Kuna ‘Mamluki’ ndani ya CCM-UVCCM

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umewatuhumu baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotoka Chama Cha CCM na kutishia kuwanyanganya kadi za uanachama kutokana na kuwa sawa na ‘Mamluki’ katika matendo yao. Kauli hiyo imetolewa juzi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho uliofanyika viwanja vya Komba wapya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ambapo Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mjini, Mohammed Ali Khalfan alisema CCM inaweza kuwanyanganya kadi za chama hicho viongozi hao.

Alisema viongozi hao ambao ni wajumbe wa baraza la wawakilishi zanzibar wameonekana kuwa na mtazamo tofauti na chama chao na hivyo kutaka wachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa kadi za chama hicho cha CCM.

Katibu huyo alisema wapo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaokwenda kinyume na maadili ya chama hicho ambao amewafananisha kutokuwa na tofauti na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI).

“Ndugu Mwenyekiti tunaomba utupelekee salamu zetu kwa hawa Wawakilishi wetu wa CCM ambao ni mamluki waambie Umoja wa Vijana wa (CCM) tunawajuwa wanavyofanya na ipo siku tutawataja majina yao hadharani” Alitishia Katibu huyo wa Wilaya.

Katibu huyo alisema kwamba UVCCM inashangazwa na Wawakilishi hao wa CCM kupoteza mwelekeo kwa baadhi yao kuvuka mipaka ya imani ya Chama chao na kuunga mkono sera na itikadi isiyotokana na Chama hicho kikongwe hapa nchini.

“Mheshimiwa mgeni rasmi kama tulivyosema tufikishie salaam zetu kwa hao Wawakilishi wanaotokana na CCM, waambia itafika wakati tutawanyanganya kadi zetu kwa sababu hawatuwakilishii chama chetu” Alisisitiza Katibu huyo.

Huku akishangiriwa na waliohudhuria katika mkutano huo Khalfan aliwapongeza Wabunge wa CCM akiwataja kama viongozi wanaotetea imani, sera na itikadi ya chama chao ndani na nje ya Bunge, akitoa wito kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM kuiga mfano huo juu ya utetezi wa kulinda na kuhifadhi Muungano.

Katibu huyo alisema faida za Muungano ni nyingi na itachukua muda kuzimaliza kuzitaja, lakini jambo la msingi kwa Wabunge na Wawakilishi kutetea kudumu kwa Muungano ambao sasa umetimiza miaka 48 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1964.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Borafia Silima Juma ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwakumbusha hasa vijana ulazima wa kuulinda Muungano huku akiwataka kuwapuuza watu wanaoubeza Muungano huo akisema haujawahusu.

“Hawa watu wanaotaka Muungano uvunjike waulizeni wameunda wao, Muungano bwana ni wetu sisi tangu zamani Afro Shiraz Party tulikuwa na imani yetu na ahadi za mwanachama ambazo ni pamoja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ” Alisema Mwenyekiti huyo.

Akitoa historia Borafya aliwaambia wanachama wa chama hicho ambao wengi wao walikuwa ni vijana kwamba Chama cha ASP ndicho kilichoungana na TANU kuunda Chama cha Mapinduzi Februari 5 mwaka 1977 katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar ambapo Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho alikuwa Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Makamu Mwenyekiti wake, Aboud Jumbe Mwinyi.

Borafia alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni matokeo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 Mapinduzi ambayo ndio yaliyokata mizizi ya Utawala mkongwe wa Kisultan Zanzibar hivyo CCM itaulinda kwa gharama yoyote Muungano huo uliopo na hakuna sababu ya kuogopa watu wenye kupinga.

Mbali na kuwaeleza wanachama hao suala la muungano, Borafya ambaye anatambulika kwa kupiga watu vijembe na kutumia lugha ya matusi wakati mwengine anapokasirika aliwashambulia viongozi wa jumuiya ya UAMSHO kutokana na elimu wanayoitia kwa umma na kusema kwamba jumuiya hiyo haina nguvu za kuwashawishi wananchi kuvunja Muungano na khasa kwa kuwa dhamira ya jumuiya hiyo inatambulika.

