Maalim awataka wananchi kushiriki sensa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na viongozi wa CUF kwa ngazi ya majimbo na Wilaya nne za Pemba katika ukumbi wa Chuo cha Benjamin Mkapa Wete Pemba.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makaazi, ili kuirahishia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa uhakika. Maalim Seif ametoa wito huo leo katika ukumbi wa chuo cha Benjamin Mkapa Wete Pemba alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwa ngazi za Wilaya na Majimbo.

Amesema Sensa ya watu na Makaazi ni muhimu kwa wananchi na serikali kwa ujumla katika kutathmini na kuandaa mipango yake ya maendeleo kwa wananchi, na kuwataka kuachana na mtazamo kuwa suala hilo linaihusu serikali pekee.

Makamu wa Kwanza wa Rais ametoa msimamo huo kufuatia wananchi wengi wa Kisiwa cha Pemba kuwa na mtazamo wa kutaka kususia suala la sensa kwa madai kuwa hawakushirikishwa ipasavyo katika suala hilo.

Sababu nyengine iliyowafanya wananchi hao kutaka kususia suala hilo ni kwa madai kuwa hawawezi kushiriki suala la sensa, huku wakiwa bado hawajatekelezewa haki zao za kisheria ikiwemo kutopewa vitambulisho vya uzanzibari ukaazi.

Amewataka wananchi kupima faida na hasara za kushiriki kwenye zoezi hilo la sensa, na hatimaye waweze kushiriki kikamilifu kwa maslahi ya maendeleo ya nchi.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa ukusanyaji wa maoni kwa ajili ya mabadiliko ya katiba, Maalim Seif amewataka wananchi kuwa huru kutoa maoni yao, na kwamba hakuna atakayeadhibiwa kwa sababu ya kutoa maoni.

“Mimi najua wapo wanaotaka serikali moja, wengine mbili, tatu, nne, na muungano wa mkataba, lakini wengine wanataka waachiwe wapumuwe. Yote hayo ni maoni na kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila ya kulazimishwa, kwa hivyo wakati wenu ukifika nendeni mkatiwe maoni hayo kwa uwazi”, alisisitiza Maalim Seif.

Amesema lengo la serikali ya Tanzania ni kuwa na katiba mpya ifikapo April mwaka 2014, na kufahamisha kuwa kwa Wazanzibari suala kubwa linalowagusa kwenye mabadiliko hayo ni suala la Muungano.

“Zanzibar tunayo katiba yetu ambayo imejitosheleza kwa mambo yetu ya Zanzibar, lakini suala kubwa kwenye mabadiliko hayo kwetu sisi litakuwa ni la Muungano, na hili haliwezi kuepukwa”, alibainisha.

Amesema Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa nchi huru iliyokuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa, na kuelezea haja ya kuwepo kwa Mamlaka kamili ya Zanzibar ili iweze kurejesha kiti chake kwenye umoja huo.

Amewataka wananchi kuangalia maslahi ya nchi yao kwanza katika mchakato wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba, na kuachana na misimamo ya vyama katika suala hili linalohusu maslahi ya nchi.

“Katiba ya nchi ni mali ya wananchi sio ya chama chochote, lakini najua kila chama kina katiba yake na hiyo ndio itabakia kuwa katiba na muongozo wa chama husika, kwa hivyo ndugu zangu naomba tulifahamu hili na tuangalie maslahi ya nchi yetu kwanza”, alifahamisha.

Makamu wa Kwanza wa Rais alitumia fursa hiyo kutoa mkono wa pole kwa wananchi walioathirika kutokana na ajali mbaya ya boti ya Mv. Skagit ilisababisha vifo vya watu kadhaa.

Amewataka wananchi kuweka imani zao kuwa suala hilo limetokana na mipango ya Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mtu angeweza kulizuia lisitokee.

Katika hatua nyengine Maalim Seif amempongeza aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasilino Mhe. Hamad Massoud Hamad kutokana na kitendo chake cha kijasiri cha kuamua kujiuzulu nafasi hiyo.

Amesema kitendo hicho cha kuwajibika kisiasa kimemjengea heshima yeye mwenyewe, chama chake na taifa kwa ujumla, kitendo ambacho linapaswa kuingwa na viongozi wengine wa nchi iwapo litatokea jambo lolote linalogusa maslahi ya wananchi.

“Mhe. Hamad amekuwa mwalimu wa viongozi wa Afrika, kwani viongozi wa Afrika hawana utamauni huo hata likitokea jambo gani, lakini yeye ameamua kujisafisha licha ya kuwa hakuwa na kosa kwa sababu safari ili haikuanzia Zanzibar”, alifahamisha Maalim Seif

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe. Hamad Massoud Hamad ambaye alikuwa akishikilia nafasi hiyo ya uwaziri, amesema aliamua kuachia nafasi hiyo siku chache baada ya tukio, ili kujijengea heshima kisiasa.

