Taarifa ya SMZ ya matukio ya uvunjifu wa amani

Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.

Aidha, Serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu. Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.

Taarifa rasmi ya serikali kwa wananchi kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani nchini

Itakumbukwa kwamba tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati Maalumu ya Mawaziri ilikutana na viongozi wa jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Masheikh kuzungumzia hali iliyojitokeza nchini katika kufanya mihadhara ambayo ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani.

Katika kikao hicho serikali iliwataka viongozi hao wanapofanya mihadhara na mikutano inayohusu masuala ya maoni ya katiba wafuate taratibu zilizowekwa kisheria.

Aidha, serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu.

Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.

Kwenda kinyuma na sheria hii ni kosa la jinai na hivyo iliwataka wananchi wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na matakwa ya sheria.

Ndugu wananchi mbali na juhudi hizo za serikali bado wapo watu wachache wasioitakia mema nchi yetu na umoja uliopo wanaendeleza kwa makusudi vitendo vya kuvunja taratibu za sheria jambo ambalo limepelekea jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria.

Ndugu wananchi serikali imesikitishwa na vitendo vilivyojitokeza vya vurugu na uvunjifu wa amani ambavyo vimeelezwa kwa kina na jeshi la polisi iliyotolewa mapema leo tarehe 25.05.2012 na kamishana wa polisi zanzibar.

Kutokana na hali hiyo serikali inawahakikishia wananchi wote kwamba itaendelea kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria vinavyoashiria kuondolea nchi yetu amani na utulivu uliopo.

Ndugu wananchi serikali inawahakikishia wananchi kwamba jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua zifaazo ili kuwahakikishia usalama wa raia na mali zao unakuwepo na hali inaendelea kuwa shuwari amani na utulivu.

Ndugu wananchi bado serikali inasisitiza na kuwaomba wananchi wote waunge mkono juhudi za serikali na kuwacha kabisa kujiingiza katika vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani na utulivu katika nchi yetu.

Hivyo tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na serikali itaendelea kuwahakikishia usalama wao.

Aidha serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao wasijiingize katika vitendo viovu na vurugu kwani jeshi la polisi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa macho kupambana na vurugu hizo na vitendo vyote vya uvunjifu wa amani.

Kwa madhumuni ya kudhibiti amani na utulivu na usalama wa wananchi wetu serikali katika kipindi hiki itachukua hatua zifuatazo:

1. Inakataza mikusanyiko ya aina mbali mbali, maandamano, na mihadhara ya aina mbali mbali ambayo haijapata kibali cha serikali.
2. Serikali inaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kufanya fujo zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya zanzibar
3. serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa amali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na mali za watu binafsi.
4. Serikali inawapa pole wananchi na taasisi zilizoathirika na vurugu hizo na kuwahakikishia kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katiak kadhia hiyo.
Na mwisho tunawaomba wananchi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Ahsanteni

Nawashukuru kwa kunisikiliza.

Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.

21 responses to “Taarifa ya SMZ ya matukio ya uvunjifu wa amani

  1. Hana mpya lengo lao nikuwazuia watu ili wasiendelee kuzinduana,wakajuwa ubaya wa dubwana!

    • INAWEZEKANA KATUMWA NA VIONGOZI WA KITANGANYIKA. LAKINI YTUNASEMA WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO ULIOJAA DHULUMA KWA WAZANZIBAR. TUTAENDELEA KUDAI HAKI YETU MPAKA TUIPATE. UMESIKIA ABOUDU PELEKA SALAMU KWA WALIO KUTUMA

  2. UDIKTETA NDIO SURA YAO HALISI NA SASA INAJIONYESHA WAZI. HILI LIMEANDALIWA NA MOHD ABOUD, BALOZI SEIF IDDI NA USALAMA WA TAIFA NA WENZAKE SIKU NYINGI SANA. WALISHAPANGA NJAMA HII KWANI WALIJUA KUA WAKIMKAMATA HUYO USTADH KIPINDI HIKI KUTATOKEA FUJO.NI KWA NINI WASIMUITE HUYO SHEKH KITUONI KWANZA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUMKAMATA? POLISI WA ZANZIBAR WAMEZOEA KUTUMILIWA LAKINI WAJUE IKO SIKU WATAYAVUA MAGWANDA WAANZE KUOMBA KAMA WANAVYOMALIZIA NA WAO WATATUOMBA SISISISI..