Bila ya kutaja dhamira ya jumuiyo hiyo, Borafya aliwataka wana CCM kupuuza maneno yatakayotolewa na viongozi wengine wasiokuwa CCM na kuwataka vijana kuwa macho na kuutetea Muungano akisema una faida kubwa ingawa hakutaja faida lakini alisema faida zipo nyingi na Zanzibar inanufaika na faida hizo.

Kwa upande wake Kada maarufu wa CCM Zanzibar, Baraka Mohammed Shamte alielezea faida mbalimbali za Muungano kiuchumi, kisiasa, na kijamii, lakini pia hasara ikiwa utavunjika na kuonya kwamba wanaoleta chokochoko hawaitakii mema Zanzibar wala Tanganyika .

Shamte alisema uhuru wa Zanzibar wa mwaka 1963 haukuwa uhuru wa kweli kwani badala ya kukabidhiwa vyama vya ZNP na ZPPP Serikali ya Uingereza ilimkabidhi Sultan wa Zanzibar kwa kuwa ndiye waliyekuwa wakimlinda, hivyo kufanya ASP kufanya mapinduzi Januari 1964.

“Mimi baba yangu ndie aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika uhuru bandia wa mwaka 1963 nafahamu mambo mengi kuliko nyie kwanza wengi wenu ni watoto wadogo hasa nyie Uamsho hamjui lolote, kwa hivyo Muungano utadumu mtake mistake” Alisisitiza Shamte huku akishangiriwa na wanachama hao.

Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) imeingia katika malumbano tokea kuanza kwa suala la katiba ambapo kila upande umekuwa ukifanya mikutano ya hadhara na kila upande kuwa na kauli yake wakati Uamsho wakitaka kuvunjika kwa muungano ambapo CCM wanasema muungano huo hauvujiki.

Uamsho imekuwa ikifanya mihadhara ya nje lakini serikali ilipiga marufuku mihadahara hiyo na jeshi la polisi kuwatawanja waumini hao kila mwisho wa wiki ambapo sasa wanatakiwa kufanya mihadhara yao ndani ya misikiti wakati chama cha CCM kikiwa kimesitisha mikutano yake na ndio kwanza kimeanza kufanya sasa mikutano hiyo tokea kupigwa marufuku na jeshi la polisi.

Advertisements

20 responses to “Kuna ‘Mamluki’ ndani ya CCM-UVCCM

 1. Mi nashangazwa na maneno ya huyu katibu wa UVCCM anaposema Wawakilishi wanokwenda kinyume na maadili ya chama chao wanyanganywe kadi kwa kuwa hawakiwakilishi chama chao!! kwani wanawakilisha chama au wanawakilisha wananchi?

 2. Haya tena wengine wanataka uhuru na wengine wanaupinga haya yote maisha tuachiwe tupumuwee hakna baraka wala borafya tupumue kwanza

  • (M) (U) (U) (N) (G) (A) (N) (O)

   (M). Muungano kwetu basi, Tumechoka taabani.
   (U). Uvunjike katikati. Sote hatuutamani.
   (U). Ukoloni wa mweusi, Umetufika rohoni.
   (N). Nasi tuongeze kasi, Kuuchukia moyoni.
   (G). Geuka ewe raisi, Nchi yetu tuihami.
   (A). Allaah atupe wepesi, Tuuzike kaburini.
   (N). Neema walofilisi, Zirudi kama zamani.
   (O). Omba kwa wetu Qudusi, Tuitikie Amini.

   By: Al’Rumhy.

