Wawakilishi wataka uwiano katika Muungano

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud akibadilishana mawazo na Muakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Bweni Nje ya Mji wa Zanzibar.

WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wametaka uwiano sawa katika nafasi za juu za Muungano izingatiwe uteuzi wa wazanzibari ili kutoa haki sawa kwa pande zote mbili. Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wametoa kauli hiyo katika kipindi cha masuali na majibu ambapo walihoji kwa nini nafasi za majeshi na polisi zinashikiliwa na watu kutoka upande mmoja wa muungano peke yake.

Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Salim Nassor Juma alisema kutokuwepo na uwiano katiak kushika nafasi za uongozi na nafasi nyeti katika utumishi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kero na inahitaji kushughulikiwa.

Aidha Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub na Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (CUF) Salim Abdallah Hamad walitaka nafasi ya mkuu wa jeshi la polisi na nafasi ya mkuu wa majeshi ya ul;inzi na usalama ishikwe na wazanzibari.

Akijibu hoja hizo za wajumbe Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa rais, Mohammed Aboud Mohammed alisema kwa mujibu wa katiba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio mwenye mamlaka ya uteuzi huo na halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.

“Hata hivyo marekabisho ya sasa ya katiba ambayo yataanza hivi karibuni ni pahala pazuri pa kuwasilisha malalamiko na kutoa mapendekezo juu ya mamlaka ya rais, toweni malalamiko yenu kwa tume na ninakunasihini mfanye hivyo” alisema Aboud.

Aboud alisema katika uteuzi wa nafasi zote za juu katiba haikuweka vigezo, uwiano wala fomula maalumu katika uteuzi na ni mamlaka aliyonayo mheshimiwa rais ambaye ni pia jemedari mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

Kutokana na kuwepo na hali hiyo Aboud alisema ni wakati mwafaka kwa wananchi pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoa maoni yao kwa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya inayoanza kazi yake hivi karibuni.

Viongozi wagoma kuhama nyumba za serikali

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema inakabiliwa na upungufu wa nyumba za kuishi viongozi wa kitaifa kutokana na tabia ya baadhi ya viongozi hao kutotaka kuhama wanapomaliza muda wao wa uongozi.

Naibu Waziri wa wizara ya maji Ardhi, Makaazi na Nishati, Muhidin Makame alisema kuwa kwa miaka mingi serikali ilikuwa na nyumba zake za kuishi kiwemo viongozi wa kitaifa lakini matatizo yaliojitokeza ni baadhi ya viongozi hao kuwa na tabia ya kutohama katika nyumba za serikali baada ya muda wao wa uongozi kumalizika.

Hayo ameyaeleza Naibu waziri huyo wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua mipango ya serikali katika kuwapatia viongozi nyumba za kuishi na kuepuka gharama za kukodi.

Alisema jambo jengine ambalo limesababisha serikali kuwa na nyumba pungufu ni uchakavu wa nyumba hizo kutokana na kutokuzifanyia matengenezo kwa muda mrefu.
“Hivi sasa serikali inaandaa mpango maalumu wa kuzifanyia matengenezo nyumba zote za viongozi ambazo zipo katika hali nzuri na pia kuzivunja kwa zile amabzo zipo katika hali mbaya ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa nyumba mpya” aliahidi naibu huyo.

Aidha naibu waziri huyo aliwataka viongozi wanaomaliza muda wao kuzihama nyumba za serikali ili kuwapisha wengine ili kuondokana na upungufu wa nyumba na kutoa nafasi kwa viongozi wengine wanaoteuliwa nafasi hizo.

Baadhi ya nyumba za serikali ambazo zinakabiliwa na uchakavu mkubwa ni nyengine kuwa katika hatari ya kuanguka zipo katika maeneo ya mazizini, migombani na chakechake kisiwani Pemba.

Zanzibar kutengeneza bendera nyingi zaidi

WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari amesema jana kuwa serikali inakusudia kutengeneza bendera za kutosha za Zanzibar ili kuondoa upungufu na kuwawezesha wananchi kuzitumia.

Akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae (CCM) Mohammed Said Mohammed ambaye alitaka kujua kama matumizi ya bendera ni kosa kisheria.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alihoji upungufu wa bendera za Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba ikilinganisha na bendera za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akijibu masuali hayo Bakari alisema sio kosa kisheria kwa wananchi kutumia bendera ya nchi yao katika shughuli mbali mbali ikiwemo kupachika katika baiskeli au gari au kutumia kwa matumizi ya sheria za nchi na sherehe nyenginezo.

“Serikali haimzuwiii mwananchi kutembea na bendera ndogo ya Tanzania wala ya Zanzibar kama ataiweka ndani ya gari yake au vyombo vya maringi mawili, hii ni fakhari kuona wananchi wanaipenda nchi yao” alisema Waziri huyo.

Waziri Bakari alisema matumizi ya bendera yanafanana katika mahala mingi duniani hasa pale ambapo wananchi wanasherehekea kitu Fulani kama vile mpira, siku ya kitaifa na kadhalika kwa sababu hakuna tatizo lolote la kisheria.

“Kama kuna upungufu wa bendera nitashirikiana na taasisi inayohusika tuweze kutengeneza bendera za kutosha ili wananchi waweze kuzipata na kuzitumia” alisema.

Hata hivyo katika majibu ya ziada Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Gavu alisema kwa hivi sasa zipo bendera za kutosha na kuwataka wananchi wende wakazinunue ambapo bendera moja inauzwa kwa bei ya shilingi 40,000.

Zanzibar ilipitisha sheria ya kuwa na bendera yake mwaka 2005 ikiwa sehemu ya kielelezo cha utaifa baada ya bendera hiyo kutokuwepo kufuatia Zanzibar kujiunga na Tanganyika mwaka 1964.

Chalezo kipya kujengwa Zanzibar

ZANZIBAR inakusudia kujenga chelezo ambapo meli na boti za kijeshi zitatengenezwa ili kuondoa mchanganyiko wa vifaa vya kijeshi na sehemu za raia.

Hayo yameelezwa katika kikao cha baraza la wawkailishi kianchoendelea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani (CCM) Ali Salum Haji aliyetaka kujua kwa nini kikosi cha KMKM kimeshindwa kufufua chelezo chake hapa Zanzibar.

Waziri alisema hivi sasa serikali imo katika mipango ya kuangalia gharama za kufufua chelezo cha KMKM ambacho ni kikosi maalumu cha maji ya Zanzibar.

“Chelezo cha KMKM kilichindwa kufanya kazi tangu miaka ya 1970 lakini hivi sasa kwa msaada wa jamhuri ya kidemokrasia ya ujerumani tuna mpango wa kufufua chekelezo hicho” alisema waziri Makame.

Alisema kampuni ya Damen Shipyard kutoka Uholanzi imo katika kufanya upembuzi yakinifu na kuangalia gharama halisi ili kazi iweze kufanyika na kwamba jeshi kuwa na chelezo chake ni muhimu.

Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba kikosi cha KMKM kutumia chelezo chake kwa ajili ya matengenezo ya boti zake na hasa ikizingatia kanuni za kiusalama.

Kikosi cha kuzuwia magendo (KMKM) ni miongoni mwa vikosi vitano vya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambavyo vina majukumu mbali mbali ikiwemo ulinzi na usalama nchini.

Vikosi vyengine ni Valantia, Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Magereza, Kokosi cha Uokozi na Zima moto (KUZ) ambavyo voye vinatambulika kisheria.

Utafiti wa madini joto ni muhimu

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kusimamia na kufanya uchunguzi wa viwango vya madili joto katika chumvi inayozalishwa na kutumika zanzibar ili kuepuka madhara ya kukosekana kwa madini hayo mwilini.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri hiyo, Dk Sira Ubwa Mamboya wakati akijibu suali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua nafasi ya wataalamu wa afya katika kushauri matumizi ya madini joto katika chumvi hasa kwa uzalishaji unaoendelea kisiwani Pemba.

Waziri alisema wataalamu wa wizara yake kitengo cha lishe kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Unicef wametoa mafunzo kwa vikundi vya uzalishaji chumvi ili kuzingatia uchanganyaji wa chumvi na madini joto.

Alisema wizara yake imetoa mafunzo kwa maafisa wa afya kusimamia viwango vya madini katika chumvi inayouzwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

“wizara ya afya kupitia bodi ya chakula, dawa na vipodozi itaendelea kusimamia na kufanya uchunguzi wa viwango vya chumvi ili wananchi watumie chumvi inayotakiwa” alisema Dk Sira.

