CCM maslahi na vitisho vya Chui wa karatasi

Na Abdallah Vuai

Wiki hii kuna kituko cha aina yake kimetokea ndani ya Chama cha Mapinduzi upande wa Zanzibar kwa wanachama wachache wa Chama hicho Wilaya ya Mjini kuasi dhidi ya mamlaka halali ya CCM. Ni kisa,. Kituko kinachoweza kuvunja mbavu pale baadhi ya Wana CCM walipotoa tamko la kuwatuma viongozi wao wa Wilaya kuwataka Makamu Mwemyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar,Amani Abeid Karume kunyanganywa kadi kwa madai wamekwenda kinyume na msimamo wa CCM juu ya Muungano.

Viongozi wale waliobariki uasi ndani ya CCM nawawafanisha na aliyekuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa African National Congress(ANC) Julius Malema. Katika mkutano huo ambao mbali ya kutaka Makamu Mwenyekiti wao Karume afukuzwe CCM,lakini pia walitaka wanachama wengine kama Mweka Hazina wa Chama hicho Zanzibar,Mansoor Yussuf Himid nae kunyanganywa kadi!

Kisa na mkasa; ni msimamo wa Hamza Hassan Juma, Mshimba Mbarouk, Thuwayba Edington Kisasi, Omar Yussuf Mzee, Mahmoud Mohammed Mussa, Haroun Ali Suleiman, Asha Bakar Makame, Salmin Awadh Salmin, Othman Masoud Othman, Nassor Salim, Mansoor Yussuf Himid katika muundo wa Muungano wakiukosoa hadharani kuwa hauna tija kwa kuwa umeshindwa kufikia kile Wazanzibari walichokuwa wakikitaka baada ya Mapinduzi ya Januari 12,1964 na matumaoni yao katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa Karume wanamtuhumu kuunga mkono mabadiliko ya muundo wa Muungano, ingawa Karume hajapata kusema aina gani ya mfumo wa muundo wa Muungano anaupendelea.

Wanachama wale wanamvumishia Makamu Mwenyekiti wao jambo ambalo hakulisema, uvumi wao ni sawa na abrakadabra inayotaka kuzuka ndani ya CCM. Mambo ya uzushi, fitna na pengine kutaka kukigawa Chama chao kikongwe katika Bara la Afrika.
Kuwepo kwa mawazo tofauti ndani ya CCM au kwenye jamii sio kosa kwani muda mfupi baada ya NEC ya CCM kukutana Dodoma mwezi Mei mwaka huu ilitoa taarifa ya kuelezea msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano kuendelea na mfumo wa sasa.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti Bara, Pius Msekwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Ujerumani idhaa ya Kiswahili alisema pamoja na msimamo huo wa CCM wanachama wake hawajafungika kuwa na mawazo au kutoa fikra tofauti na ule wa Chama chao kwenye kutoa maoni katika Tume ya Mabadiliko ya katiba.

Rais Jakaya Kikwete akizindua Tume ya Jaji Warioba nae aliweka mkazo haki ya kutoa maoni na kila mtu kuheshimu mawazo ya mwengine. Ibara ya 18(a) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema; kila mtu anao uhuru wa maoni na kueleza fikra zake.
Msimamo huo unatiliwa mkazo na Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohammed Shein alipowahakikishia Wazanzibari kwamba wako huru kutoa maoni wayatakayo, hakuna atakayeingilia.

Kitabu cha Cycles of American kilichotungwa na Arthum Schelesinger Jr anasema kutokufungwa na mawazo ya kale katika mazingira yanayobadilika kunampa kiongozi wa kidemokrasia nafasi ya kutengeneza maonjo matamu ili apendwe na kufurahiwa na wengi.

Je, viongozi wale wa CCM Wilaya ya Mjini wanadhani watapendwa kwa kukandamiza uhuru wa maoni, kuishi mazingira ya kisiasa ya kibabaishaji ambayo kwanza hayakisaidii Chama hicho,lakini pia kinaweza kukimbiwa na wanachama kwani mfumo wa vyama vingi sera na uwazi ndani ya vyama ndio kigezo cha watu kujiunga na Chama husika.

Sheria inampa mtu kuwa mwenye haki mbele ya mtu mwingine na papo hapo kuwa mwenye haki mbele ya jamii kwa ujumla hivyo, wanachama wa CCM na hasa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanayo haki ya kijamii Social justice katika suala zima la mustakabali wa mfumo wa muundo wa Muungano wanaouona unafaa.

