Hoja ya Muungano yaifunika baraza

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin kushoto kibadilishana Mawazo na Mwakilishi wa Kuteuliwa Asha Bakari Makame nje ya Ukumbi baraza la Wawakilishi huko Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.

SUALA la Muungano limezidi kutawala mijadala katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huku baadhi ya wajumbe wakitamka wazi kuwa hawataki Muungano. Katika kikao hicho ambacho tayari kimepitisha bajeti kuu ya serikali ya Zanzibar wajumbe wa baraza hilo jana walijadili bajeti ya ofisi ya makamo wa pili wa rais wakitaka serikali isimamie kupata uhuru zaidi wa kiuchumi katika muungano.

Ofisi ya makamo wa pili wa rais ndio inayotambulika kuwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali ndani ya baraza la wawakilishi.

“Mheshimiwa Naibu Spika mimi niseme wazi kwanza kwamba sitaki muungano na katika kitu ambacho nakichukia sana basi ni huu muungano maana kwa miaka 48 ya muungano huu kila siku tunaambiwa kuna kero wala hazitatuliwi basi ni uvunjike tu” alisema Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma.

Juma alisema kupigania haki ya Zanzibar haimaanishi chuki katika muungano na kwamba muungano uliyopo ni wa nchi mbili huru ambazo lazima kuwepo na haki sawa kwa pande zote mbili.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk alisema “Lazima mheshimiwa makamo wa pili wa rais tuamke muungano huu, siwo…tunataka maslahi ya Zanzibar na tunataka haki zetu zote kuanzia mapato ya gesi. Nitazuwia bajeti hii mpaka niambiwe katika accounti ya Zanzibar imepata kiasi gani kwa mapato ynayotokana na gesi maana ni haki yetu” alisema Mbarouk.

Abdallah Juma Abdallah Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) alisema viongozi wa serikali na vyama wamewekwa madarakani na wananchi hivyo sio sahihi kubeza maoni ya wananchi ambayo hawautaki mfumo huu wa muungano na kuahidi kusimama pamoja na wananchi wa jimbo lake iwapo waamua kuukataa.

“Kiongozi yeyote kuanzia rais, wabunge na hata sisi wawakilishi tumewekwa hapa kwa kuchaguliwa na wananchi na tunasimama kuwasilisha maoni ya wananchi sasa ikiwa wananchi watasema hawataki muungano, mheshimiwa naibu spika lazima tusimame nao” alisema Mwakilishi huyo na kuongeza.

“ Mimi kama mwakilishi wa chonga nasema wananchi kama watasema hawataki muungano basi nitasimama nao na nitakuwa bega kwa bega na kwa sababu wamenichagua kwa kuniamini na pia nahitaji tena kurudi katika nafasi hii na nikidharau maoni yao au matakwa nayo hawatanirejesha tena” alisema Abdallah.

Mwakilishi wa nafasi za wanawake Asha Bakari Makame (CCM) kwa upande wake aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kutoka CCM na CUF kwamba wanadhamana kubwa ya kuwatetea wazanzibari bila ya kuhofia nafasi zao na kwamba wazanzibari wanawatazama wao kwa kuwaamini.
“Mheshimiwa naibu spika ni CCM na CUF pekee tuliyopo humu ndani wananchi wanatuamini na lazima turejesha imani kwa wananchi wetu ikiwemo suala kuu la kutetea Zanzibar ndani ya muungano…kero gani hizi zisizokwisha?” alihoji Asha ambaye aliwahi kuwa waziri wakati wa SMZ .

Asha Bakari ambaye ni naibu mwenyekiti wa umoja wa CCM Tanzania (UWT) alisema ni umoja na mshikamano miongoni mwa wazanzibari ndio silaha pekee itakayoweza kuwavusha wazanzibari katika kudai maslahi yao ndnai ya muungano.

