nahodha

amekemea ya tabia ya askari wa magereza wenye kutumia mamlaka yao vibaya na kuingiza madawa ya kulevya katika vyuo vya mafunzo.Maalim Seif aliyasema hayo wakati akizungumza na waziri wa mambo ya ndani nchini, Shamsi Vuai Nahodha alipofika ofisini kwake Migombani kujitambulisha jana mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

TUTAPAMBANA NA WABADHIRIFU NA WEZI-SMZ

10 01 2011

Dk Shein akifungua kituo cha afya Pemba

WATU wenye kujishughulisha na vitendo vya uharibifu, wizi wa fedha na mali za umma wametakiwa kuacha mara moja, vinginevyo watakabiliana na mkondo wa sheria. Onyo hilo limetolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein, alipohutubia wananchi huko Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya kufungua kituo cha Afya na nyumba ya madaktari.Endelea kusoma habari hii

MAMIA WAMZIKA KADA WA CCM

5 01 2011

Salum Juma Othman

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ameongoza mamia ya wananchi kumzika Kada wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Salum Juma Othman (60).Othman alifariki juzi mchana katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alikokuwa amelazwa kwa wiki mbili akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na homa ambapo uongozi wa hospitali hiyo umethibitisha kutokea kwa kifo hicho.Endelea kusoma habari hii

KARUME AMTETEA BINTI YAKE JUU YA KIWANJA

1 01 2011

Amani Karume na Bintie FatmaRAIS Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amtetea Mwanawe Fatma Karume kuwa ndio mmiliki halali wa kiwanja kilichopo Mbweni eneo la Mfuuni ambacho kimeingia katika mgogoro kati ya Kanisa la Angalikan na mwanawe huyo.Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jana, Mbweni, Karume alisema mwanawe ana hati kamili za kiwanja hicho kutoka serikalini kwa kuwa ametimiza vigezo vyote vinavyohitajika na hivyo anastahiki kujenga kwa kuwa kiwanja hicho ni chake.Endelea kupata habari zaidi

WAANGALIKAN WADAI KUPORWA ARDHI MBWENI

31 12 2010

Waumini wakiwa katika eneo linalodaiwa kuporwa

WAUMINI wa dini ya Kikristo wa madhehebu ya Angalikana jana kwa hasira wamevamia kiwanja cha familia ya Rais Mstaafu wa Zanzibar aliyemalizia muda wake hivi karibuni Amani Abeid Karume na kuonesha hasira zao kwa kuvunja vunja baadhi ya mbao na kupindua matangi ya maji yanayotumika katika ujenzi wa jengo katika eneo la Mbweni Mjini Unguja.Waumini hao awali walikuwa watulivu wakati wa ibada ya maombi yaliyoongozwa na Kasisi Kiongozi Mathew Wilfred Mhagama wa kanisa la Angalikan la Mkunazini sala iliyofanyika Mbweni kanisa ambalo lipo karibu na kiwanja kinachodaiwa kuporwa na familia hiyo ya Rais Karume.Endelea kusoma habari hii

MAJENGO YA SERIKALI YAZINGATIE NA WALEMAVU-SEIF

30 12 2010

Maalim Seif

MAKAMU wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharif Hamad ametaka majengo yote ya serikali yazingatie mahitaji ya walemavu ili walemavu waweze kuyafikia bila ya vikwazo vyovyote.Maalim Seif ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Walemavu Zanzibar, Abeida Rashid Abdallah ofisini kwake Migombani alipokuwa akizungumza na uongozi wa ofisini hiyo ambayo ipo chini ya ofisini ya makamu wa kwanza wa rais.Endelea kusoma habari hii

AIR UTURUKI KUANZA SAFARI ZANZIBAR

30 12 2010

SEKTA mbali mbali za maendeleo za Zanzibar zitapata msukumo mkubwa kutoka Uturuki kutokana na uhusiano na mashirikiano mazuri yaliopo kati ya nchi mbili hizo.Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dr. Sander Gurbuz aliyasema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

KESI YA MCHOMAJI QURAN YATINGA MAHKAMANI

30 12 2010

MAMIA ya wafuasi wa Dini ya Kiislam wiki hii walifurika katika Mahkama ya wilaya ya Mwanakwerekwe kufuatilia kesi ya mshtakiwa aliedaiwa kuchoma moto Quran Tukufu na Novemba 16 mwaka huu.Mahkama hiyo iliyofurika watu ndani na nje ya jengo ilisikiliza mashahidi watatu upande wa mashtaka ambao wote walitoa ushahidi wa kuona tukio na kushuhudia na kushuhudia vitabu hivyo vya Quran ikiwemo msahafu, juzuu na vitabu vya kiisamu vilivyochomwa moto muda mfupi baada ya tukio.Endelea kusoma habari hii

SERIKALI HAITAFUMBA MACHO-MAALIM SEIF

29 12 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar iliyo chini ya mfumo ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa imesema itafumba macho katika suala zima la ufumbuzi wa madawa ya kulevya visiwani hapa.Kauli hiyo imetolewa juzi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad huko ofisini kwake Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi wakati akizungumza na watendaji wakuu wanaohusika na wa idara ya kupambana na madawa ya kulevya Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

SERIKALI YAAMURU KUVUNJA MAJENGO MAPYA

28 12 2010

MAKAMU wa Pili wa rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd ametoa amri ya kuvunjwa majengo ya nyumba zilizofutiwa vibali hivi karibuni katika eneo la Mombasa kwa Mchina nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Amri hiyo ameitoa mbele ya watendaji wa serikali wanaohusika na ardhi na viwanja pamoja na viongozi wa halmshauri huku akiwa ameonesha kukerwa baada ya agizo lake alilolitoa wiki iliyopita kutoheshimiwa na viongozi hao ambayo aliwaita wanafanya mambo ya kipumbavu.Endelea kusoma habari hii

KOREA KUIMARISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MAJI

28 12 2010

KOREA Kusini imeeleza azma yake ya kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya kilimo cha umwagiliaji maji.Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Young-Hoom Kim aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN AGEUKA MBOGO AWAAPISHA MAJAJI

21 12 2010

Fatma Hamid Mahmoud akila kiapo Ikulu

Hatimae Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein jana amewaapisha majaji wanne wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja.Majaji walioapishwa kwa mbwembwe wakiwa wamevalia majokho ni Jaji Abdulahakim Ameir Issa, Jaji Rabia Hussein Mohammed, Mkusa Issac Sepetu na Jaji Fatma Hamid Mahmoud ambaye ni Mwanawe Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahmoud.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WAJA JUU UPORAJI WA ARDHI PEMBA

13 12 2010

KUFUATIA agizo la Makamu wa pili wa rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alilolitoa hivi karibuni juu ya uvamizi wa ardhi unaofanywa na watendaji wa serikali na masheha katika maeneo mbali mbali, wananchi wa kisiwani Pemba wameitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya watu wenye kupora ardhi zao za kilimo.Wananchi kwa nyakati tofauti wamezungumza na waandishi wa habari na kuitaka serikali kusimamia agizo hilo alilolitoa Balozi Iddi ili warejeshewe ardhi yao ambayo wamedai kuchukuliwa na wanasiasa na wafanyabiashara nchini kwa lengo la kujinufaisha kifedha.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR YALALAMIKIWA KWA UPORAJI ARDHI

9 12 2010

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaungana na nchi nyengine duniani kote kuadhimisha siku hiyo na kwa hapa Zanzibar itazingatia mambo manne muhimu waliojitokeza visiwani hapa.Mambo ambayo yatazingatiwa katika siku hiyo ni kuendeleza maridhiano ya kisiasa yaliofika Novemba mwaka jana, kushughulikia kesi za migogoro ya ardhi, hali ya udhalilishaji wa wanawake na watoto na suala zina la ukosefu wa ajira nchini.Endelea kusoma habari hii

DK SHEIN KUWAAPISHA MAJAJI KESHO?

6 12 2010

Abdulhakim ni miongoni mwa majaji wanne wateule

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amekuwa akisitasita kuwaapisha majaji wanne aliowateuwa Novemba 29 mwaka huu kufuatia barua aliyoandikiwa na Chama Cha Mawakili Zanzibar (ZLS) juu ya uteuzi huo kutozingatia taratibu.Kusita huko kwa Dk Shein kuwaapisha tangu awateuwe kunaelezwa kuwa kunatokana na utata wa kisheria uliopo kutokana na majaji hao kutoiva vya kutosha katika taaluma ya sheria na kwa mujibu wa sheria tume ya utumishi ilipaswa kukaa kuidhinisha majina hayo jambo ambalo halikufanywa kwa baadhi ya majaji walioteuliwa.Endelea kusoma habari hii

UNYANYAPAA ZANZIBAR NI TATIZO

30 11 2010

UNYANYAPAA kwa watu wenye kuishi na vizuri vya ukimwi Zanzibar imeelezwa kuwa ni tatizo ambalo linaendelea kuwasumbua licha ya juhudi mbali mbali za kuliondosha tatizo hilo.Kwa mujibu wa watu wneye kuishi na vizuri vya ukimwi katika maeneo mbali mbali visiwnai hapa wamesema bado wanaendelea kupata shida mitaani mwao na baadhi ya taasisi wanazofanyia kazi endapo wakijulikana kama wameambukizwa vizuri.Endelea kusoma habari hii

WAANDISHI WAPIGWA MSASA WA UTAWALA BORA

23 11 2010

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Michezo Zanzibar, Said Shaaban amesema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuifanya nchi kuwa na utawala bora iwapo wataitumia kwa umakini taaluma yao.Shaaban ameyasema hayo jana katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya utawala bora katika nchi iiliyofanyika Hoteli ya Mazson’s Shangani mjini hapa.Endelea kusoma habari hii

KARUME ATUNUKIWA NGAO YA DHAHABU

27 10 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume jana ametunukiwa zawadi ya ngao ya dhahabu ya amani ya uongozi uliotukuka yeye na Mama Shadya Karume ikiwa ni ishara ya mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Zanzibar.Sherehe hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na Mgombea urais wa zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na rais msataafu Ali Hassan Mwinyi na viongozi wengine.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WA TUMBATU WAPATA UMEME

22 10 2010

WANANCHI wa kisiwa cha Tumbatu wametoa pongezi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Karume kwa kuwafikishia huduma ya umeme na kueleza kuwa kitakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kisiwani humo.Wananchi hao waliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Tumbatu ambacho ni kisIwa kilichoko Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusisitiza kuwa ni kitendo cha kihistoria.Endelea kusoma habari hii

WAISLAMU WAKERWA KUCHEZEWA QUR-AN MIKUTANONI

13 10 2010

BARAZA Kuu la Wanawake wa Kiislamu Wilaya ya Magharibi Unguja limekemea tabia ya vyama vya Siasa kuisoma Qur ani kabla ya kuanza mikutano yao na kusoma dua baada ya kumalizia mikutano, jambo ambalo wamesema haliendani na uislamu.Katika barua yao ya Oktoba 11 ya mwaka huu, iliyotolewa na baraza hilo na kusainiwa na Msimamizi Mkuu Ustadh Abdallah Mnubi Abbas imeeleza kwamba kitendo hicho ni kosa kidini na hata kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa muundo wa Serikali hauna dini.Endelea kusoma habari hii

MADEREVA WANANE WAFUTIWA LESENI

11 10 2010

MADEREVA nane wa magari ya abiria, mizigo na ya watu binafsi wamefungiwa leseni zao chini ya operesheni maalumu ya kupunguza ajali barabarani visiwani Zanzibar.Kati ya madereva hao wanne wamefungiwa kwa miezi miwili na wanne watatumikia adhabu hiyo kwa mwaka mmoja, na utekelezaji wa adhabu hiyo umeanza jana.Endelea kusoma habari hii

HATUNA KESI MAHAKAMANI-ZECO

4 10 2010

SHIRIKA la Umeme Zanzibar limesema linashindwa kufungua kesi mahakamani wakati wanapotokea udanganyifu wowote kuhusiana na matumizi ya huduma za umeme, kutokana na kushindikana kupatikana kwa mashahidi.Hayo yameelezwa na Mwanasheria wa Shirika hilo,Ali Hamad, katika warsha ya siku moja iliyowashirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali nchini iliyofanyika katika ukumbi wa ECROTANAL Mjini hapa.Endelea kusoma habari hii

KESI YA MWANDISHI KUANZA KUSIKILIZWA LEO

30 09 2010

MAHAKAMA ya Mkoa Vuga iliyopo mjini Zanzibar, jana imeanza kusikiliza kesi inayomkabili mwandishi wa habari wa magazeti ya The Guardian na Nipashe Mwinyi Sadallah, juu ya madai ya kuandika taarifa isiyo ya kweli dhidi ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume. Kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo kumekuja huku kukiwa kumepita miaka mitatu, tangu Sadallah apandishwe kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 2008, akishitakiwa pamoja na Ramadhan Mohammed Vuai mkaazi wa Chwaka. Endelea kusoma habari hii

ASHITAKIWA KWA UDANGANYIFU

30 09 2010

MKAAZI mmoja wa Kwahani wilaya ya Mjini Unguja, ametinga katika kizimba cha mahakama ya Wilaya Mwanakwereke kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Mtuhumiwa huyo ambae alitambulika kwa jina la Bw. Subira Amiri Kondo (36), alifikishwa mahakamani hapo jana kujibu tuhuma zake hizo ambazo alizikana.Endelea kusoma habari hii

HOTELI ZA KITALII ZAWAKA MOTO NUNGWI

9 09 2010

ZAIDI ya hoteli nne za kitalii na nyumba 12 za wananchi wa kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja zimeteketea vibaya kwa moto jana majira ya saa 7:12 mchana katika kijiji hicho. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema awali waliona moto na moshi mkubwa ukitokea katika maeneo yenye hoteli za kitalii na baadae moto huo kusambaa katika hoteli nyengine ambazo zilikuwa zikiwaka kwa kasi kubwa kutokana na upepo uliokuwa ukivuma baharini nyakti hizo.Endelea kusoma habari hii

WAANDISHI WA HABARI WAONYWA

9 09 2010

Hassan Mitawi

WAANDISHI wa habari wametakiwa kukataa kuwatii na kutumiwa na wanasiasa ambao wanaopenda kujinufaisha wao na vyama vyao katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar, Hassan Abdallah Mitawi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha siku moja kilichokuwa kikijadili maadili ya uandishi wa habari katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.Endelea kusoma habari hii

MLINZI WA MAKAMU AUWA KWA RISASI

8 09 2010

KIJANA Mohammed Ali Mohammed amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wanaolinda nyumba ya makamu wa rais Dk Ali Mohammed Shein Maisara Mjini Unguja.Mtu ambaye anatuhumiwa kuwa mwizi alionekana maeneo ya gereje maarufu Gofu iliyopo katibu na nyumba ya makamu wa rais Kikwajuni (Bosnia) Mkoa wa Mjini Magharibi.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WATAHADHARISHWA

6 09 2010

WANANCHI wametakiwa kuwa makini na bidhaa zinazoingizwa nchini ambazo nyingi zimemaliza muda wake hasa katika kipindi hiki cha kukaribia sikukuu baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.Tahadhari hiyo imetolewa na wataalamu wa afya baada ya kugundulika kuwa bidhaa nyingi zisizofaa kutumika kwa matumizi ya binaadamu kuingizwa nchini na kutumiwa na wananchi mbali mbali mjini na vijijini.Endelea kusoma habari hii

WENYE ULAMAVU WATAKA KUSHIRIKISHWA

5 09 2010

Adil Mohammed

WATU wenye ulemavu wamesema licha ya kuwepo haki na sheria ya kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi bado mazingira yaliopo katika utekelezaji wa sheria hiyo ni magumu kwa upande wao.Hayo yameelezwa katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari, walioshiriki wa mafunzo hayo juu ya kujua sera za watu wenye ulamavu na majukumu ya waandishi wa habari katika kuwatetea.Endelea kusoma habari hii

