Watu 33 wafikishwa mahakamani

Waislamu waliofika katika viwanja vya Malindi baada ya kutawanywa na jeshi la polisi huko Mahonda ambapo walikuwa wakienda Donge. baadhi ya watu wameumizwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa polisi wakiwemo wanawake ambao walikimbilia msikitini na kupata kichapo huko huko ndani ya msikiti

WATU  33 wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisilamu Zanzibar (JUMIKI) leo walifikishwa katika mahakama ya wilaya Mfenesini wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya mkusanyiko isivyo halali.

Watuhumiwa hao wakiwemo wanawake wa wanane, wanaume 25 na watoto wawili wa miaka 15 na 17 walidaiwa kutenda kosa hilo juzi huko Donge wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wamefikishwa mbele ya hakimu Fatma Muhsin Omar kujibu mashitaka hayo.

Pamoja na shitaka hilo, watuhumiwa hao pia walishitakiwa kwa kosa la kukataa amri ya kutawanyika, mashitaka ambayo yaliyasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Mkaguzi wa Polisi Khamis Abdulrahman.

Akiwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashitaka huyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Muhammad Nyange Haji (28) mkaazi wa Mkwajuni, Idd Makame Alawi (36) anayeishi Chumbuni, Juma Pandu Salum (30) wa Mwanakwerekwe, Kassim Abdulrahman Abdallah (30) anayeishi Mbweni pamoja na Juma Faki Juma (27) mkaazi wa Chumbuni.

Wengine ni Mohammed Juma Jongo (30) anayeishi Sogea, Khamis Humoud Khamis (39) wa Magomeni, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Salum Shaabani Hamadi (18) wa Amani, Mussa Hassan Haji (15) mkaazi wa Magomeni, Suleiman Abdallah Khamis (32) anayeishi Mwanakwerekwe, Seif Adinani Seif (31) wa Mwanakwerekwe na Mohammed Najim Suleiman (23) mkaazi wa Darajabovu.

Watuhumiwa wengine ni Khamis Ali Jamali (28) mkaazi wa Bububu, Mohammed Salum Bakari (27) anayeishi Nyerere, Mussa Hamadi Mussa (32) wa Magomeni, Othman Ali Khamis (22) mkaazi wa Tomondo, Kassim Shehe Khamis (5) wa Mahonda, Kheri Jecha Kheri (21) anayeishi Donge, Shukuru Pembe Juma (20) mkaazi wa Donge, Khamis Juma Ali (38) wa Donge na `Machano Omar Amour (27) mkaazi wa Bumbwini.

Pamoja na watuhumiwa hao, watuhumiwa wengine waliotinga katika kizimba hicho ni Ali Haji Makame (45) wa Fukuchani, Nahoda Haji Ussi (60) mkaazi wa Donge, Jabu Simai Sharif (17) anayeishi Mkwajuni, Riziki Omar Chande (42) wa Mfenesini, Halima Ali Kassim (38) mkaazi wa Bububu na Zuhura Salum Said (23) anayeishi Amani.

Wengine ni Mtumwa Haji Omar (47) mkaazi wa Kianga, Maryam Mohammed Bakari (30) wa Amani, Khadija Salum Juma (23) anayeishi Darajabovu, Hafsa Mohammed Mahfoudh (19) wa Kinuni pamoja na Saada Ali Ramadhani (28) mkaazi wa Jang’ombe.

Wote hao walidaiwa mahakamani hapo kwamba, kinyume na vifungu vya 55 (1) na 56 cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, walipatikana wakiwa wamekusanyika isivyo halali kwa dhamira ya kutenda kosa.

Sambamba na shitaka hilo, pia walidaiwa kukataa amri ya kutawanyika mara baada ya kuonywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kufanya hivyo, kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 60 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Mahakama iliambiwa kuwa, matukio yote hayo yalitokea Juni 17 mwaka huu baina ya saa 9:45 alaasiri na saa 10:35 katika maeneo ya Mahonda na Donge wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.

Wakati watuhumiwa 32 wakikana mashitaka hayo, mshitakiwa Ali Haji Makame hakuwepo mahakamani hapo licha ya kusomewa shitaka hilo, na habari zilizoelezwa mahakamani hapo zimedai kuwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Watuhumiwa wote hao wanasimamiwa na Wakili wa Kujitegemea Suleiman Salim Abdallah, ambaye aliiomba mahakama hiyo iwapatie wateja wake dhamana kwa masharti nafuu yatakayoweza kutekelezeka, ombi ambalo halikupingwa na upande wa mashitaka.

