Kukimbia kutoa maoni ni kujitia kitanzi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewahakikishia wazanzibari kuwa maoni yao hayatatupwa kapuni na badala yake yatafanyiwa kazi na serikali na kuonya kuwa kukimbia kutoa maoni ni sawa na kujitoa kitanzi. Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Sheria ya Katiba Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari huko Mapofu Wingwi, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

“Wananchi nakutoweni wasi wasi, maoni yenu hayatachakachuliwa, tume ya kukusanya maoni ina wajumbe sawa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, kamwe wajumbe wetu hawataisaliti Zanzibar”, alisema Bakari ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Mgogoni.

Bakari alisema anafahamu mawazo ya wazanzibari yalivyo hivi sasa yalivyo juu ya suala la Muungano na namna hisia zao zilivyo lakini aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kutoa maoni yao kwani ili yafanyiwe kazi na kuahidi kwamba hakutakuwa na njia yoyote ya kufanyika udanganyifu.

“Nawasihi Wazanzibari tuitumie fursa hii kutoa maoni yetu, ili Zanzibar iwe na uwezo wa kufanya mambo yake kwa maslahi ya Wazanzibari, kukimbia kutoa maoni yetu ni sawa na kujitia kitanzi”, alionya Waziri huyo ambaye kitaalumu ni mwanasheria.

Alisema kwamba tume ya kukusanya maoni itakafika Zanzibar kwa kazi, huo ndio utakuwa wakati mzuri wa kusema kitu gani wanakitaka wazanzibari katika Muungano na kumaliza kasoro ambazo wanaziona ni kero kwao na ni mambo ambayo hayafai kuwa ya Muungano.

Akitoa onyo kwa wazanzibari Bakari alisema kwamba iwapo wananchi hawatajitokeza kutoa maoni, itaonekana wameridhika na mfumo uliopo pamoja na utaratibu wa sasa wa uendeshaji wa Muungano na hivyo kupoteza fursa muhimu ya maslahi ya nchi yao.

Waziri huyo alisema tume hiyo ya kukusanya maoni ya wananchi inayoongozwa na Jaji Warioba inatarajiwa kuja wiki hii kwa ajili ya kuzinduliwa rasmi na kuanza kuchukua maoni ya wananchi juu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa upande wake amewahimiza Wazanzibari kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwa uhuru juu ya aina ya Muungano wanaoutaka, wakati tume ya kuchukua maoni ya wananchi itakapo kuja Zanzibar.
Maalim alisema fursa waliyonayo wananchi kutoa maoni yao katika mchakato wa kuandika Katiba ya Jamhuri ya Mungano ni adhimu na wala wasikubali kuhadaiwa au kutishwa na mtu yeyote na kuipoteza haki yao hiyo.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza wanachama wa CUF na wananchi wengine waliohudhuria katika mkutano wa hadhara kuwa katika miaka 48 ya Muungano wananchi hawajapata fursa kama hiyo, hivyo wasikubali kuitupa, na hasa kwa vile hawana uhakika iwapo itatokea tena katika maisha yao.

Akizungumzia msimamo wake binafsi Maalim Seif alisema ajenda kuu kwa Wazanzibari katika mchakato wa kuandika katika mpya ni Muungano, hasa kwa kuzingatia Zanzibar inayo katiba yake ya mwaka 1984 inayojumuisha mambo mengi yanayowahusu Wazanzibari, kama vile haki za binaadamu, mgawanyo wa madaraka na mambo mengineyo.

Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma na Haki za Binaadamu wa chama hicho, Salum Bimani aliwapongeza viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi kubwa wanazozichukua katika kuondoa shida za wananchi.

Alitoa mfano wa juhudi kubwa zilizochukuliwa na ambazo tayari zimeanza kuza matunda na kuwanufaisha wananchi ni kulishughulikia tatizo la usafiri wa baharini kati ya Unguja na Pemba na kupandisha bei ya zao la karafuu.

Bimani alisema wananchi wanapaswa kuwapongeza kwa dhati viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiwemo Rais Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili, Balozi Seif Ali Iddi kwa juhudi kubwa wanazozichukua kumaliza tataizo la muda mrefu na usafiri kati ya visiwa hivyo.

