Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa

Professa Issa Shivji akiwa katika moja ya mikutano iliyotayarishwa na kigoda cha Mwalimu Nyerere katika chuo kikuu cha Dar es Salaam

Sikuwahi kusikia mahali popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti “anataka” Muungano uvunjwe, yeye kama yeye. Sasa huyu mwandishi Datus Boniface halipata wapi ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia huyu wa Kitanzania, hata kama ni Mzanzibari pia? Uandishi wa habari wa aina hii ya Datus Boniface ni wa kusikitisha sana.

Tamko la DKt. Lwaitama kuhusu habari ya “Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe”
11/08/2012
JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari uliojiweka wazi katika taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na mwandishi wa gazeti moja la kila siku  (Tanzania Daima la tarehe7 Agosti 2012), Datus Boniface. Huyu mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa walithubutu kusema uongo kuwa eti “Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano..” Tena, mwandishi huyu na wahariri walioruhusu habari hiyo ichapishwe wakaenda mbali zaidi na kutumia kichwa cha habari kilichosema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’.

Nafahamu Prof Shivji tayari ameisha toa tamko juu ya upotoshwaji wa hali ya juu uliobebwa na kichwa cha habri hiki na makala nzima ya mwandishi huyu mwenye aina yake ya ujuzi wa kuandika habari, Datus Boniface. Mimi katika tamko langu sitojisemea mimi tu kama alivyosema Prof. Shivji katika tamko lake. Nitajaribu kueleza kile ambacho nilidhani kilizungumzwa na kila aliyechangia katika Mazungunzo ya yale ya Kifungua Kinywa ( Breakfast Talk), Jumatatu tarehe 6 Agosti 2012, yaliyofadhiliwa na Baraza la Habari Tanzania( MCT).

Wakwanza kuzungumza alikuwa Prof Abdul Sheriff na aliainisha kile alichotaka kibainike kama historia a sababu za kuwepo Muungano katika ya Tanganyika na Zanzibar. Alieleza kile alichotaka kieleweke kama mapungufu ya kisheria katika mchakacho wa kuwepo Muungano. Pia alieleza kile alichotaka kieleweke kama Muungano kukosa kuwa na uhalali wa kisiasa ( political legitimacy) kutokana na ushirikishwaji hafifu wa viongozi wa Serikari ya mapinduzi wa wakati huo na wananchi kwa ujumla. Akahitisha maelezo yake kwa kusema Wazanzibari walio wengi sasa hivi wamefikishwa mahali ambapo wanatamani kutumia mchakato wa kuandika katiba mpya uliozinduliwa hivi karibuni unaoongozwa na Jaji SJoseph Sinde Warioba kujadili Muungano kwa kina na kuingia kwenye maridhiano mapya juu ya kama Muungano uendeleee kuwepo na kama ndiyo kwa mfumo wa serikali ngapi. Ilikuwa wazi kuwa Prof Sheriff alikuwa haamini kuwa walikuwepo Wazanzibari wengi waliokuwa tayari kuendelea na Muungano wa serikali mbili kama wa sasa. Sikuwahi kusikia mahali popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti “anataka” Muungano uvunjwe, yeye kama yeye. Sasa huyu mwandishi Datus Boniface halipata wapi ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia huyu wa Kitanzania, hata kama ni Mzanzibari pia? Uandishi wa habari wa aina hii ya Datus Boniface ni wa kusikitisha sana.

Aliyezungumza wa pili alikuwa mimi, Dkt Azaveli Lwaitama. Mimi kazi yangu ilikuwa kujibu hoja (Discussant) za mzungumzaji mkuu ambaye kwa kweli alikuwa Prof. Abdul Sheriff peke yake. Kwanza nilimkosoa ndugu yangu, Mtanzania mwenzangu, Prof Abdul Sheriff, kwa kuomba wote tukubali kuwa viongozi wetu waliotuunganisha na kusimamia kuzaliwa taifa letu la Tanzania walikuwa watu walioongozwa na dhamira safi iliyochimbuka katika kuwa waumini thabiti wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika ( Pan Africanism) ya kutaka kuwaunganisha watu wa dola zetu hizi za watu waliokuwa wamekusanywa pamoja na wakoloni na kupachikwa majina kama Tanganyika na Zanzibar bila ridhaa ya wakazi walikuwa ndio wengi wa sehemu hii ya Bara la Afrika. Nikaeleze jinsi mbavyo mwelekeo wa viongozi hawa haukuwa wa kufungwa sana na matakwa ya kisheria bali na kile walichokiamini kingesadia kufanikisha lengo la kuwaunganisha Waafrika wote bila kujali kabila ( tribe) au uzawa ( race). Nikatolea mfano wa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoshirki katika kuimiza kuungana kwa Shiraz Association na African Association kuzaa Afro Shiraz Party ( ASP) tarehe 5 Februari 1959, siku na mwezi ambavyo mwaka 1967 vilikuja kuwa siku na mwezi wa kuzaliwa Azimio la Arusha , na mwaka 1977 vilikuja kuwa ni siku na mwezi kilizaliwa Chama cha Mapinduzi kutokana na kuunganisha Tanganyika African National Union ( TANU) na Afro Shiraz Party ( ASP).