“Mimi siogopi chochote na kwa umri huu tena naona lolote litakalonifika ni sawa tu lakini nawaambia wenzangu kwamba tuiteteni Zanzibar na tusiwe na woga maana wengine wamezowea kututisha” alisema kwa kutoa tahadhari.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alisema serikali ya Zanzibar inafanya makosa makubwa ya kuridhia kila kitu ambacho kinatolewa na serikali ya muungano.
“Ni muda mrefu wimbo ndio huo huo wa ahadi ya kushughulikia kero za muungano na kero zenyewe hazishi …kwa sababu hata hizo kamati hazipo kisheria za kutatua kero” alisema.

Jussa alitaka viongozi wa serikali kuwaunga mkono wananchi katika madai yao ya msingi kwa kuwaelekeza nini waseme wakati wa kutoa maoni ya katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwamba bila ya kutoa muongozo wananchi watababaika.

“Mimi nina imani kubwa na serikali yangu ya umoja wa kitaifa na ninaipenda lakini naomba itoe msimamo hapa katika kuwaelekeza wananchi wakadai nini wakati wa tume itakapokuja kukusanya maoni” alisema Jussa na kupigiwa makofi na wajumbe wenzake.

Aidha mwakilishi huyo aliwataka wananchi na viongozi wa siasa kutokuchanganya misimamo ya siasa pamoja na dini katika kutoa maoni kwani inaweza kuharibu na kuwagawa wazanzibari.

Awali akiwasilisha hutuba ya bajeti ya makamo wa pili ya kuomba kuidhinishiwa shilingi billioni 12.3 kwa mwaka wa fedha za 2012/2013 Waziri wa nchi Ofisi hiyo Mohammed Aboud Mohammed alisema juhudi zimekuwa zikiendelea katika kutatua kero za muungano na kwamba wajumbe wa baraza la wawakilishi wawe wavumilivu.

MWISHO

UJENZI WA BANDARI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itatumia kiasi cha dola za kimarekani 400 millioni kwa ajili ya mradi wa bandari ya Mpigarudi Visiwani Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Gavu alipokuwa akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyetaka kujua mradi wa ujenzi huo utagharimu kiasi gari cha fedha.

“Kwa gharama ambazo zinakisiwa kulingana na ‘concept paper’ ya wizara, mradi huu usingeweza kuzidi USD$ 400 millioni.” alisema Naibu Waziri Alisema hata hivyo kwa vile gharama hizo zilikisiwa miaka mitano iliyopita ingewezekana akuweka ongezeko la asilimia 10% ambapo mradi usingezidi dola za kimarekani millioni mia tano. (USD$ 500).

Akijibu suali la la fedha hizo zitatokea wapi na zina masharto gani, Gavu alisema fedha hizo hazijapatikana na hivyo masharti ya fedha yasingeweza kupatikana vile vile.

Awali Jussa alitaka kujua bandari hiyo iliyokusudiwa kujengwa ambayo ni ya kisasa pendekezo hilo limefanyiwa kazi kwa kiasi gani na limefikia hatua gani, ambapo Naibu Waziri alisema ni ya ujenzi huo upo na serikali inaendelea na mchakato wake.

Akizungumzia pendekezo hilo Naibu alisema linaendelea kufanyiwa kazi na kwa sasa serikali imeshakamilisha upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya CRB- ya China.

Naibu huyo aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba baada ya kuipitia wataalamu wameona bei iliyopendekezwa na kampuni hiyo ni millioni 800 fedha za kimarekani.

“Millioni 800 ni nyingi sana na hiyo bado serikali imo katika kutafuta njia mbadala ya kufanikisha suala hili” alisema Naibu waziri huyo.

Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba licha ya baadhi ya wajumbe wameonesha wasiwasi wao juu ya kampuni ya kichina lakini bado serikali ina matumaini na ufanyaji wa kazi ya kampuni hiyo kwa mujibu wa mkataba waliofunga.

“Mheshimiwa mwenyekiti haina maana kwa kuwa kampuni moja ya kichina imefanya vibaya na hii itakuwa imefanya vibaya kwa zile kampuni ambazo zimefanya vibaya za kichina ni nyengine lakini hii ni nyengine na bado serikali ina matumaini ya kufanya kazi yetu vizuri” alisisitiza naibu huyo.

