Benki ya wanawake kuanzishwa Zanzibar

Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto, Zainab Omar Mohammed akielezea malengo na maendeleo ya Wizara yake kwa Waandishi wa habari huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni  Zanzibar

SERIKALI ya Zanzibar inakusudia kuanzisha benki ya wanawake itakayolenga kuwainua kiuchumi wanawake wa zanzibari lakini baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wamesema mpango huo umechelewa mno kuanza. Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF) Mtumwa Kheri Mbarak na Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma waliibana serikali kuwa mpango wa kuanzisha benki umechelewa kwa muda mrefu bila ya sababu za msingi.

Waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema kuanzisha benki haihitaji kwenda kwa haraka kutokana na utaratibu wa kibenki na mtaji unaotakiwa.

“Mheshimiwa Spika serikali ina azima ya dhati ya kuanzisha benki ya wanawake lakini ili kuanzisha benki kwa mujibu wa taratibu kunahitaji mtaji wa bilioni 15 na maandalizi mengine ambayo hivi sasa hivi tunaendelea nayo naomba wajumbe wawe na subra” alisema.

Alisema taratibu zimeshaanza ikiwemo ushauri kutoka benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na washauri wengine ambao watatoa maelekezo bora ya kuanzishwa kwa benki hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wanawake na hata wanaume.

Kauli ya waziri ilikuwa ni katika kujibu hoja za wawakilishi waliotaka ufafanuzi juu ya mtaji wa kuanzisha benki ambapo baadhi yao walionesha wasiwasi juu ya ukubwa wa mtaji huo wa bilioni 15 wakati zanzibar ina wakaazi wasiozidi milioni 1.5.

Mzee alisema kiutaratibu benki inapoanzishwa nchini Tanzania inakuwa ni ya watu wote na kwamba ndio benki kuu ya Tanzania ikaweka mtaji huo lakini unafuu unapatikana wakati kikundi au mtu inapotaka kufungua benki ya jamii.

“Huo ndio utaratibu benki ya jamii mtaji wake ni shilingi milioni 500 ambapo inaweza baadae ikakuwa ikageuka kuwa ni benki kubwa yenye uwezo wa kutoa mikopo mikubwa” alisema waziri huyo.

Hata hivyo maelezo hayo hayakuonekana kuwaridhisha wajumbe ambao walishauri waziri wa fedha kushauriana na wataalamu wake pamoja na benki kuu ya Tanzania (BoT) ili kuweza kuwaharakisha kuanzisha benki ya wanawake kwa mtaji mdogo usiofikia bilioni 15.
Ahadi ya kuazisha benki ya wanawake Zanzibar ilitolewa kwa mara ya kwanza na Dk Ali Mohammed Shein wakati akiomba ridhaa ya wananchi ya kuingia madarakani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Bajeti ya wanawake yapita

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wamepitisha bajeti ya billioni 2.4 ya wizara ya ustawi wa jamii, maendeleo ya vijana, wanawake na watoto huku baadhi ya wajumbe wakilalamikia kiwango hicho kuwa ni kidogo kwa wizara hiyo.

Kama ilivyokuwa katika wizara zilizotangulia wajumbe wa baraza la wawakilishi pia walihoji uhalali wa serikali kutenga fedha nyingi kwa ajili ya mikutano na semina na safari wakati kuna mambo muhimu ya kuwahudumia wananchi.

Miongoni mwa wawakilishi waliochangia suala hilo ni pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu, Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman, Mwakilishi wa wanawake Salma Bilal (CCM) na Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura (CCM) Hamza Hassan Juma.

Wote kwa pamoja walisema kuwa kutenga bilioni 2.4 kwa wizara yenye majukumu mengi ni kudhoofisha maendeleo ya wizara hiyo na kuzorotesha malengo yalipangwa na wizara.

“Mheshimiwa Spika fedha ambazo zinatengewa wizara hii kila mwaka ni kidogo sana ni sababu zipio za kufanya hivyo wakati katika mipango ya serikali ni kuendeleza vijana na wanawake?” alihoji Rashid Seif.

Salma alisema tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi pamoja na wizara kushindwa kuanzisha miradi mingi ya kuwasaidia akina mama wanawake inatokana na bajeti ndogo lakini serikali kila mwaka inapokumbushwa marekebisho huwa hayafanyiki.

Wawakilishi Hamza na Jussa kwa upande wao walisema fedha nyingi ambazo hutengwa na serikali ni kwa safari na semina jambo ambalo zingeweza kufaa katika mipango ya huduma za wananchi ikiwa pamoja na maendeleo ya akina mama, wazee na vijana.

Akifanya majumuisho ya mijadala ya wajumbe kabla ya bajeti hiyo kupitishwa waziri wa wizara hiyo Zainab Omar Mohammed alisema kwamba wizara yake imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuwaendeleza wazee vijana na wanawake ikiwemo suala la kupiga vita udhalilishaji.

Waziri alisema wizara yake ingeweza kufanya mengi lakini kwa ufinyu wa bajeti haiwezi kutekeleza majukumu yote ambayo yanapendekezwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi.

“Suala la ajira ni suala pana sana japo kuna wizara maalumu ya ajira lakini wizara yangu imekuwa ikitoa msaada na ushauri kwa vikundi kwa vijana na wanawake ili kujiendeleza ikiwemo suala la kilimo cha mbogamboga” alisema waziri huyo.

Aidha waziri huyo aliwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kuungana katika suala la malezi ili kuepusha vijana kutojiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Akitoa ufafanuzi wa ziada waziri wa nchi ofisi ya makamo wa kwanza wa rais, Fatma Abdulhabib Fereji alisema vita dhidi ya madawa ya kulevya sio jukumu la serikali pekee bali ni la jamii nzima.

