Jamhuri ya Watu wa Zanzibar irejeshwe

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakisikiliza kwa makini hoja mbali mbali zinazotolewa ndani ya Baraza hilo huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar leo imesema kuwa matumizi ya neno Jamhuri ya Watu wa Zanzibar inawezekana ikiwa wazanzibari wengi watatoa maoni ya kulirejesha jina hilo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakari wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Landu aliyetaka kujua kwa nini jina hilo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar lilifutwa.

Jussa aliuliza “Lini serikali ya Zanzibar itarudisha matumizi ya jina la jamhuri na kuyaweka mapinduzi ya Zanzibar katiak misingi yake iliyokusudiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume?” alihoji.

Waziri Bakari alisema jina la jamhuri lilikuwa likitumika katiak sheria ya katiba ya zanzibar nambari 5 ya mwaka 1964 kama ilivyotamka sheria namba moja ya mwaka 1964 lakini baada ya kufanyika muungano jamhuri ya watu wa zanzibar ikatoweka.

“Baada ya kufanyika muungano wa tanganyika na jamhuri ya watu wa zanzibar Aprili 26 mwaka 1964 na kuundwa kwa Tanzania matumizi ya jamhuri yalififia na kufutika” alisema Waziri.

Aidha alisema jina la jamhuri ya watu wa zanzibar lilifutika kutokana na sheria na katiba zilizokuwa zikitumika na kuacha kutumia jina hilo baada yake kubuni maneno ya Tanzania bara na Tanzania visiwani.

“ Kisheria jamhuri ya watu wa Zanzibar haikufutwa bali ilikuwa haitumiki na tanzania imekuwa ikitumika kwa muda mrefu bila malalamiko yoyote kwa maana hiyo basi matumizi ya Tanzania ni halali kwa sababu kisheria jina likitumika kwa muda mrefu inakuwa halali” alisema.

Waziri huyo alisema kwa sababu jina halikufutwa kisheria ni rahisi kulirejesha tena pale wazanzibari watakapoamua kulirejesha tena kwa hiyo ni jukumu la wananchi wenyewe wa Zanzibar kuamua na serikali itaheshimu maamuzi yao.

“Kwa kupitia wajumbe wa baraza la wawakilishi kazi ya kutafuta maoni kutoka kwa wananchi wao inaweza kuwa ni rahisi juu ya matumizi ya jina la jamhuri lakini pia nafasi iliyopo juu ya machakato wa maoni ya katiba ya jamhuri ya muungano wananchi wende muyaseme mnayoyataka na maamuzi yenu yataheshimiwa” aliahidi waziri huyo.

MIMI SIO UAMSHO – MANSOOR

WAZIRI wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amekanusha kuwa yeye si Uamsho na wala hawaungi mkono kama inavyodaiwa mitaani licha ya kukubaliana na kauili mbiu yao.

“Mimi sio Uamsho wala siwaungi mkono nataka kusema wazi hapa maana kuna watu kazi yao kusingizia wenzao, lakini kwa hili la tuachiwe tupumuwe mie nakubaliana nao kwa maana kaulimbiu hii nakubaliana nayo, lakini sio vurugu zao” Alisema Waziri Himid.

Himid ambaye ni waziri asiye wizara maalumu alisema baadhi ya kauli mbinu zinazotilewa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) ikiwemo kauli mbiu yao maarufu ya “Tuachiwe  Tupumuwe”. Anakubaliana nayo.
Kauli hiyo ameitoa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi jana alipokuwa akichangia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2012/2013.

Alisema hakubaliani kabisa na Jumuiya ya Uamsho na wala yeye haungi mkono mitazamo yao na ametumia fursa hiyo pia kukanusha kwamba hahusiki nayo ingawa wapo baadhi ya watu wanafikiri hivyo kutokana na kukaa kwake kimya kwa muda mrefu.

Waziri Himid ambaye ni muweka hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar amekuwa akisema wazi misimamo yake juu ya Muungano ambapo husema Muungano una matatizo na kuna kila sababu ya kushughulikiwa lakini sio kuuvunja.

“Mheshimiwa Naibu Spika, maoni ya makundi haya yote yanaheshimiwa, lakini katika hili la kuvunjua Muungano sikubaliani na kundi hilo na tutaendelea kuwasihi wakubaliane na sisi katika kudumisha Muungano wetu maana kitu tulichokiunda na kudumu kwa miaka 48 sio jambo la busara na rahisi tuseme tukivunje” Alisema Himid.

Akizungumzia umuhimu wa kuungana alisema kwamba dunia ya leo ni ya watu  kuungana Mataifa ya Ulaya yanazidi kuungana, lakini hata Afrika hivyo sio jambo la busara kufikiria kuvunja Muungano.

Katika hatua nyengine amewakosoa baadhi ya watu wanaowataka Wawakilishi kutowasemea Wazanzibari katika madai ya Muungano kuwa wamepotoka na kitendo hicho hakikubaliki katika dhana nzima ya Uwakilishi wa wananchi.

Waziri Himid alisema ni haki ya kila mzanzibari kuzungumzia Muungano na ni dhambi kubwa kwa mtu yeyote kuwakataza Wazanzibari au Watanganyika kuzungumzia Muungano.

Alisema wao ni Wawakilishi wa wananchi ambao wamechaguliwa kuwawakilishi katika chombo cha kutunga sheria hivyo sio sahihi kutokea mtu au kikundi kikadai hawawezi kuwasemea wananchi wote.

“Mimi nasema sio sahihi kusema Wawakilishi wasiwasemee Wazanzibari maana wametuchagua tuwawakilishi humu ndani sas inakuwaje tena tusiseme..mimi nadhani sio sahihi hata kidogo, katika hili hatuwezi kuwazuia watu kusema kuhusu mfumo wa Muungano wanaoutaka.

Waziri huyo alisema ni lazima kuwepo kwa mfumo wa Muungano wenye tija ambao hautaleta malalamiko kwa kila upande. “Muungano ulio sawa na haki” Alisisitiza Waziri huyo.