KUWEPO AMANI KUNAZIDISHA IMANI-SPIKA

2 09 2010

Pandu Ameir Kificho

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amesema kwamba kuwepo kwa amani na utulivu kutasaidiwa kwa kiasi kikubwa kuzidisha ibada kwa waumini wa dini ya kiislamu visiwani hapa. Kificho aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua Itiqaf ya kimataifa inayoendelea kufanyika kwenye Madrasat Fii-sabililah Aman kwa Said wa Washoto ambayo huwashirikisha waumini wa dini ya kiislamu kutoka ndani na nje ya nchi mbali mbali.Endelea kusoma habari hii

MAMIA WAMZIKA MUFTI WA ZANZIBAR

31 08 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume jana ameongoza umati mkubwa wa waumini wa kiislamu katika ibada ya sala ya mazishi ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar Marehemu Sheikh Harith Bin Khelef Bin Khamis.Ibada hiyo ilifanyika katika msikiti wa Al Mushawar uliopo Mwembeshauri mtaa wa Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi kabda ya kwenda kupelekwa kijijini kwao Muyuni mkoa wa kusini Unguja.Endelea kusoma habari hii

MAZISHI YA MUFTI YAAKHIRISHWA

29 08 2010

MAZISHI ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Harith Bin Khelef yaliokuwa yafanyike leo viziwani Zanzibar yamekhirika kufuatia maiti yake kuchelewa kuwasili kutoka Nchini India alipofia juzi.Mufti ambaye alikuwa na umri wa miaka 85 amefariki dunia juzi akiwa matibabuni alipokuwa amepelekwa wiki tatu zilizopita ambapo alikuwa akizumbuliwa na matatizo ya mkojo muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji.Endelea kusoma habari hii

JENGO JIPYA LA MAYATIMA LAFUNGULIWA

28 08 2010

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume, amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya ulimwengu na kukua kwa uchumi ipo haja kwa watoto nao kujengewa makaazi bora yenye utulivu na yanayokwenda na wakati uliopo.Akifungua nyumba mpya ya makaazi ya watoto yatima, iliyopo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar, iliyojengwa kwa ufadhili wa Jumuiya ya ZAYEDESA, Rais Karume alisema kuwa watoto wana haki ya kuishi maisha bora ambayo yatawasaidia kupata huduma zote muhimu na za lazima ili kuweza kuwaendeshea maisha yao.Endelea kusoma habari hii

MUFTI WA ZANZIBAR AFARIKI DUNIA

27 08 2010

Mufti Harith Bin Khelef

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith Bin Khelef Khamis (80) amefariki dunia akiwa nchini India ambapo alikwenda matibabu wiki mbili zilizopita.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mufti imesema kwamba Mufti amefariki dunia jana asuhuhi katika hospitali ya Meyot Mjini Chanay nchini IdiaKatibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga amesema Zanzibar imepata msiba mkubwa kwa kuondokewa na kiongozi wake huku akisisitiza wananchi kuwa na subra katika msiba huo.Endelea kusoma habari hii

WAANDISHI WATAKIWA KUFUATA MAADILI

25 08 2010

Balozi Alfonso na waandishi wa habari

WAANDISHI wa waandishi wa habari wametakiwa kufuata maadili ya kazi zao ili kusaidia kupanuwa demokrasia hasa wakati huu ambao watanzania wanaelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Wito huo umetolewa na Balozi wa Marekani, Alfonso Leinhardt alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali katika ofisi za jingo jipya la baraza la wawakilishi Chukwani Mjini Unguja.Endelea kusoma habari hii

MWAKILISHI NA DIWANI WA CUF WAFARIKI

24 08 2010

Omar Ali Jadi

WAKATI mchakato wa uchukuaji fomu ukiingia katika siku ya tatu wagombea wawili wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefariki dunia jana visiwani Zanzibar katika matukio tofauti. Waliofariki dunia ni aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Kojani (CUF) Omar Ali Jadi (55) Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mwalimu Shani Hamada Shani ambaye ni mgombea wa udiwani wa chama hicho katika jimbo la Kikwajuni.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WALALAMIKIA MFUMKO WA BEI

14 08 2010

WANANACHI wengi wanaofunga mwezi mtukufu wa ramadhani Zanzibar wameanza kulalamikia bei za kubwa za bidhaa mbali mbali za vyakula ambavyo hutumika katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa ramadhani.Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba bidhaa za vyakula kama viazi vikuu, ndizi, muhogo na nazi bei zake zimepanda kwa kiasi kikubwa katika masoko makuu ya Mwanakwerekwe na soko la Darajani Mkoa wa Mjini Magharibi.Ndizi aina ya mtwike mkungu mmoja inauzwa kati ya shilingi 10,000 hadi 13,000 huku ndizi aina ya Koroboi huuzwa kati ya shilingi 9,000 hadi 10,000.Endelea kusoma habari hii

ABUDHABI KUJA KUWEKEZA ZANZIBAR

13 08 2010

Jeff Reynolds na Rais Karume

KAMPUNI ya viwanja vya ndege ya Abudhabi (ADAC) imeeleza nia yake ya kuwekeza katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Karume Zanzibar na kueleza namna ilivyovutiwa na hatua zilizofikiwa katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini.Rais wa Kampuni hiyo, Jeff Reynolds alieleza hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume Ikulu Mkoa wa Mjini UngujaKatika maelezo yake, Reynolds ambaye alifika Ikulu na ujumbe wake, alimueleza Rais Karume kuwa Kampuni ya ADAC imevutiwa na mazingira ya Zanzibar sanjari na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimaitaifa wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii
13 08 2010KUFUATIA idadi kubwa ya mimba za utotoni mshuleni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeahidi kuweka mkazo katika kupunguza idadi hiyo na kujenga mazingira mazuri kwa wanafunzi wa kike mashuleni.Moja ya mikakati iliyowekwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ni kuwarejesha watoto wote waliopata mimba wakiwa mashuleni na kuwataka warejee masomoni ili kumaliza masomo yao.Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwanaidi Saleh Abdalla aliyasema hayo wakati akifunguwa mafunzo ya vitendo ya siku mbili kwa waandishi wa habari juu ya kuandika habari za athari za mimba za umri mdogo na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.Endelea kusoma habari hii
8 08 2010JUMLA ya hoteli tatu za kitalii na zaidi ya nyumba sita za wananchi zimeteketea kwa moto jana asubuhi katika kijiji cha Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho walioshuhudia moto huo wamesema waliona moto mkubwa ukiwaka katika hoteli za kitalii na kutoka nje na kusaidiana na wamiliki wa hoteli hizo kwa kuuzima.Hoteli zilizoungua ni pamoja na Visitors Inn, Sau Inn na Bungalow ambapo zote zipo eneo la Jambiani ukanda wa pwani ambapo moto huo uliwaka kwa kasi kutoka na hoteli hizo kuezekwa kwa makuti ambapo moto ilishika kasi kutokana na upepo mkubwa uliokuwa ukivuma nyakati za asubuhi.Endelea kusoma habari hii.
17 06 2010RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume amesema kuwa mashirikiano kati ya Wizara ya Kilimo na Kikosi cha JKU katika kuimarisha sekta ya kilimo yameweza kuleta tija na mafanikio makubwa.Karume aliyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea bonde la mpunga la Upenja Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo alishiriki katika uzinduzi wa uvunaji mpunga pamoja na kutembelea shamba la Bambi Mkoa wa Kusini Unguja na kutembelea shamba la mahindi na mtama.Akizungumza na wapiganaji wa JKU katika mashamba hayo, Rais Karume alieleza kuwa mashirikiano yaliooneshwa kati ya JKU na Wizara ya Kilimo Zanzibar, yameweza kuimarisha sekta kilimo na kuleta matumaini ya uzalishaji chini.Endelea kusoma habari hii
9 06 2010SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imo katika mchakato wa uwekaji waya chini kwa chini kwa ajili ya

Samia Suluhu Hassan

mawasiliano ya simu ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya mawasiliano kwa urahisi zaidi.Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Bwawani Mjini Unguja kuafuatia ziara yake ya nchini China.Alisema kuwa hatu hiyo pamoja na huduma hiyo kuwafikia wananchi lakini pia ni mateghemeo yao kuwa wataifikisha hadi katika sehemu zote za Serikali ya Zanzibar kwa manufaa ya kuondokana na hali ya usumbufu wa mawasiliano.Endelea kusoma habari hii

ADB YARIDHISHWA NA MIRADI YA ZANZIBAR

8 06 2010

BENKI ya Maendeleo Afrika (ADB) imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa hapa Zanzibar kwa ushirikiano baina ya Zanzibar na Benki hiyo na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuleta mafanikio zaidi.Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo Afrka (ADB), anaemaliza muda wake hapa nchini Dk. Sipho Moyo aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume, Ikulu mjini Zanzibar.Katika maelezo yake Mwakilishi Mkaazi huyo, alimueleza Rais Karume kuwa ADB inafarajika kwa kiasi kikubwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyopo hapa Zanzibar kutokana na kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.Alisema kuwa hatua ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa mashirikiano na ADB hapa Zanzibar ni nzuri na ya kuungwa mkono katika suala zima la kuleta maendeleo na kuimarisha uchumi.Endelea kusoma habari hii

KARUME AHIMIZA USHIRIKIANO NA CHINA

28 05 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume ametoa wito wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Zanzibar na Shenzhen. Wito huo ameutoa wakati wa mazungumzo na Makamu Meya wa Shenzhen Bwana Zhuo Quinrui baada ya kupokewa rasmi na kiongozi huyo katika Hoteli ya Futian Shangrila.Rais Karume alimueleza kiongozi huyo pamoja na viongoi wengine wa Shenzhen hali ya maendeleo ya miundombinu mbali mbali iliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo inatoa fursa nzuri za uwekezaji.Alisema kuwa zipo fursa nyingi za uwekezaji Zanzibar katika maeneo ya viwanda vidogo vidogo na vya katipamoja na matumizi ya bandari na uwanja wa ndege kutokana na kuwepo kwa soko kubwa la Afrika Mashariki pamoja na soko la SADC.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR KUJADILI SOKO LA PAMOJA

17 05 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume leo anatarajiwa kufungua mkutano wa baraza la biashara la Zanzibar utakaoangalia jinsi gani Zanzibar itashiriki kwenye soko la pamoja la Afrika ya Mashariki.Lengo la mkutano huo ni kuwaelimisha wafanyabiashara wa Zanzibar juu ya umuhimu wa kulitumia soko la pamoja na kuyapatia ufumbuzi matatizo yao watakayokabiliana nayo katika soko hilo. Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Zanzibar Katibu mtendaji wa Jumuiya hiyo Ali Haji Vuai, alisema mkutano huo utatoa fursa ya wafanyabiashara wa Zanzibar kuzungumzia kero na changamoto zao zinazowakabili. Alisema karibuni wafanyabiashara wa Zanzibar wataingia katika soko la pamoja ambalo limeshasainiwa na utekelezaji wake utaanza hivi karibuni ambayo Zanzibar ni nchi pekee yenye visiwa itakayoingia katika shirikisho hilo.Endelea kusoma habari hii

UMEME WA UHAKIKA PEMBA WAFANYIWA MAJARIBIO

11 05 2010

WANANCHI wa Kisiwani Pemba wameanza kupata matunda ya mafanikio ya serikali yao baada ya umeme wa uhakika ulioungwa katika gridi ya taifa kutoka Tanga hadi kisiwani Pemba kuanza kuwashwa kwa majaribio.Umeme huo ambao umewashwa tokea juzi ikiwa ni majaribio ya kuwashwa kwake hadi hapo Juni 2 mwaka huu ambapo Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume atauzindua rasmi baada ya kukamilika kwa matengenezo ya waya zilizopita chini ya bahari kutoka Pengani Tanga hadi Wesha Kisiwani Pemba.Mradi huo wa umeme unafadhiliwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Misaada la NORAD umekamilika na kusaidia harakati za kuinua uchumi kwa wananchi Kisiwani humo kupitia mpango wa kukuza na kupunguza umasikini Zanzibar (MKUZA).Mambo mengine ambayo Shirika hilo la NORAD linafadhili ni kukamilisha kwa mradi mkubwa wa usambazaji wa umeme vijiji awamu ya tatu na ya nne unaofadhiliwa na Serikali ya Norway ambapo sasa karibu zaidi ya vijiji 64 Unguja na Pemba vimepata huduma ya nishati ya umeme.Endelea kusoma habari hii

UNDP YAFURAHISHWA NA ZANZIBAR

9 05 2010

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo Duniani (UNDP) limeeleza kufarajika na hatua za maendeleo zilizofikiwa hapa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuziweka pamoja afisi zote za Umoja wa Mataifa (ONE UN)

Helen Clarke Mkuu wa UNDP na Rais Karume

katika jengo moja, hali ambayo imeweza kurahisisha utendaji wa kazi.Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo Duniani (UNDP) Bi Helen Clarke aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume,Ikulu mjini Zanzibar.Katika mazungumzo hayo, Bi Clarke alimueleza Rais Karume kuwa mafanikio yaliopatikana Zanzibar ni makubwa na kuna kila sababu ya Shirika lake kuendelea kuyaunga mkono ili mafanikio hayo yaimerike zaidi.Bi Clarke alipongeza kwa mafanikio ya miradi inayoendeshwa na UNDP hapa Zanzibar.Akieleza juu ya kuvutiwa kwake na mipango maalum iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kuziweka katika jengo moja afisi zote za Mashirika ya Umoja wa Mataifa (ONE UN) zilizopo Zanzibar hapo katika jengo la kitega Uchumi la ZSTC liliopo Gulioni mjini Zanzibar, Bi Clarke alieleza kuwa hiyo ni hatua kubwa ya mafanikio.Endelea kusoma habari hii

BABA APONZWA NA DHAMANA YA MWANAWE

5 05 2010

Mahakama Kuu Zanzibar

MAHAKAMA Kuu Zanzibar imemfutia dhamana mtuhumiwa mmoja wa kesi ya mauwaji ya raia wa China, Hwang Hong Xing aliyeuawa Septemba 11,  baada ya mtuhumiwa huyo kutohudhuria mahakamani wakati kesi yake ikiendelea.Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu ya Vuga Mjini Zanzibar, Abraham Mwampashi anasikiliza kesi hiyo alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bimkubwa Said Bakari ambae ni mwanamke pekee anayekabiliwa na kesi hiyo ya mauaji ambaye ameyavunja masharti ya dhama aliyopewa Mahakamani hapo.Masharti hayo ni pamoja na kutohudhuria mahakamani kila siku ya kesi yake, kuripoti katika mahkama hiyo siku mbili kwa wiki siku ya Jummne na Ijumaa na kutotoka nje ya Zanzibar.Wengine waliopewa dhamana kwa kulipa milioni tano taslim kila mmoja, kuwasilisha mwaraka wa mali isiyohamishika na wadhamini watatu walioandika bondi ya shilingi millioni kumi kila mmoja ni Hassan Abdalla mwenye umri wa mika 25 mkaazi wa Michenzani na Khamis Ali Abdalla mwenye umri wa mika 36 mkaazi wa Melinne Wilaya ya Magharibi Unguja.Endelea kusoma habari hii

TUTAENDELEA KUDAI HAKI ZETU – WAANDISHI

4 05 2010

Waandishi wa habari siku ya uhuru wa habari duniani

WAANDISHI wa habari kutoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki na Kati waliokutana kwa siku mbili Visiwani Zanzibar wamesema wataendelea kudai haki kutoka katika serikali zao ili uhuru wa habari uheshimiwa katika nchi zao.Hayo yameelezwa katika kongamano la siku mbili la maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani lililofanyika katika hoteli ya Ocean View Mkoa wa Mjini Magharibi na kuwajumuisha washiriki zaidi ya 90 kutoka nchi 10 za Afrika Mashariki na kati.Akisoma maazimio ya kongamano hilo la Zanzibar, Mratibu wa Jumuiya ya waandishi wa habari wa Afrika Mashariki na Kati (EAJA), Tervil Okoko kutoka Djibouti amesema waandishi wa habari hawana budi kupambana na utamaduni wa uonevu, kupigania haki za binaadamu, amani, uadilifu, demokrasia na uhuru.Okoko amesema waandishi wanapaswa kulinda na kudumisha uhuru wa kujieleza, ambao unajumuisha uhuru wa habari, uhuru wa kuzungumza, na uhuru wa kuwa na mawazo kama ulivyobainishwa na Tamko la Ulimwengu na Haki za Binaadamu, Mkataba wa Afrika wa Haki za Watu na Tamko la Misingi ya Uhuru na Kujieleza la Afrika.Kufuatia michango mingi iliyowasilishwa katika kongamano hilo kuonekana kuna matatizo kwa upande wa wamiliki wa vyombo vya habari juu ya malipo na maslahi yao waandishi wa habari wameazimia kulinda na kushajiisha haki na maslahi ya wanahabari na waajiriwa wengine wa vyombo vya habari katika nchi zao.Endelea kusoma habari hii.