 3. HAWA UVCCM SASA WANAANZA KUPAZWA WATU WANAONGELEA MASLAHI YA NCHI WAO BADO WANA UCCM TU MPAKA LEO. TUNAWAJUA HAWA WOTE HAWANA UCHUNGU HATA CHEMBE NA ZANZIBAR KWA KUA WENGI WAO SIO WAZANZIBARI HALISI NI WALE WA KUCHOVYA WALIOPEWA UZANZIBARI NA MASHEHA WAKATI WA UCHAGUZI WA 1995 NA HUYO BARAKA SHAMTE ANAJULIKANA MATATIZO YAKE KILA KONA YA ZANZIBAR HATA NDUGU ZAKE WA BABA MMOJA HAWAMSIKILIZI. WAZANZIBARI TUSISIKILIZE MANENO YA WASALITI HAWA UVCCM TUZIDISHE NGUVU NA KAMPENI YA NYUMBA HADI NYUMBA KUHAKIKISHA MUUNGANO HUU UNASAMBARATIKA NA WAZANZIBARI TUNAACHWA TUPUMUE. KITENDO CHA UVCCM NI KUKOSA ADABU KWANI WAWAKILISHI NI WAKUBWA ZAO KICHAMA NA HAWAPASWI KUWAITA WASALITI MBELE YA KADAMNASI YA WATU BILA YA USHAHIDI MADHUBUTI. PIA WAWAKILISHI KAMA BINADAMU WANA HAKI ZAO ZA MSINGI NA HAWALAZIMIKI KUKUBALI HATA MABAYA YA CCM IKIWEMO HILI LA KUIUZA ZANZIBAR.

 4. SASA IKIWA BARAKA NA BORAFYA WANATANGAZA RASMI UAMUZI WA CCM JUU YA MUUNGANO,,, KWANI KUKAWEKWA MAONI YA KATIBA,,,, NA WAO KAMA NANI KUWAAMULIA WAZANZIBAR,,,, AU KUIHUKUMU JUMUIYA YA KIISLAM ,,,,BARAKA SHAMTE IKIWA BABA YAKO ALIKUWA NA WADHIFA ENZI HIZO SIO LEO,,UFAHAMU HILO,,,, HUU NI WAKATI WA UKWELI NA UWAZI,,, NAIOMBA SERIKALI YA CCM IMFUNGULIE GLUB YA NETBOLL BARAKA SHAMTE HAFAI KUSIMAMA JUKWAANI,,,UZOWEFU WAKE NI KUCHEZA NA WATOTO WA KIKE,,,, SIO KUWA MSEMAJI WA CHAMA,,,, BORAFYA KAMA UNA UWEZO WA KUWAFUKUZA WAWAKILISHI ,,, YANINI UPIGE KELELE VILINGENI,,, WAFUKUZE MARA MOJA KWA UWEZO WAKO,,,, HUMSHITUWI MTU HIZO NI HALBADIR ZA MBAYANA,,, KILA MTU ANAFAHAMU NINI KILICHOMO ZANZIBAR,, LABDA WALE WAPUMBAVU KAMA NYINYI NDOO WATAOKUSIKILIZA,,, LAKINI KWA MZANZIBAR HUMDANGANYI TENA,,,, ILIPOFIKIA PANATOSHA,, TUACHIWE TUPUMUE,, ZANZIBAR KWANZA,,, POROJO BAADAYE,, NILIDHANI UTASEMA BABA YAKO NDOO MUNGU WA DUNIA,,, KUMBE ALIKUWA ENZI HIZO WAZIRI MKUU,,, JEE UNGEKUWA NA NAFASI YA MHESHIMIA ABEID AMAN KARUME,,,, AMBAYE BABAYAKE ALIKUWA RAIS NA YEYE PIA AMEKAMATA URAIS,, LAKINI HAKUTHUBUTU KUJIGAMBA HATA SIKU MOJA,,, AU KUWASALITI WAZANZIBAR,,,

