‘Nilizimia kabla ya kuokoa’ Muddy

Muhsin Salum Muddy ni miongoni mwa waokoaji wa kujitolea lakini alizimia kabla ya kufika katika eneo la tukio

Muhsin Salum Muddy ni miongoni mwa wazamiaji walioshindwa kufanya kazi ya uokozi baada ya kupinduka na kupoteza fahamu wakati wa zoezi la kuwaokoa watu waliopata ajali ya meli ya Mv Skagit iliyozama katika eneo la baina ya Chumbe na Dar es Salaam jumatano iliyopita. “Sikujitambua mien a sijui nimefikaje hospitali hapa maana nafungua macho ndio najiona nipo katika kitanda na nimefunikwa branketi wakati ninavyojua niliingia katika boti ya polisi kwa kwenda kuwaokoa watu waliopata ajali” alisimulia kijana huyo na kuongeza kwamba.

“Pamoja na kwenda kuwaokoa walionusurika katika boti na kuchukua maiti nilikuwa na kamera kwa ajili ya kupiga picha lakini nikashindwa kufanya kazi zote kutokana na hali ya hewa ilivyokuwa mbaya” alisema.

Kushindwa kufanya kazi kwa Muhsin kunatokana na mawimbi makali baharini ambayo yalisababisha boti za uokozi kushindwa kutulia kufanya kazi ya uokozi ambapo waokoaji wengine walikubwa na mkasa kama wa kwake na wengine kujeruhiwa vibaya.
“Tuliondoka bandari ya Malindi majira ya saa 9:30 jioni na tukafika kule kiasi saa 12 na baada ya nusu saa ndio tukawa tunaziona maiti zikielea na watu waliokuwa hai wakiomba msaada wa uokozi huku wakihangaika sana wakionesha kuchoka wengine tayari wameshakunywa maji mengi wanataka kusaidiwa lakini haikuwa rahisi kufanya kazi hiyo” alisema kijana huyo.

Kutokana na hali ya bahari kuchafuka sana baadhi ya vyombo vililazimika kurudi bila ya kufanya uokozi ambapo Muddy anasema wenzake wengi waliokuwa ndani ya boti wakitapika na kuwa hoi kabisa kutokana na hali hiyo.

Akisimulia tukio lililomkuta kijana umri wa miaka 30 alisema wakati wakikaribia kufika eneo la ajali chombo walichokuwa wamepanda walianza kupigwa na mawimbi makali na yeye kuanza kukosa kupata kichefuchefu na kutapika na baadae kuishiwa nguvu kabisa.

Alisema wakati yeye akiwa taabani aliwaona wazamiaji wenzake wakitapika sana huku maiti na miili ya watu wanaotaka kusaidiwa wakiwa wanaonekana karibu na boti za uokozi zilizojitokeza kufanya kazi hiyo ambapo baadhi ya maiti zikizagaa katika bahari.

Huku kiza kikiingia alisema boti yao ya uokozi ilipigwa na wimbi kali na kuvunja taa za mumulika na kusaidia katika uokozi huo ambapo kazi hiyo ikashindwa kuendelea kutoka na kiza kikubwa kinachoelezwa kushindwa kuokoa watu waliopata ajali hiyo.

“Baada ya hilo wimbi kubwa sana kupiga katika chombo chetu na kuvunja taa iliyokuwa ina mwanga mkali shughuli zote zikavurugika na ndio hapo tena sikuweza kujitambua na najiona nipo hapa hospitali …najiuliza nimefikaje” alihoji Kijana huyo ambaye ni mzamiaji wa kujitolea.

Alisema eneo ambalo ajali imetokea ni karibu zaidi na Dar es salaam kuliko Zanzibar lakini anashindwa kupata majibu kwa nini boti za uokozi za Dar es salaam hazijajulishwa mapema ili kusaidia katika uokozi.

“Boti yetu ya uokozi ni miongoni mwa boti zilizofika mwanzo katika eneo la tukio, tukio limetokea unaona Wazo hill dare s salaam sasa tunajiuliza kwa nini boti za uokozi zimetoka masafa marefu Zanzibar wakati boti za uokozi zingeweza kutoka Dar es salaam na kusaidia?” alihoji tena Muddy ambaye pia ni msanii wa maigizo.

Muddy alifika bandarini mapema baada ya kupata taarifa za kuzama kwa meli ya Mv. Skagit ambapo alikuwa ni miongoni mwa vijana waliojitolea kwenda kusaidia kwa kushirikiana na wazamiaji wengine kutoka vikosi tofauti vya ulinzi na usalama.
Kwa bahati yeye aliingia katika boti ya uokozi ya polisi na kuaza safari ya kwenda katika bahari ambapo hali ya hewa ilikuwa mbaya kutokana na mawimbi na upepo mkali.

