Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI

Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR.

KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA KAULI YA MHE. MOHAMED ABOUD YENYE NIA YA KUVUNJA NA KUVURUGA AMANI YA NCHI ILIYOTOKA JANA TAREHE 2/5/2012 ZBC.

03/05/2012

NDUGU WAANDISHI WA HABARI

ASSALAMA ALAYKUM WARAHMATU -LLAH WABARAKATU

Awali nachukua fursa hii kumshukuru Allah subhana wataala muumba mbingu na ardhi mwenye kumpa Ufalme amtakae na kumnyima amtakae pia tunamtakia rehma kipenzi cha umma Mtume wetu Muhammada (S.A.W) baada ya shukurani hizo tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Rais wetu mpenzi Dr. Ali Mohammed Shein kwa uongozi wake imara uliojaa uadilifu, hekima pamoja na serikali yetu ya Kitaifa na usimamizi wake madhubuti wa kuhakikisha anatandika zulia la demokrasia na kuhubiri amani, umoja na mshikamano.

Ndugu waandishi wa habari.

Kwa kweli tumesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Mohammed Aboud aliyoitoa jana kwenye vyombo vya habari yenye lengo la kuzuia mihadhara inayoendeshwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa kusimamiwa na Jumuiya ya Uamsho JUMIKI kwa kisingizio cha sheria No. 8 ya mabadiliko ya Katiba kwa maana hiyo tunapenda tutoe ufafanuzi juu ya sheria hiyo katika ibara zake zinazohusu suala la utoaji elimu. Ibara ya 17:8 “Mtu au asasi yoyote itakayotaka kuendesha programu ya kutoa elimu juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo sharti, iwe imesajiliwa ……… na itawajibika kueleza kwa tume chanzo cha fedha ya kuendesha programu hiyo” ibara ya 21:2C “Mtu yeyote atakaeendesha programu ya elimu… kinyume na masharti ya sheria hii atakuwa ametenda kosa”

Ndugu waandishi wa habari

Napenda mzingatie kuwa:

1. programu ya elimu inayomtia mtu hatiani kwa mujibu wa sheria hiyo ni elimu inayohusu sheria ya mabadiliko ya Katiba.

2. Masharti yaliyoekwa ni kuwa Jumuiya imesajiliwa Serikalini.

3. Inalazimika kutoa taarifa tu na kueleza chanzo cha fedha sio kutaka ruhusa au kuomba kibali.

Kwa bahati nzuri Jumuiya za Kiislamu imeliona hilo mapema na tayari

programu za elimu juu ya mabadiliko ya Katiba zimemaliza kwa muda

mrefu kwa sasa hivi Jumuiya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuweza

kujua sheria za nchi na Katiba yao jambo ambalo kwa muda mrefu Serikali

haikuwa na utaratibu endelevu wa kuelimisha raia zake na hiyo ndio kazi

inayoifanya Jumuiya kuisaidia Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa sambamba

na kutoa elimu ya Kiislamu kufunza maadili mema, kudumisha amani,

umoja, utulivu na mshikamano kwa wazanzibari wote bila kujali tofauti zao

za kidini, kisiasa, rangi na ukabila pamoja na kusisitiza umuhimu wa kudai haki zao na uhuru wa maoni pamoja na kulinda mali ya umma na kutii Katiba ya Zanzibar na sheria za nchi. Ibara ya 23:1 ya Katiba ya Zanzíbar inasema “kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Zanzíbar” 23:3 inasema “watu wotewote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzíbar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu… kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya badea ya Taifa lao”.

Ndugu waandishi wa habari.

Jumuiya ya Uamsho inaendesha mihadhara kwa miaka mingi kuzingatia Katiba yake pamoja na kufuata Katiba ya Zanzíbar inayotoa uhuru wa maoni kutipia ibara ya 18 inayosema “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”.

Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.

Jumuiya za Kiislamu zinawatahadharisha watu hao na kuwataka mara moja waache kuhubiri uchochezi na uvunjifu wa amani na kuwakumbusha kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria ibara ya 12 ya Katiba inasema “ Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote” vile vile wajue hizi ni zama za uwazi haki na sheria hivyo tunawasihi wasijisahau wakavitumia vyeo na ngazi za uongozi kwa maslahi ya wachache sana wasioitakia mema Zanzíbar watambue kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Zanzíbar na sheria za nchi rejea ibara ya 14,16,23 ya Katiba ya Zanzíbar.

