Serikali: Zanzibar haijawahi kutawaliwa

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman

MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman ameshangazwa na mwanasheria mwenzake Tundu Lisu kwa kutofahamu madhumuni na malengo ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliozaa serikali ya umoja wa kitaifa. Kauli ya Mwanasheria huyo aliitoa katika baraza la wawakilishi wakati akifafanua baadhi ya mambo ya kisheria baada ya wajumbe wa baraza hilo kumtaka afanye hivyo kufuatia kauli ya ya Tundu Lisu aliyoitoa bungeni wiki hii.

“Sasa kuja kwa haya yametuonesha kwamba kuna wenzetu kumbe wana fikra kwamba Zanzibar iliwahi kutawaliwa. Maana mtu anaposema marekebisho ya 10 ya Zanzibar yamjitangazia uhuru maana yake ana fikra na huyu ni mwanasheria mtu kafika mpaka kuwa mbunge anayeaminika na chama chake lakini anasema kwa kufanya hivyo Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa?” Alihoji Othman.

Akijadili bajeti ya wizara ya makamu wa rais wa jamhuri ya muungano, huko Dodoma Mbunge wa Singida Mashariki wa Chama Cha (CHADEMA) Tundu Lisu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Zanzibar imefanya katiba kwa kujitangazia kuwa ni nchi.

Othman alisema marekebisho ya katika ya Zanzibar yalikuja baada ya hoja nyingi ambazo hazikuwa na majibu katika muungano ambayo ilikuwa ikisema ni Zanzibar ni sehemu ya muungano, lakini kama nini mkoa? Shehia? Kata? au kijiji?, haya hayakuwa na jibu katika katiba ya muungano.

Kufuatia maridhiano Zanzibar ndipo wazanzibari wakamaua kufanya kukufikia marekebisho ya 10 ya katiba yao ambayo ilifafanua kuwa zanzibar ni nchi na ndivyo ilivyo kwa sababu haikuwahi kutawaliwa kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanavyofikiria.

“Marekebisho ya 10 ilichofanya ni kusema kwamba ikiwa mtu hatambui, maana ilikuwa imeshaonesha dalili kwamba kuna wengine hawatambui hilo tena wakubwa. Sasa marekebisho ya 10 yalipokuja ni kufafanua tu, kama kuna mtu hatambui sisi wenyewe tunajitambua” alisema mwanasheria huyo huku akiungwa mkono na wajumbe kwa kupigiwa makofi.

Huku akishangiriwa na wajumbe wa baraza hilo mwanasheria mkuu alisema hakuna mtu ambaye atawazuwia kusema “Aaah katiba yenu isiwe namna gani au isiwe hivi na ndio maana unakuta katiba za muungano zipo nyingi lakini kila mmoja ina muundo wake kwa mujibu mlivyokubaliana nyinyi wenyewe”.

Mwanasheria mkuu alisifu muungano wa miaka mingi wa Uswizi ambao unatambulika na kuigwa duniani kutokana na kufuata misingi imara iliyowekwa na wananchi wenyewe.

Alisema muungano ambao umedumu na unasifiwa ni Swiss Federation kwa sababu umeanza tokea mwaka 1292 na umekwenda kwa mafahamiano hadi mwaka 1874 wakatunga katiba ambayo wameifanyia mapitio upya mwaka 1999 na nchi hiyo ina serikali 26, lugha nne rasmi na ndio muungano amabo umedumu na nchi ambayo ni imetulia duniani.

Mwanasheria huyo alisema mashirika yoye ya kimataifa yapo Uswizi kwa sababu ya muungano huo uliotumilia na kwa sababu umekuwa na misingi imara ya kuhakikisha muungano ule unaweza kuhimili mabadiliko yoyote yatakayokuja ya kisiasa.

“Mheshimiwa Naibu Spika nitumie fursa hii hapa hapa niseme wakati tupo katika mchakato wa maoni ya katiba nadhani ni wakati mzuri kuiweka sawa ile misingi ya muugano kama Uswizi”. Na kuongeza kuwa.

