Muungano huu sebu! asema Mansoor

Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amesema potelea mbali kama ni kufukuzwa katika chama chake cha CCM lakini hatasita kuitetea Zanzibar

Kwa kusikiliza mahojiano ya Mhe: Mansoor Bonyeza hapa.

Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amesema yupo tayari kunyanganywa kadi ya chama hicho lakini hataregeza msimamo wake juu ya kuitetea Zanzibar katika Muungano. Kauli ya Mansoor imekuja siku chache baada ya chama hicho wilaya ya mjini kutoa maamuzi ya kuwataka viongozi wenye kupingana na msimamo wa chama kurejesha kadi za chama hicho au kuacha tabia hiyo mra moja.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Ujerumani (DW) jana Mansoor alisema kamwe hawezi kuogopa vitisho vinavyotolewa na watu wenye kujipa madaraka na udikteta ambao hawataki mabadiliko wala mawazo tofauti.

Mansoor aliahidi kuendelea na msimamo wake katika kudai mabadiliko katika muundo wa Muungano na kusema kwamba msimamo wake hautabadilika licha ya vitisho vya baadhi ya Viongozi wa Chama hicho.

“Nimesema hayo tokea muda mrefu chama hiki kimetukuka na kina heshima na maadili yake ni baadhi ya watu wanataka kutuziba midomo lakini

Mimi sijasema leo nimesema tokea 2008-2009 juu ya msimamo wangu juu ya mfumo wa muungano na leo naendelea kusema tena hata ikipidi kunyanynganywa kadi mimi narejea tena kuwa mfumo huu wa serikali mbili sikubaliani nao na nitaendelea kusema ahivyo hivyo siwezi kubadilisha maoni yangu leo baada ya kuwa na msimamo miaka yote hayo” alisisitiza Himid ambaye ni Mjumbe wa NEC.

Aidha alisema Chama Cha Mapinduzi wilaya ya mjini hakina mamlaka ya kuitisha kikao na kutoa maamuzi kama hayo ambapo alisema ni watu wachache wenye nia ya kutaka kuwanyamazisha watu wenye maoni tofauti na wao.

“CCM wilaya ya mjini hawana mamlaka hayo, lakini pia hawana uwezo wa kutunyamazisha kwani CCM haijakataza wanachama wake kuwa na mawazo tofauti sasa nashangaa hao wanaosema sisi tumekiuka msimamo wa Chama ni msimamo upi maana mchakato wa katiba upo huru na kila mtu anatakiwa kutoa maoni yake” Alisema Himid.

Katika kuonesha kukasirika kwake na uamuzi huo wa kutaka kuwanyanganya kazi, Muweka Hazina huyo wa CCM alisema kwamba ni jambo la aibu kwa CCM Wilaya ya Mjini kufanya vitendo vya kibaguzi na vya udikteta kutaka kuwafunga midomo watu wasitoe maoni yao.

Alisema hakuna makosa kwa wana CCM kuwa na mawazo tofauti kwani kila mmoja ana haki ya kutoa maoni na kueleza msimamo wake na tabia ya kikundi cha watu kujiona wao ndio wenye mamlaka na wenye chama ni kosa na halipaswi kuachiwa.

“Hao ni ni wabaguzi hawataki watu waseme ukisema unaonekana msaliti, hao ni watu wenye mawazo mgando hawataki kusikiliza fikra nyengine wanataka wanachosema wao ndio kiwe hicho hicho hilo haliwezekani na hatutakubali” Alisisitiza.

Hata hivyo alisema zama za kusema tunakwenda na fikra za mwneyekiti umepitwa na wakati na sasa jamii kubwa inakwenda na vijana amabo wanataka mabadiliko nchini hivyo aliwashauri wana CCM kuwaachia watu watoe maoni yao kwa uhuru kwani katiba tayari imetoa uhuru huo hivyo CCM hawawezi kuwa juu ya sheria.

“Hii nchi sio ya CCM peke yake hapa kuna CUF kuna Chadema na pia kuna vyama vyengine lakini wengine hawana hata vyama sasa hatuwezi kuendelea na watu ambao hawataki kuwa na mabadiliko wenye mawazo mgando …zama hizo zimeshapitwa na wakati wakati wa kwenda na fikra za mwenyekiti umekwisha” alisema Mansoor ambaye ni Waziri aisye na wizara maalumu.

Mmweka Hazina huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alisema kitendo kilichofanywa cha kutishiwa kunyanganywa kadi ya CCM na baadhi ya viongozi hao ni cha fedheha na kimekitia aibu Chama cha CCM mbele ya wana jamii.

