Uamsho wakanusha kuhusika na uchomaji wa kanisa

Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Abdallah Said Ali ambaye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi akizungumza na Radio DW asubuhi mapema kabla ya taarifa ya kutafutwa kwao kutolewa kwa vyombo vya habari

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU

(JUMIKI)

للجنة الدعوة الإسلامية

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION

P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com

MKUNAZINI ZANZIBAR

Tarehe 27MAY2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ

 

Advertisements

32 responses to “Uamsho wakanusha kuhusika na uchomaji wa kanisa

  • ni kawaida mabadlilko yanpotokea umwagaji damu utakuepo na tabu zitatokea kwa muda fulani hakuna kinachodumu milele ila ni ALLAH { S. W} pekee ndie anaee dumu mile kitu muhimu ni kua nia ya mtendaji ipo kwenye ukweli . mkweli ndie anaelindwa na ALLAH na ukweli ndio unao leta imani na umoja vitu hivo ni muhimu katika kukomboa uhuru wa ZANZIBAR

 1. hizo mbinu za usalama wa taifa zimeshagundulika zamani,hapa haturudi nyuma na hata hiyo ngao yao ili dunia wachukie waislamu tumeshaigundua

 2. hii inawezakana ni mbinu za usalama wao wamechoma hivyo vitu na kuwasingizia watu wengine ili wahalalishe dhulma kwa watu wasio na hatia , inabidi watu watafakari , hii ni kutia fitna baina ya dini tofauti , ambayo inasababishwa na watu ambao hawataki muungano uvunjike

  • JUMUIA YA KISILAMU NA MIHADHARA YA KIDINI , WALIFANYA MATEMBEZI YA HIARI KWA SALAMA NA AMANI KAMA KULIKUWA NA HUJUMA ILIKUWA ZIFANYIKE PALE MCHANA PALIPOKUWA NA UMATI WA WATU?

   IKIWA KUNA HUJUMA ZOZOTE BADAI BASI ITAKUWA JESH LA POLISI NDIO WAKUBEBA LAWAMA KWA VILE MATEMBEZI YALIKWENDA SALAMA NA KUMALIZIKA SALAMA SASA KUBEBA VIONGOZI WA JUMUIA YA MUAMSHO USIKU NIVITENDO VYA UGAIDI KWA RAIA.

   HAYA YAMEPITWA NA WAKATI HIVI SASA USALAMA KUWAKAMATA WATU USIKU NA KUWA TORTURE, INAWEZEKANA HASIRA ZA WANANCHI KUKAMATWA VIONGOZI WAO NDIO WAMEKASIRIKA NA KUFANYA HIVYO.

 3. maandamano hayana asili katika dini
  nyinyi mmetoa wapi haya ?
  Acheni kuandamana Mtume Alidhulumiwa lakini hakuandamana
  Alipigwa mawe lakini hakuandamana nyinyi mmetoa wapi haya ?
  By Nassirusunnah waqaamiul bid’aa

 4. Waliochoma Kanisa ni Vijana wa CCM Wameonekana Wiki 1 Kabla.

  Salaaamu Nduguzangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Nchi yetu. Tafadhalini Musinichoke kwakuandika Makala nyingi. Ila nataka nkuwataarifu habari ambazo Nimezipata Kwa Mtu wa CCM ambae ni Wakaribu sana na Familia yangu.

  Mtu huyo ni Adui Wa Umoja wa Wazanzibari haliyakua yeye Mwenyewe ni Mzanzibari wa Donge na Bumbwini. Lakini ni Mtunambae yoko Msimamo wa Mbele kuitumikia CCM na Kuhujumu SUK au yoyote yule anaepinga Muungano.

  Kijana huyu anasema …” Tutawaonyesha UAMSHO kwamba cc ni Wazanzibari na wana CCM Vijana Kwani Kuchoma Makanisa Ndio lengo la kwanza Kuipaka Matope Muamsho”

  Vijana wapatao 5 walionekana katika Kanisa la Kariakoo wakati wa Usiku kuliangalia Kanisa Hilo.