Akikubaliana na hoja hizo, hakimu Fatma Muhsin Omar aliwataka watuhumiwa hao kila mmoja kujidhamini kwa bondi ya shilingi 100,000 pamoja na kuwasilisha wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, ambao kila mmoja atasaini bondi ya kiwango kama hicho cha fedha.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kuiarisha na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa, ili kupata muda zaidi wa kukamilisha upelelezi huo, ambapo hakimu Fatma aliiahirisha hadi Julai 2 mwaka huu kwa kutajwa.

Wakati watuhumiwa hao wakiwa mahakamani hapo, ndugu na jamaa zao wa karibu hawakuruhusiwa kusogea katika eneo la mahakama na kutakiwa kukaa mbali, huku hali ya ulinzi katika eneo zima la mahakama hiyo uliimarishwa kwa askari Polisi wa Kikosi cha Kuzuwia Ghasia (FFU) waliokuwa wamevalia mavazi maalumu pamoja na mikononi mwao kushikilia silaha za mabomu ya machozi ili kukabiliana na hatari yoyote itakayo jitokeza, na askari Polisi wa kawaida na wengine waliovalia kiraia kutanda kila eneo kwa madhumuni ya kuimarisha hali ya usalama.

Advertisements

17 responses to “Watu 33 wafikishwa mahakamani

 1. YA RABBI WADAMIRISHE WATANGANYIKA NA VIONGOZI WAKE! NA INAWEZEKANA KABISA WAMEINGIA MSIKITINI NA VIATU! MAPAMBANO BADO NA TUTAENDELEA MPAKA KIELEWEKE!

  • We mkuu wa mkoa wa kaskazini jua kua dunia ninjia yenye mapit0 yake,ukizingati unaungu sukari,unatafuta kumaliza kwadua hebutulia ufe kwa kudra za Allah.

 2. Kila nafsi itaonja mauti. Hii ni kauli ya ALLAH hakuna wa kuipinga. Kw hvyo m2 asijitie kiburi et kw sbb anauwezo wa kupiga wa2 mabom. ALLAH hana haraka kw waja wake hivy nyny askar achen kiburi na majivuno maisha kupita 2. Halafu nyny mna watoto jueni kwmb ipo siku ukimzulutu m2 na yy pia hatakubali.

 3. “KAMAA TADYNU TUDANU”
  Huu ni usemi wa Kiarabu wenye maana ya kuwa “Kama ulivyokopesha ndivyo utakavyolipwa”, nataka kusema nini?
  Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Kwa hakika Polisi mambo yote ambayo mnawafanyia watu wenye haki yao ya Kikatiba kwa kkuwadhulumu Wallahi Mungu atawalipa na tunamuomba awalipe hapa hapa duniani tuwaone namna gani mnavyodhalilika kama mlivyowadhalilisha Wazanzibar kwa sababu ya kudai haki yao ya msingi, baya zaidi kuwafanyia vitendo ambavyo vya udhalilishaji wanawake wa Kiislam, kwa hakika haya yote yana mwisho wake na Inshallah mwisho wake tunaomba uwe ni mbaya kwenu kama ambavyo nyinyi mnafanya mambo hayo mabaya kwa umma wa Kiislam wa Wazanzibar
  Ewe Mola hakika sisi ni dhalili, dhaifuu, wanyonge, tusio silaha ya kupigania, silaha yetu ni wewe, Ya Allah waangamize kama wanavyotaka kutuangamiza, Mwenyezi Mungu ni juu yako roho zao.
  AMMMMIIIIIIIN
  AMMMMMIIIIN

 4. Pingback: Mhadhara wa Donge washindwa kufanyika·

 5. Kwanza nichukue nafasi hii kuwapa pole wale wote walioathirika katika kadhia hii ya kudai nchi yetu,kwa hakika ni msiba ambao unahitaji subra kubwa kwani lingelitokea la kutokea lakini kutokana na rehma ya Mola wetu imekuwa ni sahali kubwa kwa wazanzibari wenzangu.
  Siku hii nilitharurika kidogo nikawa si wa kuhudhuria lakini moyo wangu umeghadhibika baada ya kuona baadhi ya walioumia katika kadhia hii.
  Hivyo nawaomba ndugu zangu wazanzibari na waislamu tuwe na subra na tuendeleze mapambano yetu mpaka kieleweke.
  Mola wetu ameshatukamilishia dini yetu na ameridhia kwetu kuwa waislamu ambayo dini ya haki.
  Wajibu wetu kuusiana haki na subra.Ewe mola wetu tumiminie subra kutoka kwako utuepushe na kumwaga damu ya waislamu wenzetu bila ya haki,