    • NIKWELI WAZANZIBARI HATUUTAKI HUU MUUNGA NO LAKINI TUTUMIE HEKIMA KATIKA KUUKATAA. KUANDAMANA SIONI KAMA NI SULUHISHO. TUSIJARIBU KUSHINDANA NA MTU AMBAYE AKISEMA ANAFANYA HAWA JAMAA WANA MABOMU NA MASILAHA KWA AJILI YETU LAZIMA HEKIMA IPITE ILI VISITUMIKE HIVYO KWA AJILI YETU. SIKAMA NAOGOPA KIFO LAKINI NAHOFU KUWA NITAJIDHULUMU NAFSI YANGU. KWANINI HATUJIFUNZ KWA MTUME S A W, ALITUNGA KATIBA BAADA YA KUFIKA MADINA NA IKAMUWEZESHA KUISHI NA MAKAFIRI KTK NCHI YAO, AKAFUNGA MKATABA WA HUDAIBIA HATIMAE UKOMBOZI KAMILI NA UHURU UKAPATIKANA,
      KWANINI NA CC TUCSHIRIKI KTK HAYO MAONI TUKATOWA YA KWETU KILA TUNALOLITAKA. A’SAA HUENDA TUKAFIKIA TUNAPOPATAKA VYENGINEVYO TUTAJUTIA NAFSI ZETU.
      TUKAE PAMOJA, TUTAFAKARI PAMOJA KISHA TUAMUE PAMOJA.

    • NA SEIF SHARIF HAMADI
      Madhali mnawapemba ndani ya serikali, kamwe wazanzibari hawawezi kujikomboa.
      Kumbukeni 1984 wazanzibari walikuwa tayari kujikomboalakini akatokea Mpemba Seif Sharif akautetea muungano na kuwaita wote waliotaka kujinasua kutoka ukoloni uke kuwa WAHAINI

      Sasa amekuja Mpemba mwengine, Mohammed Aboud kuja kuvuruga mapambano.
      Bora Pemba wajitenge wabaki na mabwana wao Tanganyika. Tumechoka wazanzibari

  3. Sisi tunasema wewe Aboud na SERIcali yako hiyo hamujawa na hoja ya msingi ya kuwatia watu ndani kwa mujibu wa sheria.
    Pili.nyinyi nyote na serikali yenu hamuna uwezo wa kuweka amani zanzibar kwa sababu
    a)sio waadilifu:Kiongozi muadilifu halalamikiwi na anaowaongoza muangalie nabii wa mwisho wa umati huu na maswahaba zake walivyoongoza serikali.Wewe na serikali yako munawadhulumu wananchi kwa kuwakosesha haki yao ya kuamua ila munataka muwaamulie nyinyi wananchi wanachokidai wamechoka kukaa katika mfumo wa muungana bali wanataka waulizwe kwa kura ya maoni sasa nyinyi munalazimisha muungano uendelee kwa misingi gani wakati idadi kubwa ya wananchi wanaukataa.
    Tatu:amani ya nchi haiji kirahic kama viongozi cio waadilifu bali amani inapatikana kwa kufuata muongozo sahihi wa uislam kwa kutumia quran na sunna.
    Nne:napenda uelewe ya kwaba uisilamu ndio dini ya amani kama jina lake linavyojieleza kwani serikali inasema haina dini halafu inasema itahakikisha amani inapatikana znz huu ni unafiq ikiwa serika inasema haina dini maana ya haina amani kwa hiyo ABOUD hizo propaganda usituletee wewe huwezi kuleta amani madam uko katika serikali iliyokuwa haina amani.Nyinyi madhalim hamukozoe kufanya uadilifu kwa sababu hiyo serikali ilipatikana kwa kuwadhulumu watu tangu asili.LAKINI MSIMAMO WETU MUUNGANO HATUUTAKI.

  4. Viongozi wenye dhamana ya znz kumbuken roho zikishasema potelea kote znaweza kufanya chochote badae cheo ni dhaman mtaenda kulizwa mlitumikia vp cheo au vyeo vyenu dunia mapita kaondoka nyerere muasisi wa mungano je wewe unaekuwa na kibri.

