Polisi yavunja sala ya kuwaombea maiti

Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kushoto ni Azzan Khalid Hamdan, Msellem Ali Msellem, Farid Hadi Ahmed, Khamis, na Mussa Juma Issa wakiswali katika Msikiti wa Mbuyuni kabla ya kusambaratishwa na Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU)

KIKOSI cha Kutuliza Ghasia (FFU) kimezua mtafaruku mkubwa katika mji wa Zanzibar na vitongoji vyake baada ya kuzunguka mji mzima wakiwapiga mabomu ya machozi wananchi. Mabomu hayo yalipigwa baada ya kufika kwenye msikiti wa Mbuyuni ambako waumini wa dini ya kiislam walikuwa wakiwaombe dua watu waliokufa kwa ajali ya meli Mv Skaget.

 
 
Askari hao wakiwa kwenye magari yao walifika eneo la msikiti huo ambapo waumini wakiongozwa na viongozi wa Taasisi za Kiislam chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumuki), walikuwa wakiomba dua.
 
 
Dua hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed ilikuwa na lengo la kuwaombea maiti na majeruhi waliopata ajali ya meli.
 
 
Askari hao walipofika kwenye eneo la msikiti huo walitoa ilani ya kuonyesha mabango yao ya kuwataka waumini hao watawanyike kwenye viwanja hivyo.
 
 
Baada ya kuendelea na ibada yao ambapo walikuwa wamemaliza sala na kuendelea kuomba dua, ndipo polisi walipoanza kurusha mabomu ya machozi na kuwatawanya watu waliokuwemo ndani ya msikiti huo.
 
 
Baada ya kuwatawanya, magari yanayokadiriwa kufikia sita ya FFU yakiwa na askari waliovalia nguo za kujihami, walianza kurusha mabomu katika eneo.
 
 
Baadaye magari hayo yalianza kuzunguka katika vitongoji mbalimbali vya mji wa Zanzibar na kuwashangaza wananchi ambao wengine walikuwa hawaelewi kilichokuwa kikiendelea.
“ Sasa tumekosa nini hadi wanakuja kuturushia mabomu huku tumewakosea nini,” alihoji mwanamke mmoja wa makamo baada ya kusikia mabomu yakipiga mfululizo.
 
 
Watu walikuwa wakikimbia na watoto huku wafanyabiashara wa eneo la Darajani wakisomba vitu vyao na kufunga maduka.
 
 
Katika maeneo ya mitaa ya Kikwajuni na Michenzani, magari hayo ya polisi yalikuwa yakizunguka na kurusha mabomu hadi katika vichochoro vya mitaa hiyo.
Advertisements

26 responses to “Polisi yavunja sala ya kuwaombea maiti

  • @msema

   Kuswalia maiti si kosa.

   Lakini issue kwao Uamsho kuwa watazidi kung’arisha C.V zao humu Visiwani. Ndio maana wamehamanika. UAMSHO JUU MADHAALIMU DOWN.

   Sasa seminar ya Wawakilishi inayoendelea ni zaidi ya UAMSHO Je! Nao mtawapiga mabomu na kuwatawanya?

   Mwiba wa Tasi umekukaeni mnao.

   MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

   JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

   “When peace fails apply force”

   SERELLY.

  • Na kukataa muungano si kosa kama ilivyo si kosa kwa anayekubali muungano. Nchi hii imeweka uhuru wa maoni katika katiba zake. Hivyo, ni wazi kabisa maoni ya watu hayawezi kulingana.

 1. hii ni hatari watu wanasikitika kupoteza maisha ya watu wengi wengine wako kwenye vurugu kwanini jamani inamaana watu wengine wamefurahi?