“Wakati mwengine napata wasiwasi nasema hii khofu yangu niiseme hapa kwamba tunaanza kubishana kuhusiana na watunza nyumba wawe wangapi, waendeshaji nyumba wawe wangapi, wawili, watatu, wanane au watano?. Lakini tatizo letu la msingi mimi nadhani ni nyumba yenyewe iweje. Kama tunaamua kuishi, maana mfumo wa sasa hivi mmoja anaishi nyumba kubwa na mwengine mabandani huko uwani huo sio utaratibu tunao”alisema mwanasheria.

Aidha aliwaambia wajumbe hao kwamba wanzanzibari wana mambo ya msingi ya kujadili kuliko kuzungumzia idadi ya watunza nyumba akimaanisha kero za muungano zilizopo na kushindwa kuafikiwa.

“Kwa hivyo mimi niwaombe sana waheshimiwa wajumbe, niwaombe na wazanzibari wenzangu na wananchi wote, kwamba huko mbele tusije tukalaumiana kwamba tumefanya marekebisho ya 10 kimakosa na tumejitangazia uhuru. Sasa hivi tuondoe fikra hizo lakini tunaweza kujieleza kwa hoja za msingi na mambo ya msingi katika hoja hii hapo ndipo tutakapojenga utawala bora ndani ya muungano” aliongeza Mwanasheria huyo.

Akitoa ufafanuzi zaidi kwa wajumbe hao kuhusu muungano Othman alisema hata suala la uraia limepewa kipaumbele katika katiba ya Uswizi ambapo mtu anapozaliwa ndipo anapopewa uraia wake.

“Pale unapozaliwa ndio panapokupa uraia, na kuna mengi ambayo nadhani tatizo liliopo kwa wenzetu ni kwamba hawajifunzi kwamba muungano ni kitu gani. Muungano ni suala ambalo nchi mbili mnapoungana, nchi zilizokuwa huru ni suala la makubaliano na mtakachokubaliana ndicho ambachi kitakuja katika katiba yenu” alisema Othman.

Othman ambaye ni mwanasheria aliyewahi kuandika waraka (paper) aliyoipa jina ‘masuala ya yasiokuwa na majibu ndani ya muungano’ aliwaambia wawakilishi hao kwamba maelezo ya Tundu Lisu yamejaa hadaa na yamejaa upotoshaji tena upotoshaji ambao umepindukia mipaka ya kweli.

“Mimi nimepata kusoma na kuangalia hiyo hutuba ya Mhe Tundu Lisu… lakini pia nimeona majibu ambayo yalitolewa na mhehsimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyesema kuwa maeelzo ya Mbunge Lisu yamejaa hadaa na upotoshaji naungana naye” alisisitiza huku makofi ya wajumbe yakitawala ndani ya baraza hilo.
Tokea kuanza kwa kikao cha baraza la wawakilishi kwa kiasi kikubwa mijadala wa bajeti umetawaliwa na suala la muungano ambapo wajumbe wengi wamekuwa wakiungana na wananchi kudai maslahi zaidi kwa zanzibar ikiwemo kurejesha kwa hadhi ya rais wa zanzibar na mamlaka kamili ndani na nje ya nchi.

Advertisements

13 responses to “Serikali: Zanzibar haijawahi kutawaliwa

 1. Nauna wanakuja wenyewe Uamsho walisema Zanzibar haijawahi kutawaliwa lakini kina Borafya wakajifanya ni wasomi kuanza kuleta fitna lakini bado ni wao wenyewe mwisha watadai kura ya maoni kuhusu muungano humo barazani wanamobishana.

 2. KARUME KAMALIZA MANENO YOTE UAMSHO AMSHA WAZANZIBARI WAKATI WA KULA DAKU UNAWADIA. WAWAKILISHI WANAANZA KUAMKA BADO AKINA BORAFYA, MOHD ABOUD, SEFU IDDI, KAMISHNA MUSSA WA POLISI NA ALI HASSAN MWINYI.