Mara nyingi haki ya kijamii ndio kilele cha demokrasia ambapo maamuzi ya nchi yapo mikononi mwa wananchi wenyewe na yafaa kutambua kuwa pasipo haki hakuna amani, Tulitegemea wakati huu ambapo Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaendelea kukusanya maoni kungekuwa na uhamasishaji wa CCM Mjini kuwahimiza wanachama wao kwenda kutoa maoni.

Kama kosa la akina Hamza Hassan Juma, Mshimba Mbarouk, Thuwayba Edington Kisasi, Omar Yussuf Mzee, Mahmoud Mohammed Mussa, Haroun Ali Suleiman, Asha Bakar Makame, Mohamed Raza Daramsi,Salmin Awadh Salmin, Othman Masoud Othman, Nassor Salim, Mansoor Yussuf Himid, na wengineo ambao wanawajibika kuitetea Zanzibar ni kosa na dhambi kwa CCM Wilaya Mjini basi historia itawahukumu kwa uzalendo wao, vyenginevyo, CCM maslahi watalia na kusaga meno kwa vigae.

CCM maslahi wanataka kuwapitisha Wazanzibari katika njia yenye miba,kiza kinene iliyokuwa na mashaka mengi huku tope za Uhafidhina zikiwanasa miguuni na kuchelewesha safari katika kufikia Muungano wenye maslahi kwa kila upande, Tanganyika na Zanzibar.

Kwa kutaka kuwanasua Wazanzibari na tope la Muhafidhina, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akitoa mada katika semina kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu katiba mpya, aliukosoa Muungano kwa kiwango ambacho kiliwaridhisha Wawakilishi.

Katika kuthibitisha udhaifu wa muundo wa Muungano, Mwanasheria Mkuu anauliza mambo kadhaa ikiwemo uhalali wa Rais wa Muungano kuchaguliwa kwa wingi wa kura kwa kuzingatia tofauti ya idadi ya watu baina ya Zanzibar na Tanzania Bara;
Uhalali wa Rais wa Zanzibar kuwa Mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri na sio Mwakilishi wa Zanzibar ndani ya Baraza la Mawaziri ili kuepuka kubanwa na Kanuni ya Baraza la Mawaziri ya Uwajibikaji wa pamoja.

Nini wajibu wa kikatiba wa Makamu wa Rais katika uendeshaji wa Serikali, Makamu wa Rais ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Muungano kuhusiana na Zanzibar kama ilivyokusudiwa na Mapatano ya Muungano? Jee ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Muungano kwa Mambo ya Muungano au Msaidizi Mkuu ni Waziri Mkuu? Hoja nyengine aliyowahi kuieleza Mwanasheria Mkuu ni pamoja na Makamu wa Rais hana urithi akimaanisha katika Serikali ya Muungano hana Mamlaka wala haiwakilishi Zanzibar na kwa mujibu wa katiba na sheria Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza akitaka tu,halazimiki.

Jee Mawaziri wanaotoka Zanzibar waliomo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano wanaiwakilisha Zanzibar au ni watumishi wa Rais wa Muungano kama walivyo Mawaziri wengine?

Jee kuna chombo chochote cha Kikatiba au kisheria kinacholazimisha Serikali mbili za Jamhuri ya Muungano kukutana, kushauriana na kufanya maamuzi ya pamoja kama Mamlaka mbili za kuendesha Jamhuri ya Muungano?

Katika mfumo wa sasa wa Serikali mbili upo uwezekano wa Serikali mbili zinazoongozwa na vyama viwili tofauti kufanya kazi kwa maelewano, Jee kipo chombo cha kutatua mizozo inayoweza kujitokeza baina ya Serikali mbili?

Maswali haya sio yangu, ni ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika mada yake kwa Wawakilishi ambayo yanatuthibitishia haja ya mabadiliko ya muundo wa Muungano ingawa wapo watu wengine kwa ulevi wa madaraka wanayafumbia macho kwa tama ya vyeo na pesa.

Msanii maarufu kule Msumbiji ,Marcelino Dos Santos katika moja ya tungo zake alisema ” We Must Plant”. Tafsiri ya haraka haraka ni kwamba tuna lazima ya kupanda, kupanda nini, mawazo ya mabadiliko katika muundo wa Muungano ambao wengi wanataka uwe wa Serikali mbili,lakini wa mkataba sio wa kikatiba.

