Zanzibar haina uwezo wa kuwa na sarafu yake

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Fatma Abdulhabib Fereji akibadilishana maweazo na Dk Bakari S, Asseid nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa haiwezi kuanzisha sarafu yake (fedha zake) kutokana na kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hairuhusu kufanya hivyo. Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee wakati kijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyetaka kujua sababu za Zanzibar kutokuwa na sarafu yake ili kuimarisha uchumi wake.

Jussa alisema sarafu ya Tanzania inaendelea kushuka thamani dhidi ya fedha za kigeni (dola) siku hadi siku na kufanya Zanzibar kuwa katika hali ngumi kiuchumi ikiwemo wananchi wake kukabiliana na mfumko wa bei na kupelekea maisha kuwa magumu.

Akijibu suali hiyo Mzee alisema kimsingi Zanzibar ina uwezo wa kiuchumi wa kuanzisha sarafu lakini katiba iliyopo hivi sasa sarafu ni suala la muungano na hivyo haitoi fursa kuanzisha sarafu yake.

“Sio kweli kwamba sarafu ya Tanzania inaendelea kushuka thamani siku hadi siku lakini ni kweli kwamba thamani ya shilingi yetu (Tanzania) ikilinganishwa na ile ya dola za kimarekani imekuwa na muelekeo wa kushuka” alisema waziri.

Akitaja sababu nyengine za kushindwa kuwa na sarafu Zanzibar, Mzee alisema hivi sasa nchi za Afrika Mashariki zimo katika mchakato (Process) za kuelekea katika kuwa na muungano wa fedha ambao utakapokamilika nchi zote katika jumuiya hiyo zitakuwa na sarafu moja tu.

“Mheshimiwa Spika kufuatia upepo huo unaovuma kuelekea katika sarafu moja haitayumkinika kwa Zanzibar kujitenga kwa kuanzisha, kuhudumia na kusimamia sarafu yake hata kama ina uwezo wa kiuchumi kufanya hilo” aliwaambai wajumbe hao.

Akielezea zaidi kuhusiana na sababu za kushuka thamani ya fedha ya Tanzania alisema ni kutokana na urari wa malipo ya nchi za nje, tofauti ya mfumko wa bei na nchi zinazofanya biashara na Tanzania na kuchafuka kwa masoko duniani.

Pia alitaja kuwepo kwa mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu kutokana na kuchelewa kwa fedha za wahisani na mikopo, na hisia za upungufu wa fedha za kigeni kuwa ni miongoni mwa sababu za kushuka thamani ya fedha za Tanzania.

Serikali kuwatunza wazee

SERIKALI ya Zanzibar imeanza kuwahakikisha kuwa wazee wanaotunzwa katika nyumba za serikali watapata milo mitatu kwa siku katika juhudi za kuwajali na kuimarisha afya zao.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa ustawi wa jamii, maendeleo ya vijana, wanawake na watoto Zainab Omar Mohammed wakati akiwasilisha hutuba ya makadirio ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013 katika baraza la wawakilishi linaloendelea.

“Kufatana na agizo la rais wizara imeamua kuhakikisha kwamba wazee wanatunza vizuri zaidi ikiwemo kupata milo mitatu badala ya miwili kwa siku pamoja na posho zao kuongezwa” alisema waziri huyo wakati akiwaomba wajumbe waidhibishe bilioni 2.4 kwa ajili ya kazi za maendeleo na kazi za kawaida za wizara yake.

Alisema katika hutuba yake kuwa wizara imeendelea kutoa matunzo na huduma kwa wazee wanaoishi katika nyumba za wazee Unguja na Pemba.

Zainab aliwaaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa jumla ya wazee 108 wakiwemo wanawake 50 watapatiwa huduma katika makaazi yao.

“Wizara imeongeza posho la wazee wanaoishi katika nyumba hizo kutoka shilingi 25,000 hadi kufikia 40,000 kwa mwezi katika nyumba za wazee za Sebleni, Limbani, na Gombani pemba” alisema waziri huyo.

Aidha alisema wazee wanaoishi katika nyumba ya Welezo posho zao zimeongezwa kutoka shilingi 7,000 hadi kufikia 15,000 na kwamba wazee wote hununuliwa nguo mpya kwa ajili ya skukuu ya Eid el Fitri.

