Waliokimbilia Somali warejea nyumbani

Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001

KATIKA hali ambayo haikutarajiwa Wazanzibari waliokuwa wakiishi Somali kama wakimbizi wamerejea nyumbani jana na kupokelewa na ndugu na jamaa zako katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. Hali ya ulinzi ulikuwa imeimarishwa na maafisa wa usalama ambapo haikuwa rahisi kwa waandishi wa habari na wapiga picha kuwasogela hadi walipotoka ndani ya ndege mbili maalumu za Umoja wa Mataifa (UN) zilizowaleta.

Sura za wa wageni hao na wapokeaji zilisajika baada ya kufika uwanja huo ambapo baadhi ya watoto wakionekana wakilia muda mfupi baada ya kutua huku wazazi wao wakiwa na furaha na kukanyanga tena nyumbani.

Wakizungumza na waandishi wa habari walionesha hisia zao za kufuwahia kurudi nyumbani na kusikitika kuwa baadhi ya wenzao wamekataa kurudi kutoka na kupata taarifa za maandamano yaliotokea Mei 27 mwaka huu na kusababisha mali kuharibiwa na baadhi ya watu kushitakiwa.

“kwa kweli watu wengi walikuwa tayari kujisajili na UNHCR tayari kurudi nyumbani lakini kitu kilichowarejesha nyuma wenzetu ni baada ya kusikia maandamano na baadhi ya matukio ya hivi karibuni kuzuwiwa kwa mihadhara na baadhi ya watu kushitakiwa….kwa hivyo wakaogopa akiamini hali haijatulia bado” alisema Mohammed Suleman na kuongeza.

“Nimefurahi sana kurudi nyumbani lakini changamoto pekee ni kuanza maisha mapya japo tumepewa msaaada na shirika la UN” alisema Mohammed Suleiman.

Suleiman alisema ameowa mke wa kisomali na amezaa watoto wawili na anatarajia kuendelea na kazi yake ya uvuvi ambayo alikuwa akiifanya huko Somali katika mazingira magumu.
Naye Abdallah Ahmed ambaye ameoa mke wa kisomali amesema wameamua kwa hiyari yao kurudi nyumbani na wako tayari kushirikiana katika ujenzi wa zanzibar.

Abdallah alisema katika maisha yao ya miaka 11 nchini Somali yalikuwa ni ya shida sana kutokana na ukosefu wa usalama pamoja na kazi za kufanya huku wakitegemea zaidi msaada kutoka kwa mashirika ya kimataifa.

Jumla ya familia 12 zenye idadi ya watu 38 wamerejea nyumbani huku baadhi yao wakiwa na wake wa kisomali na baadhi yao tayari wameshapata watoto zaidi ya wanne.

Kuhusu haki za watoto waliozaliwa nchini Somali mwanasheria mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini aliekeza kuwa watoto hao wataamua uraia wa Somali au wa Tanzania watakapofikia umri wa miaka 18.

Wakati mama zao ambao wamekuja na pasi za kusafiria za umoja wa mataifa utaratibu wa kisheria utafuatwa baadae ambapo ama watachagua kubaki na uraia wa nchi yao au kuomba uraia wa Tanzania.

Wengi wa wazanzibari hao waliokuwa wakijishughulisha na kazi za aina mbali mbali ikiwemo uvuvi pamoja na biashara wengine walikuwa tayari wameshajiunga na timu za mpira ya miguu za nchi hiyo lakini wake zao wameshindwa kuzungumza kiswahili.

“Huyu ni mke wangu lakini yeye hajui kuzungumza kiswahili lakini mimi naongea kisomali kwa kuwa mimi nilijifunza hiyo lugha” alisema mzanzibari mmoja ambaye ni miongoni mwa walioowa wasomali.

Familia za wageni hao walijitokeza katika uwanja wa ndege kuja kuwapokea jamaa ambapo kwanza walikataa kuongea na hata kutajwa majina yao katika vyombo vya habari walielezea furaha zao za kuwapokea ndugu zao hao.

“Tumefurahi kwa kweli kujumuisha na familia zetu kwa sababu ni miaka mingi tulikuwa hatuna uhakika wa kuwa ndugu zetu kama wapo hai na hasa tukisikia kila siku machafuko ya huko somali tuna wasiwasi mkubwa lakini leo tumefurahi sana” alisema mama mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa habari wa shirika hilo, Austine Makani alisema kwamba mambo mawili ndio yaliosababisha wazanzibari kuamua kurudi nyumbani.

Akiyataja mambo hayo ni kuzidi kuzorota hali ya usalama na hali ya njaa kukithiri nchini Somali pamoja na kuendelea kutengemaa kwa hali ya amani nyumbani Zanzibar.

Aidha afisa huyo alisema wazanzibari hao wageni wataanza leo jumamosi kuunganishwa na familia zao Unguja na Pemba ambapo wanaokwend aPemba watasafiri kwa kutumia usafiri wa boti na baadae kufikishwa katika vijiji vyao.