 2. Hii ya kila siku kupasua mabomu miaani inawaondosha watu hofu. Tujue kuwa siku moja hawa watapambana na polisi uso kwa uso. Hali ya barabara za Darajani na Michenzani na jinsi miti ilivyokatwa eneo la Michenzani kuziba barabara inaonesha kuwa level of militancy inaongezeka, Chonde chonde wenye mamlaka ya kutawala. Binadamu ni tofauti na Mnyama- Hali hii ya sasa ya Zanzibar si ya kuipuuza inahitaji iangaliwe kwa kina! Ni kwa nini hii hali hii hakuwepo wakati wa nyuma ambapo ukandamizaji ulikuwa mkubwa na wa wazi ! Hapo nyuma kwa mfano, watu walitoka Konde wakaja Wete tena kwa miguu kujenga nyumba za Serikali nyumba ambazo leo ni kama vihame. Watu hawa na safari yao yote hii walisimamia na mwenyekiti wa Tawi lao la Afro Shirazi au Balozi wa Nyumba kumi wa eneo lao. Hawakukugeuza njia hawa walikuja Wete wakatumika pasi na malipo hakuna alliyekataa kwa kuwa walikuwa watu wa zama hizo na wakati huu ndio uliotengeneza akili na matendo yao. Katika zama kuna Watu wake!

  Leo hali imebadilika na ukimtaka mtu kufanya jambo la hiari anakuuliza masuali tele!. Sababu za haya zinaeza kuwa nyingi lakini kubwa ni kuwa watu wanabadilika kadiri wakati unavyobadilika. Tutakuwa tunakosea tukidhani kuwa hii ni hali ya kuipuuzia au ya kuintunishia misuli. Arab Spring ilianza kama hivi na Watawala waliotisha wakaanguka na wengine wakafa kwenye mitaro ya maji kama paka! Sisi watu wa huku ambao hujaribu kuzima kila upinzani kwa kutafuta visingizio vya kwa mfano ” hawa ni Wapemba, Hawa ni Mujahiddina, Hawa ni CUF hawa ni nakadhalika nakadhalika inabidi tusome alama za wakati. Kuna visa vingi vya kutufanya tujifunze na sisi tuongozao si wachanga wa kutovijua visa hivyo!

  • Inashangaza. Jeshi la TZ, hasa polisi, ni wataalamu kupiga raia kwa mabomu wakati wa maafa hawana jipya ni kama raia wa kawaida; wanasubiri msaada toka Afrika kusini au Israel. Inasikitisha sana. Wajifunze na kuokoa si kupiga raia TU.

 3. Pingback: Hali tete Zanzibar·

 4. Ama mie sjawahi kuskia kuwa watu kudai haki yao ya nchi yao na kupingwa mabomu lakini hii ni ishara ALLAH SW anatuonesha kwamba tumekaliwa kimabavu na ukoloni mweusi ambao ni tanganyika huuu muungano hatuutaki ya nini kulazimishana banaa ntie mbona hamuskiii au ndo wale mliotanjwa kwenye qur,an baadhi ya viongozi wetu wa pale ALLAH SW aliposema (sumuun bukumun umuyun fahum laa ya rajiuu)jee mna macho lakini hamuoni mna maskio lakinni hamskiii kwa hakika kwa MOLA wenu mtarejea?ipo siku inshallah yatakwisha haya na tutakuwa na zanzibar yetu kamili amin….mbona tanganyika hampigi mabomu huko tumechokaaaaa na nyinyiiii

 5. nawewe ahmed usiwe mpuuzi naona unasema mkoloni mweusi ndiye kawakalia unataka uniambie kwamba kutokana na vurugu za jana ni kuhusu muungano? na hao FFU ni watu wa muungano au ni wazanzibar wenzenu ndio waliofanya hivyo. ninyi kwenu kina wauma kweli mkuki kwa kitu adimu(ngurue ni mtamu ila kwa binadamu ni mchungu mfanye nyie tu mbona mlichoma makanisa watu wakakaa kimya leo hii ninyi mmefuatwa msikitini eti mnanung’unika eti mnasalia maiti na dhambi mlizonazo mnamsalia nani hata mkisali kwa mazambi yenu mm naona mnajisalia laaana