  KWA REHEMA ZA MUNGU NA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NAMUOMBA MOLA AWAHUKUMU HADHARANI ADHABU MUNAYO STAHIKI ,, MAFISADI WA ARDHI NA MAHASIDI WA UMMAT MUHAMAD,,,HASBI ALLAH MINA NEEMAL WAKIL,,,,,

 5. Acheni kuongea pumba nendeni shule nyie wakereketwa hamjaenda shule siku ya uhuru wa znz haitabadilika asilan mapinduzi yanaweza kutokea mengine lkn kwanini ukweli hamuusemi acheni uselfish nyerere alisema nimechoka na uzanzibari na uislam wao someni this Zanzibar the Island metropolis eastern Africa mujue nini haki hata ikifichwa itaibuka 2 sasa TUACHIWE TUPUMUEEE NENO MUUNGANO NI KERO

 6. Nyie ni vipofu nyie au mushapewa donge. Mutabaki ivo ivo. Zanzibar itabaki kama Zanzibar yenye mamlaka kamali. Sisi hatukubali kuona rais wetu ni kama waziri tu kwa watanganyika. Sisi tunawambie Zanzibar huru inawezekana. NA KARIBU TUTAFIKA. KATU ZANZIBAR HATAGEUZWA MKOA.

 7. “Hawa watu wanaotaka Muungano uvunjike waulizeni wameunda wao, Muungano bwana ni wetu sisi tangu zamani Afro Shiraz Party tulikuwa na imani yetu na ahadi za mwanachama ambazo ni pamoja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ”

  Hizo ndio hoja za bwana borafia, nadhani amesahau kuwa wengi wetu tunafahamu kama muungano ni wa kisiasa.Muungano umejikita zaidi na maslahi ya kisiasa na ung’ang’anizi wa madaraka.Ni kwa hoja na khofu hii ya kupoteza madaraka visiwani Zanzibar, ndio iliotumika kumvua madaraka raisi wetu ilipoingia siasa ya vyama vingi.

  Sidhani babu borafia kama anaelezea jipya, ni yayo kwa hayo .Shule kitu muhimu, namshauri babu borafia akajiunga na elimu ya watu wazima kupata elimu angalau ya kujenga mbele ya umma.

  Nadhani punde nimetoka kusoma habari Bi.Fatma Karume anaunga mkono hoja ya uamsho.Anakiri kuwa kama Mzee Karume angekuwa hai, basi muungano ungekuwa na mashakani na kero zake zilizojaa.Sidhani kama unamtisha mtu kusema utamnyanganya kadi ya uanachama….Ni kama vile kujichimbia kaburi kwa kufyeka wanachama!

 8. Ha hii sasa balaa hawa CCM wengine walipita Shule gani?
  Laiti ungejuwa wewe Borafya na wenzako mngerejesha kadi nyny kwanza kabla ya hao baadhi ya Waakilishi.
  Hebu hangaikeni kidogo muisome historia na asili ya neno CCM na lengo la kuja kwake Tanzania mbona mumelala nyny. Kama kweli hasa sisi tunatarajia PEPO ya ALLAH bac katu tucngeshabikia neno CCM. Ni faraja iliyoje kama kweli munaweza kuwanyanganya kadi bac muwanyanganye mapema kabla ya RAMADHAN ili wawe ni wenye kurejea kwa ALLAH. Kamwe hajutii atakae tolewa kwny CCM.
  Unakataa harakati za UKOMBOZI huku unakumbatia chama zimo lakini au zimeliwa na mwezi?
  Mtu mzima hatishiwi nyau hapa mpaka kieleweke. Muasisi wa MUUNGANO ni KARUME lakini leo mwanawe huyo muasisi HAUWEBU tena MUUNGANO. Neno mwanawe lipigie mstari utakuwa wewe Borafya. Mke wa muasisi wa MUUNGANO ambaye inawezelana kwa namna moja ama nyengine baada ya kuhadithiwa na mumewe kuhusu kuungana alikubali bila pingamizi lakin leo na yeye kaiona dhulma nae kamwe HAUWEBU itakuwa wewe BORAFYA. Nenda huko utafute mavi ya KUKU ubanje.