Wazanzibari wengi wanaotumikia Serikali ya Muungano aghalab wamekuwa wakisahau kule walikotoka, wakifika Tanganyika wanageuka na kuwaona Wazanzibari wakorofi na baadhi ya wakati hata kuwabeza.
Tumeshangazwa na matamshi ya Waziri wa Ulinzi,Shamsi Vuai Nahodha katika michango yake katika semina ile akionekana kutetea sana mfumo huu mbovu na dhaifu wa muundo wa Muungano.

Nahodha anaeleza namna kero za Muungano zinavyoshughulikiwa katika Kamati isiyokuwa na meno ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, tumuulize Nahodha, miaka 48 kipi kimesababisha kushindwa kutatuliwa kwa kero hizo na sababu za kuzuka kwake?
Alipokuwa Waziri Kiongozi, Nahodha aliandika barua kumwandikia Waziri Mkuu juu ya maamuzi ya Baraza la Wawakilishi kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika mambo ya Muungano, barua hiyo hadi hivi leo yeye anakuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri Mkuu hajaijibu, tuseme haijafika pale Magogoni, imepotea Posta, au ndio wapo mbioni kuijibu?

Ndipo mwasisi wa Muungano, Hassan Nassor Moyo alipohoji kama kuna dhamira ya dhati ya kutatua kero hizo maana ni kipindi kirefu kimepita na pia alitoa angalizo kwamba wao enzi zao walifanya makosa,lakini makosa hayo lazima yasawazishwe na kizazi hichi.

Mwanafalsafa wa Ugiriki Socrates aliyeishi baina ya mwaka 469 BC – 399 BC siku moja aliwashangaza Wagiriki alipokwenda sokoni mkononi ameshika tochi akimulika mulika, wachuuzi walianza kumdadisi, imekuwaje leo? Akawaambia “kwenye nuru hii , kuna walio gizani.”

Kweli kuna walio gizani na ndio maana wameanza kutoa vitisho kwa wengine wakiwatishia kuwafukuza katika CCM,hapa nataka kukumbusha jambo moja,wakati fulani,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema “CCM sio baba yake wala mama yake” akafafanua “ikiwa kitapoteza sera na mwelekeo sina sababu ya kubaki ndani ya Chama hicho”

Sitaki kuamini kwamba CCM imepoteza sera, bali kuna watu ndani ya Chama hicho husasan Zanzibar hawana dira, hawana sera, wala hawana mwelekeo wanaishi kwa fitna, chuki na hawatumii bidii yao kukigeuza Chama hicho kuwa kimbilio la wengi, hawa ni ‘mufilisi’ kisiasa.

Mfumo wa muundo wa Muungano wa sasa hauwezi kusafishika kwa maji taka, lazima tutumie maji safi la salama na wala wale wanaojidanganya kuwa vitisho vinasaidia kulinda Muungano wanaota ndoto ya mchana sawa na ‘ Mfalme aliyetembea uchi’ huku watu wake wakijipanga barabarani kusifia vazi jipya la mfalme wao na wakijifanya hawaoni ubovu wa vazi jipya la Mfalme lililomweka nusu uchi kweupeni.

Tunashukuru Mungu wapo watetezi wa kweli wa Zanzibar kama Mwanasheria Mkuu anayetoa kasoro za Muungano bila woga, kama pale alipoelezea kizungumkuti cha kukosekana mfumo rasmi wa lila Mamlaka kuitambua Mamlaka Nyengine.

Othman anasema Hiyo ni kasoro kubwa sana katika Muungano na ambayo kwa bahati mbaya imejificha. Miongoni mwa athari zake ni Kwanza, ingawa Rais wa Jamhuri ya Muungano ana mamlaka kwa mambo ya Muungano ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar, masuala kama vile ya Sheria za jinai si suala la Muungano na hivyo kinga aliyonayo ya kutoshtakiwa ndani ya Katiba ya Muungano haiwezi kutumika Zanzibar kwa vile Zanzibar ina mamlaka na sheria zake za jinai.

Mwanasheria Mkuu anauliza Suala muhimu hapa ni jee Rais wa Muungano anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai ndani ya Zanzibar? .Suala hili kwa hali ya sasa linaweza kuonekana la kituko, lakini ni la muhimu sana” Anasema.

