Choo cha madawa ya kulevya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliagiza kukamilishwa mara moja kwa Choo Maalum kwa ajili ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Kitengo cha kuzuia Dawa haramu za kulevya Mrakibu Msaidizi Muandamizi wa Polisi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdulla Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Abdullhabib Fereji.

Advertisements

3 responses to “Choo cha madawa ya kulevya

 1. Ni vizuri kupata choo hiki katika Uwanja wa Ndege. Wakati huu tukisherekea kupata choo inabidi polisi waangalie namna gani watashughulikia watu wauzao hizi dawa katika maeneo ya Jangombe Uwanja Wa Taifa, Jangombe Wawi Bakery, Jangombe kwa Loffy, Jangombe Wayani na maeneo yote. Jangombe ambayo imebarikiwa kwa utumiaji wa dawa tunamuomba mtusaidie kwa kuwa shida hizi si kwa Watumiaji zinazagaa hadi majumbani mwa watu hata wasiotumia. Mkadamu nakujua ulivyo mzuri katika kazi zako, fanya kweli ili historia ikukumbuke si kwa kuangalia vyoo vya vya watumiaji wa madawa bali kwa kuzuia au kuondosha kabisa utumiaji wa wa madawa. Tukiendelea kupuuuza watumiaji, idadi yao itaongezeka na matokea haya tuyatarijie:

  1. Zanzibar kugeuka Colombia, Mexico au kama taifa jengine ambalo Serikali tayari zimeshindwa na magenge ya watumiaji wa Madawa. Dalili hizi tayari zipo na mtu asiejua aende Uwanja wa Taifa Jamgombe aone Wakaazi wa hapo wanavyoshindwa kuwadhibiti watumiaji wa madawa ya kulevya,
  2. Uchumi wa Zanzibar utadhibitiwa na waendesha biashara ya Mihadharati. Katika hali hii Siasa nayo pia itaathirika kwa kuwa leo siasa ni pesa.
  3. Kizazi cha Zanzibar kitageuka kuwa zezeta na watakaorithi generation ya waangalia vyoo hawatajua isipokuwa kubwia unga. Wakati huu ukifika nchi iliyopatikana kwa kumwaga damu itauzwa kwa kete chache za unga. Watoto wa Ibni Kinana na Ibni Khuzaimah ambao walizaliwa iliwatawale watakuwa na hali ngumu kwa kuwa itabidi wachague kati cha jiwe gumu na kisu chenye ncha.

  Chonde Chonde kina Kinanah au Kuzaimah kwa kuwa hali hii itakuwa mbaya kuliko haya yanayoendelea hivi sasa

 2. hiki kiini macho , yeye huyo sefu idi anawajuwa wote wanaoleta madawa ya kulevya na wasambazaji , wanakula pamoja msijidanye hii ni kuwahadaa wananchi, majambazi ndio wanaotutawala CCM ( chama cha majambazi ) , na kubwa la maadui ni yeye sefu iddi na msaidizi wake mwamedi abudu ambao wamewekwa na watanganyika kumlinda rais sheni na sefu sharifu wasifurukute

 3. Mimi naona, Madaw ni gonjwa sugu. Wafadhili wakubwa wa CCM ndio wakuu wa mihadharati.Lazima viongozi waweke mguu chini na iwe FULL STOP kwa mihadharati. Hatuwezi kuendelea kuona vijana wetu wanaharibika namna hii. Vijana wetu wengi wanapoteza ujana wao kwa janga hili na UKIMWI. Viongozi wetu, tunawaomba mukaombe msaada marekani waje waifanye kazi maana kama ni nyinyi wenyewe, kazi hamuiwezi. Mulipewa majina ya wauza na walataji unga na mumeogopa kuwakabili. wapeni nafasi FBI waje waifanye kazi musiogope. Kama hamujui vya kufanya tujulisheni tutakwenda kuomba kwa niaba ya wazanzibari.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s