Waziri wa wizara hiyo aliahidi kuwa wizara yake iliendelea kuwapatia posho wazee 62 ambao ni waathirika wa ugonjwa ukoma waliopo katika kijiji cha Makundeni Pemba kwa kuwapatia shilingi 25,000 kwa mwezi kwa kila mmoja.

Waziri pia alisema wizara yake imeanza kazi kubwa ya kukarabati ukumbi wa nyumba za wazee Sebleni Unguja na kutarajia kufanya ukarabati wa jiko hapo baadae wakati nyumba za wazee kisiwani Pemba katika maeneo ya Limbani na Gombani zinafanyiwa matengenenzo madogo madogo.

Wakati huo huo Zainab alisema wizara yake katika kitendo cha ustawi wa jamii imeendelea kulipa fidia kwa wafanyakazi waliopatwa na ajali wakiwa kazini na kwamba hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu jumla ya shilingi 12.7 milioni zimetumika kuwalipa wafanyakazi 19 Unguja na Pemba.

Katika hutuba hiyo alisema wizara yake ilizika jumla ya maiti 20 zisizokuwa na wanyewe Unguja na Pemba baada ya juhudi za kutafuta familia zao kushindikana.

MISAMAHA YA KODI

TAASISI na mashirika mbali mbali ya Zanzibar yamefaidika na misamaha ya kodi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 18
ndani ya miaka miwili iliyopita.

Waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo Omar Yussuf Mzee alitaja baadhi ya taasisi zilizofaidika ni taasisi za kidini, mashirika ya umma na wawekezaji.

Akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyeka kujua mamlaka ya kisheria iliyopewa kusamehe kodi pamoja na kiwango cha kodi kilichosamehewa kwa mwaka uliopita, waziri alisema mashirika mengi yamenufaika.

Alisema mwaka wa fedha ulioanzia Julai 2010 hadi Juni mwaka 2011 jumla ya billioni 18.3 zilisamehewa wakati mwaka huu ulioanzia Julai 2011 hadi Aprili mwaka huu billioni 15.7.

waziri aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba sekta ya uwekezaji ndio inayoongoza kwa kusamehewa kodi na ushuru ikifuatiwa na taasisi za serikali na taasisi za kidini ndizo zinazopata asilimia ndogo ya msamaha.
Waziri Omar alisema wizara yake ndio iliyopewa uwezo wa kutoa msamaha wa kodi na ushuru na kwamba hupokea maombi ya msamaha wa kodi na baadae kuzingatiwa na uamuzi kutolewa.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi, Abdallah Juma Abdallah kutoka Chonga (CUF) na Salmin Awadh Salmin kutoka Magomeni (CCM) walitaka kujua faida inayopatikana kwa serikali baada ya misamaha hiyo ya kodi.

Waziri alijibu kwa jumla kwamba ni katika kukuza uchumi wa nchi hasa katika kuvutia wawekezaji wneye miradi mikubwa na katikab kipindi hicho zaidi ya misamaha 400 imetolewa.

Kilimo cha mwani

WAKULIMA wa mwani wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji miti ambayo wanatumia katika ukaushaji wa mwani huo.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma katika baraza la wawakilishi wakati alipotaka kujua juhudi zinazofanywa na serikali kuwasaidia wakulima wa mwani ili waachane na ukataji miti ovyo.

Aliuliza ni lini serikali itafikiria utaratibu mbadala wa kufunga kamba za wakulima wa mwani wanapotaka kuzikatusha mwani badala ya kutumia vijiti vinavyotokana na ukataji miti.

Akijibu suali hilo waziri wa nchi afisi ya makamo wa kwanza wa rais (Mazingira) Fatma Abdulhabib Fereji alikiri kuwa ukataji wa miti ovyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kusema kwamba katika kilimo cha mwani wakulima hukata miti kwa wingi ili kupata vijiti ambavyo vinatumiwa kufunga kamba za kuweka mbegu au kukuusha mwani.