Ziara hiyo ya Maalim Seif na ujumbe wa chama chake imelenga kukagua uhai wa chama cha CUF, katika majimbo ya Mgogoni na Micheweni ambapo Bimani alisema ziara hiyo imewatambulisha kwamba bado wanachama wa chama hicho wana imani na viongozi wao na wapo tayari kufanya nao kazi kwa ajili ya kuendeleza chama chao.

Advertisements

15 responses to “Kukimbia kutoa maoni ni kujitia kitanzi

 1. wanasiasa uchwara wamefilisika kisiasa tafuteni kazi ya kufanya wacheni kuwahukumiya wazanzibar wanataka nchi yao hawataki muugano hayo ndiyo maoni ya wazanibari hata mabwana zenu watanganyika wanajuwa hilo

 2. Pingback: Kukimbia kutoa maoni ni kujitoa kitanzi-SMZ·

 3. Nadhani wazanzibari tunahitaji pia kuwa na hekima na hili, UAMSHO wanahitajika kupresurerize na pia maoni tunatakiwa tukatowe. Strategies ni kitu muhimu katika mambo mengi hata uislamu ulijengeka kwa utaratibu huo

 4. hawa watu wanatulazimisha tukatoe maoni yetu mm niwaombe uamsho siku itakayokuja tume ya katiba mashekhe wetu naomba mutuongoze watakapokuweko hao watu wa tume tunaenda kama tunavofanya mihadhara halafu wakituambia toeni maoni yenu asimame shekhe faridi ama shekh musa ama yoyote yule atuulize wazanzibar maoni yenu ni nini na sisi sote tutasema kw pamoja kua hatutaki muungano kwisha
  ndo naona masikio yao yatatoka uziwi hawa tanganyika kua muungano hatuutaki

 5. abaazanzibar on June 17, 2012 at 10:52 pm said:
  Nadhani wazanzibari tunahitaji pia kuwa na hekima na hili, UAMSHO wanahitajika kupresurerize na pia maoni tunatakiwa tukatowe. Strategies ni kitu muhimu katika mambo mengi hata uislamu ulijengeka kwa utaratibu huo

  Wewe usahihi ndugu yangu. Kwenye mapambano huchagui njia moja tu ya kupigana. Diplomacy inahitajika kuwashawishi waogopao vita na hii itafanya waunge mkono madai yaliweka mezani. Vita mara nyingi hufungua milango ya kufunga options nyengine. Angalia Syria leo.

  Historia ina Mtaja Mtume wetu alivyokubali madai ya Wapinzani wake na baadae akaiteka Makka na hivyo kuutangaza Uislamu kwa kifua mbele. Muhamad Rehema na Amani iwe juu yake alikubali katika mkataba itajwe kuwa yeye ni Muhammad Bin Abdi Llahi na isiandikwe ni Muhamad Rasul Llahi. Muhammad alijua kuwa yeye ni Mtume na watia Saini wa Upande mwengine wasingeweza kubadilisha utume kwa text au wording.

  Nabii Mussa alipotumwa kwa Firauni Mungu alimwabia Firauni kachupa Mipaka kwa kujiita Mungu. Hatahivyo, Mussa aliambiwa azungumze nae kwa maneno ya upole. Hawa wapinzani wa UAMSHO si dhani ni sawa na Firauni. Hatuja wasikia wakijita Miungu. Kuzungumza katika vikao halali ni muhimu kufanya maoni ya Waliowengi yasikike.

  Watu wengi wanaunga mkono kuwa madai ya Watu wa Zanzibar juu ya Muungano ni legitimate. Mijadala ya Barazani kuhusu Muungano pia inaonesha mapungufu yaliyomo kwenye Muungano na mahitaji ya kupata mfumo mpya. Vyovyote vile iwavyo, mabadilko hayaji siku moja na hayapatikani kwa kutumia njia moja. Ilichukua Tanzania miaka kukbali mfumo wa vyama vingi, ikachukua miongo mengine kadhaa kukbali kuandika katiba mpya. Finge hizi ndani constitution making process iliyoanza inaonesha mabaki ya kukataa kwa mamlaka kupekuliwa.

