Waasisi wa Muungano na madai ya Kizazi kipya

Vijana wanaokusanyika katika viwanja mbali mbali kufuatilia mihadhara inayohusu masuala ya Muungano ambapo kwa kiasi kikubwa vijana wansikika wakisema ‘hatutaki Muungano’ huku kauli mbiu yao ikiwa ‘tuachiwe tupumue’

Na Juma Mohammed, Zanzibar

Inaeleweka na kila mtu mwenye akili timamu na mwenye busara kwamba Muungano ni jambo la maana na lenye faida, haitazamiwi katika hali ya kawaida kutamani kuvunja Muungano, ingawa yawezekana baadhi ya watu kufikiri hivyo, lakini yafaa kufahamu kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Taifa la Marekani leo limepata nguvu na uwezo si kwa sababu ya watu wake bali ni kwa sababu ya umoja wao. Nasi katika Tanzania tunahitaji kuwa na umoja na nguvu kama zile za Mataifa makubwa pamoja na umbali na tofauti ya uchumi na maendeleo,lakini ipo siku tutakuwa kama wao.

Ndoto hii inaweza kutimia ikiwa tutaweka misingi madhubuti katika kuandika katiba mpya na kubadili mfumo wa muundo wa Muungano kwa kuwa na aina inayozungumzwa na wengi inayoonekana kukubali Muungano wa mkataba.

Bila shaka tutatofautiana katika mawazo,lakini naamini utofauti huo hautaweza kuviza uhuru wa maoni hasa ikitiliwa maanani kuwa Katiba zote mbili zimelinda haki hizo kama zilivyolindwa na mikataba ya kimataifa.

Tunaambiwa kuwa uhuru wa kujieleza ni moja ya haki yetu muhimu sana hivyo, kuwepo kwa mawazo tofauti na mitazamo katika jamii ni sehemu ya kufaidi haki hii ambayo sio hisani kwa raia . Ni haki inayoweka msingi kwa uhuru mwingine na heshima ya binadamu hapa Zanzibar.

Ipo hofu kwa baadhi ya watu hasa unapozungumzia muundo wa Muungano ubadilike kwa kubadili mfumo kutoka wa kikatiba na kuwa wa mkataba ambao utaruhusu kuendelea na Serikali mbili,lakini zote zikiwa zenye nguvu sawa na hadhi ya Utaifa nchi zao (Sovereignty).

Watu wengi wanashauku kuona mabadiliko yanapiga hodi katika muundo wa Muungano, tumeiga mengi kwa wazungu na tuige basi na miungano yao au ndio tunataka kubakia na urithi wa muundo Muungano ambao haupo popote duniani, ni dhahiri unawalakini.

Inatupasa kujiuliza muundo huu wa Muungano una kipi cha ajabu ambacho wengine hawana kama kipo cha kuiga basi EU wangeiga kwetu,lakini sikioni zaidi ya kuongezeka kwa kero za Muungano, lazima tuzikabili changamoto zinazojitokeza za wataka mabadiliko.

Natabiri ingawa utabiri wangu sio ule wa kinyota (Astrology) kwamba kuna dalili hasi kwa Wazanzibari wengi kutoikubali rasimu ya katiba mpya ikiwa haitatambua Utaifa wao tangu enzi na dahari Zanzibar imefahamika sana katika upwa wa Afrika Mashariki Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa ni miongoni mwa Dola kongwe ikizishinda zile za Ulaya na Asia.

Ubalozi wa mwanzo wa Marekani katika Bara la Afrika na Asia ulifunguliwa Zanzíbar 1837 ambao ulikuta tayari kulikuwa na wakala wa kibiashara kampuni ya John Bertram & Co of Salem Massachussets ikifanya biashara baina ya watu wa Zanzíbar na Marekani.

Waingereza nao walifungua Ubalozi mwaka 1841,Balozi wa kwanza alikuwa Luteni Kanali Muairish Atikins Hammerton,tena hapo ikawa fungulia mbwa ,Wajerumani, Wabelgiji, Wataliana, Wafaransa na Australia wakafungua ofisi za kibalozi.

Hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 18 Dola ya Zanzíbar ilikuwa maarufu ulimwenguni kote na pia ilikuwa pia na uchumi usiyoyumba wala kukumbwa na mdororo wa kiuchumi kama uliyoikumba Ugiriki kwa maana hiyo, Muungano wa mkataba utakaowarejeshea Wazanzibari utambulisho wao kimataifa ndio suluhisho la kero za Muungano.