  Walipelekwa hapo na Gari ambayo inaonesha ni Gari ya BORIFYA MTUMWA BOROFYA.. Yule aliekua Akiuza GONGO pale Muembe Rikunda.

  Mtu huyu anasema hili nitukio lililopangwa lifanyike mara moja Muamsho watakapo fanya Maandamano ya Aina yoyote ile. Na Romers zilikua zikisikika kwamba Muamsho wangefanya Maandamano tarehe 24.05.12. Lakini hakuwa. Vijana hawa walilipwa pesa Kutoka CCM Tanganyika ili waweze kufanikisha Lengo La kuiua MUAMSHO na Vuguvugu la Wazanzibari wanaodai Haki Yao ya Katiba ya Kuitishwa kura ya Maoni.

  Hivo Wana CCM wamefurahi sana kwatukio walilolifanya lakuChoma Kanisa ili Wapate Wa Waadhibu Wazanzibari wanaotaka Hakki zao na Amani ya Nchi yao.

  Niliposikia hivi nimesema sina budi ila kuandika habari hizi haraka sana ili watu wengine wajue ukweli uko Wapi.

 5. Hii haitoshi nadhani pia unahitajika kuwasilisha ushahidi huu kunakohusika, UAMSHO maana police ni hao hao waTanganyika.
  Pia tunakushukuru sana Kikwete umemzidi baba yako nyerere, maana yeye alisema Wazanzibari sitowapiga mawe kama watadai kutoka kwenye muungano loakini wewe unatuuwa kwa sababu tuu tumeamua kutamka na kuonesha hisia zetu dhidi ya utawala wa Tanganyika ila ujuwe hatutorudi nyuma asilan abadan na ukituuwa tunakusubiri huko mbele ya hakimu wa mahakimu ambaye yeye hadhulumu

 6. Hizo ni mbinu za mazayuni (zionist) ndizo wanazotumia kuupaka mavi Uislam kila pembe ya dunia hii,na kuusababisha maafaa na hasama kubwa Ulimwenguni.Tuwe macho na hawa watu tayari wamesha ivvaa zanzibar kupitia mahasidi wa chache wasiopenda maendeleo ya Zanzibar.

 7. WAZANZIBARI SASA TUMESHAJUA NANI MMBAYA WETU. HAYA YOTE YAMEFANYWA NA KUPANGWA NA IDARA YA USALAMA WA TAIFA ILI KUPATA SABABU YA KUZIMA HARAKATI ZA UAMSHO. HAPA TUSIRUDI TENA NYUMA KWANI HII NI HAKI YETU KUTOKA KWENYE MUUNGANO. WAZANZIBARI SASA TUAMKE TUJIULIZE HIVI TANGANYIKA INANG’ANG’ANIA NINI KWA ZANZIBAR? HATA ITUMIE MAJESHI NA GHARAMA NYINGI? NI LAZIMA KUNA MASLAHI MAKUBWA AMBAYO TANGANYIKA WANAYAPATA KWENYE MUUNGANO HUU NA HASAHASA HAYA MAFUTA. WAKISHAYAMALIZA NDIPO WATAKUA TAYARI MUUNGANO UFE. WAZANZIBARI TUZINDUKE TUSHIKAMANE KUVUNJA MUUNGANO HUU DHALIMU UNAOTAKA KIFISIDI NCHI YETU YA ZANZIBAR.