 6. @hatari.
  Hujielewi wala hujitambui, upo tu…watu wakisema na wewe useme.
  Hayo makanisa mliyachoma wenyewe ili mupate la kusema…ungesikiliza maneno ya uamsho ungepata kufunguka, lakini wapi unakaa unapewa tango pori tu.
  Na hao FFU wanappokea amri kutoka wapi? Nakushauri tafuta CD za UAMSHO ili uamke, makanisa znz yapo zamani wala hakuna muislamu atakaye acha kazi zake kuyachoma. Huo ni mpango uliopangwa ili kuwatoa wazanzibari ktk ajenda ya msingi kudai nchi yao.

  hatari kuwa na mawazo hayo hainishangazi maana nyie wenzetu bado mumelala. Wazaznibari wakidai haki yao munawatoa katika ajenda yao ya msingi. Hebu sikiliza baraza la wawakilishi utajua nini sisi tunahitaaji.

  Usiwe mtu wa kukurupuka, angalia vizuri muktadha unaozungumziwa.

 7. Laa haulaa!… Mi jamani natoa tahadhari tu kwa viogozi, ikiwa wamekosa washauri wazuri. Kwa jinc ya hali inavyokwenda na ninavyotabiri mimi kutokana na uzoefu wangu mdogo na maarifa yangu mepesi ni kua viongozi wasipowasikiliza wananchi matakwa yao, basi waelewe kua hali watakuja ijutia baadae (jambo ambalo halitowasaidia) Wajue kua kila jambo huanza kidogo kidogo na kukua sik hadi siku. Na ninavyotabiri ni kua hali hali hii haitosimama Abadan, na hatimae ni hasara kubwa ambapo lawama zitakuja kwao viongozi, kwa kosa lao la kutoifata katiba. Manake mi nadhani kua kama kiongozi alikua hayuko tayari kuiongoza nchi kwa katiba iliopo, ilikua atunge yake au asiingie madarakani mpaka aekewe katiba anayoiweza. kwa sababu leo imekua wananchi wanajitahidi kufanya mambo yao kwa misingi ya kikatiba, hatimae viongozi ndio huwashtumu kua wamekosea na kuwachukulia hatua za kinguvu. Tahadhari.!!! Mkumbukeni Gadafi. Mkumbukeni Hosni Mubarak na Misri yake. Kumbukeni Tunis.. Hata hivyo msiende mbali mkumbukeni DR. Salmin Amour Juma. Leo pale Kisonge washamsahau, hata kumtaja hawataki.
  Leo Viongozi hem anagalieni mazingira yalivyochafuliwa..! Mji ulivyoharibiwa..! Tena bila hapakua na sababu. Na yote hayo si mwengine ila lawama zinakuja kwenu. Angalia Michenzani miti ilivyokatwa. Angalieni palivyobadilika na kupoteza hadhi yake na mandhari yake ilokua inavutia.. Jana imekatwa mitatu, na kesho mitano, hatimae tutakua kama tupo jangwani. Nanyi ndio mtaoulizwa, na mtakosa jibu…. Mawazo ya wananchi lazima yaheshimiwe….Na eleweni kua hili halitosima ikiwa hamtowasikiliza wananchi…! Kaeni mkifikiria. ! Hii nchi ni yetu sote.

