Soma Gazeti ANNUR kila Ijumaa

‘Karume mpya’ acharuka. Ataka Zanzibar iwe na polisi, sarafu yake. Awaambia vijana wasiogope wakati ni huu. Ampasha Vuai, asema Zanzibar sio ya CCM

Waziri Willium Lukuvi ajiuzulu. Amesababisha watu kufa kwa ‘Babu’. Sema: Kweli imefika, batili imetoweka. Hatimae Dr. Haji Mponda aibuka shujaa

Hakuna adhabu atakayeegoma kuhesabiwa. Asema Mkurugenzi wa takwimu Dr. Chuwa. Ateta na Masheikh wanaowakilisha waislamu. Kipengele cha dini kikiwekwa sensa iahirishwe

Kwa kusoma gazeti hili Tafadhali Bonyeza hapa ANNUUR 1028

Advertisements

6 responses to “Soma Gazeti ANNUR kila Ijumaa

 1. HIVI NYIE CCM NAWAULIZA HUU MUUNGANO NI WA TANGANYIKA NA CCM? AU NI WATANGANYIKA NA ZANZIBAR? SISI HATUUTAKI MUUNGANO.

 2. Nyinyi CCM Zanzibar ni empty headed na hawajulikani wanalolitaka isipokuwa ukereketwa usiowasaidia kitu “shenzi type”

 3. KWA UNAYETUWEKEA HILI GAZETI LA ANNUR TAFADHALI UHAKIKISHE TUNAPATA KILA IJUMAA, NAONA IJUMAA ZINGINE HATUPATI. KWA SIYE TULIOKO NJE YA NCHI TUNATEGMEA KUSOMA HABARI ZA NYUMBANI. GAZETI HILI NDILO PEKEE LINALOANDIKA YA KWELI NA NI SAUTI YA WAISLAMU. MAGAZETI MENGINE HABARI NYINGI WANAZOANDIKA NI ZA KUPOTOSHA, NA SI KUELIMISHA. KWA USEMAKWELI NIMEVUNJIKA MOYO KUSOMA MAGAZETI MENGINE KWA KUWA UNATAKIWA UWE NA TAHADHARI KUBWA SANA, KWANI UPOTOSHAJI NI MWINGI SANA. JAKAaLLAH KHAIRAN

 4. Hii ya mambo ya watu wengi kuamuliwa na wachache ndio yalipelekea leo Zanzibar kudai iwe huru kutoka Tanganyika. Inasikitisha kuona kuwa Watu wa kizazi chetu hawajifunzi kwa makosa ya nyuma. Leo akina dadangu wansema ” asilimia zaidi ya 80% Jimbo la Uzi walitaka mfumo wa Serikali na anatmia hii kutoa hoja ya kuwa “Muungano huu wa sasa unendelee.” Mtu mwengine Barazani anasimama na kusema kuwa ” Sera ya CCM ni Serikali Mbili,”

  Wanadai hivi sijui wanajua kuwa ni bora CCM ingeachwa itumie Sera kwenye utoaji wa Huduma za lazima, ujenzi wa miundombinu, biashara na mambo mengine na hili la vipi nchi iwe au itawaliwe ikaliacha kuwa suala la watu wote. Ni kwa mfumo huu wa Chama kushika hatamu ndio mana maji yanasambazwa ka magari badala ya mabomba, ni kwa mtindo huu wa Chama kushika hatamu ndio mana Serikali ya Mapinduzi leo inaendeshwa kwa misingi ya udugu na kujuana kiasi cha kukuta katika Barazani kuna Mwakilishi wa Jimbo na Ofisa ni mtoto wake!. Hii haina maana ya kuwa huyu mtoto hana haki za kuzaliwa za kupata ajira popote pale, laknini katika hali ya kawaida usingetarajia mtoto wa mwakilishi apate ajira Barazani ikiwa mfumo wa ajira ni wa Wazi kwa kila mtu.

  Sisi tusiotaka ajira za kisiasa tunashangaa tukiona watu wakipingana na waazilishi wa Muungano juu ya aina ya Muungano huo. Akina Mzee Moyo wasema wanahitaji Mungano wa Mkataba huku wenzake wa Chama katika Chama wanasema Muungano huu huu uendelee na zaidi wanadai ” Mihili ya Dola iwe miwili” badala ya mitatu kama akina Kake kule Pemba walivyokuwa wanadai mbele ya Tume ya Katiba. Najua kake zangu na dade zangu pengine walikusudia Mihiili Mitatu, lakini kwa kuwa hawakujua hii mihilmili ni nini na walitatja Miwili kwa kuwa walitumia nyimbo ya kufunzwa na nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.