 9. Mgeni mwenyewe rasmi ni Borafya na Baraka Shamte wote 2 hawana radhi sasa sijui tuwaelewe vipi huyo Borafya endezake akauze gongo na Shamte aende akaomba markiti

 10. Kula inaweza kuktoa roho ndio Hali iliypwafika hao wajiitao vijana huyo baba Lao alisema ukweli ukidhohiri uwongo hujitenga

 11. Haya ndugu zangu si mageni katika midani za siasa za Zanzibar !! Wakati Zanzibar kulipokuwa kukidaiwa uhuru 1960 kulikuwepo watu wa aina hii hii ambao walikuwa wakipiga mayowe kuukataa uhuru kwa kusema uhuru zuwia!! sasa vijana msistaajabu kwa hali hii, tumeshayazowea!!

 12. Hii inashangza. Mwenyekiti wa CCm Taifa ameunda TUME ya kuratibu maoni ya Katiba ya Tanzania. TUME hii katika mambo inaytaka watu wayazungumze ni kutafuta namna bora ya kuimarisha Muungano, implying kwamba Set up ya sasa inakasoro. Umoja wa Vijana wa CCM wanataka Muungano huu uendelee. Yupi yu sahihi mwenyekiti au Umoja wa Vijana? Hapo nyuma watu maarufu kama akina Generali Ulimwengu walisema ni busara ” ingefanywa kura ya maoni juu ya Muungano na baadae ifate uandikaji wa Katiba.” Hawa walipuuzwa ! TUME ya KATIBA ikaundwa ! TUME imekuja na sasa tunashuhudia kura ya katika Mikutano ya TUME hii. Wengi wa wanasema husema kuwa (a) Muungano huu uendelee (b) Tunataka Zanzibar huru. Inafurahisha kuwa Mungu amesaidia kufanya Mapinduzi na sasa kura ya maoni inatokea tena kwa uwazi si ile ya siri ambayo mizengwe inaweza kufanya kubadili matokeo. Ama kweli Mungu “humtawalisha amtakae na kumdhalilisha amtakae na kwamba mikononi mwake ndio kwenye kila kheri.” Ndugu maombi ya waliowengi mara nyingi huungwa Mkono na Mungu. Wale wanataka kuwanyanganya kadi wasemao kuwa Muunano unakasoro basi wangeanza kumyangaya kadi Mwenyekiti wao wa Taifa kwa kuwa yeye ndie aliunda TUME na kuruhusu watu wajadili Muungano haliinayoashiria kukiri kuwa Muunano huu unakasoro!

 13. SADAKTA AKILIMANDE. HUU NI UTOVU WA NIDHAMU MKUBWA WA UVCCM NA HUYO BABU YAO BORAFYA. KWA NJIA YA MZUNGUKO (INDIRECTLY) HAWAKUBALIANI NA MWENYEKITI WAO AMBAE ANAONA KASORO ZA MUUNGANO AMBAZO ZINAHITAJI KUREKEBISHWA. AMETOA FURSA KWA WANANCHI KUTOA MAONI YAO KAMA WANANCHI NA SIO VYAMA VYA SIASA. IWEJE LEO HAWA VITIMBAKWIRI UVCCM WAANZE KUWATISHA WAWAKILISHI AMBAO WANA HAKI KAMA RAIA KUTOA MAONI YAO JUU YA MUUNGANO? KWELI PUMBAVU LIKIPUMBAA ……………….. INAONEKANA UVCCM ZANZIBAR HAWAJUI HATA NINI KINACHOENDELEA KATIKAA SIASA ZA TANZANIA. WAO WAMO TU KUTUKANA. SISI YETU YANAYEYAAAAA. ZANZIBAR HURU INAWEZEKANA. TUACHENI TUPUMUEEEEEEEEEEEEEEEEE.

