Makunduchi wataka Muungano wa mkataba

Tume ya marekebisho ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kukusanya maoni yake leo katika sehemu mbali mbali za Tanzania ambapo kwa upande wa zanzibar tume hiyo ilikuwa makunduchi mkoa wa kusini Unguja huku maoni tofauti yakiibuliwa

MCHAKATO wa kukukusanya maoni ya Katiba mpya nchini umeanza huku wananchi wakiwa na mawazo tofauti, na baadhi yao wakipendekeza Zanzibar iwe na mamlaka kamili. Maoni hayo yalitolewa jana katika eneo la Mzuri Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, ambako pia ilipendekezwa Muungano kati ya Tanzania uwe wa mkataba.

MCHAKATO wa kukukusanya maoni ya Katiba mpya nchini umeanza huku wananchi wakiwa na mawazo tofauti, na baadhi yao wakipendekeza Zanzibar iwe na mamlaka kamili.

Maoni hayo yalitolewa jana katika eneo la Mzuri Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, ambako pia ilipendekezwa Muungano kati ya Tanzania uwe wa mkataba. Pia baadhi ya wananchi waliwaeleza wajumbe wa Tume ya Katiba chini ya Mohammed Yussuf, wakitaka ziwepo Serikali mbili kama zilivyo sasa, huku wengine wakitaka Serikali tatu, yaani Tanganyika, Unguja na ya Kisiwa cha Pemba.

Mmoja wa wananchi hao alitaka Zanzibar iwe na mamlaka ndani na nje ya nchi, na iwe na uwezo wa kujiamulia mambo yake inavyotaka, huku akitoa mfano kuwa nchi hiyo imezuiwa kujiunga na Jumuiya ya Kislamu  (OIC) na Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa)

“Zanzibar ikiwa na Serikali yake na Tanganyika  Serikali yake, nchi mbili hizi kila moja itakuwa peke yake wala hazitaingiliana, na Muungano wetu utakuwa wa mkataba,” alisema mwananchi huyo. wajumbe 16 waliotoa maoni yao walitaka mfumo uliopo sasa uendelee lakini wakisisitiza kero za Muungano zitatuliwe.

Kwa upande wao, Hasan Ali Othman na Matona Masoud Issa, mbali na kutaka ziwepo Serikali za Tanganyika na Unguja, pia walieleza Pemba iwe na Serikali yake, na Muungao uwe kati ya Unguja na Tanganyika.

Pia baadhi ya wananchi walitaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania achaguliwe kwa awamu kwa kuachiana nafasi baina ya Bara na Visiwani. Vile vile wapo waliopendekeza Rais aendelee kuwa na mamlaka ya kuteuwa mawaziri, wakuu wa wilaya ,wakuu wa mikoa na kutaka kati ya viongozi wakuu wa kitaifa, yaani Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais mmoja wao awe mwanamke.

Baadhi ya watoa maoni walitaka kuwepo kwa makamu wawili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, moja awe Rais wa Zanzibar, kama ilivyowahi kuwa zamani. Wakitoa maoni yao katika eneo la Mtende wananchi wamekuwa na maoni mbali mbali huku wengine wakitaka mfumo uliopo uendelee na kuwepo na muungano wa mkataba na kila nchi ijiendeshe wenyewe na wapo waliotaka mfumo wa serikali tatu lakini pia wapo waliotaka mfumo wa serikali moja ili kumaliza matatizo ndani ya Muungano.

Katika mkutano huo baadhi ya wananchi wamewasilisha maoni yao kwa barua mbele ya wajumbe wa tume hiyo ambapo katika walioongea mmoja wapo alisema wananchi wengi wa Mtende wamekuwa na khofu kuongea lakini yeye anawasemea kwa niaba yao na kutaka serikali ya mfumo wa muungano wa mkataba na heshima ya rais wa Zanzibar irejeshwe pamoja na usawa na nafasi za ngazi za juu kama majeshi, usalama wa taifa na nafasi nyengine.

Abdallah Haji Ameir mkaazi wa Mtende yeye amependekeza kuwepo na serikali moja ili kuondosha matatizo ya muungano pamoja na kushauri chama chochote cha siasa kitakacholeta vurugu kifutwe hapa Zanzibar;

“Mimi napendekeza kuwepo na serikali moja tu maan haya yote yanayokuja haya yatakwisha na rais wa serikali moja awe anakaa miaka minane ikimaliza miaka minane basi aondoke na sio kila baada ya miaka mitano kunafanyika kw asababu hizi chaguzi ndio zenye kuleta matatizo” alisema Ameir.

