Tutashiriki mchakato wa katiba – Uamsho

Sheikh Farid Hadi Ahmed akitoa msimamo wa Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) juu ya kushiriki katika Mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa hapo juu na baada ya mashauriano na viongozi tofauti katika jamii, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu ndiyo imetoa uwamuzi wa kuwataka waumini na wazanzibari wote kushiriki katika kutoa maoni lakini sambamba na uwamuzi huo. Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, unapenda utoe tanbihi na tahadhari ya hali ya juu kwa tume na kuitaka ifanye kazi yake kwa uadilifu. Kwani uongozi pamoja na wazanzibari wengi kutokana na udanganyifu wa tume zote zilizotangulia za uchaguzi, bado wasi wasi mkubwa umetanda pamoja na imani ya kuwa haki haitotendeka. Vile vile tunawasiwasi mkubwa wa mamlaka za nchi kupitia watu wachache wenye lengo la kufanikisha maslahi yao binafsi, wataingilia utendaji wa tume na shughuli zake kiutendaji kwa kuiburuza katika malengo binafsi na kwa hilo hapa sisi viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu tunatamka wazi kwamba hazitonyamaza kwa udanganyifu na dhulma yoyote itakayofanyika na haitamstahamiliya wala kumuonea haya kiongozi yoyote kwa dhulma hiyo.

