CCM yalalamikia rafu katika utoaji wa maoni ya katiba

Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Zainab Khamis Shomari akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na Kikundi cha Watu kinachotaka kuharibu mchakato mzima wa kukusanya maoni ya katiba mpya unaoendea hivi sasa katika Mkoa huo.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitaka tume ya katiba kuchukua hatua dhidi ya watu wanaofanya vitendo vya udanganyifu kwa kuwasilisha barua za maoni kwa tume hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari huko Dunga Mkoa wa kusini Unguja Katibu wa CCM wa mkoa huo, Zainab Shomari alisema kumeanza kujitokeza vitendo vya udanganyifu wa watoaji maoni kwa kutumia majina bandia kwa wawasilishaji.

“Kuna jina la Said Mwema limejitokeza katika barua na baada ya barua hizo tume ilitaka kumjua huyo mtu anayeitwa Said Mwema lakini matokeo yake hakuna aliyejitokeza,  kwa hivyo sisi tuna mashaka na hao watu wanaokwenda kupeleka maoni kwa njia ya barua tukiamini kuwa zinaandaliwa na baadhi ya wanasiasa” alisema Zainab.

Akivitaja vitendo vyengine  vinavyofanywa katika mchakato huo, Zainab alisema ni pamoja na kuzomeazomea vilivyofanywa na vyama tofauti vya siasa, kuwatumia wanafunzi kutoa maoni baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa walimu wao pamoja na baadhi ya wanasiasa kuwaongoza wafuasi wao na kuwaelekeza maneno ya kwenda kutoa katika tume hiyo.

Katibu huyo alisema awali zoezi la utoaji maoni lilikuwa likiendelea vizuri lakini katika siku za hivi karibuni kumeanza kujitokeza vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisimama kutoa maoni hali ya kuwa sio wakaazi wa maeneo husika.

“Kwa nyakati tofauti wananchi wa maeneo ya Mzuri na Mtende wameshuhudia baadhi ya wazanzibari wa kutoka maeneo mengiwakifurika huko kwa lengo la kutoa maoni mbele ya tume hiyo kinyume na taratibu za nchi” aliwaambia waandishi wa habari.

Katibu huyo alisema kwamba baadhi ya wazanzibari hao bila ya kigugumizi wala khofu “wakaanza kuandika mami ya barua za kughushi na hatimae kuziwasilisha mbele ya tume ya jaji Warioba ili zikubaliwe na kuyafanya ni miongoni mwa maoni yaliyotolewa na wananchi wa vijiji hivyo”.

Akitoa ushuhuda wa matukio hayo Katibu huyo alisema Kizimkazi Dimbani baada ya kutokea hayo Dk Salim Ahmed Salim alitoa karipio kali dhidi ya wavunjaji wa sheria ambapo wananchi wa kijiji cha Bwejuu na vijiji virani walikuwa wakishuhudia vitendo hivyo.

“Tume ya katiba ililazimika kusitisha zoezi hilo ili kutumia muda huo kwa kutoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya kitendo hicho cha kihuni na atimae kuwataka waachane kabisa kuendelea kuvifanya kwa vile havina hatima nzuri kwao na wala taifa” alisema Zainab.

Aidha alisema baadhi ya walimu katika kijiji cha Bwejuu wamejitokeza baadhi ya walimu wa skuli za serikali wanaowashawishi wanafunzi wao kwenda kutoa maoni kwa matakwa ya walimu hao. Chama hicho kimesema kinaalaani vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na sheria pamoja na kuitaka tume iwe macho na vitendo hivyo na wasisite kuchukua hatia za kisheria dhidi ya wale wote ambao wana lengo la kuharibu zoezi hilo.

“CCM inatoa wito kwa wanachama na wapenda amani, utulivu na maendeleo ya taifa letu wa maeneo yote ya mikoa ya Zanzibar kuwa macho na wale wote wenye lengo la kuvuruga kwa makusudi zoezi hili, kwa kuwatolea taarifa mbele ya vyombo vya dola, ili sheria ichukue mkondo wake didhi yao” alisisitiza Zainab.

