Wazanzibari wanaogawanyika waonywa

Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Uzini (CCM), Mohammed Raza nje ya ukumbi wa Baraza la wawakilishi

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi Zanzibar wameonya kuwa mgawanyiko wa wazanzibari katika suala la kutoa maoni juu ya katiba unahatarisha malengo ya wazanzibari katika muungano. Tahadhari hiyo imetolewa wakati wajumbe hao wakijadili hutuba ya bajeti ya wizara ya katiba na sheria iliowasilishwa na waziri wa wizara hiyo Abubakar Khamis Bakari katika baraza la wawakilishi.

Walisema wakati huu wa ukusanyaji wa maoni ili kuandika katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni muhimu kwa wazanzibari kutogawanyika na kwamba msimamo wa kudai maslahi ya taifa ni muhimu kuliko misimamo ya vyama au mtu binafsi.

Waliojitokeza na kutoa tahadhari hiyo ni pamoja na Mwakilishi wa viti maalumu Asha Bakari Makame (CCM) mwakilishi wa jimbo la Uzini (CCM) Mohammed Raza, mwakilishi wa jimbo la mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu, mwakilishi wa jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk na mwakilishi wa jimbo la Kiembe samaki (CCM) Mansoor Yussuf Himid.

“Chuki baina yetu ilikuwepo kwa muda mrefu lakini mwenyeenzi mungu akatuleta baraka ya serikali ya umoja wa kitaifa hatupaswi kugawanyika tunapodai maslahi ya taifa” alisema Asha.

Asha ambaye aliwahi kuwa waziri wa serikali ya Zanzibar alisema mitazamo tofauti juu ya muungano isiwe chanzo cha kuwarejesha nyuma wazanzibari walipotoka na kuomba wanasiasa kuwa ni mfano wa kuwaongoza wananchi katika kutoa maoni kwa kuvumiliana.

“Huu ni wakati pekee na fursa muhimu sana katika historia ya nchi yetu hatupaswi kugawanyika kwa sababu zisizokuwa na msingi muelekeo uwe mmoja katika kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano na tusikubali kugawanywa” Jussa alitahadharisha.

Jussa alisema umoja wa wazanzibari itakuwa ni kuwaunga mkono viongozi waliotangulia katika kuitetea Zanzibar ambao kwa wakati huo walipata misukosuko katika utetezi wao huo.

Aliwataja viongozi hao kuwa ni muasisi mwenye wa muungano Mzee Abeid Karume, Mzee Aboud Jumbe, Maalim Seif, na hata Amani Abeid Karume ambao wote walipashikwa majina mbali mbali na kumtaka rais wa sasa Dk Ali Mohammed Shein kutoogopa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya muungano.

Akichangia katika hutuba hiyo Raza aliwataka viongozi kuanzia mawaziri wajumbe wa baraza hilo pamoja na wabunge kutoogopa kutetea maslahi ya Zanzibar na kwamba hapajakuwepo uwazi wa makubaliano katika mambo ya muungano ambayo orodha yake ilianzia mambo 11 na sasa ziadi ya 22.

Raza alisema muungano utakaotoa nafasi ya Zanzibar kujiamulia mambo yake wenyewe ni fursa muhimu ya kuendelea kiuchumi ikiwmeo suala la kujiunga na jumuiya ya Umoja wa Kiislamu (OIC) na mashirika mengine ya kimataifa.

Makame Mshimba alisema wananchi wa Zanzibe wana matumaoni makubwa na viongozi wao lakini baadhi ya viongozi kuanza kutumia majina na lugha mbaya dhidi ya wenzao wenye mitazamo tofauti ni hatari na inavunja moyo wananchi.

“Labda tusaidiwe maneno haya yanayoibuka ya mpinzani, si mwenzetu, uamsho, tupumue, maana yake ni nini? Wakati kila mtu ana fursa na haki ya kutoa juu ya muungano?” Alihoji mwakilishi huyo.

Mwakilishi wa kiembe samaki alisema wazi kwamba muungano wa hivi sasa unahitaji mabadiliko ili wazanzibari wapate fursa ya kumiliki uchumi wao ili kuweza kusaidia vijana wengi ambao hawana ajira hivi sasa.

Alisema si vyema kwa baadhi ya viongozi wakiwemo wajumbe wa baraza la wawakilishi kuonesha chuki dharau na majigambo na kuanza kutoa majina yasiofahamika dhidi ya wale ambao msimamo wao ni wa kukataa muungano.

“Huu sio wakati ule wa kutishana kama mtu ana mtazamo tofauti na wako hata wa kukataa muungano basi mwite na umpe hoja za kuunga mkono lakini sio kutumia mabavu na nguvu” alisisitiza.

