Viongozi wa Uamsho watafutwa, 40 mbaroni

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kushoto ni Azzan Khalid Hamdan, Msellem Ali Msellem, Farid Hadi Ahmed, Khamis, na Mussa Juma Issa wakiswali katika Msikiti wa Mbuyuni kabla ya kusambaratishwa na Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU)

JESHI la Polisi Nchini, linawatafuta viongozi wa Taasisi za kidini na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki) huku likiwashikilia watu 43 wanaodaiwa kuhusika na vurugu zilizotokea juzi. Viongozi wanaotafutwa na Jeshi la Polisi na ambao wanatakiwa kujisalimisha ni pamoja na Msemaji wa Taasisi za Kidini, Farid Hadi Ahmed, Kiongozi wa Uamsho, Mselem Ali Mselem, Naibu Kiongozi wa Uamsho, Azan Khalid Hamdan na na Mhadhiri wa Uamsho Mussa Juma Issa.
Lakini Naibu Kiongozi wa Uamsho, Hamdan alikanusha jumuiya yake kuhusika na vurugu hizo akisema walikuwa msikitini kuwaombea dua waliofikwa na maafa katika meli ya MV Skaget Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohamed alisema jana kuwa viongozi hao wanatafutwa kwa kosa la kuwahamasisha vijana kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu.
Alisema katika vurugu hizo, vijana hao walikata miti iliyomo pembeni mwa barabara, kuvunja vioo vya nyumba na magari , kuweka mawe na vitu vizito barabarani. Kamanda alisema viongozi hao waliomba kibali cha kufanya mikutano kwenye uwanja wa mzalendo ili kuwaombea dua waliokufa kwa ajali ya meli ya Mv Skagit lakini polisi ilikataa kutokana na amri ya serikali kuzuia mihadhara.
Kamanda Azizi alisema kwa kuwa kundi hilo la Uamsho linafahamika kwa ubishi ndipo jeshi hilo lilipeleka polisi kwenye uwanja wa Mzalendo ili kuzuia mkusanyiko wa wafuasi hao wa Umsho.
“Polisi waliwahi kuwazuia wafuasi hao wasikusanyike kwenye viwanja hivyo lakini viongozi wa Uamsho waliwatangazia wafuasi wao wakiwataka sasa wakusanyike kwenye viwanja vya msikiti wa Mbuyuni karibu na eneo la Malindi,” alisema Kamanda.
Alisema muda wa kuomba dua ulipofika viongozi hao waliingia msikitini lakini watu wengi zaidi walikuwa nje ya msikiti huo.
Kamanda alisema kilichoendelea kwenye msikiti huo ni viongozi huo ni kwa viongozi hao kukashfu viongozi wa serikali na kuwataka wafuasi wao kutounga mkono muungano.
Alisema wakati hayo wakiendelea,wafuasi wa Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi. Alisema ndipo Jeshi la Polisi likaamua kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na maji yenye kemikali za kuwasha.
Akijibu tuhuma hizo, Naibu Kiongozi huyo wa Uamsho, Hamdan vurugu hizo zimesababishwa na polisi wenyewe kwani wao walikuwa msikitini wakiomba dua waliofikwa na maafa ya ajali ya Mv Skaget.
“ Tunasikitika sana viongozi wa dini kuhusishwa na vurugu zilizotokea jana (juzi), kwa kweli sisi hatuhusiki na vurugu hizo na tumeshangazwa na Jeshi la Polisi kuvamia msikitini na kuanza kuwatawanya waumini waliokuwa wakifanya ibada,” alisema.
Alisema baada ya sala hiyo walitoa mawaidha ya kuwataka waumini wao wasiilaumu serikali katika tukio la ajali na wachukulie kwamba huo ni mtihani kutoka kwa Mungu. Hamdani alisema hata kama vijana hao walibeba bendera za Uamsho wao lakini hawana uhusiano wowote na jumuiya yao.
“Bendera ni kitambaa ambacho mtu yoyote anaweza kuwa nacho na isichukuliwe kila mwenye bendera ya Uamsho ni mwanachama wa jumuiya hiyo,” alisema
Alishangazwa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kwa kurusha mabomu hadi mitaani hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania wanaomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao waliopotea katika ajali ya meli.

Advertisements

13 responses to “Viongozi wa Uamsho watafutwa, 40 mbaroni

 1. Inalillha waina illah rajiunnn huyu kama hana hata aibu anasema uwongo na ramadhani hii?ama kweli Kuna mafisadi katika smz hizo zilianza vipi wakati waumini walikuwa mskitini na kuwaombea ndugu zao kama c wao polisi kutumia mabomu yangetokea hayo Leo wanawasingizia eti uamsho wameanza fujo Ama kweli hawa washenzi tena c watu kabisa bora angeitwa John tujue kuliko kuitwa azizi ushenzi mtupu serikali hii Hatuutakiiiii muungano

 2. Hapo sijaona sababu yakufanya warushe mabom kwani kuomba duwa kwa kukusanyika nivibaya kwa kawaida ya wisilamu nilazima 2ungane ndipo 2kamilishe ibada