Nilisisitiza kuwa leo tunaweza kuyaona wazi mapungufu makubwa katika taratibu za kisheria zilizogubika mchakato wa kuunda Muungano lakini si vizuri kusema eti tuukatae Muungano kutokana tu na mapungufu haya ya kisheria. Si vizuri na si busara kusahau kuwa Muungano uliundwa kwa sababu za dhamira ya kuunganisha Washiraz, Waafrika, Waarabu, Wahindi na Wazungu na kuwaweka pamoja kama Waafrika waumini wa Umajumui wa Kiafrika (Pan Africanism), wawe wa dola lilosimikwa na wakoloni la Zanzibar au dola lililo simikwa na wakoloni la Tanganyika. Mwalimu Nyerere na Mzee Abedi Karume walisukumwa na kutaka kuunda taifa ya Kiumajui wa Kiafrika jipya la TANZANIA, baada ya kuona Mzee Jomo Kenyata wa Kenya na Ndugu |Milton Obote wa Uganda hawakuwa tayari kwa wakati huo, mwaka 1964, kuunda dola jipya ambalo lingeongozwa na itikadi ya vuguvugu la utaifa wa Umajumui wa Kiafrika ( Pan Africanist nationalist movement) la Shirikisho la Afrika Mashariki.

Kwa waasisi hawa wa Muungano taratibu za kisheria hazikupewa kipaumbele bali dhamira safi ya kutenda liloonekana kuwa la manufaa kwa wananchi walio wengi wa sehemu hii ya Afrika. Tukumbuke kuwa Mzee Karume na Mwalimu Nyerere walikuwa wanafanya kazi katika mazingira ya kivuli cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964 mwezi mmoja baada ya Uhuru wa Zanzibar tarehe 9 Desemaba 1963 uliopatikana kwa kufuata taratibu za kisheria lakini matokeo yake yakapinduliwa kijeshi tarehe 12 Januari 1964 kwa vile taratibu hizo za kisheria zilitumika kukwepa kupatikana kwa ridhaa ya kisiasa ya walio wengi katika kupatika Uhuru ule wa Zanzibar wa Desemba 1963!!

Nilitumia muda kuelezea jinsi ambavyo tabaka la mabepari uchwara Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar lilivyokuwa na ushawishi mkubwa juu ya uongozi wa serikali ya Muungano na serikali ya Zanzibar. Nilianisha kuwa hii ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya kukosekana kwa wanasiasa madhubutu wenye ushwaishi ndani ya CCM ya miaka kuanzia 2006 wenye utashi wa kutetea dhamira ya waasisi wa Muungano waliokuwa waumini wa itikadi ya Ujamaa na Umajumui wa Kiafrika. Nikabainisha kuwa utetezi wa mfumo wa serikali unatolewa kikasuku na viongozi wa juu wa CCM ya wanamtandao ya kuanzia mwaka 2006 ni utetezi wa kinafiki kwani juhudi za makusudi za kuutetea Muungano kwa vitendo hazikuwa dhairi. Niliorodhesha nyanja kama uteuzi wa wakuu wa vyombo vya dola kama polisi na jeshi la wananchi au Benki Kuu ambao ungekuwa umefanywa kwa lengo la kulinda Muungano hata kero za Muungano zinazotajwa na wanasiasa wa Zanzibar zingekuwa pungufu.

Nilisahau hata kutaja jinsi wana-CCM wa kundi la Mtandao walivyozima kwa njia za hila na hiyana kupatikana kwa Rais wa awamu ya Nne Mzanzibari, yaani Dk. Salim Ahamed Salim mwaka 2005. Nilibainisha kuwa hii ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya watetezi wa dhati wa Muungano wa Serikali Mbili wenye kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere kama mimi, wanaosukumwa na kuwa waumini wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika, kukikri kuwa kwa sasa ukitaka kulinda Muungano katika mazingira ya sera za uchumi na siasa za uliberali mambo leo lazima kukuballi kuwepo kwa Muungano wa serikali Tatu.

Nilitumia muda mrefu zaidi nikieleza kufurahishwa kwangu na msimamo wa mwanasiasa kijana wa chama cha Chadema, Mheshimiwa Zito Kabwe, kuelezea, katika gazeti la kila wiki la Fahamu hivi karibuni, kuwa mwalimu wake wa nje ya darasa Dk Lwaitama sasa alikuwa anaunga mkono dhana ya kutafuta kuulinda Muungano kwa kuridhia kuwepo kwa Muungano wa serikali Tatu. Nilielezea jinsi Mheshimiwa Zito alivyofafanua kuwa dhana hii ya kuulinda Muungano kwa kukubali sera ya serikali Tatu amekuwa nayo kwa muda sasa na ingelenga kuwepo kwa Serikali na Bunge la Muungano. Serikali hii ya Muungano ingekuwa ndogo, yenye kushughulikia mambo ya Muungano machache. Mimi mwenye nilielezea kuwa niliishapendekeza mahali pengine kuwa labda Serikali ya Muungano ingekuwa na wizara kuu zisizozidi nne au tano zenye uteuzi wa mawaziri wa sawa kwa sawa, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, huku Urais wake ukiwa kwa zamu.