Mansoor alisema baadhi ya watu wamefika mbali na kuanza kutoa vitisho kuwa utawala wa kisultani utarudi wakati katiba hazitoi fursa hiyo na kwamba wazanzibari pia walipindua ili kujitawala na hivyo kamwe Zanzibar haitaweza kurejesha utawala wa kisultani.

“Sisi tunaotaka mabadiliko eti tunambiwa tunataka kumrejesha sultani hii nchi ilipinduliwa na sultani gani anayetaka kurudi Zanzibar? Tusiwatishe mabibi zetu na wazee wetu waliopo huko mashamba kwa kusema maneno ya uongo hapa sultani hawezi tena kurudi” alisema waziri Mansoor.

Mikakati yawekwa kupambana na madawa ya kulevya

SERIKALI inakusudia kuweka mikakati imara ya kupambana na madawa ya kulevya visiwani Zanzibar kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali ikiwa pamoja na kuwabaini wafanyabiashara wakubwa wa biashara hiyo.

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya makamo wa kwanza wa rais, Fatma Abdulhabib Ferej wakati akijibu suali kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu na kusema kwamba vita dhidi ya madawa ya kulevya sio kazi nyepesi.

Jussa alitaka kujua mikakati ya serikali kupitia ofisi ya makamo wa kwanza wa raia katika kukabiliana na changamoto ya kurudi upya kwa uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya katika mitaa ya mji wa Zanzibar.

Waziri huyo alisema kuwa tayari ofisi yake imekutana na wadau mbali mbali wanaohusika na udhibiti na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili kupata maoni yao juu ya namna ya kulikabili tatizo hilo shughuli ambayo ilifuatiwa na mkutano uliozungumzia kwa kina changamoto zilizoibuliwa na wadau hao pamoja na mikakati mipya.

Alisema ofisi ya makamo wa kwanza wa raia pia iliandaa kikosi kazi kilichojumuisha taasisi mbali mbali za dola zilizo katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kuandaa njia maalumu (road map) ya utekelezaji wa sheria ya madawa ya kulevya Zanzibar.

“Naomba mjumbe pamoja an wawakilishi wengine kwa jumla wa baraza hili kuwa na subra kwa kipindi ambacho mchakato wa ukamilishaji wa roadmap hiyo ukiendelea naamini kukamilika kwa mchakato huo kutakuwa ni dira kwa taifa letu katika kupambana na madawa ya kulevya nchini” alisema.

Aidha waziri huyo alivitaka vyombo vya dola vilivyopewa jukumu kukamiliana na tatizo hilo kuongeza kasi ya utendaji kazi zao ili kunusuru vijana wa taifa ambao ni wahanga wakubwa katika janga la madawa ya kulevya.

Fatma alisema kati ya mwaka 2010 hadi juni mwaka huu kesi 339 ziliripotiwa ambapo baadhi zimechukuliwa hatua na nyengine zinaendelea kuchukuliwa hatua katika ngazi za polisi na mahakama.

Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba sambamba na kudhibiti madawa ya kulevya pia ofisi yake inaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari pamoja na kusaidia vijana ambao wamekusudia kuachana na madawa ya kulevya ambao wapo katika nyumba za soba house Unguja na Pemba.

“Kwa kutambua mchango wa taasisi zisizo za serikali katika suala zima la mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, ofisi yangu kupitia tume ya kuratibu na kudhibiti madawa ya kulevya ilitoa milioni 9.9 kwa nyumba tisa za soba houses Unguja na Pemba” alisema.

Waziri huyo alisema ofisi yake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo na kutoa wito wa taasisi nyengine mbali mbali za kijamii kwa jumla kuendelea kutoa msukumo na michango katika kuendeleza mbele harakati dhidi ya madawa ya kulevya visiwani Zanzibar.

Advertisements

8 responses to “Wazanzibari wanaogawanyika waonywa

 1. nimefurahishwa sana, na kauli za viongozi wetu hili linaonesha ukomavu wa siasa walionao, inshallah mola awape moyo huo huo waendelee kushikamana kwa ajili ya kuikomboa nchi yetu, tukibaki na hali Allah nae atakuwa nasi, inshallah ameen.

 2. (M) (U) (U) (N) (G) (A) (N) (O)

  (M). Muungano kwetu basi, Tumechoka taabani.
  (U). Uvunjike katikati. Sote hatuutamani.
  (U). Ukoloni wa mweusi, Umetufika rohoni.
  (N). Nasi tuongeze kasi, Kuuchukia moyoni.
  (G). Geuka ewe raisi, Nchi yetu tuihami.
  (A). Allaah atupe wepesi, Tuuzike kaburini.
  (N). Neema walofilisi, Zirudi kama zamani.
  (O). Omba kwa wetu Qudusi, Tuitikie Amini.

  By: AlRumhy.