Alisema kwamba msingi wa Muungano ni mkataba na sio katiba ambapo ikiwa kutakuwa na mfumo bora na wenye tija Zanzibar itakuweza kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa, kujiunga na mshirika mbalimbali ya Kimataifa akiyataja kwa uchache kama FAO,FIFA, Benki ya Dunia, UNFPA, WHO na mengineyo.

“Tukiwa na mfumo mzuri ambao utaifanya Zanzibar kuwa na kiti chetu UN, tuweze kujiunga na Jumuiya za Kimataifa tutakuwa tumeweka msingi mzuri katika Muungano wetu.

Waziri Himid aliwanasihi wazanzibari kutokubali kuondoshwa kwenye malengo yao kuhusu suala zima la Muungano na umuhimu wa kila mtu kutoa maoni yake wakati Tume ya Katiba itakapoanza kuchukua maoni ya wananchi hapa nchini.

“Nawaombeni wananchi wenzangu itakapofika Tume ya Mheshimiwa Jaji Warioba twendeni tukatoe maoni yetu na wala tusikubali kupoteza malengo yetu kwa sababu ya mtu au kikundi fulani, kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” Alisema Waziri huyo.

Waziri Himid alisema katika harakati za kuelekea mchakato wa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumekuwepo na kaulimbiu miongoni mwa wananchi ya “Tuachiwe tupumuwe” ambayo imeasisiwa na Uamsho katika madai ya kuidai Zanzibar huru.

BALOZI NDOGO ZANZIBAR

SERIKALI ya Zanzibar inapendelea kuona nchi mbali mbali zilizopo na ubalozi hapa Tanzania zinafungua balozi ndogo upande wa Zanzibar ili kuimarisha mahusiano mema.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Amani (CCM) Fatma Mbarouk Said aliyetaka kujua ni nchi ngapi zimefungua ofisi yake Zanzibar.

Waziri Aboud alisema serikali inaendelea na itaendelea kuwasiliana na ofisi mbali mbali za kibalozi zilizopo Dar es salaam ili zifungue ofisi zao Zanzibar.

“Tunataka ofisi za kibalozi zilizopo Dar es salaam ziwepo na Zanzibar ili kuimarisha zaidi mahusiano” alisema Waziri huyo.

Akizitaja nchi tano zenye ofisi za kibalozi ndogo Zanzibar mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi, ni China, India, Misri, Msumbiji na Oman ambazo zina ofisi zake hapa Zanzibar.

Aidha alitaja Uingereza, Sweden Norway na Denmark kuwa zina mabalozi wa heshima wenye makaazi yao hapa Zanzibar.

UPUNGUFU WA WATAALAMU KATIKA HALMASHAURI

WAZIRI wa Nchi ofisi ya rais Dk Mwinyihaji Makame Mwadini amesema upo upungufu wa watendaji na wataalamu katika halmashauri mbali mbali Unguja na Pemba.

Akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile (CUF) Mohammed Haji Khalid aliyekaa kujua juhudi za serikali katika kuimarisha juhudi za utendaji kwenye hamlashauri ya chakechake Pemba. Dk Mwinyihaji alisema serikali inaweka mikakati ya kuimarisha serikali za mitaa.

“serikali katika kulitatua tatizo hili tayari imetayarisha sera ya serikali za mitaa na imeweka mikakati maalumu ya kuongeza wataalamu wa aina mbali mbali” alisema Dk Mwinyihaji.

Waziri huyo alisema wizara yake imewasilisha maombi maalumu katika ofisi ya utumishi wa umma kwa ajili ya kupata wataalamu na kuondosha tatizo la upungufu wa nguvu kazi katika halmashauri zote za Unguja na Pemba.

Alisema katika mpango huo wanasheria wataajiriwa pamoja na wahasibu ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato madogo madogo katika halmashauri hizo na kuimarisha serikali za mitaa.

Zanzibar ina wilaya 10 na halmashauri kadhaa ambapo wajumbe wa baraza la wawakilishi wamekuwa wakilalamikia kutokuwepo na utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa mapato.

UWAJIBIKAJI SERIKALINI NI HABA

KUTOKUWEPO kwa ufanisi wa kazi katika baadhi ya taasisi za serikali ya zanzibar kunatokana na tabia ya utoro.

Kauli hiyo imetolewa ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea hapa Zanzibar na waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora, Haji Omar Kheri wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub.

Ayoub alitaka kujua sababu zinazopelekea watendaji wakuu kushindwa kusimamia majukumu yao na kuruhusu tatizo la utoro na uvivu kuendelea katika maeneo ya kazi.

Waziri Kheri alisema “Tatizo la uvuvi, utoro ruhusa za harusi, maulidi na mazikoni ni mambo ambayo hupunguza ufanisi wa kazi na kupoteza muda mwingi kazini. Hii inatokana na kutosimamiwa ipasavyo” alisema waziri.

Waziri alilaumu baadhi ya watendaji katika taasisi za serikali kwa kushindwa kusimamia majukumu yao kutokana na tabia ya muhali.

“Kwa kuwa tabia hii ya muhali imejengekea kwa miaka mingi sio rahisi kuondosha mara moja hata hivyo kila mmoja wetu kwa pale alipo lazima atekeleze wajibu wake ipasavyo kwa mujibu wa sheria” alisema.

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin alitaka kujua mipango iliyopo ya kuondosha tatizo la muhali katika sehemu za kazi ambapo waziri alijibu kuwa kuna utaratibu maalumu umeanzishwa kuwapima watendaji.

Waziri Kheri alisema zipo sheria za umma pamoja na sera ambazo zinatoa adabu kwa uvivu, utoro na asiyewajibika na kutaka watendaji watumie sheria hizo ili kuimarisha ufanisi.

“Kwa sasa kila wizara ina mpango kazi wa robo mwaka na kila mtumishi hupangiwa majukumu ya kufanya kwa kila siku ipo pia suala zima la kutathimini watendaji kwa kutumia fomu maalumu ya upimaji, utendaji wa wafanyakazi, haya yatasaidia kuondosha muhali” alisema waziri huyo.

 

MWISHO

 

Bajeti ya serikali yapita bila kupigwa

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi jana wamepitisha bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 huku serikali ikiahidi kushughulikia malalamiko ya wajumbe wa baraza hilo.