 8. yote haya yaliotokea yamesababishwa na viongozi waserikali ya smz kama wangewasikiliza nini wazanzibari wanata haya yasingalitokea ila bado muda wa kuyatatua haya upo, enyi viongozi kumbukeni muna jukumu kubwa mbele ya ALLAH na mutaulizwa wasikilizeni wazanzibar maoni yao kabla hali haija ongezeka kuwa mbaya zaidi

  • BIN KHAMIS HAYA YOTE YAMESABABISHWA NA WATU 2 MAARUFU MMOJA MZALIWA WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR MMOJA MYAMWEZI HAO NDIO WALIO SABABISHA MACHAFUKO ZANZIBAR

 9. Natanguliza shukurani zangu za dhati kwa viongozi wa UAMSHO, kwani wametufunua macho. Wazanzibar hatu paswi kurudi nyuma, hii ndio fursa PEKEE tuitumieni, naona tunakaribia kabisa kuipata nchi yetu. Tumuombe MUUNGU Atusaidie.Aaaamin

 10. MAWAZO YANGU KAMA NI MZANZIBAR KINACHOTAKIWA CHA KUFANYWA KUWEZA ZANZIBAR KUWA NA DOLA YAKE NI NJIA HII NA NI NJIA NYEPESI NA ASILIMIA MIA 100. WAZANZIBAR WATAFIKA WATAKAPI NI KUAMUA KWA WAFANYA KAZI WOTE WANAO ISHI ZANZIBARNA HUSASAN RADIO . TELEVISION , WALIMU . MAPOLISI .N.K MADAKITARI WAO WANAHITAJIKA KUENDA KAZINI KAMA KAWAIDA NA KUHUSU WATU WA REDIO NA TELEVISIO WAWE NA KAULI HII YA KWAMBA HAWATORUSHA MATANGAZO YOYOTE TANGAZO LAO LA KWANZA LA KURUDI KAZINI NI KUTANGAZA KWAMBA RAIS WA ZANZIBAR ANASHIRIKIANA NA WAZANZIBAR WALIO MCHAGUA AU AMEJIUZULU

  . KAMA NI MZANZIBAR

 11. KAMISHNA MUSSA INAONEKANA UNA AJENDA YA SIRI NA UAMSHO KWANI UNASEMA UTATUMIA GHARAMA YOYOTE ILE KUWAKAMATA. HII KAULI HAIONYESHI KUA UTAWATENDEA HAKI BALI UNAONEKANA UNAFUATA SHINIKIZO TOKA KWA VIONGOZI FULANI.KUNA USHAHIDI GANI KUA VIONGOZI WA UAMSHO WALISHIRIKI? KAMA NI KUSHTAKIWA BASI JESHI LA POLISI NDIO LA KUSHTAKIWA KWANI BADALA YA KUMKAMATA HUYO IMAMU WANGEMUITA KITUONO NAAMINI ASINGEKATAA KUENDA. JESHI LA POLISI LINAFANYA KAZI KIZAMANI YA KUKAMATAKAMATA OVYO NA WATU WANAPOBISHA WANATUMIA NGUVU NA HII NDIO CHANZO CHA VURUGU.

  • KAMISHNA ANAOGOPA KUKOSA TONGE YA WALI NDOMANA KATUMIA KAULI HIYO IL.I KUWATISHA WAZANZIBARI WOTE. LAKINI TUNASEMA HATISHIKI MTU WALA HAOGOPI MTU. WAZANZIBARI TUACHIWE TUPUMUE. VIONGOZI WOTE WASERIKALI WANAITUMIKIA KANISA KATOLIKI KAMA WAONGO WAHE WAPISHE.

 12. Kwa kweli sasa wakati umefika viongozi wa nchi kwa haya yaliotokea ndio mujue km wananchi wamechoka na hawataki muungano na pamoja na njama zenu zote tumezigundua haswa kwa viongozi wa tanganyika wasio na imani na sisi viongozi wa zanzibar nyinyi ni wazanzibari wacheni kuwasikiliza hao madhalimu wasikizeni wananchi wanasemaje sisi kila tukipigana wao kwao ndio faraja tunawaomba kuwa na uwamuzi sahihi wa nchi yenu.

