Watawala na haki ya maoni Zanzibar

Mkuu wa Mkoa ya Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi

Ujio wa mchakato wa katiba mpya na katazo la baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar kuzuia mikutano ya hadhara ya wananchi na Asasi zisizokuwa za kiserikali kuzungumzia suala zima la mchakato wa katiba ni mwendelezo wa kubana uhuru wa kujieleza. Tumewasikia Wakuu wa Mikoa ya Pemba,Dadi Faki Dadi wa Kaskazini na yule wa Kusini, Juma Kassim Tindwa wakiweka masharti magumu na urasimu usiokuwa wa lazima eti kama Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam(JUMIKI) mikutano yake haifai. Wakuu hao wa Mikoa wamekataza kabisa kufanyika kwa mikutano ya aina yoyote katika Mikoa yao.

 

Sababu zao hazikubaliki hata kidogo kwani ukiacha haki ya asili ya watu kukusanyika,lakini Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatoa haki kwa wananchi kukusanyika na kutoa mawazo yao kupitia katika makongamano,mihadhara,semina na siku hizi wengine wameamua kutoa mawazo kupitia mitandao ya kijamii.

Kabla ya wakuu hao wa Mikoa, SMZ kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohammed Abad Mohammed ilitoa tamko la kuelekeza iwapo kuna vikundi au Asas iza kiraia zinazotaka kufanya mikutano,makongamano kuhusu mchakato wa katiba mpya sharti wawasiliana na Tume ya Katiba kupata Kibali.

Sawa hakuna tatizo kufuata sheria,lakini mbona hatujasikia upande wa pili wa Muungano wakikimbushwa suala hilo? Demokrasia ya vyama vingi inatoa nafasi kwa kila mtu kushiriki katika kutoa maoni juu ya namna mambo anavyotaka yawe katika nchi yake.

Chini ya dhana ya demokrasia wananchi bila ya kuwa na uwakilishi wanaweza kupendekeza na kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, kijamii, kisheria, na kiuchumi,kama ilivyo sasa suala zima la kuwa na Katiba.

Kwa kupitia demokrasia,Zanzibar ikiwa ni sehemu ya nchi inayofuata misingi hiyo, wananchi wake wamepewa uwezo wa uamuzi wa mambo kwa kuwa uendeshaji wa Serikali utabaki mikononi mwa wananchi wenyewe hivyo, umma unaweza kuwa na hata uwezo wa kimahakama ingawa mara nyingi wananchi hupewa uwezo wa kutunga au kupitisha sheria tu.

Vipi Mkuu wa Mkoa anazuia wananchi kutoa maoni kupitia mikusanyiko yao ambayo inalindwa chini ya Katiba? Mpaka lini mtaendelea kuwa na hofu na wananchi wenu, kinaogopwa kitu gani?

Hivi Mkuu wa Mkoa angeruhusu mikutano hiyo kufanyika angekosa au kupungukiwa kitu gani? Kama kuna shaka pengine kunaweza kutokezea uvunjifu wa amani kwanini vyombo vyenye kujuku la kulinda amani na usalama visijipange kudhibiti hali hiyo?

Mbona pale Serikali inapotaka kufanya maandamano ya kuunga mkono maamuzi yake inawatumia wananchi wale wale ambao leo inawakataza wasikusanyike kwa visingizio kedekede kwamba kuna viashiria vya uvunjifu wa amani au subirini Tume mtoe maoni yenu, watu wanauliza kama Tume ingekuwa haipo watu wasingetoa maoni?

Tofauti na maandamano yanayopendwa na watawala, lakini pale baadhi ya raia wanapoamua nao kufanya mikutano au maandamano yao kudai hiki au kile, ama maandamano ya kuelezea hisia zao, ilidaiwa ni maandamano haramu na ikiwa waandamanaji watakaidi amri halali ya Serikali waliambulia vipigo!

Tunafahamu hofu ya baadhi ya Viongozi wa SMZ hawapendi kuwachukiza viongozi wenzao wa SMT hasa pale linapojitokeza suala la Muungano na zaidi wakati huu hapa Zanzibar wananchi walivyokuwa na shauku ya kutoa maoni yao namna wanavyotaka muundo wa Muungano uwe.

Hapa ndipo nongwa inapoanza,lakini kama watu wangekuwa wanafanya mikutano ile ambayo Serikali inataka ifanyike kwa kupendezwa nayo kusingekuwa na tatizo, kusingekuwepo na chembe ya kalipio sio Mkuu wa Wilaya au Mkoa.