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI-ZANZIBAR
24/06/2012

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

MSIMAMO WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISILAMU ZANZIBAR JUU YA MCHAKATO WA KATIBA.
Kila sifa njema zinamstahikia Allah (S.W.T), rehema na amani zimuendee Mtume wake, ahli zake na wafuasi wake wote waliomfuata kwa wema.
Baada ya vikao tofauti vya uongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Zanzibar, zimeonelea kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni kuhusu katiba mpya kwa sababu kuu zifuatazo:
1. Vikao vyote vya uongozi vilikataa katakata suala zima la kususia na ilikubalika azimio la kuwa tusitoe mwanya kwa maadui zetu wasioitakia mema nchi yetu Zanzibar wakutusemea na kutoa maoni dhidi ya nchi yetu ya Zanzibar.
2. Kushiriki kwetu tunatengeneza hoja ya vitendo na kuzidi kuuthibitishia ulimwengu na serikali yetu ya umoja wa kitaifa chini ya uongozi imara wa Rais wetu mpenzi Dkt Ali Muhammed Shein kuwa Jumuiya za Kiisilamu hazina nia mbaya wala hazijapata kuwa na nia mbaya ya kuleta vurugu au kuvunja amani kama lilivyofanya jeshi la polisi tarehe 17/06/2012 huko Mahonda, Donge, Mkokotoni na maeneo mengine pamoja na kunajisi msikiti na kuharibu mali ya misikiti ikiwemo kuunguza mazulia ya msikiti wa Mahonda. Pia kuwapiga mabomu ya moto waumini wasio na silaha ndani ya sala na kuwadhalilisha wanawake kwa kuwavua nguo na kuwajeruhi vibaya sana.
3. Kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Shein katika suala la umoja ni nguvu na kutotoa mwanya kivitendo wa kuwagawa wananchi wa Zanzibar, kwani Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisilamu kwa muda wote baada ya kukabidhiwa na Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu kazi ya kuelimisha UMMAH wa kizanzibari kupitia mihadhara ilikuwa ikisisitiza kwa nguvu zote umuhimu wa umoja. Imani yetu sisi viongozi kuwa “KWA UMOJA WETU TUTASHINDA”.
4. Kushiriki kwetu kutaweka rekodi sahihi na halisi ya wazanzibari ndani ya tume ya kupokea maoni juu ya mchakato wa katiba mpya ili kuipa fursa tume hiyo na hasa wakurugenzi kutoka Zanzibar pamoja na wabunge na wawakilishi katika Bunge la katiba kuitetea nchi yetu Zanzibar na kumrejeshea Rais wetu heshima ya kutambulika kimataifa na kuifanya nchi yetu iwe na mamlaka kamili ya kujiamulia kwa uhuru bila ya kuingiliwa.
5. Kutumia fursa hii ya mchakato wa katiba mpya kuimarisha muungano wa kijamii na kuondoa dhulma ya muungano wa kiserikali ulioidhulumu nchi yetu kiunyama haki zake za kimataifa na hata za kitaifa na kufikia hadi kuifuta nchi yetu ya Zanzibar katika ramani ya dunia.
6. Tamko la wazi la mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji wa maoni kuhusiana na katiba mpya Mh. Jaji Warioba alilolitoa mbele ya waandishi wa habari alipoizindua tume hiyo mjini Dar-Es-Salaam siku ya Jumatatu 18/06/2012 kwamba maoni yoyote yataheshimika na kuzingatiwa ikiwemo suala zima la muungano pamoja na yale maoni ya watu wanaoukataa muungano. Lakini bado wazanzibari tunawasiwasi mkubwa sana…
Kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa hapo juu na baada ya mashauriano na viongozi tofauti katika jamii, Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu ndiyo imetoa uwamuzi wa kuwataka waumini na wazanzibari wote kushiriki katika kutoa maoni lakini sambamba na uwamuzi huo. Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, unapenda utoe tanbihi na tahadhari ya hali ya juu kwa tume na kuitaka ifanye kazi yake kwa uadilifu. Kwani uongozi pamoja na wazanzibari wengi kutokana na udanganyifu wa tume zote zilizotangulia za uchaguzi, bado wasi wasi mkubwa umetanda pamoja na imani ya kuwa haki haitotendeka. Vile vile tunawasiwasi mkubwa wa mamlaka za nchi kupitia watu wachache wenye lengo la kufanikisha maslahi yao binafsi, wataingilia utendaji wa tume na shughuli zake kiutendaji kwa kuiburuza katika malengo binafsi na kwa hilo hapa sisi viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu tunatamka wazi kwamba hazitonyamaza kwa udanganyifu na dhulma yoyote itakayofanyika na haitamstahamiliya wala kumuonea haya kiongozi yoyote kwa dhulma hiyo.
Pia umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, zinatoa wito kwa wazanzibari wote pamoja na viongozi wa kisiasa kuungana na wazanzibari wote na kutumia fursa hii ya mabadiliko ya katiba kudai Zanzibar yetu huru. Kauli mbiu yetu iwe…
“…TUNATAKA NCHI YETU ZANZIBAR NA TUNATAKA MAMLAKA KAMILI YA ZANZIBAR…”.
Sambamba na hili, tunaomba viongozi wetu wa kisiasa wasiwaingize wazanzibari katika MTEGO wa watanganyika wachache wanaotaka kuidhulumu Zanzibar kwa kuwatamkisha wafuasi wa CCM kukariri maoni ya kutaka serikali mbili sambamba na kuwatamkisha wafuasi wa CUF maoni ya serikali mbili na mkataba ili isemwe mwisho wa rekodi za tume kuwa wazanzibari wanataka serikali mbili na kulitupia mbali neno la mkataba hatimae ni kubakishwa serikali zilizopo kama zilivyo na muungano wa dhulma dhidi ya Zanzibar uliodumu kwa muda wa nusu karne na kuwatia wazanzibari katika kitanzi cha nusu karne nyengine.
Tunawatahadharisha wazanzibari tusiingie katika mtego huo, TUUNGANE sote kwa kauli moja TUNATAKA HESHMA YA RAIS WETU, TUNATAKA HESHMI YA NCHI YETU, TUNATAKA HESHMA NA MAMLAKA KAMILI YA NCHI YETU. Huu si wakati wa kunadi sera za vyama tukifanya hivyo lazima tutajigawa na kuwapa nguvu maadui zetu, umoja wetu ndiyo silaha yetu. Tupaze sauti zetu kwa sera ya uzalendo:
“…TUNATAKA NCHI YETU YENYE MAMLAKA KAMILI (FULL SOVEREIGNITY)…”
Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu unapenda kuwathibitishia waislamu na wazanzibari wote kwa ujumla wao kuwa tupo palepale katika lengo kuu la kuitaka nchi yetu Zanzibar kwa gharama yoyote ile na bado tutaendelea kudai nchi yetu mpaka tone la mwisho la uhai wetu. Tunawataka wazanzibari wote sambamba na kujitokeza kwa wingi kutoa maoni ,tuendelee kwa wingi zaidi katika kuorodhesha majina yetu kwa umoja wetu sote katika fomu maalumu iliyoandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu kukusanya majina ya wazanzibari wanaodai haki yao ya kikatiba ya “KURA YA MAONI” kuhusu Zanzibar na muungano, Jee! Wanautaka au hawautaki? Haki hii ya kudai kura ya maoni imo ndani ya katiba yetu ya Zanzibar ibara ya (80A). Kwa haki hiyo HATUNA MJADALA, tusiogope kauli za Wakuu wa Mikoa wanaopotosha wananchi kwa silaha ya vitisho wakiwa wanayakini na kutambua kua hawana haki hiyo. Wazanzibari hiyo ni haki yetu ya kikatiba na tutaendelea kuidai kwa amani MPAKA TUIPATE ZANZIBAR YETU HURU YENYE MAMLAKA KAMILI.
Serikali zote duniani, mara nyingi zinalinda malengo yake kwa mtutu na vitisho lakini kwa upande wa wananchi mara nyingi sana matakwa yao hubezwa na kutupiliwa mbali, hivyo kwa kuzingatia hayo hatuna budi kujenga ngome imara, na kwa mantiki hiyo tunaanza safari yetu kwa kuweka ulinzi imara baada ya kumtegema Allah (S.W.T) kuunganisha nguvu yetu na kujipima kiutendaji. Allah amejaalia nguvu yetu ni katika umoja wetu kivitendo lengo la azimio letu hili ni kuhakikisha tunatoa shindikizo la kutosha ili haki itendeke, kwa maana hiyo basi tunatangaza rasmi kwamba tunawaunga mkono waislamu wenzetu wa Tanganyika katika suala zima la kuikataa sensa ya taifa. Mbali na sababu zao za msingi, kwa upande wa Zanzibar tunasababu ya msingi na ndio kipaumbele chetu, sijengine ila ni nchi yetu na tunatamka wazi kwamba, HATUTOSHIRIKI SENSA MPAKA TUIPATE NCHI YETU KWANZA.

