Waziri Hamad ajiuzulu

Mawaziri wanaohusika na usafiri baharini Zanzibar, Hamad wa kulia Dk Harison Mwakyembe na Said Ali Mbarouk waziri wa habari wakitoa taarifa kuhusiana na ajali ya meli juzi katika ukumbi wa ZBC Zanzibar

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.

“Tarehe  20 Julai,2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea Julai 18,2012” Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.

Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.

“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa  Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.

Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.

Advertisements

5 responses to “Waziri Hamad ajiuzulu

  1. Huu ndio ujasiri na uungwana ukiona mambo huyawezi unayaachia kistaarabu. Huu ni mfano kwa viongozi wengine inafaa waige kutoka kwa mh. Hamad. Changamoto kwa Dr. Shein jee utaweza kuwawajibisha watendaji wako waliojaa rushwa na miundombinu mibovu katika taasisi na wizara zao?

  2. Hongera sana mheshimiwa hii inaonesha jinsi gani gani chama cha CUF kilivyo makini ktk uongozi wa kuwajibika Big up

  3. Hongera mh hamad kwa kuwajibika kisiasa na huo ndio ustaarabu wa mwanasiasa aliekomaa kisiasa, umekijengea heshma chama chako na jimbo lako la ole, na tunampongeza mh rais kwa kuunda tume ya uchunguuzi wa ajali, lakini hata hivyo bado tunajiuliza masulai mengi ambayo hayajapata majibu.
    1. yale mapendekezo ya Mv spice yameeingia mitini? na sasa hivi kuna hii mpya au yatatolewa kwa pamoja.

    2. Kuna kamati ziliundwa ndani ya baraza letu tukufu likagundua ifisadi wa kutisha na tukaahidiwa hatuwa zitachukuliwa sijui zimechukuliwa kimya kimya? au maamuzi ndo yako njiani kutolewa? haya tupo tunasuburi.

    WAKATI NI UKUTA UKIPAMBANA NAO UTAKUUMIZA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s