Pia Jumuiya zinapenda kuchukua fursa hii kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 17:8 na 21:2C kwa kuzingatia uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar. Pia kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo hiyo No.8 ya mabadiliko ya Katiba kinachoipa Tume uhuru na mamlaka kamili ambayo Mhe. Mohamed Aboud anaonekana kuvikiuka na kuingilia kazi za tume kwani Katibu Mkuu wa Tume hakuwa na taarifa yoyote wakati Jumuiya zinawasiliana nae akiwa bado ndio kwanza anataka kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao.

Imani yetu huu ndio Mwanzo wa uvunjifu wa sheria hiyo. Tunapenda kumkumbusha Mhe. Mohamed Aboud maneno ya Rais Dr. Shein aliwataka wananchi wa Zanzíbar wanaishi kwa umoja na mshikamano inapaswa hitilafu ziondolewe ili Wazanzibar waishi vizuri kwa amani na utulivu na kamwe asitokee mtu akiwa ana lengo la kuivunja amani iliyopo rejea gazeti la Zanzíbar leo lenye kichwa cha maneno TUSICHAFUE AMANI toleo No 3743.

Ndugu waandishi wa habari .

Tunapenda kumalizia taarifa hii kwa kutoa shukurani zetu za dhati kwa jeshi la polisi kusimama imara katika kudumisha amani ya nchi na kutokubali kuburuzwa na hao wachache wasioitakia mema nchi yetu ya Zanzíbar.

Ahsanteni sana.

Nakla:

Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,

Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar,

Waziri wa Katiba,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais,

Jeshi la Polisi,

Idara ya Mufti Zanzibar ,

 

19 responses to “Serikali imekwenda mchomo- JUMIKI

  1. Hee ! Kazi ipo baina ya wenye kutetea haki [Jumiki] na wenye kutetea dhulma kina Mohammed Aboud, Balozi Idi na wenziwao. Inshaallah haki itasimama.

    • A/allaykum Ndugu zangu Wazanzibar kesho ni ijumaa kwa hio ndio siku ya Kumshtakia Allah kwa dua kubwa kubwa za hawa wanafiki na wababaishaji walio kumbatia Dunia na wakaasha uadilifu.

  2. Kwanza napenda kukumbasha kwamba hawa sio viongozi wa UAMSHO tu bali ni pamoja na taasisi nyengine mbali mbali za Dini ikiwemo JUMAZA, waandishi tunaomba mtumie phrase ya “JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR” ili kuonesha sura halisi ya UMOJA WETU.

    Alhamdulillah huu ndio msimamo wetu kama walivyoutanguliza KAKA zetu As-haabul-kahfi, Nabii Mussa kwa Firaun na Mtume {s.w} na Maswahaba wake {r.a} kwa Makurayshi. Na mwisho waliipata Nusra ya Allah {s.w}
    Ndugu zangu tushikamane kikweli kweli mpaka tuupate uhuru wetu mahbuub. MASHEIKH tuko pamoja mpaka kieleweke.

    Moh’d (MADUDU) Aboud angalia umekuja Duniani kutafuta radhi za Allah {s.w} na sio kugombana na Masheikh kwa ajili ya tumbo lako eheee! Madrasa kama umesoma hukusomeshwa na polisi isipokuwa umesomesha na Masheikh na ulikuwa ukiwapa tabu sana maana ni kichwa ngumu hufahamu kirahisi hata muungano umeshindwa kuyaona madhara yake- maana ninashaka kama umefika angalau Juzuu ya pili, wenzio hao wanaokutuma washaona mbaaali wewe mwenzangu mie ndio unajifanya shehaaata haya mkataa la Mussa hupata la Firauni, endelea bosi masharubu kugombana na wenye NDEVU langu jichoo, na kusudi haina pole. Kocha wenu Komandoo yuko wapi leo ? Leo hii ukimtoa barabarani na ukamwambia tayari tushafika chooni anza kukojoa bila shaka atakojoa tu, Jee! Mbona leo hatukuoneni mkitembea na yeye kwenye mikutano,semina na hafla zenu mbali mbali ? Wapiii ! Mmemtupaa na kumsaliti ili mtanuwe au vipi ? Basi na wewe naona huko mbali kukumbana na kipigo cha Allah (s.w). Nani asiyejua kuwa Masheikh hawa hapa Zanzibar ndio wenye kujitahidi kilillah katika kuujenga Umma wa kiislamu Zanzibar ukilinganisha na kina-Juma Faki, Soraga, Khamisi Haji n.k (Allah ajaalie watubie) ambao wao kijio ndio main first and last target {shabaha kuu ya mwanzo na ya mwisho} yao bwana.
    Chunga usigombane na waja wa Allah utaumbuka, mwambie na Ustadh wako Seif Ally Idd huu upepo mwengi sio ule wa CUF na CCM 2001.

    JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA
    vyama na njaa zenu baadae.
    Nawasilisha.
    SERELLY.

  3. Allah atajaalia kila la kheir katika kuelekea kudai utaifa wa Zanzibar, kila kwenye uzito faraja itakuwq mbeleni…

  4. Inabidi hwa kina Mohammed Aboud tuwashitaki kwa Mola Mtukufu, wanahitaji kusimamiwa SALA za usiku kisha tumuachie Mola yeye ajua nia ya muheshimiwa huyu na yeye Mola Jallaa wa Alaa ajua jinsi gani ya kumuadhibu, lakini tumpeni muda kidogo tuone huenda akajirekebisha tabia yake hii potofu, pia akumbuke mafirauna wengi wamepita huko nyuma wako wapi hivi sasa, kumbuka ujabari wako huo utaishia kwenye kaburi ambalo kama ukioneshwa hayo utakayukumbana nayo basi ungehamia msikitini kuomba maghfira kwa mola wako juu ya makontena ya mijidhambi uliyonayo.

  5. Asalamu Alaykum. Nina heshima kubwa kukaribisha maoni ya kila mchangiaji na naahidi kuheshimu mawazo hayo. Hata hivyo, kwa ajili ya kulinda mila na desturi adhimu za Kizanzibari, sitachapisha maandishi yoyote yanayokwenda kinyume na utamaduni wetu, matusi au dharau ya mchangiaji mmoja dhidi ya mwengine kwa hivyo nawashauri tunapochangia tuwe tunatumia lugha za kistaarabu. Ahsanteni. Salma Said

    • @Da Salma Said,
      Dada yetu na wewe unataka kuungana na hawa maluuni , tuachie tuwape kichapo cha laana maana hawataki kuheshimiwa maluuni hawa na wala hawaheshimu maamuzi ya Wanzanzibari,
      Hatuutaki muungano, hatuutaki muungano, hatuutaki muungano, hatuutaki muungano

  6. Inasikitisha sana kuona kuwa serikali hii ambayo tulioitegemea kutuongoza katika kuelekea katika haqi zetu, kuwa inajiandaa kuzuwia Wazanzibari wasizidai haqi zao!! Si hashaa kwa njia hii Zanzibar tukaangamia kwa majanga yasio na haja. hakuna ambacho muamsho na wanaosimama nao ambacho wamekisema nakukidai kinachokwenda kinyume na sheria. Uamsho kimesajiliwa, na kinatumia haqi zake Kilillahi kuelimisha uovu kwa njia ya uhalali. kuwazuwia kikundi hichi kufanya ibada na kuelimisha wananchi wa Zanzibar ni kuchochea mtafaruku ambao hauna faida na Zanzibar. wapeni fursa watu hawa wafanye wajibu wao, maadhal hawavunji katiba na hawavunji amani katika nchi hii!! Kinachoogopwa ni kitu gani?

  7. Pingback: SMZ yaifunga mdomo UAMSHO·

  8. Serekali yeyote dhalim inaogopa raia wake na hii yetu inaogopa raia wake wameona watu wengi wanaelimika na kujiunga na uamsho sasa wameona wazuiye mihadhara thubutu kesho swala maisara na taarifa nilizo nazo j,pili Donge kwa mfalme Shamhuna muuza bahari.

  9. hongera bi salma sasa inaonekana umekuwa tulikuwa tunakushangaza kurusu matusi tena makubwa makubwa kutukanwa viongozi wa nchi wangekuharibia na hata kupelekea kushtakiwa kwa defamation kuwa makini sana vijana wamejawa na jazba baada ya busara

    • Mkuu hashtakiwi mtu hapa, wacha woga wako, ni kiongozi gani mwenye hadhi na heshima yake alotukanwa isipokuwa wale wasiojiheshimu na viaraka wa Tanganyika kina Moh’d Abudu, Sefu Iddi, Shamhuna na wapumbavu wenzao au baba zako ?