Himid alisema yeye ametokana na mifupa ya Chama cha Afro Shiraz (ASP) hivyo suala la kuwepo kwa dhana ya wanachama wa madaraja ndani ya CCM halipo kwa kuwa Chama hicho kinaheshimu misingi ya haki za binadamu na kuwataka wenye kudhani kwamba wao ndio wana mamalaka zaidi kuliko wengine waache tabia hiyo.

Hivi karibuni chama cha mapinduzi CCM wilaya ya mjini kilitoa tamko la kuwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi, akiwemo Muweka Hazina wa CCM Zanzibar, Mansoour na makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar kuacha mara moja kukiuka maadili ya chama chao kwa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya muungano.

Jana akihojiwa na DW, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisikika akisema kwamba viongozi wanaokwenda kinyume na madili ya chama chao watatakiwa kwenda kujieleza katika vikao na iwapo watathibitika wamekwenda kinyume basi watanyanganywa kazi au kufukuzwa.

Nape alisema mwana yoyote CCM hawezi kwenda kinyume na maadili ya chama chake na iwapo atakuwa na msimamo mwengine usiokuwa wa chama hicho basi atatakiwa kuwasilisha maoni yake ndani ya vikao na iwapo maoni hayo wajumbe hawatayaridhia basi atalazimika kurejesha kazi ya chama hicho iwapo yeye hatokubaliana na msimamo wa kikao.

Akijibu suala hilo Himid alisema kuwa Nape hawezi kugawa matabaka wanachama wa CCM, wale wa Tanzania Bara na Zanzibar kwani wote ni wanachama wanahaki sawa mbele ya sheria na katika CCM.

“Sisi Watanzania hatuna uhuru, yeye amegawa kwa utabaka, sisi ni watu wazima tuna haki na uhuru,  Nape hawezi kutwambia sisi watu wazima kwamba tukasema anayotaka yeye, ule wakati wa ndio Mwenyekiti haupo kila mtu ana haki yake kutoa maoni na hata Tume ya Jaji Warioba inasema hivyo” Alisema Himid. Na kuongeza kwamba.
“Mimi naichukulia kuwa hii ni njama ya kutaka kuwaziba midomo Wazanzibari, hatujakiuka miongozo wala sheria tutaendelea kusema kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano, hii nchi asilimia kubwa ni vijana na vijana wanataka mabadiliko na hilo haliwezi kukwepwa” Aliongeza.

Licha ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa mbali ya kueleza msimamo wa Chama hicho, lakini amesema wanachama wake hawafungiki kuwa na maoni na mitazamo tofauti katika mchakato wa katiba mpya.

“Mie nadhani kuna baadhi ya watu wana fikra za udikteta, haiwezekani twende kwenye kutoa maoni tukasema tunataka Serikali mbili kama ilivyosema CCM sisi ni watu wazima tuna haki zetu na tusichaguliwe la kusema na kwa nini tuzibwe au tufungwe midogo?” Alihoji.

Mansoor amesema msimamo wake kuhusu mfumo wa muundo wa Muungano utabakia kama ulivyo kutaka kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika muundo huo kwani kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka Zanzibar ambayo hayapatiwi ufumbuzi kutokana na kuwepo kwa muundo dhaifu wa Muungano.

Alisema hakuna mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano, lakini ni lazima kukawepo kwa Muungano wenye maslahi ambayo hautakuwa na kero na ndio maana wamekuwa wakitoa maoni ya kutaka mabadiliko ya muundo na sio kuvunja.

“Mimi pia nakubali muungano una manufaa, lakini sikubaliani na mfumo wa Muungano na ndio maana tunasema kwa mfumo huu sebu(sitaki)” alisema Mweka Hazina wa CCM Zanzibar.

Tokea kuanza kwa machakato wa katiba wazanzibari wengin wamekuwa na maoni ya aina mbili tofauti ambapo wapo wengine wakitaka muungano kama ulivyo uendelee na wengine wakisema wanataka muungano wa serikali mbili zenye mamlaka kamili na zenye kuirejeshea Zanzibar ya kuingia mikataba na nchi za nje na baadae kuwe na mkataba.

Advertisements

18 responses to “Muungano huu sebu! asema Mansoor

 1. Hongera za dhati, namna hio.Nape ni bwamdogo tuu, zama leo unamtisha nani kumnyang’anya kadi ya chama ? Vyama vimejaa nchini kupita kiasi.Labda Nape alidhani chama kilichopo nchini ni CCM pekee.