  Ukiangalia utaona kuwa Zanzibar sasa inapita Kipindi kigumu- huku watu wake wakiburuzwa na Wanasiasa wengi wao wakiwa hatari kwa kuwa wao ni kama chui waliovaa ngozi ya kondoo. Watu hawa asububhi husema Muungano huu uendelee, jiioni wakasema hatuutaki. Falsafa hii ya kigeugeu ni hatari kwa kuwa hufanya mtu asijulikane alitakalo. Umoja wa Vijana wa CCM kwa mfano, walisema hapo nyuma watu wanakataa Muungano wanyanganywe kadi. Juzi wanasema wana CCM wa huru kusema aina ya Muungano wautakao. CUF nao walishikilia Serikali Tatu leo wanawambia watu wao wadai Muungano wa Mkataba wakati mwengine kuwa hali ngumu jamaa zangu wakiulizwa wafanue huu mktaba kwao una maana gani.

  Katika hali hii ya kuchanganyikiwa watu wangu ambao wengi ni wana Elimu ndo au hawana kabisa wanajukuta wakitoa mambo hata wasioyajua- ni muhimu kwa wanasisa kutangaza misimamo yao iliwafuasi wao wajue wanaeleke wapi!

 5. CCM mna nini? Sikijui nauliza.

  Fikirieni jamani, Ni sote twajiumiza.

  Haya mambo hadi lini? Bara kujipendekeza.

  Tuamueni jamani, Zanzibar kuitukuza.

  Tusipokua makini, Tutakwenda kuulizwa.

  Wabara ni visirani, Hawachoki kutuviza.

  Chama ekeni pembeni Nchi kuiendeleza.

  Hem na linganisheni, Hwenda mkatoka kiza.

  Ni miaka hamsini, Sisi wametulemaza.

  Chuki kujaza nyoyoni, Wenyewe kututatiza.

  Sasa twasubiri nini? Nchi yetu kuikuza.

  Muoneni Salmini, Alivyotandwa na kiza.

  Macho yake hayaoni, Duniani amepazwa.

  Amekua masikini, Maisha kwake ni adha.

  Ni dua za wahaini, Kuwatupa magereza.

  Hata wake Juma Duni,* Jela kumtelekeza.

  Kahisi miaka kumi, Kwake haitomaliza.

  Akajifanya muhuni, Kufuru kuitangaza.

  Kutangaza hadharani, Tasbihi kuibeza.*

  Kuitia mfukoni, Kufanya analoweza*

  Akadhani mitihani, Kwa Allaah ishamaliza.

  Sefu yu madarakani, Yeye yupo kwenye kiza.

  Basi nanyi zindukeni, Msije mkateleza.

  Na Allaah kazi haoni, Hata nyinyi kuwapaza.

  Nchi yetu tuihami, Iwe basi kuchuuzwa.

  Twataka mjiamini, Muwe mfano wa Raza.

  Nanyi tunawathamini, Na mzidi kupendeza.

  Nawaaga kwaherini, Hayo ndo niloyawaza.

  Andikeni hapo chini, Kama nimewachokoza.

  ****Juma Duni (Ni mtoto wa dada ake) Yaani ni mjomba wake.
  **Kuna siku Komando Salmini alitangaza kwenye kiriri kua kama tasbih ndio inayompa imani, basi anaiweka pembeni, na aliitowa kuwaonyesha watu na kuitia mfukoni kwenye koti. Kwamba kuanzia hapo ni mwendo mdundo. Atafanya tu lolote analotaka. Kwaio wapemba wakakiona cha mtema wa kuni. Ikawa virungu ndio viburudisho vyao. FFU ilikua ikipata mazoezi vizuri katika miili ya watu. Na Kisonge Maskani ilikua zikimwagwa pesa kwa kuwatukana wapemba tu (WASO HAYA WANA MJI WAO) ilikua ni sera kuu. Wakati wowote taarab za kejeli kwa wapemba haikosekani. Wapemba wanoishi majumba ya Michenzani ilikua wanatamani ardhi ipasuke wazame na Block zao. Huyo ndio kamanda wa Udongo. Mungu ampe maisha marefu na azidi kumuonyesha na ampokonye neema zake kidogo kidogo nae aone utam wa dhiki. Kampokonya neema ya macho, ampokonye pia neema ya kusikia, pia na ya miguu, mwisho aparalaiz mwili mzima na aendelee kubaki iwe ni kumbusho kwa vizazi vyetu vijavyo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s