Advertisements

15 responses to “CCM yalalamikia rafu katika utoaji wa maoni ya katiba

 1. Aslaam Aleykum. Kwa uzoefu wangu wa siasa za nyumbani Zanzibar, ukiona CCM imelalamika, ujue walishacheza rafu. Wanataka huruma, labda wamegundua kuzidiwa kete na wale wanaopingana na msimamo wao khs maoni ya Katiba. Si ndio hawa tuliosikia mwenzao ameandika barua ya maoni yanayofanana na kukabidhi wananchi wa jimbo lake la Makunduchi? Si ndio hawa CCM, chama dola?
  Mama mia…

 2. Ivi wewe mh unasema maneno haya unamdanganya nani asiejuwa. Unafanya watu ni mbunbu kiasi hichi. Nani asiejuwa kuwa viongozi wa serikali yenu ya ccm pamoja na wakereketwa wa ccm ndio waliowaruni watu kwa kuwapa sh 10,000/ ili wakatowe maoni waliowapangia. Ee wana ccm wacheni kujitowa kimasoso wacheni utashi wa kisiasa, hebu kuweni wazalendo au nyie hamutaki kuona Zanzibar na mamlaka yake ya kidola. Sisi tunasema hata mukafanya vipi zuweni uongo lakini sisi tutashinda tu kwa ngu za Mungu. Hamuna uwezo mbele ya Mungu. Bandari sasa twaiona na karibu karibu tutapumua kwa nafasi. ZANZIBAR HURU KWANZA. Sisi HATUUTAKI MUUNGANO. WENGI WAPE USIPOWAPA WATACHUKUWA TU KWA WINGI WAO. Wanzanzibari wengi HAWAUTAKI MUUNGANO. Musiwalazimishe mutakuIvi wewe mh unasema maneno haya unamdanganya nani asiejuwa. Unafanya watu ni mbunbu kiasi hichi. Nani asiejuwa kuwa viongozi wa serikali yenu ya ccm pamoja na wakereketwa wa ccm ndio waliowaruni watu kwa kuwapa sh 10,000/ ili wakatowe maoni waliowapangia. Ee wana ccm wacheni kujitowa kimasoso wacheni utashi wa kisiasa, hebu kuweni wazalendo au nyie hamutaki kuona Zanzibar na mamlaka yake ya kidola. Sisi tunasema hata mukafanya vipi zuweni uongo lakini sisi tutashinda tu kwa ngu za Mungu. Hamuna uwezo mbele ya Mungu. Bandari sasa twaiona na karibu karibu tutapumua kwa nafasi. ZANZIBAR HURU KWANZA. Sisi HATUUTAKI MUUNGANO. WENGI WAPE USIPOWAPA WATACHUKUWA TU KWA WINGI WAO. Wanzanzibari wengi HAWAUTAKI MUUNGANO. Musiwalazimishe mutakuIvi wewe mh unasema maneno haya unamdanganya nani asiejuwa. Unafanya watu ni mbunbu kiasi hichi. Nani asiejuwa kuwa viongozi wa serikali yenu ya ccm pamoja na wakereketwa wa ccm ndio waliowaruni watu kwa kuwapa sh 10,000/ ili wakatowe maoni waliowapangia. Ee wana ccm wacheni kujitowa kimasoso wacheni utashi wa kisiasa, hebu kuweni wazalendo au nyie hamutaki kuona Zanzibar na mamlaka yake ya kidola. Sisi tunasema hata mukafanya vipi zuweni uongo lakini sisi tutashinda tu kwa ngu za Mungu. Hamuna uwezo mbele ya Mungu. Bandari sasa twaiona na karibu karibu tutapumua kwa nafasi. ZANZIBAR HURU KWANZA. Sisi HATUUTAKI MUUNGANO. WENGI WAPE USIPOWAPA WATACHUKUWA TU KWA WINGI WAO. Wanzanzibari wengi HAWAUTAKI MUUNGANO. Musiwalazimishe mutakuIvi wewe mh unasema maneno haya unamdanganya nani asiejuwa. Unafanya watu ni mbunbu kiasi hichi. Nani asiejuwa kuwa viongozi wa serikali yenu ya ccm pamoja na wakereketwa wa ccm ndio waliowaruni watu kwa kuwapa sh 10,000/ ili wakatowe maoni waliowapangia. Ee wana ccm wacheni kujitowa kimasoso wacheni utashi wa kisiasa, hebu kuweni wazalendo au nyie hamutaki kuona Zanzibar na mamlaka yake ya kidola. Sisi tunasema hata mukafanya vipi zuweni uongo lakini sisi tutashinda tu kwa ngu za Mungu. Hamuna uwezo mbele ya Mungu. Bandari sasa twaiona na karibu karibu tutapumua kwa nafasi. ZANZIBAR HURU KWANZA. Sisi HATUUTAKI MUUNGANO. WENGI WAPE USIPOWAPA WATACHUKUWA TU KWA WINGI WAO. Wanzanzibari wengi HAWAUTAKI MUUNGANO. Musiwalazimishe mutakuja juta.