Wizara kuu zingelihusu mambo ya ndani ( yaani uhamiaji, uraia, polisi), mambo ya nje ( yaani ulinzi wa nje na mahusiano ya kimataifa), uratibu wa mambo ya fedha na mipango ya uchumi ( yaani sarafu, sera ya uwekezaji, mambo wa ushuru, na kodi), na miundo mbinu inayoitaji uwekezji mkubwa( teknohama, uzalishaji na usambazaji umeme, usafiri wa bahari na maziwa, reli, na anga). Hata haya mambo ya muungano mengi yake baadaye yangelishugulikiwa na Jumuya ya Afrika Mashariki kadili itakavyo kuwa inaimarika kuelekea kuwepo kwa Shirikisho la Afrika Mashariki.

Nilielezea pia jinsi Mheshimiwa Zito alivyokuwa amependekeza kuwa kungelikuwepo serikali mbili za Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar zilizo sawa kila moja ikiongozwa na Waziri Mkuu na kila moja ikisimamiwa na Baraza la Wawakilishi. Nikaeleza jinsi Mheshimiwa Zito alivyopendekeza katika uchanguzi mkuu kungewepo uchanguzi wa Rais na Makamu wa Rais Mwenza wa Serikali ya Muungano na Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano pamoja na Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Tanzania Bara na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Tanzania Zanzibar . Muda mwingi niliutumia katika kuunga mkono mawazo haya ya awali ya mwanasiasa huyu kijana na mzalendo , Zito Kabwe nikionesha furaha yangu kuwa mwanasiasa kijana wa chama cha upinzani cha Chadema kama huyu ameweza kuona mbali kiasi hiki kuliko viongozi wa sasa wenye ushawishi ndani ya chama kilichouasisi Muungano cha CCM.

Nakumbuka katika mjadala uliofuata mchango wangu mwanahabari mwanandamizi amabaye ni Mhariri Kiongozi wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile, alionyeshwa kuvutiwa mapendekezo haya ya jinsi ya kunusuru Muungano nay eye kupendekeza kuwa ingekuwa vizuri ikiwa Tanzania Zanzibar itaitwa Tanzania Visiwani!. Lengo la wachangiaji wote siku hiyo lilionekana kutafuta njia za kuzidi kuimiza kuukubali utambulisho wa kujiita Watanzania, iwe mtu ni anatokea kuwa mkazi wa Tanzania Bara au mkazi wa Tanzania Zanzibar na polpole kufifisha mawazo ya kubanguana kwa misingi ya Utanganyika na Uazanzibari. Mimi nilisisitiza kuwa utambulisho wa kwa misingi ya Utanganyika na Uazanzibari, majina tuliyopachikwa na wakoloni, ulikuwa ni utambulisho uliokinzana na kuwa waumini wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika, ambayo ndiyo ilituunganisha katika kupigania uhuru wa bendera miaka ya 1940 na 1950.

Kwa lengo hili hili la kuufanya utambulisho wa Utanzania ushamili zaidi na zaidi, na kufifisha mwelekeo wa kubanguana kwa misingi ya Utanganyika na Uazanzibari, pendekezo langu liloonekana kuridhiwa katika andiko la Mheshimiwa Zito lilikuwa kuwa Mawaziri Wakuu wa Seriakali za Tanzania Bara an Tanzania Zanzibar wangeteuliwa na vyama vya siasa vilivyoandikishwa ki- Muungano kama sasa kutegemea ni chama kipi au muungano wa vyama vipi ungekuwa umepata viti vingi au kura nyingi katika changuzi za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi husika.

Pendekezo langu lilikuwa kuwa kutokuwepo kwa uchanguzi wa wakuu wa serikali ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kungesaidia katika kupunguza, polepole, ushabiki na hamasa za kisiasa zinazojikita kwenye utanmbulisho wa Utanganyika au Uzanzibari. Haya yote lengo lake lingekuwa kutafuta njia za sasa za kuendelea kuwaenzi waasisi wa Muungano, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume, ambao dhamira yao ilikuwa nzuri ya kuunganisha Waafrika wote bila kuwabagua kwa misingi ya kabila, rangi, dini, uzawa au upande wa bahari ya Hindi mtu alikokuwa anaishi kwa sasa au hapo nyuma.