TANZANIA INAONGOZA KWA UHURU WA HABARI- KARUME

3 05 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid

Rais wa Zanzibar, Amani Karume

Karume amejigamba mbele ya waandishi kwamba Tanzania inaongoza kwa kuwa wingi na uhuru wa vyombo vya habari nchini ikilinganishwa na nchi nyingi katika Bara la Afrika. Rais Karume amesema kuwepo na wingi wa vyombo vya habari Tanzania ni ushahidi tosha wa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari kama dalili ya kupanuwa demokrasia na uhuru wa kujieleza pamoja na kufuta misingi ya utaala bora chini ya mfumo wa vyama vingi nchini.Karume alisema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna katika kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani iliyoadhimishwa na washiriki zaidi ya 90 kutoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki na Kati iliyofanyika hoteli ya Ocean View Zanzibar.Alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi ambazo zinaongoza kwa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari ambapo waandishi wanafanya kazi zao bila ya vikwazo vyovyote tofauti na nchi nying ambazo waandishi wa habari wanakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo kuuawa, kutekwa nyara na mambo tofauti kutokana na kutekeleza majukumu ya kazi zao.Endelea kusoma habari hii

UTORO UNAZIDI SHULE ZA MSINGI

15 04 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema asilimia kubwa ya wanafunzi wa shule ya msingi hawaendei na masomo yao kutokana tatizo la utoro na kuishia darasa la saba.Akizungumza na walimu wakuu wa shule mbali mbali wa mkoa wa mjini Magharibi Unguja, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman alisema asilimia saba ya watoto hawamalizi shule jambo ambalo linapaswa kushughulikiwa.Alisema tatizo hilo ni kubwa ambalo linasababishwa na mambo mbali mbali ikiwemo wazazi kupuuuza masuala ya elimu na walimu kutoshughulikia suala zima la wanafunzi.“Hili tatizo ni kubwa na hatuwezi kuliwacha bila ya kushughulikia ni lazima wazazi, masheha na walimu wakuu mlishughulikie suala hili ili kujua chanzo halisi ya watoto kuacha kuendelea na masomo” alisema Waziri huyo.Waziri Suleiman aliyasema hayo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kuacha shule ambapo alifanya mkutano wake na walimu wakuu, madiwani na masheha katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Haille Selassie Unguja.Endelea kusoma habari hii.

WANANCHI WAMEPOTEZA IMANI NA VIONGOZI-MCHUNGAJI

4 04 2010

KIONGOZI wa Kanisa Kuu la Anglikana Zanzibar, Mchungaji Stanley Nicholaus Lichinga amesema idadi ya wapiga kura inapungua kila mwaka kutokana na wananchi kukosa imani ya viongozi.Akizungumza katika mkesha wa maombi ya siku ya Pasaka Mchungaji huo alisema viongozi wengi wamepoteza muelekeo na kukiuka maadili na hivyo kusababisha wananchi wengi kupoteza imani na viongozi wao ambao walitegemewa kuwa mstari wa mbele katika kufuata maadili.“Hivi sasa msisimko wa vyama vingi unaendelea kudhorota na kusababisha kupungua kwa wapiga kura kwa sababu wanasiasa kupoteza maadili na wameweka maslahi yao mbele badala ya maslahi ya taifa na ndio sababu ya utekeleaji wa majukumu yao umekuwa ukiporomoka kila siku”, alisema kiongozi huyo.Akizungumzia suala la maridhiano ya kisiasa Mchungaji huyo alisema wananchi wamekuwa na matumaini makubwa juu ya kuwepo maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa na viongozi wa vyama vya siasa hivyo kuna kila sababu ya kutolewa elimu ya kutosha ili kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili washiriki kutoa maamuzi kwa nchi yao.Alisema kwamba ipo haja kwa viongozi kufuatia maridhiano yaliyofikiwa Zanzibar kutekeleza majukumu yao kwa kuwapatia haki wananchi ili kila mmoja apate haki yake ya kujiandikisha na kupiga kura achague kiongozi amtakaye ambaye atakayejali watu na taifa badala ya kujenga uadui na kufarakisha wananchi kwa misingi ya kisiasa.Endelea kusoma habari hii

MV. SERENGETI YATEKETEA KWA MOTO

13 03 2010

MOSHI mkubwa umetanda visiwani Zanzibar jana baada ya Meli ya MV Serengeti kuteketea kabisa kwa moto kando ya Bandari ya Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ilipokuwa imeegeshwa ikisubiri safari ya kwenda Pemba.Meli hiyo ambayo inayomilikiwa na Kampuni ya Jack Enterprises iliyosajiliwa Zanzibar ambayo hufanya safari zake Tanga, Pemba na Dar es salaam imeanza kuungua kwa moto majira ya saa 700 mchana.Kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wanasema meli hiyo ilikuwa imeegeshwa kando ya bandari ambapo baadhi ya mabaharia wanane waliokuwemo ndani wameweza kuokolowa haraka muda mfupi baada ya moto huo kuwaka kwa kasi kubwa.Moto huo ulikuwa ukiwaka kwa kasi kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma katika bahari ya hindi na kusababisha hali ngumu kwa kikosi cha wanamaji na waokoaji ambao walikuwa wakijaribu kuuzima moto huo kwa takriban masaa mawili.Hadi sasa chanzo cha moto huo bado hakijulikani lakini Mrajis wa meli Zanzibar, Abdallah Mohammed amesema ni mapema mno kujua chanzo chake pamoja na thamani ya mali na mizigo iliyokuwemo ndani ya meli hiyo hadi hapo tathmini kamili itakapofanywa.Endelea kusoma habari hii

MAREKANI WASHUTUMIWA

10 03 2010

VIONGOZI wa kimishionari waliohamishiwa Visiwani Zanzibar wamemuomba Balozi wa Marekani Alfonso Leonhardt Nchini Tanzania kuingilia kati mzozo uliopo kati yao na viongozi wakuu wa Shirika la African For Jesus la Tanzania. Viongozi hao wamesema kumekuwepo na matatizo katika shirika hilo ambalo linaendeshwa na wakuu kutoka marekani kwa takriban mwaka sasa lakini hakuna juhudi zilizochukuliwa dhidi ya viongozi hao ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu sana.Wamesema wamesikitishwa sana na namna shirika hilo lilivyowatelekeza ambapo hivi sasa wanashindwa kuendesha shughuli za kazi zao pamoja na za kijamii ambazo wanapaswa kuzifanya kama ni viongozi wa dini ambao wamesomea na kuhitimu masomo yao.Akizungumza na waandishi wa habari, kwa niaba ya viongozi wenzake kumi, Mkurugenzi wa huduma wa shirika la African For Jesus in Tanzania, Pastor Peter Banekwa yeye na wenzake watatu wamehamishiwa visiwani Zanzibar kufanya kazi za kiroho na kuihudumia jamii ya kizanzibari amesema hivi sasa wapo katika mazingira yasioeleweka kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kimaisha.“Sisi tunataka balozi wa marekani tuonane naye kwa sababu hili shirika ni la marekani na linaendeshwa na wamarekani na wao wanatunyanyasa kwa kweli sisi wametuondosha katika vituo vyetu vya kazi wamekuja kututelekeza” amesema Banekwa.Endelea kusoma habari hii

HUDUMA YA UMEME MWEZI HUU

2 03 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wananchi wake kuwa wavumilivu wakisibiri huduma ya umeme ambayo huenda ikarudi tena Machi 9 mwaka huu iwapo kazi iliyopangwa itafanyika kama ilivyotarajiwa.Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupokelea umeme huo cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Kauli ya Meneja huyo imekuja siku chache baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuilaumu serikali na shirika la umeme kuwa imekuwa kimya juu ya suala hilo na kuwaachia watu kuvumisha uvumi mitaani amba huwa unawavunja moyo wananchi mbali mbali visiwani hapa.Mbarouk aliwaambia waandishi jana kwamba kazi hiyo utengenezaji umeme iliyobaki ni kuunganisha waya za umeme kutoka nchi kavu na baharini ambapo kazi hiyo inatarajiwa kuchukua muda mdogo kutoka sasa.Alisema kazi ya kuunganishwa kwa waya toka katika vituo vya Fumba Mjini Unguja hadi Ras Kiromoni Tanzania Bara itachukua muda wa siku tatu ambapo mafundi kutoka nchini Norway wanafanya kazi hiyo usiku na mchana ili kukamilika.Mbarouk amesema anatarajia mnamo Machi saba mwaka huu kazi hiyo itakuwa imemalizika na Machi nane kutafanyika vipimo vya majaribio kwa kuwashwa na Machi tisa ndio huduma a umeme itakuwa imepatikana kamili kwa kuwashwa moja kwa moja.Endelea kusoma habari hii

MOSHI WA JENERETA WAUWA WANNE

3 02 2010

WATU wanne wa familia mmoja wamefariki dunia baada ya kuvuta hewa inayosadikiwa kuwa na sumu iliyotokana na moshi wa jenereta katika eneo la Kibweni Bububu Nje kidogo na mji wa Zanzibar.Ajali hiyo imetokea majira ya usiku mkubwa juzi huku madirisha ya vioo ya nyumba inayomilikiwa na Ali Shamsi Salum yalikuwa yamefungwa na kusababisha hewa inayotokana na genereta lenye ukubwa wa KVA 4.1.kuingia ndani na kushindwa kutoka nje ya nyumba hiyo.Naibu mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar, Mussa Ali Mussa alithibitisha kutokea ajali hiyo na kusema kwamba katika ndnai ya nyumba hiyo kulikuwa na watu sita lakini wanne alifariki na watu wanne ndio waliofariki watatu walifariki hapo hapo na mmoja wao alifariki baada ya kukimbizwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.Akiwataja walifariki dunia katika ajali hiyo Naibu Mkuruenzi huyo alisema ni pamoja na mama mwenye nyumba Safia Shaaban Shadadi (51) kaka wa mama huyo Ahmed Shaaban Shadadi (48), mgeni kutoka Canada Anwar Saleh (26) na mfanyakazi wa nyumba hiyo Sikuzani Nassor (18).Antar ambaye ni mgeni na alikuja visiwani Zanzibar kutoka nchini Canada alikuwa na mpango wa kusafiri na kurudi zake Canada siku ya Alhamisi (leo) huku mmiliki wa nyumba hiyo Ali Shamsi Salum alisalimika katika ajali hiyo kwa kuwa siku ya tukio alikuwa amelala katika nyumba yake ya pili kwa mke wake mwengine eneo la Michenzani Unguja.Endelea kusoma habari hii

TUTAISAIDIA ZANZIBAR -WATAALAMU

22 01 2010

TAASISI ya Elimu ya Wataalamu wa Upasuaji Kichwa na Uti wa mgongo (NED), kutoka nchini Spain imeahidi kushirikiana na wataalamu wa Zanzibar kwa kuanzisha Kitengo kitakachotoa huduma hiyo hapa nchini.Akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume, Ikulu mjini Zanzibar, Rais wa Taasisi ya (NED) Profesa Jose Piquer kutoka hospitali Kuu ya Upasuaji wa Kichwa na Ute wa mgongo huko Valencia nchini Spain, alimueleza Rais Karume kuwa Taasisi yake imevutiwa kuja kufanya kazi Zanzibar.Katika maelezo yake, Dk. Piquer alimueleza Rais Karume kuwa kutokana na hatua za maendeleo zilizofikiwa katika sekta ya Afya hapa Zanzibar ipo haja ya kuanzisha utoaji wa huduma hiyo kwa wananchi.Alieleza kuwa kutokana na mafanikio hayo, Taasisi yake iko tayari kutoa ushirikiano wake kwa Madaktari wazalendo hapa nchini kwa kuanzisha Kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Mnazi Mmoja, hapa Zanzibar.Alisema kuwa miongoni mwa shughuli ambazo taasisi hiyo yenye makao makuu yake Valensia nchini Spain inazokusudia kuzifanya hapa Zanzibar ni pamoja na kutoa huduma kwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa wa kichwa na ute wa mgongo.Aidha, alieleza kuwa lengo jengine la Kitengo hicho ni kusaidi kutoa elimu kwa madaktari wazalendo pamoja na kusaidia kutoa vifaa vitakavyosaidia katika matibabu hayo.Endelea kusoma habari hii

RAIS MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI TUNGUU

18 01 2010

UONGOZI na Wadhamini kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar, umeeleza azma yake ya kuendelea kutoa mashirikiano katika kuimarisha sekta ya elimu hapa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi za masomo kwa Wazanzibari nchini Saudia Arabia. Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa Chuo Kikuu cha Zanzibar , kilichopo Tunguu Profesa Muhamad Omar Zubeir wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume, Ikulu mjini Zanzibar.Profesa Zubeir ambaye alifika Ikulu, akiwa pamoja na ujumbe wa Bodi hiyo ulioko Saudi Arabia, alieleza kuwa kumekuwa na mashirikiano na uhusiano mzuri kati ya uongozi wa chuo hicho na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Alisema kuwa kutokana na hatua na mafanikio yaliofikiwa hapa Zanzibar katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kuwa makubwa kuna haja ya kuungwa mkono ili yaweze kuimarika zaidi.Profesa Zubeir alisema kuwa uongozi huo uko tayari kutoa nafasi za masomo ya aina mbali mbali katika vyuo vikuu vya Saud Arabia zikiwemo nafasi za elimu ya juu ya masomo ya Dini ya Kiislamu hasa katika Chuo Kikuu cha Madina.Endelea kusoma habari hii

MISITIKI YAFUNGWA DUA YAOMBWA UWANJANI

16 01 2010

MISIKITI yote jana ilifungwa ili kupisha swala ya pamoja ya Ijumaa iliyoandaliwa maalumu kumuombea rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ili wakamilishe dhamira yao ya kuwaunganisha Wazanzibari.Maombi hayo, ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Maisara mjini Unguja baada ya kufungwa kwa misikiti yote, yalikuwa yawashirikishe viongozi hao wawili, lakini Rais Karume hakuweza kuhudhuria.Mufti mkuu wa Zanzibar, Sheikh Harith Bin Khelef ndiye aliyeiwakilisha serikali katika swala hiyo.Maombi yalianza kwa dua ya kuiombea Zanzibar kuelekea uchaguzi mkuu na baadaye kuwaombea viongozi hao wawili waliokutana mara kadhaa faragha kujadili mustakabali wa Zanzibar.Rais Karume na Maalim Seif wamekuwa na mikutano ambayo imeelezewa kuwa ina lengo la kuinusuru Zanzibar dhidi ya machafuko yanayotokana na chaguzi na kuzika tofauti zao za kisiasa.Swala hiyo ilifanyika kando ya nyumba ya Fatma Karume, ambaye ni mjane wa rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.Dua hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazolenga kuweka umoja wa Wazanzibari na kuwaomba viongozi hao wawili wasirudi nyuma katika kuendeleza umoja huo na mshikamano waliouanzisha.Waandaaji wa swala hiyo walisema kutohudhuria kwa Karume si tatizo katika ibada hiyo kwa kuwa lengo la dua ni kuwaombea viongozi hao wakuu wa vyama vya siasa walete umoja na mshikamano. Endelea kusoma habari hii