Nimekwenda kwenye mikutano kadhaa ya Jumuiya za kidini ambayo mbali ya kutoa elimu ya uraia kuhusu mambo ya katiba,Muungano,lakini pia wahubiri wamekuwa wakitumia mikutano hiyo kutoa nasaha za kidini kwa waumini wao.

Tofauti na mikutano ya kisiasa ambayo huwa haihutubii wala kuhubiri namna ya kumpeleka mwanchi peponi au mbinguni. Huwa inahutubia sera za chama husika na yale yanayomuwajibikia mwanachama wao kuyatekeleza ili chama chao kipate kuingia madarakani.

Lakini cha kushangaza viongozi hawa wa Serikali wanapoitazama na kuitolea hukumu mikutano ya kiraia inaelekea huwa hawana wanachokiona wala kukisikia isipokuwa huwatazama watu waliopo na kuzichambua hisia zao.

Inaelekea wazi kwamba baadhi ya vigogo hawa wa SMZ na zaidi wale Wakuu wa Mikoa kule Pemba wanapofanya hivyo inaonesha kwamba nafsi zao huchukizwa wanapoona mikutano ya hadhara ya UAMSHO imehudhuria na umati wa Wazanzibari.

Hivi inakuwaje Kiongozi kwa nafasi yake Serikalini kama Mkuu wa Mkoa aende kwenye mkutano wa hadhara wa UAMSHO au wananchi wengine kwenye hadhira isiyokuwa ya kisiasa akaanza kuwatazama watu kwa vyama vyao vya kisiasa.

Bila shaka huo ndiyo mtazamo wake ambao unamsukuma kuwachukia tu wananchi wanaotoa fikra na mitazamo tofauti na yake, Anachukizwa kuona Wazanzibari kwa umoja wao wamo katika kutetea maslahi mapena ya nchi yao kupitia Katiba mpya. Hataki kuona wananchi wanatoa maoni yao kwenye mikitano ya hadhara japo ni haki yao kama raia.

Inashangaza sana kuona kwamba kama kuna watu wanajitokeza kutoa mawazo yao juu ya mchakato wa katiba au uhusiano uliopo kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanganyika au na Zanzibar bila ya kuzingatia ukweli wa hoja zao anachukuliwa kama mchochezi na msaliti!

Muungano umejadiliwa na kuzungumzwa na viongozi hata wa CCM wenyewe ambao wengine walielezea kwa kina umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika maamuzi yanayohusu mustakabali wa nchi yao.

Akihutubua miaka 23 ya kuzaliwa kwa CCM,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar wakati huo, Hassan Mussa Takrima alizungumzia pamoja na mengine matatizo ya Muungano.

Takrima alisema “La tano, Zanzibar bwana ilipochanganywa ikawa Muungano, wengine wanafikiri hazikuwa nchi, hizi zilikuwa nchi! Zanzibar ina chama chake wakati huo Afro Shiraz, na Tanganyika ilikuwa na chama chake TANU.

Akaendelea kusisitiza “Kiserikali ndiyo ukapatikana muungano wakati wa Mzee Karume, kichama tukapata chama wakati wa Mzee Jumbe. Lakini ni kwa ridhaa ya watu, tumeulizana humu hivi. Je, hili…. Au mmesahau, labda wale wengine waliokuwa wanafanya madudu tu yasiyofahamika hata utaratibu hayana”

Sio dhambi kwa Wazanzibari leo kuzungumzia mustakabali wao kuhusu Muungano wautakao kwani imedhihirika wazi kuwa nguvu za maamuzi katika nchi ya kidemokrasia ni za wananchi wenyewe.

Mpaka lini Wazanzibari watakubali kugawiwa kwa misingi ya itikadi ya kisiasa,kieneo. Kwa nini viongozi wa kisiasa kama walivyo wale wa kidini badala ya kuweka maslahi ya Zanzibar kwanza, wao wanaweka mbele maslahi binafsi?

Ni jambo la busara kwa sasa Wazanzibari kuwa kendelea kuwa wamoja kwani huu si muda wa kupingana wenyewe kwa wenyewe yafaa kutambuwa kuwa fursa iliyopatikana ya kuandika katiba mpya ni ya kipekee katika historia ya nchi yetu, hivyo,mchezo wenu ndio mauti yetu.

Ni wakati wa kutazama maslahi ya Zanzíbar kwanza na mustakabali wa Wanzanizbari kwa ujumla wao, uwe Mkuu wa Mkoa,Wilaya,Sheha,Waziri,Mwanasiasa,wanazuoni ni lazima sasa tuungane kutetea maslahi ya Zanzíbar yetu.

