Suluhu haijapatikana kuhusu sensa

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makaazi Zanzibar Mwalim Haji Ameir akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ali mwinyikai hayupo pichani katika mafunzo ya Wanahabari kuhusiana na Sensa ya watu na Makaazi ambayo itafanyika Jumamosi ya Tarehe 25Agosti kuamkia Tarehe 26 Agosti 2012.

SERIKALI bado inaendelea kufanya juhudi za kuwashawishi viongozi wa dini na makundi mengine yaliotishia kususia zoezi la sensa ili kufikia muafaka kabla ya zoezi hilo kufanyika Agosti 26. Hayo yamebainika wakati wa mafunzo ya siku tatu ya sensa kwa waandishi wa habari waandamizi na wahariri waliopo Zanzibar ambapo walipata muelekeo wa sensa hiyo.

Wawezeshaji kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu Zanzibar waliwaambia waandishi wa habari kuwa makundi hasa ya kidini ikiwemo Uamsho hawajapuuzwa na viongozi wa serikali pamoja na ofisi ya mtakwimu wamekuwa wakifanya juhudi za mara kwa mara kufanya mazungumzo.

“Sensa ni muhimu na tunataka kila mtu ahesabiwe kwa hivyo viongozi wetu wanaendelea na kuwashawishi viongozi wa dini wanaosusia wasifanye hivyo” alisema Mayasa Mahfoudh ambaye ni afisa mwandamizi wa katika ofisi hiyo ya mtakwimu.

Mtakwimu mkuu wa serikali Mohammed Hafidh alisema waandishi wa habari wana nafasi na mchango mkubwa wa kuhakikisha kwamba sense ya mwaka huu inafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Tuna changamoto katika kufikia siku ya sensa yenyewe lakini kwa kushirikiana na wananchi viongozi katika ngazi zote pamoja na waandishi wa habari tunaweza kufikia malengo na kumfanya kila mtu ashiriki” alisema katika hoteli ya Chavda iliyopo Mji Mkongwe.

Aidha Hafidh aliwaambia waandishi kwamba maandalizi kwa upande wa Zanzibar yamefikia katika kiwango cha kuridhisha ikiwemo ramani na kuainisha vituo 3,074 vya kuhesabiwa watu.

Alisema changamoto kubwa ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanakuwa na elimu na muamko juu ya umuhimu wa sensa nchini.

Washiriki wa mafunzo hayo kutoka vyombo vya habari mbali mbali walionesha wasiwasi wao juu ya tamko la viongozi wa dini kutoka bara na Zanzibar likiwakataza wafuasi wa dini wasusie zoezi hilo.

Walisema tamko hilo linaweza kuleta athari kubwa katika zoezi hilo iwapo viongzi wa serikali watalipuuza na kushauri umuhimu wa pande mbili hizo kukutana na kukubaliana kwa pamoja ili lengo la sensa litimie.

Afisa habari wa sensa Zanzibar, Salama Njani alitoa wito kwa vyomb vya habari kutenga muda na nafasi ya kutoa elimu kwa wananchi licha ya kuwepo upungufu wa fedha za kulipia matangazo katika vyombo hivyo.

Alisema ni wajibu kwa waandishi wa habari kujitolea zaidi kusaidia taifa kwa sababu sensa inalenga katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

 

Advertisements

2 responses to “Suluhu haijapatikana kuhusu sensa

  1. asalam alykum sensa hii ya TANZANIA ni jambo ambalo kisheria halikubaliki nani DHULMA kwa WAISLAM kwa sababu ya kukosa moja ya kipengele muhimu cha kuingizwa nacho ni kpengele cha UDINI kwa hivyo sissi kama waislam wa TANZANIA hatuitambui na tutaendelea kuwashajihsha wengine juu ya kulijua hili kwa 7bu ni kipengele muhimu ambacho nchi mbali2 kuu za ulimwenguni huingiza iweje wao TANZANIA wasiingize huku TBC karibun walitangaza kama idadi ya WAISLAM ni chache TANZANIA sasa hizo takwimu wamepata wapi? HATUTOSHIRKI SENSA MPAKA kipengele cha dini kiingizwe………

  2. Sensa ya Tanzania haitakuwa na muitikio mkubwa kwa vile serikalli ya SMZ & SMT zinatwaliwa na kiburi, kwanini waislamunsiku zote wawe watu wa kupuuzwa tu? Hapa Wislamu tuwe makini maana hawa viongozi wetu ni wababishaji.

    Kuingiza kipengele cha “dini” katika dodoso la sensa sio Udini kama baadhi ya watu wanavyopotosha. Lazima kuwepo na taarifa sahihi kuhusu dini za watu.

    Kwa upande wa Zanzibar hakuna haja ya kuhesaiana katika pakacha moja kama machungwa. Ni vizuri kama tutalimaliza hili la Muungano baadae hayo mengine yatafuata. Hapa sasa wanatwambia tuko milioni moja, wakifanya sensa yao watasema mara hii tumefikia milioni moja ili baadae taarifa hizo zitumike kisiasa.

    hakuna sensa kwa kuwapuuza Waislamu na kuwapa nafasi maaskofu, kama SMZ & SMT hamajataka kusikiliza madai ya Waislamau wahesabuni hao mliokubaliana nao (Wakristo pekee)….

    Na sisi Wazanzibar hatutaki kuhesabiwa mpaka tupate nchi yetu……

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s