  5. Amani ya nchi yetu ni muhimu sana kwa jamii yetu na kwakua Viongozi wa Serikali wana hubiri Amani kwani sasa hawawaiti Jumiya zote na kuwasikiliza na baadae kutoa fat-wa itakayo waridhisha kama ni kuvunja Muungano mtawasikia kauli zao na sababu zao za msingi lakini kuwakamata na kuwapiga mabomu wala haito saidia kubwa itazidisha ghasia na virugu tu nataka niwatanabahishe Viongozi wa Serikali kwamba pahala popote bila ya utaratibu kuufuta basi kinacho tokea ni fujo tu .Sisi wanazibari tuna kifungu katika katiba yetu kinacho turuhu kutofanya jambo lo lote la kitaifa bila kufanya kura ya maoni sasa hapa pana tatizo gani wakati huo ndio utaratibu wetu ,Jee tungeliufuata kungekuwa na vuru gani .

  6. KUUKATAA MUUNGANO SIO SABABU YA KUFANYA FUJO NA KUCHOMA MAKANISA NA MABAA HIYO SIO SOLUTION YA KUISHINDIKIZA SERIKALI IKUBALI MATAKWA YA WACHACHE KAMA HIVYO CHA MUHIMU ISUBIRIWE KURA YA MAONI JUU YA KATIBA MPYA HAPO KILA MTU ATATOA MAONI YAKE KUWANYANYASA WATANZANIA BARA HNA KUWAHARIBIA MALI ZAO HUO NI UJINGA WA BAADHI YA WATU WAKISHIRIKIANA NA VIBAKA MMHIVI JUMUIYA YA UAMSHO NDIVYO ILIVYO AGIZA KWELI CHA MUHIMU WATU WAU WARUDI KWENYE MEZA YA MAZUNGUMZO NA WALA SIVYENGINEVYO

    • Ingekuwa ujinga kama wazanzibari wangewafuata Bara na kuchoma Makanisa. Lakini wenyewe watanganyika mmekuja kukivamia kisiwa kiduchu kisichokuwa na ardhi halafu mnajenga majumba ya kukufuru mbele ya silka ya Kizanzibari halafu muachiwe tu. huo utakuwa UKHANITHI NA UBARADHULI

  7. hizi zote ni mbinu za usalama wa taifa tanganyika , na vikaragosi vyao akina abudu na sefu , muungano hautakiwi mtaitia nchi katika umwagaji damu , angalieni syria hakuna amani wananchi wakisema basi ni vyema wanasiasa waachie ngazi , MUUNGANO BASIIII wewe mwamedi kiabudu kilicholaaniwa na Mungu

  8. hawa hurambishwa damu ya Mmbwa kabla hawajapewa madaraka wakawa watumiliwa bila kutafakari,,, huondokewa na iman iliyo wakuza na kuwaleya,,,hawamjuwi mungu wala hawajali dhambi,,,, hakuna wa kuwahukumu ila aliye wapa dhamana hio na hakuna mwengine ila ni ( allah subhana wataala) ewe mola wetu kisikie kilio cha wazanzibar,, uwahukumie haki,, umdhalilishe kila dhalim,, hapa duniani kabla siku ya hesabu, ameen ameen ameen,,

  9. serikali inazitaka vurugu, kwa sababu wananchi wengi wanaandamana Muungano hawautaki kwa nini wao wachache wautake Muungano kwa kulinda maslahi yao,? salama zanzibar haijapakana na nchi kavu ipo baharini lakini kama ingalikua nchi kavu basi silaha hata sisi wananchi tungalikua nazo, hatuutaki muungano