RAIS KARUME ASAMEHE WAFUNGWA

11 01 2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume ametoa msamaha kwa wafungwa 39 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Ni kawaida kwa kila zinapofika sherehe za Mapinduzi, Rais Karume kutoa msamaha kwa wafungwa wanaostahiki ili nao waungane na wananchi wenzao katika kusherehekea sherehe za Mapinduzi.Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar katika kifungu chake cha 59 kinampa Rais uwezo wa kutoa msamaha kwa mfungwa yeyote alioko gerezani kuwa huru au kupunguziwa adhabu.Sheria hiyo inampa Rais uwezo wa kutoa msamaha kwa mfungwa mmoja mmoja au kwa kundi.Misamaha kama hiyo imeanza kutolewa na kiongzi wa awamu ya mwanzo Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambapo ilikuwa kila zifikapo sherehe za Mapinduzi huwaachia huru wafungwa wanaostahiki ili nao waweze kusherehekea siku hiyo adhimu.Msamaha huo umewahusisha wafungwa mbalimbali kutokana na vigezo tofauti vikiwemo uzee,maradhi,waliobaksha muda mfupi kumaliza kifungo chao, wanaofuata maadili mazuri, wafungwa wasioweza kufanya kazi kutokana na uzee au ugonjwa na mengineyo.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR KUSHIRIKI MIKUTANO YA UN

11 01 2010

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Makaazi Duniani ‘UN-HABITANT’ limeiahidi Serikali ya Mapinduzi zanzibar (SMZ) kushirikiana na Mamlaka ya Maji zanzibar (ZAWA) katika kuhakikisha huduma hiyo inaimarika vyema visiwani hapa pamoja na kuhakikisha zanzibar inashiriki katika mikutano ya UN.Ahadi hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Anna Tibaijuka wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume katika mazungumzo yake Ikulu Mjini Unguja.Dkt. Tibaijuka alisema shirika hilo litahakikisha Zanzibar inapata ushiriki katika Mikutano ya UN kupitia Shirika hilo ili kuweza kutoa michango yake ukianzia Mkutano ujao wa mwezi Mei mwaka huu.Alisema shirika lake litashirikiana vyema na ZAWA na limefarajika kwa uwepo wa taasisi hiyo na utendaji wake wa kazi ambao utalirahisishia Shirika lake kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.Alisema kuwa Shirika hilo litasaidiana vyema na ZAWA katika kuwajengea uwezo wananchi wa Zanzibar katika kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini.Endelea kusoma habari hii

BARAFU KUTOKA BARA NI MARUFUKU-SMZ

7 01 2010

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepiga marufuku uletwaji na uuzaji wa barafu Visiwani Zanzibar kutoka Tanzania bara.Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya serikali iliyotolewa na Mkurugenzi wa afya wa hospitali mkuu ya Mnazi Mmoja, Dkt Juma Rajab imesema kumezuka tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kusafirisha barafu kutoka Tanzania bara jambo ambalo ni hatari kiafya.Taarifa hiyo ambayo imerushwa hewani na vyombo vya habari vya serikali ikiwemo Televisheni Zanzibar (TVZ) na Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) ikiwataka wananchi kujiepusha na matumizi ya barafu hizo ambazo hazina uhakika wa usalama kiafya.Rajab amesema barafu hizo huletwa Zanzibar kufuatia tatizo la umeme lililotokea mwezi uliopita ambazo huwekwa katika vifaa ambayo havina uhakika wa usalama ikiwemo vipolo, maguni na mifuko ambayo inadhaniwa kutokuwa salama kwa matumizi ya binaadamu.Alisema kabla ya barafu hiyo haijawekwa katika vipolo na maguni huzongereshewa aina ya chengachenga (pumba) ndani yake na baadae kufutikwa katika vyombo hivyo na kusafikirishwa kutoka Tanzania bara hadi Zanzibar kwa ajili ya matumizi.Endelea kusoma habari hii

SMZ IFANYE JUHUDI ZA UMEME-WADAU

18 12 2009

SERIKALI YA Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kuhakikisha inachukua hatua za kutosha ili kuhakikisha maeneo yote ya kibiashara na yasiokuwa ya kibiashara yanapatiwa huduma ya maji pamoja na kuwekwa kwa generator za dharura kwenye vianzio vyote vya maji.Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kutokea hitilafu ya umeme iliyotokea siku ya Alhamis tarehe 10/12/2009 ambapo serikali imeunda kamati ili kutathmini athari zitakazotokea kwa wafanyabishara na hasa wale wa Sekta ya Utalii katika kipindi hichi cha msimu wa utalii.Kamati hiyo imewajumuisha Afisi ya Katibu Mkuu Kiongozi na wajumbe kutoka sekta binafsi kama Jumuiya ya wafanyabishara Zanzibar (ZNCCIA), Jumuiya ya Wawekezaji wa utalii (ZATI), na Jumuiya ya watembezaji watalii (ZATO). Na kwa upande wa serikali imejumuisha Kamisheni ya Utalii na Mamlaka ya Uwekezaji (ZIPA)Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habarí na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ali Khalil Mirza imesema kamati hiyo imewaomba wawekezaji na wananchi kw aujumla kuwa na subra katika kipindi hiki ambacho umeme umekosekana nchini.Endelea kusoma habari hii

ZANZIBAR KUWA GIZANI WIKI TATU

14 12 2009

WAKAZI wa Unguja watakosa umeme kwa tatu kutokana na kulipuka na kuungua kwa kifaa katika kituo cha kupokelea umeme wa gridi ya taifa kilicho eneo la Fumba.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Shangani wilayani Mjini Magharibi jana, Waziri wa Maji, Ujenzi, Ardhi na Nishati, Mansoor Yusuph Himid alisema kuharibika kwa mitambo hiyo kumesababishwa na kuzidiwa nguvu kutokana na kuongezaka kwa matumizi ya nishati hiyo.Mansoor alisema Serikali ya Mapinduzi (SMZ) imechukua hatua madhubuti kurekebisha tatizo hilo na kuahidi kulimaliza ndani ya wiki tatu.“Serikali inachukua juhudi kurekebisha tatizo hilo na tunawaomba wananchi wavumilie wakati mafundi wa shirika la umeme Zanzibar na wataalam kutoka Afrika Kusini wakijitahidi kurekebisha,” alisema Waziri Mansoor.Endelea kusoma habari hii

MIKATABA YA HAKI ZA BINADAMU NI TZ

5 12 2009

TUME ya haki za Binadamu imesema suala la mikataba ya kimaifa kuhusu haki za binadamu si suala la Zanzibar ni jukumu la Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.Kauli ya tume hiyo imetolewa na Kamishna wa tume hiyo Tanzania Bernadeta Gambishi, katika Semina ya siku mbili iliwashirikisha viongozi wa Serikali na viongozi wa vyama vya siasa ambayo ilikuwa ikijadili mpango mzima wa haki za binadamu nchini iliyofanyika ukumbi wa Hoteli ya Mazson’s Mjini Unguja.Gambishi alisema kuwa hali hiyo inatokana na kuwa Wizara inayoshihulikia masula ya ushirikiano wa kimataifa ipo katika Serikali ya Tanzania tu na kuwahusu wa Tanzani wote wakiwamo wa Zanzibar.Alisema kuwa wakati mikataba hiyo inapotakiwa kutiwa saini au kuanzishwa basi wahusika wake ni kutoka wizara hiyo, ila Zanzibar nayo hupewa nafasi ya kuchangia kabla ya kufikishwa sehemu husika ya Kimataifa kwa ajili ya hatu zaidi.Hata hivyo nao baadhi ya wajumbe wa warsha hiyo wakichangia katika ukumbi huo walisema kuwa wana wasi wasi mkubwa kwa jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar , kutoshirikishwa katika kamati ya utungaji wa rasimu ya haki za walemavu Tanzania kutokana na ishara zake tayari zimeshaanza kuonekana mapema.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona Zanzibar, Muhammed Kassim Abdallah ambaye alisema kuwa hivi karibuni Tanzani bara walianza kazi ya utungaji wa rasimu ya haki za walemavu ili kuziwezesha jumuiya hizo kuweza kujipatia haki zao pamoja wao wenyewe katika maisha yao.Endelea kusoma habari hii

MUJIANDAE KUWEKEZA-RAIS KARUME

5 12 2009

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, ametowa wito kwa wananchi wa ndani na nje ya Zanzibar kuanza kujiandaa kuekeza vitega uchumi vyao Kisiwani Pemba kwani ndoto ya kupata umeme wa uhakika kisiwani humo imeanza kutimia. Rais Karume aliyasema hayo jana baada ya kuzindua kazi za shughuli za uwekaji waya utaopeleka umeme kutoka Tanga na kuelekea kisiwani Pemba,uzinduzi ambao ulifanyika Mkoani Tanga.Rais Karume alisema ndoto ambayo serikali ya Zanzibar ilioyokuwa ikiiota ya kuwa na umeme wa uhakika kisiwani Pemba imetimia na ni vyema kwa wananchi wa Zanzibar hasa waliowekeza nje ya Zanzibar kurudi kuekeza kisiwani Pemba.Alisema kuwepo kwa umeme wa uhakika baada ya mradi huo kukamilika ni moja ya sehemu kubwa ya kuimarisha maendeleo ya Zanzibar ambapo itawawezesha wananchi kukuza fursa za kiuchumi hivi sasa kisiwa humo.Rais Karume alisema kukuwa kwa fursa za kiuchumi kisiwani Pemba, ni moja ya juhudi kubwa ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeichukua kwa lengo la kulipatia ufumbuzi tatizo la upatikanaji umeme kisiwani Pemba. Akitoa maelezo kwa waandishi wa habari katika Ikulu ndogo ya Tanga mara baada ya kurudi katika uzinduzi huo na kuangalia waya huo uliokuwemo katika meli ya NEXANS SKAGERRAK kutoka nchini Norway alifahamisha kuwa hatua hiyo itakuwa yenye kwenda sambamba na ukuaji wa Uchumi wa Zanzibar kutokana na maridhiano yaliopo ambayo yataimarisha amani na utulivu nchini.Endelea kusoma habari hii

ZNZ YAKHOFIA USALAMA BAHARI YA SOMALI

3 12 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imeshindwa kutoa taarifa za ujio wa meli ya Mv. Skagerak iliyobeba waya wa mradi mkubwa wa umeme kutoka Tanga hadi Pemba kutokana na sababu za kiusala katika bahari ya Hindi.Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, aliwaambia waandishi wa habari kwamba kutokana na hali ya kiusalama kwenye ukanda wa Somalia serikali iliamua kukaa kimya kuogopa kutekwa nyara na maharamia wa nchi hiyo.Hata hivyo alsiema meli iliyobeba waya hizo ambazo zitatumika katika mradi mzima wa kupeleka umeme kisiwani Pemba tayari imeshawasili juzi visiwani Zanzibar.Alisema serikali kwa kushirikiana na Kampuni inayosimamia mradi huo ya NEXANS imeamua kukodi meli mbili za kiusalama ambazo ziliweza kufanikisha kuvusha waya huo hadi nchini Kenya na baadae kukabidiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.Waziri huyo alisema hivi sasa meli iliyobeba waya huo ipo katika Bandari ya Mkoani Tanga ikiwa chini ya ulizi wa Manuari mbili za kiusalama za Kikosi cha KMKM.Alieleza kwamba kazi za kulaza waya huo baharini baada ya uzinduzi wa mradi huo zinatarajiwa kuanza Disemba 9, 2009 ambapo matarajio ya awali itakamilika Disemba 17 mwaka huu.Endelea kusoma habari hii

NJOONI MUWEKEZE ZNZ-KARUME

30 11 2009

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amezitaka taasisi za fedha nchini kuwekeza na kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.Rais Karume alisema jana eneo la darajani wakati akifunguwa tawi la Benki ya NMB ambalo ni la kwanza kufunguliwa katika visiwa vya Zanzibar.Alisema wafanyabiashara na wakulima iwapo watasaidiwa kupewa mikopo wataweza kuendesha shunguli zao bila ya kutegemea serikali na azma ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini itakuwa imetimia.Alisema hadi sasa taasisi za kifedha ikiwemo mabenki nchini hayajawekeza zaidi katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwaendeleza wakulima na wajasiriamali wadogo wadogo nchini.Karume alisema kilimo bado ni tegemeo na uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar hivyo taasisi za fedha zinayo nafasi kubwa ya kupanuwa biashara zao kama watawekeza katika sekta ya kilimo.”Sekta ya kilimo bado ni uti wa mgongo wa taifa kwa asilimia 70% ya wakulima wanategemea kilimo cha uzalishaji wa mazao mbali mbali…..taasisi za benki zinawajibika kuwekeza katika kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula nchini”alisema Karume.Endelea kusoma habari hii

WAISLAMU MTAMBUENI MUFTI-SORAGA

28 11 2009

KATIBU wa Afisi ya Mufti Shekh Fadhili Suleiman Soraga amewataka viongozi wa dini ya kiislam nchini kumtambua Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Harith Bin Khelef kuwa ni kiongozi wa waislam kama Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alivyomtambua Rais Amani Karume kuwa ni rais halali wa Zanzibar.Alisema ni vyema viongozi wa dini wakaiga mfano na mwenendo wa wanasiasa hao ambao kwa muda mrefu walikuwa hawafahamiani vizuri lakini sasa wote wapo kitu kimoja katika kuhakikisha amani na utulivu vinapatikana kwa jamii nzima ya kizanzibari.Shekh Soraga aliyasema hayo jana wakati akitoa nasaha kwa waislam baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Eid El-Hajj, huko katika viwanja vya Msikiti wa Mwembe Shauri uliopo Mjini Unguja. Alisema wakati umefika kwa masheikh, maimamu na viongozi wa dini kukaa pamoja na kuacha tofauti zao zisizo na maana katika dini kwa kumtambua Mufti Mkuu ambaye amechaguliwa kwa mujibu wa misingi ya kisheria hapa nchini kwa kuwaongoza waislam.Alifahamisha kuwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa kiislam vya kwenda kinyume na maamrisho ya kiongozi wao wa dini ambaye ni mufti ni wazi kuwa vinakwenda kinyume na mafundisho ya Uislam.Endelea kusoma habari hii

ZNZ WATAKA MGAO WA SAMAKI

25 11 2009

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haina taarifa zozote kuhusiana na kupata mgao wa samaki waliovuliwa na meli ya Kigeni katika bahari Kuu ya Tanzania (Samaki wa Magufuli) mwaka huu.Samaki hao walitarajiwa kugaiwa hivi karibuni baada ya Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, John Pombe Magufuli kutangaza katika vyombo vya habari Mjini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema kuwa Serikali haijui lolote kuhusiana na kufaidika na mgao wa samaki unaogaiwa huko Tanzania Bara. Kwa mujibu wa Waziri Magufuli tani 296.32 za samaki aina ya jodari zilizokamatwa zikivuliwa na wavuvi kutoka nje katika bahari ya Tanzania kwenye Ukanda wa Uchumi wa bahari Kuu nchini watagaiwa katika taasisi 115, zilizopitishiwa maombi yao kupata kitoweo hicho.Zanzibar imekuwa na wasi wasi juu ya kupata mgao huo wa kupata samaki baada ya serikali kukiri kuwa hakuna tarifa yoyote iliyopokelewa kutoka serikali ya Muungano inayoeleza kuhusu mgao wa samaki hao na namna Zanzibar itakavyofaidika nao.Waziri Hamza alisema kwamba taarifa walizozipata kuhusu samaki hao ni kupitia matangazo ya magazeti yanayotaka taasisi zinazohitaji samaki hao kuomba, lakini serikali haina taarifa rasmi kutoka serikali ya Muungano inayoelezea hilo wala hakuna barua yoyote iliyopokea.Endelea kusoma habari hii