10 responses to “Watawala na haki ya maoni Zanzibar

  1. Kelele za mlango.
    Tulikosa kukata minyororo ya kidhulma ya Tanganyika 1984 wakati kiongozi wa juu Alhaj Aboud Mwinyi mwenyewe alikuwa hautaki muungano, naapa hattaipita tena fursa kami ile. Hasa kwa sasa vingozi wa juu wa Zanzibar wanachaguliwa na Mabwana zetu Tanganyika.
    Mapambano ya Alhaj Jumbe yalikuwa magumu na mazito kwa sababu alijiandaa vyema. Nyerere alibanwa kila kona na alikuwa hajui pakutokea. Ndipo Nyerere alipoamua kuwatumia vibaraka wachache wa Zanzibar kumpinga Jumbe. Kiongozi Mkuu alietumiwa kumpinga Jumbe na hatiamae kumungusha na baadae kuzadiwa Waziri Kiongozi alikuwa Maalim Seif Sharif Hamad. Ilifika hadi Maalim Seif akawaita WAHAINI akina Wolfgang Durado kwa msimamo wao wa kuitetea Zanzibar na kuupinga muungano. Leo nawashangaa watu kwa kujipa matuamini huku wakijua kuwa Maalim Seif huyuhuyu si Waziri Kingozi bali ni Makamo wa Rais .

    Madhali bado tuna Wazanzibari waliokwenywe nyadhifa kubwa serikalini kama akina Maalim Seif, wazanzibari tusahau tena tusahau kama itatokea siku Zanzibar itakuwa huru na hadhi ya utaifa wake kurudia.

    Maneno yangu haya mtayakumbuka hasa kwa wale watakayoyabeza wakati huu. Tumechelewa na tumelewesha na kasumba za akina Maalim Seif kumbe huku anajali maslahi na tumbo lake tu.

  2. Sisi hatuutaki muungano lakini wakubwa ndio wanaonufaika na maslahi yao binafsi. Hili ndio lililopelekea hao wakuu wa Pemba akina Tindwa na wenzake kupiga marufuku harakati za UAMSHO kisiwani Pemba. Hawa wanatengenezi ugali wao tu lakini hawana uchungu wa Zanzibar. Huu umoja na mshikamano wa Wazanzibar ulioletwa na UAMSHO kwa kusaidiwa na nguvu za ALLAH ni tishio kwao. LAKINI SISI TUKO IMARA NA WALA HATURUDI NYUMA MUUNGANO HATUUTAKI NA TUTASHINDA TU KWA NGUVU ZA MWENYENZI MUNGU NA UMOJA WETU. Sisi tunajuwa muna dola lakini kaeni mukijuwa sisi tu dola ya Mwenyezi Mungu na nyinyi hamuna uwezo wa kumzidi Mwenyeenzi Mungu. SISI TUKO IMARA NA INSHALLAH TUTASHINDA KWA UWEZO WA ALLAH. MUUNGANO HATUUTAKI HATUUKIIIÍÍIIÍIÌ

    • mie nime mzanzibar wa kizazi kipya hii nchi katu sio ya viongozi kwa sasa tumeshatoka gizani hatuwezi kurudi tukadhani kivuli chetu ndo kila kitu,kwa sasa mwanga tumeshauona hatuwezi kua na fikra za 1984,kwanza nilikua sijazaliwa hivyo nguvu zangu zote ni kuiona zanzibar inaninufaisha nikiwa huru ndani ya nchi kamili ya zanzibar

  3. nd dadi na wengineo wenye fikra kama hizo sina zaidi ila ku…………yooooo . nenda uka……………..we ., ms………e mkubwa , uso kama…….so………..

