Walemavu wengi hawana ajira serikalini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji akitoa taarifa rasmi ya serikali kuhusiana na maadhimisho ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayofikia kilele chake tarehe 26/06/2012 kila mwaka

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imekiri kukabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa ajira za watu wenye walemavu nchini. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Abdulhabib Ferej wakati akijibu masuala ya wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Chukwani Mjini Zanzibar.

Waziri huyo alisema bado suala la ajira kwa watu wenye ulamavu ni changamoto kubwa inayoikabili serikali.
“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikiri mbele ya wajumbe wa baraza hili tukufu kwamba suala la ajira kwa watu wenye ulemavu ni changamoto kubwa katika taifa hili” alisema.

Alisema katika kuona watu wenye ulemavu wanapata ajira, tayari ofisi yake ishawashasilisha ofisi ya rais, utumishi wa umma na utawala bora taarifa ya wale ambao kwa njia moja au nyengine wenye sifa na wataweza kuajiriwa katika wizara za serikali.

Awali katika suala lake la msingi Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF) Mwanajuma Faki Mdachi alitaka kujua wizara ina mpango gani wa makusudi wa kuwaajiri watu wenye ulamavu kutokana na kuwepo kwa malalamiko kuwa hawapewi ajira serikalini licha ya kuwa na sifa zitahiki.

Waziri Fatma alisema suala hilo linafanyiwa kazi ili watu wenye ulemavu wapatiwe ajira kulingana na alimu zao.

Akijibu suala la utekelezaji huo iwapo umeshaanza katika wizara ngapi Fatma alisema katika kipindi hiki itakuwa ni vigumu kupata idadi halisi ya wizara ngapi zimeshatekeleza agizo hilo la kuwaajiri.

“Naomba kupitia baraza lako tukufu kushirikiana na ofisi ya rais na utumishi wa umma na utawala bora kuliangalia tena suala hili ili kujua hali halisi ya ajira kwa watu wenye ulemavu katika wizara za serikali” alisema Waziri huyo.

Akijibu masuala ya nyongeza juu ya kuwashughulikia na kuwapatia vigari watu wenye ulemavu, Waziri Fatma alisema suala hilo ingawa serikali haina fedha za kutosha lakini tayari imetenga katika bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2012/2013 ili kuwapatia vifaa watu wenye ulamavu.

“Mheshimiwa mwenyekiti sitaki ku priemty bajeti yangu lakini kwa ufupi tu naweza kusema kwamba katika bajeti ya mwaka huu wa fedha tumetenga fungu kwa ajili ya vifaa vya watu wenye ulamavu ingawa sio kubwa lakini litasaidia kulinga na hali zetu na huku tunaendelea na kutafuta wafadhili wa kutusaidia katika kuwaendeleza watu wenye ulemavu …ni yetu ni kuwasaidia kwa hivyo tunategemea tutafanikiwa” aliahidi mbele ya wajumbe wa baraza hilo.

Advertisements

One response to “Walemavu wengi hawana ajira serikalini

  1. TUKIPA NCHI YETU INSHALLAH WOTE WATAPATA AJIRA tena watfanya kazi katika mazingira mazuri rais wetu mpendwa dr shein atachagua hadi mabalozi wa nje walemavu kitu muhimu ni JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA. WATUWACHEEEEE TUPUMUEEEEEEEEEEEEEEE.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s