Baadhi ya wazamiaji wakiwemo waandishi wa habari walitakiwa kujitolea kwenda kuwaokoa watu waliopatwa na maafa lakini wengi wao kufika karibu na tukio walishindwa kusaidia kuokoa kutoka na hali ya mawimbi kupiga kwa kasi na baadhi ya waokoaji kuanza kuokolewa wao kwa kusaidiwa.

“Mtu yeyote ambaye anaweza kuogelea na kutoa msaada wa uokozi tunamuomba apande juu ya meli ili twende katika eneo la tukio tuanze kazi” maafisa wa KMKM walisikika wakisema bandarini hapo majira ya saa 11 jioni.

Taarifa za tukio la kuzama kwa boti ya Mv Skagit zilianza kusambaa majira ya saa 7:30 lakini harakati za uokozi zilichelelewa mno kuanza licha ya viongozi wa juu kupata taarifa hizo mapema.

Waandishi wa habari na wananchi wa kawaida walishuhudia harakati za kwenda kwenye uokozi majira ya saa 11 jioni huku wazamiaji wakihangaika kutafuta mafuta ili kukimbilia katika eneo hilo.

Kuchelewa kufanya uokozi iliwachochea wananchi kuilamu serikali na watendaji kwa uzembe na kushindwa kuimarisha huduma za uokozi nchini licha ya kutokea ajali za baharini mara kwa mara.

Wakijitetea mbele ya waandishi wa habari mawaziri wa wanaohusika na usafiri Hamad Masoud Hamad (Zanzibar) na Dk Harison Mwakyembe (Tanzania Bara) walisema tukio la kuzama kwa meli hiyo lilikuwa na muda mfupi sana takriban dakika tano ambapo haingekuwa rahisi kuharakisha uokozi.

Advertisements

4 responses to “‘Nilizimia kabla ya kuokoa’ Muddy

  1. Jamaani, KMKM munaomba msaada wa uokozi wa uzamiaji kwa wananchi. Kweli hamkuwezeshwa, mulifunzwa siasa zaidi kuliko uaskari. Kama alivyosema Mh. Ali Mzee nyinyi ndio Jeshi la Zanzibar la siku za karibuni hivi. Mukowapi Zanzibar Navy.
    Na pale Dar zimejaa boti za Polisi, moja inaitwa Ngunguri ku counteract Neno Ngangari. What a shame!

  2. Watawezaje na wao waliingia kazini kwa kadi za Chama. Wakati huu wa kutafuta Zanzibar kuwa sovereign state inabidi pia jeshi hili liangaliwe!

  3. UZEMBE HAUNA MJADALA KILA KONA. KUANZIA SERIKALI YENYEWE, NA WATENDAJI WAKE. HIVI HII IDARA YA MAAFA KAZI YAKE NI IPI KAMA SIO KUPANGA MIKAKATI YA KUZUIA MAJANGA? WAO WANAFIKIRI KAZI YAO NI KUSUBIRI MELI ZIZAME WAKAE KUPOKEA MICHANGO ILI WAIBE KIDOGO. HAWA NDIO WALIOPASWA KUJIUZULU MWANZO AKIWEMO WAZIRI HUSIKA NA IDARA HII. SERIKALI KAMA HAIJANUNUA MELI ZA UHAKIKA TUSUBIRI MUDA SIO MREFU KUTOKEA JANGA JENGINE KAMA HILI. WATU WA VISIWANI USAFIRI WA MELI NDIO WA KAWAIDA VIPI SERIKALI MNASHINDWA KUTAFUTA MELI YA KUWASAIDIA WAZANZIBARI. KAMA TATIZO NI FEDHA SHENI UZA MASHANGINGI YOTE YA MAWAZIRI NA WAPE RAV 4 ZINATOSHA. MISAFARA YAKO, WASAIDIZI WAKO NA HAO MA FIRST LADIES IPUNGUZWE WENGINE WANA FIRST LADIES WANNE. BADALA YA KUTUMIA MAGARI MATATU TUMIA MBILI MISURURU YA MAGARI YA FFU ACHANA NAYO HIVI UTAOGOPA WANANCHI WALIOKUCHAGUA HADI LINI AU HAWAKUKUCHAGUA. PUNGUZA WATUMISHI WASIOKUA NA KAZI HASA VIKOSI VYA SMZ IKIWA WAMESHINDWA KWENDA CHUMBE TU KUOKOA WATAWEZA NINI HAO? VUNJA VIKOSI VYOTE HAVINA MAANA YOYOTE ZAIDI YA SIASA. HIVI VALANTIA NA ZIMAMOTO NA UOKOZI WANAKAZI GANI IKIWA HAWANA UWEZO WA KUOKOA MELI CHUMBE PAMOJA NA KUJIUZULU WAZIRI WA MIUNDOMBINU BADO SERIKALI NZIMA NA HASA SOMO SHENI INAPASWA KUJIUZULU KWA KUSHINDWA KUWAWAJIBISHA WATU WAKO NA BADALA YAKE UNALINDA MUUNGANO TU..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s