“…ZANZIBAR HURU IKO NJIANI… UMOJA WETU NDIO SILAHA YETU…”
WABILLAH TAUFIQ
…………………
Sheikh, Farid Hadi Ahmed.
0777421813
MSEMAJI MKUU WA UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISILAMU ZANZIBAR.

NAKALA:
Mh. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Mh. Katibu Mkuu CUF
Mh. Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar
Ofisi ya Umoja wa Mataifa Zanzibar
Mabalozi wote nchini
Vyombo vya habari
Waislamu wote Tanzania

Advertisements

15 responses to “Tutashiriki mchakato wa katiba – Uamsho

 1. Sisi Wazanzibari tunakuungeni mkono mia kwa mia katika hili kwani nyinyi ndio viongozi pekee ambao TUNAWAAMINI NA TUNAWASIKILIZA. Hatuungi mkono Kiongozi yoyote wa siasa wa Zanzibar kwani wanaonekana kujali maslahi ya matumbo yao badala ya maslahi ya nchi. Zidumu fikra za Viongozi wa Uamsho!

 2. Pingback: Anonymous·

 3. Umoja ni nguvu badala ya kuhadaliwa na wana siasa hatimae tumepata viongozi wa kututetea mpaka kieleweke hakuna sensa wala nini tutahisabwa tukiwa huru sio tukiwa watumwa

  • kaka umoja ni nguvu kweli lakini umoja gani huo?hawa uamsho si viongozi bali hawa ni wafanya kazi wa wana siasa hawa wanatumwa tu na mengi wata kubali hivi ni lipi uamsho walisema kama wao? na wajiandae kujibu maswali mbele ya ALLAH wamesababisha watu kuumizwa na kupata majeraha na hali walikuwa wakifabya ukanumba tu na wala si kweli eti walikuwa wana ugomvi na smz bali smz ndio ili wapa kazi hiyo ya kuwavuta wa zenj kijanja kwanz na stail ya kususia kisha kukubali