WAZEE NI HAZINA KWA TAIFA-KARUME

24 11 2009

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amesema kuwa wazee ni hazina ya taifa hivyo ipo haja ya kuwapenda na kuwajengea mazingira bora ya kuishi.Kutokana na hali hiyo, Rais Karume amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuwatunza na kuwaenzi wazee kwani wao pia ni sehemu ya jamii.Rais Karume aliyasema hayo leo mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa juu ya Huduma kwa Wazee, uzinduzi uliofanyika katika hoteli ya Ocean View mjini Zanzibar, ambapo Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha na Mama Shadya Karume pamoja na viongozi wengine walihudhuria.Rais Karume alisema kuwa tokea awamu ya kwanza ya urais wa marehemu mzee Abeid Karume katika mambo muhimu aliyoyafanya ni kuwajengea wazee mazingira bora kwa kuwajengea nyumba za kuishi.Aidha, Rais Karume alisema kuwa Serikali ya awamu ya tatu ilitangaza matibabu bure, elimu bure, huduma za afya bure pamoja na kutoa heka tatu tatu yote hayo ni kwa lengo la kuwasaidia wananchi wapate huduma bora.Rais Karume alisema kuwa katika hatua moja wapo ya kuwaenzi a kuwatunza wazee ni kuwahakikishia marekebisho yao ya pencheni kwa kuzidisha kiwango ikiwa ni pamoja na kupewa fedha hizokwa kila wiki badala ya mwisho wa mwezi.Endelea kusoma habari hii

DKT BILAL AHIMIZA ELIMU ZNZ

21 11 2009

WAZIRI Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Muhammed Gharib Bilali amewataka Walimu wa Shule mbali mbali kuongeza jitihada zaidi katika ufunduishaji wao kwa wanafunzi ili kuweza kurejesha heshima ya Zanzibar ya kutambulika kielimu katika mwambao wa Bara la Afrika na duniani kote.Alisema ipo haja kubwa kwa walimu kutumia muda wao mwingi katika kufikiri njia muafaka za kuirejeshea Zanzibar sifa yake iliyopata kipindi cha miaka ya nyuma katika fani ya utoaji wa elimu kwa wageni na wenyeji.Dkt Bilali aliyasema hayo jana katika sherehe maalum zilizoandaliwa na Jumuiya ya Shule za Madrassa visiwani Zanzibar katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) Mjini Unguja.Alisema wakati umefika kwa walimu kujituma zaidi katika ufundishaji wao kwa kutafuta njia mbadala ambazo zitaweza kusaidia katika kwenda sambamba na mabadiliko ya ukuaji wa elimu hapa nchini.Alifafahamisha kuwa Zanzibar ina historia kubwa katika fani ya elimu na kuwa ni miongoni mwa nchi moja wapo zinazotoa elimu za kiwango kizuri na cha kutambulika duniani kote.Kiongozi huyo alisema kuwa ni vyema kwa walimu hao ili kuweza kufanikiwa kwa haraka basi wakasoma zaidi historia za walimu waliopita miaka ya nyuma ambao walikuwa ni vinara katika fani ya utoaji wa elimu hapa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

RAZA AMKANA MKWEWE MAHAKAMANI

18 11 2009

KESI aliyofungua Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar, Mohammed Raza Hassanali (48) dhidi ya Abdul Hussein Rashid imechukua sura mpya baada ya Raza kumkana mtuhumiwa kuwa sio baba mkwe wake mbele ya Mahakama ya mwanzo ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.Akiwasilisha ushahidi wake mbele ya Hakimu Janet Nora Sekihola, Raza alisema kwamba mshitakiwa huyo sio baba mkwe wake na hana uhusiano wowote nae kama inavyodaiwa katika kesi hiyo aliyoifungua dhidi ya Abdul Hussein.Mfanyabishara huyo alikuwa akijibu hoja za upande wa utetezi baada ya kujitokeza suala hilo mahakamani hapo ambapo Raza alisema kwamba mshitakiwa sio baba mkwe wake na kuitaka mahakama kuamini ushahidi wake huo alioutoa.Abdul Hussein Rashid amefunguliwa kesi ya uzembe na ukorofi kwa tuhuma za kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Raza kwa kumhusisha na tuhuma za wizi na mauaji dhidi ya ndugu zake.Hata hivyo Raza alisema mshitakiwa hana ushusiano nae isipokuwa ni mwanachama wake katika msikiti wa madhehebu ya Kishia uliopo Kiponda kati kati ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

RAZA AONYWA NA MAHAKAMA

6 11 2009

MFANYABIASHARA Maarufu Zanzibar Mohammed Raza, amepewa onyo rkali na Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi kutokana na kitendo chake cha kuidharau mahakama hiyo.Mahakama hiyo iliyo chini ya Hakimu Janet Nora Sekihola imelazimika kumpa onyo hilo Mfanyabiashara huyo baada ya kuangua kicheko mahakamani hapo wakati mahakama hiyo ikiendelea na shughuli zake za uendeshaji wa kesi.Katika onyo hilo, mahakama hiyo imemfahamisha kuwa, kitendo hicho ni cha dharau mbele ya mahahakama, na kumtanabahisha kuwa endapo ataendelea tena mahakama hiyo italazimika kumchukulia hatua za kisheria.Raza aliangua kicheko hicho mahakamani hapo, wakati Wakili wa utetezi katika kesi ya uzembe na ukorofi inayomkabili mtuhumiwa Abdul Hussein Rashid ambaye ni Baba Mkwe wa Mohammed Raza, kuiambia mahakama hiyo kuwa mteja wake huyo hakuweza kufika mahakamani hapo, kutokana na kukabiliwa na maradhi ya baridi (stroke).Wakili huyo wa utetezi Rajab Abdalla Rajab wa Kampuni ya AJM Solicitor & Advocate Chamber ya Mjini Zanzibar alidai mbele ya mahakama kwamba mteja wake huyo pamoja na kuruhusiwa kutoka hospitali alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu lakini bado maradhi hayo yanasumbua.Kufuatia kauli hiyo iliyotolewa na Rajab Mohammed Raza ambae ni mlalamikaji katika kesi hiyo ilimfanya aangue kicheko mahakamani hapo kwa sauti kubwa na kulazimika kupewa onyo kwa mujibu wa sheria za mahakama.Endelea kusoma habari hii

MSISAINI WARAKA-SMZ

2 11 2009

haSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewataka walimu wote nchini kutoweka saini katika waraka wa madai ya walimu wa Zanzibar ya posho la silimia 25 ulitolewa na Chama Cha Walimu (ZATU) hivi karibuni.Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwanaidi Saleh Abdallah aliwaambia waandishi wa habari jana katika mkutano wake uliofanyika Mazizini Mkoa wa Mjini Unguja kufuatia mvutano uliojiotokeza kati ya walimu na wizara.Naibu huyo alisema waraka uliotolewa na chama cha walimu una lengo la kuwapotosha walimu na wananchi kwa ujumla kuonekana kuwa serikali yao haishughulikii maombi ya walimu wake.“Chama cha walimu inaonekana kuingilia suala ambalo hawalielewi mwanzo wake kwani hawakuhusika katika kutoa maombi ya kurejeshewa kwa asilimia 25 na wala hawakuhusika katika hatua ambazo serikali inazichukua hivi sasa. Nia yao ni kutaka kujipatia umaarufu kwa jambo ambalo serikali imeshalipitisha maamuzi na liko katika maandalizi ya kuchukuliwa hatua” Alisema Katibu Mkuu huyo.Endelea kusoma habari hii

MAIMAMU WATAHADHARISHA

1 11 2009

JUMUIYA ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) imeitaka Tume ya Uchaguzi faridZanzibar (ZEC) kusitisha zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa lengo la kutoa nafasi ya kushughulikia matatizo ambayo yamekuwa yakisababisha vurugu na watu wengine kujeruhiwa kwa kupigwa mapanga majumbani mwao.Hayo yameelezwa jana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Muhiddin Zubeir Muhiddin alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jumuiya hiyo Mkunazini Mjini Zanzibar.Alisema kwamba hivi sasa kumekuwa na vitendo vimekuwa vikijitokeza vya uvunjifu wa amani na umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar kutokana na baadhi ya wananchi kuvamiwa majumbani mwao na kupigwa mapanga nyakati za usiku na kutoa mfano tukio la watu kupigwa katika kisiwa cha Tumbatu Unguja na lile la Ziwani Kisiwani Pemba.Kiongozi huyo alisema kwa msingi huo Jumuiya ya Maimamu inawaomba wananchi wajizuwie kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura hadi hapo Jumuiya itakapojiridhisha kuwepo kwa usalama wa kutosha wa wananchi na mali zao.Endelea kusoma habari hii

MAMILIONI YAIBWA WIZARA YA ELIMU

30 10 2009

wizara_znzWATU wasiojulikana wanaoaminika kwamba ni wezi wamevunja kasha la fedha la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na kufanikiwa kuiba kiasi kikubwa cha fedha Wizi huo unaamika ulitokea usiku wa manane hivi karibuni baada ya watu kuvunja madirisha ya ofisi ya kuhifadhia fedha na kuingia ndani walikofanikiwa kuiba jumla ya milioni 23 taslim.Kamishna wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Mussa Ali, alithibitisha kutokea wizi huo na alieleza kuwa watu kadhaa ndani ya Wizara hiyo wameanza kuhojiwa kuhusiana na wizi huo ambao umetokea hivi karibuni.Hata hivyo, alisema licha ya kuwepo mahojiano hayo hadi sasa hakuna mtu aliyeshikwa kwa tuhuma za wizi huo lakini upelelezi huo unaendelea.Alisema Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kufahamu watu walihusika wa tukio hilo ili kujua wizi huo na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watu waliohusika na tukio hilo.Watu walioitwa na jeshi la polisi na kuhojiwa ni pamoja na Mlinzi wa Wizara hiyo aliyekuwa zamu siku ya tukio, Washika fedha, Mhasibu na watendaji wengine ambao hakuwatajwa majina yao kutokana na sababu za kiusalama.Endelea kusoma habari hii

REKODI YA KARUME HAIJAVUJWA-NAHODHA

30 10 2009

WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, amesemanahodha1 rekodi ya miaka minane ya uongozi wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume katika utendaji kazi hakuna kiongozi yoyote aliyeweza kuivunja hadi sasa.Nahodha aliyasema hayo juzi wakati akifunga Kongamano la wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar lililokuwa likizungumzia kuwaenzi waasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar na ambalo lilifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, kwa kuwashirikisha Wasomi wa Vyuo Vya Zanzibar.Vyuo vilivyoshiriki Kongamano hilo ni Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, (ZJMMC), SUZA, Chuo Cha Ualimu Benjamin Mkapa na Nkurumah, Chuo Cha Kiislamu Zanzibar na Pemba na Chuo cha Afya. Vyengine ni Chuo Cha Utalii, Chuo cha Utumishi Zanzibar, Chuo cha Ufundi, Mbweni, Mikunguni, Chuo Cha Waandishi wa Habari cha CCM na Chuo cha Fedha cha Chwaka Alisema, wasomi wa vyuo vya elimu ya juu wanapaswa kuona elimu wanayoipata baada ya kumaliza masomo yao wanaifanyia kazi vilivyo ili waweze kuwa na rekodi ilioachwa na Muasisi wa Taifa la Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume, kwani hakuna kiongozi yoyote katika kipindi cha miaka minane aliyeifikia.Endelea kusoma habari hii

WANAMSUMBUJI WAPIGA KURA ZNZ

30 10 2009

KUPIGAKURAIKIWA zimebakia siku chache kwa wananchi wa Msumbiji kushiriki uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, jumla ya Wanamsumbiji 900 wa maeneo mbali mbali ya Zanzibar, wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo.Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu, utakaohusisha kumchagua Rais wa nchi hiyo pamoja na wabunge ambapo utashirikisha mikoa 11 na Wilaya 121 za nchi hiyo.Wagombea ambao hadi sasa wamejitokeza kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi huo, ni watatu akiwemo Rais wa sasa wa nchi hiyo, Armando Emilio Guebuza wa chama Tawala cha FRELIMO, David Simango wa chama cha MDM na Alfonso Dhlakama wa Chama cha RENAMO.Zanzibar ina wananchi wa Msumbiji katika maeneo kadhaa ya vijiji vya Zanzibar, katika Wilaya ya Kati Unguja kikiwemo kijiji cha Ndagaa, Dunga, Kiboje na Hanyegwa Mchana.Akizungumza na Zanzibar Leo, Mjini Zanzibar, Balozi mdogo wa Msumbiji, Bernado Lindimba, amesema jumla ya Wanamsumbiji 900 waishio Zanzibar, tayari wamethibitishwa kuwa na haki ya kupiga kura katika kinyang’anyiro hicho.Endelea kusoma habari hii

MKONO WA ALBINO WAOKOTWA ZNZ

JESHI la Polisi Visiwani Zanzibar limeokota mkono wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) ufukweni mwa bahari ya Hindi katika eneo la Kizingo, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema jeshi lake limeokota mkono huo mmoja wa albimo majira saa 11.00 juzi jioni.Amesema jeshi la polisi lilikuwa katika kazi za kawaida walipata taarifa kutoka kwa raia wema ambapo ni wavuvi wa eneo hilo la Kizingi waliokuwa katika shughuli zao za kazi waliona kitu kisicho cha kawaida ndipo walipoiarifu polisi.Alisema Polisi wamelazimika kuupeleka mkono huo katika hospitali Kuu ya Mnazimmoja, ambako madaktari wanaufanyia uchunguzi zaidi kabla ya kutoa taarifa kamili.Kamanda Bakari alisema kwamba hadi sasa haijafahamika kama kuna mtu amefanyiwa hujuma Zanzibar au mkono huo umetolewa nje ya Zanzibar kwa kuvutwa na maji kwa kuwa umeonekana katika ufukwe wa bahari.Kamanda huyo alisema hadi jana hakukuwa na taarifa yoyote ya kutoweka mtu mwenye ulemavu wa ngozi, baada ya Poilisi kufanya uchunguzi katika vituo mbali mbali.Hata hivyo, alisema kuna uwezekano mkono huo ulifika katika eneo hilo kwa shughuli za uganga kutokana na mazingira uliyokutwa, ambapo ulikuwa umezunguushwa kitambaa cheusi.Endelea kusoma habari hii.

