Viongozi wenye kuzuwia maoni ya wengine washitakiwe

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yussuf Mohd Yussuf akitoa hotuba ya Kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai ili kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Kumpata Mgombea Uwakilishi Jimbo la Bububu kufuatia Kifo cha aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo,Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rashid Seif Suleiman ameishangaa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kushindwa kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanaowatisha wanachama kwa kutoa maoni tofauti na mtazamo wao.

Akichangia mada ya sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakar, Waziri Rashid Seif alisema kuna kila sababu ya kukamatwa kwa viongozi hao wa CCM wenye tabia ya kutoa matamshi ya vitisho kwa watu wenye kutaka mabadiliko ya mfumo wa muundo wa Muungano.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba inakataza mtu au taasisi kumzuia mtu mwengine kutoa maoni yake au kumlazimisha aseme anavyotaka yeye, sasa hawa viongozi wa CCM wanaotaka kuwanyanganya kadi Wawakilishi wao si wanakiuka sheria hii” Alisema Waziri Seif.

Waziri huyo ambaye alichukuwa nafasi ya Waziri aliyejiuzulu kufuatia kuzama kwa meli ya Mv. Skagit hivi karibuni, alisema kwamba atashangaa sana ikiwa Tume ya Jaji Warioba itakaa kimya kutokemea au kuwachukulia hatua wale wote wanaotoa vitisho dhidi ya watu wenye mitazamo na maoni tofauti kuhusu Katiba mpya.

Alisema kila mtu yuko huru kutoa maoni yake mbele ya Tume na si haki kwa mtu au Chama chochote cha siasa kuwalazimisha wanachama wake kutoa maoni ambayo hayatokani na mitazamo yao binafsi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT)   Zanzibar , Asha Bakar Makame amewataka viongozi wenzake ndani ya CCM kutowatisha wanachama wanaotoa maoni wasiyoyapenda.

Akichangia katika semina hiyo, Makamu huyo Mwenyekiyi ambaye ni Mwakilishi wa Viti Maalum alisema ni jambo la kushangaza katika ukuaji wa demokrasia wakajitokeza watu kuanza kuwazuia wengine kuwa na mawazo huru kwenye mchakato wa kupata Katiba mpya.

“Jamani tusitishane, kama CCM kila mtu ni CCM hapa, hakuna mtu asiyenijua msimamo wangu kuhusu Chama ninakipenda na nitakitetea,lakini si vizuri kuanza kutishana kwa kuambiana huyu hivi huyu vile haifai jamani” Alisema Makamu Mwenyekiti UWT.

Makamu huyo Mwenyekiti wa UWT alikumbusha kwamba wakati wa kutafuta maridhiano ya kisiasa Zanzibar wapo wana CCM na Viongozi waliopinga suala hilo ,lakini hakuna mtu aliyeadhibiwa, hivyo aliwataka kuvumilia katika suala zima la maoni tofauti kuhusu Muungano.

“Wakati tunakwenda kwenye kura ya maoni mwaka 2010 wapo wenzetu wengi walipinga, tena walikuwa wakijulikana,lakini hakuna mtu aliyetiwa adabu na Chama ingawa msimamo wa kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ulikuwa ni maamuzi ya Chama chetu tulikutana Butiama na Dodoma tukakubaliana…mbona hakutiwa adabu mtu” Alihoji Asha Bakar.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura(CCM),Hamza Hassan Juma alisema Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Kikwete hajazuia kutoa maoni tofauti isipokuwa aliwataka wananchi kuvumiliana maana kila mtu atakuwa na maoni yake.

“Mimi nampongeza sana Mwenyekiti wetu,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa siku ile akizundua Tume pale Ikulu, alisema kama wewe uyapendi mawazo ya mwenzio na yako pia kuna wasiyoyapenda,lakini la muhimu kustahamiliana” Alisema Mwakilishi huyo.

Hamza aliongeza kwamba CCM ni Chama bora na kamwe hakiogopi mageuzi na ndio maana hata mageuzi ya kisiasa mwaka 1992 ilisimamia vema na nchi ikaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hivyo hata katika suala la maoni kuhusu Muungano halitakuwa na matatizo maana wananchi wako huru kutoa maoni yao .