 4. Tuko pamoja na viongozi wetu wa JUMKI NA UAMSHO. Sisi hatuna haja ya vurugu isipokuwa hizi tume zimetuchosha kwani ni tume zilizowekwa kwa kutekeleza matakwa ya viongozi. Sisi tunajuwa kuwa huu ni mtego umeshaekwa na utekelazaji wake tunautilia mashaka. Sisi tokea mwaka 1995 tulikuwa tukichezwa shere na tume hizi mpaka hii leo sisi sote imani imetutoka kwa tume hizi zinazoundwa kwa hila ya kutudhulumu haki yetu. Lakini ilivyokuwa viongozi wetu wametuamuru tushiriki sisi tutashiriki kutowa maoni yetu. Sisi sote tunaka ZANZIBAR YETU YENYE DOLA KAMILI SIO ZANZIBAR YENYE DONDA. Inshallah kama haki haikutendeka mutatuuwa sote lakini hatukubali kuonewa tena. ZANZIBAR HURU INAWEZEKANA TUMECHOKA NA UKOLONI WA KITANGANYIKA. TUACHENI TUPUMUWE KWA NAFASI KATIKA NCHI YETU.

  • hatuko pamoja na wasanii hawa wa kidini inamaana siku wakisema yesu ni mungu pia tutakuwa nao pamoja?hawa si walikuwa wakisoma aya na hadithi za kukataa ,mambo haya sasa wame shushiwa aya mpya?

   • Mashekhe si wasanii kama wanasiasa wakati utathibitisha usiwe na haraka ndugu yangu hata nyama ya nguruwe inahalalika kwa dharura itakua mchakato wa katiba? kuna ajenda ya siri wale maadui walikua wanatamani msimamo uwe ni kususia na tayari wamejipanga kuhujumu viongozi
    na kwa kweli wamechukia sana kwa nini wametoa msimamo huo wa kuingia jambo jengine mashekhe wametwambia kua uamuzi huo umepitishwa zamani sana ilibakia tuming tu ndo mana maadui wa zanzibar

 5. Ni kwl UWAMSHO wamedhamiria kuikomboa ZANZIBAR. Kw sbb hata mm kabla niliamini kwmb kutokwenda kushiriki ni kutoa mwanya kwa madhalim lakini kw msimamo waache watafute njia nyengine ya kutokea. Jaman jaman katu tusiache kushiriki kwnye maoni na kamwe tusiende kwnye SENSA. Zanzibar kwanza SENSA baadae. Tuondoeni tofauti zetu za VYAMA ili tufikie lengo letu. Niwazi kabisa kw m2 yeyote anaedai serikali moja,mbili hata tatu bado uzalendo wake unamatatizo. Tunachodai ni ZANZIBAR HURU YENYE MAMLAKA KAMILI na sio 1,2, wala 3. TUWACHIWE TUPUMUE BWANA

 6. Rumhy Suleyman (Mkoroshoni)

  Good Idea…! Ni kweli hata mi nilikua sina raha kabisa kwa ukosa uamuzi wa juu ya hili, japo nilikua naamini kua c vyema kwenda kuihalalalisha ndoa ya haramu (MUUNGANO) iliofungwa na huyu Mal3uun Nyerere pamoja na Mh. Abeid A. Karume, kwa vile ni kujitia kitanzi na kuwapa nguvu zaidi ya kutunyonya wakiwa na ushahidi wa katiba mpya ya Muungano itayopatikana kupitia cc wenyewe. Lakini pia ilikua nahisi kua kuna hatari vile vile tucposhiriki, kuchelea kuwapa fursa Maadui zetu peke yao kuifinyanga Zanzibar wanavyotaka wao bila ya kuwemo fikra zetu, matakwa na mawazo yetu na kujitawala uwanjani kwa kutusemea, hatimae kuja kujutia kwa nini?…! na wakati ndo umeshapita. Ila pamoja na imani zangu hizo ilikua bado naheshimu mawazo ya Viongozi walonizidi elimu, maarifa, hekima, umri na uzoefu, mawazo ambayo yamekua sambamba na kile nilichokua nakiwaza kwa upeo wa ufahamu wangu kwa kujifunza kupitia kwao. Na sasa nashkuru kua nimekua huru kiakili kwa uamuzi niloupata kupitia kwa masheikh ambao naamini ndio njia sahihi kati ya njia mbili nilokua baina yake.
  Na pia natoa Changamoto kwa vijana wenzangu walio wazalendo kutumia mda wao sana katika kufikiria mambo ambayo yataisaidia nchi yetu bila kujali Sera zetu za kivyama wala ukabila, kutumia fursa ya kutoa maoni yalio sahihi japokua sina uhakikia asilimia 100 kua hii tume ina kheri nasi, wala cjui hasa lipi walolikusudia. Ila nna uhakika kua kushiriki ni Bora kuliko kususia…! Nami nawakilisha…
  Al’Rumhy Suleyman.