VIONGOZI WAPUNGUZIWE MZIGO

NAIMAWANAHARAKATI wa kutetea haki za binaadamu wametaka viongozi wa wakuu wa nchi kupunguziwa mzogo na badala yake kuachiwa mahakama kutoa maamuzi ya mwisho katika utekelezaji wa adhabu ya kifo nchini.Ushauri huo umetolewa na washiriki wa kongamano la wazi lililofanyika jana katika ukumbi wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar, Madungu Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba katika maadhimisho ya siku ya kufutwa kwa adhabu ya kifo duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka.Washiriki hao wamesema kwa kuwa sheria za adabu ya kifo ipo na katika katiba lakini utekelezjai wake unakuwa mgumu na kutokana na viongozi ambayo ni marais ndio wanaopaswa kuweka saini ili hukumu hiyo itekelezwe basi ni vyema mzogo huo ukaondoshwa kwa marais na wakaachiwa mahakama.“Marais wetu sijui wana imani sana au hawapendi kuuwa na ndio maana hawataki kuweka saini katika hii adhabu ya kifo hata kama mtu amehukumiwa kuawa kwa maana hiyo basi tunashauri hii adhabu ya kifo isainiwe mahakamani yaani mahakama imalize kila kitu ili viongozi wetu tuwapunguzie mzigo huu” alishauri Mwalimu Saleh Nassor.Endelea kusoma habari hii

WANANCHI WAPEWE ELIMU

WASAIDIZI wa sheria kisiwani Pemba wamesema ipo haja ya kutolewa elimu zaidi kwa wananchi kuhusiana na masuala mbali mbali hasa 1yanayohusu uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mwakani 2010.Wasaidizi hao wameyasema hayo katika kikao chao cha pamoja katika ukumbi wa kituo cha huduma za sheria kiliopo kisiwani pemba ambacho hufanyika kwa lengo lakujadili masuala ya uandikishaji na upigaji kura kwa sasa ambapo wamesema elimu ya wananchi ni ndogo na inapaswa kutolewa kwa kuwa ni muhimu kujua sheria za uchaguzi kabla ya kuingia katika uchaguzi wenyewe.Wakizungumza katika kikao chao cha kutathimini hali ya elimu kwa wananchi wamesema bado elimu inahitajika zaidi kwani wapo watu ambao uelewa wao hauridhishi na wanahitaji kupata elimu kwani suala la uandikishaji wa daftari la kudumu la wpaiga kura linaloendelea hivi sasa baadhi yao hawalijui.Wamesema kumekuwepo na utata mkubwa kati ya katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi Zanzibar na uanzishwaji wa vitambulisho na ndio maana kumekuwepo na matatizo ambayo wananchi wanashindwa kufahamu na matokeo yake ni kuwanchanganya akili hasa wale waliokuwa hawana elimu.“Hizi sheria kwa hakika zina utata kwanza inapingana na katiba kwa hivyo wananchi wengi hawa wale wlaiokuwa hawana elimu ndio wanakanganywa vichwa vyao kwa hivyo mimi nadhani suala hili tulijadilia kwa kina ili wananchi wanapoelezwa wafahamishwe vizuri sana na waweze kufhamau maana sheria yenyewe binafsi ina utata” walisema wasaidizi hao wa sheria kisiwani Pemba.Endelea kusoma habari hii.

MAFUTA YAADIMIKA PEMBA

mafutaKISIWA Cha Pemba kinakabiliwa na ukosefu wa mafuta ya magari na ukosefu wa umeme kwa wiki ya pili hivi sasa na kusababisha shughuli nyingi za serikali na za kibiashara kusimama.Uhaba huo wa mafuta ya disel na petroli unatokana na kuharibika kwa Meli ya Mv. Mkombozi ambayo ndiyo inayotumika kusafirisha mafuta hayo kutoka Dar es Salaam hadi kisiwani Pemba ambapo kwa sasa imeelezwa meli Mv. Sahara ndio itakayochuka nafasi ya kusafirisha mafuta hayo lakini bado haijafahamika yataletwa lini kisiwani hapa.Wafanyabishara wa wa vituo vya mafuta hayo hulazimika kuuza kwa magendo katika miji cha Chake Chake na Wete kufuatia uhaba huo ambapo lita moja ya petroli hivi sasa huuzwa kwa shilingi 2500 badala ya bei yake ya zamani shilingi 1440.Mafuta ya disel huuzwa kwa shillingi 1850 kwa lita badala ya bei zake ya zamani shilingi 1320 ambapo patikanaji wake ni was shida kuwa na baadhi ya vijana huwa wamepata biashara ya kwenda vituoni nyakati za usiku mkubwa na kuchukua mageloni ya mafuta na baadae kwenda kuyauza vichochoroni kwa bei kubwa zaidi.Mwananchi imeshuhudia vijana hao saa 5:20 usiku wakiwa na mageloni ya manjano mikononi katika kituo cha mji wa Chake Chake wakisema wananunua kwa bei ya juu na wao watauza kwa bei ya juu kwa kuwa mafuta yameadimika na haijulikani lini tatizo hilo litakwisha kwani hali kama hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara katika kisiwa hicho.Endelea kusoma habari hii.

MTOTO WA MIAKA 14 AUWA MWENZAKE

MTOTO wa umri wa miaka 14 Samir Faraj Kheir anashilikiwa na Jeshi la letter 173Polisi kutokana na kumuuwa mwenzake Khalfan Zaidi Abadi (14) kwa kumlenga jiwe la kichogo na kumsababishia kifo hapo hapo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Hemed (Bugi) amelithibitishia Mwananchi Jumapili kwamba ni kweli mtoto huyo amefariki jana majira ya saa 8 mchana baada ya kupigwa jiwe na mwenzake baada ya kutokea mabishano ya mchezo wa mpira wa miguu.“Hawa watoto walikuwa wakicheza mpira lakini nadhani timu moja ilifungwa kwa hiyo timu ya pili ikaona imechezewa faulu ndio wakaaza kurushiana mawe na huyu mmoja akampiga ndipo lilipompata na kufariki hapo hapo kwa sababu alipigwa eneo la nyuma cha kichwa yaani kichogoni na alipotez adamu nyingi” alisema Kamanda Bugi.Amesema wakati watoto hao ambao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi wakicheza mpira kuna timu moja ilifunga time nyenzake na ndipo mtoto timu moja ilianza kubishana na timu nyengine na kuanza kusababisha ugomvi wa kurushiana mawe ambapo Samir alirusha jiwe na kumrushia Khalfan ambapo lilimpata jiwe la kichogo na sehemu iliyotoboka ilikuwa ni ndogo lakini ametoka damu nyingi kichwani.Endele kusoma habari hii.

AFYA YA DK SALMIN YAIMARIKA

DSC02660RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya macho na kupelekwa nchini China hivi sasa hali yake inazidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu.Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umegundua hivi sasa Dk. Salmin ameanza kupata nafuu baada ya kuumwa kwa miaka kadhaa huku jicho lake moja likionekana naona sawa sawa na jengine ndilo limekuwa likimsumbua ambapo hivi karibuni anatarajiwa kurejea tena katika matibabu ya jicho la pili.Dk. Salmin maarufu kama Komandoo ameanza kupata nafuu baada ya kupelekwa katika hospitali moja ya nchini Oman mwaka huu ambapo aliporejea alipata nafuu na hivi sasa jicho lake moja limeanza kuona vyema isipokuwa anakabiliwa na tatizo la jicho la pili ambalo anatarajiwa kutibiwa na hilo.Awali Dk. Salmin alipelekwa Nchini China na kurejea Juni 2006 na toke hapo hali yake ikawa ya mashaka licha ya kupatiwa matibabu ambapo alipatiwa miwani maalumu ya kuonea, alitakiwa kutenga muda wa mapumziko, kutozungumza sana pamoja na kutakiwa kukaa sehemu yenye utulivu ili kuepuka zogo ambalo lingeweza kumsababishia matatizo katika mishipa yake ya kichwa kw amuda wa miezi sita kutumia utaratibu huo.Endelea kusoma habari hii.

ZNZ WAONGOZA KATIKA TAHFIDH QUR-AN

MWANAFUNZI Suleiman Seif Said (18) kutoka Zanzibar amefanikiwa IMG_0214kushika nafasi za kwanza katika mashindano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu katika safu ya juzuu 30, kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yaliofanyika Bwawani Visiwani Zanzibar.Suleiman alijipati nafasi hiyo baada ya kujipatia alama 100, huku akiwaacha wenzake tisa wakimtangulia nyuma, ambapo kutokana na ushindi wake huo alikabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja, simu ya mkononi pamoja na baiskeli ambayo haipungui thamani ya shilingi 80,000.Naye Mohammed Moge Aden (20), kutoka nchini Kenya aliweza kuinasa nafasi ya pili kwa kujipatia alama 94.5, ambapo na kuzawadiwa shilingi 750,000, simu ya mkononi pamoja na Baiskeli.Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano hayo ya juzuu 30, iliweza kurejea tena kwa Mwanafunzi Ali Khamis Makame (19), kutoka Zanzibar kwa kujipatia alama 94, na kujipatia zawadi ya shilingi 600,000, simu ya mkononi pamoja na baiskeli kama alivyoapata wenzake wa mwanzo.Lakini pia wanafunzi wa ngazi tofauti waliopata kushikilia nafasi ya nne hadi kumi waliweza kuzawadiwa shilingi 250,000 kila mmoja bila ya kuangaliwa alama zao ila kilichongaliwa zaidi ni ushiriki wao mzuri katika mashindano hayo.Endelea kusoma habari hii

NAHODHA MGENI RASMI ITIKAFU ZNZ

nahodha1WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Itiqaf ya Kimataifa itakayofanyika Masjid Fiysabililahi Amani kwa Saidi wa Shoto kuanzia mwezi 20 Ramadhan mwaka huu. Itiqafu hiyo ya Kimataifa hufanyika kila mwaka msikitini hapo na kuhudhuriwa na waislam kutoka sehemu mbali mbali duniani ikiwa na lengo la kuwahamasisha waislamu katika kumuelekea Mola wao hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Mwenyekiti wa Itiqafu hiyo,Sheikh Ame Wadi Ame, aliyasema hayo wakati akizungumza na Mwandishi wa habari hizi katika Madrasatu Fiysabililahi Amani iliyopo nje kidogo na mji wa Zanzibar.“Itikafu safari hii Mgeni Rasmi tumemualika Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Shamsi Nahodha katika ufunguzi, lakini kwa ufungaji bado hatujamjua nani kwa hiyo siwezi kukupa jina kamili la mgeni rasmi katika ufungaji lakini tutwajulisha inshaallah”alifahamisha.Endelea kusoma habari hii

MALARIA INAWEZA KWISHA ZNZ-WHO

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Margaret Chan ameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumaliza kabisa maradhi ya Malaria hapa Zanzibar kufuatia mafanikio makubwa yaliyokwisha dk. shanpatikana.Dk. Chan aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume.Katika maelezo yake, Mkurugenzi Chan alisema kuwa mafanikio yaliopatikana Zanzibar ni makubwa na kuahidi Shirika lake kuendelea kuiunga mkono katika kupambana na maradhi hayo na mengineyo.“Naiunga mkono Programu ya ‘Kataa Malaria’ lakini kilichopo hivi sasa ni ‘Maliza Malaria’, kwani mafanikio makubwa yamepatikana Zanzibar na kwa mujibu wa mikakati iliyopo kuna uwezekano wa kumaliza kabisa Malaria”,alisema Dk. Chan.Aidha, Dk. Chan alieleza kuwa WHO pamoja na Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yataendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kupambana na maradhi ya Malaria, Kipindupindu na maradhi mengineyo.Alieleza kuwa changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni kuimarisha zaidi upigaji vita Maradhi hayo kwa kuhakikisha yanamalizika kabisa.Katika mazungumzo yake hayo, Dk. Chan alieleza kuwa katika nchi za Afrika na zinazoendelea imeonekana Zanzibar kupiga hatua nzuri na kuweka historia katika kupiga vita Malaria.Endelea kusoma habari hii.

KIDONGO CHEKUNDU IPO HALI MBAYA

HOSPITALI ya wagonjwa wa akili Kidongo Chekundu Zanzibar inakabiliwa na upungufu wa wataalamu muhimu katika fani za tiba akiwemo mwanasaikolojia.Akizungumza na waandishi wa habari hospitali hapo katika maandalizi wa kuchangia fedha kwa ajili ya shughuli mbali mbali za hospitali, Daktari Dhamana Abdi Mohammed alisema kwamba kwa ujumla hali sio nzuri ya wataalamu kutokana na hivi sasa kuwepo na mtaalamu mmoja raia wa Cuba anayesaidia tiba katika hospitali hiyo.Alisema kwamba wanahitaji watalaamu watano akiwemo wa fani ya saikolojia, mtaalamu wa mambo ya huduma za jamii, daktari wa magojwa ya akili, na wauguzi ambao kwa sasa wanatosheleza lakini kada nyengine zilizobakia hazina wataalamu kabisa.Hata hivyo Daktari Dhamana huyo alisema serikali imekuwa ikichukua juhudi katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ambapo mtaalamu mmoja anasomeshwa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza tatizo hilo lakini aliomba msaada zaidi kwa wadau na jamii kuona umuhimu wa kusaidia hospitali hiyo.Endelea kusoma habari hii.

JAJI ATEULIWA BILA YA USHAURI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Amani Karume amefanya uteuzi wa Jaji Mkuu bila ya kushauriana na Tume ya Utumishi ya Mahakama imebainika.Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Dk. Salimserikali na mahakama, zinasema Rais Karume amemteua Hamid Mahmoud kushika tena wadhifa huo baada ya kuwa amestaafu kwa hiari na kulipwa mafao yake.Ofisa Mwandamizi katika Ofisi ya Waziri Kiongozi amethibitisha kwamba Rais Karume tayari amemteuwa Hamid.Alisema, “Unachokisema ni kweli. Tayari Mzee (Rais) ameteua Jaji Mkuu baada ya kuwa amestaafu na hapana shaka katiba imevunjwa maana utaratibu unaobainishwa na katiba haukufuatwa.” “Hivi wewe unafikiri mambo yanaendeshwa kikatiba hapa. Mwenyewe akishasema hakuna wa kuuliza,” alisisitiza.Taarifa za kuaminika kutoka serikalini zinasema, Hamid alistaafu kwa hiari Aprili mwaka huu akiwa na umri wa miaka 60.Hata hivyo, anaendelea na wadhifa huo, baada ya kuteuliwa tena bila rais kushirikisha Tume ya Utumishi ya Mahakama.Endelea kusoma habari hii.

MAKAAZI HOLELA YAKWAMISHA MRADI WA POSTA

MAKAZI holela na ukosefu wa miundo mbinu ya barabara nchini ni moja ya changamoto kubwa inayokabili mradi wa simbo za posta Tanzania.Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Daftari jana wakati akizungumza katika semina ya siku moja juu ya majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na maelezo kuhusu mfumo mpya wa anuani na simbo za posta kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.Dk Daftari alisema suala la mipango miji na maingiliano ya utawala ni miongoni mwa mambo yanayofanya ugumu wa mradi huo kuweza kutekelezeka kwa wepesi.Alisema mradi wa anuani mpya za Kitaifa za Simbo za Posta utasaidia kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini hasa vijijini na kupunguza umasikini.Hata hivyo Dk. Daftari alisema katika kuimarisha mradi huo mpya suala la kuwepo kwa majina ya mitaa pamoja na barabara utahitajika ili kurahisisha mawasiliano hayo zaidi vijijini ambapo huduma hizo zinahitajika zaidi.Naibu Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba kuwepo kwa anuani sahihi za majina katika mitaa na barabara hurahisisha mawasiliano ya barua kwa taasisi mbali mbali ikiwemo makampuni yanayotoa huduma za biashara hiyo.Endelea kusoma habari hii.

KIPINDUPINDU CHAPIGA HODI ZNZ

WATU zaidi ya 40 wanadaiwa wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Micheweni na wawili wakiwa wamepoteza maisha baada ya kuibuka kwa maradhi ya kuharisha (kipindupindu) katika wilaya hiyo Kisiwani taka8Pemba.Taarifa kutoka kiswani humo zimeeleza kuwa idadi ya watu wanaotapika na kuharisha imekuwa ikiongezeka kila muda lakini hadi jana hakuna taarifa yeyote iliyotolewa na serikali kuhusiana na maradhi hayo ambayo yameanza kuathiri wananchi kadhaa hadi sasa.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Sultan Mohammed Mugheiry amewaeleza baadhi ya waandhi kwamba kwamba hana muda wa kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa amezongwa mno ya kufuatilia mjadala wa vikao vya Bunge vinavyorushwa moja kwa moja katika televisheni za Tanzania Bara.“Tafadhali niache unaona nafuatilia Bunge kupitia televisheni” alisema Waziri Mugheiry kwa mkato baada ya kutakiwa kueleza nini chanzo cha maradhi hayo na watu wangapi wamekufa huko kisiwani Pemba tokea kuanza kwa maradhi hayo.Endelea kusoma habari hii

SHEHA AMWAGIWA TINDI KALI PEMBA

SHEHASHEHA wa Shehia ya Ole Muhogoni Mkoa wa Kaskazini Pemba Mussa Ali Kombo amemwagiwa tindikali usoni na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.Kamanda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi amethibitisha kutokea tukio hilo majira ya saa mbili usiku na kuahidi kuwatafuta wote waliohusika na kuwachukulia hatua kali za kisheria.Alisema jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kuweza kujua zaidi chanzo cha tukio hilo pamoja na kuwatia mikononi watu waliofanya kitendo hicho cha kikatili.Chanzo cha tukio hilo inasadikiwa ni kufuatia zoezi la daftari la uendelezaji kastika daftari la kudumu la wapiga kura katika kisiwa cha Pemba,ambalo linaratibu wapiga kura wapya na wale wa zamani kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani.Chama cha mapinduzi Mkoa wa Mjini Magharibi kimetoa taarifa kwa vyombo vya habari leo hii mjini Unguja huku kikilaani kutokea kwa tukio hilo linalotishia amani. Endelea kusoma habari hii.