  10. Jamani viongozi mimi nawashauri kwakuwa 99.9%ya Wakaazi wa Zanzibar ni Waislam kwanini hawa mashekhe wetu ambao ndio viongozi wa Uislam hatuwapi nafasi ya kuielimisha jamii yetu ya Kiislamu , mimi kwa uwono wngu mdogo nahisi waachiwe waijenge Nchi yao kimaadili , Kimtazamo na Kiutekelezaji ,Namini hawa si wendawazimu na ndio MwenyeziMungu akawafungua mioyo yao na akawatanua akilizo kwa kuwajazia Kurani tukufu .Sasa tuwatumie ili waiweke Nchio yetu katika ustaarabu wakimaadili ,tuwape nafasi za makusdi katika kuijenga ZANZIBAR YETU ,naamni kiwango walicho fikia si kidogo na jamii imewaelewa vya kutosha hata leo mukiamua kuwazuia kumbukeni kwamba mtaleta utata kati nchi yetu na mimi nata niwakumbushe kitu .Kwa kawaida gharka ya Mwenyezimungu itakapo tufikia haitangali huyu ni nani na yule ni nani itawakumba wote ,na nyiniy viongozi wa serika mnao jipangia mabaya mjue vita havina macho vikiingia hata wewe familia yako itapata shida naomba niwashauri bure ziachieni wana JUMIKI wafanye kazi zao bila ya kuwabugudhi ili nchi hii iendelee na kuwa na amani na ustaarabu pia nawaomba musimamie upigwaji wa kura ya maoni kama wanavyo sisitiza wao kuridhiana ni muhimu katika jamambo lolota lenye utata , hebu fikirieni baada ya maridhiano ya CUF NA CCM Nchi yetu imekuwa na utulivu wa kiasi ganiu ? Pia upendo kwa Wanachi wa Zanzibar umekuwa kwa kiasi Gani ? Mimi naamini hali hii kuna watu hawipendi binafsi lakimu Mwenyezi Mungu hatokuwa pamoja nao Ishalla .

  11. Ndugu Mzalendo mimi nimeanzisha huu mtandao tokea mwaka 2008 na tokea nimeanzisha nimeandika maneno hayo unayoyaona kwamba nahitaji michango yenye kufuata maadili na nimeyaandika maneno haya kabla sijapokea hata comment moja kutoka kwa mchangiaji lakini kwa kujua kwamba kuna watu watachangia nikaona niandike maneno hayo na kama utafungua katika ukurasa ulioandikwa zanzibaryetu juu kabisa upande wako wa kulia utaona maneno hayo ya utangulizi kwa hivyo sio kwamba nimekuwa sasa baada ya kupokea maneno ya matusi na kashfa bali nimeyandika muda mrefu maneno hayo na kuwafahamisha wafuatiliaji wa habari zangu watumie lugha ya heshima na kusisitiza nidhamu katika mtandao huu. Amma suala la kushitakiwa ndugu yangu Mzalendo mimi naamini siwezi kushitakiwa kwa sababu sio mimi ninayetoa maoni hayo na siwezi kumzuwia mtu kutuma maoni yake ila kwa kuwa nimesisitiza awali kwamba kusiwe na matusi basi naamini kwamba hilo ni lake mtu mwenyewe ikiwa atakuwa anaandika lugha ya kashfa na ya matusi lakini kwa upande wangu huwa anjitahidi kujizuwia kutochapisha kwa sababu msimamo wa mtandao huu ni heshima za kila mmoja wetu. Salma Said

    • Hongera Dada yetu, tunakupa HEKO kubwa kwa kutuekea BLOG hii adhiim, tutaheshima ustaarabu kwa moyo mkunjufu, lakini wacha tuwachape hawa vibaraka wa Tanganyika.

  12. Sasa Wazanzibari tuzungumzie KURA YA MAONI Zanzibar, tuwaachie Katiba lao na wala tusidili nalo ilo dubwana lao tusijekujitia kitanzi kipya Wazanzibari.

  13. Yaonekana Bwana Aboud amekurupuka, atueleze amepata mamlaka ya kuisemea kutoka wapi ?

Leave a reply to khasamo2012 Cancel reply