MWISHO

UKOSEFU WA WALIMU YA SAYANSI

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekiri kuwepo kwa uhaba wa walimu wa sayansi katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Zahra Ali Hamad aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kufuatia suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua ni sababu gani zinazochangia kuwepo kwa uhaba wa walimu wa sayansi nchini.

Zahra alisema uhaba wa walimu wa sayansi katika skuli za Unguja na Pemba unatokana na wanafunzi wengi kutofaulu masomo ya sayansi katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita na hivyo kupelekea vijana wachache wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya ualimu kwa masomo ya sayansi.

Akijibu suali la kwa nini wizara ya elimu imeshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo Zahra alisema “Ni kweli waheshimiwa wajumbe wizara iliahidi kulipatia ufumbuzi suala hili lakini ufumbuzi huo hauwezekani kupatikana mara moja na inahitaji muda wa kuweza kulitatua tatizo la upungufu huo”.

Alisema wizara imepata vibali vya uajiri wa walimu wapya katika mwezi wa Aprili 2012, amabpo wizara iliajiri walimu 197 wenye shahada na stashahada mbali mbali wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi.

Katika mwezi wa juni 2012 alisema wizara imepata kibali chengine cha uajiri wa walimu 111 wenye shahada na stashahada za ualimu wakiwemo walimu 48 wenye shahada ya kwanza ya masomo ya masomo ya sayansi.

Naibu waziri huyo alisema kukosekana kwa walimu hao kunaweza kuchangia katika kushindwa kwa wanafunzi kufnaya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita.

Aidha kushindwa kwa wanafunzi hao pia kunachingiwa na wanafunzi kutopendelea kusoma masomo ya sayansi kwa dhana ya kuwa ni masomo magumu au wanafunzi huliogopa somo la hisabati ambalo ndilo somo la msingi.

“Ni kweli skuli ya Muyuni na skuli nyengine zina uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi. Uhaba huu unatokana na wanafunzi wengi kushindwa kufaulu masomo yao na kujiunga na vyuo vikuu” alisema Naibu huyo.

Zahra alisema wengi wa waombaji wa mafunzo ya ualimu wamefaulu katika masomo ya sanaa kuliko sayansi na hivyo masomo ya sayansi hukosa walimu na tatizo hilo ni sio kwa skuli za zanzibar peke yake bali ni Tanzania nzima.

Hata hivyo alisema wizara imeandaa mafunzo ya ualimu kazini kwa walimu wasio na sifa za kufundisha masomo ya sayansi ili kuinua uwezo wao na hatimae waweze kudumu kuyafundisha masomo hayo.

Akizungumzia mikakati ya wizara yake katika kuhakikisha tatizo hilo linapungua Naibu Waziri alisema mpango wa wizara yake ni kuajiri vijana waliomaliza kidato cha sita na kufaulu masomo ya sayansi ili kusaidia kupunguza uhaba wa walimu wa sayansi.

 

Advertisements

19 responses to “Hoja ya Muungano yaifunika baraza

 1. Inafurahisha kuona Wawakilishi wanasoma alama za wakati. Wakubwa katika Muungano ni lazima wabebe lawama kwa kushindwa kwao kuwa wakweli kuhusu Muungano huu.

  • naam hili la lawama kwa wakuu wa muungano bila mjadala lazima walikubali, kama wao waonavyo kuwa kuna kero zamuungano kwa muda wa nusu karne wameshindwa kulitatua, hakuna sababu isipokuwa ni dharau tu. mimi binafsi kama mwanachi wa Zanzibar. nalitupia lawama hili kwa serikali yangu ya umoja wa kitaifa, lazima walitatue….lazima…..wakuu wa Muungano si wakuaminika! jee nanyie mtabaki kuridhia kila wanalolisema kama walivyoridhia serikali za awamu zilizopia?

 2. hutuuuuutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, muuungano mctubabaihe hakuna cha kero wala nini

 3. mimi naungana na yoyote anae ukataa muungano hata awe nani na wawakilishi wamejitahidi kidogo lakini bado wanatakiwa wote waweke msimamo mmoja isipokuwa mimi simuelewi huyu Asha Bakari kwenye mikutano ya sisiemu huwalaani wanaokataa Muunguno barazani anawaunga mkono sijui ana msimamo gani!!!!