Nilisisitiza umuhimu wa itikadi ya Umajumui wa Kiafrika kwa kusema hata kama itatokea ushawishi wa tabaka lenye kutaka kuvunja Muungano wakawashauwishi Wazanzibari kwa sasa kuridhia kuuvunjika kwa Muungano basi Watanzania Bara waendelee kujiita Tanzania Bara na Wazinabari waendeleee kujiita Tanzania Zanzibar, kama Wasudani Kusini walivyoridhia kujiita Sudani Kusini licha yakupata uhuru. Mapendekezo yote haya yangesaidia kuimiza kuendeleza juhudi za kusimika utambulisho wa Kiumajumui wa Kiafrika wa U-Tanaznia ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Hii nngekuwa kama ilivyo kwa kama kuendelea kuwepo utambulisho wa Sudani kwenye utambulisho wa Wasudani wote, Kusini na Kazikazini!!!! Sielewi uandishi wa Datus Bonaface ni wa aina gani uliomruhusu kusuka maneno kutoka kwenye mchango wangu hapo juu wakusema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’ au eti “ Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano..” Inasikitisha sana kuwepo waandishi wa aina hii na wahariri wanaoruhusu uchapishwaji wa uongo wa kiwango hiki!!!

Wachangiaji kadhaa walifuata mchango wangu kabla ya Prof Shiji kutoa mchango wake ambao ameulezea vizuri sana katika tamko lake kuhusu upotoshwaji wa hali ya juu ulifanywa na mwandishi Datus Bonaface pamoja na wahariri walioruhusu habari hii ya uongo kuchapishwa. Laiti kama wahariri wale wangeomba ushaidi wa kanda ya kilichozungumza wangegundua mara moja kuwa mwandishi Datus Bonaface ni mwandishi wa ajabu kweli kweli. Naliambatisha Tamko la Prof. Shivji kama alivyolitoa, na nalo bila shaka yeyote ninaonesha wazi kuwa Prof. Shivji kamwe hakutamka mahali pale kitu chakumfanya mwandishi aseme eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’ au eti “ Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano..” Inasikitisha sana kuwepo waandishi wa aina hii na wahariri wanaoruhusu uchapishwaji wa uongo wa kiwango hiki!!!

Mwl. Azaveli Feza Lwaitama
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Jukwaa la Dira Afrika Mashariki
&
Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu,
Kitengo cha Falsafa,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com
+255784432696/ +255782807728
Agosti 11, 2012
Tamko la Prof. Shivji kuhusu habari ya “Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe”
09/08/2012
JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimeshitushwa na gazeti moja la kila siku  (Tanzania Daima la tarehe7 Agosti 2012) lilonipandikizia maneno katika kichwa chake cha habari kwamba ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’. Siwezi nikamsemea Dr. Lwaitama lakini kwa upande wangu sijasema wala kumaanisha kwamba ‘Muungano uvunjwe’.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/08/tamko-la-prof-shivji-kuhusu-habari-ya-shivji-lwaitama-wataka-muungano-uvunjwe.html#ixzz23DFLG3lr
Mosi, kwamba wasomi, wakiwemo wanahabari, wana jukumu zito la kutokupinda  ukweli wa kihistoria kwa lengo la kuhalalisha mtazamo na msimamo wao kuhusu  Muungano. Nikatoa mfano wa jinsi Merehemu Sheikh Karume anavyodekezwa  katika msimamo wake juu ya Muungano. Wasemaji hapa bara wanamsifu kwa kuwa  muasisi mwaminifu na mshabiki mkubwa wa Muungano tangu mwanzo. Huko  Zanzibar, wasemaji hawachoki kumnukuu Mzee Karume kuwa tangu mwanzo yeye  hakutaka Muungano isipokuwa alikuwa anafikiria Shirikisho.

Wanaendelea kusema kwamba aliposaini Mkataba wa Muungano, Mzee Karume alifikiri kwamba anasaini Shirikisho la Serikali tatu, lakini kutokana na kiwango cha  elimu yake hakuelewa vizuri mantiki na maana ya alichokuwa anasaini.

Nikaendelea kueleza kwamba maelezo haya yote mawili hayaungwi mkono na ushahidi wa kihistoria. Ukweli ni kwamba, Mzee Karume aliingia katika Muungano kutokana na hesabu zake mwenyewe za kisiasa. Muungano kwake ulikuwa njia ya kuondoa upinzani, au upinzani tarajiwa, wa utawala wake. Yaani ilikuwa ni tendo la mwanasiasa yeyote yule kudumisha utawala wake (political survival).

Na kwa watawala wote wa Zanzibar waliomfuata, wakiwemo wa upinzani, ndivyo ilivyokuwa. Wamekuwa wakitumia mwavuli wa muungano wakati utawala wao uko hatarini na kushawishi wananchi wao dhidi ya muungano wakitafuta umaarufu wa kisiasa.

Nikitoa mfano nikasema kwamba kuna taarifa kwamba chama kimoja huko Zanzibar kinapandikiza pendekezo la ‘muungano wa mkataba, sio wa katiba’ bila ya kueleza waziwazi maana yake. Ukweli ni kwamba huwezi ukawa na muungano wa mkataba bila kwanza kuuvunja muungano. Kwa hivyo, wanachoshawishi moja kwa moja ni kuuvunja muungano. Basi waseme hivyo badala ya kujificha nyuma ya pazia la ‘muungano wa mkataba’.