Katika uwanja huo wa ndege hakukuwa na afisa yeyote wa juu wa serikali aliyekuja kuwapokea wazanzibari hao na haikufahamika mara moja sababu za kukosekana kwa kiongozi wa serikali kufika uwanja wa ndege.

Hata hivyo baadae katika mkutano na waandishi wa habari na maafisa wa UNHCR waliowashindikiza wazanzibari hao kutoka Somali baadhi ya maafisa kutoka uhamiaji walifika na kuwatoa wasiwasi wazanzibari hao kwamba hali ya usalama utakuwepo na wajisikie wapo huru.

Hii ni mara ya pili shirika hilo la UNHCR kuwarejesha nyumbani wazanzibari walikuwa nchini Somali kutokana na kuimarisha hali ya amani Zanzibar.

Zaidi ya wazanzibari 2000 walikimbilia Mombasa Kenya na baadae kuhamishiwa katika kambi za wakimbizi za Somali kufuatia mac hafuko ya kisiasa yaliotokea baada aya uchaguzi mkuu wa 2000.

Advertisements

6 responses to “Waliokimbilia Somali warejea nyumbani

 1. Chama cha CUF kimeonyesha dharau kubwa kutokujitokeza kuwapokea ndugu zetu waliokimbia machafuko ya mwaka 2000.
  Nimesema dharau kubwa kwani tayari wao ndio walichangia kuwapeleka Viongozi mbele katika SUK na leo kuonekana wakubwa katika serikali , pia ni kutokana na mchango wa ndugu hawa waliokimbilia mwahali kunusuru maisha yao.haikuwa na haja ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao katika siku hiyo ikiwa waliokuwa hai wamedharauliwa.
  Basi hata mmoja kufika kiwanja cha ndege na kukiwakilisha chama cha CUF katika mapokezi ya ndugu zetu hawa?
  Ikiwa chama cha CUF kimedharau kuwafariji ndugu zetu hawa,ni kweli kesho kitarefusha mdomo na kuomba kura zao?
  Si mambo ya aibu mgeni amefika hujaenda kumpokea kesho unamtaka aje akusaidie kupiga makoongwe ni kweli mgeni huyo atakujaa?
  Shutuma hizi na azisome Maalim SEIF kisha atafakari yeye na waliomzunguka katika chama chake kwani kimewagusa na kitakumbukwa maisha japo kwa udogo wa suali wanavyoliona ,lakini mimi nasema tukio si dogo na historia itajikumbusha na itajikumbusha katika kampeni za kuomba ridhaa za hao waliotoka somalia na sisi tulio hapa.
  Pia litakuwa kichocheo kikubwa wakati huo wa kuomba ridhaa zao kuwapigia kura ili wapate ureda kama huu wa leo ,

 2. Mimi sishangai kuwa hakukua na kiongozi hata mmoja wa serikali hapo uwanja wa ndege kuwapokea hao wakimbizi kwani hao hao viongozi waliopo serikalini ndio waliosababisha hao Wazanzibar kuwa wakimbizi.

  Kwahiyo wanaona aibu kuja kubanwa na maswali ya waandishi wa habari kwani wao ndio chazo cha yote hayo.

 3. Haitoleta sura nzuri kama hakuna kiongozi yeyote wa serikali – bila kuangalia chama anachotoka – alokwenda kuwapokea na kuwasalimia. Wiki zilopita tuliona katika habari wananchi wa Sudan ya kusini wakirudi kwao kutoka Israel na wakapokewa na kiongozi wa serikali. Sasa na serikali basi japo kuonyesha dunia kuwa inawajali wanannchi wake basi angejitokeza japo mmoja kuwafariji ili watu waone kuwa wanakaribishwa kwa mikono miwili nchini kwao.

 4. THESE ARE JUST MINOR ISSUES WHICH ARE USED BY THOSE WHO ARE AGAINST ZANZIBAR’S INTERESTS TO DERAIL US AGAINST OUR COMMON ENEMY “THE UNION” LET US FOCUS ON THIS AND THEN WE WILL COME BACK TO THE ISSUE OF WAKIMBIZI LATTER ON. AS LONG AS THEY ARE BACK HOME AND SAFE IT IS OK. FROM NOW ON LET EVERYONE CONCENTRATE ON HOW THIS NIGHTMARE “THE UNION” CAN BE CRUSHED DOWN.

  • Ebwana upo sawa, tukizungumzia jengine lolote zaidi ya Muungano tutajenga sahau, katika kukumbuka ishu hizi(Kuupinga Muungano) hazikuaza leo wala jana ila kila zikizuka mara keki imejiandika, sijui kanisa limechomwa moto, msikiti umevunjwa. ilimradi tusahau kuupinga Muungano, kwa sasa hatudanganyiki “short & simple” TUSIANGALIE JAMBO DOGO LIKATUGOMBANISHA, sisi ni wamoja la CCM na CUF ni la Wazanzibar wote. hivyo bas shime alaikum katika kuupinga Muungano.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s