Hakuishia kwa Rais wa Muungano,pia aliuliza kwa Rais wa Zanzibar anapokwenda Tanzania Bara. “Pili, suala kama hili ni muhimu kujiuliza kwa Rais wa Zanzibar anapokuwa ndani ya Tanzania Bara. Tatu, Katiba haijaweka bayana masuala ya mashirikiano ya kimahkama hasa katika utekelezaji wa amri za Mahakama za pande mbili. Jambo pekee lililoelezwa ni upelekaji hati za Mahakama”

Kwa maswali hayo yasiyokuwa na majibu ndipo pale haja na ulazima wa kuwa na mfumo wa muundo wa Mungano wa mkataba unaposhika nafasi kwani kwa mazingira yalivyo njia pekee na bora ya kuweka sawa nyumba yetu ni kufanya mabadiliko ya muundo.

Advertisements

13 responses to “CCM maslahi na vitisho vya Chui wa karatasi

 1. hao wote uliowataja nd mwandishi ni maadui wakubwa wa waznz, wasijitie kujikosha buree kuwa hawautaki muungano uliopo , kwa kifupi wanatafuta njia za kupata kuungwa mkono na waznz vipofu , ili watuletee jini jingine lenye jina tofauti ktk muungano lakini , utwana na ubwana utabakia pale pale na nguvu ya dola itakuwa kwa watanganyika, ujumbe wangu kwao wasijishughulishe wao wamekaa miaka na kunufaika binafsi na familia zao na muungano , hivi leo kweli ndio wameshtuka kuwa huu muungano haufai? wasitubabaishe, muungano utavunjika kwa uwezo wa Mungu , na wao hawapati kitu bora waanze kukusanya vyao kabisa vilivyobakia wakaongeze mali zao ughaibuni kabla ya kufunguliwa kesi na serikali ya wananchi znz inayokuja kwa uwezo wa Mungu itayokuwa haina wizi wala ujambazi ndani yake kila jambo litafanywa kwa haki na sheria bila kujali tofauti yoyote. Narudia tena akina Karume hawatakiwiiiiiiiiiii, majambazi wakubwa wa nchi , kubwa la maadui limeshakufa vimebakia vifaranga vyake vinaleta bughuza

 2. Pingback: CCM maslahi na vitisho vya Chui wa karatasi·

 3. Bila shaka nakala nzuri. Mwandishi ameeleza uwazi kabisa na hakuficha. Sisi sasa hivi ni kwenda mbio tukapata uhuru wetu Siku ya UHURU wetu, Raisi wetu asimame pale mbele ya ulimwengu na kuitangaza JAMHURI YA WANANCHI YA ZANZIBAR. Hatuutaki muungano na tunasonga mbele. ala hatubabaishwi na lolote lile.

 4. @ feisal umelala usingizi mzito ndugu yangu amka ! , bado unafikiri kuwa huyo raisi ambaye tayari keshasema ataulinda muungano atakuwa na waznz?

 5. HATUUTAKI MUUNGANO MUSITUBABAISHE KWANINI MUNATUN’GAN’GANIA? TUAMKENI TUSHIKAMANE PAMOJA TUACHENI ITIKADI ZA VYAMA HUU SI WAKATI WA KUTETEA CCM NA SERA ZAKE TUDAINI NCHI YETU ZANZIBAR VIONGOZI WALIOKO MADARAKANI NI VIONGOZI WA MUUNGANO NA WAO WANAULINDA. Haya sote tumeyabaini katika huu mchakato ni kuwa maoni yanayotolewa ni maoni ya ccm na wala sio maoni ya watu wenyewe. Jamani hii nchi si mali ya ccm. WAZANZIBARI SOTE TUNASEMA HATUUTAKI MUUNGANO. ENYI MASHEHA NA NA WAKUU WA WILAYA ONENI VIBAYA MUNACHUKUWA WATU MUNAWARUBUNI KUTOKANA NA UNYONGE WAO WAENDE KUTETEA MUUNGANO KWENYE TUME YA MAONI. INSHALLAH NA NYIE MUNGU AWADHALILISHE MUWE NI WATU DUNI NA MUDHALILIKE DUNIANI NA AHERA. ZANZIBAR HURU BILA MUUNGANO INAWEZEKANA. HATUUTAKII MUUNGANO AU MUTATUUWA SOTE? MUSITULAZIMISHE. MUTAKUJA JUTA BAADAE.