Akijibu hoja za wajumbe mbali mbali kabla ya bajeti ya billioni 648.9 kupitishwa na wajumbe hao, Waziri wa fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema suala la kudhibiti mapato ambalo limelalamikiwa na wajumbe wengi litafanyiwa kazi.

“Mheshimiwa Spika inaonekana baadhi ya wajumbe wako wana uelewa mzuri katika kudhibiti mapato, nitamuomba makamo wa pili wa rais ili tushirikiane katika kutoa mawazo yatakayoweza kuzidisha mapato kwa serikali” alisema Mzee.

Waziri huyo alikiri kuwa bado upo mwanya wa uvujaji wa mapato ya serikali katika idara za serikali na sekta binafsi hali ambayo inahitaji mbinu za kudhibiti.

Mzee alieleza kuwa bajeti ya mwaka huu imetoa muelekeo wa kupunguza matatizo ya ajira pamoja na kuimarisha semta ya elimu na afya ili wananchi wengi waweze kunufaika.

“Serikali imetoa kipaumbele katika afya hasa maslahi ya kwa madaktari, ununuaji wa vifaa na katika sekta ya elimu ambapo vikalio ‘desk’ vitanunuliwa kuondosha usumbufu kwa wanafunzi” alifafanua.

Akizungumzia kuhusu suala la ajira na upatikanaji wa umeme wa kudumu visiwani zanzibar, Waziri alisema serikali haina uwezo wa kutoa ajira kwa vijana wote isipokuwa mipango iliyopo ni kuimarisha sekta isiyokuwa rasmi.

Alisema vijana amabo hawana ajira wakiwemo wanawake wanatakiwa kujiunga katika vikundi ili wapate mikopo ya kuanzisha miradi mbali mbali na kuweza kujitegemea kwa sababu ajira sio lazima serikalini.

Kuhusu umeme Mzee alisema tatizo lililojitokeza ni kwamba miradi mingi ya umeme ya kujitegemea inahitaji fedha nyingi ambazo hivi sasa serikali haina na kuendelea kutegemea umeme unaotoka Tazania bara.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi walipokuwa wakijadili bajeti hiyo walilaumu serikali kwa kushindwa kuwa na mipango madhubuti kuwa na umeme wa uhakika na kuondokana na kutegemea Tanzania bara.

Katika kujadili bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2012/2013 suala la uvujaji wa mapato pamoja na muungano lilitawala mjadala huo na mawaziri pamoja na mwanasheria mkuu wakiwataka wajumbe na wananchi kwa ujumla kutokuwa na jazba na kutumia fursa ya kutoa maoni kwa tume ya Warioba.

MWISHO

Polisi jamii imefanikiwa

SERA ya polisi jamii imeleta mafanikio makubwa katika kupunguza uhalifu na kuleta utulivu ndani ya jamii ya kizanzibari tangu kuanzishwa kwa mfumo huo.

Hayo yameelezwa katika kikao cha baraza la wawakilishi na waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais, Mohammed Aboud Mohammed akijibu suali la mwakilishi wa nafasi za wanawake, Mwanaidi Kassim Mussa aliteka kujua changamoto zinazoikabili jeshi la polisi.

Waziri alisema miongoni mwa changamoto ni kulinda amani nchini, ukosefu wa vitendea kazi na nyumba za kuishi askari.

“Jeshi la polisi likishirikiana na wadau wengine limefanikiwa kupunguza uhalifu na kuleta utulivu ndani ya jamii ya Zanzibar. Tunafaa tuendelee kushirikiana na kuendeleza mafanikio yaliopatikana” alisema Aboud.

Akizungumza changamoto nyengine alisema serikali ya jamhuri ya muugano imekuwa ikitoa fedha ya kumaliza matatizo yaliyomo katika jeshi la polisi ikiwemo ununuaji wa vitendea kazi na nyumba za kuishi polisi.

“Bajeti ya polisi inayotoka katiak serikali ya muungano inajumuisha Zanzibar na katika mwaka wa fedha uliopita 2011/2012 jeshi la polisi kwa upande wa Zanzibar liliidhinishiwa matumizi ya zaidi ya bilioni 11” alisema.

Aidha waziri alitoa wito kwa wadau mbali mbali kuendeleza ushirikiano na jeshi la polisi ikiwemo kutoa misaada ambao utasaidia kuimarisha utendaji wa jeshi hilo.

Mwakilishi Mwanaidi alitaka kujua mipango ya serikali itaifanyia lini matengenezo nyumba za polisi ambazo ni chakavu na hazilingani na hadhi yao.

Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo, walilalamikia Serikali ya Muungano kwa kushindwa kuimarisha Jeshi la Polisi ili litekeleze majukumu yake kwa ufanisi.

Mwisho.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeongeza bajeti ya chakula kutoka Sh. Milioni 400 hadi Sh. Milioni 600 kwa mwaka huu wa fedha ili wanafunzi wa vyuo vya mafunzo (jel) waweze kupata milo mitatu kwa siku.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini aliliambia hayo Baraza la Wawakilishi jana wakati akijibu swali la Mohamed Haji Khalid (Mtambile, CUF), aliyetaka kujua mipango ya kuwezesha wanafunzo wa vyuo vya mafunzo kupata milo mitatu kwa siku moja.

Mwakilishi huyo pamoja na wawakilishi wengine waliouliza maswali ya nyongeza walisema wanafunzi kuendelea kupata mlo mmoja kwa siku inatia aibu vyuo vya mafunzo, idara inayozalisha mazao mbalimbali yakiwemo ya chakula kama muhogo na mpunga.

“Kwa sasa mambo ni mazuri, serikali inajitahidi kuhakikisha wanafunzi wanaishi maisha ya furaha kulingana na matakwa ya haki za binadamu. Baadhi ya vyuo tayari wameanza kupata milo mitatu kwa siku pamoja na kuwa na vyoo vya kisasa,” alisema Dk. Mwinyihaji.

Waziri Dk. Mwinyihaji alisema uimarishaji wa haki za binadamu katika vyuo vya mafunzo utafanywa hatua kwa hatua kulingana na upatikanaji wa fedha. Alisema wanaharakati wa haki za binadamu pia wamekuwa wakishinikiza serikali kufanya hivyo.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wamekuwa wakilalamika kwamba hali ya katika vyuo vya mafunzo Zanzibar ni mbaya ikiwemo suala la kuendelea kujisaidia kwenye ndoo, maarufu kama mtondoo.

