Kesi ya Mchomaji Quran Yatinga Mahkamani

MAMIA ya wafuasi wa Dini ya Kiislam wiki hii walifurika katika Mahkama ya wilaya ya Mwanakwerekwe kufuatilia kesi ya mshtakiwa aliedaiwa kuchoma moto Quran Tukufu na Novemba 16 mwaka huu.

Mahkama hiyo iliyofurika watu ndani na nje ya jengo ilisikiliza mashahidi watatu upande wa mashtaka ambao wote walitoa ushahidi wa kuona tukio na kushuhudia na kushuhudia vitabu hivyo vya Quran ikiwemo msahafu, juzuu na vitabu vya kiisamu vilivyochomwa moto muda mfupi baada ya tukio.

Chini ya muongozo wa waendesha mashtaka, Khamis Jaffar Mfaume, Othman Kassim na Raya Msellem. Mashahidi waliotoa ushahidi wao hapo jana ni Tausi Abdallah (32), Hafidh Khamis (12) na Mzee Said Omar Hamad (57).

Waendesha mashtaka walidai mshtakiwa Ramadhani Hamda Tuma (28) mwenye kabila ya Msukuma mkaazi wa Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja, alitenda makosa mawili. La kwanza ni kufanya kitendo kinyume na kifungu cha 74 (i) (b) Sheria No. 6/2004 Sheria ya Zanzibar na kosa la pili ni kukashifu dini kinyume na kifungu 117 na 27 Sheria No. 6/2004 Sheria za Zanzibar.

Walidai Novemba 16 mwaka huu majira ya saa 2.30 usiku huko Mombasa Wilaya ya Magharibi mshtakiwa alichoma moto hadharani Msahafu na Juzuu pamoja navitabu vya dini ya Kiislamu kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa jamii ya kiislamu.

Katika jambo lililowashangaza wengi mshtakiwa aliiomba mahakama imrejeshe rumande kutokana na hali iliyojionesha ya waumini kuhudhuria kwa wingi mahakamani hapo ambapo alisema no bora arudishwe kwa ajili ya usalama wake.

Hatimaye Hakimu wa Mahkama amekubali ombi ilo na ameiahirisha kesi hiyo hadi Januari 11 Mwakani kusikiliza mashahidi zaidi na mshtakiwa akiwa chini ya ulinzi mkali alirudishwa rumande baada ya Mahakama kuzingatia usalama wake kutokana mazingira yaliopo.

Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, Katibu Ofisi ya Mufti Zanzibar ambaye alikua miongoni mwa waumini waliokuwepo Mahkamani hapo alikuwa aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi na waiachie sheria ichukue mkondo wake Huku akisisitiza utulivu wakati suala hilo linashughulikiw ana vyombo vya sheria.

Wakizungumza nje ya mahakama hiyo waumini hao wameema wateheshimu sheria ichukue mkondo wake lakini wangependa kuwa karibu na keshi hiyo ili kujua hatima ya suala hilo linavyoendeshwa mahakamani hapo ambapo waliahidi kutofanya chochote amabcho kitakuwa kinyme na sheria zaidi ya kusikiliza na kuondoka.

One response to “Kesi ya Mchomaji Quran Yatinga Mahkamani

  1. sinabudi kumshukuru allah mwingi wa rehma , kwa nilijaalia kunipa hali njema .hii ni kawaida yao hawa wahamiaji kutoka tanganyika ,kufanya vitendo kama hivi visivyo vumilika imekuwa kawaida yao kutaka kuhatarisha amani, iliyokuwa imewekwa na wazee wet2 kwa miaka na miaka ,kwanza hawahishimu nyumba za ibada utawaona wakipita mbele ya msikiti ndipo utakapo waona wakiimba nyimbo zao haliyakuwa wanaona waislamu wamo katika sala, sasa hata ule mwezi mtukufu wa ramadhani nao hawauheshimu wanauza vyakula ktk mwezi huo mchana kweupe hiyo yote ni dharau na kejeli wanayoionesha.

Leave a comment