 2. Nakupongeza MH. MANSOUR KWA MSIMAMO WAKO USIOTETEREKA. Na huo sio kuwa ni peke yako. Mawazo yako yanalingana na Wazanzibar walio wengi sana. Sote tumechoka na mfumo huu tulionao wa muungano. Wazanzibar tuacheni kasumba tushikamane tuigomboe Zanzibar kutoka kwa Mkoloni mweusi. Tuacheni usiasa na utabaka. Zanzibar huru inawezekana. JAMANI AMKENI TUIJENGE ZANZIBAR TUSIBAGUWANE. SISI TUSHACHOSHWA NA MUUNGANO HUU TULIONAO KWA NINI MWATULAZIMISHA? HATUUTAKI MUUNGANO. MUTATUUWA SOTE UWEZO MUNAO? SISI TUNATEGEMEA MUNGU TU. NA TUNAAMINI TUTASHINDI.

 3. Nakujua mshikaji msimamo wako hautetereki,nakupongeza kwa hilo nalo ni la kimataifa linastahiki tunzo ya oscar ,
  umekuwa mkweli mara zote na mwenye msimamo madhubuti ,tena jana tu niliwaambia ambao tukijadiliana suali la vuai nikawaambia atapata jibu mjarabu.
  Hakujakucha muarbaini upo chini ya nyumba hauhitaji kuagiziwa india,tuko nawe mheshimiwa na nakualika pale pale kwenye kahawa yetu,honi ikilia tu mzee khamis atatupa cha kufungua mdomo,kisha maneno hujibiwa na maneno sio nguvu au vita.

 4. Pingback: Mweka hazina wa CCM-Zanzibar, Mansoor Yussuf asema "Muungano huu sebu!"·

 5. inabidi kuwa waangalifu ktk uamuzi huu wa nd himidi , inaweza ni mkweli amejua ukweli , na inawezekana ametumwa na chama tawala kama mamluki kuwababaisha watu na kuwapotosha wenye msimamo , yeye anazungumzia muungano wa katiba , waznz hawataki muungano wowote kwa sasa , wanataka uvunjike kabisa , tuwamurike hawa kina himidi na wengine ambao wanaweza kuibuka kabla ya kusheherekea chochote , wenye kuweka maslahi yao mbele kuliko ya nchi ,

 6. Pingback: Muungano huu sebu! asema Mansoor·

 7. HONGERA MANSOUR WEWE NDIE AINA YA VIONGOZI TUNAOWAHITAJI ZANZIBAR. USITETEREKE WAZANZIBARI SOTE TUNAOIYAKIA MEMA ZANZIBAR TUKO PAMOJA NAWE. WACHA WAKUFUKUZE CHAMA TUTAKUPA JIMBO KWA TIKETI YA CHAMA CHOCHOTE KILE UTACHOJIUNGA NACHO. HUYO NAPE NI BWAMDOGO TU ANADHANI ANAWEZA KUKUTISHA WEWE. ACHANA NAE HUYO MPUUZI NAPE HAJUI SIASA WALA HAJUI NINI DEMOKRASIA. HAELEWI KAMA WEWE NI MZANZIBARI NA UNA HAKI YA KUA NA MAONI YAKO KATIKA HILI. HII SIO LA VYAMA HUYU JAMAA NAPE KASOMA WAPI SIASA? KAMA NI LA VYAMA CUF, NCCR, CHADEMA NA WENGINE KILA MMOJA AWE NA LAKE? HILI NI LA WANANCHI HASA WAZANZIBARI. TUACHE UVYAMA TUIKOMBOE NCHI. ZANZIBAR HURU BILA YA MUUNGANO INAWEZEKANA.

 8. Karibu Uzanzibari karibu utandawazi kwaheri ubaguzi na siasa za chuki.

  One Zanzibar one people one Nation

  Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza— shengesha za ubaguzi baadaye

 9. sikilizeni mahojiano kwenye sauti kwa kina , msifurahie jambo msililolijua, ndugu himidi hajasema kuvunjwa muungano, bado ukimsikiliza vizuri anajigonga kwa CCM na Kikwete , ukiona hivyo lazima ujue huyu hayuko tayari kupoteza nafasi yake ya ulaji kwa ajili waznz ndio maana huanza kusifu wale wenye nguvu zaidi yake ili wasije kumjeruhi kumbe hajui mwenye nguvu zaidi ya mola hakuna , msikurukupuke tu kuanza kupongezana , huyu hafai , katumwa na serikali na chama chake ,muwe waangalifu. Muungano wa aina yoyote hautakiwi visiwani huu ndio ujumbe.