MATAJIRI WAPELEKWA KIINUA MIGUU

WAFANYABIASHARA watano wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kuiibia Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) mamilioni ya fedha akiwemo mfanyabiashara Maarufu Nassor Said Nassir (Bopar) anayemiliki maduka kadhaa ya bidhaa mbali mbali visiwani Zanzibar.Mfanyabiashara huyo maarufu Zanzibar Mkaazi wa Kiembe samaki Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja anadaiwa kuiibia Benki ya Watu wa Zanzibar dola 880,000 kwa kushirikiana na mwenzake Sleyum Mbaraka.Mwendesha mashitaka katika kesi hiyo iliyosomwa katika mahakama ya Mkoa Vuga Mjini, Khamis Suwedi alisema wafanyabiashara hao wawili walitenda kosa hilo mnamo Machi 11 mwaka huu baada ya kula njama na kuiba fedha hizo kinyume na sheria.Bopar ni mfanyabiashara maarufu Zanzibar mwenye asili ya Asia aliyekuwa akiingiza bidhaa za mchele, unga wa ngano, na bidhaa nyenginezo katika soko la ndani la Zanzibar ikiwemo mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na serikali ya mapinduzi Zanzibar.Endelea kusoma habari hii

HAPANA MAANDAMANO-POLISI

letter 141SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi, kupiga marufuku Maandamano yalioandaliwa na vyama vya siasa kwa madai ya kuwapo kwa kikundi kinachotafutwa kwa kutaka kufanya vurugu, Polisi Mkoa wa Mjini wamekamata silaha mbili, majambazi watatu na bomu moja.Silaha hizo zimekamatwa jana katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Zanzibar, baada ya kufanyika kwa operesheni maalum ya kuwasaka majambazi yanayotumia silaha kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo.Hapo awali Polisi ilitangaza kuzuiya maandamano hayo kwa vile kumekuwa na taarifa mbali mbali juu ya kuwapo kwa kundi la watu ambao hadi sasa wanatafutwa kutokana na kutaka kutumia fursa ya kuwapo maandamano hayo kusababisha uvunjifu wa amani.Hali ya wasi wasi huo Polisi ifahamisha kuwa hawaelewi ni kitu gani kundi hilo linakusudia kufanya fujo hizo kwa muda gani na sehemu ipi wanendeleza mkakati wa kufuatilia watu hao wanaokusudia kufanya fujo. Endelea kusoma habari hii.

TUNAIPONGEZA SMZ-VYAMA

SIKU chache baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutaka suala la mafuta na gesi asilia kuondoshwa katika orodha ya muungano vyama vinne vya siasa nchini vimeandaa maandamano ya amani ya kuunga mkono DSC04923msimamo huo wa serikali.Wakizungumza na waandishi wa habari ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar, viongozi wa vyama hivyo walisema mandamano hayo yamaendaliwa kufanyika siku ya jumamosi wiki hiiAmbapo lengo ni kuonesha hisia za wazanzibari kupinga mafuta na gesi asilia kuwa ya Muungano.“Tunapenda kuwajulisha wananchi kwamba siku ya Jumamosi tujitokezeni kwa wingi sana kuiunga mkono Serikali katika suala hili ambalo ni maamuzi yetu sote tunataka mafuta yasiyo ya Muungano” Alisema Juma Ali Khatib, Katibu Mkuu wa Chama cha TADEA.Alisema alisema katika hoja hiyo, ni vyema watu wakafahamu kuwa Wazanzibari si wakorofi, wala sio kama ni watu wasiotaka muungano lakini wanasimamia maslahi yao ya kiuchumi kwani upande wa Tanzania Bara gesi imekuwa ikizalishwa katika Kisiwa cha Songosongo lakini haijawahi kuwanufaisha wazanzibari.Endelea kusoma habari hii.

KIELELEZO CHA UTAWALA BORA-KARUME

karumeRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amesema kuwa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ni kielelezo cha utekelezaji wa kuimarisha demokrasia na utawala bora hapa Zanzibar. Rais Karume aliyasema hayo leo katika maadhimisho ya miaka saba ya kuanzishwa afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Zanzibar na ufunguzi wa jengo la afisi hiyo katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya jengo la afisi hiyo Miembeni Mjini Unguja. Katika maelezo yake Rais Karume alisema kuwa ilipoanzishwa Afisi hiyo mwaka 2002 madhumuni makubwa ya serikali ilikuwa ni kuimarisha usimamizi wa sheria za nchi kwa taratibu za kitaalamu na zinazoendana na mfumo wa kisasa unaokubalika kimataifa. Alisema kuwa jambo jengine ni kujenga imani ya raia kwamba hakuna mtu atakaeshitakiwa kwa uonevu au kuacha kushtakiwa hata kama ametenda kosa kwa sababu tu ya upendo, kujuana au misingi mingine isiyokubalika kisheria. Rais Karume alisema kuwa kuanzishwa kwa Afisi hiyo kunatokana na serikali kutambua kwamba vitendo vya jinai vinaleta sio tu uvunjifu wa amani bali vinarejesha nyuma ujenzi wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa jumla.Endelea kusoma habari hii

MAREKANI YAFURAHISHWA NA MRADI WA MALARIA

DS%205416[1]SERIKALI ya Marekani imeeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizochukuliwa na Zanzibar katika kupambana na Malaria na kueleza kuwa Zanzibar imekuwa ni kigezo katika kupambana na maradhi hayo kutokana na mafanikio iliyoyapata. Hayo yameelezwa na Mratibu Mkuu wa Mpango wa Rais wa Marekani ya kupambana na Malaria Bwana Timothy Ziemer wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume Ikulu mjini Zanzibar. Katika maelezo yake Bwana Ziemer alimueleza Rais Karume kuwa mafanikio yaliopatikana Zanzibar katika kupambana na Malaria ni makubwa na kuahidi kuendelea kuyaunga mkono ili yazidi kuleta mafanikio zaidi. Alieleza kuwa Zanzibar imekuwa ni mfano mkubwa sana unaochukuliwa na Marekani katika kueleza mafanikio yaliopatikana katika kupambana na Malaria kwa nchi nyengine zilizokatika mapambano ya maradhi hayo. “Zanzibar ni historia ya mafanikio ni mfano kwa nchi nyengine zilizo katika mapambano ya Malaria …kwani hata Rais Bush katika mazungumzo yake mengi juu ya suala hilo alikuwa akiitolea sana mifano Zanzibar”,alisema Ziemer.Endelea kusoma habari hii

NEMBO YETU HUTUMIWA VIBAYA-RED CROSS

CHAMA Cha Msalaba Tanzania kinalalamikia matumizi mabaya ya nembo ya msalaba mwekundu, hilali nyekundu kwa taasisi za serikali na binafsi hapa nchini.Akizungumza katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yalioandaliwa na chama hicho Mjini hapa, Mratibu wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania ofisi ya Zanzibar , Ubwa Suleiman alisema kuwa imekuwa ni mazowea sasa kwa taasisi mbali mbali kuvunja sheria ya matumizi ya nembo hiyo.Mratibu huyo alisema kuwa sheria namba 71 ya mwaka 1962 ya bunge la Tanganyika inaelezea matumizi ya nembo ya msalaba mwekundu hilali nyekundu ambapo adhabu kwa watakao kiuka sheria hiyo ni shilingi 150.“Kwa kweli kumekuwa na matumizi mabaya ya nembo ya msalaba mwekundu na hilali nyekundu wako wanaotumia katika vituo vya afya, magari ya kubebea wagonjwa jambo ambalo hivi sasa tumo katika kulifanyia kazi” alilalamika Mratibu huyo.Endelea kusoma habari hii.

MISAADA IELEKEZWE VYUONI-SORAGA

Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Suleiman Soraga, amewashauri wafadhili kujikita zaidi katika utoaji wa misaada katika vyuo vya Qur-an badala ya kuegemea upande wa miskiti.Alisema pamoja na misaada kuhitajika sehemu yoyote ile katika taratibu za dini yetu ya kiislam, soragalakini ni wazi kuwa Sehemu za vyuo vya Qur-an zimekuwa zikisahaulika kila mara.Soraga alizidi kufahamisha kuwa ni wafadhili wengi wamekuwa wakielekeza nguvu zao katika misikiti, hali ya kuwa vyuo vinayumba.Alisema kusaidia misikiti sio kitendo kibaya lakini ni vyema wafadhili hao wakatambua kuwa vyuo vya Qur-an ndio msingi wa dini na inahitaji kusaidiwa ili watoto wapete elimu ya dini yao kama inavyosaidiwa misikiti.“Siwakatazi wafadhili hao kuchangia miskitini, lakini kuna umuhimu mkubwa hivi sasa jicho la ufadhili wa misaada ikiwamo ya ujenzi likaelekezwa katika vyuo vya Qur-an”alishauri Soraga.Endelea kusoma makala hii.

WASAIDIENI ELIMU MASIKINI -NAHODHA

chiefWAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai Nahodha, amewashauri wafadhili wanaotoa misaada ya chakula na nguo kwa masikini kutumia nafasi hiyo kwa kuwapatia elimu bora.Alisema kupatiwa ilimu kutawawezsha kupata ufanisi mzuri wa kuweza kujituma wao wenyewe kupitia elimu waliyoipatapa na kuachana na tabia ya kusubiri misaada kutoka kwa wafadhili kila siku.Shamsi aliyasema hayo katika ufunguzi wa Redio ya kiislamu iitwayo Nuru katika Msikiti Sahaba pamoja na Chuo cha masomo ya kompyuta na kazi za Amali eneo la Daraja Bovu Mkoa wa Mjini Magharibi.Radioa na chuo hicho vyote vinamilikiwa na Kampuni ya Al-Nour Charity Agency For The Needy iliyoanza shughuli zake mwaka 1990 na kupata usajili mwaka 2003 visiwani Zanzibar.Nahodha alisema ni vyema kwa wafadhili kuangalia upya mtazamo huo wa kutoa msaada wa elimu kwa masikini itakayowasaidia katika maisha yao yote, jambo ambalo ni msingi wa maendeleo. Endelea kusoma habari hii.

KIKWETE ATUNUKU NISHANI ZNZ

kikwete znzRAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewatuku Nishani askari 18 wa Jeshi la Wananchi Tanzania, (JWTZ), kanda ya Zanzibar.Sherehe hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Michezo katika Kambi ya Bavuai, na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali na vikosi vya Serikali ya MAapinduzi Zanzibar (SMZ).Nishani ambazo walivishwa askari hao ni ya Utumishi uliotukuka, Nishani ya muda mrefu na Nishani ya utumishi mrefu na tabi njema.Askari hao walikabidhiwa Nishani hizo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Generali Davis Adolf Mwamnyange, kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Askari ambao walivishwa nishani hizo ni 18 ambapo kati ya askari hao 17 walivishwa nisani ya Nishani ya utumishi mrefu na tabia njema, ambapo askari hao walilitumikia jeshi hilo kwa kipindi cha miaka 15 ambapo kati yao wapo waliostaafu na wengine walishafariki. Endelea kusoma habari hii.

BODI YA SHIRIKA YAFUNDWA

WAJUMBE wa Bodi ya Shirika la Umeme Zanzibar, wametakiwa kuhakikisha wanasimamia majukumu yao ipasavyo kwa kutekeleza miradi mitatu ya umeme ili kuifanya Zanzibar kuwa na umeme wa uhakika.Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi Zanzibar, Tafana Kassim Mzee, umemealiyasema hayo katika sherehe fupi ya kuwakaribisha Wujumbe wa Bodi hiyo wapya na kuwaaga wajumbe wa zamani, sherehe ambayo ilifanyika katika Hoteli ya Ocean View iliyopo Kilimani Mjini Unguja..Naibu Waziri huyo alisema ni lazima bodi hiyo ione umuhimu wa kufanikisha miradi mitatu ya kuweza kupatikana kwa umeme wa uhakika vile ni moja ya malengo yanayohitajika kufanyiwa kazi katika kipindi hichi.Akiitaja miradi hiyo Tafana alisema ni wa umeme wa kutumia mawimbi ya bahari, umeme wa kutumia taka na umeme wa upepo.Alisema ni lazima miradi hiyo iweze kushughulikiwa kwa vile tayari limekuwa likipigiwa makele na watu wengi juu ya kuongezwa kwa vyanzo vya umeme ambapo utaiwezesha Zanzibar kuwana njia mbadala ya upatikananji huduma hiyo. Endelea kusoma habari hii.

PROFESA HAROUB HATUNAE TENA

MHADHIRI Mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam, Professa Haroub Miraji Othman, 66, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hoteli ya Abuso Shangani mjini Zanzibar. Kwa mujibu wa msemaji wa professor%20Haroub%20Othmanfamilia hiyo, Ali Uki alisema kifo cha Professa Othuman kilitokea ghafla akiwa usingizini. Alisema wakati mkewe akimuasha, alistuka alipoona Dk Othman haamki na ndipo alipoita watu kumsaidia. Alisema mkewe pia aliomba msaada wa kuitiwa daktari ili aende kumpima na kuthibitisha kwamba taarifa za kuthibitisha kifo chake zilitolewa majira ya saa 1:30 asubuhi.  Professa Othman alifika mjini hapa juzi asubuhi akitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na Professa Thomas Burgess, Ali Sultan Issa na Maalim Seif Sharif Hamad kiitwacho ‘Race Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar”. Endelea kusoma habari hii.

WAZANZIBARI MUUNGANE-DK SALIM

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU) Dk. Salim Ahmed Salim amewataka wazanzibari kushikamana katika kudai haki zao na kuacha kutumia visingizio visivyokuwa na msingi ambavyo vinaweza kuongeza joto la kisiasa na kukwamisha maendeleo ya Zanzibar. Dk. Salim proameyasema hayo muda mfupi baada ya kuzindua kitabu kilichotungwa na Professa Thomas Burgess, Ali Sultan Issa na Maalim Seif Sharif Hamad kiitwacho ‘Race Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika ukumbi mpya wa Al- Yamin Funguni Mjini Zanzibar. Alisema tofauti za kisiasa hazina budi kuwachwa kwani zinaweza kuchangia migogoro katika nchi hali ambayo inaweza kusababisha machafuko kama nchi nyingi za Afrika ambazo zimeingia katika vita bila ya kutarajia kutokana na kushindwa kuvumiliana na kuendekeza mambo madogo madogo ambayo hayana faida kwa taifa. Endelea kusoma habari hii.