 3. Mhe.Mwanasheria, Licha ya yote uliyosema barazani, sisi wazanzibari tunaona kama tuliotawaliwa na bara sababu, nyie viongozi wetu hamuonekani kama muna ubavu wa kuitetea maslahi ya wazanzibari. Linalopitishwa na CCM Dodoma ndio munalolikubali bila kuhoji. Hii ndio inayowapa watu nadhiria ya kuwa tumetawaliwa. Kutawaliwa sio lazima uambiwe kuwa umetawaliwa lakini, vitendo vyenyewenu ndivyo vinavo tufanya tufikirie hivo. (SADOMASOCHISM:the derivation of pleasure from the infliction of physical or mental pain either on others or on oneself). Huu ndio uhusiano wetu na bara.

 4. Mheshimiwa nakujua sana msimamo wako juu ya Muungano huu wa Pwagu na Pwaguzi. Lakani ukweli bwanaa! Tumetawaliwa vibaya sana, kwa sababu ni mental colonization ambayo gradually imeanza kujitafsiri in actions mpaka verbally ambapo kabla ya huyu Tundu jisu Mizengo Pinda na hata Mahakama ya Rufaa Tanzania ilisemwa waziii! Kuwa “ZANZIBAR SIO NCHI”.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 5. muongo mkubwa alosema hatujatawaliwa nani musiwe munakaa mbele ya vyombo vya habari kuuza sura zenu mbaya wakati muna sura za chuma tokea uhuru mumetutawalisha kwa watanganyika mpaka leo mwaendelea halafu mwasema zanzibar hatujatawaliwa au mwata mutuone twabanjishwa kunazi kw uvizi ndo mjue kua tumetawaliwa
  wanafiki wakubwa nyie laanatllah
  mutuache tupumue tena tomechoka na utawala mbovu na usio na tija

 6. Pingback: Serikali: Zanzibar haijawahi kutawaliwa·

 7. Hatujatawaliwa kwa kuwa tuna katiba, bendera na serikali yetu ya bandia ya kuendeshea mambo ya ndani ya mkoa wetu lakini kiutendaji wa kitaifa tumetawaliwa na watanganyika kwa miaka 48 sasa. hotuba ya Tundu Lisu ina hadaa kweli lakini na ukweli pia umo, nanukuu “Mambo yote yaliyoongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano baada ya mwaka 1964 yalikuwa nje ya Makubaliano ya Muungano na nje ya Sheria ya Muungano na kwa hiyo yalikuwa batili”. jee huu nao ni upoteshaji?
  Ningekubaliana na mwanasheria kama angesema maoni ya Tundu Lisu yana ukweli na upotoshaji ndani yake. Hata hivyo afadhali kidogo Mhe. Masoud amejirekebisha kutoka na kauli zake za kuhoji “je, kama wanandoa wanakosana ndio ndoa ivunjwe?” akipigia mfano wa Muungano na kero zake. Inaonekana aliifumbia mambo sheria ya talaka katika Uislamu pale ambapo ndoa ina matatizo sugu na kero zisikwisha mfano wa miaka 48 ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
  Wakati umefika wa Kurudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuupa muungano huu uliopo talaka 3.

 8. ASITULETEE USHWAHILI HUYU JAMAA, KWANI TANGANYIKA UMETAWALIWA? MUUNGANO WA ZNZ NA T/NYIKA ULIZAAA TANZANIA KUWA NDIO NCHI INAYOJULIKANA KIMATAIFA NA SMZ KUACHWA ILI ISAIDIE SERIKALI YA MUUNGANO KATIKA HARAKATI ZA MAENDELEO, MAANA YAKE T/NYIKA NA ZNZ KIMATAIFA HAZIKUWA NCHI TENA BAADA YA MUUNGANO. SASA HAO WAZNZ WANALETA UHUNI WA KUIPA MAMLAKA ZNZ KUWA KAMA NCHI INAYOJITEGEMA ANGALI ILISHAUNGANA NA NCHI NYINGINE NA KUZAA NCHI HUSIKA SIO HAKI, NDIO MAANA TUNDU LISU ALASEMA ILI TWENDE SAWA KATIKA HILI TUANZISHE SERIKALI YA T/NYIKA AU TUACHANE KABISA, is not fair. huu muungano wa namna hiyo ni kuwalelea waznz bure hatuutaki bora ufe.