Naye kwa upande wake Kidawa Harouna Jecha kutoka shehia ya Mtende yeye alisema anataka kuwepo na serikali ya muungano na serikali ya zanzibar ili kuwepo na bunge na baraza la wawakilishi na pia aliwasilisha maoni yake kwa barua.

Haji Makame Mussa yeye aliunga mkono wa serikali mbili na pia alisema wananchi wengine wanaona tabu kuongea kutokana na kuona aibu kuja mbele kuongea lakini wana maoni yao wanataka kuyatoa lakini alisema “Mimi naongea kwa niaba yao lakini wetu wanaona aibu kuja hapa usoni kuzungumza lakini wengi tunaunga mkono mfumo huu wa serikali mbili” alisema Jecha.

Wajumbe wengine wa Tume ya Katiba waliopo Zanzibar ni Dk Salim Ahmed Salim, Dk Sengendo Mvungi, Kibibi Mwinyi Hasan na Richard  Lyimo.

Advertisements

38 responses to “Makunduchi wataka Muungano wa mkataba

 1. Twambie basi dada wamesemaje huko tena twambie mmoja mmoja alivosema ili wakumuombea dua tumuombee na wakumuapiza tumuapize

 2. angalia watu wa tume walivyowachukua hawa watu wetu ambao wanawatumia vibaya kwa unyenyevu na unyonge walio nao , ili wafanikishe wanachotaka kwenye katiba feki, muungano hatuutaki , hio ndio message kwa majambazi ya tume , watafuteni wasomi halafu muwaulize nini mnawaonea hawa kina mama wanyonge kuwa mnasikiliza kumbe hewa tu , mnawadanganya wala hamuoni aibu wala vibaya nyinyi wanafiki

 3. Sasa jambo hili ndilo nilikuwa na wasiwasi nalo kabla hata haujaanza huo mchakato wa katiba, kuwa wananchi hawajaelimishwa maana au vipi kutoa maoni. Tume ishasema kama watu wakitoa maoni basi yatolewe na ufafanuzi, sio kwa jazba wala sio kusema tu. Ukisikiliza sauti ‘audio’ ya hao waloshiriki utangundua kuwa hawajui nini wanapaswa kufanywa.

 4. Muheshimiwa kidogo nimepata wasisi kutokana na haya maoni ya baruwa. Naona kama hii inaweza kuwa ni janja ya kutaka kucheza ule mchezo wa kata funuwa. Sisi tunatowa indhari maoni ya baruwa yanatutia wasiwasi. Tumeshaumwa na nyoka tokea 1995 na sasa tukiliona hili la maoni ya baruwa linatutisha. Tunaomba viongozi wa UAMSHO WASHUGHULIKIE HILI NA LIPATIWE UFUMBUZI UNAOFAA.

 5. Kwa upande wao, Hasan Ali Othman na Matona Masoud Issa, mbali na kutaka ziwepo Serikali za Tanganyika na Unguja, pia walieleza Pemba iwe na Serikali yake, na Muungao uwe kati ya Unguja na Tanganyika. Duh hapa ndio kwenye mtihani zaidi.

 6. Mchangiaji moja jana Mtende alionya kuwa hii inaweza kuwa janja tu kwani hapo nyuma ” tuliwahi kuambiwa tukatae Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Tukataa na Serikali ikaundwa;” alisema Mzee huyu.

 7. Haya ndiyo maoni ya baadhi ya ndugu zetu wa Makunduchi. Tumeyasikia jinsi yalivyokosa mwelekeo wa Zanzibar, ingawa wana uhuru wa kusema wanavyopenda. Inaoneshea wenzetu kwa kiasi kikubwa wameridhika na hali ilivyo. Sijuwi wasomi wetu wa Makunduchi wamefanya kazi gani mpaka kwa kiasi kikubwa umma wa Makunduchi ukakosa mwelekeo namna hii katika kuitetea Zanzibar. Kwa sasa nahisi umma wa Makunduchi unapotoshwa sana na wanasiasa ambao hawajali isipokuwa matumbo yao tu. Ndugu zetu, wasomi na wataalamu kutoka Makunduchi mna jukumu la kuuwelekeza umma namna ya kuitetea Zanzibar kwa maslahi ya Zanzibar yote au haya ndiyo kweli maoni yanayowakilisha watu wa Makunduchi. Nahisi kuwa hivi sasa tunaongozwa ni ushindani wa vyama na ukaidi, lakini mbele ya safari kama maoni yenu yatapita basi tutakuja lia na kujuta ambapo tutakuwa tumechelewa mno. Mola awawafikishe Wazanzibari kile chenye kheri nao duniani na akhera.