  • sasa haya makubwa!! hii tume inachukuwa maoni tu, na badae kutapigwa kura ya maoni, si mgojee hio kura kwanza!! mnalalamika nini?

  • Medy wewe unajifanya Mpemba kumbe unajaribu kuleta kejeli na ubaguzi kwasababu Mpemba anapoandika kiswahili hawezi kuandika hatuwebu tena hatuwebu. Mpemba ni muandikaji mzuri wa Kiswahili. Ukweli utabakia palepale kuwa sio wapemba tu wanaokataa MUUNGANO ni Wanzibar wote kwa ujumla.

 3. ZAINAB WALIOFANYA HIVYO NI HAROUN ALI SLEMAN NA SAMIA SULUHU NA WANAJULIKANA NI WA CHAMA GANI. NA MSIMAMO WAO NI UPI KWA KUA WANALINDA MASLAHI BINAFSI. KUMBUKA MLITUDANGANYA MIAKA MINGI NA MKAFANIKIWA SASA UAMSHO IMETUZINDUA NA HAKIKA MUUNGANO HUU UTAKUFA TU MWAKA HUU. TUACHENI TUPUMUE.

  • Mimi binafsi sipendi hata kidogo kudhaniana mambo ambayo hatujayafanyia uchunguzi. “No research no right to speak” Pia sipendelei sana kuhusisha vyama vya siasa, kwani tutazida kuchochea chuki kati yetu. Unaweza ukataja chama ila utoe na ushahidi wa kuridhisha kuhusu jambo unalolizungumzia.

 4. Bi shomari bi shomari bi shomari we haya tena makubwa leo CCM ZNZ ndio inalalamika kuibiwa kuchezwa shere. Doh! “its true that everything has it last” Na bado dada huo mkoa wanafiki wengi mambo ni hayo je mkija KWETU itakuwaje?
  Ewe MOLA wape nguvu wenye nia njema na ZANZIBAR na utucmamishie ya RABI JAMUHURU YA ZNZ HURU. Vilevile ya ALLAH YA JARIM wadhalilishe wale wote wenye nia MBAYA na ZNZ. Amin amin amin

 5. Brother mawazo yako yamewafikiana na yangu wakati ninasoma hii makala liniuona ukweli huu ndani ya akili na experience yangu nikataka nije nitumie neno sympathy (huruma) kwenye comment yangu kuonyesha namna ambavyo CCM wanavyosaka uhalalishaji wa matumizi ya nguvu,vitisho na unyanyasaji dhidi ya watetezi wa Zanzibar dhidi ya Muungano huu wa Pwagu na Pwaguzi.