“Suala la kuwakataza kina mama ambao ndio wengi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani kukata miti kwa ghafla ni vigumu hata hivyo hatua mbali mbali zimekuwa zikichukuliwa na serikali kupitia taasisi zake zikiwemo wizara ya mifugo na uvuvi ili kuwashajiisha kuachana na kukata miti ovyo” alisema waziri.

Katika juhudi za kutafuta mbadala wa matumizi ya vijiti katika kilimo cha mwani, waziri huyo alisema majaribio yamefanyika kwa wakulima wa mwani katika kijiji cha Uzi Ng’ambwa ya kupanga mwani kwa kutumia mawe na mpira.

Waziri alisema majaribio hayo yameonesha mafanikio makubwa na yalitekelezwa na jumuiya ya wakulima wa mwani wa Uzi (Uzi Seaweed Farmers Association – USFA).

Aidha aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kuwa majaribio mengine yamefanyika katika maeneo ya Fundo na Tumbe Kisiwani Pemba ambapo kampuni ya BIRR kwa ufadhili wa mradi wa MACEMP ambako kunalimwa mwani mnene na pia kumeonesha kuwa kilimo hicho kinaweza kufanyika kwa kutumia m mianzi na malighafi nyengine za kuelea.

Waziri Fatma aliwataka wajumbe wa baraza hilo kwa kushirikiana na wananchi kuhifadhi mazingira ili kuepusha Zanzibar katika hatari ya athari zinazotokana na uharibu wa mazingira.

Udhalilishaji wanawake na watoto

LICHA ya juhudi zinazoendelea za kuelimisha jamii juu ya haki za wanawake na watoto nchini udhalilishaji ikiwemo vitendo vya ubakaji bado vinaendelea na kuathiri maendeleo ya wanawake na watoto.

Waziri wa ustawi wa jamii maendeleo ya vijana wanawake na watoto, Zainab Omar Mohammed aliyasema hayo wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.

Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba insikitisha watoto wengi bado wamo katika hatari ya kudhalilishwa na kwamba wizara yake pamoja na vitengo mbali mbali ikiwemo kitengo cha mkono kwa mkono (One Stop Center) inapokea kesi kila siku.

“Mheshimiwa mwenyekiti bado kuna tatizo la udhalilishaji nchini watoto wengi pamoja na wanawake wanadhalilishwa ikiwemo kubakwa, kulawitiwa, kupewa ujauzito na kukashifiwa kimwili” alisema waziri huyo kwa masikitiko.

Katika kipindi cha mwaka uliopita alisema wizara yake imepokea jumla ya malalamiko 215 ya udhalilishaji wa watoto yanayohusu kubakwa, kulawitiwa, na udhalilishaji mwengine wa kimwili.

Pia alisema katika kituo cha mkono kwa mkono jumla ya kesi mbali mbali za udhalilishaji 689 zilipokelewa na kushughulikiwa huku wizara ikipokea malalamiko 393 yanayohusu matunzo na kugombani watoto Unguja na Pemba.

Alisema wizara kupokea malalamiko hayo na kuyafuatilia ili kupata ufumbuzi kwa kushirikiana na walalamikaji na walalamikiwa pamoja na vyombo vya sheria ikiwemo polisi na mahakama.

Zainab alisema kesi nyingi zimekuwa hazisogei mbele kutokana na ukosefu wa ushirikiano na wazazi ambao watoto wao wamebakwa kutojitokeza kutoa ushahidi au kuwa na muhali wa kuwataja watuhimiwa.

“Kwa bahati mbaya wengi wanaofanya vitendo vya udhalilishaji ni wana familia babu, baba, mjomba, kaka, jirani na ndugu wa karibu ambao wote hutumia nafasi ya ukaribu kukwamisha kesi zinazopelekwa polisi na hata mahakamani” alilalamika waziri.

Waziri aliwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi pamoja na jamii ya wazanzibari kwa jumla kushirikiana kuhakikisha kwamba vitendo vya udhalilishaji watoto na wanawake vinakomeshwa ili kuiweka jamii katika maadili mema.

UTENGENEZAJI WA BARABARA

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wameitaka serikali kuharakisha ujenzi wa barabara wa Mbuyu Tende Mkoa wa Kaskazini Unguja ambao upo katika hali mbaya ya kusababisha usumbufu mkubwa wa usafiri kwa wananchi.

