Mwandishi afariki dunia- Buriani Halima

Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Zanzibar Leo, Halima Abdallah amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda kwa zaidi ya miezi mitatu sasa amefariki leo na maziko yatafanyika leo huko nyumbani kwao Michenzani karibu Madema

Mfanyakazi wa shirika la magazeti ya serikali Halima Abdalla Omar, amefariki  dunia asubuhi huko nyumbani kwao Miembeni  Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar. Mfanyakazi huyo alizikwa jana katika mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya mwanakwerekwe yaliyopo wilaya ya magharibi.

Halima aliajiriwa na shirika la magazeti ya serikali oktoba 18 mwaka 2008, baada ya kuhitimu mafunzo ya uandishi wa ngazi ya cheti katika chuo cha uandishi wa habari Zanzibar. Na kufanya kazi katika gazeti la Zanzibar Leo hadi anafikwa na mauti.

Mwaka 2011, mwanahabari huyo alijiunga na chuo cha uandishi wa habari zanzibar, kwa masomo ya stashahada kabla ya kuahirisha masomo kwa sababu za ugonjwa.

Hadi kufariki kwake, Halima alikuwa mfanyakazi wa shirika la magazeti ya serikali na mwanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari Zanzibar akichukua fani hiyo ya uandishi wa habari ngazi ya Diploma.

Halima alizaliwa juni 8 mwaka 1984 na kuishi na wazee wake Jang’ombe mjini hapa na alimaliza masomo yake katika skuli masasi mwaka 2004 na kujiendeleza katika skuli ya Hamamni ambapo alimaliza mwaka 2006.

Marehemu Halima aliugua miezi mitatu iliyopita baada ya kupata matatizo ya kiafya na kufnayiwa upasuaji wa kichwa na tumboni ambapo aligundulika kuwa na ugonjwa wa cancer na kupatiwa matibabu wakati akiwa ndani ya matibabu hayo alifariki dunia ghafla akiwa nyumbani kwao ambapo alikuwa akiishi na mama yake mzazi. Safari ya Halina ni safari yetu sote wanaadamu ila kila mmoja atakwenda na wakati wake hatuna budi kumuombea maghfira kwa Mola na kumtakia safari ya kheri inshallah Mwenyeenzi Mungu amlaze mahali pema peponi ameen.

Advertisements

7 responses to “Mwandishi afariki dunia- Buriani Halima

  1. huu ndio mwisho wetu sote, kama aliandika habari za ukweli na uadilifu kwa ajili ya manufaa ya wananchi mungu atamlipa maradufu , na ikiwa alikuwa miongoni mwa waandishi wenye kuandika habari za uongo ili kujipendekeza kwa watawala apate sifa na mafao ya kidunia basi sasa yamekwisha , hao aliokuwa akijipendekeza kwake hawatomfaa chochote huko aliko , mungu akurehemu. Ni funzo kwa waandishi waliopo wajirekebishe kabla ya kukutana na mola wao.

  2. Mungu amjalie amsamehe makosa yake na amuepushe na adhabu ya kabri na amlinde na moto wa jahanam. Amin

  3. Inalillahi waina ilaihirajiun.Mungu aiweke roho ya marehem pahala pema peponi Amiin.Pia awape subra wafiwa wote.

  4. Kifo cha Mpenzi huyu kiwafundishe akina Juma Muamedi watumiao kalamu zao watakavyo. Halima Mungu aiweke roho yako peponi

  5. إنّا لله و إنّ إليه راجعون Kwa baraka ya mwezi huu mtukufu Mwenyezi Mungu amzidishie Rehma Zake na subira kwa watu wake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s