Meli tatu zafutiwa usajili kuepusha ajali

Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Malindi Mjini Zanzibar

Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo. Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.

 

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.

 

Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo.

 

Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao.

 

“Tnafanya operesheni kabambe hadi  meli zote ambazo hazina kiwango zimeondoka katika bandari yetu” alisema Kombo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri baharini Zanzibar.

 

Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.

 

Kufuatia sheria hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili kinyume na maeneo ya Zanzibar.

 

Akizungumzia Meli ya Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50  hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo ilivyo.

 

Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.

 

 

 

 

Advertisements

5 responses to “Meli tatu zafutiwa usajili kuepusha ajali

  1. AMA HILI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KULETA MELI KUBWA HAPA MHESHIMIWA UMETUDANGANYA. HEBU TUAMBIE MELI HII ITAKUJA LINI. NI MPYA AU NI MTUMBA? KAMA NI MPYA MIKATABA YA KUIUNDA IMETIWA SAINI LINI? HAYA NI MANENO YA UONGO YA SMZ AMBAYO TUMESHAANZA KUYAZOEA. KILA SIKU MNATUAMBIA MELI IKO NJIANI INAKUJA. ILIVYOKUA NYINYI NA WAKE ZENU HAMPANDI MELI WALA HAYAWASHUGHULISHI. IKO SIKU MJUE TU MTAULIZWA KWA HIZI ROHO MNAZOZIPOTEZA KWA UZEMBE NA UJINGA WENU.

  2. Nyie musitubabaishe hakuna meli wala boti munatubabaisha. Munatengeneza ugali wenu tu. Hata hizo meli mulizozifutia usajili tukujaona nyie nyie mutazirudishia usajili. Hamna lolote rushwa rushwaaa imetawala Zanzibar jamani munatuuwaaa. VUNJA MUUNGANO UNATUMALIZA. ZANZIAR HURU BILA MUUNGANO INAWEZAKANA. TUSHIKAMANE PAMAJA TUTASHINDA.

  3. Swali je mlipokuwa mnazisajili hzo boti hamkujuwa kama hazina viwango au rushwa ilitawala kwanza siamin kama mmezifungia kwan nakumbuka baada ya ajali ya spice muliifungia mv. Serengeti mlijuwa kwamba haina viwanga muda simrefu serenget ikaelea hamuon kama mnachza mchezo wa danganya toto.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s