  10. Haya ya watu kusema hawataki Muungano huu kama ulivyo yalisemwa pia na CHADEMA katika Mkutano wao wa Jumamosi tarehe 26, 2012. Tundu Lisu alisema na akawataka wana CHADEMA kudai hili wakati TUME ya kAtiba itakapopita. Najua kwa hapa Zanzibar tatizo nikuwa watu hawataki kusubiri hadi TUME iwafike kusema waliyonayo kuhusu Muungano. Kukosa subira kwa Wati wa visiwani kwatokana na sababu zifiatazo:
    1. Wana wasiwasi kuwa TUME hii iliyoundwa inaweza kusema yaisemwa na kuheshimiwa na watu waliyoituma. Hapo nyuma TUME ya Jaji Nyalali ilisema kuwa idadi kubwa ya watu walikataa mfumo wa vyama vingi lakini Mamlaka iliinunda ikakataa kuheshimu hilo. Hatuoni sababu kwa nini leo historia isijirudie.
    2. Kwa sababu ya SMZ kushindwa kutumia raslimali zilizopo vizuri watu wengi wanaishi kwa kubahatisha na wamo katika hali mpito baina ya mauti na uhai. Unapokuwa katika hali kama hii yoyote ajae na pendekezo la kukusaidia unamfanya ndie mwenza. Watu wanaoona UMASHO ndio waliombele katika kutafuta suluhisho la shoda zao na ndio maana wanakubali wito wao wa kutosubiri TUME ndio waseme juu ya Muungano. Hili lingeweza kuepushwa kwa Serikali yetu kuamuru kura ya mani kabla ya mambo mengine yoyote kutokea. Jeneral Ulimwengu hivi karibuni alizungumza kuwa si busara kutaka watu waboreshe kitu wasichotakitaka. Ni kwa nini watu hawafuati usia wake.
    3. Kama kuna wa kuwalaumu kuhusu yanayotokea Zanzibar basi watu wa ZAnzibar waliokatika Ofisi za Muungano kule bara. Ofisi ya VICE President, Kitengo cha SMZ, Home Affairs na MFA wanastahili lawama kweli. Kero zote zinazungumzwa hapa ambazo ndizo zinazopelekea erosion ya patience among general public hazijaonekana kushughulkiwa na hawa ipasavyo. Katika hali hii watu ni lazima wawaone jamaa hawa ni wasaliti na wajenge Imani na Mashekhe amao naona wanaonewa tuu kwa hawawashi hawazimi.
    4. Zanzibar ina viongozi tofauti na wale wa mwanzo. Marehemu Mzee Karume alikuwa kigezo. Si Kama Mtu kwa wafuasi wake lakini aliwaonesha watu njia. Mzee huyu alilima na watu makondeni, alijenga na watu majumba na alifanya kazi zote. Watu kwa kutumia kigezo chake walijuma na Zanzibar ikabadilika. Viongozi wa leo wa kazi ni Press Conferencena vyumba vyenye baridi kali. kisha kwa sababu ya kula ovyo na kazi nyepesi wanapata Sukari na Shinkizo la damu kwa wa India. Katika hali kama hii ya watu kukosa kiongozi mfano ni lazima watafanya yanapendeza na yasiyopendeza.

  11. Tuachieni tuamu nini tunataka leo mpo hapo madarakani kesho mtaondoka kama wenzenu walo tanguliya wasemaji wa ikulu wako wapi sasa na nyiny mtaondoka Muheshimiwa Saifu Idi Ulikuwa mtu mpole kabla ya kupata ulwaa cheo kibaya mtu hubadilika tubuu M/ Mungu akusamehe

  12. Kukataa muungano sio sababu ya kufanyia vurugu watu wa bara na kuwaharibia mali zao, itakuaje watu wa bara nao wakiamua kufanyia hivyo ndugu zenu walio bara?

    • Hakuna mtu wa bara alieharibiwa mali . Au unataka kusema Kanisa ni la watu wa Bara? Baa ni za watu wa Bara?
      Wabara watakuwa nahaki ya hata kuwafukuza Wazanzibari wakiona kuwepo kwa kunadumaza mustakabali wa nchi yao na sila zao