 6. Kuna msemo wa kiswahili unasema ” bahari haiweki uchafu” ndiyo hivyo Wazanzibari tunona njia inazidi kufunguka na sasa tuanelekea kweupeni. Bila ya shaka kila mwenye uwezo wa kupima muelekeo wa mamabo kwa kutumia vigezo sahihi hawezi kupingana na usemi kwamba mabadilikoyanakuja.
  Kwa miaka yote CCM imekuwa ikitumia vitisho na ghilba kama njia kuu ya kufikia malengo yake, sasa muda huo umekwishwa. Ukiangalia kituo cha kutaka kuwapokonya kadi wanachama ni kitendo cha fedheha kubwa kani wanaotaka kufanya hivyo kwanza hawana meno ya kutafunia na pili wamechelewa maana muda wa kuyafanya hivyo umeshapita.

  Cha msingi Wazanzibar tusipate taabu ya kutaka kumjua mwema na mbaya, muda utaamua nani ndiye na nani siye, kwa mantiki kuwa mtu kama Haroun aliyepiga mbio huku na kule kuwataka wananchi kupiga kura ya hapana katika suala la SUK sasa amejitokeza tena ati naye anatetea maslahi ya Zanzibar. Ni kichekesho. Wanachotafuta hawa ni “mass legitimacy” uhalali wa ummah, lakini wapi! muda umepita. Wataruka wakitua hili gari limeshapigwa starter litatembea bila hata ya makonda wengi. Zaznibar sasa inaelekea kuzuri, tusiruhusu watu wachafu kutuharibia uzuri huu, waache wapige kelele sisi tusonge mbele.

  ZANZIBAR HURU YENYE MAMALAKA KAMILI KWANZA!!!!!

  • hata mm nashangaa sana wakati karume yuko madarakani hakufichua maovu hayo yote sasa ndio anayaona hayo kwamba hayafai siku zote alikuwa wapi? na pia kama yeye kweli hajaridhika na mfumo wa muungano hu0ou mbovu mbona hakusema ili wananchi wampende zaidi amefaidika vya kutosha na familia yake ndio anajipendekeza wakati watu wa hali ya chini wanaumia haumwi itabidi apelekwe mental wakamfanyie uchunguzi.

 7. Pingback: Ccm maslahi na vitisho vya chui wa karatasi·

 8. Kipindi hiki si cha kunyoosheana vidole! Watu ambao wanadai mfumo wa Muungano huu uendelee hawana justifications silizonzito. Kwa mfano utasikia kwenye mikutano ya Mchakato wa Katiba Mtu moja moja anakuja na kusema ” Mimi fulani bin Fulan, miaka ———- wa Shehia ———– nataka Muungano huu endelee na zaidi maoni yang8 yamo kwenye barua.” akitakiwa aseme yaliyomo kwenye barua japo kidogo hawezi! Wanasema husema Muungano huu uendelee na Wakuu wa Mikoa wabaki kuwa Wakuu wa Mikoa, Wa Wilaya Wabaki kuwa Wakuu wa Wilaya na mihilimili milwili ya Dola ibaki- Hili ndio huwa jipya kwa sasa Mihimili ya Dola tuliyonayo ni mitatu! Wanafanikiwa kuitaja mitatu basi husema na bei ya karafuu inogezwe! Mimi hucheka nikaona jinsi mawazo ya kuchangiwa yalivyo mabaya! Hukumbuka msemo wa Kiswahili wa kuwa ” nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma!

  Watu wanaotetea mfumo wa Muungano huu na kutaka ulindwe hawako tofauti na hawa waambiwao wataje mihimili mitatu wakataja miwili! Tofauti yao ni kuwa hawa wanatetetea ilikulinda toge zao na wale wanatetea ili kulinda uhusiano na viongozi wa vyama vyama vyao ambao ukienda kwenye mikutano huwangoza hwa watu kama Mussa alivyowangoza Wana Wa Kondoo katika zama zake! Mama moja kule Ziwani Pemba alikuja na barua na huku akiongozwa namna ya kuiwasilisha! mama huyu alipopata nafasi ya kusema alisema yaliyo katika moyo wake ” Mimi wanangu Muungano si utaki!.” Alipoulizwa sababu akasema yeye mwenyewe anajua na asiiulizwe! Katika ktuo hiki pia tuliona Kijana mdogo akitia challenges ziliwashinda wakubwa kabisa. Huyu nilimfananisha na Nabii Ibrahim alivyokataa kuabudu miungu ya jamaa zake kwa kuwa aliona Mungu wa kweli yupo! Wazee hawa ambao nisingependelea waendelee kuambatana na TUME kwa wao ni watu Wakubwa na Waheshima walitetetea hoja ambaz hazina uhalisi na huyu kijana akwashinda !

