Mkutano wa kimataifa wa mazingira Rio+ 20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Fatma Abdulhabib Fereji akizungumza na baadhi ya watendaji wa ofisi yake pamoja na waandishi wa habari kuhusiana na matokeo ya mkutano wa Rio+20 uliofanyika nchini Brazil tarehe 20-22 Juni, 2012

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wametakiwa kujipanga ili waweze kushiriki katika mikutano ya kimataifa, kwa lengo la kuwasilisha maoni ya wananchi kwenye mikutano hiyo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji ametoa changamoto hiyo ofisini kwake Migombani, wakati akitoa muhtari kwa waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa Rio uliofanyika nchini Brazil tarehe 20-22 June mwaka huu.

Amesema wajumbe wa baraza la wawakilishi kupitia kamati zinazohusika, walishindwa kushiriki kwenye mkutano huo kutokana na kutojipanga mapema, jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa ili waweze kushiriki kwenye mikutano ijayo.

Amesema ushiriki wao ni muhimu katika kujenga uelewa wa mambo mbali mbali wanayowasilishwa na kujadiliwa katika ngazi ya kimataifa, na kuweza kuyaeleza na kuyatekeleza kwa wapia kura wao. Akizungumzia kuhusu mafanikio ya mkutano huo kwa Zanzibar, Mhe. Fatma Fereji amesema Zanzibar inaweza kunufaika na mkutano huo kutokana na nchi wanachama kuweka msisitizo wa ushirikishwa wa wadau kupitia makundi mnbali mbali yakiwemo ya wanawake, watu wenye ulemavu na taasisi zisizo za kiserikali.

Amesema kutokana na matokeo ya mkutano huo, serikali inafanya maandalizi  ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano huo, sambamba na kuwajengea uwezo wananchi ili wafahamu zaidi faida zitokanazo na ushiriki wa mkutano huo.

Mkutano huo uliojadili maazimio ya Rio ya mwaka 1992 mjini Rio de Janeiro Brazil, ulizishirikisha nchi mbali mbali duniani ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s