Aaidha, wajumbe hao wanaishindikiza serikali kujenga jela maalum kwa ajili ya wanafunzi watoto na kuwatenganisha na watu wazima. Kitendo hicho wanalalamika kuwa ni kinyume cha haki za binadamu.

Mwisho.

Ukosefu wa wataalaumu

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeendelea kufunga mikataba na baadhi ya wastaafu kutokana na upungufu wa wataalamu katika baadhi ya sekta, amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Haji Omar Kheri.

Akijibu swali la mwakilishi wa Muyuni, Jaku Hashim Ayoub (CCM), Waziri huyo alisema jumla ya watumishi 30 ambao wamefikia umri wa kustaafu wanaendelea na ajira serikalini.

“Watumishi 25 ambao walikuwa wastaafu tumeingia nao mikataba ya kuendelea kuitumikia serikali katika idara mbalimbali, watano ambao tayari wameshastaafu tumewaajiri kwa mkataba katika sekta ya afya (wawili), Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na Ikulu mmoja ambaye ni mwandishi wa hotuba za rais, alisema.

Waziri Kheri alisema bado serikali inahitaji utaalamu, ujuzi na uzoefu maalum ambazo zitasaidia katika kuharakisha maendeleo, ndo maana baadhi ya wastaafu wanaonekana serikalini.

Alieleza vijana ndo nguvu ya taifa na kwa kufuata maelekezo ya kisheria kwa mwaka huu wa fedha serikali itawaajiri zaidi wafanyakazi 2,500 ili kusaidi kupunguza tatizo la ajira nchini.

21 responses to “Jamhuri ya Watu wa Zanzibar irejeshwe

  1. Pingback: Jamhuri ya Watu wa Zanzibar irejeshwe·

  2. Ni kweli watuachie tupumue.haki na uhuru wa znz ndio msingi mkuu wamadai yetu.Tunahiaji znz yenye hadhi kimataifa

  3. JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR K WANZA.
    Nawaomba wawakilishi msiogope huu ni wakat wa kusema hakuna wa kukuzur turejeshe JWZ KWANZA.halaf ndo tupange mambo mengine ss hatupo znz ila tupo pamoja nanyi maendeleo ya nchi yanajengwa na wananch wenyewe tushikamane tuwe wamoja tuijenge nchi yetu irud kama zamani hakuna lisowezekana M.mungu atupe nguv na atujalie tuipate jamuhur yetu kwanza.TUCHIWEEEE TUPUMUEEEE.

  4. Mheshiwa Mansour uniniangusha bwanaaa!… Kwani kuwa uamsho ni dhambi ya kisiasa au woga umeanza kukunyemelea?.

    Mheshimiwa vurugu za UAMSHO au za polisi? Teteeni Dini yenu au hamjawaona wenzenu Wakatoliki na Wakristo Bungeni
    wanavyowalinda na kuwatetea Maaskofu na Mapadri wao?

    Wacheni kujifanya Impatial mpaka mnawadhalilisha Masheikh, Uislamu na Waislamu si sahihi.

    Baya mpaka ma-bar mmeanza kuyatetea au nayo ni nyumba za Ibada za wakristo-wafalme wa Zanzibar?
    Moh’d Aboud challenge kwako hii.

    Au ndio kukutea unga wako Mheshimiwa Mansour usije ukamwagwa na kina Borafya Mtumwa Borafya wapika Gongo?

    Kama msimamo wa pamoja unahitajika basi ni muhimu viongozi wa kisiasa na wa Dini (Uislamu) mkae pamoja mtuambie the way foward vinginevyo tutazongana wenyewe kwa wenyewe halafu watanganyika watutie changa la macho.

    Halafu kama tutakubaliana Muungano wa Mkataba (Confederation Union) na sio ule wa Kikatiba (Federation) ambapo huu wa federation ni kitanzi kingine, basi mambo yatakayoingizwa ndani yake yasiwe haya:-

    1. Ulinzi,
    2. Utamaduni,
    3. Elimu yote,
    4. Uraia,
    5. Fedha,
    6. Mambo ya nje,
    7. Uraisi,
    8. Vyama vya kisiasa.
    9. Mipaka

    Mengine naomba muongeze wanaukumbi.

    MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

    JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

    “When peace fails apply force”

    SERELLY.

    • Asalam, Mheshimiwa Mansoor yakhee nakusihi sana acha woga juu ya Muungano, watanganyika ni watu wa kuambiwa ukweli tuu, na sio masuala ya kuleta negotiation ya aina yeyote kwao sababu ni kwamba wameshatutuuga vyakutosha sasa WATUACHIE TUPUMUE. Uamsho sio kikundi cha fujo bali ni Jmuiya ya kiislamu na yenye usajili halali katika serikali ya Jamuhuri ya watu wa Zanzibar. Tunakwambieni Polisi nyinyi ndio usalama wa raia lakini inakuwa kinyume chake ni wachafuzi wa amani na utulivu.Nyinyi ni watumwa wetu kwa kuilinda haki na usalama wa raia lakini badala yake munatupiga mabomu,virungu na kutukamata na kupanda mahakamani, tunakwambieni “ONE DAY YES” kAMA ALIYOSEMA Alhaj Abdu Jumbe na sasa yanadhihiri kAZI Kwenu Polisi
      itakuwa CCM haiwezi kukuokoa !!!!!!!! Mambo wanayotakiwa watanganyika wayawache kama yalivyo ni:-
      Mafuta yetu na maliasili zote zilizopo Zanzibar.
      Masuala yote ya Ushuru na Forodha (TRA) Mwisho msasani.
      Bandari huru /Free port
      Mambo yote ya jumuiya za Kimataifa nakadhalika. TUACHIENI TUPUMUEEEEEEE!!!!!!!