 10. na kama hamkuangalia vizuri huyu ndie atasababisha kuwagawa wananchi wenye msimamo na kuleta kufarikiana. Na kuna mtu anamsifu kuwa sawa na AA Karume , hii imetokea wapi , lipi zuri alikuwa nalo Karume kwa waznz? zaidi ya udikteta wakati wa utawala wake na dhuluma tupu na mauaji ya watu wasio na hatia wakati wa mapinduzi kipi kizuri kafanya? kujenga nyumba za michenzani na kiwanja cha watoto cha kuchezea huku amezitoa roho za mamia kama sio maelfu , yupo kwa mola kama mazuri atalipwa na kama mabaya anaona joto ya jiwe muda huu.

 11. WAZANZIBAR SOTE HATUUTAKI MUUNGANO NA TANGANYIKA WANAOTUMIA TRA KUHAMISHA MALI ZA ZANZIBAR. Wakitaka muungano utavunjika hawakutaka muungano utavunjika tu ng’ombe weusi wa TANGANYIKA kuingia znz mwisho mwaka huu.

 12. Mungu ailaze roho ya KAFIR NYERERE mahali pabaya motoni (ameen) hakika nyerere ndie aliemuua rais wa kwanza wa smz ABEID AMAN KARUME.

 13. Aleykum Salaam.

  Kuitetea Zanzibar Katika Muungano.

  Mtu yoyote ambae anadai kuitetea Zanzibar katika Muungano, hawezi wakati huo huo kudai Muungano uvunjike. Iwapo Muungano utavunjika, hiyo Zanzibar utaiteteaje katika Muungano ambao umeshavunjika? Lazima kuitetea Zanzibar katika mfumo wa Muungano ambao unatoa haki sawa kwa nchi mbili ambazo zimeungana. Mwanzo wa haki hizo ni katika kuongoza Muungano kwenye safu zote
  za Serikali ya Muungano, kuanzia ngazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Nchi mbili zikiungana huwa zinasaka “Equity” kwenye huo Muungano. Uwiano wa haki huleta usawa kwa pande zote mbili na kuchelea upande mmoja kujihisi wametawaliwa au wamemezwa. Kujihisi au kuwa na hesia ya kutawaliwa huleta unyonge wa kuhisi kuna ukosefu wa utetezi; maana kwenye utetezi kamili, hakuna kupunjwa, kunyanyaswa, au kuonewa. “In politics, perception is everything”. Kwenye siasa, kilakitu hutokana na hesia. Ukihisi unadhulumiwa, huwachi kulalamika.

  Kwenye nchi zinoungana kisiasa, tatizo la kwanza ni kupanga safu ya uongozi utoridhisha sehemu zote za Muungano. Mara nyingi, katika kuepuka vurugu za kuchagua Rais mpya wa Muungano, mapendekezo ni kwamba Rais wa nchi moja ndie awe Rais mpya wa huo Muungano. Hii humaanisha kwamba Rais wa ile nchi nyengine awe Makamo wa Rais, ili wale Marais wawili kabla ya Muungano, waongoze serikali ya Muungano kwenye safu ya Rais na Makamo wake. Pia, humaanisha kwamba baada ya kipindi au vipindi muafaka, na yule Makamo au kiongozi mwengine kutoka nchi yake, aweze kuongoza kwenye safu ya Urais wa Muungano. Na upande wa pili wa Muungano utowe Makamo wa Rais.

  Katiba ambayo tumepania kuibadili, imetamka wazi kwenye hilo, na watetezi wa Zanzibar hilo wamelifurahia. Katika Katiba mpya, bora hilo libaki, na katika kutilia mkazo “Equity” na uwiano utaochelea migogoro na malalamiko ya kuelemewa, ni bora Katiba itamke wazi juu ya suala la kupishana na kuwepo zamu kwenye Urais na vyeo vyengine vya juu.