 14. Waumini sote tunaamini kwamba Mungu hasemi uongo.Na watu kama hawa borafya Mungu kawataja kwenye quran kama wana macho hawaoni wana masikio hawasikii wana mdomo hawasemi, mm najiuliza hv hao waliohudhuria wakishangilia wanazo akili au ndio bendera boss wao upepo uvumako ndiko waelekeako kama hivo sivo bas wangemuuliza huyo boratumbo (borafya) kitu gani kilichomfanya makamo wa kwanza wa CCM zanz kulazimishwa ajiuzulu urais wa znz na huyo baba yao wataifa kule dodoma? Kusoma muhimu jamani. ZANZIBAR HURU INAWEZEKANA (INSHA ALLAH)

 15. Maneo haya hapa chini yawe zawadi ya Wanasiasa wa Unguja na hasa wale wanaohubiri utenganisho wa dini na siasa. Pia awaendee watakao naasi za kisiasa na huku wakikosa sifa kama alizozitaja Plato hapo chini. Sisi inatuuuma sana kusikia mtu anadai nafasi ya kisiasa huku akikosa sifa hata za kuongoza nyumba yake.

  The City-State
  A Brief Summary of Plato’s Ideal State

  The good life is possible only in and through society (State). Society is a natural institution. Man is essentially a social and political animal. The State exists for the sake of the good life. Now according to Plato, the aim of the good society is neither freedom, nor economic well-being. Rather, the aim of the good society is justice. A true State, therefore, must be conformed to justice (the Ideal of which exists in the World of Forms). And so the state does not decide what is just. Justice is an object of knowledge, that is, it is one of the forms. That is why the Statesman must be a Philosopher. If not, he will only lead the state downwards toward self-destruction. Justice in the state is analogous to justice in the individual, and the state must be structures after the pattern of justice in the individual. Now the soul has three parts, according to Plato:

 16. Shule hii ni kwa ajili wanaodhani kuwa watu hawategemeani.
  Why We Form a Society
  Imagining their likely origins in the prehistorical past, Plato argued that societies are invariably formed for a particular purpose. Individual human beings are not self-sufficient; no one working alone can acquire all of the genuine necessities of life. In order to resolve this difficulty, we gather together into communities for the mutual achievement of our common goals. This succeeds because we can work more efficiently if each of us specializes in the practice of a specific craft: I make all of the shoes; you grow all of the vegetables; she does all of the carpentry; etc. Thus, Plato held that separation of functions and specialization of labor are the keys to the establishment of a worthwhile society.
  The result of this original impulse is a society composed of many individuals, organized into distinct classes (clothiers, farmers, builders, etc.) according to the value of their role in providing some component part of the common

 17. Biidhnillah Taala tunamuomba Allah kwa nguvu zake na rehma zake na uwezo wake inshaa Allah… inshaa Allah… yaa Rabbana uwashinde na uwaadhibu hapa hapa duniani kabla ya siku kiama wale wote wanaokwenda kinyume na kuikandamiza dini ya kiislam inshaa Allah ya rabbana wape maradhi yasotibika kama ulompa sharon (laanatullahi alayhi) na wakilala vitandani wawe wanayanadi na kuyakariri yale machafu yao…!! Aaaamin.

 18. Borafya & Baraka

  Mnaweza kumnyang’anya naniii?

  Mansour,Raza, Hamza, Asha Bakar,Mama Fatma Karume, Mama Shadia au Mshimba?

  Fanyeni tucheke.

  Huu ni Mkurupuko Camp, Mtaweza vipi wakati mwenyekiti wa CCM Zanzibar kaufananisha Muungano na madawa ya kulevya ndani ya ndege? Mnafikiri atakuacheni sio? Tutamsaidia mpaka mtahama visiwa hivi.
  TUACHIWE TUPUMUEEEE!

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  SERELLY.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s