Alisema baadhi ya wazazi wanafikiria kuwa jukumu la ulezi ni la walimu na serikali pekee wakati msingi wa malezi huanzia nyumbani kwa wazazi wake.

Advertisements

4 responses to “Benki ya wanawake kuanzishwa Zanzibar

 1. HIYO BENKI MOJA TU YA PBZ WAKOLONI WAMEIKALIA KIFUANI IFE ILI BENKI ZAO ZA CRDB, NMB, NBC, BANK M NA NYENGINEZO ZIPATE KUTAMBA HAPA ZANZIBAR. NNA HAKIKA BENKI HIYO ITAKUFA CHINI YA MIAKA MITANO. KUNA HAJA YA KUANGALIA MAMBO YA MSINGI KATIKA HILI KWA KUANZISHA BENKI AMBAYO ITATOA MIKOPO KWA WANAOTAKA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA NA MIRADI MIKUBWA AMBAYO ITATOA AJIRA KWA WENGI. BENKI HIZI ZA AKINA MAMA ZITAKUA HAZINA TOFAUTI NA MIFUKO YA AMANI NA KIKWETE AMBAYO ILIKUA ZAIDI NA LENGO LA KUJIIMARISHA KISIASA CCM NA MATOKEO YAKE WAKEREKETWA NDIO WALIOPEWA MIKOPO WAKAACHWA WAJASIRIA MALI KWA SABABU ZA SIASA. HEBU TUAMBIENI NI WANGAPI WALIONUFAIKA NA MIFUKO HIYO NA WANAENDELEZAJE HIYO MIKOPO? HII BENKI NI UBABAISHAJI MTUPU.

 2. Sasa hamjabainisha itakuwa inafuata Islamic Banking System au mnataka kuwaendelezea u-secular Mama zetu katika kipindi hiki ambapo Islamic Banking Injuctions zimeanza kutekelezwa Worldwide?.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 3. Daangu Bi Zainab Serikali haianzishi Bank. Bank ni biashara, Serikali ikianzisha Bank itakufa kama zilivyokufa taasisi nyengine. Ni kwanini Nynyi waheshimiwa wanawake hamuanzishi taasisi yenu kisha mkauza hiza kwa watu na taasisi nyengine na baadae watu wengine watakao bila kujali gender wakaingia kwa mfumo wa hisa na baadae SMZ ikangiza hisa zake na huku uendeshaji ukibaki chini yenu. Njia nyengine ni kwa PBZ kuuza hisa zake kwa watu mkiwemo nyinyi wanawake waheshimiwa. Hii itaongeza nguvu za PBZ na pia kuwapa fursa wanawake wenye hisa kukopa na kujiendeleza. Dadangu inabidi tufahamu kuwa mkopo wa Bank haufanyiwi biashara ya maandazi. Kama hili ndio lengo la kuanzisha Bank ya Wanawake basi bora Mungu asiwapeleke huko!

 4. Ee nyie hamuoni munajidanganya. Kwanza vunjeni muungano ndio muanzishe hiyo benki ya wanawake. Hamuna mamlaka kwa sasa kufanya hivyo. Hebu tazameni hii PBZ HAINA UHURU KAMILI INAONGOZWA NA BOT. PBZ HAINA UWEZO WA KUDHIBITI FEDHA KWA KIWANGO KIKUBWA IMEWEKEWA MIPAKA NA BOT. JEE HII BENKI MUTAKAYOANZISHA ITAKUFA TU. ZANZIBAR HURU KWANZA. VUNJENI MUUNGANO MUSIULINDE TUACHENI TUPUMEe nyie hamuoni munajidanganya. Kwanza vunjeni muungano ndio muanzishe hiyo benki ya wanawake. Hamuna mamlaka kwa sasa kufanya hivyo. Hebu tazameni hii PBZ HAINA UHURU KAMILI INAONGOZWA NA BOT. PBZ HAINA UWEZO WA KUDHIBITI FEDHA KWA KIWANGO KIKUBWA IMEWEKEWA MIPAKA NA BOT. JEE HII BENKI MUTAKAYOANZISHA ITAKUFA TU. ZANZIBAR HURU KWANZA. VUNJENI MUUNGANO MUSIULINDE TUACHENI TUPUMEe nyie hamuoni munajidanganya. Kwanza vunjeni muungano ndio muanzishe hiyo benki ya wanawake. Hamuna mamlaka kwa sasa kufanya hivyo. Hebu tazameni hii PBZ HAINA UHURU KAMILI INAONGOZWA NA BOT. PBZ HAINA UWEZO WA KUDHIBITI FEDHA KWA KIWANGO KIKUBWA IMEWEKEWA MIPAKA NA BOT. JEE HII BENKI MUTAKAYOANZISHA ITAKUFA TU. ZANZIBAR HURU KWANZA. VUNJENI MUUNGANO MUSIULINDE TUACHENI TUPUMEe nyie hamuoni munajidanganya. Kwanza vunjeni muungano ndio muanzishe hiyo benki ya wanawake. Hamuna mamlaka kwa sasa kufanya hivyo. Hebu tazameni hii PBZ HAINA UHURU KAMILI INAONGOZWA NA BOT. PBZ HAINA UWEZO WA KUDHIBITI FEDHA KWA KIWANGO KIKUBWA IMEWEKEWA MIPAKA NA BOT. JEE HII BENKI MUTAKAYOANZISHA ITAKUFA TU. ZANZIBAR HURU KWANZA. VUNJENI MUUNGANO MUSIULINDE TUACHENI TUPUMUWE.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s