Uhuru wa habari sasa kitanzini

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Omar Yussuf Chunda

Kutokana na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo vya habari ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wasemaji katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo vya habari kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO

Tel: 0255 24 2237325/0255 24 223 7313 Idara ya Habari Maelezo
Fax: 0255 24 2237314 P.O. Box 2754
E-mail:habarimaelezo@yahoo.co.uk, maelezozanzibar@zanlink.com Zanzibar maelezozanzibar@hotmail.com, maelezozanzibar@gmail.com

09/08/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara ya Habari(MAELEZO) tunawakumbusha tena waandishi wa habari juu ya ulazima wa kuwa na kitambulisho cha kufanyia kazi ya uandishi wa habari Zanzibar kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo(Press Card) kwa mujibu wa sheria Zanzibar.

Aidha, waandishi wa habari kutoka nje ya Zanzibar hawataruhusiwa kufanyakazi ya uandishi wa habari mpaka pale amepata ruhusa ya Idara ya Habari Maelezo kwa mujibu wa sheria ya usajili magazeti N0 5 ya mwaka 1988 ya Zanzibar.

Kutokana na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo vya habari ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wasemaji katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo vya habari kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Hivyo, kuanzia tarehe 1/09/2012 waandishi wa habari wote wakiwa kazini ni muhimu kuonyesha kitambulisho kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo.

Aidha,, tunasisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria ya usajili wa magazeti sheria N0 5 ya mwaka 1988,kifungu cha 13 kinasisitiza kwamba mtu yeyote atakayechapisha Kitabu, Magazeti, Vipeperushi, Vijarida,Ramani na Chati lazima awasilishe nakala tatu si zaidi ya siku 14 baada ya kuchapishwa kwa Mrajis Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Kutofanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria ya Usajili Magazeti na Vitabu N0 5 ya mwaka 1988 hatua za kisheria zitachukuwa kwa atakayekiuka.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
09/08/2012

Advertisements

10 responses to “Uhuru wa habari sasa kitanzini

 1. Ndugu zangu Wazanzibari mimi ni mmoja wa waumini wakuu wa Muungano. Hata hivyo, kwa mambo kama haya, ni ishara ya wazi kuwa Wazanzibari mmejipanga kutubagua sisi Watanganyika.

  Maelekezo anayoyasema Waziri huyu ni aibu. Ni bora aseme wazi tu kuwa Waandishi wa Tanganyika wakija Zanzibar wakajisajili pale Maelezo badala ya kuzunguka.

  Hivi anataka kusema Mtangazaji wa VOA au BBC akitaka kumpigia waziri na wakurugenzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliowaelekeza wasitoe habari kwa ‘waandishi’ inabidi apande ndege kutoka Washington au London kuja Zanzibar kupata kibali kwanza?

  Hii ni aibu. Kwa mawazo yangu Waziri mwenye kutoa kauli kama hizi ana ufinyu wa fikira na hastahili hata kuendelea kushika wadhifa huu amepitwa na wakati.

  Wahafidhini wa aina hii ndiyo tunaopaswa kuwaondosha madarakani haraka. Dunia inazungumza kufungua milango yeye anafunga?

  Sasa naelekea kukubaliana na wanaosema tuvunje Muungano, kisha tuweke visa na kila upande uende kwa mwingine kwa kuomba visa. Nawajua watakaoumia zaidi nao wanajijua.

  Tusifike huko. Hizi sheria za kipuuzi tuzifute haraka ni aibu kubwa katika karne hii Serikali kutoa kauli kama hizi zisizo na mashiko.

  Deodatus Balile

 2. Aslaam Aleykum;

  Ni sheria hiihii iliyotumika Aprili mwaka 2005 kunifungia kufanyakazi ya UANDISHI wa HABARI ndani ya Zanzibar. Wakati adhabu hiyo inatolewa, Ali Mwinyikai ndiye alikuwa Mkurugenzi wa idara hii ya Habari Zanzibar. Leo Mkurugenzi ni Yussuf Omar Chunda.

  Nilitumikia adhabu ile kwa siku 10, ilipoingia siku ya 11, niliitwa kuchukua kitambulisho kilichokwishaandaliwa tayari. Shinikizo za watu mbalimbali watetezi wa haki za binadamu, yakiwemo mashirika ya kimataifa na mabalozi zilichagiza hata kuisukuma SMZ kuamua kunipa kitambulisho hicho bila ya kujaza fomu.

  Wakati ule nilikuwa nafanyakazi Habari Corporation, nikiwa pia na safu kwenye gazeti la RAI, niliyoipa jina la Waraka Kutoka Unguja.