Aidha Naibu waziri huyo amesema wameshirikiana na jumuiya ya wazalishaji chumvi kisiwani Pemba (Association of Zanzibar Salt Prcessing Organisation – AZASPO) ili kuwanunulia madini joto na kuwakabidhi wao kama ni wadhamini na wasimamizi wa vikundi vyote vya uzalishaji chumvi.

“Lengo la kufanya hivyo wao AZASPO walitakiwa wawauzie wazalishaji na pesa wanazokusanya waziendeleze kwa kununulia madini joto ikiwa ni fedha za kimzunguko (revolving fund)” alisema naibu huyo.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, ukosefu wa madini joto unasababisha matatizo mbali mbali ya kiafya ikiwemo kutoimarika kwa mifupa mwilini na maradhi ya uvimbe shingoni (goiter).

Zaidi ya bilioni 1.5 zatolewa kwa vikundi

ZAIDI ya shilingi bilioni 1.5 zimetolewa kwa vikundi vya ujasiriamali Zanzibar hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu kupitia mfuko wa rais Kikwete na Rais Karume.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman wakati akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa nafasi za wanawake, Mwanaidi Kassim Mussa ambaye alitaka kujua ni wananchi wangapi walinufaika na mfuko huo kwa upande wa Zanzibar.

Waziri alisema jumla ya mikopo 750 ilitolewa ikiwemo watu binafsi, vikundi vya wajasiriamali, saccos na vikundi vya kiuchumi ambapo sehemu ya fedha hizo tayari zimesharejeshwa.

“Fedha zilizorejeshwa ni zaidi ya milioni 765,000 hadi kufikia Aprili mwaka huu ambapo ni sawa na asilimia 50. Jumla ya wanawake 170 katika mkoa wa mjini magharibi wamepata mkopo huo kati ya wanawake 276 waliopewa mkopo kwa Zanzibar nzima” alisema waziri huyo.

Waziri Suleiman aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo kwamba waazilishi wa mfuko huo ambao ni marais wa Tanzania na Zanzibar, maarufu mfuko wa JK na AK wanadhamira ya kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwaendeleza wananchi wenye kipato cha chini ili kupunguza umasikini nchini.

Mfuko wa JK na AK ambao umeanzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kupunguza umasikini na ukosefu wa ajira nchini unaowanufaisha zaidi ni makundi ya akina mama kupitia miradi yao mbali mbali.

Advertisements

12 responses to “Wawakilishi wataka uwiano katika Muungano

 1. Asalamu Alaykum. Nina heshima kubwa ya kukaribisha maoni ya kila mchangiaji na naahidi kuheshimu mawazo hayo. Hata hivyo, kwa ajili ya kulinda mila na desturi adhimu za Kizanzibari, sitachapisha maandishi yoyote yanayokwenda kinyume na utamaduni wetu. Tafadhali toa maoni yako kwa kwa uhuru kwa kutumia lugha za kistaarabu bila ya jazba wala matusi ili wengine wasome na kuyafahamu maoni yako. Na iwapo unahitaji kuuliza masuali au kupata ufafanuzi wa jambo lolote ambalo hujalifahamu basi usisite kuwasiliana nami kwa kutumia barua pepe: muftiiy@yahoo.com au simu nambari. +255777477101. Shukran. Salma Said.

  • Salma pamoja na kutwambia tuheshimu ktk kutoa maoni.

   Mimi nakuuliza zile habari za uongo na kupotosha unazoziandika kwenye gazeti la mwananchi jana kuhusu harakati za UAMSHO huko Donge wewe tukuelewe vipi?

   • bi salma ni mwandishi wa serikali lazima ataandika habari za kuwapendezesha viongozi wake, lakini akumbuke kifo ndicho kinachompeleka mtu kutambua aliyoyatanguliza kama mabaya au mazuri , ndugu yangu bi salma ukumbuke fani yako inaweze kukupeleka peponi au motoni , chaguo ni lako, hao unaowapendelea hawatokusaidia ktk siku ngumu ya hukumu ambapo hao wote viongozi wetu watakuwa dhalili kuliko mavi

 2. Issue ni Muungano tu. Ufe ufe tena uvunjike basi. Zanzibar bila ya Muungano ndio asili yake finish.

  Sarafu inashushwa na madudu ya Watanganyika shida tunapata wote. Aaaaa…. hiyo itakuwa ngumu.

