Sote tupige vita madawa ya kulevya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, akipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (kushoto) Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji (wa pili kushoto) wakati walipkuwana katika hafla ya chakula cha jioni, iliyoandaliwa na Rais wa Brazil,….kwa viongozi waliohudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) uliomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Rio de Jeneiro, nchini Brazil.

Tukiwa katika harakati za maadhimisho haya wengi wetu kwa njia moja au nyengine tumeguswa na athari za matokeo ya matumizi ya dawa za kulevya , tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya nchini linadhihirishwa na ongezeko la vijana waliojitumbukuzi katika matumizi hayo ambao wamekuwa wakifika katika vituo mbali mbali na kuhitaji huduma. Matumizi ya dawa za kwa njia ya kujidunga sindani imekuwa ni tishio na chanzo cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na maradhi mengine mbali mbali yanayopatika kwa njia ya damu ( blood borne infections). Hali hii imepekela vijana wengi nchini wanaotumia dawa za kulevya kuambukwiza ugonjwa wa UKIMWI. Utafiti uliofanywa mwaka 2005 hapa Zanzibar ulionyesha hali ya kutisha ya maambukizi hayo iliyofikia asilimia ishirini na nane ( 28%) kwa wanaojidungu na kubadilishana sindano

TAARIFA MAALUM YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MHE. FATMA A. FEREJ KWA WANANCHI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UPIGAJI VITA MATUMIZI NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA DUNIANI- 25/06/2012

Ndugu Wananchi

Mabibi na Mabwana

Assallam Alleykum,
Awali ya yote ni wajibu wetu kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kwa kutujaalia uhai na uzima siku hii adhimu ya leo . Aidha napenda nichukue nafasi pia kwa niaba yenu kumuomba Mola atupe na sisi pia Rehema na Baraka zake katika maisha yetu yote na nchi yetu kuendelea kuwa na amani, utulivu na masikilizano – AMIN

Ndugu Wananchi

Kama ilivyo kawaida yetu leo kwa mara nyengine tena nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya Jamii ya Kimataifa inaungana na mataifa mengine Duniani katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya.
Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Duniani (International Day Against Drug Abuse and Illicit Trafficking) huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Juni Duniani kote na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Dawa za Kulevya na Uhalifu ( United Nations Office on Drugs and Crimes – UNODC).
Ndugu Wananchi
Siku hii adhimu imeasisiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly) mnamo mwaka 1987 na huwa ni ukumbusho kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na Jamii ya Kimataifa kwa ujumla juu ya azimio lenye lengo la kuwa na jamii iliyositirika na kuwa huru na matumizi ya mihadharati.
Harakati za maadhimisho ya siku hii hulenga zaidi katika kuongeza uelewa na kuishajihisha jamii kufahamu mafanikio na changamoto zinazoikabili dunia juu ya tatizo la dawa za kulevya na kuandaa mikakati mbali mbali katika kukabiliana nalo.