Jambo la pili nililorudia ni kwamba tuliangalie suala zima la muungano kwa mtazamo na maslahi na matakwa ya Umma wa Zanzibar na Umma wa Tanzania bara, hususan matabaka ya hali ya chini. Katika hali yao kimaisha – kiuchumi na kisiasa – hakuna tofauti kati ya wananchi wa Zanzibar na wananchi wa Tanzania bara. Uduni wa hali yao ni uleule; ukosefu wa ajira ni uleule; kutokuwa na mfumo wa dhati wa demokrasia unaojali walalahoi ni kulekule.

Kwa hivyo, umuhimu kwao ni mshikamano wao kuboresha mifumo ya uchumi na siasa. Wasiburuzwe na wanasiasa na vyama vyao kwa maslahi yao binafsi ya muda  mfupi ya kudumisha, au kuingia kwenye, utawala.

Jambo la mwisho nililogusia ni kwamba kiini cha suala la muungano si idadi ya serikali (mbili au tatu) bali ni mgawanyo wa madaraka (distribution of power) kati ya  dola la Zanzibar na dola la Muungano. Na katika hili kila muungano duniani ni wa kipekee kutokana na hali halisi yao ya kihistoria na uwiano wa kisiasa. Sisi pia tukiwashirikisha wananchi kikamilifu na tukaelewa vizuri matakwa yao tunaweza kubuni muundo wetu wa muungao ambao ni wa kipekee bila kujali idadi ya serikali.

Nimeona niweke wazi mtazamo wangu kwa sababu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa na hulka ya kupotosha mambo kutokana na ushabiki wao bila kujali madhara  yanayoweza kutokea.

Mwishoni ningependa kusema kwa dhati kwamba uvunjaji wa muungano hauwezi kuwa kwa manufaa ya walio wengi. Ukweli ni kwamba unaweza ukasambaratisha  nchi na jamii zetu pande zote mbili za muungano. Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na  Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo.

Kama alivyosema Mwalimu, ukishaonja nyama ya mtu basi utaendelea kumtafuna.

Issa Shivji
Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Agosti 8, 2012

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/08/tamko-la-prof-shivji-kuhusu-habari-ya-shivji-lwaitama-wataka-muungano-uvunjwe.html#ixzz23E7prLao

Advertisements

19 responses to “Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa

 1. Pingback: Alichokisema Dkt. Lwaitama na Prof. Shiviji ni hiki hapa·

 2. Sio lengo la Wazanzibar kutokomeza uzanzibari wao,sisi tunajivunia uzanzibari wetu kuliko utanzania ambao ulikuja kwa njia ya kinyemela.
  Hatuwezi kukubali kupoteza utaifa wetu na kujididimiza katika mikono ya Tanganyika bila kujuwa mwisho wake.
  Kwa mawazo yangu na wazanzibari waliowengi kuunusuru muungano huu nikufanya ushirikiano wa mambo machache ambayo hayataingilia mambo ya ndani ya nchi nyengine.
  Pia wizara za ndani na nje zisiwe katika kapu la muungano kwasababu uwiyano wa watu katika nchi mbili hizi haufanani kabisa.
  Tunataka tuweke utaratibu wa pasport baina ya Tanganyika na Zanzibar ili kupunguza uingiaji wa watu kiholela kutoka sehemu mbali mbali za afrika ikiwemo Tanganyika.
  Tunaomba viongozi wetu wasiendelee kuamua masuala yanawagusa wananchi kwa kuzingatia maslaha yao binafsi.
  Kwapamoja tunategemea kuwa haki itapatikana pindi wananchi wa visiwani wakipatiwa fursa ya kura ya maoni na kuulizwa aina ya muungano wanaotaka au kama wana maamuzi mengine ambayo wanayataka.
  Huika uhuru wetu,huika zanzibar na visiwa vinavyotuzunguka.

 3. UNASIKITIKA NINI NA WAANDISHI WOTE WA TANGANYIKA HUU NDIO UANDISHI WAO WANAOUJUA? MARA NGAPI WAMEANDIKA HABARI ZA UONGO NA ZA KUBUNI DHIDI YA UAMSHO NA ZANZIBAR HASA PALE ILIPOTOKEA KUCHOMWA KWA MAKANISA. TULISEMA KUA HWA WAANDISHI NI WAONGO LAKINI KWA KUA LILIKUA NI ZANZIBAR NA UAMSHO YAKAPUUZWA. SASA YANAWARUDIA WENYEWE NA MTAWEZA KUONA NI KIASI GANI TANZANIA WAANDISHI WA HABARI NI WACHACHE MNO. AHMED RAJAB, ULIMWENGU, RIOBA, SALIMSALIM NA IDRISSA. WALIOBAKIA WOTE NI WAGANGA NJAA TU