  4. HUU NI MTEGO TU SIO JAMBO JIPYA
    Assalam alkm,
    Kafiri akikuona umekwama hukuzidishia kwamo jengine sahaba wa Mtume saw aliesusiwa kusemezwa kwa kukhalifu amri ya kwenda vitani makafiri walimfata wamritadishe aache subra katika mda ule walitaka wamuoengezee kosa jengine, wazanzibabar kuingia katika uhangiaja wa katiba ni kuongeza idadi ya matatizo.
    Kwanza nawaasa wale ndugu zangu ambao bugudha yao huwazidi wakashindwa kujizuia wakaandika matusi ya dhahiri nawaomba kwa nasaha ya dini yetu (uislam) asitutelezeshu Iblisi tukamuasi Allah tupigane hali ya kuwa ni waislamu tusitoke katika amri za Allah sw na (kwa hili sikusudii tusiwaseme watu uovu wao hata, tuwaseme ili wajirekebishe au tujue vyema kuwa huwa hawafanyi makosa kwa bahati mbaya bali kwa makusudio hasa ili tujue namna ya kuamilina nao)
    Kisha niwapongeze wazanzibar wote (walioamka) kwa muamko wetu wa kuichukia kufru hii iliofanywa na wazee wetu kwa bahati mbaya, nawapongeza kwa kuichukia lakini pia kudhamiria kuiondoa na vp tuvumilie madhila haya yasiokoma na hali tu wazee waliteleza katika kutuingiza. Kitabu chetu (Qur-an) inawataja kwa kuwafedhehi wanaojifunga na misimamo ya urithi ya wazee wao inapokuwa misimamo (Mibovu) …(ee wanafata) ijapokuwa wazee wao hawakujua walifanyalo! (madhara yake) …
    Sisi hatufai kuwa hivyo na ndio maana sasa tuko namna hii tunasema haswa muungano huu ni wa KIKAFIRI uliochunga toka mwa mwanzoni mpaka mwishoni kwake (Inshaallah iwe karibu mno) maslahi ya kafiri. Kwa hivyo kuukataa sio tu ni haki ila ni WAJIBU sisi hatufungiki na maneno ya kipuuzi yaliotungwa na walevi (mda mwingi) tunayo Dini yetu na Qur-an pamoja na Sunnah ndio huchipukia misimamo yetu, hatutaki kuburutwa kama watu wasiokuwa na pakushika nyinyi viongozi wetu kwa kuwa ni waislamu tungetarajia kuwa mngetusaida na tungekuwa na misimamo sawa DHAHIRI SHAHIRI leo mnatuacha na kutuzushia eti sisi tutavunja amani. Hivi mlipokuwa mnatutumia kama ngazi za kufikia nyadhifa zenu tulikuwaje (malaika na sasa ni mabilisi sisi) sio ndio sisi tunatoka mikutanoni na nyimbo za vikundi yvenu vya dhulma (vyama vyenu) wengine tunatoka mnazimmoja (Unguja) na wengine mkutano wetu ulikuwa kibanda maiti nasi wakibanda maiti tunazizua daladala zinazotoka M/mmoja na zimepakia ndugu zetu maskini tunawapiga mawe, magongo wengine tunawapokonya nguo hadi tunawaweka uchi, kama haya madogo hatukupoteza uhai wa ndugu zetu shumba, darajabovu, mtendeni, micheweni nk kwa sababu zenu na kwa maslahi yenu ile ilikuwa ni AMANI vyama hivi haviendelezi bado mikutano yao au vimefutiwa usajili?
    Lakini kila wanapotokeza wenzetu wakazungumza kinyume na matakwa yenu japo maneno ya MUUMBA mnazua kuwa wanavunja amani sheikh Kurwa aliekataza kufru za utalii alikuwa akivunja amani lakini jambo hili alilifahamu hata Karume Baba wala hamkumuenzi kwa hili, wakaja simba wa Mungu kuwachapa tu vibakora watembea utupu ili kuwatisha sio kuwajeruhi mkazua watavunja amani leo mmekataza hata watoto wasifundishwe kwa vibakora na kumuandalia atakaekhalifu amri hii adhabu ya kali, mmejitia pambani mnaishiriki kufru mnampinga hata Allah na Mtume wake (saw) hivi ndio kutafuta amani? Nyinyi mmefikia kikomo cha khiana mnampinga kimisimamo rais wa pili wa Zanzibar aliepinga muungano kidhahiri mpaka akatunga na vitabu vya kuonesha uovu wake. Kama haitoshi hamjui viongozi kuwa tiba ya makosa ni kujirekekebisha kila uchwao mnadangaya kwa namna nyengine mpaka tuwatukane?
    Sasa mnapita mkidanganyia eti katiba mpya itaondoa matatizo tulionayo Zanzibar hivi ni kweli mnapotamka maneno haya mnakuwa hamko hadhiri au huku mnastaghafiru kimyakimya, katiba ambayo kwanza imekataa maoni yatakayotolewa yakihusisha DINI, pili katiba itakayotupilia mbali maoni yoyote yatakayojadili Muungano, tatu katiba ambayo haitosikiliza maoni kuhusiana na nafasi ya urais. Katiba hii ndio sasa mnachomeka watu kwa siri sehemu mbalimbali hata katika hii mitandao (hata huu)kuhimiza wazanzibar tutoe maoni yatatusaidia kwa mtindo upi nasi kwetu DINI ndio cha kwanza nanyi hamuitaki katiba hii ya kikafiri itatusaidia vp katika sula la muungano hali ya kuwa Muungano huu ni jambo TUKUFU kwenu halifai kujadiliwa na sisi. Alhamdulillah sisi wazanzibari ni waislamu lakini lau visiwa hivi vingekuwa vya makafiri watupu basi pia KATIBA hii isingekuwa na faida kwao kulingana na kipengele cha kutolujadili muungano huu uliooza, jee sisi Waislamu mnatukhadaa Allah sw atawarejeshea kwenu khadaa hizi kwani hata mmoja wenu akiandika katika zanzibar yetu au mumlete ahutubie katika mihadhara yetu haswa au radio zetu basi tutambaini kuwa katumwa na hatutamfuata akatutia kitanzini kisha motoni.
    SISI HATUTAKI TENA KATIBA MPYA YA KIKAFIRI bali isio na hata punje ya hisia ya uwanadamu mnatutega tushiriki mfanye kufru zenu na mseme tulikubaliana KIKATIBA. tunataka zanzibar yenye dini yake.