“Niliamua kujiuzulu nafasi ile kwa nia njema, sikulazimishwa wala kupokea shinikizo kutoka kwa mtu yoyote”, alisema Hamad Massoud.

Alisema kwa sasa akiwa Mwakilishi wa wananchi na kiongozi wa chama hicho, ataendelea kushirikiana na viongozi na wanachama katika kukijenga zaidi chama hicho ili kiweze kufikia malengo yake iliyojiwekea.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais aliwataka wananchi wa kisiwa cha Pemba kuendeleza utamaduni wa kufutari kwa pamoja ili kuongeza upendo miongoni mwao.

Maalim Seif alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti baada ya kushiriki katika futari ya pamoja aliyoiandaa kwa wananchi wa mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba iliyofanyika Ukumbi wa kiwanda cha makonyo Wawi na viwanja vya Ikulu ya Wete.

Advertisements

6 responses to “Maalim awataka wananchi kushiriki sensa

 1. MAALIM HEBU SEMA KWELI watujua wazi kuwa sensa mara hiyi hamna . kinachokupa kupiga debe nini tena au na wewe unawatafuta wazanzibari wakuharie

 2. Asalam aleykum,
  umoja ni muhimu sana katika jamii ya kiislamu na ni njia pekee itakayoleta ukombozi. Masheikh zetu walishatoa tamko kwamba hatutoshiriki sensa. Kabla ya kutoa hilo tamko jumuiya zote zilikaa shura na kufikia muafaka kwamba hatutoshiriki sensa. Kama unakumbuka tamko la kutoshiriki sensa lilitolewa kwa pamoja na lile tamko la kushiriki kwenye maoni ya katiba mpya. Sheikh Mselemu (AMIRI) aliwakumbusha tena waislamu kutoshiriki sensa hii juzi kipindi cha dua. NI WAJIBU WETU KUFUATA MAELEKEZO YA MASHEIKH ZETU.
  KULE TANGANYIKA KULIKUWA NA MZEE ANAITWA TAKADIRI. ALIWATAHADHARISHA WAISLAMU KWAMBA NYERERE ATAKUJA KUWABAGUA WAISLAMU. WAKAMWONA HANA MAANA. WALIMTENGA ILI WAENDELEZE SIASA ZAO ZA TANU. NA MZEE HUYU ALIVYOKUFA, WAISLAMU WALIKATAA KUMZIKA, MPAKA NYERERE ALIVYOWAAMBIA WAENDE WAKAMZIKE. YANI WAISLAMU WANASAHAU MAELEKEZO YA DINI YAO, MPAKA KAFIRI AWAELEZE WAFANYE HIVYO. MADHARA YALIYOWAFIKA WAISLAMU TANGANYIKA KILA MWENYE MACHO NA MASIKIO AMEYAONA NA AMEYASIKIA, NA MADHARA YAMEFIKA MPAKA HUKU ZANZIBAR. KAMA WAISLAMU WA TANGANYIKA WANGEFUATA KAULI YA MZEE TAKADIRI WANGEKUWA NA TAHADHARI “RIGHT AT THE BEGINNING”. LAKINI WAPI BWANA, WAKALEWESHWA NA USEMI “SIASA NA DINI HAVIINGILIANI” , MARA TUNAFUATA SERA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA, WAKATI NYUMA YA PAZIA ANAUIMARISHA UKATOLIKI KWA GHARAMA YEYOTE.
  CHA KUFAHAMU NI KWAMBA KUTOFANYA JAMBO FULANI NI LAZIMA UTAKOSA FAIDA YA HILO JAMBO KWA WAKATI HUO, WATU WA UCHUMI WANAITWA “OPPORTUNITY COST” KAMA SIKOSEI. HATA ALLAH (SWT) ANASEMA KAMA UNATAKA DUNIA TUTAKUPA LAKINI KESHO AHKERA HUNA KITU.
  UKIJA KWENYE SUALA LA SENSA NI KWAMBA KWA SASA MASLAHI HAKUNA KWA WAISLAMU KUWE ZANZIBAR AU KUWE TANGANYIKA. MASHEIKH ZETU WALITOA SABABU MBILI ZA KUTOSHIRIKI:
  1. KUWAPA SUPPORT WAISLAMU WA TANGANYIKA. NA KULE TANGANYIKA PIA KULIFANYIKA SHURA PALE DODOMA, KUTAKA SERIKALI IWEKE KIPENGELE CHA DINI KATIKA KUHSABU WATU NA PIA WAHAKIKISHE KUWE NA UWAKILISHI SAWA KUTOKA KATIKA KILA DINI KWA WAFANYAKAZI WA KUHSABU SENSA. SERIKALI ILIKATAA BILA SABABU. RAISI KIKWETE AKASEMA SENSA YANYE KIPENGELE CHA DINI HAIJAWAHI KUFANYIKA, WAKATI ILISHAWAHI KUFANYIKA MWAKA 1957 NA MWAKA 1967. MUFTI WA BAKWATA ALIKUWA KWENYE HII SHURA NA AKAUNGA MKONO KUTOSHIRIKI SENSA, LAKINI BAADA YA SIKU KADHAA AKASEMA WAISLAMU WASHIRIKI SENSA. WANAVYUONI WAKAMWELEZA MUFTI WA BAKWATA KWAMBA TULIKAA SHURA NA TUKATOA MSIMAMO, NA HATUJAKAA SHURA NYINGINE KUBATILISHA ILE KAULI TULIYOITOA. KWA HIYO WAISLAMU KWA UJUMLA HAWATOSHIRIKI SENSA KUTOKANA NA DHULMA INAYOENDELEA. KWA HIYO TUUNGE MKONO KWA HILO KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO, NA INSHAALLAH SENSA YENYE HAKI YAWEZA FANYIKA WAKATI MWINGINE WOWOTE HATA IKIWA MWAKANI.
  2. MASHEIKH ZETU WALISEMA HATUTOSHIRIKI SENSA MPAKA ZANZIBAR IKO HURU, IMEPUMUA, UHURU UKIPATIKANA MWAKA HUU HATA MWAKANI SENSA WAWEZA KUFANYA. BY THE WAY KUNAWEZA KUWEKA DATA BASE YA WATU WOTE NA INAKUWA UP-TO-DATE. MTOTO AKIZALIWA TU RIGHT AWAY ANAINGIZWA KWENYE DATA BASE. HAKUNA HAJA YA KUFANYA SENSA PHYSICALLY. KWANI KUFANYA PHYSICALLY ERROR NI KUBWA KULIKO KUWA NA DATA BASE KWENYE COMPUTER AMBAYO KILA WAKATI DATA ZAKE ZINAKUWA HAI
  KWA HIYO NDUGU WAISLAMU, KUTOSHIRIKI SENSA NI KATIKA IBADA KWA SASA KWA KUWA TUNAPINGA DHULMA.
  MIYE BINAFSI NIKO BEGA KWA BEGA NA MASHEIKH NA SI VINGINEVYO, UISLAMU IMEJITOSHELEZA KWA KILA HITAJIO. KAMA SHURA ITAKAA TENA NA IKASEMA TUSHIRIKI SENSA HAPA TUTASHIRIKI. LAKINI KWA MSIMAMO ULIOPO SASA KWA MASHEIKH NA WANAVYUONI WANAOTETEA HAKI ZA WAISLAMU MSIMAMO UPO PALE PALE KUTOSHIRIKI. NA MIYE KAMA NI MUISLAMU NINAE MUOMBA ALLAH ANIJAALIE LA KHERI DUNIANI NA AKHERA SITOSHIRIKI HIYO SENSA INSHAALLAH.
  ALLAH ATUJAALIE MWISHO MWEMA NA ATUPE NGUVU TUWASHINDE MAKAFIRI, AMIIN