  5. umesahau , na wizara ya mambo ya ndani na uhamiaji hayatakiwi kuwa ktk ushirikiano , kwa wale mabaradhuli wanaotaka kutumia neno jamhuri , hii itasaidia nini? kwani mbabe akijisifu anaweza hili au lile ndio kweli ? hatutaki jamhuri hewa enyi mabaradhuli wa baraza la watu wasiosoma

  6. hao wafanyakazi ikiwa hamuwalipi misharaha ya kutosha , unategemea watakuwepo kazini muda wote? si lazima waende kwengine wakatafute rizki ya ziada ili wafikishe mwezi , na wakibaki kazini basi ujue kuna rushwa ndio inayowaweka ,

  7. Muhimu na kwa mkato kabisa kusiwe na Wizara ya Muungano!
    Jamhuri ya watu wa zanzibar na mamlaka kamili.
    Ikiwa ni Muungano uwe wa kupiga vita madawa ya kulevya,Muungano wakupiga vita maradhi ya kuambukiza na mengineyo kama hayo!!

  8. Muungano utakaokuja usijihusishe na mambo haya hapa chini. Muungano huu katika maumbile yake uwe ni kiongozi ambae mamlaka yake ni very ceremonial ! Kazi yake itakuwa ni Kulinda Muungano kama vile Kingdom ya Saudi inavyolinda Misikiti miwili mitakatifu.
    1. Ulinzi,
    2. Utamaduni,
    3. Elimu yote,
    4. Uraia,
    5. Fedha,
    6. Mambo ya nje,
    7. Uraisi,
    8. Vyama vya kisiasa.
    9. Mipaka
    10. Raslimali ikiwemo Bahari kuu- Kwa Zanzibar kumiliki Bahari Kuu itajiongezea mapato.

    • MBONA MMESAHAU KUSEMAMA MUUNGANO UKIVUNJWA KILA MTU ARUDI KWAO MZENJI KWAO MBARA KWAO HAPO NDIPO MUUNGANO UTAKUWA UMEFUNJWA

  9. @msema.

    *Uko sahihi ndugu yangu kipenzi, Wizara ya mambo ndani na uhamiaji
    LAZIMA YATOLEWE NJE NJE TENA NJEEE.

    *Mishahara bado ni issue, kwanza midogo pili haitolewi kwa wakati na wakati mwengine haitolewi kabisa kabisaaa!

    Mfano mzuri ni wizara ya elimu ambapo Walimu wapya 2012 mpaka leo hawaja lipwa mshahara wao wa mwezi wa nne 4/2012 wakati mkataba wao unaonesha wameajiriwa tarehe 2/4/2012.

    Baya zaidi vijana hawa baada ya kuona kuna kila dalili za kuliwa pesa zao na maafisa wa Wizara ya Elimu, wakaamua waunde tume maalum ili kufuatilia mshahara wao huu, tume hii baada ya kufika wizara ya Fedha walithibitishiwa kuwa pesa zao tayari zishatumwa wizara ya Utumishi. Baada ya kufika Utumishi pia wakathibitishiwa kuwa tayari mishahara yao 2 ya mwezi wa nne (April/2012) na wa tano (May/2012) ishatumwa kwa pamoja kwenda Wizara ya Elimu, Wizara ya utumishi pale pale mbele ya vijana hawa iliwasiliana na maafisa wa Wizara ya Elimu na kuwataka wawape mishahara yao miwili kama inavyotakiwa. Cha aibu zaidi ni kuwa maafisa hawa wa Wizara ya elimu awali waliwadanganya walimu hawa kuwa eti “mshahara tuliotumiwa hapa kutoka Wizara ya Fedha ni mmoja tu wa mwezi wa tano (May/2012)”. Lakini kama tunavyojua Zanzibar ni ndogo vijana hawa wakati wanakwenda Wizarani ili kupokea mishahara yao walikuwa taarifa kamili kutoka kwa baadhi ya watumishi wa Wizara fedha kuwa mishahara yao miwili ya April na May/2012 imetumwa kwa pamoja Wizarani kwao, kwa hivyo walijua tangu awali kuwa ule uliotolewa pale na maafisa wa Wizara ya Elimu ulikuwa ni UONGO na dalili ya WIZI.

    Cha kusikitisha ni kwamba vijana hawa wa Kizanzibari na wa Kizalendo waliokataa kulisaliti Taifa lao la Zanzibar wakaamua kubaki Zanzibar badala ya kwenda kulitumikia Taifa la Watanganyika kama ilivyoanza kuzoeleka kwa baadhi ya vijana ambao mara tu baada ya kukhitimu masomo hutafuta ajira katika mataifa mengine ikiwemo Tanganyika na kumwachia Dr. Ally Moh’d Shein Waziri wa Muungano asiyekuwa na Wizara maalum Janga lake la kiginyingi dhidi ya Elimu ya Wazanzibari, hawajapewa pesa hizo mpaka leo hii yaani mpaka sasa hivi, wamebaki wakisikitika tu kwa machungu ya ukatili waliofanyiwa.

    Zaidi ya hapo wanatume waliochaguliwa pesa hizi miongoni mwa vijana hawa wamekuwa wakipokea SMS za vitisho vya kufukuzwa kazi kwa kuwa eti hawana SUBRA na ni watovu wa ADABU.

    Haya ninaushahidi nayo. Na mwenye shaka aseme nitampa namna ya kupata uthibitisho kamili.

    Je! Ndugu yangu unatamaa ya Zanzibar kuinua elimu katika Mazingira kama haya ya kimazingile mwanambiji?

    Je! Huu ndio utawala bora wa haki na sheria unaotutangazia kila siku Bw Moh’d Aboud?

    Je! Nchi hii kosa ni kupinga Muungano tu lakini kuludhulumu watu ni halali na ruhusa?

    Je! Kilio cha walimu hawa Serikali hamjakisikia au mnasubiri waandamane muwaue na kuwatesa ili kupunguza wapinga Muungano huu wa Bwana YESU mtakatifu?

    Lakini haya! Jifunzeni kwa Husni Mubaarak ambaye kaishia kwenye kiharusi na kusima sima kwa mapigo ya moyo.

    MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

    JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

    “When peace fails apply force”

    Nawasilisha.

    SERELLY.