  • Sasa ndo umemuelewa.! Ukweli na yeye hautaki. Kwani wewe ukiwa usingizini kipindi cha ramadhani usiku wa manane, mara akaja mtu akakuuliza kua unataka DAKU, unamjibu kua hutaki Daku. Lakini baada ya kuamka hassa na kuona kweli sahani inatoa mvuke, si unatamka kua Daku unalitaka bali huthibitisha kwa vitendo hassa kwa kujipanga wa mwanzo kutaka kula….Lakini hio huja baada ya kuamka. Kwa hio ucshangae kuona Mh, Asha Bakari kwa mcmamo wake alokua nao akiwa kwenye mkutano wa CCM. Wala ucmhukumu hata kumlaani, kwani alikua ucngizini. Saivi ndo ameshaamka wacha aseme lililo sahihi na linalokubalika kimantiki Coz saivi ndo yuko macho kwa kuamshwa na Hakika ameamka, na kweli inaleta faraja kuona ana ucngizi mwepesi kuamka mapema, ila bado wapo wenye ucngizi mzito.
   Nilishawahi kusoma makala inayosema kua “INGEKUA UAMSHO WANANISIKILIZA MIMI, BASI NINGESEMA HII MIHADHARA BASI INATOSHA” Lakini mi naamini haitoshi wala hakuna sababu ya kurudi nyuma. Mi naamini kua bado wapo wenye ucngizi mzito tuwaombee Mungu wazidi kuamka kwa wito wa UAMSHO. Na nampongeza Mh. Asha Bakari kwa kua makini, kushtuka mapema, na natumai kwa kupitia kwake wataAmka wengine………..UAMSHO hakuna kurudi nyuma, kazi yenu inalipa, wala hakuna wa kuwalipa zaidi ya Allaah, na matunda yake ndio hayo, na maua yanachanua, coz naamini bado matunda mengine yatakuja.

   • Al’Rumhy Suleyman (Mkoroshoni)
    Sasa ndo umemuelewa.! Ukweli na yeye hautaki. Kwani wewe ukiwa usingizini kipindi cha ramadhani usiku wa manane, mara akaja mtu akakuuliza kua unataka DAKU, unamjibu kua hutaki Daku. Lakini baada ya kuamka hassa na kuona kweli sahani inatoa mvuke, si unatamka kua Daku unalitaka bali huthibitisha kwa vitendo hassa kwa kujipanga wa mwanzo kutaka kula….Lakini hio huja baada ya kuamka. Kwa hio ucshangae kuona Mh, Asha Bakari kwa mcmamo wake alokua nao akiwa kwenye mkutano wa CCM. Wala ucmhukumu hata kumlaani, kwani alikua ucngizini. Saivi ndo ameshaamka wacha aseme lililo sahihi na linalokubalika kimantiki Coz saivi ndo yuko macho kwa kuamshwa na Hakika ameamka, na kweli inaleta faraja kuona ana ucngizi mwepesi kuamka mapema, ila bado wapo wenye ucngizi mzito.
    Nilishawahi kusoma makala inayosema kua “INGEKUA UAMSHO WANANISIKILIZA MIMI, BASI NINGESEMA HII MIHADHARA BASI INATOSHA” Lakini mi naamini haitoshi wala hakuna sababu ya kurudi nyuma. Mi naamini kua bado wapo wenye ucngizi mzito tuwaombee Mungu wazidi kuamka kwa wito wa UAMSHO. Na nampongeza Mh. Asha Bakari kwa kua makini, kushtuka mapema, na natumai kwa kupitia kwake wataAmka wengine………..UAMSHO hakuna kurudi nyuma, kazi yenu inalipa, wala hakuna wa kuwalipa zaidi ya Allaah, na matunda yake ndio hayo, na maua yanachanua, coz naamini bado matunda mengine yatakuja.

