Uamsho ni sawa na waamsha daku

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume, akiwahutubia Wanachama wa CCM wa Jimbo la Rahaleo katika ukumbi wa Tawi la CCM Gulioni

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Amani Abeid Karume amewafananisha Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI) kuwa sawa na waamsha daku wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kuwataka Wana CCM kubakia na misimamo yao katika suala la Muungano.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika Jimbo la Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Dk Karume alisema kwamba CCM haijalala hivyo wanachama wa CCM hawana sababu ya kuwa na hofu na Uamsho kwani wao hawakulala na wenye kuamshwa ni wale waliolala.

“Kwani nyie mmelala mpaka muamshwe, nyie mko macho eti…hao ni kama wale wanaoamsha daku utakasirika, lakini ukiamka unasema ahaa kumbe muda wa kula daku tena hofu ya nini” Alisema Dk Karume na kuwachekesha waliohudhuria mkutano huo.

Makamu huyo Mwenyekiti alilazimika kutoa maelezo hayo baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja, Borafia Silima Juma kueleza wasiwasi wa wanachama wa CCM kuhusu vurugu zilizotokea mwezi Mei mwaka huu na harakati kundi la Uamsho.

Dk Karume akijibu hilo, alisema juhudi za kuiweka Zanzibar katika hali ya maelewano ilifanywa na Jumuiya za Kimataifa na Mataifa kutoka nje, lakini hawakuweza kusuluhisha migororo ya kisiasa iliyodumu kwa takriban miongo mitatu, lakini baada ya Wazanzibari wenyewe kuamua kuacha tofauti zao maridhiano yalifikiwa mwaka 2009.

Akitoa historia feru na miafaka na maridhiano Dk Karume alisema wakati wa utawala wake walihakikisha kabla ya kumaliza kipindi cha utawala wake anaiwacha Zanzibar ikiwa salama, yenye umoja na mshikamano na isiyokuwa ya vipande vipande ambapo hali hiyo ilifanikishwa baada ya kufikiwa kwa maridhiano ya kisiasa baina ya Chama ch Wananchi(CUF) na Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Mimi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad tulikutana Ikulu na kukazungumza kwa nini kumaliza tofauti zetu maana sisi sote ni wamoja na leo mafanikio yake ndio haya ya Zanzibar imetulia kwa hivyo natoa wito wa kuendeleza umoja huu” Alisema Dk. Karume.

Akizungumzia suala la maoni kuhusu Muungano, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM alisema watu wote wanaotoa maoni kimsingi wanatumia haki ya kikatiba na kidemokrasia hivyo wana CCM wanachotakiwa ni kuendelea kusimamia azma ya ujenzi wa chama chao huku wakiendelea kuheshimu misimamo yao bila ya kuyumbishwa.

Dk Karume alisema hoja ya Muungano wako baadhi ya watu amewasikia wakitaka Muungano uendelee, wengine wakishauri ufanyiwe marekebisho na mabadiliko huku wengine wakitaka uvunjike.
“Msipatwe na homa, ondoeni hofu na wasiwasi , waacheni masheikh wajibishane na masheikh wenzao na sisi wanasiasa tutafute majibu mjarab yatakayofaa ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha vijana wetu kutambua mahali tulikotoka, tulipo sasa na kule tuendako”Alisema.

Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alitamka bayana kuwa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi njia pekee ni kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura ili kushinda katika kila uchaguzi na si kinyume chake.

Mkutano huo uliofanyika katika Tawi la Gulioni ambako alizungumza na wanachama wa matawi mawili la Gulioni na Mwembeladu ni wanachama wachache waliohudhuria tofauti na matarajio ya watu wengi ambapo kuliwekwa mabomba nje ya tawi hilo lakini wasikilizaji walikuwa kidogo mno.

Viongozi walioambatana na Dk Karume ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Yussuf Mohammed, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mjini Borafya Silima, Mbunge wa Rahaleo,  Abdallah Juma Abdallah (Maabodi), na Mwakilishi wake Salim Nassor (Aljazira), Mwakilishi wa Chumbuni Machano Othman Said, Isa Haji Gavu Mwakilishi wa kuteuliwa, Mussa Perera Silima mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM. na wanachama wachache wa chama hicho.

Advertisements

15 responses to “Uamsho ni sawa na waamsha daku

 1. “Msipatwe na homa, ondoeni hofu na wasiwasi , waacheni masheikh wajibishane na masheikh wenzao na sisi wanasiasa tutafute majibu mjarab yatakayofaa ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha vijana wetu kutambua mahali tulikotoka, tulipo sasa na kule tuendako”

  Nadhani hili la kutafuta majibu mujarab na hoja za kuutetea muungano, ndio tatizo kuu la wana CCM.Uongozi wa CCM Zanzibar umeshindwa kutetea na kutoa hoja za kuendelea na muungano bila ya kutuonesha faida zilizopo au zilizopatikana katika kipindi chote cha muungano.Badala yake wanaamua kutisha na kutumia vyombo vya dola kuleta vurugu…..Vurugu ni dalili za mtu kushindwa na hoja

 2. Big up Dr. karume maana mifano yako mimi huwa inanimaliza “hao ni kama wale wanaoamsha daku utakasirika,lakini ukiamka unasema ahaa kumbe muda wa kula daku” maana yake hata kama utakasirishwa sababu ya uhafidhina wa kiccm lakini utambue kuwa unapaswa uamke kwa ajili ya jambo muhimu sana “SOVEREIGN ZANZIBAR” Heko Uamsho kwa kazi kubwa mliyoifanya!