  10. anna
    on June 21, 2012 at 8:25 am said:
    MBONA MMESAHAU KUSEMAMA MUUNGANO UKIVUNJWA KILA MTU ARUDI KWAO MZENJI KWAO MBARA KWAO HAPO NDIPO MUUNGANO UTAKUWA UMEFUNJWA

    Ana

    Si rahisi kukusoma wewe ni mtu aina gani. Hata hivyo, maneno yako yaonesha jinsi ulivyomchanga na kwamba huna sifa za kujiunga na ukumbi. Ni lazima ukumbuke kuwa wanayoyadai Watu kutoka Zanzibar si kutengana kwa watu au watu kuhama kutoka maeneo waliyopo na kurudi walikotoka. Madai ya watu Wa zanzibar ni mabadiliko ya Mfumo wa Muungano iliyakidhi haja, mahitaji na mazingira ya leo na haya pia yatakusaidia nawe unae utaifa usioeleweka.

    Kila mtu anazungumza vyake kuhusu sababu za Muungano huu wa Zanzibar na iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na sasa Tanzania Bara. Kuna wanaouhusisha na Vita Baridi na Wale wanaouhusisha na Pan Africanism. Si Kazi yangu kusema lipi kati ya makundi haya ni sahihi. Ninalojua ni kuwa Muungano huu ulifanywa na huku ukiacha masuali ya kisheria na kimuundo bila majibu. Miaka 48 baadae kutokana na watu kudadisi mambo kwa kina watu wanaibuka na kuuliza uhalali wake, manufaa yake na wale wenye busara wanauliza hivi lakini katika context ya mwelekeo wa Muungano siku zijazo. Hawa pengine ndio hao waundao Tume ya Kukusanya maoni wakaweka Terms of Reference za kukataza kuzungumza Muungano kisha wakahalalisha kuuzungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari. We do not know, if this is about diffusing the mounting ant-union tension or embracing the truly urge for change in the union set up to build up a stronger and viable union. Katika Dhamira yoyote ile watu hawa ni lazima wapongezwe kwa kusoma na kuheshimu mahitaji ya wakati.

    Ana ukisoma historia hiyo ya kuanzia abolition of Slave Trade ambayo pengine ndiyo uliyosma Watu wa Zanzibar na Wa Bara hawatafuatiani. Watu hawa wamechanganya damu, nasaba na mali. Muungano si uliiochangia haya yatokee. Nakumbuka katika kijiji chetu alikuwepo Mzee Ali Mngoni, Babu Pesa Mbili na hawa walifia kwetu miaka mingi kabla ya mimi kuzaliwa. Wakati nawaona walishaishi hapo kwa umri wao wote.

    Vile vile huko bara kama kuna watu kutoka Zanzibar kila sehemu. Wengi wao wanafanya kazi za maana hawauzi njugu au miili yao wakati wa usiku. Hawa wanalipa kodi na sijui kuna mtu aliyetari kuwafukuza kwa hali yoyote ile. Maneo ya watu wende kwao yanazungumzwa na watu wenye vichwa vikubwa na ubongo wa mende, pengine kama wewe. Ivi huoni Wageni waliokwenye nchi nyingi na Wanaishi madamu tuu hawavunji sheria. Sisi tunaamini kuwa mabadiliko yanayozungumzwa si ya kuvunnja Muungano bali ni kkuimarisha ili uwe na uhalali na ukidhi mahitaji ya sasa.Ana kama kuna Wazenji au Wabara watakaorudi kwao kwa sababu hii basi pengine ni wale wasio na cha kupoteza ambao lolote lile wanaliunga mkono. Ikiwa wewe ni miongoni mwao basi Minal Faadhin – utaunga mkono mradi huu.

    Ana katika kipindi hiki ambacho tunatafuta jinsi bora ya kujenga nchi hii si busara kuleta chokochoko za kiujimbo au nyenginezo. Au umetumwa ufanye kazi ya kuwatoa watu kwenye mwelekeo ilii wazungumze vitu sivyo! Busara inahitajika ndugu yangu! “When the earth falls, it falls upon the children of the earth! mind you my sister!