Mwakilishi wa Jimbo la Mtemwe (CCM) Abdi Mosi Kombo na Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF) Kazija Khamis Kona walilalimika kwamba barabara ya Kijini – Mbuyu Tende inahitaji matengenezo ya haraka.

Akijibu suali hilo Naibu Waziri wa wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano, Issa Haji Ussi alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 48.7 ni miongoni mwa barabara zitakazofanyiwa upembuzi yakinifu na sadifu (Feasibility Study) ambayo itakuwa katika kiwango cha lami.
“Mheshimiwa Spika napenda kuliarifu baraza lako kwamba hatua ya mwanzo ya kutafuta kampuni za wahadhisi washauri imekamilika na kuwasilishwa kwa mfadhili wa mradi ADB ambaye amekubali kuendelea na hatua ya pili ya kumtafuta mhandisi mshauri” alisema Ussi.

Akivitaja vijiji vitakavyonufaika na baada ya ujenzi wa barabara hiyo kuwa ni Matembe- Muyuni (kilomita 6.5) Njia nne -Umbuji – Uroa (kilimita 11), Mkwajuni -Kijini (kilimita 5.5), Kichwele – Pangani (kilimita 4), Fuoni Kombeni (kilomita 6.7) na Jozani -Ukongoroni -Charawe (kilomita 15).

Naibu waziri alisem ajenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami utaanza mara moja baada ya kupatikana kwa fedha na kuahidi wajumbe kuwa serikali inaendelea na juhudi za kutafuta fedha hizo kutoka kwa wafadhili wa maendeleo.

 

Advertisements

8 responses to “Zanzibar haina uwezo wa kuwa na sarafu yake

 1. Ama kweli “ZANZIBAR NI NCHI” Lakini kiuongozi wa Serikali “ZANZIBAR SIO NCHI”

  Wewe unaacha kupanga maendeleo ya Zanzibar ati kwa kuzingatia katiba ya Muungano wakati Watanganyika wanapotaka kuibana Zanzibar huipuuzilia mbali katiba hiyo na kufanya yao?

  Omar Yussuf Mzee unatukera na unatuvunja moyo bwanaa!. Jamani Wazanzibar tumelaaniwaaa, wogaa, njaa, au nini? Aah sawa. Iko siku.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Napinga huja yako Omar Yussuf Mzee.

  SERELLY.

 2. Jamani kiswahili ni lugha yetu ,kichwa cha habari kinasema ZANZIBAR HAINA UWEZO WA KUWA NA SARAFU YAKE hapo hapo ,zanzibar ina uwezo wa kiuchumi wa kuanzisha sarafu lakini katiba iliyopo hivi sasa sarafu ni suala la muungano na hivyo haitoi fursa ya kuanzisha sarafu yake
  Sawa tunakubali maelezo yaliyoainishwa japo majibu yanapingana lakini ni sawa tu alimradi tumeshafahamu.
  Wawakilishi lazima wakubali kufahamu kwamba katiba si Qur’ani inaweza kubadilishwa ,la umuhimu kuwa na sarafu yetu zanzibar itakuwa na tija katika kuendeleza uchumi wetu?(HASA KWA VILE UCHUMI SI SUALI LA MUUNGANO) ikiwa itakuwa na tija ni kwa nini suali hili lisipewe kipaumbele? na tusibakie na dhana ya kuwa hawakubali hawakubali kwani wasiokubali ni nani ? na kwa nini hawatokubali ?
  kila nchi inaangalia maslahi yake kiuchumi au ndio mmejiweka na kupweteka bila ya kulifanyia kazi? na bila ya kulifanyia kazi tukabakia hawakubali .matokeo yake hawatokubali kwa ukimya wetu ,lakini tukiwakabili na kuliongelea suali la fedha iwe hawatokubali kutakuwa na faida gani ya muungano wakati tunadhoufika kiuchumi.
  Mbona wao ikiwa jambo ambalo hawalikubali au wanalikubali wanalifanyia kazi na kuona matokeo yake kukubalika linalokubalika na kukatalika linalokatalika.
  Hili linafaa lifanyiwe kazi tena kazi ya ziada kama suali la mafuta,vyenginevyo hatufiki pahali tutabakia CCM OYEE,CUF OYEE.