 6. kupiga watu waliokimbia na kujihihifadhi ndani ya msikiti hii ni haki?wako wapi waliokuwa mahodari wa kulaani kuchomwa makanisa mbona hatuwaoni?viko wapi vyombo vya khabari?wako wapi watetezi wa haki za binaadamu?hawa waliojeruhiwa kwa kipigo cha polisi sio binaadam?ingekuwa mkusanyiko ule ndio wa askofu mokiwa na kondoo wake waliopotea hivi mngewazuia?labda niwakumbushe waheshimiwa ya kwamba wazanzibari kama wazanzibari muungano hawautaki na nyinyi hilo munalijua dhahir lakin nyinyi mnalazimisha,mmesahau yaliomtokea husni mubarak?katumia polisi katumia janjaweed kama hawa wa kwetu kapiga sana watu kaua watu kaeneza sana propaganda ooh hawa hawapendi amani oh hivi ni vikundi vya wahuni mara hawa siasa kali mara wanafana na alqaeda je mwisho wake ukawaje? kama mnaakili tena ya kuzingatia wala hatutafika huko lakin mkiwalazimisha watu itakuwa hatari.anae lazimishwa ni punda na sio binaadam na lait kama punda angepewa akili walah asingebeba mzigo wa mtu yoyote.

 7. Mimi naona ingetumika approach ya Mashekhe kutemblea misikiti wakizungumza na Waumini badala ya hii ya kuandamana makundi ya Watu. Hii itazuia watu kuumia lakini pia haitawapa nafasi wale wakatao mikusanyiko kwa kisingizio cha uvunjifu wa amani. Ndugu Zanzibar ni fragile katika kila hali. Huko tunakoelekea ni kuzuri kwa kila mtu lakini intachukua muda kukufikia. Vile vile maandalizi yake yanategemea ni kiasi gani kwa sasa Zanzibar ina baki bila kuyumba kiuchumi na kijamii.

  Wasiopenda Zanzibar ibaki hivi wanafanya juhudi ya kuiyumbisha. Angalia Dar baada ya Vurungu za hapo nyuma mabango ya matangazo ya Mkutano wa CCM yalisema “VURUGU ZA UAMSHO – CCM kutoa TAMKO. Hii inajenga picha ya kuwa CCM kwa sasa haina ajenda nyengine isipokuwa UAMSHO- ili hali si kweli. Katika hali hii UAMSHO inabidi ifanye mambo kwa tahadhari isiangukie mtego.

  Hali ya Uchumi wa Zanzibar pia ni tete – unategemea utalii ambao unahitaji utulivu. Vurugu zikiendelea mambo yataharibika na hiyo sisi tuakuwa kama kima wakataao kula mazao ya Mkulima. Kenya kwa sasa inagharimika tayari kutokana na ugomvi wa Alshabab. Duni hii ni kama kiganja na mawasiliano yanakwenda kwa kasi kubwa ya ajabu.

  Najiua ni muhimu kudai Zanzibar iwe huru lakini ni muhimu pia kuona madai haya yanatolewa pasi na umwagikaji wa damu. Kama ni ufikishaji wa ujumbe basi kwa CD zilizotawanywa na mihadhara iliyofanyika basi ujumbe umefika. Mtu moja moja anaweza pia kufikisha ujumbe wa kukataa Muungano kama vile tufikishavyo ujumbe wa neno la Mungu na hii inaweza kutokea katika kiwango cha Familia hadi kwenye vijiwe vyetu.

 8. Naungana na mwenzangu hapo juu, hata viriri vya sala ya IJUMAA kutumika kudai haki yetu mpaka kieleweke .
  JUMIKA , ajishughulishe door to door kukusanya saini na CDs kuonesha kila mtaa kwa kina mama,
  kurudi myuma si kushindwa bali ni kujipanga vizuri

 9. JAMANI! HAKI INAPO DHIHIRI BATIL HUJITENGA ! LEO HII NAONA MAJINA YA FAMILIA YA HAO WANAOJIITA WAZAWA WAPINGA UAMSHO! LEO NAWAONE HAYA! JEE ENYI WAANDIKA MATUSI KACHORORA HAKI INAKUJA! JEE NA HAWA WAMETOKA MTAMBWE AU MKANYAGENI? MUSIWASEMEE WADONGE! LET THEM SAY! ACTION SPEAK LOUDER THAN WORDS! WALLAH KUVUKA NGUO KWA WACHAWI WA NCHI HII KUNAKARIBIA! BABU WA KISARAWE UPO? UMRI UMEENDA TUBU KWANZA! ACHA FITINA!

