Utalii Endelevu kusaidia nchi kiuchumi

Said Ali Mbarouk ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar akifungua mkutano wa kimataifa wa Utalii Endelevu kwa niaba ya Balozi Seif.

UTALII Endelevu utasaidia kukuza uchumi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ikiwa serikali pamoja na wadau wataweza kuweka mikakati bora ya kuendeleza utalii. Hayo yameelezwa jana katika hutuba ya Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa kujadili changamoto katika dhani ya utalii endelevu uliofanyika hoteli ya Zanzibar Beach Resort nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

“Utalii unaozingatia kuhifadhi na kulinda mila, mazingira na vyanzo vya uchumi ni muhimu katika nchi zetu hasa kwa Tanzania na Zanzibar ambayo hivi sasa tegemeo lake kubwa ni utalii” alisema Said Ali Mbarouk waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kwa niaba ya Balozi Seif.

Alisema japo kuwa utalii umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka 20 katika Tanzania lakini bado hakuna mikakati endelevu itakayoweza kuimarisha utalii na kutoa tija kwa wananchi na kwamba wakati umefika kwa kuweka mikakati itakayojenga uchumi imara kwa kutegemea utalii.

Mkutano huo uliowajumuisha wasomi, wataalamu, watunga sera na wadau mbali mbali wa utalii kutoka nchi 15 duniani, Balozi Seif alisema mkutano huo unafanyika kwa wakati mbapo serikali zinahitaji kupatafikra mpya za kuendeleza utalii na wakati huo huo kuwa na faida kwa wananchi.

“Ni wazi kuwa uchumi katika nchi nyingi za kiafrika zinategemea sana ujasiriamali ambao wanafanya biashara ndogo ndogo na biashara nyingi kwa hivi sasa zimo katika sekta ya utalii kwa hivyo ni muhimu wasomi wasaidie serikali kuweka mipango bora ya utalii endelevu” alisema Balozi Seif katiak hutuba yake.

Mapema akimkaridhisha mgeni rasmi, Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Professa Rwekaza Kamandala alisema ni muhimu kwa wasomi kutoa mawazo yao kuangalia athari za utalii kijamii kiuchumi na kisiasa ili kujenga utalii utakaoleta mabadiliko katika nchi.

“Lazima tufahamu kwa kina utalii utakavyotuletea mabadiliko kwa sababu kwa hivi sasa sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika uchumi wetu” alisema Professa Mkandala.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mkutano huo Dk Lufumbi Mwaipopo mada 38 zinatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano huo wa siku mbili ambao unalenga kujadili changamoto katika utekelezaji wa utalii endelevu katika nchi zinazoendelea.

Katika mada zilizotangulia kuwasilishwa jana, mtoa mada Mwanafunzi John Ngoja kutoka chuo kikuu cha Marekani amesema kufanya utafiti katika masuala ya utalii endelevu ni muhimu ili kutoa njia bora za kuepukana na changamoto mfano rushwa ili kujenga utalii wenye manufaa kwa wote.

Bwana Alon Gelbman katika mada yake inayohoji kama utalii unaweza kujenga amani hasa katika mipaka ya nchi mbali mbali, alisema hivi sasa kuna ushahidi wa kuwa utalii unachochea kuleta amani kutokana na watalii kuingia au kuvutika ikiwa nchi ipo na amani.

“Kwa hivi sasa ni changamoto kwa serikali mbali mbali kuhakikisha mazingira yanakuwepo ili kuwavutia watalii ambao wanavutiwa na utamaduni pamoja na vivutia mbali mbali na suala zima la amani na utulivu yakipewa muhimu” alisema Alon.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya utalii kwa Tanzania na Zanzibar, Bi Julia Bishop alisema kuwa bado zipo changamoto kadhaa ambazo zinahitaji kushughulikiwa katika sekta yautalii ili kufikia lengo la kuwa na utalii endelevu.

Akizitaja changamoto hizo ni pamoja na wawekezaji wa utalii kuwa na mitaji modogo, uwelewa wa wananchi kuhusu utalii hauridhishi na uchache wa mikakati ya kuendeleza vivutia vya utalii nchini.

“Tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja kwa sababu kwa mfano kwa Zanzibar utalii wa hivi sasa unachangia pato kubwa la uchumi wake kwa hivyo ni muhimu vivutio vya Zanzibar kama utamaduni, makumbusho na mazingira asili kuendelezwa na kupewa kipaumbele katika programu za serikali” alisema Bishop.

Nchi zilizoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Botswana, Israil, Nigeria, India, Korea Kusini, Iran, Mexico, Sweden, Uingereza, Namibia, News Zealand, Afrika Kusini, Amerika na Ujerumani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s