 3. KWA MAPWAGU HAWA TUNAOWACHAGUA HAPO NDIO MWISHO WA UWEZO WAO WA KUFIKIRI. WAMESHABWETEKA KUA KILA KITU MPAKA WARUHUSIWE NA WALIOWAWEKA MADARAKANI TANGANYIKA. SI MUMEMSIKIA SHENI ANAVYOSEMA ATAULINDA MUUNGANO HATA KAMA UTASABABISHA WAZANZIBARI KUWA HAWANA LOLOTE. SARAFU, MAFUTA, UCHUMI, BAHARI NA HATA ARDHI. KWA MANTIKI HIYO, LAZIMA WAZANZIBARI TUKAE CHINI NA KUTAFAKARI KUA VIONGOZI WETU WANAFANYA KAZI KWA MASLAHI YA MUUNGANO NA SIO YA WAZANZIBARI.

 4. mi naona kizungu mkuti maelezo ya huyu musheshimiwa anaehusika na fedha hajijui wala hajitambui

 5. Kauli za viongozi wetu zinanipa wasi wasi kila uchao, mfano ” kimsingi Zanzibar ina uwezo wa kiuchumi wa kuanzisha sarafu…sarafu ni suala la muungano na hivyo haitoi fursa kuanzisha sarafu yake”

  Hii ni kushindwa kujenga hoja kwa baadhi ya viongozi wetu, kwani hata hiyo sheria iliyotumika kupitisha sarafu ya pamoja ya Bunge la Tanganyika 1965, Bunge halikuwa na mamalaka ya kufanya hivyo kisheria na hili wasomi wengi wamelizungumza mfano ukisoma maandishi ya Professa Shivji. Yeye anasema kuwa sheria iliyopitisha uwepo wa sarafu moaja ya Tanzania ni batili kwa kule kukosa sifa ya theluthi mbili za kila upande kwani tujiulize Wabunge kutoka Zanzibar wako wangapi bungeni hata waweze kupinga uwepo wa sheria inyoikandamiza Zanzibar?

  Nionavyo mimi viongozi wa Zanzibar ni dhaifu, wao ili wafanye jambo mpaka likubaliwe na mabwana zao. Nitatoa mfano, tulipotaka kuweka serikali ya SUK/GNU. Baadhi ya viongozi wa Bara walitumia hila kulipinga suala hilo huku wakipata msaada kwa viongozi wa Zanzibar waliozowea kupewa mbeleko kutoka Bara kuitawala Zanzibar kwa kutumia wizi wa kura na mbinu nyengine za kiuharamia.

  Ndio hawa leo ati katiba hairuhusu. Mbona kuna mambo katiba inaruhusu wala hawathubutu kuyagusa. Mfano TRA, suala la mafuta yote hayo walishakaa na kuyatolea maazimio na kufikia maamuzi lakini je wamechukua hatua yoyote? Udhaifu tu na woga.

  Nije katika suala la pili, waziri Mzee kwa kushindwa kujenga hoja ana singizia ati Shirikisho la Afrika ya Mashariki lina mchakato wa kuwa na sarsfu moja. Namnukuu hapa anasema

  “….sasa nchi za Afrika Mashariki zimo katika mchakato (Process) za kuelekea katika kuwa na muungano wa fedha ambao utakapokamilika nchi zote katika jumuiya hiyo zitakuwa na sarafu moja tu”

  Hapa inaonekana kuwa hata hiyo Zanzibar ikiwa huru na kuwa mwanachama kamili (full-memebership) katika vyombo vya kikanda na kimataifa itaburuzwa tu! Hebu waziri Mzee angalia Uingereza ilivyokataa kuisalimisha sarafu yake (paundi), kwa kulinda uchumi wake?

  Nionavyo mimi kama kweli tunaitaka Zanzibar iwe huru tusipigane tu kutaka mabadiliko katika Muungano pekee, lakini pia wakuanza nao ni hawa vibwetere wanaopewa mawizara wakashindwa kuwajibika.