  MUUNGANO HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  SERELLY.

 3. Napongeza juhudi ya serikali kutaka kuwatoza kodi watumishi wa muungano. Ila ni kwa nn yanayopangwa baraza la waakilishi ni mazuri lakini hayatekelezwi? Wawakilishi huu wakati wa kuulizia madil joto hizo madin zipo kibao cha msingi kwnz rejesha hadhi ya mamlaka kamili. Vp m2 unampa madin joto hali ya kuwa kula yake inamsumbua nyny habari. Wananch 2kila 2kishiba 2takuwa na mawazo ya kimaendeleo lkn kinyume na hvyo 2tawaza kula kesho wapi na c jengine. Ww ni muwakilish wakilisha kero za wa2 wako sio madin joto,nyumba za viongozi wakat kuna wananch kwao mvua kero jua kero hawana pa kukaa. Mumechaguliwa nyny na nyny wenywe mubadilike.

 4. hatutaki uwiano tena ni miaka 48 sasa tunataka turejeshe hadhi na heshima ya zanzibar yetu, zanzibar zamani ilikua na passpoti leo iko wapi, rais wa znz sasa ni kama waziri mwengn ktk serikali ya muungano, mfanya biashara wa znz anatozwa ushuru mara 2 tra na zrb, wakati bara ni tra tu, hatuutaki muungano hauna tija na cc yaa allah tusaidie tuikomboe nchi yetu.

 5. KWA MUJIBU WA MH.ABOUD, HAKUNA HAJA YA KUREKEBISHWA TENA KWANI MIAKA 48, SI KIPINDI KIDOGO CHA SUBRA KWA WAZANZIBARI KWA NINI WAENDELEE KUSHIKILIA MAREKEBISHO NA SI KUUVUNJA ? KWANI IKIONEKANA HAJA YA KUUNGA TENA SI UTAUNDWA? MBONA EAC ILIVUNJWA NA SASA IMERUDI TENA ? WAZIRI SIKILIZA MAONI YA WANANCHI NDIYO WALIOKUCHAGUA NA KUWA HAPO ULIPO HAO WAKIAMUA FUJO HAPATOSHI HAPO UJUE?

 6. Pingback: Wawakilishi wataka uwiano katika Muungano·

 7. Nikisikiliza Baraza nashindwa kufahamu ni kiasi gani mahitaji ya mtu wa kawaida yanazungumzwa. Nimevutiwa na hoja za Mheshmiwa Hija akikataa ushuru wa bandari ili kuchangia madawati. Wawakilishi inabidi kuidai Wizara ya Fedha itafute njia ya kutanua wigo wa ukusanyaji wa mapato. Kwa mfano sekta ya Ujenzi ni miongoni mwa Sekta ambazo zahitaji kuratibiwa ili wahusika nao wachangie. Mtumishi wa Serikali mwenye kipato cha chini kwa mwezi alipa kodi lakini fundi wa kujenga apatae zaidi ya milioni halipi chochote. Katika hali ya kuwa na taasisi bora na zilizowazi sekta hii ya ujenzi inaweza kuchangia pia.Hapo nyuma najua SMZ iliwahi kufikiria kutengeneza Sera ya Ujenzi. Wawakilishi ulizeni mambo kama haya badala ya kuuliza mambo ya kuchekesha.

  Chanzo chengine cha mapato kingekuwa malipo yatokanayo na Uwakala wa Ukodishaji nyumba au huduma nyenginezo. Kwa sasa madalali wa ukodishaji nyumbani na huduma nyengine wanajikusanyia mapato yasiyolipiwa kodi. Eneo hili pia linahitaji kuzungumzwa kwa kuwa ni eneo ambalo mahitaji yake yanaongezeka. Wawakilishi lizungumzeni hili ijapokuwa nyinyi wengi ndio wenye nyumba za kupangisha. Sera inabidi ziandaliwe ili huduma zipatikane kupitia kwa uwakala ili mapato yapatikane.