 13. Ndugu zangu wa zanzibar mimi naomba niwahusie jambo mmoja chochote cha duniani sio chako hata nchi uliyozaliwa kwa wakati huu si yako. muungano tunaozungumzia leo uhalisi wake wengi tunadhani pale wahasisi wa nchi hizi walipoamua kuchanganya udongo hivyo kuutengua leo utachukua marais wa sasa kuvunja kile kijungu tu inatosha na zanzibar itakuwa nchi peke yake,kama tunadhani ni hivi la tumekosea, huu muungano asili yake hasa huko juu kwa mabwana wakubwa wa kidunia hivyo watakaloa wao la kidunia halina mjadala hivyo kwa wao huu muungano unafaida kwao basi utabakia, hii dunia yao mungu amewahaidi hivyo atawapa wao zaidi kuliko hatakavyo mpa muislam unless sasa muislam uipende dunia kama kwa hili linalofanyika mungu atakupa lakini madhara yake yatakuwa makubwa na pengine utaharibu akhera yako. Wewe akhera yako mungu atakupa zaidi kuliko atakavyo mpa wa hii dunia.
  Hili neno huru tuliweke la mwisho kabisa kwenye vinywa vyetu na ikiwezekana tulisahau kwani kwa muumini hasa dunia ni jela chochote kinachohusiana nacho hana budi kuepukana nacho, allah allah tujiepusheni na fitna na tusije tukaona nchi nyingine wameandamana wananchi wamefanikiwa kupata wanachotaka na sisi tukaiga la nchi hizo karibu zote sasa wanajuta bora ya yule waliyemtoa kuliko wanayowakuta sasa na haya yote tunayaona sasa.
  Pengine tulichonacho ni bora kwetu sisi kuliko hicho tunachokitaka hila siku zote binadamu huwa hatutambui hilo mpaka masahibu yanapotukuta, muhimu ni kumuomba mwenyezi mungu kama muuungano ni wa kheri kwa sote basi haudumishe barka na kama ni wa shari basi yenye ndio hawe mwamuzi lakini sio leo tukamsikiliza mtu yoyote yule na mawazo yake au yao kwa sababu kitu au jambo fulani haliko sawa akilini na machoni tukawafuata la we are muslim,we are of best nation hence we expect of ourselves the best na vipi tutafanikisha hilo amesema bwana mtume S.A.W katika hadithi sahihi ya kuwa tushirikiana kiushauri na watu lakini mshauri wetu wa mwisho awe yeye muumba na yeye atatupa lile lilo bora kwetu hivyo kuna salah kama istikhara tunaweza kusali na Allah akatuongoza katika hili na mengineo in sha allah.
  Leo alhamdulilah muislam una uhuru wa kufanya ibada na masahala mengine ya kidini, unapata riski yako na watu wako na una mahala pa kujihifadhi shukuru sana hili au haya si madogo ni neema kubwa sana kwani kuna wenzetu hawana haya lakini yote hatujui kwa sababu hatukujahaliwa kutembea na kuona. Kama mtu anaiba serikalini au anafaidika na mafuta na mengine kuzungumzia na kukichukia vile vitendo inatosha kwa dunia ya sasa kwani pia ni dalili ya kuwa ni watu wenye imani kutokana na hadithi ya bwana mtume S.A.W na kama kuzungumzia na kuchukia moyoni haitoshi basi wewe na watu wako hama zanzibar fanya hijra nenda pale penye nafuu na wewe kwani bwana Mtume S.A.W yeye pia aliondoka makka na laiti ya kuwa kazaliwa kakulia pale njama na vitimbi dhidi yake vilipozidi na wee fanya hivyo kama kweli unatafuta na kufuata kigezo bora.
  Mimi ninahamini hamja choma moto kanisa lakini katika vurugu kuna madhara na kuna wengine wanatumia ule upenyo kutimiza yale waliyoyaweka moyoni na kueneza fitna na lawama kwa vyovyote vile zitawaangukia wale walengwa na walengwa ni sisi ushauri wangu tukalitengeneze lile kanisa na tununue gari lengine kwa ajili ya askofu,hii ndio tabia za watu wa amani,la mwisho hizi ni zama za fitna kuishinda fitna inabidi tuumize vichwa na tumuombe mwenyezi mungu atusaidie tuzishinde fitna na sio kukurupuka na kuamaki tutashindwa daima.

  Asalam alykum.