 8. Maoni ni haki ya kila mtu ila ni kwa nini unapotwambia Serikali 2 tuendelee nazo hutupi faida tukaelewa. Eee bwana muungano unaenda zake mara hii kwa uwezo wa ALLAH msishtuke hata MCHELE CHUWA lakini lengo letu sio CHUWA ni kupika wali. Watakuja kwenye wenye kujielewa tutawaeleza watafahamu

 9. uyu anaetaka serekali 3 tanganyika unguja na pemba sjui ni mfuu huyu kafufuka wakati asipojielewa au sijui kua ni zombee mana halina akili wala halina elimu wacha elimu ya shule hata ile elimu ya kijamii ya kujielewa mwenyewe na kutambua familia yke hana hawa ndo wale wanaotumiwa kutia chokochoko kw walimwende na watu kama hawa katika jamii wanajulikana wanaume kama mabintii wenzake karlos hawa
  mm sifikirii kama unaweza kumbagua muunguja na mpemba mana kama asilimia 99.9% wazanzibar ni waislamu basi asilimia hiyohiyo ndo waunguja na wapemba walivochanganya na ndo mana karne zote hizo hakukua na serekali ya unguja wla pemba serekali ilokuwepo ni zanzibar
  uyu jamaa aloongea hivi si mzanzibar huyo kaletwa ili atumiwe hapo machinga

 10. MAONI NI PINGU KUMBUKENI WAZANZIBARI WENZANGU ISIWE MNAFATA MKUMBO TU, FIKIRI ATHARI YA KILE UNACHOKITOLEA MAONI ATHARI ZAKE KWA MIAKA 20 MBELE NA KIZAZI CHAKO KITAKUJA KUISHI JE ? FIKIRI KABLA YA KUTOA MAONI.

 11. JAMANI JITOKEZENI KWA WINGI KATIKA KUTOA MAONI YENU KWA MASLAHI YA ZANZIBARI YETU, MSIPOKWENDA WATAAMUA WANAVYOTAKA JUU YA NCHI YETU JAMANI HAO, TUSIKUBALI KUSEMEWA NA WACHACHE WASIOTUTAKIA MEMA NA NCHI YETU ADHEIM.

 12. ENYI WANAJAMII WA MKOA WA KUSINI UNGUJA MNANINI NYIE? MBONA MNASEMA VITU AMBAVYO HAVIPO, NANI KASEMA PEMBA SI SEHEMU YA ZANZIBAR ACHENI USIASA NDUGU ZANGU TUOKOE NCHI YETU YA ZANZIBARI ILISHAZAMA BADO KIDOGO TU. HIVYO HAMJUI KUWA ZANZIBAR NI KITOVU CHA WANACHUONI, MASHEIKH NA MAWALII SASA IKOWAPI ZANZIBAR ILE SIO PEMBA ILE NI ZANZIBAR, TUSHIKAMANE KUILINDA NA KUITETEA ZANZIBAR IWE HURU JAMANI KWA UMOJA WETU.

 13. DR. SALIM, HAKIKISHA UCHAKACHUAJI HAUCHUKUI NAFASI WALA VISHAWISHI WAKATI WA KUKUSANYA MAONI YA RAIA, HIYO NI DHIMA UMEBEBA WAZANZIBARI WAKOMACHO, KUWA MAKINI.

 14. ama kweli unafikiri salimu hemedi salimu yupo kwa ajili ya waznz? huyu ni adui mkubwa wa waznz kama hujui na kipenzi cha watanganyika ndio maana kapewa hii kazi ya kuwatoa mhanga waznz , japokuwa umri wake anakaribia kwa mungu lakini haoni anaangalia maslahi ya kidunia ngoja arejeshe namba ndipo atakiona cha mtema kuni kama anavyokiona babaake mwl nyerere huko kaburini, daktari salimu hemedi salimu kumbuka kufa kwaja , rekebisha na utubie kwa mola kabla ya kufika kwake, na njia ya kutubu ni rahisi waznz hawataki muungano , ukifanya vinginevyo kumbuka nimekuonya usije kusema hukukumbushwa .