  5. Ujumbe huu hasa nakusudia umfike Mheshimiwa Dadii ambaye ni wa kulaamiwa kwa kuruhusu Mkoa wa Kaskazini hasa Micheweni iwe maisha ni masikini. Jamaa yangu huyu ambaye anaelimu ya dini kidogo na mzawa wa mjini Wingwi nilifikiri ataumiza kichwa kuibadili Wilaya ya Micheweni ili watu wa Kwa Shaame Mata, waamini kuwa inawezekana kuitumia Ardhi waliyonayo kujitosheleza kwa chakula kama ilivyokuwa siku za nyuma ambapo watu wa Shinene walisafiri kuja na wakirudi wakabeba vichwani mtama, uwele na sanli na mambo mengine. Ndugu yangu huyu kuanza kukataza mikutano ambayo ni msingi wa watu kuzungumza njia mbadala na kupeana nasaha za namna ya kuishi amekwenda mbali mno.

    Jamaa yangu Dadi ivi huoni watu kuwa kila siku kwenda Shinene na Puunda kuchukuwa chakula nkazi? Mie nakulaumu vyo kuwa hweweza ata kuongoza wavyelewo, kakizo, dadezo wakajitosheleza kwa chakula- wakawa hawahangaiki kwa kisabeho, vishuka au vijio- Ningekuwa mimi kazi yangu ya kwanza nigehakikisha hili linafanyika tena kwa ufanisi mkubwa. kabla sija fanya mambo ya kuivunja katiba iliyoniweka Madarakani.

    Jamaa yangu Dadi wakati wa kabla ya SUK tuliona ulivyowatumia Masheha has Wa Fundo na Wa Kambini kuzuia vijana kupata vitambulisho wa ukaazi. Tunakumbuka Viwanja vya Skuli ya Kambini vilipogeuzwa uwanja wa Mapambano huku wewe ukiongoza Vikosi vya SMZ kukandamiza haki za Watu za kuzaliwa. Kwa kuwa haya yamepita na Watu kusameheana ni bora usiwatonese vidonda.

    Jamaa yangu Dadi Wilaya yetu ya Micheweni injaa rasilimali – kuna watu, misitu, ardhi na bahari ela indoda kwa umasikini. Kazi twavyaliana tuu. Wewe Dadi ungefanya kazi ya kuwaelekeza jamaa zetu namna bora ya kuzaa na kuzitumia rasilimali zilizopo ili maisha yao yawe bora. Maisha yao kuendelea kuwa ya ndege kuamka mashariki wakiuchuma magharibi na kulala mashariki na kuendelea kwa dhari ni aibu kwako na hustahili kuijtokeza mbele ya watu kutaka mambo makubwa.

    Hili la kuwa umepiga marufuku mihadhara inaonesha ni kiasi gani umbali na watu unaowangoza. Mihadhara hii sehemu kubwa inamtaja Mungu ambaye kwa kusahauliwa kwakwe Zanzibar imengia katika uoza wa Rushwa na mabaya mengine. Mihadhara hii inahimiza uadilifu ambao Serikali unayoiyongoza haina.Mihadhara hii inahimiza umoja ambao miongoni mwenu mnaupinga. Mihadhara hii inaleta mawazo mbadala ambayo pia ni muhimu kwa kuwa hakuna jamii inayoendelea kwa kutumia falsafa ya aina moja tuu.