  • Soud umeongea mengi lakini mengi kati yao ni pumba.
   Kama we unautaka uwo muungano ulikua uwe wazi tu muamsho tukupige dua.

   • Naam la kwanza ni kuondosha kwa mkono lakini pia linapokuja swala la hadith,kuna hadithi nyingine zinaendana na wakati hasa zile ambazo zina option zaidi ya mmoja ndani yake juu ya jambo hilo hilo mmoja nasema haya kutokana na munasaba wa kiimamu wa sunni ambao wanatumia kipengele cha kufanya Qiyas kuhusianana na mas-hala ya fiqh la kwa madhahabu mengine nimeyasoma lakini si haki juu yangu comment juu yao nita comment kila ambacho mimi nina kipractise. Linapokuja swala la hili hadithi kwamba tunapoona ovu tuliondoshe, tukishindwa tulikemee na tukishindwa kabisa basi tulichukie moyoni hakika hii ni daraja la chini la imani haimaanishi ya kwamba imani yako ni dhaifu.Ya bora kuwa na imani japo nduchu hiyo ni salama kwetu kwani tutakuwa ni wenye kuamini na mwenyezi mungu amewasifu wenye kuamini na mpaka surah yao peke akawashushia kuliko kuwa na kibri kwani mwenye kuwa na japo punje ya kibri kwenye nafsi yake ni haraam kwa mtu huyo kusikia ile harufu ya peponi. Lakini wengi leo tunasahau ya kwamba mengi maovu either sisi tunayatenda au watu wa nyumbani kwetu au karibu zetu wanayatenda lakini tujiulize tumefanya nini kwani hapa ndio hasa hasa hili swala la kuondosha kwa mkono linatakiwa lifanye kazi je tunafanya hivyo? Sisi hatujakamilika katika dini hatuwezi kufanya a-z tujitahidi kufanya kile ambacho allah ametujalia na kile ambacho hatukuweza in shaa allah hatatusamehe yenye ni mwingi wa kusamehe.
    Mimi niliposema tujitahidi tulitengeneze hilo kanisa si kumaanisha ya kwamba tutauendeleza ukafiri nilimaanisha mimi ya kwamba ingawa na tofauti zetu za kiimani still ni jukumu letu sisi waislam kuwa na mahusiano mazuri na watu wanaotuzunguka. Wengine tunaamini kutoa dawah ni maneno lakini ni hasa ni vitendo, Mtume alikuwa bora si tu alikuwa bora wa maneno yake lakini hasa alikuwa bora wa vitendo vyake ndio mana ameweza na bado anaendelea kuwa kipenzi cha mabilioni ya watu. makafiri wa sasa hawana muda wa kusikiliza maneno ya mtume waamini, vyombo vya taarifa hawana muda huo pia hila wana muda wa kuonyesha vitendo vya waislam hasa vile visivyofaa lakini kama leo tutajivisha vitendo vizuri hiyo itakuwa dawah tosha maneno yatakuwa ni yenye kukamilisha ile dawah. Kulitengeneza kanisa haimaanishi ya kwamba lengo letu wamshirikishe mwenyezi mungu ila kwa dunia ya sasa kidogo unachofanya kina athari katika mioyo ya watu na pengine hii ikawa sababu ya watu wa dini nyingine kuona ya kwamba kumbe uislam huko tofauti kabisa na tunavyoufikiria na ikawa sababu ya wao kuufatalia uislam na mwisho kuingia. Hawa watu wa dini nyingine wako karibu sana na uislam quran inasema hivyo jambo dogo na zuri katika uislam watakaloliona in shaa allah itakuwa sababu ya wao kuingia uislam lakini kwa sasa kidogo inakuwa ngumu ingawa wengine wanaingia alhamdulilah kwa sababu nchi karibu nyingi waislamu wanapigana na kuuana hii inachangia kuwapotosha juu ya dini hii nzuri. Hivi vitendo tukitaka tusitake vinasaidia kuendeleza ukafiri si haya tu kama si wewe au mimi nduguyo leo tuna mambo ya kikafiri majumbani mwetu ambayo yanatutoa katika akida za kiislam,mambo haya ni ya kuyapa kipaumbele zaidi kwani uislam unaanza kwa sisi wenyewe na watu wa majumbani kwetu kwanza kisha ndio utoke nje.
    @Mwenye uchungu na znz kuna watu wakisoma hili jina lako tayari ushawapa nafasi katika akili yao kujenga taswira juu yako. mwenye kujifananisha na kitu fulani au kujipa sifa fulani hata kwa masihala basi malaika wanamwandikia mtu huyo sifa au jina alilojifananisha nalo na siku ya kiyama anaitwa kwa jina hilo au sifa hiyo sasa ndugu yangu utapenda kweli siku hiyo nzito uitwe mwenye uchungu na znz au ungependa uitwe mwenye uchungu na akhera anyway majina si muhimu kinachojali sana ni amal njema. Mimi ndugu yangu sina ninachotaka zaidi ya kuona uislam unaenda mbele na tunaufuata uislam kwa maneno na vitendo, mimi sina ninachotaka zaidi ya kuona watu regadless tofautii zetu za kiimani tunaheshimiana na kupendana ingawa ni angalabu, hakuna zaidi ya waislamu wa zanzibar na bara tukapendana,kueshimiana na letu likawa mmoja,hakuna ninachotaka zaidi ya kuona kizazi chako na changu kinapata elimu na watu wanafaidika na elimu na sisi tumelala makaburini japo wanatukumbuka kwa dua, hakuna ninachotaka zaidi ya alichonijaalia mimi allah na wewe upate na tena zaidi, hakuna ninachotaka zaidi ya kukutakia akhera na wazanzibar,wabara na waislamu wote.Hayo ni maswala ambayo mimi niko radhi na kujitaidi kuyapigania mpaka mwisho wangu lakini mashala ya muungano, sijui jamhuri na mengineyo la,siwezi kubeba dunia na akhera. Kila la akhera na fi ammana bi llah kwa kila jambo la kheri.