  Sheria inayosemwa Zbar inafanana kwa mengi na Newspaper Act ya 1976 ya Tanzania Bara, ile inayotumika kufungia na kufuta usajili wa magazeti.

  Kwa wewe uliyeko Dsm na Bara kwa jumla, hutapata utetezi utaposhikwa na kudai unacho kitambulisho cha MAELEZO Dsm. Unajua suala la habari si miongoni mwa mambo ya Muungano. Kila upande una sheria yake.

  Ndiyo hali ilivyo nchini petu, bado tu watawala wa Jamhuri yetu hawataki kufuta sheria hizi kandamizi.

  Haya twendeni kama tutafika.

  Jabir Idrissa

 3. Ushauri huu kauchukua Kisonge kavuka nao njia mpaka ofisini mwake kwenda kutisha watu.
  Kazoae Cadre wa CCM.

  Lakini Inshaa-Allah tuko na nyinyi waandishi wetu vipenzi na kwa pamoja Allah yuko na sisi. Na wewe Balile Mungu atakusaidia tu.

  Najua Mwinyi Sadalla hajalengwa maana kashaahidiwa kuezeka nyumba yake kwa kupaza sauti za dhulma, lakini kila karo hujaa, na hili likijaa watahama nyumba maana kuzibua hawajui wanajua kujaza tu.

  Lakini dhulma hazitadumu kwa mbinu hizi za ukandamizaji wa waandishi wa habari na raia bali sauti za wanyonge zitasikika na zitamuangusha Dhaalima kibuku.

  Salma Said & Jabir Idrissa bila ya kumsahau Mr. Othman Miraji endeleeni kututetea tu tutafika by the Power of Almight God the Creator of the 7 Earths as well as the 7 Heavens.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 4. maneno aliosema nd deodatus ni murua ,kila mtu achukue nchi yake , waznz tupate uhuru kamili , namshangaa nyerere alikuwa kimbelembele kupigania nchi za kusini mwa afrika zipate uhuru , kumbe ndumilakuwili anawatawala waznz kwa mabavu , huko alipo anaona malipo ya kazi yake

 5. Hapa hatutakii muungano @deo@nyie watanganyika ni wabaguzi namba 1 mie binafsi yangu nilikwenda uhamiaji wa dar,kufanya passport na cheti changu ninacho wakaniambia ww hatukupi passport nenda kafanye znz ww c wa hapa dar mie binafsi yangu bora muungano uvunjike na sisi tuitwe raia wa znz na c Tanzania au Tanganyika kila mtu awe na chake Zanzibar kwanza kujuana bdae

 6. Hapa hakuna kurudi nyuma mpaka kiweleweke , tuhakikisha heshima ya nchi yetu inarudi akipenda Allah (s.w) tupo makin huu mzziki mzito ss hivi . Jina la Tanzania hatulitaki tena wa zanzibar . litafuteni Tanganyika yenu na mapema kabla hapajakuwa km somali hapa. .Tupo tayari kufa kwa ajili ya kusimamisha utawala wetu zanzibar wenye mamlaka kamili. vyama badaye nchi kwanza.

 7. HAYA MNAYOYAONA LEO SISI TUMEYAONA ZAMANI. WATU WENYE SIFA NA UWEZO WAPO WANAPEWA NAFASI WATU KAMA HUYU CHUNDA AMBAE AMESHASTAAFU MARA MBILI NA HAKUNA ASIEJUA KUA HANA UWEZO WA KUA MUANDISHI WA HABARI. LENGO LA TAMKO HILI NI KUWAZIBA MIDOMO WAANDISHI WA ZANZIBAR NA BARA WANAOFICHUA UOZO UNAOFANYWA NA SERIKALI ZOTE MBILI. NAKUBALIANA NA HUYO NDUGU WA MWANZO KUA VIONGOZI WA NAMNA HII KATIKA KARNE HII YA 21 NI AIBU NA KITUKO. WATU WANATAFUTA KILA NAMNA YA KUBORESHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI HAWA MAFALA WA SMZ WANAZUIA. MNATUTIA AIBU WAKATI MWENGINE HATA KUSEMA MBELE ZA WATU KUA NI KUTOKA ZANZIBAR. CHUNDA FANYA KILA HALI UZUIE NA MITANDAO YA INTERNET MAANA HIYO HAMNA UWEZO NAYO. HATA MKIBANA VIPI TUNANJIA NYINGI ZA KUWABANUA. MTATOA TU HABARI MTAKE MSITAKE PUMBAAAAAF.

 8. Wamepitwa na wakati hao vipi mbloger nao mtawapa vibali pia ipo wapi freedom of expression huko ndio kuishiwa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s