 4. Ni momi kipofu kiasi gani asiyeona mapungufu ya muungano huu wa Tanzania ambapo unaonekana wazi wazi kunufaisha upande mmoja wa Tanzania bara. ni dhulma iliyoje kwa watanganyika kukosa chombo cha maamuzi na kutumia kivuli cha muungano kuwadhulumu Wazanzibar kiasi kwamba Wazanzibari kukosa mwelekeo na kutamani kuaza maisha nje ya muungano? ni kutokana na dhulma ya kisiasa na kiuchumi wanayotendewa na wezao wa Tanganyika hivi tuseme Zanzibar hakuna mtu mwenye sifa ya kuwa Rais wa muungano, ama mkuu wa majes

 5. waliosema ni kweli muungano uvunjike unafkiri nn tena sasa hauwezi ukawa una ng’ombe 100 ukaungana na mwenye ng’ombe 10 lazima mwenye kidogo atapelekesho kwasababu anakidogo watuache WATUACHE TUPUMUEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE RESPECT IMPOTENT

 6. zanzibar ni kwanza mambo ya tanzania visiwani hapa hakuna, jina Zanzibar halikuletwa na wakoloni kama mjinga lwaitama anavyodai,, Zanzibar ni jina kongwe na lilikuwepo tangu karne ya tatu,,ambapo ilifika hadi kuitwa ZANJI EMPIRE,, nadhani tanganyika ndio iliyoletwa na wakoloni wa kijerumani, kama lwaitama hafahamu mwambieni hivyo. Kwetu sisi ZANZIBAR ni kwanza mambo mengine baadae.

 7. MIMI HUA NAPATWA SANA NA MAPROFESA NA WASOMI WA TANZANIA KAMA HAWA AKINA SHIVJI NA LWAITAMA. WANAPOTOA PAPERS ZAO UTASIKIA WANAMNUKUU NYERERE AS IF HUYU NYERERE ALIKUA HAKOSEI KAMA VILE ASTAGHFIRULLAH ALIKUA MTUME. WHO IS NYERERE AFTER ALL?. NYERERE WAS NON OTHER THAN A DIKTETA SAWA NA MADIKTETA WENGINE WA AFRIKA KAMA IDDI AMIN NA NGUEMA. TOFAUTI YAO NI KUA AMIN NA NGUEMA WALIKUA HAWAJIFICHI NA NYERERE ALIKUA AKIJIFICHA. DIKTETA ANAYEJIFICHA HUA MBAYA ZAIDI MAANA ANAUA NA ANASHREHEKEWA KWA SIFA ZA KUA MWANA DEMOKRASIA. NYERERE SIO SIRI ALISHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUWAPOTEZA WAZANZIBARI WASOMI WA WAKATI ULE KAMA OTHMAN SHARIFF, TWALA, MDUNGI USSI, HANGA NA WENGINE WENGI ILI KULAZIMISHA MUUNGANO KWA KUWA ALIJUA KUA WASOMI WALE WALIKUA NI KIKWAZO. WASOMI HAWA WANAPOMTAJA NYERERE WANATUTIA SISI WAZANZIBARI KICHEFUCHEFU KWANI WANAVYOMUONA WAO NYERERE NA TUNAVYOMUONA SISI WAZANZIBARI NI TOFAUTI KABISAAAAA. TUACHENI TUPUMUEEEEEEEE..

 8. Me ckubali km nyinyi Watanganyika Mmesoma napinga hasa suala hilo na km mmesoma bac ni kama Mmetia maziwa kwenye chupa ya mafuta ya taa, yaani nyinyi Mnasema Mh Karume aliupenda Muungano? Msitudanganye Na huyo Nyerere alijifanya anaakili sn na kumrubani Mzee karume mbona Kenyata kamshindwa? na Mfute Mawazo kua Zanzibar ni Tanzania

 9. Pingback: Tetesi: Kutoka Zanzibar : Tanganyika yakalia Billions za Zanzibar [Climate Change]·

 10. Nyie pigeni debe tu lakini sisi wazanzibar muungano huu hatuutaki. Tunataka Zanzibar iwe huru na mamlaka yake kamili. Tunataka tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar. Pawe na paspoti baina ya zanzibar na Tanganyika, sanjari na hilo tunataka pawe na kitambulisho cha uraia wa Zanzibar. ZANZIBAR BILA YA MUUNGANO INAWEZEKANA. HATUUTAKI MUUNGANO.