  Mtu anapewa wizara halafu kazi yake kukariri maneno ya mabwana zake tu! Hana jipya, ni sawa na huyu waziri wa muungano haoni hata aibu ati anajidai kuna kero za Muungano wameweza kuzipatia ufumbuzi. Thubutu. Muungano wenyewe ni kero lakini masikini sijui hili halielewi au ni tamaa. Sijui.

  Mimi nasema Wazanzibari wenzangu kazi bado tunayo, kwa kuwapa uongozi watu wasio na sifa ila kutumia ukada wa vyama tu, na kulipa fadhila kazi bado ipo, tena kubwa.

  ZANZIBAR HURU KWANZA. MUUNGANO HATUWEBU.

  AMANI IKISHINDIKANA, TUTATAFUTA MBADALA MWENGINE. KULETA MABADILIKO.

 6. Aslama aleykum kwa uno wangu hapa tusitafute mchawi anaedhofisha uchumi wa Zanziba na maendeleo yake. Mchawi wetu ni MUUNGANO. Mungano ndie mchawi hasidi anaetufisidi. Nashukuru kusikia baadhi ya wawakilishi wameshaliona hilo. Sasa kama mushaliona hilo kwa ni tusiuvunje huu MUUNGANO unaoturudisha nyuma kimaendeleo. Leo tunasema tuna Waziri wa Fedha? au tunawaziri wa fedheha? Ivi ni waziri gani wa fedha aliekuwa hana udhibiti na fedha za nchi yake. Jamani wakati umefika viongozi wa juu sio wakati tena wa kuulinda na kuutetea Muungano. Hebu unganeni na raia zenu ukataeni huwo Muungano. Musilinde na kutetea Mchawi atatumaliza. Fikirieni UHURU WA ZANZIBAR KWANZA NI MUHIMU. Musijali maslahi yenu. Viongozi musikubali kuwa vibaraka wa muungano sisi wananchi hatuutaki Muungano sasa nyie munaogopa nini na mupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Hebu itisheni kura ya maoni muone live ni kiasi gani muungano unavyokataliwa na wananchi Wazanzibar. TUACHENI TUPUMUWE. MUUNGANO HATUUTAKI MUSIULINDE WALA MUSIUTETEE HUU UTAVUNJIKA TU KWA UWEZO WA Aslama aleykum kwa uno wangu hapa tusitafute mchawi anaedhofisha uchumi wa Zanziba na maendeleo yake. Mchawi wetu ni MUUNGANO. Mungano ndie mchawi hasidi anaetufisidi. Nashukuru kusikia baadhi ya wawakilishi wameshaliona hilo. Sasa kama mushaliona hilo kwa ni tusiuvunje huu MUUNGANO unaoturudisha nyuma kimaendeleo. Leo tunasema tuna Waziri wa Fedha? au tunawaziri wa fedheha? Ivi ni waziri gani wa fedha aliekuwa hana udhibiti na fedha za nchi yake. Jamani wakati umefika viongozi wa juu sio wakati tena wa kuulinda na kuutetea Muungano. Hebu unganeni na raia zenu ukataeni huwo Muungano. Musilinde na kutetea Mchawi atatumaliza. Fikirieni UHURU WA ZANZIBAR KWANZA NI MUHIMU. Musijali maslahi yenu. Viongozi musikubali kuwa vibaraka wa muungano sisi wananchi hatuutaki Muungano sasa nyie munaogopa nini na mupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Hebu itisheni kura ya maoni muone live ni kiasi gani muungano unavyokataliwa na wananchi Wazanzibar. TUACHENI TUPUMUWE. MUUNGANO HATUUTAKI MUSIULINDE WALA MUSIUTETEE HUU UTAVUNJIKA TU KWA UWEZO WA Aslama aleykum kwa uno wangu hapa tusitafute mchawi anaedhofisha uchumi wa Zanziba na maendeleo yake. Mchawi wetu ni MUUNGANO. Mungano ndie mchawi hasidi anaetufisidi. Nashukuru kusikia baadhi ya wawakilishi wameshaliona hilo. Sasa kama mushaliona hilo kwa ni tusiuvunje huu MUUNGANO unaoturudisha nyuma kimaendeleo. Leo tunasema tuna Waziri wa Fedha? au tunawaziri wa fedheha? Ivi ni waziri gani wa fedha aliekuwa hana udhibiti na fedha za nchi yake. Jamani wakati umefika viongozi wa juu sio wakati tena wa kuulinda na kuutetea Muungano. Hebu unganeni na raia zenu ukataeni huwo Muungano. Musilinde na kutetea Mchawi atatumaliza. Fikirieni UHURU WA ZANZIBAR KWANZA NI MUHIMU. Musijali maslahi yenu. Viongozi musikubali kuwa vibaraka wa muungano sisi wananchi hatuutaki Muungano sasa nyie munaogopa nini na mupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Hebu itisheni kura ya maoni muone live ni kiasi gani muungano unavyokataliwa na wananchi Wazanzibar. TUACHENI TUPUMUWE. MUUNGANO HATUUTAKI MUSIULINDE WALA MUSIUTETEE HUU UTAVUNJIKA TU KWA UWEZO WA Aslama aleykum kwa uno wangu hapa tusitafute mchawi anaedhofisha uchumi wa Zanziba na maendeleo yake. Mchawi wetu ni MUUNGANO. Mungano ndie mchawi hasidi anaetufisidi. Nashukuru kusikia baadhi ya wawakilishi wameshaliona hilo. Sasa kama mushaliona hilo kwa ni tusiuvunje huu MUUNGANO unaoturudisha nyuma kimaendeleo. Leo tunasema tuna Waziri wa Fedha? au tunawaziri wa fedheha? Ivi ni waziri gani wa fedha aliekuwa hana udhibiti na fedha za nchi yake. Jamani wakati umefika viongozi wa juu sio wakati tena wa kuulinda na kuutetea Muungano. Hebu unganeni na raia zenu ukataeni huwo Muungano. Musilinde na kutetea Mchawi atatumaliza. Fikirieni UHURU WA ZANZIBAR KWANZA NI MUHIMU. Musijali maslahi yenu. Viongozi musikubali kuwa vibaraka wa muungano sisi wananchi hatuutaki Muungano sasa nyie munaogopa nini na mupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. Hebu itisheni kura ya maoni muone live ni kiasi gani muungano unavyokataliwa na wananchi Wazanzibar. TUACHENI TUPUMUWE. MUUNGANO HATUUTAKI MUSIULINDE WALA MUSIUTETEE HUU UTAVUNJIKA TU KWA UWEZO WA ALLAH.