Advertisements

12 responses to “Viongozi wenye kuzuwia maoni ya wengine washitakiwe

 1. Jamani tusilumbane Wazanzibar, Allah ameshatuonesha njia ya kheri lililobaki sasa ni kuifuata tu maan tayari tumeshatoka mbali wakati tukigombanishwa, kunajisiwa, kipigwa na hata kuuliwa na maadui zetu. Nawaombeni tushikame katika hili kwani kwa mwana-CCM kuwa na Maoni tofaouti haina maana kuwa ametoka ndani ya CCM isipokuwa tu anapigania HAKI yake ya kujitawala na kuwa HURU ikiwa kama ndio malengo ya MAPINDUZI.
  Hebu leo angalieni Benard Membe ametamka waziwazi kuwa anataka kufanyike KURA YA MAONI Sahara Magharibi na wanailazimisha Morocco ikubali suala hilo ila bado Morocco hajaonesha nia hiyo maana Membe anasema suala hilo la kura ya maoni Wasahara wataamua kujitenga ili waondokane na mashaka ya kutawaliwa na Morocco ila hawa Watanganyika HATAWAKI IFANYIKE KURA YA MAONI ZANZIBAR kwanini au ndio wanajua kuwa TUTAJITAWALA na sisi ili tuondokane na MATESO, HUZUNI NA SIMANZI ZA MKOLONI MWEUSI? Tujiulize na baadae tupate JIBU LA HALI HII.
  MUDA WA KUAMUA NI SASA TUKICHELEWA KITAOZA!!!1

 2. Pingback: Viongozi wenye kuzuwia maoni ya wengine washitakiwe·

 3. Wataalamu walioandika kuhusu jamii wanasema ” because social dynamics focuses on individual level behavior, and recognizes the importance of heterogeneity across individuals, strict analytic results are often impossible. Instead, approximation techniques, such as mean field approximations from statistical physics, or computer simulations are used to understand the behaviors of the system. In contrast to more traditional approaches in economics, scholars of social dynamics are often interested in non-equilibrium, or dynamic, behavior.That is, behavior that changes over time”.

  Maelezo yya hapo juu ni ushahidi kuwa watu wanabadilika kufatana na zama wanazoishi. Tanzania ya leo si ile ya Mwalimu Nyerere kama ilivyo CCM yenyewe hivi leo. Hivyo hivyo kwa Zanzibar na watu wake nma taasisi wanazojitengenezea. Mtu anaweza kuamini Mawazo yake lakini ni bora aone haramu kutaka mawazo haya yaaminiwe na kila mtu. Ni vizuri pia kila mtu akubali mawazo yenye kutofautiana na yake. Ni muhimu kwa wanasiasa kufahamu kuwa ni ubaya mkubwa kuwa na Taasisi au falsafa yenye sura ya Kidola. David Stark, 1992,pp.229-304 akichambua hali ya Ulaya Mashariki anasema ” The logic of state socialism was to render the party central nervous system. It was institution, giving life, logic and functions to other subsidiary institutions. When communist party hegemony died, institutions died and, with that, roles roles and rules.” Hali hii iinaweza pia kuikumba nchi yetu na ndio mana kunakuandika Katiba ili nchi iongozwe kwa mujbu wa mahitaji ya sasa. Ni bora wanaozungumza waachwe pengine wao wanajipya na la kusaidia

 4. Enyi CCM Hamuna jipya mie naona musiseme kitu chochote kuhusu maoni kwasababu ndio nyie munaotetea msimamo wa sera za ccm na kufanya mikakati ya kuzuwia harakati za UAMSHO na ukombozi wa Zanzibar. Leo hii kwa kuwa mwataka kura mwaja na maneno matamu kwa kuwa mwataka kura. Musipate tabu sisi tushawajuwa kuwa nyie ni wanafiki na kazi yenu kubwa ni kufisidi na kufanya fisadi katika aridhi ya Mungu. Sisi lengo lenu tushalijuwa mwataka kura tu. Musitubabaishe. Tushachoka na janja zenu. Hatutaki hatuki nyie ni wanafiki na matapeli wa mawazo ya raia zenu. HATUUTAKI MUUNGANO. ZANZIBAR HURU KWANZA.

 5. CCM mna nini? Sikijui nauliza.

  Fikirieni jamani, Ni sote twajiumiza.

  Haya mambo hadi lini? Bara kujipendekeza.

  Tuamueni jamani, Zanzibar kuitukuza.

  Tusipokua makini, Tutakwenda kuulizwa.

  Wabara ni visirani, Hawachoki kutuviza.

  Chama ekeni pembeni Nchi kuiendeleza.

  Hem na linganisheni, Hwenda mkatoka kiza.

  Ni miaka hamsini, Sisi wametulemaza.

  Chuki kujaza nyoyoni, Wenyewe kututatiza.

  Sasa twasubiri nini? Nchi yetu kuikuza.

  Muoneni Salmini, Alivyotandwa na kiza.

  Macho yake hayaoni, Duniani amepazwa.

  Amekua masikini, Maisha kwake ni adha.

  Ni dua za wahaini, Kuwatupa magereza.