 15. haya yamepanga zamani ili izame zanzibar me naona bora tupigane kue hakuna cha kiongozi ala tume ya maoni kama omali hakuna atomkalia mtu kimabavu.na titoteeeeeeeeeeeeeeeeeeee, lakini muungano hatuuutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

 16. Hamwachakaaaa? Kwanza jibuni halafu Ndio tujuwe serikali ngapi?
  Kuna aloutaka muungano kuliko sheikh Almarhum Hassan bin Ameir na Mwishowe yamemkuta ya kufukuzwa Tanganyika, basi nanyi hamkusoma tu, mungu akamleta na Marhemu Maalim Idirisa Abdulwakil kukutanabahisheni naye yamemkuta, halal mara tatu sasa subirini na haya , msije lia na mtu.

 17. pemba ndio wabaguzi ndiomaana. hawa ndio watu wenye akili nyingi za kuzaliwa wamenena sana Hasan Ali Othman, na Matona Masoud Issa, mbali na kutaka ziwepo Serikali zaTanganyika na Unguja, pia Pemba iwe na Serikali yake, na Muungao uwe kati ya Unguja na Tanganyika. hapa patamu nawaunga mkono

  • usiwe mpuuzi, nawe umekuwa kama hujasoma, au ndio wale vibaraka vya kikoloni, acha tabia ya kuchochea utabaka, usiasa, na uvisiwa. Kama hivyo mbana zanzibar inaongozwa na serikali ya umoja wa kitaifa au hulijui hilo, kama hulijui uliza usiwe na kiherehere alimradi nawe uandikwe tu kwenye computa.

   • kama imekukere ndio utajua ninyi ndio mmeanzisha utabaka na ninakwambia tunasubiri tu tusikie mbara mwenzetu kaumizwa au kauwawa huku kwetu wapemba ni wengi sana nasi tutalianzisha muunguja tutamwacha tutadili tu nawapemba maana ndio wabaguzi warangi. Maana tunandugu zetu huko zanzibar wanatuambia wamebaguliwa kila wakipita kejeli kila wakienda kejeli ss tunawasubiri huo ubaguzi wenu uanze

  • Anna kuwa na akili hebu njoo huku zanzibar kisha ufanye utafiti wapi wapo watanganyika wengi kati ya unguja na Pemba. ukweli ni hivi Watanganyika wanyonge wengi wako Pemba mashambani hao wenye mdom ni wachache na wapo Unguja. UNGUJA NI UNGUZA kama mtu ameshindwa kuishi BARIADI atawezaje kuishi unguja? utaunga mkono kitu usichokijua. WAPEMBA SI WABAGUZI NDIO MAANA WAPO WENGI HUKO KWENU hebu nenda ukafanye utafiti kwanza.

   LAKINI TATIZO NI NYINYI MNAOWAGAWA WAZANZIBARI KWA FAIDA ZENU BINAFSI MPATE MTAWANYE UOVU MMEONA KUWAONEA WATU WA PWANI HAITOSHI NDO SASA MNATAKA MUTUGAWE. zungumza hoja usijaze utumbo weweee

   • SS KWA TAARIFA YAKO MM NIKO ZANZIBAR NA NINAYAONA TENA SIKO MBALI NAISHI HASWA KUNAKO WAPEMBA NIPO DARAJA BOVU

 18. mimi nilikuwa ni mmoja wa watu wanaohudhuria mihadhara ya uamsho na kuwaunga mkono lakini kila siku zinavyozidi naona bado tuko na mahasidi wengi hapa zanzibar wasiojijua wanafanya nini na wanataka nini katika nchi yetu tokea nilipoanza kusikia watu wa kusini wanavyotoa maoni yao na wengine kupeleka barua hatujui wameandika kitu gani…..basi naomba mungu bora sote tuikose zanzibar iwe serikali moja imezwe na watanganyika halafu baada ya miaka 25 ijayo nina uhakika kutakuwa hakuna mzanzibari halisi hata mmoja atakae baki Zanzibar itakuwa na watanganyika na wazungu watupu angalau hizi chokochoko za mie muunguja na wewe mpemba zitakwisha kabisa…..kama ilivyofanya mombasa na wakenya……mijitu haina akili kila wanavyotaka kusaidiwa kuikomboa Zanzibar wao ndio kwanza wamelala fofo…..bye bye Zanzibar