 4. Pingback: Hoja ya Muungano yaifunika baraza·

 5. Tunaamini kwmb kwa uwezo wa ALLAH, DHULMA hii ya MUUNGANO mara bac. Ila kuna baadhi ya WAAKILISHI bado wanajifanya hawaja elewa ila BECAREFUL WHEN THÊ TIME COME katu hautuwaachi mara hii. Nyinyi mnaojifanya hamuwelewi tunaamini mtakuja tu kutaka KURA hapo ndio mtaelewa kwa VITENDO kabisa. Lakin mm binafsi nina matumaini makubwa kwmb mara hii tunatoka bila wacwac. Hata TWINES wanatofautiana ingawa walitoka sehemu moja itakuwa wawakilishi waliotoka sehemu tofauti hali wakiwa na tabia tofauti.

 6. Pamoja na yote inasikitisha sana kuwasikia Wawakilishi wengine wakihusisha Wapemba na kukataliwa kwa Muungano. Hawa jamaa hasa wale waliopanda hadi walipo kwa kadi za Chama inabidi waelweshwe kuwa ni kuvunja Katiba kumbagua mtu ama moja kwa moja au kwa njia nyengine yoyote ile. Maneno yao inabidi wayachunge ili Wapemba walioko Bara wasifanywe ndio maadui wa Tanzania. Mimi ningekuwa Barazani ningewapa Waheshimiwa Wawakilishi Communication Skill Course wakati wanaingia. Hii ingewasaidia kutofautisha kikao rasmi na kijiweni na pia wangejua namna ya kutumia lugha.

  • Al’Rumhy Suleyman (Mkoroshoni)
   Hawa wanaoOngelea uPemba na uUnguja mi nashindwa hata kuwaelewa. Manake hata kama ndo kweli ingekua waPemba ndio wanaokataa Muungano, ilistahiki wao ndio wawaone hao wapemba ndio wakombozi wao kwa kuwatetea nchi yao ya Unguja ipumue, ili na wao waonje neema ya Unguja yao.. Manake wao hukaa wakiandika pale Maskani ya KACHORORA kariakoo “MUUNGANO HUU NI WA TANGANYIKA NA UNGUJA, NYINYI WAPEMBA HAUWAHUSU” Pengine wanazo hoja, mimi siwezi kuwalaumu, lakini Hivi kweli hawa wana akili? Japo ingekua kweli Muungano ni wa Tanganyika na Unguja, Hawajiskii kua ni Wajinga kua wameungana na Wenzao halafu kila kitu katika Muungano kikawa kinaangukia upande wa pili. Kwa mfano: Katika Muungano utakuta (Rais wa Muungano) anatoka Tanganyika. (Waziri wa Afrika mashariki) anatoka Tanganyika. (Gavana wa Fedha) anatoka Tanaganyika. (Waziri Mkuu) anatoka Tanganyika. (Jaji Mkuu) anatoka Tanganyika. (Waziri wa mambo ya nje) anatoka Tanganyika. (Spika wa Bunge) anatoka Tanganyika. (Naibu Spika) anatoka Tanganyika. (Msajili wa vyama) anatoka Tanganyika. (Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi) anatoka Tanganyika. (Mkuu wa jeshi) anatoka Tanganyika. (Mkuu wa Polisi) anatoka Tanganyika. (Mkuu wa usalama) anatoka Tanganyika. (Mkuu wa uhamiaji) anatoka Tanganyika. (Mkuu wa Necta) anatoka Tanganyika. (Katibu Mkuu wa CCM) anatoka Tanganyika. (Viwanda) Tanganyika. (Makampuni) Tanganyika. (Balozi za umoja wa Mataifa) Tanganyika.
   Kwa kweli ni mcba usiokadirika. Manake la kusikitisha zaidi, mwisho huandika “MUUNGANO UDUMU DAIMA” Wenzao wa KISONGE washaerevuka wamekaa kimya kuona hatma ya Zanzibar yao, coz na wao pia wana uchungu na nchi yao kwa kuyapoteza yote hayo. Mwisho namalizia kufahamisha kua huu Muungano unawakera WaUnguja na WaPemba, na wote hao ndio wanaopigania kutaka waachiwe “WAPUMUE”
   Nami nawakilisha na kuwasilisha.