    Kama haya yote si mema basi jamaa yangu kunchemsa – Kaa Wingi ya Pwana au Njuguni au Mapofu ucheze bao ukisafiri utako – siasa huiwezi !

  6. DADI LAZIMA AFANYE KILA ANALOELEKEZWA NA MABOSI WAKE KWANI ANAJUA FIKA KATIKA NCHI AMBAYO UONGOZI HHUA UNATOLEWA KWA SIFA YEYE HAFAI. AMEENDELEA KUBAKI HAPO KWA KIASI KIKUBWA KUKANDAMIZA WATU NA HAKI ZAO.AMEDIRIKI KUWANYANG’ANYA MASHAMBA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI ILI AWAPE WAZUNGU KWA KUMFURAHISHA BWANA WAKE. DHULMA HAIDUMU KUMBUKA SANA WEWE DADI FAKI. IKO SIKU VYOTE HIVYO UTAVIACHA HAPAHAPA. YUKO WAPI LEO KOMANDOO NA WENZAKE WALIOKUA WAKIVUNJA MAJUMBA YA WATU KWA JEURI, KIBRI NA KEEDI? NA WEWE IKO SIKU UTATAKA UWAONE ULIOWADHULUMU HAKI ZAO UWAOMBE MSAMAHA LAKINI WAPI. NA HIYO SIKU NAONA HAIKO TENA MBALI MAANA SASA UNAINGILIA MPAKA KATIKA ANGA ZA DINI. HAKIKA DADA UMEKWISHA. WAZANZIBARI HUU SASA SIO MUDA WA KUTUPIANA LAWAMU BALI NI WA KUUNGANA NA KUTAFUTA NJIA LIPI TUFANYE KWANI UKIONA HAWA JAMAA WANAEKA VIKWAZO VINGI UJUE LIMEWAPATA PABAYA NA KWA SASA HAKUNA KURUDI NYUMA. MUUNGANO HUU WA KITAPELI AMBAO UNAWANUFAISHA VIONGOZI TU NA FAMILIA ZAO HATUUTAKI. DADI ANAUTETEA KWA SABABU ANA KITUO CHA MAFUTA MOROGORO ALICHOKIJENGA KWA FEDHA YA WIZI WA VIWANJA NA MASHAMBA YA SERIKALI ALIVYOVIUZA PALE WETE. HIVI KWA NINI TUME YA OMAR ALI SHEHE HAIMCHUNGUZI HUYU DADI?

  7. Mkombe ndugu yangu hebu tueleze msimamo wako ndani ya nafsi yako Unautaka Muungano huu haramu au huutaki. Kwani huu sio wakati wa kutupiana lawama. Makosa yalianza kufanywa tokea na wazee wetu hapo awali kupigania uhuru halafu wakauuza kwa bei poa. Na hawa wa sasa wanamalizia hivyo vilivyobakia kama bahari, mafuta, nk. Inavyoonekana Shkh una chuki binafsi na nadhani hii barza sio pahala pake. Wazanzibari hivi sasa kazi yetu ni moja tu kukabiliana na adui huyu MUUNGANO ambao unaifanya Zanzibar kupoteza kila kilicho chake mpaka sasa tumepoteza utamaduni, silka, imani na ikiwa MUUNGANO huu utaendelea kuna hatari ya kupoteza hata dini. Angalia ajira siku hizi kama una jina la kiislamu inakua tabu kupata. Pia angalia yalipotiwa moto mabanda Kiwengwa Balozi Seif Idi alivyokua mkali kisa mabanda ya watu wanaoupiga vita Uislamu ndani ya nchi ya Waislamu yametiwa moto. Alifika hadi kutaka watu wale wapewe hati miliki za ardhi kinyume na sheria. Ni mara ngapi maafa kama yale yanatokea na Balozi hawi mkali? Watu kwa uzembe tu wamesababisha vifo vya zaidi ya watu 2000 kwenye Spice Islander hatukumsikia hata siku moja Balozi akiwa mkali zaidi ya kupokea michango ambayo hadi leo ameshindwa kutoa mahesabu ya kiasi kilichokusanywa na kutumika hadharani. Iko siku ajue CAG atzifanyia ukaguzi hesabu hizo kwani hakuna alie juu ya sheria.

Leave a reply to Mzanzibari halisi Cancel reply