Imani yangu ni kwamba hakuna anayeitakia mema Zanzibar akaibuka kupinga Muungano wa nchi mbili hizo ambazo ziliungana bila shuruti ambapo mahusiano baina ya Tanyanyika na Zanzíbar yalianza tangu enzi za zama za mawe( stone age) na hadi kufikia Muungano baada ya wananchi wa nchi mbili kuamua kuunganisha na kuzaliwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Muungano wowote ule ni maelewano kati ya wananchi wa zile nchi zinazohusika,hivyo hakuna Muungano isipokuwa ni ule utakaokubalika na Wazanzibari ulio wa haki,usiokuwa na mkubwa wala mdogo.

Inaelekea Wazanzibari wanataka Muungano utakaowaridhisha ulio wazi na wenye mipaka ya mamlaka inayoeleweka ikiwemo fursa ya kujiamulia na sio kupangiwa bila ya hayo Wazanzibari wa leo wataukataa Muungano kwa heshima kwani zilizoungana ni nchi mbili zilizohuru na sawa.

Dhana ya kuwa na mfumo mpya ni kusaliti Mapinduzi ni dhana potofu na mfu haina mashiko kwa Wazanzibari wa leo kwani Mapinduzi hayo yameota mizizi katika nyoyo za watu na katika kila nyanja ya jamii Wazanzibari na lengo kuu la mapinduzi ni Wazanzibari kujitawala na kujiamulia wenyewe.

Mfumo mpya wa muundo wa Muungano hautakuwa wa kipekee kwani zipo nchi nyingi zimeungana katika mfumo wa aina hiyo na Muungano wao umekuwa wenye tija na nguvu usiokuwa na kero sugu.

Mambo ya kukosekana kwa uwazi ndio yanayoleta matatizo siku zote kam kutokubainishwa wazi uwepo wa Serikali ya Tanganyika ambayo kwa muundo uliopo Serikali ya Tanganyika imejificha upenuni mwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapaswa kuwahudumiwa kwa usawa na pande zote,Tanganyika na Zanzíbar.

Afrika Magharibi wana Muungano wenye nchi 15 unaoitwa ECOWAS ukisimamiwa na chombo chao Tume ya ECOWAS ambao kila nchi zilizojiunga zimebakia na Utaifa wake(Sovereignty ),lakini wamekubaliana baadhi ya mambo tu kuungana ikiwemo pasi moja ya kusafiria.

Katika Mkataba wa Muungano Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zilikubaliana kuunda serikali moja kamili ya Jamhuri (SOVEREIGN REPUBLIC).

Muundo huu wa Muungano umezifanya nchi za asili kutokuwa nchi kamili kwa maana ya Dola(Sovereign state) inayoitwa Zanzibar wala Tanganyika bali kuwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo ndivyo “Sovereign Republic” au “Sovereign State” chini ya hati ya Muungano. Muundo wa sasa ume

Muungano wa mkataba utaifanya Zanzibar kuwa na sifa ya Taifa kamili ambalo litajiamulia mambo yake wenyewe iwe kukopa,kuazima,kujiunga na mashirika ya kimataifa na mambo mengine, Tanganyika nayo ikiwa na Utaifa wake,itarejea hadhi na sifa yake katika pwani ya Afrika Mashariki kama ilivyosimuliwa na wasafiri wa kale waliotembelea eneo hili waliotajwa katika kitabu cha Periplus of the Erythraean Sea, hili linatatizo gani?

Kwa sasa kwa upande wa Zanzibar kinachokosekana ni Utaifa, mambo yote yanayohitajika inayo, ina eneo la ardhi, watu, Baraza la Wawakilishi, ina sehemu ya Utendaji, ina mahakama, bendera,wimbo wa Taifa kwa maana hiyo haitakuwa vigumu ikiwa mfumo wetu wa Muungano utakuwa wa mkataba.

Vuguvugu la mabadiliko linaonekana kushika kasi kila kona, kila mtu anazungumzia Muungano huku hoja pendwa ni “Tuachiwe tupumuwe”maamkizi ndio hayo mtu akikutana na mwenzake anamsalimia kwa tuachwe tupumuwe,wengine ufanya mzaha “haa tutaachiwa tupumuwe kweli”

Japo kuwa kwa kipindi kirefu na naweza kusema tangu kuasisiwa kwake Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilichukuliwa ni dhambi na usaliti kuzungumzia kasoro za Muungano au kutofautiana kisera na kimtazamo ama na wanasiasa au hata watu wengine katika jamii, ni watu waliaminishwa kuona kama ni kitu kitakatifu kisichoweza kujadiliwa.