 7. nd jussa mbona unaegeka jiwe, sisi hatutaki masuala ya kutoa maoni kuhusu katiba , hivi nyie viziwi hatutaki muungano , suala la katiba halipo tenaaaaaaaaa , eleweni nyie vipofu wenye macho lakini hamuoni ,

 8. Bado baadhi ya watu wanaofaidika na muungano wanaendelea kuutetea,na wanakuja na maneno yale yale kua kero zitatatuliwa, hawa ndio wale wanaojali maslahi yao na kuitelekeza zanzibar. mimi niko moshi nasoma ila naskia uchungu jamani wenzetu hawa wanavotudharau, hua nabishana nao mpaka husikia kutaka kulia. natamani miaka yangu ya kusoma iishe nirudi home zenji.mana nimechoka, wenzetu wamejazwa kasumba mbovu kuhusu zanzibar, napata wakati mgumu kuzirekebisha. na hapa ndipo walipotufikisha viongozi wetu, tunaonekana maskini tusionapahala pakuenda, hatuna vyuo vya kusoma, hatuna bodi ya mikopo, n.k.
  ila naamini ipo siku sio mbali haya yataisha, na hizi dharau zao zakuona wao ndio tunawategemea kwa kila kitu zitafika mwisho. ewe mola tusaidie na utuwepesishie kuiokomboa znz yetu. aaamin

 9. “When foolish laugh it doesn’t means a happiness”
  WATAKE WASITAKE MUUNGANO ZANZIBAR. Ukisema WAPEMBA ndio hawataki MUUNGANO pia ni sahihi lakini uwe na kumbukumbu za KITAALUMA kwmb neno ZANZIBAR lina maana ya UNGUJA na PEMBA kitaaluma. Kimackani kama wanavyodai watu wengine ni sawa. Lakini pia tujaalie na hapa UNGUJA wapo wachache ambao hawataki MUUNGANO je hawa Waunguja wachache hawana haki ya KISIKILIZWA kama watu wa MUUNGANO wa upande wa pili? Tafadhali ndugu waakilishi nijibuni bac ili tujue. Msitushuhulishe ikiwa hamjui kitu nyamazeni mtapata THAWABU nyinyi waakilishi MATUMBO. Hakuna ktk sheria zote mbili ya bara na znz sehemu inayosema kwa watu WACHACHE hawana haki ya kusikilizwa. Acheni kuwatofautisha watu ikiwa unahic wengi wao wanautaka MUUNGANO ss nn kinakukausha mdomo wakati ilikuwa tu utusaidie kupigania kupitishwa KURA YA MAONI watu tuulizwe tutajibu utapata MUUNGANO wako safi kabisa.
  “When the foolish laugh it doesn’t means happiness”

 10. ivi wanaoinanga pemba wakasema muungano ni tanganyika na unguja muungano huo uliwekwa na kutiwa saini na mama yake pamoja na nyerere wakiwa kitandani, mana mm ninavojua na ninavoona wa2 wanagombania kukombolewa zanzibar kutoka kw mkoloni mweusi na sio unguja sasa yeye anaesema muungano ni uunguja na tanganyika mama yake alikuwa malaya wa nyerere, akinvulia nguo kitandani kumridhisha nyerere kamwambia hivo kua huo ndo muungano wetu
  mm sijawahi kusikia kama kuna nchi ya unguja wala pemba sijaona mm katika historia
  nawambia hivi nyie mlokuwa hamna la kusema tafadhalini wala la maana ya kuuonge mnajifanya watoto katafuteni maziwa ya mama enu mkanyonye si ni watoto nyie hamjua lipini lipi ramadhani inakuja musitake kutufanya ramadhani yetu yende kombo

 11. HILI LA KUTUMIA LUGHA ZA UPEMBA NA UUNGUJA LINAFANYWA MAKUSUDI ILI KUTUGAWA TUACHE KUPAMBANA NA ADUI MUUNGANO. KWA HILI WAMEFELI HAKUNA KURUDI NYUMA MPAKA KIELEWEKE. TUACHENI TUPUMUE.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s