  • @ soud

   Bwana sikiliza “WOGA na HIKMA vinatafautiana kwa mstari mwembamba sana sana” Hivyo uwe na udhu unapotembea juu ya uzi baina ya hikma na woga.

   Mambo yako mengi uliyoyasema humu ukumbini ni ya kiwoga woga tu. Sio ya Istiqamah and confidence against hypocrites along with their relative disbelievers.

   Je! Hujajifunza hapo kwenu Tanganyika wazee wakiislamu walipowakusanya waislamu kuupinga uzinduzi wa elimu ya dini mseto tena kwa mawe, mpango uliosimamiwa na wakristo na BAKWATA akiwemo Marehemu Sheikh Gorogosi bila ya kujali upinzani wa Waislamu wa awali?

   Je! Leo huu mpango wa dini mseto upo au umesita?

   Je! Kama wangefuata hizi hikma (WOGA) zako leo tungekuwa wapi waislamu?

   Je! Hukumbuki tamko la serikali ya Tanganyika (MUUNGANO) na Maaskofu juu ya Mahakama ya Qadhi Tanganyika, kuwa haitakuwepo na ikibidi watamwaga damu?

   Je! Hujasikia taarifa ya serikali Bungeni kupitia Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda a.k.a “Zanzibar si Nchi” aliposema kuwa utaratibu unaendelea kwa wasomi wakiislamu kukaa na kuratibu structure ya mahakama hiyo na mambo mengine ili ianze ku-exist?

   Je! Kama waislamu wangechukua hatua zako hizi za kuchukia moyoni hii hatua ingifikiwa?

   Waislamu wa aina hii wanapendwa sana na Wamarekani na kama watakujua kwa msimamo wako huu watakujengea nyumba ndani ya New York.