    Reply ↓

  11. UWAJIBIKAJI SERIKALINI NI HABA .
    Nafikiri kila mmoja wetu anajua sababu zinazopelekea kwa wafanya kazi kutokuwajibika makazini na kama hamjua basi ni hivi nawambia,hivyo kazi kwenu, kufumbia macho au kutafakari mawazo yangu ,lakini katu wafanya kazi hawatawajibika mpaka yatekelezwe mambo haya yafuatayo:-
    1.Mishahara.
    Kila mfanya kazi anahitaji kupata mshahara wa kumkimu mahitaji yake vyenginevyo hakutakuwa na lifanyikalo kwa ufanisi
    2.ajira bomu.
    Asilimia kubwa ya wafanya kazi wa serikali ni bomu hawajui dhamana zao,utakuta mtu ameajiriwa bila ujuzi wa ajira anayoshikilia hivyo kupelekea asijue kujipanga vyema katika utekelezaji wake.
    3.kazi moja wafanya kazi watano au sita.
    Kutokana na kutokuwa na taaluma ,serikali huajiri watu tu bila kutathmini kazi ambayo itafanywa na hao watu,kumbe kazi yote ambayo inahitajiwa kufanywa na watu watano inaweza kufanywa na mtu mmoja mwenye taaluma na mwenye kujipanga vyema katika nafasi hiyo ,hata kumbana asiwe na nafasi au dharura za kipuuzi kama mlizozitaja za kutoa vijisababu vya arusi,maziko,kuuguliwa nk.
    4.Mawaziri , Mkatibu wakuu,Wakurugenzi Bomu
    Viongozi niliowataja hapo juu ni bomu wamekabidhiwa wizara ambayo hakuna hata mmoja mwenye taaluma ihusianayo na wizara husika ,bila shaka kutakuwa na uwajibikaji mbovu.
    5.Utashi wa kisiasa
    Hapa ndipo kufeli kwenyewe,kwamba waliokabidhiwa wizara wana utashi wa kisiasa na sio wenye ujuzi na wizara hiyo ,kadhalika wafanyakazi wa chini wanasubiri maagizo ili wayafanyie kazi lakini hakuna maagizo yanayotoka katika ngazi za juu kutokana na kujipanga kwao sio kwa taaluma ila kwa siasa .
    6.Kujuana ndio kupata ajira sio taaluma uliyonayo.
    Waajiriwa wengi wa kizanzibari wameajiriwa kutokana na kujuana ,wafanya kazi wengi wamepachikwa katika kazi bila kujua majukumu yao mifano mizuri tu ipo ,moja angalia waajiriwa bandarini.
    7.Msongamano wa waajiriwa wengi kuliko kazi yenyewe
    Waajiriwa katika kazi za serikali ni wengi kuliko kazi ambayo inahitajika kufanywa na kima cha watu walioajiriwa.utaona pahali panahitaji wafanya kazi 12 ili kila mmoja awe makini katika utendaji wake ,hapo wataajiriwa 40 .sasa unataraji uwajibikaji gani ? wakati kila mmoja anamtegea mwenziwe.
    8.Wizi au Rushwa.
    Waziri , katibu mkuu au Mkurugenzi atakua anayo sifa moja au zote katika hizi mbili,unataraji uwajibikaji gani ikiwa mdogo anajua issue hii inatendeka kwa viongozi wao kweli kutakuwa na heshima hapo?,au uwajibikaji?bali kutakuwa na kulindana kwani mdogo nae atakwapua anapopatia nafasi ya kufanya hivyo ,ni nani wa kumkemea ikiwa chanzo ni kiongozi?
    9.Waziri,katibu mkuu au mkurugenzi kufika kazini kwa kuchelewa au kuondoka mapema.
    Hili litafuatiwa na wafanya kazi wadogo wadogo pia kwani kiongozi akichelewa na mdogo atachelewa au kiongozi akikimbia mapema na mdogo hali kadhalika atauwasha mapema pia.
    10.Punch in punch out.
    Hakuna utambulisho wa mfanya kazi ameingia saa ngapi na ametoka saa ngapi,ikiwa kipo chombo cha kumuorodhesha wakati alioingia na wakati aliotoka bila shaka wafanya kazi wataheshimu wakati kwani akiwa amechelewa ni lazima akatwe katika mshahara wake wakati aliokuwa hayupo hali kadhalika akiwa ametoka mapema.
    11.Raisi ndio kigezo.
    Raisi atakuwa anafanya mambo kinyume kwa hiyo waliochini yake watafanya kinyume nyume.
    Raisi atakuwa anajilimbikizia kila kitu majumba ,mashamba,biashara ,machimbo na mengine msiyoyajua ,waziri wake atafata kigezo cha mkubwa wake hali kadhalika wanaofuata wote watakuwa wakila chungu kimoja .nchi ndogo kama zanzibar hakifichikani kitu kila mmoja atajua na ndipo hapo itakuwa vurugu mechi .
    Mambo yote haya niliyoyataja hapo ni ya kuzingatiwa nyenginevyo vurugu mechi itakuwa aluta continua.
    Nani wa kumlaumu ikiwa wewe mwenyewe unaezungumza haya madhambi yako katika uwajibikaji hayabebeki unataraji nani atakaetua mzigo wa mwernziwe?

    • @ ali

      Uko sahihi, naunga mkono hoja.

      Watu wapo kisiasa zaidi (kivyama), hawajui kuwa vyama tunatakiwa tuvitumie kama ngazi na nyenzo za kuleta maendeleo yatokanayo na ushindani wa kiufanisi na kiutendaji baina ya vyama na mwishowe kuwajengea wananchi tabia ya kuvipenda na kuviunga mkono vyama kwa mujibu jitihada zake katika ufanisi wa uletaji maendeleo badala ya kuviunga mkono vyama kwa misingi ya u-Unguja, u-Upemba, ukabila n.k. Na waweze kubadili vyama wakati wowote kwa vipimo hivyo hapo juu na sio watu kuamini kuwa mtu akiwa CCM basi ni CCM tuuu…! au kama CUF basi ni CUF tuuu…!

      MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

      JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

      “When peace fails apply force”

  12. Picha hiyo ya wawakilishi hapo juu inadhihirisha kwamba bado wawakilishi wetu ni mbumbumbu.
    Kwa nini nikasema hivyo,huu ni ulimwengu wa computer si busara kutia picha kama hiyo kuonesha wawakilishi wapo katika kikao cha kuiwakilisha nchi wakiwa hata mmoja hana lap top ya kumueka update katika mambo yake ya baraza ,ni aibu kumuonesha mtu picha kama hiyo na kumwambia hili ndilo baraza letu la kutunga sheria.
    Sijui kama wapo ambao wanajua kutumia hiyo laptop,ikiwa wapo basi ni vipofu kama ambao hawajui.
    Mshahara wa siku moja wa muakilishi anaweza kununua laptop lakini la haula sijui wameelekea wapi ikiwa hali yenyewe ya watunga sheria za nchi ni hivyo,kisha waziri anajibu masuali katika baraza sijui anatumia kigezo gani na huu ni ulimwengu wa computer ?
    Lakini tusisahau pesa ya kununua computer ataongeza mke mwengine mdogo wa kutembea nae katika gari kwani yule wa zamani hana shepu nzuri mbele ya watu.
    Sawa tu kisha maneno mengi ya kisiasa nyaufu ,kumbe mbele kiza.

  13. ndugu yangu ali , hizo laptop bora zisiwepo , manaake wengi wao watashindwa kuzitumia kwa kazi , itakuwa watu wanachezea gemu , nasema hivi kwa sababu utafanya SMZ ipate kisingizio cha ulaji kwa kuagizia laptop kwa kila mwakilishi , bora watumie hizo kalamu na karatasi.
    ndugu yetu Anna , muungano ukivunjwa sio maana yake kila mtanganyika au mzanzibari arudi kwao , kutakuwa na makubaliano kama vile ilivyo nchi za ulaya, mfaransa anaweza kuishi na kufanya kazi ujerumani na vivo hivyo kwa mjerumani kuishi ufaransa, kwa hio watu wote wanaowadanya watu kuwa muungano ukifa maana yake kila mtu arudi kwao si kweli , wazanzibari na watanganyika wengine wamechanganya damu , uhusiano wetu wa kindugu utabaki pale pale , lakini kila mtu atakuwa na serikali yake , tutashirikiana kwenye mambo yatayokubalika kama biashara , viwanda , kilimo , kazi n.k

  14. Heko wajumbe wa baraza la wawakilishi. Semeni musiogope huu muungano unatukereta. Tunataka Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili sio hewa. Wafanyakazi hawawajibiki ipasavyo kwa sababu nyingi ikiwemo mishahara midogo isiokidhi kwa kunulia hata chakula. Miundo mbinu finyu katika taasisi za serikali na uhaba wa vitendea kazi unapoteza ufanisi wa kazi. Ajira za kazi pamoja na nafasi za uongozi kutolewa kijomba jomba na wala sio kwa uwezo wa utendaji au sifa za mtendaji. Marekebisho makubwa yanahitajika lakini yote haya yamekaliwa na JINAMIZI LA MUUNGANO. Hivi leo Zanzibar haina umiliki yakinifu wa fedha zake mwenyewe ufanisi ni vigumu kapatikana. Sisi Wazanzibar hatuutaki MUUNGANANO TUNATAKA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR YENYE DOLA KAMILI. SIO JAMHURI JINA TU.