 8. NAHISI WAZANZIBAR WAMESAHAU MSEMO HUU WA RAIS WAO

  MUUNGANO HAUTAFUNJIKA NITAUTETEA NA KAMA WAKIWAITA MKAANDAMANE MSIENDE. Uamsho imepingwa marufuku kuweka Mikutano ya aina yoyote ile.-DR SHEIN

  • Nikweli DR Shein ni rais wetu na tunapaswa kumsikiliza lakini tuliompa huo uraisi ni ss hivyo na yy ana jukumu la kutenda yale wananchi tunayoyataka

 9. ivi mm niwaulize wazanzibar tupo hatupo au tumelala ivi tutadhalilishwa hivi mpaka lini kila siku watuonee wao tu ivi sie hatuna mikono hatuna maarifa kw nini tusitumie akili kama wao wanatumia silaha kweli kw kujitokeza mikono mitupu hatuwawezi ila tunaakili naomba tuzitumie tumechoka kunyanyaswa na wao hivi wanatuvotufanyia hawa askari na sie tukiwa tumetulia wanatuona thalili na hatuwezi kupigana nao ivi hawa ffu wako wangapi hapa zanzibar wnakaa wapi na femilia zao kw nini watunyanyasie ndugu zetu halafu wao wastarehe na familia zao mm nataka miti tusiiyangushe barabarani tukayaangushe majumbani mwao wao wanatumua risasi kw kutuuwa wanatumia risasi kw kuwasha moto
  hivi sisi hatuna silaha za kuuwa hatuna petrol ya kuwasha moto mana hii ni jihadi walianza kivyama sasa watuharibia uislamu hata mungu yuko radhi kupigana jihadi kw uislamu na kutetea maslahi ya waislamu
  tumechoka nac tunajianda sasa watuache tupumue

 10. Wewe kijana kuwa na nidhamu na dabu zako ukichangia ktk habari hizi. wewe nani unayejua kuwa watu fulani wana madhambi? au umepewa jukumu hilo la kuandika madhambi yetu? Pumzi zisikuhadae utakuja kujuta. Kuwa makini mdogo wangu

 11. YOTE TISA, KUMI MUUNGANO HAUTAVUNJIKA. Uamsho kimeshaambiwa ni kikundi kidogo cha wahuni kwahiyo Msikifuate-DR SHEIN

  @Kwa m2 aliyesema muwafuate FFU nyumbn na kuwabomolea majumba hii inadhihirisha jinsi gani Mlichoma makanisa kwa kukusudia. NA OLE WENU MJARIBU KUBOMOA MAJUMBA HAYO MTAONA ZANZIBAR NI NDOGO NA MTAFIA JERA TENA ZA TANGANYIKA SIYO ZANZIBAR

  DR-SHEIN-muislam
  Kikwete-muislam
  Makamu wa rais-muislam
  Jaji mkuu-Muislam
  Mkuu wa Polisi -muislam

  MNAJIUA WENYEWE KWA WENYEWE

 12. @Okey. Watu hawazungumzi kwa jazba kuwa ipo siku nao polisi watapata kipigo cha raia wema waliochoka kupigwa mabomu. Hii ni kanuni ya kimaumbile. Hata babu zetu walikuwa raiya wema wa serikali za kikoloni lakini walipochoka waliingia njiani kuziasi serikali hizo.

  Kwa hivyo polisi nao wasione kila siku watawapiga raia mabomu bila ya kosa. hivyo tutarajie mema kwa raia wakati polisi wetu hawatendi mema? Huo ni wazimu ndugu yangu. Hata mtoto ukimpiga sana mwisho huwa sugu, hata akipigwa huona kitu cha kawaida kwake.

  Na hilo kanisa lenu mlilolichoma linakuuma sana? Si kuna kesi ipo mahakamani? Cha msingi muwe wavumilivu subirini kama UAMSHO wametia moto makanisa watahukumiwa tu, mna wasiwasi gani? Mbona hamjiamini.

  Lazima tujue kusoma alama za nyakati, Muungano huu hata muyachome makanisa yote muwasingizie UAMSHO basi kazi bure, hautadumu kwa vile raiya hawana imani nao.

  “DHULMA HAIDUMU, NA IKIDUMU HULETA MAAFA”

  ZANZIBAR HURU KWANZA, POROJO NYENGINE BAADAE.

  TUACHIWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE………TUPUMUEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE……

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s