  Baba moja Katika kituo cha Gombani ya Kale alisemna kuwa anaungamkono Muungano kwa kuwa Waasisi ambao ni “wazee wetu” hawakuwa Wapumbavu! Sijui yeye huyu jamaa ni karibu kiasi gani na marehemu Karume ambaye leo mtoto wake wa kuzaa “anadaiwa kushabikia mabadilliko katika Muundo wa Muungano huu wa sasa.! Watu kule kwetu ukikubuhu hukuita juvuli la mvule! Hatujui kuwa kwa msimamo huu Karume na wenzake ni vivuli vya Mvule !

  Ukiangalia watetezi wa mfumo huu wa Muungano utaona wanashabikia wimbo wasioujua! Mara Wakuu wa mikoa, mara mihimili miwili maa mitatu, mara bei ya karafuu inongezwe, mara waasisi si Wapumbavu nakadhalika nakadhalika. Mzee moyo juzi alitoa msimamo wake na sijua kama yeye si miongoni mwa waasisi wa Munnungano huu. Wenyekujua akiwemo President Kikwete wanaona Muungano huu unahitaji mabadiliko ili ukabiliane na mahitaji ya sasa ! TUME hii ya Mabadiliko ya Katiba ni dalili za kuonesha mahitaji ya mabadilko sasa hayaepukiki.Pongezi nyingi zimfikie Comrade Kikwete kwa kusoma alama za wakati! Huu ndio uananasisa kwa kuwa kwenye siasa vitu hubadilika kulingana na wakati na mahitaji! Ni nani alifikiri kuwa baadahi ya pro changes today wangebadilika kiasi hiki ilihali hapo nyuma walikubali hali iwe hivi hata kama watakula udongo! Hawa ni waumini wa kweli wa siasa nahivyo wastahili wapongezwe! Ali endelea kuandika kwa kuwa Mwenyezi Mungu kasema ” Tumemfunza mwanadamu kwa kalamu” Najua siku moja hawa wapingao watakuwa vinara wa mabadiliko pia kwa kuwa Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga!

 9. A/laykum.

  Zanzibar kumekuchaa!. Dufu limenoga babaa. Na CCM disco limeingia mmasai. Haya haya haya twendee, vuta shemeree mpaka maji watayaita mma. Ee walizowea hawa paka mwitu.

  Wakwezi viroboto wabiringisha mav—- sasa eti wanaungana kumuuwa tembo wataweza? Wazalendo tulieni tucheke.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 10. @akilimalimende usimpambe Rais Kikwete kumwita comrade , kama ni comrade wa kweli tunataka muungano uvunjike kila mtu achukue time yake aendeleza nchi yake , mwambie aondoe majeshi yake aliyoyaweka kama yeye ni mkweli na mwadilifu na anakwenda na wakati kabla hatufikia hatua za kina tunisia, egypt , syria na libya , tukaanza kuuana bure , kama diplomasia ikishindwa hali hua kama hio ya kuuana , msije kusema hamkutahadharishwa , kusababisha maafa na hasara , dalili ya mvua mawingu mimi si mtizamaji nyota wala juju, hii hata kipofu na kiziwa anaweza kutabiri. Nd Kikwete mwogope Mungu kabla hujakutana nae ndugu yangu msiwadhulumu wanyonge wa znz wamekukoseni nini? Kumbukeni mnyonge huvumilia lakini akifika ukomo hasira zake hazitohimilika , mtakuja kuanza kuwatafuta kin Bankimoon waje kusuluhisha wakati kwa sasa unaweza kuzuia hali hio isifanyike

 11. Mi nadhani wanaotetea muungano usivunjuke nao tuwapokonyeni kadi za uzanzibari au tuwapelekeni mental tukawapime jamani tusiwalaumu si akili zao bangi tu hiyo stimu zao zikiisha watatuelewa wenyewe hao

 12. WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO NA TANGANYIKA. Hatimae Waziri wa elimu zanzibar ALI JUMA SHAMHUNA aiba mishahara ya waalim wa zanzibar. Walim hao wafika Hits Fm radio yatangaza.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s