Lakini kadri siku zilivyokuwa zikipita ndio utakatifu umepotea tena kwa kasi ya ajabu kama ulivyopotea ujamaa wa kale baada ya kushindwa kuhimili misukosuko ya ubepari na utandawazi wa kileo.

Haya naweza kuyaita ni mabadiliko ya falsafa kwa Wazanzibari ambao baada ya miaka 48 ya kuishi katika mfumo wa Muungano wa kikatiba uliozaa kero zilizoshindwa kutatuliwa kwa miaka yote hiyo, ndio wamebuni falsafa ya kudai Muungano wa mkataba.

Njia za kudai mabadiliko zinatofautiana, sisi wengine hatukubaliani kamwe na njia za fujo na za kibaguzi, maana amani na utulivu ni mambo muhimu,hatuwezi kuchezea amani kwa kisingizio cha kudai haki,lazima tuzitii sheria tena bila kushurutishwa, tuwaheshimu viongozi wetu, wazee na kila mtu.

Fujo,hamkani, vurugu hazina maana kwani hata Malcom X aliamua kuacha falsafa ya ‘Jino kwa Jino’ au (Militant Philosophy) kwenda falsafa ya ‘Ukipigwa Shavu la Kulia Geuza na la Kushoto’,ijapokuwa Tanzania hapigwi mtu wala kuonewa,nimeweka mfano huo kuonesha ulazima wa kutunza amani na kuacha kabisa vurugu.

Kuna kisa maarufu cha Malcom X ambacho kinapatikana katika barua yake kutoka Makka( A Letter from Mecca) ambaye alikuwa akiwachukia wazungu,lakini baada ya kwenda hijja Makka mwaka 1964 Saudia Arabia huko aliwakuta wazungu waislamu, wahindi, kila aina ya watu ambao walikaa pamoja,wakila na kufanya ibada kwa pamoja.

Alijifunza kwamba tatizo sio Uzungu bali ni mfumo wa kibepari wa Marekani, kwa mnasaba huu tatizo sio Muungano ni mfumo wa muundo wa Muungano wenyewe ndio maana watu wamekuwa wakipaza sauti kutaka ufanyiwe mabadiliko.

Umuhimu na umaarufu wa Zanzibar haukuanza leo wala jana, pamoja na udogo wake kama kisiwa, iliwavutia wengi kibiashara na kuna mikataba ya kimataifa ambayo iliingia nayo kama ule wa Ujerumani,Marekani iliyohusu ushirikiano wa kibiashara na kidiplomasia.

Watu wa Afrika ya Mashariki, Uarabuni, Ulaya, Bahari ya Hindi na Mashariki ya Mbali wote wanatambua umuhimu huo ambao ulitokana na maendeleo yaliyokuwa yamefikiwa Zanzibar kwa wakati huo.

Kuna dhana kwamba Zanzibar haiwezi kusimama yenyewe kiuchumi, hii sio sahihi, yapo mataifa yanayofanana na Zanzibar kijiografia,idadi ya watu rasilimali,yameweza kusimama yenyewe isipokuwa siku hizi lazima ushirikiane na wenzako,kwa hivyo mbali ya kuwa katika Muungano unaweza kujiunga na Jumuiya mbalimbali za kikanda.

Viongozi wetu wasome wakati tulionao,wajifunze kutokana na matukio ya kilimwengu, ile enzi ya kuwa na viongozi wa maisha kama walivyojitangazia akina Dk. Hastings Kamuzu Banda,Idd Amin, Bedel Bokasa,Mobutu Sese Seko na Mathias Nuema haipo tena.

Wanasiasa wazee na wale wenye fikra mgando lazima wakae chonjo kupisha damu changa au kizazi kipya, wakati wa kufikiri kuwa tunaweza kuwa na ‘Mawaziri wa Maisha’, ‘Wabunge wa maisha’, ‘mabalozi wa maisha’, ‘Wakuu wa Mikoa wa Maisha’, ‘Wakuu wa Wilaya wa Maisha’ umepitwa na wakati, tenda wema nenda zako usingoje shukurani.

Tunawashukuru wazee wetu kwa kuliongoza Taifa hadi hapa tulipofika, wametufanyia kazi nzuri, sasa ni zamu ya vijana kwa kufuata kanuni ya mbio za vijiti huna sababu ya kuzunguka uwanja wote utapinduka kwa kwikwi kwa kujawa na pumzi,ukifika mita mia mpe mwenzako ndio mwendo wa kileo.