 11. KWA SISI WAZANZIBARI HATUSIKII TENA LOLOTE ZAIDI YA MTUACHE TUPUMUE. HAYA MMEYAPALILIA WENYEWE KWA KUTUDANGANYA NA KUTUNYONYA NA MWISHOWE KUCHUKUA KILA KITU CHA ZANZIBAR NA KUKIFANYA CHA MUUNGANO. URAISI ULIKUA KWA ZAMU MKAGEUZA SASA MARAISI WANATOKA TANGANYIKA TU. HAIJAWAHI HATA SIKU MOJA MKUU WA JESHI,POLISI, USALAMA WA TAIFA, GAVANA WA BENKI KUU, MKUU WA CUSTOMS AND INCOME TAX, UHAMIAJI NK AKATOKEA UPANDE WA ZANZIBAR AU HIZI TAASISI NI ZA TANGANYIKA PEKE YAO AU HAKUNA WAZANZIBARI WENYE SIFA AU HAWAPASWI KUSHIKA NAFASI HIZO NI ZA WATANGANYIKA PEKE YAO? MLIWADANGANYA WAZEE WETU VYA KUTOSHA MPAKA WENGINE WAKAAMINI KUA ZANZIBAR BILA YA TANGANYIKA HAIWEZEKANI. SASA HII NI KARNE MPYA YA VIJANA HAMWEZI KUDANGANYA WATU WOTE WAKATI WOTE. KAMA MUUNGANO UBAKIE BASI UWE WA MKATABA NA YAWE MAMBO MACHACHE TU LA SIVYO ACHILIA MBALI UVUNJIKE HAUNA FAIDA YOYOTE NA ZANZIBAR. UNAWANUFAISHA WATANGANYIKA ZAIDI WAO NDIO WANAOSHIKA NAFASI ZOTE KWENYE MUUNGANO. MFANO MDOGO TU NI SHIRIKA LA MAFUTA (TPDC) AMBALO TUNAELEZWA KUA NI LA MUUNGANO. KUANZIA MTU WA JUU KABISA MPAKA MFAGIAJI OFISI NI WATANGANYIKA HAKUNA MZANZIBARI HATA MMOJA. SASA HAPA KUNA FAIDA GANI YA KUUNGANA? NA HII IKO KWENYE MASHIRIKA NA WIZARA ZOTE ZA MUUNGANO ULINZI, MAMBO YA NDANI, FEDHA NK. TUAMBIENI KATIKA HIZO WIZARA NA MASHIKA YANAYODAIWA KUA NI YA MUUNGANO IDADI YA WATUMISHI NI WANGAPI WANAOTOKEA TANGANYIKA NI WANGAPI NA WAZANZIBARI NI WANGAPI. MUUNGANO HUU NI WA UNYONYAJI TU.ZANZIBAR HAIFAIDIKI NA CHOCHOTE NA NDIO MAANA WAZANZIBARI TUNASEMA TENA NA TENA TUACHIWE TUPUMUEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.

 12. Zanzibar bila muungano inawezekana ,lngawa Zanzibar ndani ya muungano ndio yenye manufaa Zaidi, wengi wanao amini Zanzibar nje ya muungano wame elemea zaidi kwenye nadharia ambayo naifanananisha na riwaya ya Marehemu Shaaban Robert ya nchi ya “Kufikirika na Kusadikika” .
  Wengi waumini wa Zanzibar Nje ya muungano hawajatueleza ki undani zaidi faidi ya Zanzibar ikiwa nje ya muungano zaidi ya kuegemea zaidi katika historia ya Zanzibar ya 1947 …. .
  uchumi wa dunia unabadilika nilazima tungalie tuendako …mfumo wa dunia uenaelekea katika uwingi kwa maana ya shirikisho nchi zote duniani zinalenga huko ..(European Union ,Umoja wa Falme za Kiarabu ; U.S.A ).
  Tuangalia mfumo gani wa muungano utakaotufaa kwa manufaa ya wa Zanzibari wote .

  Ukweli nikwamba wengi tunafauta mkumbo hakuna Mkakati wa maana kutuhakikishia maslahi yetu nje ya muungano, Je Tukishapumua Itakuaje ?
  Tutakua kama URUSI baada ya kusambaratika kwa USSR wajanja wachache wakajichukulia Utajiri wa Nchi Na kuwaacha walala hoi wakiendelea kua masikini ….