 19. ww anna nikuambie kua wapemba sio wabaguzi usilolijua ni usiku wa kiza waulize hao ndugu zako kw nini wanasema wanabaguliwa hao ndugu zako wakiwa huku wanajipendekeza kw wazenji kuwata kimapenz dini haituruhusu na msitulazimishe kuwapenda hatuwataki we jingalieni na mjipime na swala kumpiga mpemba naona utajisimbu ungepigana na tumbo lako kwanza mpemba yuko bara lakini hauzi dawa ya mende wala kukunguni na hizo bidha na uzuri wa biashara niwapemba ndo wanaowachangamsha nyie
  inavooneka hata historia ya kwenu huijui upo upo tu wafuata mkumbo ata ukiona watu wavua chupi na ww utavua bila hata ya kujua sababu ya kuvuliwa chupi

  • ww nakulinganisha na taira au kichaa anayewataka nyie kimapenzi ninani ninyi ni sawasawa na mabasha. ss kwa taarifa yako wapemba mtarudi kwenu wabaguzi wakubwa nyie ss kwani wazawa wa unguja hawawataki unguja na wanataka ninyi wapemba muo na serikali yenu? hapo ndio ujue kuwa wapemba wanamatatizo. hata sisi muungano hatuutaki

   • @ anna
    Wewe anna inaonyesha wazi nyinyi watanganyika mlivyokua mafisadi na wenye roho mbaya. Hamuwezi hata kuficha ubaya wenu hata kwa dakika moja, wakati watu wanadai muungano huu wakifisadi mliotuletea kwa roho zenu mbaya uvunjike kwa amani na kila upande uwende kivyake wewe unatuletea maoni yako ya kikafiri na kibaguzi. Huyo aliedai Pemba iwe na serikali yake si muunguja huyo ni kichogo kama wewe na ndio wanaotia fitina kati ya waunguja na wapembe.

   • Ama kweli hasira ya mkizi furaha kwa mvuvi. Mtu anae wapendelea waunguja mema hawezi kabisa kujaribu kuwabagua na Wapemba. Anaejaribu kufanya hivyo bilashaka atakua anatumia sera za kikoloni (devide and rule policy) ili kuwatawala watu. Sisi kwa sasa tuko macho hakuna ataeweza kutubagua kama ilivyokuwa zamani. Anna wewe ni msaliti kwasababu unadai hamuutaki muungano wakati wenziwako wanaung’ang’ania na kama wewe huutaki muuungano mbona unawaunga mkono waunguja ili wawabague wapemba kisha wao(waunguja) waendelee kujiunganisha na watanganyika? huo utakua si muungano? Anna Usitutoe kwenye mada yetu ya msingi ya kua Wazanzibari kwa umoja wetu hatuutaki MUUNGANO.

   • WAZAWA WA UNGUJA NDO NANI WANAOSEMA WAPEMBA WARUDI KWAO NI WATANGANYIKA WALIOKIVAMIA KISIWA KAMA CHAO MBONA HATUJASIKIA WAPEMBA WAKIWAMBIA WAUNGUJA WARUDI KWAO KTUKA PEMBA. HAP KUNA KITU MNACHOKITENGENEZA ILA HAMTAWEZA KWA UWEZO WA ALLAH. KWA TAARIFA HAKUNA MZANZIBARI HATA MMOJA AMBAYE HAJAHUSU SEHEMU ZOTE MBILI ZA VISIWA ASIYE NA BIBI UNGJA YUKO PEMBA MJOMBA UNGUJA. MBONA NYIE MMEJAZANA DARESALAAM ILHALI MNJUWA KUWA SIO KWENU TANGULINI MZARAMU KUITWA ANNA. WEWE NA WENZAKO MBONA MNANG’ANG’ANIA DAR KAMA KWENU NANYI RUDINI KWENU. NA SIS TUTAUNGA MKONO HOJA YA WAISLAMU WA BARAZA KUU LA KUGAWANA MIKOA TUONE KAMA MTAWEZA KUISHI HUKO MAPORINI. TANGA DAR PWANI YOTE SI MIKOA YENU NYINYI NI WAVAMIZI MNAO KIMBIA KWENU NA KULETA FITINA KWENYE MIKOA YA WATU. ONA MNAVYOJIDHALILISHA TANGU LINI BINAADAMU MWENYE AKIL AKACHUKIA KUTAJIWA KWAO. ZANZIBAR OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.