Tuujadili Muungano kwa nidhamu,hekima na busara bila kusahau kufuata na kuzitii sheria za nchi huku tukitambuwa tunalo jukumu moja kubwa la kwenda kutoa maoni katika Tume ya Katiba wakati utakapofika maana hiyo ndio fursa pekee ya wananchi kuamua aina ya mfumo wa muundo wa Muungano wanaoutaka chini ya katiba mpya.

Advertisements

15 responses to “Waasisi wa Muungano na madai ya Kizazi kipya

 1. Hatunashida ya aina ya muungano tunachohitaji ni KUVUNJA MUUNGANO ikiwa kuna mtu anahitaji muungano aende yeye peke yake. Hivi hawa baadhi ya watu wanaakili kwl mpaka muda huu (still) unangangania muungano si bure ipo namna. Tucwe watumwa wa mawazo tuziacheni akili zetu ziogolee mageuzi huu si wakati wa kusema MUUNGANO. Mm nahic mtu kama hana cha kuandika bac afuate SUNNA ya MTUME(s.a.w) atapata thawabu kuliko kuropokwa akijipotezea (MASS OF ZANZIBARIS) kwa watu wanaomuheshmu. Hv nyny muonao andika haya hiv ni kwl hasa ni WAZANZIBAR kw sbb inashangaza kw m2 timamu kusema kwmb wazanzibar wanataka muungano. Tuacheni tupumue na kasumba zenu. THE REPUBLIC OF ZANZIBAR FIRST.

  • muungano urekebishwe ikiwa ni pmj na kumrejeshea rais wa znz mamlaka kamili, bandari, wawe na maamuzi juu ya jambo wanalolita coz kuvunja muungano sio suluhisho coz hv ss znz ktk mawizara kuna mawaziri waznz lkn utendaji hamna
   Kuwa makini ktk maamuzi na sio kukurupuka ukaja kumtafuta mchawi

 2. we muandishi uloweka habari inaonesha umlevi,huna akili au ni kibaraka wa mtu kakutuma kuja kusema twataka muungano ww km mwanao umeozesha bara na unaona muungano ukivunjika utakuathiri mwambie mkweo ukuchukue na ww akakuweke na mwanao ila mswla yasio eleweka usituwekee hapa.

  ahsante kwa maoni yako lakini nadhani tunahitaji hoja za msingi na lugha ya kistaarabu kuliko matusi na maneno yasio na maana.

  Ahsante

  zanzibaryetu

 3. unajua, muungano c tatizo lakini hawana tunaoungana nao, c watu wazuri, hawatutakii mema, kwanza mila, desturi, silka zetu ni tofauti, me nahic tutarejesha hadhi yetu pale tutakapojitawala wenyewe, miaka 48 c kidogo bado miaka 2 nusu karne, baci tena hatuna tulichopata tuachiwe tupumue.

 4. tanzania hapigwi mtu?unataka kutwambia hawa waliopigwa hivi juzi na kujeruhiwa ili kuwa ni haki yao?ukitumia kalamu yako kuandika la kheri utapata malipo yako hapa duniani na akhera.na ukaandika ya shari nayo vilevile utalipwa.moja ya sharri mbaya uongo na mtume saw aliwahi kuulizwa muumin khasa anaweza kuiba mtume saw akasema ndio.akulizwa tena muumin anaweza kuzini akasema ndio.akaulizwa je muumin anaweza kusema uongo mtume akasema hapana muumin hawezi kusema uongo.

 5. Hatuutaki muungano kwanini munatun’gan’gania. Hivi nyie hamuoni munalazimisha kitu ambacho wananchi wameshakiona kuwa hakina maslahi kwao. Kumbukeni kila alie madarakani ni mchunga na iko siku mutaulizwa kwa muliyawafanyia watu. Sisi katu haturudi nyuma. Inshallah tutashinda nyie pigeni mabomu lakini juweni hamuna nguvu mbele ya Mungu. Sisi tupo na msimamo ule ule ZANZIBAR HURU KWANZA HATUUTAKI MUUNGANO TUNATAKA ZANZIBAR HURU. Tuacheni tupuwe.

 6. NYIE MNAPIGA MAKELELE WANAOKUSALITINI NI HAOHAO NDUGU ZENU WALIOKO MADARAKANI WAAMBIEN WASEME .KARUME DR SHEIN SEMENI KAM AHAMTAKI MUUNGANO

  • UHURU WA ZANZIBAR NI KUANZIA D.SALAAM MPAKA ZIWA VITORIA UNAJUA HAYO nataka unijibu inatoka ISTANBUL TURKEY

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s