  Katika hali ya sasa eneo hili ambalo ni muhimu halijapata msukumo mzuri – Wenzetu washaanza kuzungumza namna ya kulisimamia ili watu wengi zaidi wafaidike. Tunahitaji kubadilika badala ya kuachia mambo yende kiholela tukipeleka lawama zetu kwa Mwenyezi Mungu. Kufeli kwetu kusihusishwe naye kwa kuwa kuna aya nyingi za Quran zinazokataa Mungu kuhusishwa na majanga yaliyokuja kwa sababu ya mikono yetu.

  mara nyingi ameHawa watu ambao wengine wanajiitMatarajio ni kuwa Sera hii ingeainisha mambo mengi ikiwemo nafasi ya sekta ya ujenzi.

  epukana na vianzio vya mapato

 8. wapumbavu kweli na majuha kwani hizo nafasi za mkuu wa majeshi au polisi hata wakipewa waznz zitasaidia nini wakati jeshi lote asilimia 99 ni watanganyika , hili ni tatizo la kuwa na watu wasiosoma kwenye baraza , hili halina tofauti na mabaraza ya kwenye kona limejaa vihiyo , ikiwa jeshi litakuwa na uwiano huo mnaotaka sisi watanganyika tutaweza vipi kuwadhibiti mkitaka kufurukuta ? majuha waliwao

 9. TANGAZO MUHIMU SANA KWA WAZANZIBARI

  Assalamu alaykum Wazanzibari wote walioko ndani na nje ya nchi:

  Kutokana hali ya mambo ya harakati ya kuikomboa Zanzibari tumeonelea kutoa taarifa kwa Wazanzibari wote tushikimane pamoja ktk kuikomboa nchi yetu kwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yetu ktk Tume la katiba, hii ni kwa7bu Tayari Watanganyika wameshatoa ruhusa juu ya kuujadili Muungano huu wa kuhuni ikiwa tunautaka au hatuutaki.

  Nanukuu kutoka kwa Jaji Warioba
  “Wale wote ambao hawautaki muungano wajitokeze kwa wingi ktk utoaji wa maoni na yatazingatiwa na kufanyiwa kazi”, sasa mimi kama mimi naona bora Wazanzibari tuende tukaukatae huu muungano hadharani mbele yao hawa Watanganyika ili tuone ikiwa hawatayafanyia kazi ndio hapo tutapigana uso kwa uso, roho kwa roho, jino kwa jino na damu kwa damu.

  Wazanzibari tunatakiwa tunatakiwa tuseme hivi:
  “Mimi fulani bin fulani……, Mimi siutaki muungano huu na ninachokitaka ni Zanzibari ilio huru, yenye mamlaka kamili kama nchi nyengine duniani kutokana na hali ya muungano huu wa kidhalimu ulipotufikisha Wazanzibari na kero kuwa nyingi kiasi ambacho hakuna haja tena ya kuzitatua, ”
  Ikiwa kuna marekebisho ktk haya ya kuzungumza ndani ya tume la katiba tujadiliane pamoja ili tupate kauli nzuri

  Lakini pia Wazanzibari tunatakiwa Tuendeleze kuungamkono harakati zetu za kuutafuta UHURU kupitia Jumuia za MUAMSHO kwa7bu ni muhimu sana harakati hizi.
  HARAKATI ZA MUAMSHO ZIENDELEE KAMA KAWAIDA TUSIRUDI NYUMA WAZANZIBARI WOTE.

  HATUUTAKI MUUNGANO, HATUUTAKI MUUNGANO, HATUUTAKI MUUNGANO,HATUUTAKI MUUNGANO,

  • NYIE KAMA HAMUUTAKI MUUNGANO ISIWESABABU YA KUGOMBANA NA WABARA WALIOKO ZANZIBAR NA KUWATOLEA LUGHA ZA KEJELI, KUCHOMA MAKANISA HUO CO MUUNGANO MUNAOUTAKA KWANI WAZANZIBAR WALIOKO BARA NANI ANAYEWATUKANA NA KUWANYANYASA? MTAANI UKIPITA MASHAKA MATUPU KWANINI MSIGOMBANE NA SERIKALI ETI MNAGOMBA NA WABARA WALIOPO HUKU KWENU ZANZBAR HIYO SIYO SOLUTION. NA TUNACHOTAKA WABARA MUUNGANO UKIVUNJWA KILA MTU ARUDI KWAO MZANZIBAR ATUDI KWAO NA MBARA ARUDI KWAO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s