    HATUUTAKI MUUUUUUNGANOOOO HATUA YA MWANZOI HATUA YA PILI TUTASHIRIKIANA NA WAISLAMU WA TANGANYIKA KUREJESHEWA HAKI ZAO IKIWEMO MIKOA YAO TAJIRI DAR, PWANI TANGA TABORA, ARUSHA N.K NENDENI MKAVAE PEDOOO HUKO PORINI.

  • Tatizo la Kusini yote ni kuwa watu wamekuwa woga sana. na wala hawtaki kukubali maoni ya mageuzi. Mimi nahisi kama ingewezekana Pemba kuwa na utaifa wake ki kweli na roho safi basi hata ulaya wangetaka kuungana na wapemba kwa sababu ni watu FLEXIBLE. na wanaojali utu na thamani ya mwanadamu. W apemba hawaweki mbele upemba wao bali mafanikikio yao hapa duniani na akhera. Na ndio maana hata ukienda nje ya Pemba utawakuta wamejiimarisha kama vilkle pale ninpao.

   • vile vile ss wabara hatuutaki muungano kwa sababu muhimu kwanza. tunaitaka tanganyika yetu, pili vilevile wazanzibar walioshikilia madaraka au ngazi huku tanganyika warudi kwao ili watanganika wapate madaka na kila mtu akaingoze nchi yake, nne kuzarauliwa na kukejeliwa tumechoka kila ukipita huku zanzibar wakishajua ww ni mbara na ubaguzi zanzibar umeshaanza haswa kwa wabara wenzangu, bungeni tunawataka watanganyika tu ambao wanajua umuhimu wa nchi yetu na kuitetea jamii yetu ya kitanganyika na nitafurahi sana muungano ukivunjwa kila mtu arudi kwao.

   • Unaposema kila mtu arudi kwao utakao unakosea. hao wazanzibari wanaoshiklia madaraka SMT hawapo kwa niaba ya zanzibar bali ni aina fulani ya kuwaneemesha wachache ili wengine waendelee kuumia. Kama unafahamu historia rudi nyuma katika historia ya Senegal kipindi cha ASSIMILATION POLICY. Ufaransa ilijaribu kuwahonga baadhi ya wasenegal ili kuendelea kuitawala Senegal na wako wasenegal walioshikilia madaraka ndani ya serikali ya senegali kama LEOPARD SENG’HO. Muungano tunaoukataa wazanzibari ni ule wa dhulma wa serikali moja kuhodhi madarka muhimu ya nchi nyengine yenye historia kubwa duniani.
    Zanzibar na wazanzibari ni watu wenye utamaduni wa kuingiliana na watu na mataifa yote duniani. ukienda London utawakuta wazanzibari na mitaa yao usiseme huko bara kwenu.

    ISHU SIO KILA MTU KURUDI KWAO ISHU NI KILA MTU KUHESHIMU MAMLAKA YA MTU MWENGINE. THATS IS OUR DEMAND

   • idd ckiliza mm ninajisikia hasira kusika wabara wenzangu waliopo huko zanzibar wananyanyasika kwa sababu moja mzanzibar akishajua ww ni mtanganyika lugha za kejeli mara wawaite machogo, mara muungano hatuutaki, mnang’ang’ania zanzibar kwenu bara ni wamaskini haswa wanawake ndio wanapatatabu kama kweli zanzibar ni nchi inayoendeshwa kidemokrasia mbona wabara hawana uhuru wa kujiamulia utamwambiaje mtu avae dira au majabu wakati mtu hajazoea na tangu azaliwe hajawahi kuvaa mbona wazanzibar waliopo huku bara hatuwaambiii wavae pedo, suruali, au watembee vichwani bila kujifunika?. alafu ikitizama bara wazanzibar ni wengi sana na hakuna anayewanyanyasa wala kuwabagua tunaishi kama ndugu iweje wabara waliopo hko kunyanyasika mfano hao wanaofanya kazi kwa mahoteli wanapotoka au kuingi manyumbani vijana huvamia na kuwanyang’anya walichonacho na kuwaambia zanzibar mtaikimbia tu hatakama hamtaki. na ukimchukulia hatua hakuna chochote atakachofanywa. ss kwanini kila mtu asirudi kwao wakati ubaguzi umeanza mapema? mm upande wangu kwa hali hii ya ubaguzi ulioanza ni bora kila mtu arudi kwao kwa sababu muungano ukishavujwa hakuna atakae ishi kwa nchi ya mwenzie kwa amani.