 7. HAPA MCHEZO UMEKWISHA VIONGOZI WETU WAMEISALITI NA KUIUZA NCHI. BADALA YA KUWATUMIKIA WANANCHI WANATUMIKIA MUUNGANO. NDIO MAANA TUNASIKA BAADHI YAO WAKITAMKA BILA YA AIBU KUA WATAULINDA MUUNGANO KWA NGUVU ZAO ZOTE. NILITEGEMEA WATASEMA TUTAWAULIZA WANANCHI. HUU NI USALITI NA NILIJUA KUA TUMEKWISHA PALE BILA YA AIBU ALIPOKUBALI KUAPA KAMA WAZIRI ASIE WIZARA WAKATI WOTE WALIOMTANGULIA HAWAKUFANYA HILO. AKIENDELEA TENA MIAKA MITANO IJAYO HUYU ATAIMALIZA NCHI KUINAKAMIZA KWA WATANGANYIKA. VIONGOZI ZINDUKENI MMEKAA KAMA MLIOLISHWA LIMBW……. NCHI INAPOTEA KWA KASI KATIKA RAMANI YA DUNIA KATIKA AWAMU HII YA DR SHENI KULIKO AWAMU NYENGINE YOYOTE ILE.

 8. ndugu wawakilishi msije kukubali hata siku moja kuwa na sarafu moja ya jumuiya ya afrika mashariki, euro imegonga mwamba ktk EU , na hao wenzetu wana uchumi mzuri kuliko wetu , msije kubebwa, ndio maana tunataka muungano uvunjike tuwe na sarafu yetu nd omari yusufu muzee , usiwe kama mtu aliyekuwa hakusoma, ingawa waswahili wamesema elimu huondoa ujinga sio upumbavu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s