 3. hayo maneno ya wawakilishi yana walakini , wanazungumzia kutoa maoni , na kuendelea kwa muungano, badala ya kuzungumzia kuvunjika kwa muungano , wote wanafiki wakubwa wanaogopa mabwana zao tanganyika au wamepewa chochote, tunasema muungano hatuutaki , hakuna la suala la kutetea maslahi ya znz ktk muungano , hee hamuelewi viziwi , vipofu?

 4. MuunGano jamani Hatuutakiiiii sie wananchi kwanini mnatulazimisha?inshallah Allah yupo pamoja na sie namini ipo siku utavunjika tu amin tishikamane wazanzibar kuidai nchi yetu Mpka kieleweke hapa tunechoka na dhulmaa angalieni viongozi Allah atustiri yasije kutokea kama ya egpty umma ukamua na kutoa kuanzia rais Mpka wale wanaotupinga Haya tupo yana mwisho Haya inshallah hakuna nguvu km ya umma

 5. Hawa watu wanaonadi sera za uvyama katika maslahi ya zanzibar sasa hivi hawana nafasi. Sisi tunawapa heko viongozi wote pamoja na wawakilishi wetu walio bega kwa bega na raia zao katika suala la kudai ZANZIBAR HURU YENYE MAMLAKA KAMILI. Hawa ndio viongozi wa wananchi. TUNAWALANI VIONGOZI WOTE WANAO LINDA NA KUTETEA MUUNGANO WAO TUNAWAJUWA KUWA WAMEWEKWA KWA MASLAHI YAO NA MUUNGANO TU. Sisi hatuutaki muungano huu wa kidhulma. Tusilumbane na kugawanyika makundi. NAAMINI TUTASHINDA KWA UMOJA WETU TUKISAIDIWA NA MUNGU. Nyie akina Borafia zindukeni wakati umefika au ndio nyie ……, muliopotea. ZANZIBAR HURU INAWEZEKANA KARIBU KITAELEWEKA UMOJA WA WAZANZIBAR NDIO SERA YETU ITAYOTULETEA KUVUNJA MUUNGANO.

 6. A/Alaykum.

  Broo Mansour Yussuf Himid vipi huyu Mheshimiwa Haroun Ally Suleiman mnamshughulikia vipi?

  Maana kasumba zake za kuwapa pesa Tshs 10,000/= raia wakatoe maoni yake bado anaiendeleza na wiki iliyopita walikuwa katika kijiji cha Fumba.

  Ushauri wangu kaeni naye mumfahamishe ili awe pamoja na wenziwe aache huu mchezo.

  Kama hatabadilika basi msitulaumu sisi vijana kwa sababu tunapajua pa kumpata na nini cha kumfanyia ili kunusuru nchi yetu. Sisi hatupo kwenye matani kwa wakati huu wala hatuhitaji ruhusa ya mtu kwenye hili. Gohead katuachia zamani Babu yetu mpenzi Abeid Aman Karume.

  Uzalendo leo vyama jana.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha Ombi na Onyo kwa niaba ya Vijana wa Taifa.

  SERELLY.

 7. wazanzibar msiotakamuungano swali no 1 muungano unawatianjaa? Au. Unawavunjia heshima? Au. Nimchanganyiko wa ujinga nauzembe wa kimawazo Si kwamba napenda au sipendi bali keleleza baazi ya wazanzibar zinaniumiza kichwa hawajadilimaendeleo yao bali Ni muunganotu. Kunahasalagani kati ya tanganyika? Na zanzibar? Kamasio tunawabeba sisi hatunanjaa bwana aunamnagani vipi bana sinasema na wewe unaepinga muungano kamavipi hamazanzibar kajifiche

  • Yaani mie hawa Viongozi wa zanzibar hata sijuwi oki Vipi wamezaliwa znz wamekulia hapo wanaijuwa chini juu jinsi hapo zamani znz ilivyokuwa n’a sasa ilivyo . Waangalie visiwa vya wenzetu caribik .n.k jinsi walivyoendelea kwa biashara ya wageni tu . awatiza nchi za ulaya miaka ikisha ya raisi wananchi wakichanguwa chama wanachokitaka kinaendelea chama kipya lakini nyumbani ccm ikipata ikikosa wao ndo wenye ambri tumeshinda . Nyie viongozi wa zanzibar funguweni mabichwa tenu yalokuweko n’a maki ndani kayatoweni akili hammnahata kidogo nyie wajinga wakubwa nendeni mukasome wapumbavu wakubwa nyie kisiwa cha zanzir mukiokowe mulitengeze kisiwa chenu vijana wapate kazi. Vijana wanaenda schule wabongo wanawafelisha hawana la kufanya tena ndomana waanaanza kula madawa ya kuvywa kwasababu zanzibar gamma kampuni ama kujindesha Enyewe watanganyika wamekupokonyeni cuite nyie ndio sababu vijana kula madawa ya kulezwa kwasababu zanzibar hakuna kazi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s