Wengi waliofariki ni watoto na wanawake

Miili ya watoto wadogo ikisubiriwa kutambuliwa katika uwanja wa maisara ambapo bado umati mkubwa umekusanyika kusubiri kutambua maiti zao waliofariki wengi wao ni akina mama na watoto

MAITI za ajali ya Mv Skagit zilizosafirishwa kwenda Dar es Salaam ziliondolewa bila kufuata utaratibu hali ambayo imevuruga utunzaji wa kumbukumbu za vifo vya ajali hiyo. Mratibu wa upokezi wa maiti za ajali hiyo, Abdulbaq Habib alisema jana mjini kwamba kasoro hiyo imesababishwa na Idara ya Maafa ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Bila kutaja idadi ya maiti zilizosafirishwa kwenda Dar es Salaam, Mratibu huyo alisema ziliondolewa bila kujua ni maiti gani na zenye namba gani.

“Tunapopokea maiti tunaandika namba, na zinapotambuliwa tunataja kwamba maiti yenye namba fulani ni mtu ambaye tunamtaja kwenye jina letu kwa ajili ya rekodi,” alisema.

Habib alisema kuna maiti zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha hospitali ya Mnazi mmoja ambazo zilisafirishwa bila kufahamu ni za majina gani na namba zipi licha ya kutambuliwa na ndugu zao.

“ Kwa hiyo hadi sasa kwenye rekodi zetu kuna maiti ambazo zimetambuliwa na ndugu zao lakini hakuna kumbukumbu zilizopo,” alisema Habib.

Maiti wazikwa na serikali

Maiti zote 10 ambazo hadi jana zilikuwa hazijatambuliwa zimezikwa na serikali kwenye eneo la makaburi ya Kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar baada ya kusaliwa na mashehe wa dini ya kiislamu.

Hata hivyo maiti hizo hazikuzikwa kwa wakati mmoja, kwani kila maiti ilisaliwa kwa wakati tofauti kwenye viwanja vya Maisara na kupelekwa kuzikwa kwenye eneo hilo.

Mzungu ashindwa kutambuliwa

Mzungu ambaye alikufa kwenye ajali hiyo na ambaye uraia wake bado haujajulikana, bado hajatambuliwa.

Taarifa zilizopatikana zilisema serikali inafanya juhudi kuwasiliana na balozi za nchi mbalimbali ili kutambua mwili huo.

Maofisa wa balozi mbalimbali wamekuwa wakifika kwenye Hospitali ya Mnazimmoja ili kuangalia mwili huo kama ni kutoka katika nchi zao.

Watu wa kutoka katika mataifa mbalimbali yakiwemo ya Uingereza, Marekani, Ubelgiji, Ujerumani, Kenya na Burundi waliokuwemo kwenye meli hiyo.

Ndugu wa waliokufa wazungumza

Musa Ahmed, mkazi wa Mwanakwerekwe ambaye ni ndugu wa marehemu Ali Hassan, aliyekufa kwenye ajali hiyo alisema ajali hiyo inatokana na ubovu wa boti hiyo.

“ Kama ajali hiyo imesabishwa na upepo mkali basi meli nyingi zingezama, kwa sababu upepo baharini ni jambo la kawaida, ninachoamini ni kwamba meli hizo ni chakavu,” alisema.

Alisema serikali ikiendelea kutochukua hatua ya kurekebisha usafiri wa meli basi kila mwaka yataendelea kutokea maafa.

Mkazi wa Kisiwandui, Athuman Mussa ambaye amepoteza ndugu yake kwenye ajali hiyo, alisema serikali inatakiwa kuchukua hatua kali kumaliza tatizo la ajali za meli Zanzibar.

“Bila kuzipiga marufuku meli chakavu, ajali za meli zitaendelea kupoteza wananchi hapa Zanzibar,” alisema.

Zabibu Mahmoud ambaye amepotelewa na mama yake na ndugu yake anasema ameanza kukata tamaa kutoka na kuwa hadi sasa zoezi hilo likifikia ukingtoni hajaona miili ya wazazi wake.

“Mimi mama yangu ameondoka dar es salaam kuja Zanzibar nilikuwa ndani ya daladala nikapigiwa simku nikampokee mara nasikia kuwa kuna meli na nilipowasiliana na nyumbani nikaambiwa meli iliyopata ajali ndio hiyo hiyo waliopanda jamaa zangu ….” alisema huku akiwa na huzuni kubwa.

 

Advertisements

One response to “Wengi waliofariki ni watoto na wanawake

  1. Inna Lillah Wa Inna Ilayh Rajuun. Masikini watoto hawa adhimu laiti tungekuwa na serikali sikivu kweli na viongozi wanaojali wananchi, hasa wanyonge, kama wale waliosafiria chombo kile, WATOTO HAWA WANGENUSURIKA. Ni sawa na kusema serikali zimeua watoto hawa. Lakini ndo yamepita maana si tayari tushamsingizia Mwenyezi Mungu. Kama vile hakutupa akili na maarifa ya kujikinga na majanga au basi kusaidia dharura inapotokea.
    Haya twendeni tu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s