 3. Angalau ‘option’ ya Karume ya kutojibishana na uamsho naiafiki, nadhani Borafya alitaka Karume atukane na kutoa mbovu kwa uamsho kama afanyavyo yeye, ila hili la watu wanaotoa maoni kuheshimiwa nakubaliana na Karume kuwa ni haki ya kikatiba na hivyo iheshimiwe…kama katiba inasema muungano unaweza kuvunjika kwanini wenye maoni ya kuuvunja wasiyatowe!

 4. Dr. Karume sina shaka na ww tokea zamani ila ss umeidhihirisha CCM kwmb na ww UMEAMKA. Hongera ila ningeomba ukae na baadhi ya CCM wenzako ili uwaelekeze kwmb muhimu ni ZANZIBAR kwanza. Kama BORAFYA una hofu na hujui la kusema bac sema hivi “mm Mzanzibar nataka mamlaka ya nchi yangu Zanzibar kimataifa na heshma ya Rais wangu kimataifa na heshma ya nchi kimataifa” ukimaliza hayo bila kupoteza mda unaweza kushuka au kama unataka kutia mbwembwe unaweza kuendelea” usihofu ndugu ytu ww ila MBISHI kidogo lakini afadhali kwmb unaelewa. Naamini unaipenda ZANZIBAR bila shaka.
  Wow ss borafya uzalendo kwnza mungu ampe nguvu.

 5. MWENYE MACHO NAAONE! NAONA KUNA MWANGAZA KIDOGO! NAONA KWA MBALI JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR! MUAMSHA DAKU NI MTU MWEMA… MASHEKHE WAJIBIZANE NA MASHEKHE MUME FAHAMU? KEEP IT UP WEWE MZALENDO WA KWELI? BALOZI UMEFAHAMU? SALMA TUWEKEE VIDIO TUMEONE USO WAKE ALIVYOKUWA AKIONGEA!

 6. Asante Dr. K maneno yako ni sawa sawa. Nadhani hawa wasifahamu ni bora ulivyowafahamisha. Tunakotoka tulikuwa na Zanzibar yenye mamlaka kamili ya kidola. Tulikuwa na pesa yetu na heshima yetu kimataifa. Tulipo sasa hatuna mamlaka ya kidola raisi wetu ni sawa na waziri tu katika muungano. Tunakokwenda ni kufutwa SMZ na Zanzibar kuwa ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania. Eee jamani CCM ZANZIBAR UJITI NA MACHO TAHADHARINI. Acheni siasa Teteeni Zanzibar. Kuweni wazalendo. Zanzibar huru kwanza. Heko UAMSHO KWA KUAMSHA WALIOLALA LAKINI ENDELEENI KUAMSHA KUNA WENGINE WAMELALA FOFOFO. Nakupa big up Dr. KARUME NAJUWA UNAUCHUNGU WA ZANZIBAR NA INAKUUMA. Inshallah karibu TUTAACHIWA TUPUMUWE.

 7. Kwanini Borafya anawasiwasi tunajua original hatoki hapa lakini sasa hatutizami nani katoka wapi muhimu ni mzanzibari sishangai kutoka mpia beni hadi alipofika akapelekwa kwenye vyoo vya flashi kwenye mikutano ya watu ni kubwa hilo kwake, na mpiga beni atazungumza nini mbele za wenyekusikiliza na kusikia maneno ya ukweli, wenye ubongo wenye kupambanua mambo ni kweli wameamshwa na kama si hao waamsha daku basi Ramadhani ingewakatikia njiani, si ingekua hasara ? lakini sasa wameamka na watafunga na fungu watapata , Dr katumia lugha ya ndani tu lakini kakusudia watu wamefaidika, thumb up!!!

 8. Ahsante Dk.Karume kwa ujumbe wako mwanana ambao kwa kila mwenye akili haitaji kuuliza nini ulikua unamaanisha. Borafya alitaka karume atukane lakini mwenzake anaijua zanzibar na wapi wazanzibar wanataka kwenda. big up my ex president. mungu akupe moyo huo huo,
  unanimaliza kwa mafumbo yako mzee,mana yale mazimwi ya ccm yasioelewa hapo umeyamaliza.
  mungu akueke uishuhudie zanzibar ikipata uhuru wake wa kweeeliii

 9. Huyo Borafia kazoea matusi tuu, sasa leo kaaibika mbele ya bosi wake maana Karume ameuwelewa Uamsho vzuri sana.

  • Mzeee katumia maneno ya hekma kwa wale wenye akili hambiwi tizama jamani acheni kuwa wabishii huyu mzee anatamani sana kuwa znz huru tuwe makini jamani tuitete kwanza znz yetu vyamaa bdaee eeeeeeeeeeeeeee

 10. Hongera Dr Karume ulichokisema kila Mzanzibari mwenye uchungu na nchi yake amekuelewa. Maneno yako ni juu ya mstari na umesaidia sana kuendeleza kazi iliyoanzwa na uamsho kwa wale ambao wanaonekana ni wazito wa kufahamu mambo. Kama wana akili timamu nadhani wamekufahamu vyema bosi wao. Hongera Dr Karume wewe kweli ni mmoja kati ya wenye uchungu na Zanzibar na hili hukulianza leo. Polisi maneno mazima ya ex president mmeyasikia au bado mna uchu wa kuwapiga mabomu uamsho huku mkiachia majambazi yakituua kwa risasi?

 11. CCM wilaya ya Mjini Borafya Silima jamani huyu borafiya gani sio huyu pidofile au kwa jina jengine kitangi alorejeshwa nchi ya uk baada ya kutumikia kifungo chake ?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s