 3. maoni yenu mazuri sana na tunapaswa kuyaheshimu. Suala la kufuata maamiri wetu ni jambo la msingi sana. Lakini mm mawazo yangu yapo tafauti na wale wanaodai kuingizwa kipengele ktk maswali ya sensa. Mtashangaa kusikia hvyo ila muendelee kusoma maoni yangu. Kuingizwa kpengele cha dini kunaweza kuleta matatizo kwa waislam hasa kwa upande wa Tanganyika. Mm ninao uzoefu japo kidogo ktk mambo haya ya sensa, katika zile karatasi zao znaitwa madodoso ambazo baadae ztatiwa ktk mashine ambayo haisomi maneno bali husoma code za namba, e.g muislam code 1 mkristo 2 n.k. Na ni wazi kuwa makarani wa sensa wengi Tanganyika watakuwa wakristo. Na lile dodoso anaehojiwa huwa haoni kinachojazwa na karani. Sasa mkristo akimuliza muislam dini na akajibu muislam, unadhani atamjazia no. 1? Hapana, lazima atamjazia 2 ili wakristo waonekane wengi. Tuzngatieni hilo jamani.

 4. Kuhesabiwa hakutengui msimamo wa kudai Zanzibar kuwa Mamlaka na Mamlaka yake. Katika kipindi hiki cha kudai haya hili la kuhesabiwa lisifanywe ni miongoni mwa shuruti hizo. Tatizo kubwa ni kuwa kuhesabiwa kutafanywa katika level ya household ni ni shida kujua ni nani amekuli au hakukubali kuhesbiwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s