  Hapa tulipofika si mahali paku paachia au kufanya mambo ya kuturudisha tuliko toka ambako area commissioner alikuwa Alpha na Omega alitandika watu bakora hadharani huku akicheka, alilazimisha aozwe mtoto wa watu ka nguvu akijua kuwa mapenzi ya nguvu hayadumu na tumeyaone matokeo baadae, alilazimisha watu wasimame mvuani wakisubiri rais hata kama bado yu Unguja, alilazimisha watu watoke Konde wakajenge Nyumba Wete, majumba ambayo baadae yameachwa kama vihame na kana kwamba hayakujengwa na watu waliolazimishwa. Historia ya Zanzibar ina mapungufu mengi. Wengi tulisubiri zama za Watu kusameheana na hazikuja. Kwa sasa tukiwa na makovu ya nyuma tungedai autonomy ya Zanzibar pasi na kutoneshana.

  Reply ↓

 6. Ni kweli maneno yako @abaazanzibar, tunahitaji lakini inabidi haraka sana tuwasomeshe wenzetu mambo yaliyomo katika katika kongwe iliwajue tunavyobanika wengine wanafuata kutokana na hali mbaya za maisha lakini sababu hawazifahamu hasa, tunahitaji kutoa elimu kubwa ili hatimaye tuonyeshe hasa huo muungano hauna nguvu kama hawakutia kapuni maoni, wasijewasema tu muungano hatutaki kuna mambo ya uhamiaji, tuwe na passport zetu peke yetu na kuweza kudhibiti uhamiaji kama zanzibar, hatuhitaji TRA yaani watu wajue vitu kama hivi

 7. Mimi nadhani hekma ni kitu muhimu sana hapa na katika mapambano ni lazima mutafute silaha za aina tofauti, Uamsho wanatoa shinikizo zuri sana kwani ukitaka elfu kumi omba kumi na tano ili upewe hiyo kumi ila naona pia ipo haja ya kujia ndaa juu ya kuwa na maoni ambayo ni “very constructive” ili hawa jamaa wasije wakatupiga kwa statistical figures.

 8. Binafsi Napenda kuwashauri wa znz wenzangu tuende tukatoe maoni yetu siku zikifika, tukiacha kwenda watatumwa watu wakatusemee kisha ionekane sisi sote ndio tuliosema, hatuuhitaji muungano ila nahii pia ni fursa ya kuukataa huo muungano. shime tukatoe maoni yetu

 9. nafikiri kama wanataka tukatoe maoni , tukubaliane wote oni letu liwe moja tu tusimame wote kwa pamoja mbele ya hio kamati yao feki , na kusema ‘ HATUTAKI MUUNGANO ‘ halafu wote tutoke nje tuelekee majumbani mwetu

 10. Tunachokwambieni nyinyi Tanganyika kuwa Muungano hatuutaki hata kuusikia!!!!! Mmeshatukandamiza vyakutosha na kutuburuza sana hivyo TUACHENI TUPUMUE!!!!!!

 11. MUUNGANO NI HIARI AU LAZIMA? NYERERE ALISEMA” Muungano ni kama nguo ikwatosha wazanzibari wataivua…”. KWA NINI IMETUTOSHA MNALAZIMISHA KUENDELEA NAYO WATANGANYIKA? SAFARI HII MPAKA KIELEWEKE INSHAALLAH.

 12. SERIKALI ZOTE MBILI ZITAMBUE ZILICHAGULIWA NA RAIA KWA WINGI WA KURA, HIVYO HAO HAO WALIWACHAGUA NDIYO HAO HAO WANAOKATAA MUUNGANO KWA NGUVU ZA IDADI YAO, KWANINI SASA HAMTAKI KUWASIKILIZA?

 13. Mimi naona viongozi wetu wa CUF nao wanalewa raha tangu walipewekwa kwenye fupa. Washasahau kauli zao walipokuwa wakipanda majuukwaani wakati wa kampeni zao. Tuseme wao hawajui wazanzibari wanataka nini? Hivi kauli zetu hawazisikii? HATU TAKI MUNGANO.

  • MIMI NAFIKIRI HILI LA KUDAI ZANZIBAR HURU SI LA CHAMA FULANI, PIA NAONA SI VYEMA KULIHUSISHA NA CHAMA FULANI NDIYO MAANA HATUTUMII BENDERA ZA CHAMA HATA KIMOJA, TUSIHUSISHE NA SIASA TAFADHALINI WASOMI WENZANGU, TUSISITIZE UMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s