   Mjomba hueleweki, mara tuchukie moyoni , mara tuchukue hatua ya vitendo majumbani, mara tulijenge Kanisa, mara dini yetu bado hatujakamilika tufanye kila tunaloliweza tusiloliweza mashaa Allah tutasamehewa. Haya maneno yako sitaki kuyachambua kwani umejijibu mwenyewe kwa mwenyewe, lakini nakushauri uyatafakari mwenyewe, hii ni aibu please think bigger out of the box.

   Lakini nikuulize swali moja tu kwenye maneno yako hapo juu.
   Qs. Uliposema tulijenge Kanisa ulikusudia tulijenge kwa mikono (Vitendo) au kwa moyo (tulipende)?

   Kwa kukusaidia sisi mbali ya kwamba limebomolewa na wao wenyewe, hatuwezi kujenga Kanisa kwa moyo wala mikono.

   Tunakuomba utufuatilie ndugu zako tunavyouvuta uzi dhidi ya Mfumokristo hapa Zanzibar. Kila la kheri Sheikh Ilunga tumekusikia tumeanza kushughulika. Tunaomba Dua zenu hatumwi mtoto mara hii. Huu ni upepo mwengine si wa CCM dhidi ya CUF, hapa ni Uislamu dhidi ya waliodhidi yake wanaotuibia ardhi, heshima, mamlaka, mali na hata kutuulia watu kisa Uislamu wetu.

   Lakini usivunjike moyo ni utoto tu ukikuwa utaacha. Endelea ku-contribute, the more you contribute the more you improve as well as understand.

   MUUNGANO HATUUTAKI.

   JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

   “When peace fails apply force”

   Nawasilisha jibu.

   SERELLY.

 14. Alioyasema muheshiwa ni mazuri na ninayaheshimu ila hiyo hadithi ya mtume saw ulioitoa ukimbuke kama la mwanzo linasema ukiwa unaweza ondosha kwa mkono na hiyo kuchukia ni ya mwisho na huo ni udhaifu wa imani na kuhusu waislam kujenga kanisa kanisa ni jambo ambalo haliwezekani mtume saw amesema yoyote atakaeanzisha jambo la kheri atalipwa hadi kwisha kwa jambo hilo hali kadhalika atakaeanzisha jambo baya sasa huoni kuwa waislam watachangia kupeleka ukafiri mbele? Aliyechoma ndie atakaelipa. Allahu aalam.