 3. M/MUNGU ANASEMA MUNAFIKIRI MUTAINGIA PEPONI KIRAHISI RAHISITU AKIMAANISHA KUWA KAMA HUJAFANYA KAZI YA KWELI NA KUJITOLEA KTK DINI KAMWE PEPO YA MUNGU HUISIKII HATA HARUFU. KWAHIYO BASI HII NI MAREJEO YETU LAZMA TUPAMBANE NAO ILI KUPATA NUSRA YA MUNGU TUSIKATE TAMAA NUSRA YA MUNGU IKO KARIIIBU INSHA ALLAH TUTASHINDA (MUUNGANO HUU USHAELEKEA KIBLA KARIBU TUTAUCHINJA

 4. HUU NDIO UWEZO WA MWISHO WA JESHI LA POLISI LA TANZANIA NA HASA HASA ZANZIBAR. WAKATI KAZI YAO NI KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO WALIPOTAKIWA KWENDA KUOKOA MELI ILIYOKUA INAZAMA NA ROHO ZA WATU ZAIDI YA MIA MBILI JIBU LAO HAWANA MAFUTA. KUPIGA MABOMU UAMSHO MAFUTA YA MAGARI WANAYO. HIVI KAZI YA POLISI TANZANAIA NI KUPAMBANA NA UAMSHO TU. INAONEKANA KATIKA KUPAMBANA NA UAMSHO WANA UWEZO NA RASILMALI ZA KUTOSHA LAKINI KUOKOA ROHO ZA WATU HAWANA UWEZO. PIA WANAONEKANA POLISI NI MAHODARI WANAPOLIKOROGA KUWATUPIA UAMSHO. HII NI MARA YA PILI WANASABABISHA FUJO NA BAADAE KUWAKAMATA VIONGOZI WA UAMSHO. EEEE KAMISHNA MUSSA NA KAMANDA AZIZ JUMA JUENI DUNIA TUNAPITA TU NA KESHO MTAULIZWA. MNAJIDHALILISHA KUTUMIKIA MFUMO ………….. KUDHALILISHA UISLAMU. MUJUE IKO SIKU MUTAFUNGWA MFUNGO WA PIPI NA MTATUPWA PAHALA PEMBAMBA NA PADOGO NA MAVYEO YENU HAYO NA HAO WANAOKUTUMENI KUUDHALILISHA UISLAMU NA WAISLAMU WATAKUKIMBIENI NA KUWAACHIA MZIGO WENU. EE MOLA SISI WAJAWAKO HATUNA NGUVU NI DHALILI TUNAKUOMBA NDANI YA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI UTUKINGE NA MADHALIMU WANAOTUPIGA MABOMU HATA KWENYE IBADA KWA KUWAFURAHISHA WASOUTAKIA MEMA UISSLAMU.

 5. Pingback: Angalia unafiki katika Zanzibar Kuna watu Daraja Mbili First Class na Secound Class ambao ni wananch·

 6. Naona sasa hata kwenda misikitini kusali fardhi Kutahitaji kibali cha polisi, maana pia kusali ni mkusanyiko..
  Tumefikishwa hapa na Watawala.

 7. Kwani huyo Dr, Shein ni M/mungu? kama akisema iwe ndio fatwa? M/mungu kasema musidhulumu wala musidhulumiwe na amri ya M/mungu haipingwi mbona huyo Dr, Shein anaipinga? sasa kwanini yeye asipingwa hiyo nchi si milki yake mihadhara ni haki ya Waislam mbona haendi kuzuia makanisani watu wasihubiei?

 8. Sasa Kama Amri ya M/mung haipingwi jiulize kwanini wamepigwa Mabomu???

  Mikutano ya Aina yoyote ya UAMSHO imepigwa Marufuku Zanzibar.. Au hukumsikia DR SHEIN???

  MNACHOMA MAKANISA HALAFU MNAENDA KUWAOMBEA WATU,KATUBUNI KWANZA DHAMBI HIYO.

  • Inaonekana kama kuna washabiki wawili: (1) wanaoshabikia kutiiwa kwa amri ya mungu na (2) wanaoshabikia kupingwa. Kwa hiyo bwana mkubwa wewe unashabikia kupingwa kwa amri ya mungu, tena kwa kutumia mabomu? Jiangalie. Suala si uamsho, bali ni uislamu unaosakamwa kwa gharama zote hizo.

 9. Kamanda Azizi we ni muislamu, na kila ambalo unalifanya ujue iko siku utaulizwa, leo unadanganya binaadamu wenzi kwa kusema uongo bila hata ya aibu. Nikuulize masuali matatu tu
  1) Dua msikitini ilianza saa ngapi?
  2) Mabomu mulianza kupiga wapi?
  3) Barabara zilianza kuchafuliwa saa ngapi?

  Maana kaa ukijua leo unadanganya wanaadamu wenzio ambao kwa kweli wanajua kila kitu juu ya kile ambacho unachikifanya, ni sawa na kua unamdanganya mtu ambae anajua kila kitu juu ya kile unachomdanganya. Lakini jueni kua sisi vijana siku ambayo mtamueka ndani faridi, Mselem. Azzan, Mussa Juma au yyt yule wa UAMSHO basi jueni kua ndio mtatangaza wenyewe kua muungano ushavunjika maana hakitoeleweka. Msitufanye wazanzibar kua mabwege “Enough is Enough”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s