ZEC KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UANDIKISHAJI

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa kutumia kadi za teknoloji ya kisasa linatarajiwa kuanza kufanyika kuanzia Julai 6, katika kijiji cha Micheweni Wilaya Kaskazini Kisiwani Pemba. Afisa Uhusiano wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Idrisa Haji Jecha amewaambia waandishi wa habari kwamba Tume hiyo imeamua kuanza zoezi hilo kisiwani Pemba ambapo zoezi katika Wilaya ya Micheweni litamalizika Agosti 9, 2009na kuingia katika Wilaya ya Wete Agosti 3, 2009 hadi Septemba 13, 2009 na kwa upande wa Wilaya ya Chake Chake wao wataanza Septemba 14, hadi Oktoba 25, 2009. Afisa huyo alisema wilaya ya Mkoani zoezi lake litafanyika kuanzia Novemba 2, 2009 na kumalizika Disemba 7, 2009 ambapo tume imepanga kuwaandikisha makundi tofauti yalioweza kutimiza taratibu za sheria uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984. Jecha alisema uendeshaji wa zoezi hilo utafanyika kwa awamu mbili tofauti na awamu ya pili zoezi hilo litafanyika katika maeneo mbali mbali ya mikoa ya Unguja ambapo ratiba yake bado haijatolewa hadi sasa lakini wakati ikikamilika wananchi watapata taarifa kupitia vyombo vya habari. Endelea kusoma habari hii.

MAITI NYENGINE ZAOPOLEWA ZANZIBAR

KIKOSI cha wazamiaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kimeopoa maiti tatu na kuziona nyingine nne zikiwa zinaelea na hivyo kufanya idadi ya miili ya watu waliofariki katika ajali ya boti ya Mv. Fatih inayomilikiwa na kampuni ya Seagul, kufikia kumi. Kikosi hicho kiliwasili jana kutoka jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza nguvu kwa kushirikiana na wazamiaji 30 kutoka Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) katika kuokoa watu kwenye ajali hiyo iliyotokea Ijumaa majira ya saa 3:30 usiku.

Waokoaji wakitoa maiti

Waokoaji wakitoa maiti

Awali kulikuwa na maiti tatu zilizoopolewa na habari zinasema maiti tatu zilizoopolewa jana zilipatikana ndani ya boti. Maiti zilizopatikana jana ni za Ashura Suleiman Mtege na watoto wawili Ali Haroub Mohammed, (3), na Mukrim Mohammed, (6). Maiti ya mama iliyopatikana jana ilikutwa ikiwa na mtoto aliyemfunga mbeleko. Mtoto huyo anakisiwa kuwa na umri wa miaka mitatu. Watu waliokuwepo kwenye Bandari ya Malindi kushuhudia uokoaji, walionekana kuongezeka majonzi baada ya kushushwa kwa maiti ya mama huyo na mtoto wake. Endelea kusoma habari hii.

MELI YA MV. FATIH YAZAMA ZANZIBAR

MELIMELI ya mizigo inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul, Mv Fatih imepinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar usiku wa kuamkia jana na watu watatu wamethibitika kupoteza maisha huku juhudi za uokoaji zikiendelea. Mamlaka ya Udhibiti na Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra), ilisema meli hiyo iliyopinduka saa 4:00 usiku wa kuamkia jana, ilikuwa na abiria 25 na mizigo yenye uzito wa tani 76, ilipinduka na kuzama ikiwa tayari imekaribia kutia nanga katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar ikitokea Dar es Salaam.

BONDE LA BUMBWISUDI LAREJESHWA

RAIS wa Zanzibar na Amani Abeid Karume amesema kuwa hatua za makusudi zitaendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha miundombinu ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini. Rais Karume aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na DS 6626wakulima huko katika bonde la mpunga la Kibokwa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika sherehe ya uzinduzi wa Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji maji kwa mabonde ya Kibokwa na Bumbwisudi. Mapema kabla ya uzinduzi huo Rais Karume alitembelea Bonde la Bumbwisudi na kuangalia kilimo cha mpunga katika bonde hilo kutoa shukurani kwa wakulima kwa juhudi wanazozichukua na hatua waliyofikia katika kuimarisha kilimo cha mpunga wa kumwagilia maji na kusisitiza azma ya serikali ya kuzidisha ushirikiano na wakulima hao ili kuweza kupata mafanikio zaidi. Endelea kusoma habari hii.

MAJAMBAZI WAUA ASKARI WAWILI WA KVZ

ASKARI wawili wa kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ) jana wameuawa hapo hapo baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi. Katika tukio hilo lililotokea majira ya saa 3:00 usiku pia alikiwemo raia mmoja ambaye alijeruhiwa vibaya kwa risasi katika sehemu ya mguuni na kuanguka chini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo aliwataja watu wawili waliouawa kuwa ni wa vikosi vya serikali ya mapinduzi Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

MIGOGORO YA ARDHI TISHIO ZNZ

MWENYEKITI wa Kituo cha Huduma za Sheria Professa Haroub Othman amesema kwamba migogoro ya ardhi inayojitokeza Zanzibar itasababisha maafa katika siku za baadae iwapo serikali itashindwa kuitafutia ufumbuzi wake.PROF. Hayo ameyaeleza katika uzinduzi wa ripoti haki za binaadamu ya mwaka 2008 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha SUZA na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Ali Mzee Ali. Alisema kwamba kituo cha huduma za sheria Zanzibar kimekuwa kikipokea idadi kubwa ya kesi zinazohusiana na ardhi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba na waathirika wakubwa ni wananchi masikini katika maeneo hayo. “Tatizo la ardhi ni kubwa sana hapa Zanzibar mimi nasema iwapo serikali haitokuwa makini katika kulitazama suala hili siku za usoni tutakuwa na maafa makubwa hasa kwa wananchi kwa sababu ardhi ni rasilimali inayotememewa na wananchi” alisema Professa. Endelea kusoma habari hii.

MAGARI MABOVU YAKAMATWA ZNZ

gari la manispaa likitafuta meza eneo la darajaniJUMLA ya Magari mabovu 126 yamekamatwa yakitoa huduma za uchukuzi na usafirishaji wa abiria yakiwemo yanayomilikiwa na baadhi ya vigogo katika manispaa ya mji wa Zanzibar. Magari hayo yamekamatwa katika operesheni maalumu uliyoanza kufanyika juzi na kuwashirikisha askari polisi, bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) pamoja na Idara ya Usafirishaji visiwani. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban alisema katika zoezi hilo la siku moja magari 610 yalikamatwa na kufanyiwa ukaguzi ambapo magari 126 yalibainika kuwa ni mabovu na yanatoa huduma kinyume na sheria. Alisema miongoni mwa makosa yaliobainika ni kuwepo gari zinazotoa huduma za uchukuzi na usafirishaji zikiwa hazina taa wala breki vitendo ambavyo ni kinyume na sheria ya usalama barabarani nchini. Endelea kusoma habari hii.

NDEGE YA RAIS KARUME YASHINDWA KUTUA ZNZ

Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume ameshindwa kuhudhuria katika maadhimisho ya miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 3yalingozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete jana katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es salaa. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa kutoka tanzania bara na Zanzibar lakini Rais Karume ameshindwa kuhudhuria maadhimisho hayo baada ya hali ya hewa kuchafuka na hivyo ndege ya serikali kushindwa kutua katika uwanja wa kimataifa wa Zanzibar. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Rais Karume kushindwa kuhudhuria sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu alipoingia madarakani mwaka 2000 baada ya Rais Mstaafu Dkt Salimn Amour Juma (Komandoo) kumaliza kipindi chake cha uongozi. Endelea kusoma habari hii.

WAZANZIBARI WAJADILIANA KUHUSU MUUNGANO

Wakati watanzania leo wanaadhimisha miaka 45 ya Muungano wa Tanyanyika na Zanzibar, Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud amesema wakati umefika Serikali ya Tanganyika ikarejeshwa. Hayo ameyaeleza katika mada yake IMG_0386iliyowasilishwa katika kongamano la kitaifa kwa niaba yake na Mwanasheria Ali Omar ambalo limewashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar, viongozi mashuhuri wasomi, na viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo wa CCM na CUF. Aboud alisema kwamba serikali ya Tanganyika irejeshwe ili iweze kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya muungano kwa upande wa Tanzania bara ili kuwa na mfumo kama unaotumika Zanzibar. Endelea kusoma habari hii.

MAANDAMANO MARUFUKU- POLISI

jumikiJESHI la Polisi Zanzibar limepiga marufuku maandamano ya kuunga mkono msimamo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuhusu suala la mafuta na gesi asilia kutolewa katika orodha ya mambo ya Muungano. Maandamano hayo yaliokuwa yameandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) yalipangwa kufanyika jana katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba na kuhudhuiwa na idadi kubwa ya wazanzibari ambao kwa takriban mwezi wa pili sasa kumekuwepo na gumzo kubwa kuhusiana na sula hilo la kuungwa mkono serikali. Kwa mujibu wa barua ya jeshi la polisi ya Aprili 24,2009 yenye kumbukumbu namba W/MJN/58/VOL.1/10 iliyosainiwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mjini Unguja SP. Mkadam Khamis Mkadam imepiga marufuku maandamano hayo. Endelea kusoama habari hii.

MAISHA YA JUU YAWATUMBUKIA NYONGO VIJANA ZNZ

KUMEIBUKA genge linaloonekana kuwa ni la kifalifu ambalo linasafirisha vijana wa kitanzania na kuwapelekea nchini Israil kwa madai ya kuwapatiwa kazi na maisha bora Imefahamika kwamba genge hilo hata hivyo haliwaambii ukweli wa safari hizo vijana na zaidi ya vijana watano wa Zanzibar wamenusurika vifo baada ya kushambuliwa na askari wa Israil katika mpaka wa Misri na nchi hiyo wakati wakijaribu kuvuka na kuingia Israil Mmoja wa vijana hao Abdul Mohammed aliiambia Mwananchi katika mahojiano malumu kwamba ni mazingira hatarishi sana waliokumbana nayo kwa vile vijana hawatayarishwi kujua uvukaji wenyewe ni wa mbinde kwa kuvuka senyenge, kutambaa kama wanajeshi na kushambuliwa na askari wa Israil wanaowazuwia kwa kila hali wanaoingia nchini kwao. Endelea kusoma habari hii.

TUSIWAITE MAFISADI- KANISA

Kanisa la Anglikan MkunaziniKanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar limesema hakuna haki ya kuwaita matajiri wezi au mafisadi hadi hapo watakapohukumiwa na kupandishwa katika vya sheria ambavyo ndivyo vyenye haki ya kuthibitisha hilo. Kauli hiyo imetolewa na Mhashamu Askofu Augustine Shao Shao wa Jimbo la Zanzibar katika Kanisa la Katiliki la Minara Miwili liliopo Mji Mkongwe Mkoa wa Mjini Magharibi katika ujumbe wake wa mkesha wa pasaka juzi. “Ndugu waumini, kwa mika hii ya karibuni kumezuka kitu kinachowaitwa wenye mali wezi na mafisadi. Kama kweli tunapenda kuendeleza ukweli aliofunua Kristu katika ufufuko wake, hatuna haki kuwaita wenye mali/tajiri wezi au mafisadi mpaka watakapohukumiwa na sheria husika kwamba kweli wao ni wezi na mafisadi kwa mapana yake” alisisitiza Askofu Shao. Endelea kusoma habari hii.

NIMEFURAHI KUFUNGWA GUANTANAMO BAY-MZAZI

Siku chache baada ya kuapishwa kutangazwa Jela ya Guantanamo Bay kufungwa, Mama wa Mtuhumiwa wa Ugaidi, katika Balozi za Marekani Jijini Dar es Salaam na Nairobi, Bimkubwa Said Abdallah (56) amesema bimkubwaamefurahishwa na uamuzi wa Rais mpya wa Marekani Barack Hussein Obama kwa kutaka kufungwa kwa jela ya Guantanamo Bay . “Ninamshukuru sana sana Rais wetu mpya wa Marekani kwa kutoa amri ya kulifunga jela ya Guantanamo bay lakini pia tunshukuru kuwa watoto wetu watafutiwa kesi walizokuwa wamebambikiziwa…” amesema huku akitokwa na machozi mama huyo. Amesema haoni kama kuna haja ya kufungua kesi dhidi ya serikali ya Marekani kwa kumuweka jela kwa miaka kadhaa lakini jambo kubwa analolitaka ni kurejeshwa mwanawe nyumbani na iwapo atakuwa ameathirika ataomba atibiwe. Endelea kusoma habari hii.

MALI ZA SMZ ZIKAMATWE – MAHAKAMA

Court_znzMAHAKAMA Kuu Zanzibar imetoa amri ya kukamatwa magari sita likiwemo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kushindwa kulipa millioni 104.3 za matengenzo ya Ikulu ndgo ya Micheweni kama ilivyoamriwa na mahakama hiyo. Uamuzi huo umetolewa na Naibu Mrajis wa makahama kuu Khamis Ramadhan Shaaban ambaye pia alikuwa akisikiliza kesi ya madai iliyokuwa imefunguliwa na Kampuni ya ujenzi ya AHLY CONSTACTION CO. LTD. yenye maskani yake Kisiwani Pemba. Magari yalioamriwa kukamatwa kwa amri ya mahakama yapo pia magari mawili ya kikosi cha Zima Moto na Uokozi yenye namba za usajili KZU 402 Toyota Bus aina ya Rosa, Toyota Canter yenye namba za usajili KZU 199 na gari la Waziri aina ya Toyota Prado Land Cruzer lenye namba za usajili WN(AR) (TMV) aina ya Prado. Endelea kusoma habari hii.

TISA WAFA KWA AJALI BUNGI

WATU 9 wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa katika ajali ya gari ya abiria iliyotokea  katika Kijiji cha Bungi Miembe mingi , Mkoa wa Kusini Unguja baada ya gari hiyo  kugonga Muembe. Kamanda wa Polisi Mkoa  huo, Rashid Seif alisema gari hiyo yenye namba za usajili, ZNZ 69572 ilikuwa ikifukuzana na gari nyegine kwa dhamira ya kuipita, lakini ghafla ilitokea gari aina ya Escudo yenye namba Z-821 ambayo ilikwaruzana na kupoteza mweleko. Kamanda Rashid amewataja waliofariki kuwa ni Juma Msuri Juma, Mwanajuma Abdallah Ramadhan, Daud Makame Haji, Juma Machano Kombo, Ramadhan Haji Makame. Wengine ni Hanifa Kassim Juma, Jokha Mohammed Ali, Fatma Ali Vuai na Abdallah Hassan Kombo. Endelea kusoma habari hii.

WAGONJWA WA TB WAONGEZEKA TANZANIA

Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya kifua kikuu (TB) duniani imeelezwa kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi 22 zenye hali mbaya ya maradhi hayo ambayo huleta usumbufu mkubwa kwa jamii. Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Zanzibar, Sultan Mohammed mugeiryMugheiry alipokuwa akihutubia kilele cha maadhimisho hayo yaliofanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo aliwataka wananchi kutoficha maradhi na kufika katika vituo vya afya kwa kupata tiba. Mugheiry alisema kwamba kwa wastani Tanzania ina wagonjwa 66,000 kila mwaka wakati kwa Zanzibar peke yake ina wastani ya wagonjwa wapya kati ya 350 na 400 ambayo ni idadi kubwa sana ikilinganishwa na idadi ya watu wa Zanzibar wanaofikia millioni moja. Endelea kusoma habari hii.

JUSSA AWAPA MOYO VIJANA ZANZIBAR

SADC WATAKA UCHUMI UIMARISHWE KATIKA BARA LA AFRIKA

UKOSEFU WA MAJI WATHIRI WAGONJWA MNAZI MOJA

Uhuru wa habari wajadiliwa

WATAALAMU kadhaa wa vyombo vya habari kutoka Barani Afrika wamesema bado sekta ya habari inakabiliwa na changamoto kadhaa barani Afrika na kutaka vyombo vya habari vishikamane katika kukabiliana na changamoto hizo.Wakiwasilisha mada katika mkutano wa siku mbili uliowajumuisha wataalamu mbali mbali ambapo wamesema licha ya kumekuwepo na juhudi mbali mbali katika kuimarisha vyombo vya habari vya Afrika lakini bado kunahitajika nguvu za ziada katika kukabiliana nazo.Endelea kusoma habari hii

Advertisements

One response to “Jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s