  Kila Katiba huwa na Yaloagizwa, Yaloelezwa, na Yanotegemewa kutokana na itikadi. “Traditions” ni kitu muhimu katika uteuzi wa viongozi, na katika Muungano ni lazima kujenga itikadi ya kuteua viongozi kutoka pande zote mbili. Watetezi wa nchi zao ni lazima kusimamia hilo. Lazima kuwe na “Deliberate attempt” Jaribio la makusudi na la dharura kutoa zamu kwenye uongozi, ilimradi watoteuliwa wakidhi sifa zinotegemewa. Hayo yamefanyika katika historia ya Muungano wetu, na sioni kwanini iwe mwiko kuirejea historia hiyo. Katika demokrasia, wengi wape kutokana na wingi wa kura, na tusipofanya jaribio la makusudi na la dharura kuwapata viongozi wa safu za juu kutoka sehemu zote za Muungano wetu, basi wengi watatoka sehemu moja na kuendelea kujenga hisia kwamba sehemu moja ya Muungano imeelemewa. Ndio maana kuna wengine wanajihisi wamesakamwa na wanaomba waachiwe wapumuwe.

  Tunapopata fursa ya kuchagua viongozi wa juu, kama vile Rais wa Jamhuri ya Muungano, ni vyema wale wanaodai kuitetea Zanzibar wawe mstari wa mbele katika kumpata mgombea bora kutoka Zanzibar na kumsaidia ili ateuliwe. Hili ni muhimu kufanyika, hasa baada ya uongozi wa ngazi ya juu kabisa kukamatwa na viongozi kutoka sehemu moja ya Muungano kwa muda mrefu. Mwenyekuitetea Zanzibar kikweli kwenye hilo, hawezi kudai kwamba hakuna Mzanzibari anofaa kwenye wadhifa huo. Anayechukua msimamo huo, anachangia Zanzibar kusakamwa na kukosa pumzi. “Tuacheni tupumuwe” aambiwe na yeye pia. Mzanzibari anayewakataa wagombea wote kutoka Zanzibar na kumuunga mkono mgombea kutoka bara kwa hali na maji aendelee kutawala, asidai kwamba anaitetea Zanzibar na kudai “Tuacheni tupumuwe”. Kwani kwenye kusakamwa na Bara, na yeye si alichangia? Ya yeye alichangia katika kutukosesha pumzi, ilimradi yeye apumuwe vizuri zaidi baada ya kutuuza. “We were sold down the river to the highest bidder by our own kith and kin”. Kikulacho kinguoni mwako.

  Umefika wakati Watanzania tuwe makini sana. Tutetee haki zetu kwenye Muungano wetu, na tujizatiti katika kuepusha “Dhana” ya aina yoyote ya kwamba upande mmoja wa Muungano wetu, umeelemewa. Tuunde Katiba mpya itoondowa dhana ya kutawaliwa na tutoe fursa kwa pande zote ziachwe zipumuwe. Tukishindwa kwenye hilo, tutajitakia maradhi. Na wahenga walisema “Maradhi ya kujitakia; Mtu hapewi pole”.

  Balozi Karume.

  • Mwenyezi Mungu amzidishie Balozi Karume, hekima na busara katika kuuhakiki na kuutathmini muungano wetu.

   • na mwenyezi mungu akuzidishie laana ktk dunia hii na kaburini , malaya mkubwa mungu unamjua wewe?

   • samahani kwa kutumia lugha mbovu hapo kwa nd najma , ndugu mhariri unaweza kuihariri hio lugha , vidole viliteleza

 14. nyinyi akina karume hatuwataki kabisa , ndio mliosababisha haya yote , maradhi mmeleta nyinyi n familia yenu , kwa hio tukitaka tuwe huru kwanza ni kuwaondoa akina karumes wote kwenye system , wewe ni miongoni mwa wale wanaotaka kulinda muungano usituambie au kutushauri chochote bora kaa kimya, hatutaki muungano wa aina yoyote ule kama umetumwa kuandika hii makala rudi kwa mabwana zako ukawaambie, na huu muungano ukivunjika tu watu wa kwanza kutolewa kwenye system ni nyinyi , kwa hio bora uendelee kushabikia muungano , kwani ukivunjika petu patupu ,

 15. hii makala imendikwa kumpatia umaarufu himidi , kwa kutumia lugha ‘sebu’ angalieni ndugu waznz msije mkayumbishwa , hawa karumes ndio wanyonyaji na masultani wakubwa, wameibia nchi kila kitu, wamejilimbikizia vyeo , mali , ardhi na vitega uchumi vyote , ni majambazi babu kubwa kama hamkutahadhari , huyu himidi na mwanzake huyu aneyejiita balozi badala ya kuheshimu jina alilopewa na mamaake , wote ni mamluki wa tanganyika , ukumbusho utawafaa wenye kuzingatia!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s