Serikali yadhamiria kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kombe la ushindi la “Jihadi Cup” kwa kepteni wa timu ya Sayari iliyoibuka kidedea kwenye ligi hiyo iliyozishirikisha timu 9 za daraja la pili na tatu kwa wilaya ya mjini.

Mashindano ya soka katika Jimbo la Magogoni yajulikanayo kwa jina la “Jihadi Cup”, yalifikia kilele chake jana kwa kuzikutanisha timu za Sayari na Taifa Jipya za jimbo hilo ambapo timu ya Sayari iliibuka kidedea. Mtanange huo uliopigwa katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya siasa na chama cha soka Zanzibar ZFA akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamojan na Mwakilishi wa Jimbo hilo ambaye kabla ya uteuzi wa hivi karibuni uliompeleka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo.

Timu ya Sayari iliibuka mshindi wa kombe hilo la Jihadi na kukabidhiwa pamoja na mambo mengine Kombe na shilingi laki nne taslim, baada ya kumshinda mpinzani wake timu ya Taifa Jipya kwa mikwaju ya penalty.

Dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa timu hizo kuwa na nguvu sawa ya kufungana na (mabao 2-2) na ndipo sheria ya kupiana mikwaju ilipochukua nafasi yake ambapo Sayari ilishinda mikwaju yote 5 dhidi ya Taifa Jipya iliyopoteza mkwaju mmoja na mwisho kuugomea ikijua kuwa tayari imeshashindwa.

Akizungumza baada ya mtanange huo uliomalizika wakati wa magharibi na kuonekana kupata mashabiki wengi na kuyapiku hata mapambano ya ligi kuu ya Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alisema Serikali ya Awamu ya Saba imedhamiria kurejesha hadhi ya soka Zanzibar.

Amesema mashindano hayo yameonakana kupata mafanikio makubwa hasa ikizingatiwa kuwa timu zilikuwa na nidhamu ya hali ya juu huku zikiwaunganisha vijana bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Ametoa changamoto kwa timu za Zanzibar kudhamiria kuwa washindi wakati wanapoingia kwenye mashindano mbali mbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa na kuachana na mtazamo finyu wa kuingia kwenye mashindano hayo kama washiriki au wasindikizaji.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni ambaye ndiye mlengwa wa mashindano hayo Mheshimiwa Abdillahi Jihadi Hassan alisema lengo la mashindano hayo yaliyozishirikisha timu 9 za daraja la pili na tatu katika Wilaya ya Mjini ni kuibuwa vipaji vya vijana kwenye soka na hatimaye kuviendeleza.

Alisema michezo ni ajira na afya, hivyo vijana hawanabudi kushiriki katika michezo mbali mbali hasa wa soka ili kujijinga kiafya na kujiandalia mazingira ya ajira.

Katika risala ya kamati ya michezo hiyo ya “Jihadi Cup” iliyosomwa na afisa habari wake Ali Cheupe, walisifu mafanikio yaliyopatikana na kumpongeza Waziri Jihadi kwa jitihada zake za kutafuta wadhamini wa ligi kuu ya Zanzibar alizozichukua ambazo zimezaa matunda kwa kampuni ya vinywaji ya “Grand Malti” kukubali kuidhamini ligi hiyo.

Wamewashauri viongozi wa kitaifa na soka kutobeza udhamini huo ambao ni muhimu katika kuendeleza soka la Zanzibar.

Advertisements

7 responses to “Serikali yadhamiria kurejesha hadhi ya michezo Zanzibar

 1. huu ni wakati wa kupigania uhuru wa znz na sio mipira , msilewe na madaraka, kumbukeni majukumu yenu kwa raia na nchi , haipendezi wala haifurahishi.

 2. wito kwa wananchi wote wenye hekima na maarifa kugomea kwenda kwenye mipira , haileti tija wala maendeleo kwa muda huu mpaka muungano uvunjike, tujenge nchi upya , halafu ndio tuangalie michezo wakati huduma za jamii zimetoshelezwa. WANANCHI WOTE WITO KUTOKWENDA KUANGALIA MPIRA WA LIGI YOYOTE.

 3. CUF Niwasaliti wa ZNZ na ‘JIHADI CUP’ ni jina tu, kama kweli ni JIHAD inakuwaje mnaunga mkono ufadhili wa Kampuni la pombe?

  Au jihadi ya tumboo?

  Mimi ndio maana sitaki kuwa CUF wala CCM maana lengo ni matumbo tu husasan ya wakubwa, tena CCM ndio hatari zaidi. Leo ingekuwa CUF bado hawajaingia kwenye mduara (SMZ) bila shaka ungemsikia Waziri Jihadi na Maalif Seif wakibweka na wakiuponda ufadhili huu mal’uuni. Lakini wapiii! Funika kombe mwanaharamu apite, ndio kwanza wanapongezana kwa kuutafuta na wanahimizana wasiupoteze. Kiufupi balaa hili limeletwa na CUF, maana Waziri wa Uvuvi alikuwa katika wizara ya habari na michezo na akautafuta mtihani huu mpaka kaupata katuingiza mtegoni, tusitegemee kutetewa na CUF wala CCM daima hawa sasa lao moja, nalo ni mlo kwa namna yoyote.

  Kama wanasiasa hamkuitetea ZNZ leo basi Jumuiya na Taasisi za Kiislamu tunao tunaimalizia kazi padooogo palipobakia. Lakini tukimaliza tusije tukamuone Fisi yoyote anafuata mikono eti ikidondoka aifaidi, tutamkomesha mtu.

  Liondosheni Kampuni la wafalme wetu Watanganyika {TBL} hapa Kijiji ZANZIBAR.

  MUUNGANO HATUUTAKI

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.
  Dawn in Zanzibar.

  Nawasilisha najua huenda nitakatukanwa na wana….

  SERELLY.

 4. Maalim Seif hatuamini kuwa hii inawezekana. Serikali yako na hasa baadhi ya Mawaziri kutoka CUF (mawasilano kw mfano, wanaonesha kuwa hawawezi kuongoza. Michezo ni muhimu sana lakini hii haiwezekani kwa kuwa bado Serikali imejaa rushwa na wizi na hakuna jasisri wa kuindosha. Hospital ya Mnazi moja watu wanafanya vipimo bila kupewa risiti. Kitengo cha Mapinduzi Kongwe ambako watu wanaotaka kuajiriwa na kusoma hupita unaweza kupatana bei ya kupigiwa muhuri. Mtu moja hivi karibu alijaziwa katika maabara ya Mnazi moja kama amefanya uchunguzi wa stool na yuko sawa kumbe si kweli alijaziwa for convenience ili jamaa akusanyae mapato akusanye kwa chap chap! Maalim hamuwezi hili bora waachieno UAMSHO wataongoza na watawafanyia watu uadilfu!

 5. Wakati umefika sisi hatunahaja ya mpira wala kombe. Mpira hautufai umeingia pombe. Si hatuutaki muungano.

 6. Kwangu muhimu katika picha hiyo ni kuwepo Ali Karume….kuna mengi ya kusema katika hilo na picha ilikuwa itambue kuwepo kwake.

 7. “Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alisema Serikali ya Awamu ya Saba imedhamiria kurejesha hadhi ya soka Zanzibar.” Sisi tunataka kurejesha hadhi ya serikali ya Zanzibar sio soka.
  Kuwepo kwa Ali Karume kunamaanisha kuwa urafiki wa karibu baina ya Maalim Seif na ukoo wa Karume. Kumbuka kuwa ukoo huu hivi karibuni ndio ulioonekana kuifisidi Zanzibar.

  Hatari, mti na macho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s