Ndugu Wananchi
Maadhimisho haya huja na kauli mbiu au ujumbe mahsusi ambao huwa dira katika ufanikishaji wa shughuli mbali mbali zenye mnasaba na siku hii adhimu. Ujumbe wa Mwaka Huu “ Tujenge Jamii Yenye Afya Bila ya Dawa za Dawa za Kulevya” ( Global Action – Healthy Communities Without Drugs) unalenga zaidi katika kuhamasisha kuwepo kwa misingi mizuri ya kijamii yenye afya njema na ushiriki wa sekta nyengine mbali mbali katika kukabiliana na janga la dawa za kulevya. Ujumbe unazidi kutanabahisha kwamba licha ya changamoto zinazoikabili dunia kwa hivi sasa juu ya janga hili, misingi thabiti na imara ya kijamii, kifamilia na ushiriki wa sekta mbali mbali una nafasi muhimu na ya kipekee katika kuleta mabadiliko na kukabiliana kikamilifu na janga hili.
Taarifa ya taasisi ya Umoja wa Mataafa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu inaonyesha kwamba watu karibu millioni mia mbili na kumi (210,000,000) hutumia dawa haramu za kulevya duniani kote , matumizi ya dawa hizo huwaacha karibu watu laki mbili (200,000) wakipoteza maisha kila mwaka. Aidha matumizi na usafirishaji wa dawa hizo yamekuwa si tishio kwa afya za watumiaji pekee bali pia ni tishio kwa amani, usalama, ustawi wa jamii na maendeleo kwa ujumla kwa mataifa duniani kote.
Ndugu Wananchi
Tukiwa katika harakati za maadhimisho haya wengi wetu kwa njia moja au nyengine tumeguswa na athari za matokeo ya matumizi ya dawa za kulevya , tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya nchini linadhihirishwa na ongezeko la vijana waliojitumbukuzi katika matumizi hayo ambao wamekuwa wakifika katika vituo mbali mbali na kuhitaji huduma. Matumizi ya dawa za kwa njia ya kujidunga sindani imekuwa ni tishio na chanzo cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na maradhi mengine mbali mbali yanayopatika kwa njia ya damu ( blood borne infections). Hali hii imepekela vijana wengi nchini wanaotumia dawa za kulevya kuambukwiza ugonjwa wa UKIMWI. Utafiti uliofanywa mwaka 2005 hapa Zanzibar ulionyesha hali ya kutisha ya maambukizi hayo iliyofikia asilimia ishirini na nane ( 28%) kwa wanaojidungu na kubadilishana sindano
Ndugu Wananchi
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya iliyopewa masuala mtambuka ikiwemo hili la mapambano dhidi ya dawa za kulevya imetoa msukumo mkubwa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini. Baadhi ya maeneo ambayo yameweza kutekelezwa ni: –
a) Kufanya mapitio ya Sheria ya Udhibtiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar ( Sheria Nam 9,2009) iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi.
b) Mafunzo juu ya dawa za kulevya kwa wadau mbali ikiwemo Vyuo vya Mafunzo, Mahkama, na Taasisi za dini.
c) Kuendeleza programu maalum za kuwafikia watumiaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao ( outreach work), taaluma kwa jamii kupitia vyombo mbali mbali na pia huduma za ushauri nasaha kwa wateja.
d) Msukumo mkubwa katika uanzishwaji wa huduma za makaazi za marekebisho za kuacha matumizi ya dawa za kulevya maarufu Sober Houses.
e) Ruzuku kwa ajili ya uendelezaji wa huduma za marekebisho kwa vijana wanaoacha matumizi ya dawa za kulevya. Jumla ya nyumba tisa zimepatiwa ruzuku hiyo Unguja na Pemba.
f) Utoaji wa taaluma kwa watendaji wanaotoa huduma katika makaazi hayo ya nyumba za marekebisho.
NduguWananchi Ni jambo la faraja kuona kwamba kuanzishwa kwa huduma za makaazi kwa vijana wanaoacha matumizi ya dawa za kulevya (SOBER HOUSES) zinazoendeshwa na taasisi zisizo za kiserikali zimeonyesha mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Katika kipindi cha Julai 2011 hadi Machi 2012 jumla ya vijana 501 tayari wameweza kupata huduma kupitia nyumba hizo Unguja na Pemba.

Ndugu Wananchi

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais iliyopewa dhamana ya uratibu na udhibiti wa dawa za kulevya itaendelea kutoa kila aina ya msukumo kwa taasisi zisizo za kiserikali ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Ndugu Wananchi
Tunaendelea kushuhudia mwamko wa ukuaji wa huduma na juhudi za vijana wanaotumia dawa ya kulevya kutaka kujikwamua na janga hilo, juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.
Aidha, jamii inapaswa kuunga mkono harakati za vita dhidi ya dawa za kulevya nchini na taasisi zilizopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria zinapaswa kufanya kazi zake kwa makini na kwa uadilifu mkubwa .
Ndugu Wananchi
Kwa niaba yenu naomba nichukue nafasi hii kulipongeza tena Jeshi la Polisi kwa nadharia iliyobuni ya Ulinzi Shirikishi ambayo imeonyesha mafanikio makubwa katika baadhi ya shehia . Kumekuwa na mifano mizuri ya shehia ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuchukua juhudi za makusudi za kukabiliana na vitendo visivyoendana na maadili ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, juhudi hizo zinapaswa kupongezwa.
Ndugu Wananchi
Napenda kutoa wito kwa shehia na jamii kwa ujumla kuona kwamba wakati umefika sasa wa mafanikio hayo kuigwa katika shehia na maeneo mengine ili kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini.

“ZANZIBAR BILA YA DAWA YA KULEVYA INAWEZEKANA”

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s