  Tahadhari:

  Mkianza kutuharibia tutakuharibieni. La hamuamini anzeni mtaona na ukale ng’an’ganizi wenu huo.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Naunga mkono hoja @Brother Jabir Idrissa.

  SERELLY.

 6. Wewe Bi Shomari unasema nini wewe hebunyamaza ulikuwa Waziri ukashindwa itakuwa katibu Mwakani utakuwa Shekha uje ugawe Kanga hiyo ndo CCM Dada usivamiye meza wakati hujuwi yanayo zungumzwa

 7. Mimi nilijua toka mwanzo huu mpango wa Barua ungeharibu. Ivo mtu haitoshi kusema tu kisha akaondoka. TUME ndio ya kulaumiwa kwa kuendekeza hili. Kule Kizimkazi Dimbani Kijana moja wa kike alileta barua yake na za Wazee wake watatu. Huu mchakato si sawa na Maziko kama ni Fadhi Kifaya.

  Nilidhani wangeacha wale wanaohudhuria kutoa maoni yao si wanaowakilishwa. Is not about getting more people regstered, it is about regstering credible opinions. Hawa Kina wanaolalamika ni bora yawakute kwa kuwa hawajui wakifanyacho.

  Jamani ileweke kuwa sisi sasa hatuandiki MKUZA III ambayo lazima ya reft Ilani ya Uchauzi ya Chama. Sisi unaandika KATIBA. Misimamo ya Vyama iwacheni enyi msiofahamu mambo. Tuelezeni Tanzania hii miaka 50 ijayo iweje. TUMe ya Katiba ilikosea sana kutowapa kozi ya alau ya ABC kuhusu katiba hawa vinogozi wajao kwenye vikao vya kutoa maoni na kutaka watu waseme wanayotaka.

  Vile vile ni lazima tufahamu kuwa hapa haturekebishi Katiba tunaandika upya. Nyinyi muonao Watu wa Zanzibar ni kama watoto wenu mnakosea sana. Watakao juta huko mbele ni watoto wetu kwa sote tuakuwa tumeondoka! Watu ambao wanaona watakosa kazi kwa kuruhusu maoni tofauti wasiwe na wasi wasi hii Katiba hadi kutumika itachukua miaka kabla ya kutumika. Wakati huo Akina dadangu hamnatakuwa tena nguvu za kufanya kjazi wakati huo. Achia kizazi kijacho kikjingee musakbali wake!

 8. POLENI SANA

  Pole sana dada yangu Bi Zainab, mimi nashangaa sana chama changu cha CCM kwanini kila siku hufanya vitu ambavyo Wazanzibar wanavijua juu chini, nje ndani halafu wao ndio hujitia kulalamika, naona mwaka huu tumechemka maana sasa upepo umebadilika. Nakiomba chama changu cha CCM kisome alama za nyakati laa si hivyo mtapoteza wanachama wenu kwa kosa lenu wenyewe, hebu angalieni chama cha wananchi CUF kiko kimya kinaangalia upepo unapo kwenda ndiko na wao wanakokwenda sio kama wafinyu wa kufikiri laa wanajua kua sasa Wazanzibar sio watu wakuwadanganya kichama huu ni wakati wa UAMSHO sio CUF wala CCM ni UAMSHO.

  Kuchukia UAMSHO nikujipotezea hadhi yako. Na waomba sana wakuu wa CCM msikilizeni MH. Amani ingawa nae pia mnamchukia lakini huyo sasa ndio Makamu Mwenyekiti wetu, jifunzeni kwake hata jana tu kwenye Ijtmai ameongea maneno mazuri km utayatafakari kidogo maana kasema hivi “Jambo wakilikamata vijana hilo basi lazima liangaliwe kwa makini la sihivyo munaweza mukapoteza hata nguvu kazi”. Poleni sana CCM wenzangu uongo wetu hauna nafasi tena kilichobaki ni kuungana na wenzetu kudai Nchi yetu. Maana kwa sasa hakuna asiyejua kua Muungano si muungano ila nyinyi ndio mnaolazimisha hebu wambieni wawakilishi wetu kua wawe kama wa CUF japo kua wanautaka moyoni mwao kwa sasa wajidai hawautaki hilo ndio suluhisho la maisha ya CCM