  15. Zanzibar yetu ni Nchi kamili leo tuomba mabalozi wadogo kwa sababu gani ? Sote tunalisimamia suala hili la kuthibitika Nchi yetu ni vigezo gani tutakavyo vitumia na kupelekea kupata balozi wadogo ,Kwa usahauri wangu sisi Zanzibar tuwatangazie viongozi wa nchi mbali mbali kwamaba katika kujenga mahusiano na nchi zao tunahitaji mabalozi na sisi tutapeleka mabalizi wa nchi yetu, Msingi wa kutekeleza jamabo hili ni kupata kiti chetu cha umoja wa Mataifa hivyo basi Wazanzibar tusimamie jambo hili kwa wingi wetu kuanzia viongozi ,hadi waongozwa letu tukilisimaia naamini tufikia pahala pazuri kwa uwezo wa MwenyeziMungu,pia ninawomba mawairi musiwe na woga wowote juu ya kudai nchi yenu na sisi tuko pamoja nanyi atakae ogopa kwa ajili ya kuchunga tonge yake ajue atakuwa mnafiki na hatokuwa pamoja na Wazanzibar wenye kuidai Jamhuri yao . WATUACHE TUPUMUE

  16. WAHESHIMIWA WAWAKILISHI NIVVYEMA KUONDOA WOGA KATIKA KUDAI HAKI, MAANA WOGA NI ADUI WA MAENDELEO,NINA HAKIKA WENGI MNAFAHAMU KUWA UAMSHO KWA SASA SIO TU KIKUNDI CHA WATU BALI NDIO KAULI ZA WAZANZIBARI,FANYENI UTAFITI WA KISOMI MTALIGUNDUA HILI. WAMO CCM WENGI TU NA CUF WENGI SANA,SASA HILI NIJAMBO LA KULICHUKULIA SIRIOUS NA KAMA MKILICHUKUA KISIASA KAMA MNAVOLICHUKUA MIMI NAONA IKO SIKU TUTAKUJAZINGANA ZANZIBAR MAANA HAKUNA KITU KIBAYA KULIKO WADHULUMIWA KUJA WAKAPATA MWAMKO.NYINYI VIONGOZI MUNA TABIA YA KUYACHUKULIA MAMBO KIURAHISI URAHISI KWA MFANO WAHESHIMIWA MNAKUMBUKA KUWA ZANZIBAR ILIFUTIWA MITIHANI MKAUNDA TUME MKAKUBALI KULIKUWA NA UDANGANYIFU,WENZETU BARA WATU WACHACHE TU WALIAMUA KWELI KUFUATILIA KWA SOMO MOJA TU NA IKABAINIKA KWELI NECTA WAMEWANYIMA WATU HAKI ZAO HASA WAISLAMU NA NDIPO KWA SOMO HILO LIKATOLEWA TENA MATOKEO KWA MARA YA PILI NA WAISLAMU WENGI TU WAKAWA WAMEFAULU, BE SERIOUS OUR DEAR LEADERS.

  17. Napenda kuchukua nafsi hiii kumpongeza mwakilishi wetu MHE;MANSOOR YUSSUF HIMIDI kwa kua yeye ndie kiongozi angalau anawakilisha wazanzibar ,pia nachukua nafasi hii kupinga kauli yake aliyosema ‘DUNIA YA LEO MATAIFA MENGI YANAUNGANA SIO TATIZO KWA MUUNGANO WETU ULIODUMU KWA MIAKA 48 KUVUNJIKA’ Ni kweli kwamba mataifa mengi duniani ynaungana lkn katika kuungana kwao sio kama TANZANIA mhe, hata kama wanaungana basi ni haki ya kila mwananchi wa nchi hio kuuzungumzia huo muungano na kupewa nafasi kubwa ya kusikilizwa lkn ss wazanzibar hamna nafasi kama hio mhe ilifika kipindi serikali ya TANZANIA ilitamka kuwa ‘watu wasizungumzie muungano “jee kweli kuna mashirikiano hpo vile vile hayo mataifa yanayoungana huwa ynfiki mda wanakaa kitako na wanaujadili muungano wao penye kasoro wanakerebisha lkn ss utawasikia viongozi tunakerebisha lkn huoni hata kimoj kinachokerbishwa ,kauli yetu mda umefika mhe,:kama waswahili walivyosema “za mwizi ni 40″ mhe zimefika .hata mukisema wazanzibar wasiiunge mkono uwaamuzi w kikundi au jamii ya watu katika kuvunja muungano hio tamaaa ondoa mhe kamwe hatutawasikiliza kwa hilo na hakuna hata mmoja kati ya wazanzibar takae kusikiliza mhe.hicho unachosema kuwa UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU ‘kwa sasa ujumbe huo ondoa akilini mwako mhe tunakupenda sana waznzibar lkn hapo sote hatutokuunga mkono mhe.ila tunaisubiri hio tume ya kusikiliza porojo la waznzibar ‘nimeiita hivyo kwa sababu mwazo yao yote yatatiwa kapuni” tutajua moja mhe endapo hatutasikilizwa mhe TUNAKUAHIDI KUWA ZANZIBAR HAKUTO KALIKA MHE kueni makini mhe TAHADHR-KABLA-L-ATHAR”NAKUTAKIA KAZI NJEMA .

Leave a comment