   • Anna nimekuelewa na mimi nahisi umenielewa tatizo lako kama ulivyosema una hasira. hakuna sehemu dunia hii pasipo na ubaguzi kama wewe umeshuhudia wazanzibari wakiwabaguwa watangayika mimi nimeishi Shy tabora na hata dodoma na huko kote nimeshuhudia wazanzibar wakibaguliwa. Ila wanaofanyan haya ni wachache kam ilivyo kwa hapa zanzibar. Nakubali na nakuomba nawe ukubali wazanzibari wamefanyiwa fadhila nyingi na watanganyika kama ilivyo kwa watanganyika pia kufadhiliwa na wazanzibari. Mimi binafsi nimesaidiwa na mtanganyika sehemu ambayo nilikuwa nakabiliwa na hatari kubwa baada ya gari yangu kubata ajali katikati ya pori la Itigi na Tabora. lakini pia kama nilivyotangulia huko nyuma kuwa faida ya zanzibar huru itawaneemesha hata watangayika. Nimeingia shinyanga nikakodi nyumba ila kijijini kwetu Pemba tuna wanyantunzu wamepewa nyumba bure na kila msimu uishapo huondoka. sasa kinachotakiwa na wazanzibari ni ZANZIBAR HURU hakuna binaadamu mwenye akili aliyekuwa tayari kuendelea kuwa Mtumwa. Zanzibar tumekuwa watumwa wa tanganyika kwa muda mrefu sasa tumechoka.
    Kuhusu kivazi hilo ni suala la kiimani kama untakumbuka vizuri mwanzoni mwa miaka ya 2000 daresalaam kulitokea maandamno mkubwa ya waislamu waliokuwa wakipinga sheri ya ugaidi. katika maandamano hayo mwandishi mmoja wa TVT alipigwa na vyombo kuvunjwa huku wahusika wakidai kuwa alikuwa havaa vizuri wakikusudia kiislamu.

    Kule ufaransa ilipitishwa sheria ya kupinga vazi la Hijabu. HUKO mbali tuje hapa hapa Tanzania katika mji wa Tabora wanafunzi waislamu wanaovaa hijabu bila kujali kuwa wametoka wapi wnadhalilishwa na wengine kuvuliwa.
    Mwaka 2007 au 2008. mtoto wa mufti wa Tanzania sheikh Simba alipinga amri ya kuvaa tai juu ya hijaab katika skuli ya UHURU SHINYANGA. suala lile lilfika hadi kwa rais na kijan yule akjuilikana tanzania nzima hebu angalia inawezekana vipi kuvaa tai juu ya hijaab. najuwa utashangaa haya ukweli ni kwamba hata vyombo vya habari vinachangia kuficha ukweli fulani na kuibua uongo fulani.

    GHASIA ZA HIVI JUZI NIPASHE BAAADA YA KUKOSA UONGO WA PICHA WAKACHUKUWA PICHA YA MOROGORO WAKASEMA NI GHASIA ZA ZANZIBAR LAKINI WALIPOFUATWA WALISEMA WAMEKOSEA. ANGALIA KOSA HILO HILO LIKAFANYWA TA TANZANIA DAIMA BILA KUOMBA RADHI. SHIDA NI KWAMBA WATANGANYIKA MMEHODHI KILA KITU NA MNASEMA KILA MTAKACHO SISI TUKISEMA TWAAMBIWA WABAGUZI. MBONA TUNDU LISSU HASAKAMWI WAKATI ANASEMA MANENO MBAYA ZAIDI YA HAYA YETU KUFIKA HADI KUSEMA ZANZIBAR WAMESHA VUNJA MUUNGANO MATAMU HAYOOOO. KUWA MUELEWA USIWE MTAWALIWA. SAMAHANI KWA MAKLA NDEFU

    Kama wapo wazanzibari wenye chuki na wtanganyika bila ya wao kufanyiwa uovu watakuwa wanafanya dhambi na hawkubaliki.