  Kwa upende mwengine hebu angalieni mnalalamika kuwa watu wamepewa vibahasha vya maoni na vyama vya siasa wakati Zanzibar nzima inajulikana kua Haroun, Samiha na Kificho ndio waliowapa watu bahasha zenye pesa (10,000/=) na maoni ya kutoa juu ya serikali moja, ila watu wamewagomea na kutoboa siri na ndio maana Mh Haroun akataka kujisafisha kwenye baraza la wawakilishi kua yeye hahusiki na kadhia hiyo. Je! nikuulize suali Mh Zainab kuna chama chengine chochote kilicho jitoa kimasomaso kama si CCM.
  Wakatika umefika, lazima tubadilike, mabomu, polisi, mbwa, virungu sio solution bali kusikilizwa kwa wananchi juu ya wanachokitaka sasa ndio solution. Mambo yakukaa tukang’ang’ania sera za vyama yamepitwa na wakati hasa juu ya suala hili la katiba kueni wazalendo wa nchi hii ili muende sambamba na wananchi la sihivyo majuto ni mjukuu huja muishoni. Wazanzibar wanachotaka ni WAACHIWE WAPUMUE huu si ujinga ni haki ya msingi iliotokana na udhalilishaji wa Watangantika.

  Poleni sana CCM. Time imefika, tubadilike.

 9. Nakumbuka mara nyingi ktk utoto wangu ninapofanya kosa huwa namshingizia mwenzangu! ili nionekane msafi! huu ndio utoto unaofanywa na machakubimbi wa CCM! wako peke yao lkn wanaanza kutishana kwa vivuli vyao, maskini nyii! uwanja wa nyumbani munalia ugenini sijui itakuaje? watu wameamka !UAMSHO hangera kwa kazi iliyotukuka! bi zainab ni kweli kuna wanasiasa wenye mashati wanataka kuharibu hili zoezi! sasa kwanini huwaiti kwenda kuwalaumu! kwani hamuna matawi? naona hali kwenu ni mbaya! hata bado pumzika bibi wameshidwa wenye meno! soma wakati siasa haipo tena! au huamini? kazi kwisha? mutakimbia kwa husda zenu ! zanzibar kwanza!

 10. Binafsi sishangai sana viongozi wa CCM kama Zainab na Mhe. Panya, hawa watu wapo katika karne mpya lakini mawazo yao bado ni ya kizamani.

  kwanza: dhana ya kuwa baadhi ya watu wanawatolea maoni watu wa kijiji fulani haina mantiki kwa sababu mtu yoyote anaweza kuandika barua na kutaja jina lolote na pahala popote anapotoka na wala isiwe lolote kwa kuwa barua hizo zinaweza kuwasiliswa katika ofisi ndogo ya tume iliopo kikwajuni, Gofu.

  Pili: ni lazima watambue kuwa maoni yanaweza kutolewa kwa njia tofauti ikiwemo kwa kuzungumza mbele ya tume, barua na kupitia web page/tovuti ya tume ya mabadiliko ya katiba. tovuti ambayo haijaweka mipaka ya kumfunga mtu kwa jina, eneo wala utambulisho maalum. ( ID no)

  Tatu: mwisho wa siku tume itasema haya ni maoni ya Wazanzibari na siyo wa kusini, kaskazini au Mjini magharibi.

 11. qua-an kweli ni kitabu cha haki ALLAH amesema “NA HAYO NDO MASIKU TUNAVYO YABADILISHA BAINA YA WATU” yani leo ww utatamba kesho huna kitu. ah! leo ccm mumekua dhalili hivyo? na wala bado . nusra ya ALLAH inakuja wanyonge nasi karibu tutapumua INSHALLAH

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s