  Hata wake Juma Duni,* Jela kumtelekeza.

  Kahisi miaka kumi, Kwake haitomaliza.

  Akajifanya muhuni, Kufuru kuitangaza.

  Kutangaza hadharani, Tasbihi kuibeza.*

  Kuitia mfukoni, Kufanya analoweza*

  Akadhani mitihani, Kwa Allaah ishamaliza.

  Sefu yu madarakani, Yeye yupo kwenye kiza.

  Basi nanyi zindukeni, Msije mkateleza.

  Na Allaah kazi haoni, Hata nyinyi kuwapaza.

  Nchi yetu tuihami, Iwe basi kuchuuzwa.

  Twataka mjiamini, Muwe mfano wa Raza.

  Nanyi tunawathamini, Na mzidi kupendeza.

  Nawaaga kwaherini, Hayo ndo niloyawaza.

  Andikeni hapo chini, Kama nimewachokoza.

  ****Juma Duni (Ni mtoto wa dada ake) Yaani ni mjomba wake.
  **Kuna siku Komando Salmini alitangaza kwenye kiriri kua kama tasbih ndio inayompa imani, basi anaiweka pembeni, na aliitowa kuwaonyesha watu na kuitia mfukoni kwenye koti. Kwamba kuanzia hapo ni mwendo mdundo. Atafanya tu lolote analotaka. Kwaio wapemba wakakiona cha mtema wa kuni. Ikawa virungu ndio viburudisho vyao. FFU ilikua ikipata mazoezi vizuri katika miili ya watu. Na Kisonge Maskani ilikua zikimwagwa pesa kwa kuwatukana wapemba tu (WASO HAYA WANA MJI WAO) ilikua ni sera kuu. Wakati wowote taarab za kejeli kwa wapemba haikosekani. Wapemba wanoishi majumba ya Michenzani ilikua wanatamani ardhi ipasuke wazame na Block zao. Huyo ndio kamanda wa Udongo. Mungu ampe maisha marefu na azidi kumuonyesha na ampokonye neema zake kidogo kidogo nae aone utam wa dhiki. Kampokonya neema ya macho, ampokonye pia neema ya kusikia, pia na ya miguu, mwisho aparalaiz mwili mzima na aendelee kubaki iwe ni kumbusho kwa vizazi vyetu vijavyo.
  By: Suleiman Al’Rumhy. Mkoroshoni.

 6. na mimi najitokeza, kusapoti yako hoja. ni wengi walitubeza, walitufanyia vioja. nuru imesha chomoza, ni wakati wa umoja. zanzibar kuikweza, tupumue kwa faraja. tuache kucheza cheza, kote pemba na unguja. chuki zilizotokeza, zi siharibu umoja. amin!

  • Kwa nini muwazuie? Kutoa yao mawazo.

   Lazima wafikirie, Watokane na uozo.

   Nchi si ya kwenu nyie, Msitutie vikwazo.

   Mkajiona ndo nyie, Mkafanya mtakavyo.

   Chama ndio chenu nyie, Na Moyo ndie wa mwanzo.

   Rai zetu msikie, Mtuepushe na bezo.

   Tena msituchezee, Kwetu hamna uwezo.

 7. CCM kama Chama cha siasa hakina lengo la kuwazuia au kuwanyima uhuru wanachama wake katika kutoa maoni ili kuweza kutengeneza na kupata katiba mpya. Kila mwana CCM ana uhuru wa kutoa maoni yake kwa kadri ya ufahamu wake kwa maslahi ya taifa letu, jambo la muhimu ambalo mwana CCM anasisitizwa ni kufuata vyema na kuheshimu misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii kama ilivyoelekezwa katika kifungu no. 9 na 17 cha sheria no. 8 ya mwaka 2011 ya mabadiliko ya katiba.

 8. Wewe umelala au unasema hayo unafikiri sisi ni vipofu. Sisi tumeshuhudia kwa macho yetu wanachama wa CCM wakipangiwa cha kwenda zungumza kwenye tume na waliokuwa wakizungumza wote walikuwa na mtiririko mmoja. Leo kwa kuwa mwataka kura jimbo la bubu ndio mwabadilisha maneno? Si nyie nyie CCM Muliotamka hadharani kusisitiza msimamo wenu na mukataka kuwanyan’ganya kadi za ccm wanachama wenu wenye maoni tafauti na yenu? Sasa leo mbona mwageuka kwa kuwa mwataka kura bubu? Sisi tumeshawajuwa janja yenu. MUUNGANO HUU HATUUTAKI. ZANZIBAR HURU KWANZA. VYAMA NA SERA ZA VYAMA BAADAE.@Najma.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s