 7. SAID; KHAMIS
  KAULI MBIU TUACHENI TUPUMUWE EEEEEEEEEEEEEE
  Wanzibar wote tuukatae muungano kwa nguvu zote na sio ubabaishaji wa serikali 1, 2. 3 , 4 .5 au 7
  hatuuuuuuuuuuuutakiiiiiiiiiiiii MUUUNGANOOOOO Basi tena tumechoka dhulma ya nusu karne

 8. Ndugu yangu @juakalisana.
  Hukuona kilichoandikwa kwa sababu jua ni kali sana.
  Sasa ni kweli walitumia aya kukataa mambo lakini hawakutumia aya kuhalalisha tume ya katiba.
  Walichokisema ni kwamba baada ya vikao tofauti walivyofanya wanajua wazi hakuna tume itakayochukua mawazo yao ya kuvunja muungano lakini wanashiriki kwa kutowapa mwanya maadui zao bcouse wacpoenda watu wakwenda kusema wanavyotaka kwa sababu pamoja na kuwa uamsho ina
  nguvu kubwa lakini bado kuna makundi mengi hawaungi mkono hoja za uamsho na wate ni waislam wenziwao hivyo sababu kubwa iliyowafanya uamsho washiriki ni haya makundi ambayo wao uamsho wanayajua.
  Kwa sababu hiyo ndio ikawafanye wakashiriki kwa wingi ili kuzima hoja za haya makundi.
  Lakini hata wakingia kwenye mchakato mcmamo ndio ule ule hatutaki muungano tunataka zanzibar yetu mulioikalia kimabavu miaka 48 sasa.
  Hapa hakuna cha kutatua kero za muungano wala kubadili mfumo wa muungano cc muungano uvunjike kwanza halafu ndio kama pana haja ya kuungana tena kwa mkataba maalum.
  Elewa ya kwamba kafiri hajui kutenda uadilifu kwa hiyo tume ina ongozwa na kafiri na iliyopita pia iliongozwa na kafiri kwa hiyo tuctegemee hata kwa aclimia 10 kutendewa uadilifu.
  Mara zote wamewekwa makafiri kuongoza tume ya katiba kwa sababu makafiri wanajua hii ndio nafac pekee ya kuwamaliza waislamu katika nyanja zote ndio maana hawajathubutu kumueka muislam kwa sababu muislam anaweza kutumia imani yake kutenda udilifu lakini kafiri hawezi kufanya uadilifu ndio maana wakamchagua.
  Jambo jengine ni kuwa hata mtume alishiriki mkataba wa hudaibia wakati alijua kwamba makafiri hawawezi kutimiza ahadi walizoekeana lakini kumbe ilikuwa ndio sababu ya kukomboa mji wa makka.
  Natumai umenifahamu.

 9. A/Alaykum.

  Alhamdulillah, hii ndio faraja ya kuongozwa na Masheikh kwa sababu wapo too strategically , argumentationally and wisely moving with a high braveness.

  Nilipata mashaka makubwa sana juu hatima yetu pale nilipoisoma makala ya msimamo wa Zanzinet juu katiba mpya na ile ya moja yenye title “Muungano wa Mkataba” katika blog ya http://www.mzalendo.net hii ni kutokana ana zile sababu za msingi zinazojitokeza kati ya Wazanzibari na watu wa Ireland ya Kaskazini katika kuzidai nchi zao kupiti kura maoni, ambapo kwa Zanzibar matokeo yake yalikuwa yanaonesha wasiwasi mkubwa sana sana wa kuingizwa kitanzini.

  Sasa mambo yamekaa pazuri. Tuko pamoja Wazanzibar wote Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar, Masheikh, Viongozi wa Siasa, Wafanyakazi, Wakulima, Wanawake na Wanaume tunataka Zanzibar yenye mamlaka kamili nje na ndani.

  MUUNGANO HUU HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  Nawasilisha.

  SERELLY.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s