 9. Akili ni nywele kila mtu ana zake. Mwanasheria wetu na wajumbe wetu msikurupuke nyinyi ndio SERIKALI mbona hajielewi mna jikaza eti sie hatujatawaliwa acha kujitia aibu ww mwanasheria. Tundu lisu hajakosea hata kidogo ile nichangamoto kwenu acheni ulafi nyinyi. Sasa wewe Mwanasheria kama huwelewi acha mimi nikueleze kidogo tu jinsi tulivyotawaliwa.
  1. Tumepoteza utaifa wetu kitu ambacho hata ww unakubali na umetutolea mfano SWIZ FEDERATION kwmb kila nchi ina utaifa wake wetu sisi ZNZ upo wapi?
  2. Fedha yetu imepotea na kihistoria tulikuwa na pesa zetu.
  3. Uchumi wetu umehodhiwa mfano halisi ni kuhamisha Bandari kuu ZNZ.
  4. Kupoteza maadili kutokana na kuzidiwa na wageni bila ya UTARATIBU maalumu.
  5. Kushindwa kujiamulia kile kinachotuhu sisi kama sisi na hata kile tunachoshirikiana kama nchi kwa mfano katiba ya ZNZ inasema sheria yoyote ambayo itapitishwa ili kufanya kazi ZNZ lazima naomba neno lizingatiwe sana (LAZIMA) ipitishwe kwenye BARAZA LA WAAKILISHI kwanza ndio ifanye kazi. Swali; Je sheria ya mabadiliko ya katiba ilipitishwa barazani na kujadiliwa na wajumbe wa baraza? Kama jawabu haijapitishwa bac tusaidie wewe mwanasheria nini MABADILIKO haya hayajaheshimu KATIBA ya ZNZ?
  6. Kupoteza nguvu za RAIS wetu na kufanywa WAZIRI tena asie na wizara.
  7. Kupoteza thamani kwa askari wetu(vikosi) RAIS wetu leo hana ujasiri hata wakukagua vikosi vyake kama AMIRIJESHI wa VIKOSI.
  Mnataka tutawaliwe vipi tena? Nyinyi wasomi tunawaheshime tafadhalini tafadhalini msikurupuke kama hatujataliwa ilikuwa BARAZA la waakishi likatae kutiwa ile saini ya MABADILIKO YA KATIBA na sababu zipo katiba imesema sheria ijadiliwe ipate ridhaa sio ije itiwe saini. Sisi wananchi tunahofu na nyazifa zenu ila pole tena pole mwanasheria wetu be confident. Nina mengi ila wanawaheshimu viongoz wangu wengne nawapenda ALLAH awape nguvu na uwezo wa kuisimamisha JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Amin amin amin

 10. Pingback: Zanzibar imejitangazia kuwa huru kwani tuliwahi kutawaliwa? – Mwanasheria Mkuu, Zanzibar·

 11. AO WENGINE KINA B.F CJUI KAMA WATAAMKA TENA NAONA KAMA WAMEFARIKI KABISA. JAMHURI YA ZANZIBAR KWANZA VYAMA BAADAE

 12. hawa mawaziri wetu kujilabu ndio kawaida yao wakiambiwa ukweli wanatuletea ngojera tutawaliwe vipi zaidi ya hivyi hatuamui kitu mpaka kipate baraka za dodoma lisu kasema kweli na hao wanafik wenzie huyu waziri wampigia kofi kulinda vitumbua vyao tuwacheni tupumue

 13. YA MANENO YA TUNDU LISSU HAYAKUJA KWA BAHATI MBAYA BALI NI KATIKA ZILE DUA ZETU ZA KUTAKA ALLAH ATUBAINISHIE KILA MWENYE BAYA NA ZANZIBAR. KATU HAYA YASINGESEMWA ILA NI KUDHIHIRISHA YALE WALIYOKUWA NAYO VICHWANI MWAO KUHUSU ZANZIBAR. HAWA JAMAA WANGEPENDA SANA KUIONA ZANZIBAR IKIWA HAINA MBELE WALA NYUMA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s