  13. Ah! 2shayazowea hayo , magap 2mefanyiwa. Hebu kumbuken MSIKT WA MWEMBE CHAI

  14. KATIKA HILI WALA TUSITAFUTE MCHAWI KWANI MCHAWI No 1 NI RAIS KIKWETE NA No2 NI KAMISHNA MUSSA. HISTORIA INATUFUNZA KUA SERIKALI YA TANZANIA HIJAWAHI KUKOSEA NA KUKUBALI KUA IMEKOSA HATA MARA MOJA TOKEA ILIPOASISIWA. MWAKA 2001 ILIUA WAZANZIBARI BILA YA SABABU NA HAIKUKUBALI KUA ILIKOSEA. MAUAJI YA MWEMBECHAI NA ARUSHA NK. NA SASA HILI LA ZANZIBAR. INACHOKIFANYA NI ULE USEMI WA BOSS IS ALWAYS RIGHT. LAZIMA ATOKEE JASIRI AMWAMBIE KIKWETE KUA HAPA MH. UMEKOSEA. NA PIA KAMISHNA MUSSA. NASEMA HIVI KWA SABABU ZIFUATAZO:
    TUMEZOEA MIAKA MINGI KUTUNGA KATIBA BILA YA KUWASHIRIKISHA WANANCHI. HUJIFUNGIA CHUMBANI WEREMA NA CHENGE WAKAITUNGA NA KUILTA BUNGENI NA BAADA YA HAPO WANANCHI TUNAIHESHIMU. MWAKA HUU KIKWETE AMETAKA KUWAONYESHA MABWANA ZAKE MATAIFA YA MAGHARIBI KUA YEYE NI MTU WA DEMOKRASIA KWA KUJITIA KUTAKA KUWASHIRIKISHA WANANCHI. ANAFANYA HIVYO HUKU AKISAHAU KUA ASILI YA SERIKALI YA TANZANIA NI UDIKTETA NA ALIPOONA WANANCHI WANASHIRIKI KIKWELIKWELI ASILI IMEKUJA JUU NA ANAANZA KUWAPIGA MABOMU. KAMA HUWEZI DEMOKRASIA USIJITIE HASHUO ENDELEA NA MTINDO ULEULE WA ZAMANI HAKUNA AMBAE ATAKUULIZA. WAZANZIBARI TULIKAA KIMYA NA HATUKUA TUKIHOJI ILA MLIPOJITIA HASHUO KUTAKA TUSHIRIKI NDIO TUMEANZA NA IMEKUA NONGWA.BWANA KIKWETE DEMOKRASIA HUJAIWEZA BADO. TUNGA KATIBA YAKO WEWE NA WANSHERIA WAKO. UKITAKA SISI TUSHIRIKI USTUEKEE VIKWAZO AU KUTUCHAGULIA LIPI LA KUSEMA. SISI WAZANZIBARI TATIZO LETU NI MUUNGANO NA KAMA TUSIUSEME VUNJA TUME YAKO HATUNA HAJA NAYO.
    KAMISHNA MUSSA KAMA HIVI NDIVYO JESHI LA POLISI ZANZIBAR LINAVYOFANYAKAZI NA WEWE UNAPASWA KUBEBA LAWAMA NA ULITAKIWA UWAJIBISHWE. HIVI NI KITU GANI KILICHOKUPA KUMKAMATA HUYO IMAMU WAKATI ULIKUA UNAONA HALI IMESHAKUA TETE? NI KWA NINI USISUBIRI MPAKA HALI IKAPOA NDIO UKAMKAMATA? LAZIMA ASKARI WAKO WAJIFUNZE SAIKOLOJIA NA KUA WAO NDIO WALIOLIKOROGA HILI NA WEWE NDIE MKUU WAO UNAPASWA KUWAJIBIKA. HUO UKALI WAKO DHIDI YA UAMSHO HAUSAIDII KITU. UZEMBE WAKO NA KUTOKUJUA WAJIBU WAKO KUMESABABISHA HASARA KUBWA KILA UPANDE. MALI ZA WATU, TAASISI, SERIKALI ZIMEHARIBIWA. MABOMU YALIYOPIGWA NI FEDHA ZA WALIPA KODI NA PIA KUSAFIRISHA VIFARU VYA JWTZ KUJA ZANZIBAR. KAMA SIO UZEMBE WAKO NA KUTOKUJUA KAZI NA WAJIBU WAKO NAAMINI HILI LISINGETOKEA. POLISI ANEJUA KAZI NA WAJIBU WAKE KUA NI KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO ANGEZUIA KUMKAMATA YULE SHEHE JANA NA AKAFANYA HIVYO SIKU NYENGINE. INAONYESHA KAMISHNA MUSSA ULIKUA NA AJENDA YA SIRI MAANA MIDOMO ILIKUA INAKUTETEMEKA KUA UTAWAKAMATA VIONGOZI WA UAMSHO KWA GHARAMA YOYOTE ILE. HAYA HAO WAKAMATE KAMA WEWE NI KIDUME KWELI. KWENYE NCHI YENYE UTAWALA BORA WEWE NI MTU WA KUSTAAFISHWA KWA MANUFAA YA UMMA. UZEMBE WA ASKARI WAKO NA WEWE MWENYEWE NDIO CHANZO CHA YOTE HAYA NA HASARA ZOTE ZINAZOFUATIA.

Leave a reply to Salim Cancel reply