 13. MIMI NADHANI KAKA ULIYETANGULIA HUELEWI NINI WAZANZIBARI WANACHOTAKA. KAMA WATU DUNIANI WANAKIMBILIA MUUNGANO MBONA HAKUNA HATA NCHI MOJA ANGALAU ILIYOOMBA KUJIUNGA NA MUUNGANO HUU? NA KAMA NI MZURI KUNA HAJA GANI YA KUUNDA MPYA WA AFRIKA MASHARIKI? HUU UKWELI SIO MUUNGANO BALI NI UKOLONI NA WAZANZIBARI WALIPINDUA KUONDOSHA UKOLONI. SISI WAZANZIBARI HATUKATAI MUUNGANO ILA TUNAKATAA UKOLONI. TUVUNJE MUUNGANO HUU AND THEN TUTAJIUNGA KAMA ZANZIBAR NA MUUNGANO WA AFRIKA MASHARIKI. HEBU TUELEZE WEWE UMESIKIA TOKEA MUUNGANO HUU WA KINYONYAJI ULIPOANZA RAISI AKATOKEA ZANZIBAR? MKUU WA JESHI, USALAMA, BoT NA TAASISI NYENGINE ZOTE. HEBU TUTAJIE TAASISI MOJA TU YA MUUNGANO INAYOONGOZWA NA WAZANZIBARI UKIACHA ZILE ZA KISIASA. MUUNGANO WA UAE, USA, EUROPE NA KWINGINEKO NI MUUNGANO WA USAWA NA SIO NCHI MOJA KUZICOLONISE NYENGINE. HUU WA KWETU HAKUNA LUGHA YOYOTE ILE INAYOFAA KUUITA ZAIDI YA UKOLONI.NA NDIO MAANA WAKENYA, WARUNDI, WAGANDA WANYARWANDA HAWAUTAKI WANATAKA TUANZE UPYA. HII NI NAFASI NZURI KWETU TUUVUNJE MUUNGANO HUU NA TUJIUNGE NA HUO MKUBWA WA AFRIKA MASHARIKI. HII NDIO MAANA YA TUACHWE TUPUMUE. KAMA NI WAJANJA KUJILIMBIKIZIA MALI MBONA HILI LIMEANZA SIKU NYINGI TU. HUJAWAHI KUSIKIA WATU WAKITAMKA KUJIVUA MAGAMBA? HAYA PIA NDIO YANAYOTUFANYA TUUKATAE MUUNGANO HUU KWANI UNAWANUFAISHA ZAIDI HAO WATU WENYE MAGAMBA AMBAO NAAMINI UNAWAJUA.

 14. HATUTAKI MUUNGANO WA AINA YOYOTE ILE , NYIE HATA MJIITE MAPROFESA TUSHAKUJUENI NI WANAFIKI TU MNALIPWA NA SERIKALI , NDUGU WASOMAJI MSIYUMBISHWE NA HAWA KUJIITA MAJINA MAKUBWA MAKUBWA , MBONA HATA SALIMU HEMEDI SALIMU ANAITWA DR , SI WANAPEWA TU DEGREE FEKI ZA HESHIMA ETI , MSIDANGANYIKE NA YOYOTE WANAZNZ , MUUNGANO BASI HUU , LABDA ATEREMKE NABII ISA ( as) KUTUSHAURI TUNAWEZA KUBADILI MSIMAMO , VINGINEVYO , ZANZIBAR HURU ALUTA CONTINUA

 15. Hakuna nani wala nani hapa tuachweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee tupumueeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee zanzibar kwanza na mamlaka yake kamiili inshalllah biidhin llah yatakuwa tu amin,,wazanzibar tushikamane kwa kmba 1 ya ALLAH S.W kuidai nchi yetu amin……..wazanzibar tupendane kuidai nchi yetu…..

 16. achilia mbali kuwa mwenyekiti wa kigoda , hata ungekuwa mwenyekiti wa kiti cha enzi cha nyerere , tushakujua kuwa huna lolote ni pumba tu , karibu utaingia kaburini lakini bado unazungumza uwongo ndugu shivji hivi unafikiri huyo babaako nyerere atakusaidia huko kaburini?

 17. MAWAZO YA NYERERE YALIKUA SAWA WAKATI ULE NA SIO SASA. UKIMTAJA NYERERE NA FALSAFA ZAKE KWA KIZAZI CHA WAKATI HUU INAKUA KAMA KITUKO AU KUMDHALILISHA BABU WA WATU VILE. NADHANI PROFESSA NA WENZAKO DR ZAVAELI INABIDI MUWE CRITICAL NA SIO KUJA NA KU QUOTE FALSAFA ZILIZOPITWA NA WAKATI ZA NYERERE. MNADHANI NANI ATAWASIKILIZA LEO HII MKIMTAJA NYERERE? TUAMBIENI KWA KINA NINI FAIDA ZA MUUNGANO MUWEZE KUTUSHAWISHI TUUKUBALI. SISI KIZAZI CHA LEO TUMEKULIA KWENYE MUUNGANO NA TOKEA WAKATI WOTE HUO HATUJAWAHI KUONA ZURI HATA MOJA LA MUUNGANO ZAIDI YA MAGUNIA KWA MAGUNIA YA MAKERO YASIOKWISHA NA KUIDHOOFISHA ZANZIBAR KWA KILA HALI. KAMA HAMNA LA KUTUAMBIA NI VYEMA MKABAKIA KIMYA TU WAZANZIBARI SASA TUNAYEYAAAAAAAAA. HAKUNA TENA KURUDI NYUMA. TUACHENI TUPUMUE. MKE AKIKUKATAA NI WAJIBU KUMPA TALAKA.

 18. ikiwa kweli waznz wanafaidika na muungano , kwa nini basi hamuuvunji ili waone hasara gani watapata bila muungano , kwa nini mnang’ang’ania kuwepo huu muungano ? dunia hii hatoi mtu shilingi kumfaidisha mwengine , vipi tanganyika iwe inaifadisha znz bila sababu? MUUNGANO pelekeni shimoni ,halafu tuone nani anapata faida na nani hasara , mnang’ang’ania kama mavi na njia kubwa zilivyokamatana?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s