 10. Binafsi nadhani sasa tuendeleze kutoa elimu pasi na kukusanyika , mi nadhani inatosha, mihadhara iliyotolewa na uamsho inatosha, hawa jamaa wanatafuta sababu tu na tuendeleze kuidai nchi yetu hata katika viriri vya ijumaa badala ya kukusanyika. hakuna ujombozi upatikanao kirahisi, kuna watu watapoteza maisha katika hili na wengine kuwa vilema wa milele, ila hatutochoka.

 11. KUNA WENGINE TUTAPOTEZA UHAI WETU NA WENGINE TUTAKUA VILEMA WA MILELE KATIKA HARAKATI HIZI ZA KUIDAI NCHI YETU, HAKUNA UKOMBOZI UPATIKANAO KIRAHISI NA WALA HAKUNA DHULMA IONDOKAYO KIRAHISI. ILA HAWA JAMAA NA WAPINGE WANAVOPINGA ILA MWISHO WAO UNAELEKEA, TUMECHOKA KUDHALILIKA.
  TUWE NA SUBRA KATIKA HILI

  • Yarabi tunakuomba kama ulivyosema niombeni nitakupeni nasi tunakaomba yarabi ilinde zanzibar yetu na waislam wote wa zanzibar yarab kila ajae kwa shari, ivunje yake dhamiri, asiweze kusimama. anaefanya dhamira kwenye yetu mihadhara Mola umpe madhara asiijue dunia, nchi hii ipe neema kwa amani na salama utupenjema afia yarab ilinde nchi yetu wasingie madhaif , wakawa na mbovu nia amiinnnnnnnnnnnnnnnnn Jamhuri ya watu wa zanzibar kwanza

 12. Mtihani kwako mh Shein, mwenzio Salmiin Amour alifeli ktk ishu ya Sheikh Kurwa akapiga watu na kuwadhalilisha sasa mungu anamdhalilisha yeye amekimbiwa na mke, mungu kampa upofu nk, nawe shein angalia kiti hicho washakalia wengi wakaondoka.

 13. MUUNGANO HAULINDWI KWA KUPIGA WANANCHI WLIOUNGANA MABOMU NA RISASI. KAMA HAWAUTAKI WAPENI NCHI YAO HUKO NAKO PIA NI KUIMARISHA MUUNGANO. MTATUMIA MAJESHI NA BUNDUKI MPAKA LINI KUIMARISHA MUUNGANO? ENYI KIKWETE NA HAO WENZIO HEBU TUMIENI AKILI NA SIO MAGUVU KULINDA MUUNGANO. UNAWEZA KUMCHUKUA PUNDA HADI MTONI LAKINI HUWEZI KUMLAZIMISHA KUNYWA MAJI

 14. Naumia sana nikiskia wananchi wenzangu wanapoteseka kisa wanaelezea hisia zao ninacho viongoz wa juu wa smz wasishughulikie mandaman na wangalie nin wananch wanachadai wanaweza kufanikiwa kusupress mihadhar na makongaman lakin nivigumu kwa jesh la polisi kujakusupress chuki ya wazanzibar wanaoteswa na polisi ambao si wenyej wa znz wala si ndugu ktk iman waheshmiwa viongoz wa smz angalien msigongeshwe vichwa na ndugu zenu na mkawauwa kupitia jesh la mungan huku upande wa pili wenzetu wametulia na wanandika kwa sura mbaya juu ya znz tunaipenda aman lakn ktk hali iliyopo znz aman huenda ikiwa ni ndoto kwn kukitokea fujo smt inaleta majesh kutoka t bara je hamuangali kuna nini hapo pamoja tunaweza kuifanya znz ni visiwa vya aman.

 15. Waislam wenzangu wanaodhulumiwa si muamsho bali waislamu wa zanzibar kuna watu wanashadidia dhulma iliyopo lakn wakumbuke mtume anasema asiyejali shida za waislamu wenzake si ktk sisi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s