  • Naam la kwanza ni kuondosha kwa mkono lakini pia linapokuja swala la hadith,kuna hadithi nyingine zinaendana na wakati hasa zile ambazo zina option zaidi ya mmoja ndani yake juu ya jambo hilo hilo mmoja nasema haya kutokana na munasaba wa kiimamu wa sunni ambao wanatumia kipengele cha kufanya Qiyas kuhusianana na mas-hala ya fiqh la kwa madhahabu mengine nimeyasoma lakini si haki juu yangu comment juu yao nita comment kila ambacho mimi nina kipractise. Linapokuja swala la hili hadithi kwamba tunapoona ovu tuliondoshe, tukishindwa tulikemee na tukishindwa kabisa basi tulichukie moyoni hakika hii ni daraja la chini la imani haimaanishi ya kwamba imani yako ni dhaifu.Ya bora kuwa na imani japo nduchu hiyo ni salama kwetu kwani tutakuwa ni wenye kuamini na mwenyezi mungu amewasifu wenye kuamini na mpaka surah yao peke akawashushia kuliko kuwa na kibri kwani mwenye kuwa na japo punje ya kibri kwenye nafsi yake ni haraam kwa mtu huyo kusikia ile harufu ya peponi. Lakini wengi leo tunasahau ya kwamba mengi maovu either sisi tunayatenda au watu wa nyumbani kwetu au karibu zetu wanayatenda lakini tujiulize tumefanya nini kwani hapa ndio hasa hasa hili swala la kuondosha kwa mkono linatakiwa lifanye kazi je tunafanya hivyo? Sisi hatujakamilika katika dini hatuwezi kufanya a-z tujitahidi kufanya kile ambacho allah ametujalia na kile ambacho hatukuweza in shaa allah hatatusamehe yenye ni mwingi wa kusamehe.
   Mimi niliposema tujitahidi tulitengeneze hilo kanisa si kumaanisha ya kwamba tutauendeleza ukafiri nilimaanisha mimi ya kwamba ingawa na tofauti zetu za kiimani still ni jukumu letu sisi waislam kuwa na mahusiano mazuri na watu wanaotuzunguka. Wengine tunaamini kutoa dawah ni maneno lakini ni hasa ni vitendo, Mtume alikuwa bora si tu alikuwa bora wa maneno yake lakini hasa alikuwa bora wa vitendo vyake ndio mana ameweza na bado anaendelea kuwa kipenzi cha mabilioni ya watu. makafiri wa sasa hawana muda wa kusikiliza maneno ya mtume waamini, vyombo vya taarifa hawana muda huo pia hila wana muda wa kuonyesha vitendo vya waislam hasa vile visivyofaa lakini kama leo tutajivisha vitendo vizuri hiyo itakuwa dawah tosha maneno yatakuwa ni yenye kukamilisha ile dawah. Kulitengeneza kanisa haimaanishi ya kwamba lengo letu wamshirikishe mwenyezi mungu ila kwa dunia ya sasa kidogo unachofanya kina athari katika mioyo ya watu na pengine hii ikawa sababu ya watu wa dini nyingine kuona ya kwamba kumbe uislam huko tofauti kabisa na tunavyoufikiria na ikawa sababu ya wao kuufatalia uislam na mwisho kuingia. Hawa watu wa dini nyingine wako karibu sana na uislam quran inasema hivyo jambo dogo na zuri katika uislam watakaloliona in shaa allah itakuwa sababu ya wao kuingia uislam lakini kwa sasa kidogo inakuwa ngumu ingawa wengine wanaingia alhamdulilah kwa sababu nchi karibu nyingi waislamu wanapigana na kuuana hii inachangia kuwapotosha juu ya dini hii nzuri. Hivi vitendo tukitaka tusitake vinasaidia kuendeleza ukafiri si haya tu kama si wewe au mimi nduguyo leo tuna mambo ya kikafiri majumbani mwetu ambayo yanatutoa katika akida za kiislam,mambo haya ni ya kuyapa kipaumbele zaidi kwani uislam unaanza kwa sisi wenyewe na watu wa majumbani kwetu kwanza kisha ndio utoke nje. Kila jambo na nia na nia yetu si mbaya. Niswamehe kama nimekukosa kwa mawazo yangu ila ndicho allah alichonifungulia au nimekosea mungu pekee ndio amekamilika na tuzidi kuelemishana na kutakiana amani na kheri.

 15. Mh sudi nimekuelewa ila unaposema hadithi inaendana na wakati unamaanisha hii hadithi imepitwa na wakati au,na unaposema tufanye ambayo tunayoyaweza tusioyaweza mungu atatusamehe ndugu yangu kwa hilo naomba uombe msamaha kwa mola wako na usisubutu kulisema tena kwenye maeneo kama haya kwani watu wakifata maneno yk hy utakuwa ushapotosha jamii na dini yao jengine kaka mungu amewasifu wenye kuamini na sio wenye imani dhaifu naomba kaangalie tena hatuwezi kuwa na imani dhaifu km ww wacha tupiganie halali yt.

 16. Narudia tena hatuwezi kujenga kanisa sisi waislam haizuru na tuonekane wabaya kuliko kumuasi mungu, mungu anasema (na usimuasi mungu kwa kumtii kiumbe) sudi mung anasema makafiri wanajifanya wapo karibu na waislam lkn ni wt wabaya sn tunatakiwa tuwe macho tusijisahau wana lao hawa ukaribu wao hauna wema kwetu rudia kaangalie tena kwani sikila anaecheka na ww anakupenda wengine lao moyoni kama nyinyi mnoun’gan’gania muungano lenu liko moyoni sasa tumeshtuka macho wazi uamsho wametuamsha DHULMA BASI TUMECHOKA

 17. Pingback: Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar·

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s