    HOJA: TUNATAKA ZANZIBAR HURU YENYE MAMLAKA YAKE SUALA LA MTU MMOJA MMOJA LITAFUATA BAADAE.
    ANNA TUSAIDIE TUIPATE ZANZIBAR YETU NA NITAKUALIKA KWENYE SHEREHE YA KUSHEREHEKEA UHURU WA ZANZIBAR Inshallah

 20. a.alaikum.Jamani Wanzanzibar tuweni macho tusing’ang’anie CCM na CUF kwanza tuekeni maslahi ya taifa letu mbele kisha mengine yatafuata fuata baada.Au si tulikubali UMOJA WA KITAIFA ili tuwe na msimamo na kauli moja? au?. Watanganyika wametunyonya sana tuzinduke tudai haki na heshima ya taifa letu.Wao hawa hawana akili waache wafuge mapishi ya NYERERE.Kusema eti wataomkesea heshima mungu wao Nyerere kuna haja gani yakuendelea kuishi na kuungana na watu wasio hata mawazo?
  Jamani hii ndio fusra ya ukombozi wetu,TOKA KWA MKOLONI MTANGANYIKA NA MFUMO WAO WA KANISA KATOLIKI.Hebu oneni ujinga wa NECTA kuhusu elimu ya Tanzania wanaichakachua na juzi tu wameadhirika.
  KERO KUBWA ZA UKOLONI WA MUUNGANO NI:-
  * KATIBA MBOVU
  *MAPATO NA UTMIAJI WA RASILIMALI
  *ELIMU
  *KUINGIA MIKATABA
  *AINA YENYEWE YA MUUNGANO
  Mwisho sisi ni 1.something kwa nini watung’ang’anie lazima kuna jambo watufanyia. Na kama hatuutaki muungano tukatae upuuzi wao wa SENSA maana wataka waujue idadi watumalize nge hao,walafi wasio na nia njema na sisi

 21. Hawa watakusanya maoni lakini ni bure 2.Me naamini hayatafanyiwa kazi tukitaka kujua hilo tungojee pale itakapoamuliwa utaona 2 ndio mana wengine hawatak kuchangia mana wanaona bure wengine washaona mbali hao

 22. SASA HAPA SI SUALA LA UAMSHO WALA CHAMA CHA SIASA BALI NI VYEMA VIONGOZI KUWACHA KUWALAZIMISHA WAPIGA KURA WAO KUFUATA MAONI YAO. BALI NI VYEMA KILA MZANZIBARI KUWA HURU KUITETEA ZANZIBAR. HATA HAO WA MAKUNDUCHI NAO WANGEPENDA KUWA NA TAIFA LILILO HURU THE PROBLEM IS WANAOGOPA VIONGOZI WAO. HII NI KWA SABABU WAMEZOEA KUPEWA FADHILA FULANI FULANI. WAKUMBUKE KUWA ZANZIBAR HURU ITAWANUFAISHA WATU WOTE HATA HAO WATANGANYIKA. KWANI NI WASUKUMA WANGAPI WANAKUJA KUCHUMA KARAFUU ZNZ? NA MSIMU UKIISHA HAOOOOOOO SHY AU MWANZA. ZANZIBAR HURU INAWEZEKANA TAUCHE WOGA.

 23. Ndugu zangu wamakunduchi.
  Sijakusudia wamakunduchi wote bali wale waliotoa maoni yao kutaka pemba iwe na serikali yao mbali,sasa nasema wamefikiri sana suali hilo au wamekurupuka nalo tu bila mizani?
  Bila pemba zanzibar imejimaliza na baada ya muda mfupi tu mabadiliko yataonekana.
  Kama walichonacho unguja na pemba wanacho lakini baadhi ya walichonacho pemba unguja hawana.
  1,Karafuu ambazo ni uti wa mgongo wa taifa hili
  2.Mafuta ambayo yanatarajiwa kuchimbwa na ndio mvutano mkubwa na bara.
  3.Sehemu kubwa ya ardhi yenye rutba.
  Kwa uchache yaliyobakia yote ambayo unguja wanayo na pemba wanayo lakini ole wetu mambo mawili ya mwanzo yakikosekana kuchangia katika uchumi wa unguja itakuwa tumejimaliza .
  Kama ni utalii basi pemba utalii utaimarika zaidi ya unguja.
  Kwa hiyo tusiwe wajinga wa kukurupuka kichuki na bila ya kuwa na sababu za kimsingi kutaka kujigawa huyu nani na yule nani.
  Tokea uanze ulimwengu visiwa hivi ni vimoja na kama uwezo wa kuviunganisha na kukifanya kisiwa kimoja bila kupanda meli tungelifanya hivyo na wenye maradhi ya chuki kwa wapemba wakapata maradhi ya kuwamaliza.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s